*ALINIONA KUWA MWAMINIFU*
π² πΌ π± π΅ π· π΄ π΄
*0762879363*
©2016
NAWASALIMU NYOTE, KWA JINA LA YESU!!✋πΎ
Leo Bwana Yesu ambaye ni mwaminifu (El Melech Ne'eman), amenipa hili jambo. Nimejiridhisha 100%, kwamba hili ndilo liliujaza moyo wake pia.
Neno *_Mwaminifu/Faithful_*, (Χ ΧΧΧ-Ne'eman>Hebrew/ΟΞΉΟΟΟΟ-PistΓ³s>Greek), ni yule anayedhihirisha kushikamana na kitu bila kuacha (constant/consistent), bila kugawanyika nia (undivided/single-minded), kwa mtu au kitu, asiyeweza kukuangusha (staunch/loyal), anakupa uhakika (assurance/reliable). Mwaminifu anatenda yote bila kupunguza, hakuangushi *(KUNA WATU WENGI TU, WAMEWAHI KUMWANGUSHA MUNGU/THEY FELL GOD)*
1 Timotheo 1 : 12 *_Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;_*
MTUME PAULO ANATUPA SOMO, KWAMBA SIFA YA UAMINIFU, NDIYO KIVUTIO CHA YEYE KUKIRIMIWA YALE ALIYOPEWA KATIKA UTUMISHI. KUMBUKA SISI NI MAWAKILI (ADVOCATES) WA MUNGU, INGREDIENT MUHIMU KATIKA HUO UWAKILI WETU NI KUWA WAAMINIFU (1KOR 4:1). TUMEOKOKA WOTE, LAKINI UAMINIFU, AMBAO NI TABIA YA NDANI, ITATUTOFAUTISHA TU MBELE ZA BWANA MKUBWA, YESU KRISTO. NA KIASI CHA UAMINIFU KITATOFAUTISHA KIASI CHA KUAMINIWA, AMBAKO HUKO NAKO KUTATOFAUTISHA NUMBER OF TASKS/RESPONSIBILITIES. TAWI LIKIZAA (UAMINIFU), LINAKUWA PRUNED✂π±π΄, ILI LIZAE ZAIDI. KWA HIYO MWINGINE HAAMINIWI, KIASI CHA KUPEWA MENGI KUFANYA KATIKA UFALME. NA WENGINE WALISHINDWA KUWA WAAMINIFU KWA VICHACHE, SO HAWAKUPEWA KINGINE. MWINGINE AMEBAKI ANAIMBAπ€πΉ, AKIDHANI NI MTUMISHI KATIKA SHAMBA LA BWANA, KUMBE AMEBAKI TU NA KIPAWA CHAKE CHA ASILI (TALENT-KARAMA YA MWILI), AMBAYO HATA WCB NA YA MOTO BAND WANACHO. KIPAWA CHAKO CHA KUZALIWA NA UWEZO WA KUPAMBA SAUTI KAMA CELINE DION, KILIHITAJI UAMINIFU KWA MUNGU, ILI UFANYE HUDUMA YA ROHO, KWA HICHO KIPAWA.
Tumekuwa tukiona mambo ya kiroho kwa mafumbo mfumbo. Sio lazima iwe hivyo, Mungu anatamani saa nyingine asema wazi not in riddles (Hesabu 12:6ff), Lakini kigezo cha kuyapata mambo kwa wazi sana ni UAMINIFU. Mungu alipoona siku za Musa kufa, zimekaribia, alisaka mwaminifu ili amwagize kazi, asingeweza kuweka yeyote ambaye angekuja kumwangusha Mungu badae.
Kumbukumbu la Torati 31 : 14
*_Bwana akamwambia Musa, Tazama, siku zako za kufa zinakaribia, umwite Yoshua, nanyi mkajihudhurishe katika hema ya kukutania, ili nipate kumwagiza kazi. Musa na Yoshua wakaenda, wakajihudhurisha ndani ya hema ya kukutania._*
KWA HIYO KAMA ULIONA KUNA TOFAUTI, YA MAJUKUMU/TASKS/RESPONSIBILITIES KWA WATU KATIKA UTUMISHI, NI UAMINIFU NDIO SABABU. MWINGINE UNAHISI KAPENDELEWA. UKIMWEKA KATIKA KUHUBIRI ππ½, KATIKA MAOMBI ππ½, KATIKA UIMBAJI ππ½, KATIKA KARAMA ZA NGUVU ππ½, KATIKA KARAMA ZA UFUNUO ππ½, KATIKA MAONGOZI ππ½, FURSA ZA KIHUDUMA ZOTE ZINAMWANGUKIA YEYE, KIBALI KISICHOKOMA KWA MUNGU NA WANADAMU, KILA ANAPOKUWA POSITIONED ANAFIT TUU. YESU ANAMWAMINI HUYO, KUWA HATO-MWANGUSHA. MUNGU ALIJARIBU KUMWAMINI SAULI BEN'KISH, KWA UTUMISHI FULANI WA KUANGAMIZA WAAMALEKI, SAUL FELL GOD, MUNGU AKAJUTA π£. UNAONAJE MUNGU AKAKUAMINI KUKUPA KARAMA KUBWA YA MIUJIZA, HALAFU GHAFLA TUNASIKIA SKENDO YAKO YA UMEANGUKA KWENYE UZINZI??? YOU HAVE FALLEN GOD, AU MUNGU AMEKUPAKA MAFUTA YA UIMBAJI π€πΉπΈ, UKIIMBA WEWE TUNAHISI MBINGU ZIMESHUKA, HALAFU GHAFLA TUNASIKIA, UMEVUNJA NDOA (DIVORCE), ULE UTUKUFU WOTE UNAKUWA UMEUBADILI, NA KUMWANGUSHA MUNGU.
*MOYO WA SOMO*
*_VIASHIRIA VYA UAMINIFU, KWENYE MAISHA YAKO BINAFSI/NA KWA MUNGU_*
πMUDA GANI WA USIRI UNAKAA NA BWANA (PRIVACY WITH GOD)
Mtu ambaye haishi kwa kuigiza, ambaye hana maisha ya kiroho ya maonesho (show-off), hatakuwa na bidii ya kuonekana kwa watu, kuzidi vile anavyo tamani kuonekana kwa Mungu (Zaburi 84:7). Je! Unazo nyakati za kukaa mbele za Bwana kwa kutafakari kwa utulivu, ili usikie mashauri yake kwako? Maana kama moyo wako umempa, ukikaa katika utulivu mbele zake, utamsikia kwa namna nyingi tu, anatoa comments zake kwako. Kwamba *_"Mwanangu, hili unalong'ang'ania sipendezwi nalo, fanya hili"_*. Sasa ukiona unapenda kuwa na nyakati nyingi za kuwa katika meditation/tafakari kwa Mungu, ili upate opinions za Mungu, ni dalili za wazi, WEWE NI MWAMINIFU KWA MUNGU.
*NB:*
The real you (wewe halisi), sio yule anayesimama madhabahuni π€, wala wewe halisi, sio yule wa kwenye grupu la wasap la wapendwa. Bali wewe halisi (The real you) ni wewe uwapo katika usiri (privacy). Ukiwa pekeako chumbani, usiku unafanya nini, unachati nini na watu wa jinsia zingine, yule ndio wewe halisi. Huyu mwingine wa Haleluya +Amen nyingi grupuni, umemuazima tu temporarily!!!!
π HAUTAFUTI NAFASI YA KUTENDA DHAMBI.
It sounds strangely, lakini hii ni hakika. Ukiisha kuokolewa, ukahamishwa na kuingizwa katika ufalme wa Mwana wa pendo la Mungu (Kolosai 1:13), unakuwa umetengwa na mazingira ya dhambi (kuitamani). Mtu anatafuta nafasi ya kutenda dhambi mweyewe.
Luka 22 : 6
*_Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano._*
Yaani Yuda pamoja na mazingira ya dhambi kuwa adimu, aliyasaka mwenyewe ili azitimize dhambi zake. Ndivyo kwako usiye mwaminifu, mazingira ya kuzini hayapo, nyumbani kwenu hata kuingia na binti haiwezekani, lakino unaamua kumtembelea binti alikopanga, unajua yuko peke yake, na ni usiku, eti alisahau kitabu chake cha tenzi au chajaππ ya smartfone, sasa gua ya kumpelekea ulivyo-set, ni kutafuta nafasi ya dhambi. Mtakaaje kachumba kamoja π¦πΎππΎππΎπ§π½, unafanya lile kosa la Mithali 7:21, you prolong a talk with a different sex folk. Mtaanguka bila shaka. Mtu mwaminifu, hatafuti nafasi ya kutenda dhambi.
π KUWEKA RATIBA ZA MAMBO YA KIROHO, BILA SHURTI NA UNAZISIMAMIA MWENYEWE.
Sahau kuhusu ratiba zenu za fellowship na kanisani. Mtu mwaminifu anajitahidi kujionesha kwa Mungu, hivyo mvali na ratiba za majority, ataweka ratiba yake ya kufunga/fasting. Kwa mfano jichunguze ukiona umeweka ratiba binafsi let say kuamka kuomba, unaset alarm clock⏰, na uko strick na hiyo ratiba, ni wazi wewe hufanyi show-off, uko serious na mwaminifu. Sipendi kuhubiri mambo nisiyoyatenda (Rumi 2:21ff). Kwa mfano katika rekodi zangu, ndani ya hii miezi miwili, sijawahi kulala usiku na kuamka asubuhi, bila kuamka saa nane usiku kuomba isipokuwa siku 1 tu ambayo nilisafiri Dar-Bukoba, nilizidiwa sana, niliamka muda ule wa kuomba nikajiruhusu mwenyewe kupumzika. Unaweza kuona, hiyo sio ratiba ya mchungaji, niko strict na hiyo ratiba, nikiamka nimezidisha nusu saa, naugua naumia sana sana. Nini kinanisukuma bila kukosa, saa nane za usiku kupiga kelele ceaselessly, sio kwa wiki moja, huo ni msisimko tu, na sio nguvu kamili; UAMINIFU.
π JE! MATOLEO UNAYOTOA KWA SIRI KAPUNI NA PAHALA PENGINE, YANASHABIHIANA NA YALE UNAYOTOA UKIWA KWENYE KIPAZA SAUTIπ€ AU TV πΊ???
Huu ni uhuni wa namna yake. Yaani ile sadaka ya kapuni, umetupia buku 1,000/=, Lakini walipowaita mbele mtaje, mtatoa nini kwa ajili ya Gospel outreach, ukashika kipaza sauti, na kusema unatoa Cash TZS/= Laki tano. Usanii huu ni mtamu sana, kazi itasonga mbele, ila yule Mungu aonaye sirini atakuobserve tuπ€, wala hataku-qualify kwa utumishi wake (1Tim 1:12)
πJE! WATU WANAKUAMINI KWA VITU VYAO?
Uaminifu kwa Mungu, unaathiriwa pia, na hali yako ya uaminifu kwa watu. Je huwa ukiazima vitu vya watu, unarudisha kwa wakati? Ukikopa unalipa? (Biblia inasema, asiye haki hukopa wala halipi/Hana nia ya kulipa). Je unarudisha kikiwa kizima au kibovu, kama umeharibu wachukua hatua zipi, au unakausha, ili waaijue kilijaribikia wapi? Je watu wanaweza kukuamini kukupa pesa zao utunze? Ukishika pesa za huduma haujikopi (na ukishindwa ku-refund unamezea)? , Tunasoma habari za waaminifu, walikuwa wakipewa pesa, hakuhitajika internal auditor kutoka kamati ya PAC, aje acheki matumizi, unawajua??
2 Wafalme 22 : 7 *_Lakini hawakuulizwa habari za ile fedha waliyokabidhiwa; maana walitenda kazi kwa uaminifu._*
π KWA HABARI YA MAHUSIANO πππ
Je! Weww mwenye ndoa, bado unatumiana meseji za mapenzi na outsiders? Yaani una mme au mke. Ila bado kuna mahali upo bize kutext your so cuteπππππ, i love you, unanimaliza, nakuwazagaπ, unafanya na unafiki hadi wa kuhonga kiMPESA π·πΆπ°, huku unajua umetoka kumjibu mkeo kuwa kuna vitu havijakaa sawa ofisini, hivyo huna hela ya saluni. Ukifanya haya, hata kama unaendelea na huduma, wewe msanii bro!
Kijana wa kike au wa kiume, kama unadiriki kufanya *_Multi-Bonding_*, yaani kuna wadada wawili au zaidi, wote umewapa ahadi ya kuwaoa, au umesema unawapenda, mdada ume-YESππ wakaka wawili au zaidi, utatuficha sisi, But Yesu anajua moyo wako, hauko mwaminifu kwake, hutapata faida yoyote. Hukatazwi kupenda hata mara laki. Lakini ukiona unaweza kumtamkia mdada *NAKUPENDA*, ikiwa kuna mwingine umemtumainisha penzi hilohilo, wala hamku-break up ile bond ya agano la maneno, Wewe nawe msanii/muigizaji.
YESU AKUPONYE KAMA UNA HAJA YA KUPONYWA, NIMETUA MZIGO NILIOTWIKWA USIKU
Mwl Proo
0762879363
All Truth Whatsapp Group
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment