*KATIKA TOBA KUNA TUMAINI, HATA KAMA KOSA NI KUBWA*
Na Mwl Proo
*_(Mjumbe wa Matengenezo)_*
0762879363
Bwana akae nanyi!! ✋🏾
Hauna sababu ya kuikosa mbingu kwa kweli hii, utakayojifunza leo. Labda uwe umechagua mwenyewe, maana Mungu alituumbia uhuru wa kuchagua, hatulazimishwi katika lolote hata kama ni jema.
Toba ya kweli, ni dawa kamili. Neno hili toba, tutalielewa kwa usahihi toka katika asili yake katika kiebrania. Neno תשובה _*(Teshuvah)*_ maana yake kurudi. Kurudi wapi? katika hali ya asili. Katika usahihi wa maana ya neno hilo Teshuvah, limejumuisha mambo matatu,
➰Kujutia matendo yasiyofaa (Regret of misdeeds)
➰Kufanya maamuzi thabiti ya kubadilika (Decision to change)
➰Kufanya maungamo ya wazi (Verbal expression of one's sins)
*KATIKA UYAHUDI*
KUNA SIKU 10 MAALUM KWA AJILI YA KUFANYA TESHUVAH (TOBA). KATIKA MWEZI WA TISHREI (1,2) UNAITWA MWEZI WA MAPUMZIKO, NDIPO WANAKUWA NA SHEREHE IITWAYO _*Rosh Hashanah (sherehe kama za mwaka mpya)*_ NDANI YA SIKU 10, KUIFIKIA SIKU YA UPATANISHO IITWAYO _*Yom Kippur*_NDIPO WAO HUTUMIA KUFANYA HIYO TESHUVAH (TOBA).
Sasa neno hili Teshuvah la kiebrania hutamkwa *"tashuv hey"*, Neno la kwanza Tashuv maana yake kurudi, lakini herufi hii ya Hey (H) ni ileile ambayo ipo mwishoni mwa jina la Mungu YHWH yenye maana ya Malchut(Kiebrania), neno hili lina maana sawa (synonimous) na Neno Shechinah (Shekina), neno hili Shekina maana yake ni jinsi ambavyo Mungu, anajidhihirisha kama Mungu asiyeshindwa/asiye na ukomo wa nguvu/mwenye enzi (Sovereign) kwa viumbe wake.
Jina Yerusalem (Mji mtakatifu) ni neno la kiebrania *_Yerushalayim (Yira Shalem)_*, maana yake ni hali ya ukamilifu wa kicho/ogofyo la kimungu.
Ambapo Israel walipokaa sawa kiroho, Shekina (udhihirisho wa utukufu) ulikaa juu yao. Na walipokosea kwa kutenda dhambi, ikasukuma kuondoka kwa Shekina (Shechinah), na wakaishia kuteswa na maadui au kupelekwa utumwani. Swala kama lile la kubomolewa kwa hekalu 🏛, ilikuwa ni kiashiria halisi cha hali mbaya ya kiroho ya Yerushalayim (Haya huweza kumkuta mwamini katika maisha yake, ndio maana lazima ujifunze namna ya kutengeneza maisha yako ya kiroho). KWA WAKATI WAKO, FUATA HII LINK UPATE SOMO MAALUM LA KUTENGENEZA MAMBO YA KIROHO YALIYOHARIBIKA
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
http://alltruthjohn1613.blogspot.com/2016/09/namna-ya-kutengeza-mambo-yako-ya-kiroho.html
SASA TESHUVAH, NI TUKIO LA KUREJEZA ULE UKAMILIFU KICHO CHA JINA LA BWANA, NA KURUHUSU SHECHINAH KUIFUNIKA YERUSHALAYIM TENA, AMBAYO KWA LEO NI MOYO WAKO NA MAISHA YAKO KWA UJUMLA.
*MOYO WA SOMO*
WANA WA ISRAEL WALIWAHI FANYA KOSA KUBWA MNO, AMBALO HUENDA NI KAMA LAKO, LAKINI WAKO AMBAO WALIJUA KUWA KWA MUNGU, KAMA UKIFANYA TESHUVAH (TOBA YA KWELI), LIKO TUMAINI JIPYA. TUSOME;
Ezra 10 : 2
*_......Sisi tumemkosa Mungu wetu, nasi tumeoa wanawake wageni wa watu wa nchi hizi; lakini kungaliko tumaini kwa Israeli katika jambo hili._*
MIONGONI MWA MAMBO AMBAYO MUNGU ALITAHADHARISHA SANA, NI KUOA MATAIFA (INTERMARRIAGES WITH GENTILES). SASA ZAMA HIZI SIO TU RAIA, MPAKA MAKUHANI WALIKUWA WAMEKWISHA OA WANAWAKE WA MATAIFA NA WAMEKWISHA ZAA NAO. 👨👩👧👦👨👩👧👧👨👩👦👦. LAKINI YULE SHEKANIA MWANA WA YEHIEL, ALIJUA YUKO MUNGU AMBAYE PAMOJA NA HILO KOSA BAYA MNO, KUNA TUMAINI KAMA WATATUBU, NA KULIPA GHARAMA YA TOBA.
Hivi nani aliafanya meanderings za dhambi kama Ahabu? Aliyemuoa Yezebel, aliyeleta mungu mgeni, akaivuruga nchi yote kwa ibada ya sanamu, na bajeti kubwa ya ikulu ilitumika kulisha mamia ya manabii wa baali walioletwa na Yezebeli. Lakini baada ya kukutana na Eliya Mtishbi, na akatamkiwa yale mabaya, hakusubiri yamkute, alijivesha magunia akajinyenyekeza kwa Mungu, Naye Mungu akaifutilia mbali ile adhabu kwa wakati Ahabu isimkute (1Falme 21:20-29).
Ni toba ndiyo ilivifunga vitabu vya hukumu, juu ya mji wa Ninawi usipigwe kiberiti(sulphur) cha Mungu 🔥🔥🔥.
*NINAZUNGUMZA NA WEWE MTUMISHI*
LEO NIPO HAPA KAMA SHEKANIA, UPO MCHUNGAJI AMBAYE UMEAMUA KUJIKAZA. ULIANGUKA KATIKA UZINZI, UKAMPA BINTI UJAUZITO, UKAONA HIYO AIBU NI KUBWA, UKASHAURI ATOE MIMBA, ILI UTUNZE HUDUMA. WEWE MTUMISHI AMBAYE UKIJISIKILIZIA NDANI YAKO, UNAONA WAZI ULE UDHIHIRISHO WA SHECHINAH HAUPO, INGAWA UMEJIKAZA KUENDELEA NA HUDUMA. NAZUNGUMZA NA WEWE MWIMBAJI, AMBAYE MOYONI UNAGUNDUA HUMGUSI MUNGU, UMEBAKI TU UNATUMIA KIPAWA CHA MWILINI KUTAFUTA RIDHIKI 🍞. KUNA JAMBO ULIFANYA, NA UMELIFICHA, LAKINI LIMEUFICHA ULE UTUKUFU SHEKINAH-KIND. YOU NEED TESHUVAH (You regret of your wrongdoing, you decide to change and you confess/verbal expression). HIYO YA TATU INAITWA GHARAMA YA TOBA, WENGI HAWAITAKI, ILA NDIO UFUNGUO 🔑. KATIKA EZRA 10:3 TUNASOMA;
_*Haya basi! Na tufanye agano na Mungu wetu, kuachana na wake zetu, na wale waliozaliwa nao, tukilifuata shauri la bwana wangu, na shauri la hao wanaoitetemekea amri ya Mungu wetu; mambo haya na yatendeke kwa kuifuata torati.*_
👆🏼👆🏼👆🏼👆🏼HIYO INAITWA GHARAMA YA TOBA. KAMA ITAKUGHARIMU KURUDISHA PESA ULIZOPORA, DO THAT, KAMA IKIKUGHARIMU KWENDA KWA MMEO KUMWAMBIA KWAMBA HUYU MTOTO SI WAKO, NILITOKA NJE YA NDOA NIMPATA, AU MUME UNA MTOTO URAIANI, UNATUMA MATUMIZI, MKEO UMEMFICHA, TOBA YA KWELI, ITAHUSISHA KUMWAMBIA TU. IKIKUGHARIMU KUSIMAMA MBELE YA WATU, KUSEMA KWAMBA ILE MIMBA NILIYOIKATAA NI YANGU KWELI, DO IT PLEASE. KWENYE GHARAMA YA TOBA, UTAMSIKILIZA ZAIDI ROHO MTAKATIFU AU USHAURI WA WATUMISHI WA MUNGU, SIO MAMBO YOTE UTAPASWA KULIPA GHARAMA, MAANA WAKO AMBAO WALIJIPELEKA POLISI KUSEMA MIMI NDIYE NILIYEUA ILE FAMILIA, WAKATIWA KATIKA VIFUNGO VYA MAISHA (BWANA AKIAGIZA NENDA, MAANA HUENDA KUNA ANAYETUMIKIA KIFUNGO NA HANA HATIA). KWA KUWA HII GHARAMA HULIPWA MTU AMEKWISHA TUBU, ANAYO NAFASI YA KUMSIKIA ROHO MTAKATIFU. NILIMSIKIA EV. EPHRAIM MWANSASU, YEYE ALIKUWA NA BASTOLA 🔫, AMBAYO NI SILENCER, ALIPOTUBU ALIISALIMISHA POLISI MWENYEWE. NARUDIA TENA GHARAMA YA TOBA UTAPASWA KUSIKILIZA MAONGOZI YA ROHO MTAKATIFU AU WATUMISHI, MAANA YAKO MENGINE YANAWEZA KUWAHARIBU WENGI BAADA YA KUPONYA, YAKAHARIBU KABISA. SAA ZINGINE GHARAMA YA TOBA INAKUWA NI KUTENDA TU MATENDO YA HAKI ZAIDI YA MWANZO. ZAKAYO ALIPOTUBU, AKAAMUA KULIPA GHARAMA YA TOBA KWA KUWARUDISHIA WALE ALIO WANYANG'ANYA MARA 4 YA KILE ALICHODHULUMU.
Ufunuo 2 : 5
_*Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza.*_
*GO FOR TESHUVAH, USIKUBALI KUISHI NA DHAMBI UNAYOIJUA, INAYOKUZUILIA SHECHINAH. HAUNA SABABU YA KUACHWA SIKU YA UNYAKUO, HAUNA SABABU YA KUIKOSA MBINGU. KWANZA UTADAIWA NINI UKITUBU?.*
Mwl Proo
(Prosper Kadewele)
0718922622
ATG whatsapp group (0762879363)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment