Monday, November 27, 2017

AYAITAYE MAJI YA BAHARI

*AYAITAYE MAJI YA BAHARI*

*_Na Mwl Proo_*

Pokeeni salamu zangu kwa jina la Yesu.
Kwa kadri ninavyoendelea kujifunza maandiko matakatifu ya Biblia, nakosa sababu ya kuishi maisha ya kawaida. Ninapousoma ukuu wa Mungu huyu aitwaye BWANA (Yesu), naanza kupata uvivu wa kujishughulisha na vitu visivyo na impacts kubwa (sizungumzii kujishughuliza na mambo manyonge ile ya Warumi). Lakini nasikia mwasho rohoni (nawashwa), kwamba huyu Mungu wangu, kwa uweza wake huu na nguvu za kutenda, sipaswi kukaa na maisha yasiyomdhihirisha huyu Mungu mkuu. Na ndio maana nimejiset tayari,  kuona kazi kubwa za Mungu. Kabla sijajua kuwa nina karama ya kuponya au la (Ingawa nimeshuhudia kwa mikono yangu uponyaji mkuu kwa watu), kabla sijajua kama nina karama ya miujiza au la (ingawa nimeishuhudia miujiza siku zote katika maisha ya utumishi wangu), lakini ndani yangu, sikubali kuwa na maisha, yasiyo-mdhihirisha huyu Mungu mkuu. Na ndio maana ndani yangu najihoji, ni nini kitanizuia kufufua mfu itakapobidi, bado niko darasani, Roho wa kweli, ananifundisha elimu hiyo ya kufufua, darasa likikamilika nitaanza kazi. (Siwazi kwamba ni jambo gumu, au la kushangaza, sema tu mifumo ya kidini, tuliyorithishwa hata huku kwenye ulokole, ilitusetia ndani yetu vitu tofauti na kweli ya Mungu).

NAOMBA TUANZE KUPITIA MAANDIKO KADHAA, YATUTIE WIVU WA MUNGU (Zab 69:9).

Amosi 5 : 8
_*mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza kwa usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; Bwana, ndilo jina lake;*_

Amosi 9 : 6
*_Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; Bwana ndilo jina lake._*

DAAAH!! KAMA WATU WA MUNGU LEO, TUNGEUJUA UWEZO KAMILI WA MUNGU ULIVYO, KAMA ALIVYOJIFUNUA KWA UNABII WA MAANDIKO NA ANAVYOJIFUNUA NDANI YETU, MAMBO HAYANGEKUWA HIVI YALIVYO SASA. MUNGU NI MWENYE UWEZO KATIKA, AKILI ZAKE HAZITAFUTIKANIKI  *_(UNFATHOMABLE GOD)_*. UNAPOSOMA MAANDIKO YA KINABII, HAKIKISHA UNAUNASA UFUNUO UPI ALIUPATA NABII HUYO, KUHUSU MUNGU.

KATIKA MAANDIKO YANGU YA MSINGI (AMOS 5:8, 9:6) YANATAJWA MAMBO YA AJABU SANA. NA NIKUOMBE MSOMAJI WANGU, KWA WAKATI WAKO, SOMA KWA MARA MOJA SURA NNE ZA KITABU CHA AYUBU (SURA YA 38,39,40 NA 41). SURA HIZO NI BWANA ANAONGEA. KITHIOLOJIA ZINAITWA *_TOUR ON NATURE_*, MUNGU ALIPOONA MIJADALA MINGI YA AYUBU NA AKINA ELIFAZI MTEMANI, AKINA SOFARI NA ELIHU, AKAGUNDUA WANAYATIA GIZA MASHAURI KWA MANENO YASIYO NA MAARIFA (Ayubu 38:2), AKAAMUA KUMWINGIZA AYUBU DARASANI, KAMA HIVI LEO TUNAINGIA CLASS.

KILICHOTOKEA WAKATI WA UUMBAJI WA MWANZO 1, MUNGU ALIYAITA MAJI, LAKINI KILICHOTOKEA PALE BAHARI YA SHAMU (SEA OF REEDS), MAJI YALIMUONA TU MUNGU👁👁,  YAKOGOPA, YAKAACHIA NJIA WATU WA MUNGU WAPITE.

Zaburi 77 : 16
*_Ee Mungu, yale maji yalikuona, Yale maji yalikuona, yakaogopa. Vilindi vya maji navyo vikatetemeka,_*

KUNA MAMBO YANAFANIKIWA KUKUKINGA USIPITE KAMA UPO MWENYEWE, BILA MUNGU. LAKINI VITU VILIVYO HAI MA VISIVYO HAI, VINAVYOONEKANA NA VISIVYOONEKANA VYOTE VINAJISALIMISHA KWA MUNGU MKUU.

Habakuki 3 : 10 *_Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake._*

🏔⛰🗻🌊👈🏾VITU VISIVYO HAI, HAVIWI KWAZO KWA MUNGU, WALA HAVIPASWI KUWA KWAZO KWA WATU WAKE. YESU ANAITWA BWANA WA ASILI YOTE (MASTER OF NATURE).ALIPOUAGIZA UPEPO/DHORUBA ITULIE ⛵, ALIDHIHIRISHA HILO.

*MOYO WA SOMO*
Shetani anajitihada kubwa, za kutupumbaza tusiyaone tuliyokirimiwa. Unakuta watu wa Mungu, wamekabwa koo na masumbufu ya dunia hii kiasi cha kutopata nafasi ya kuutafakari ukuu wa Mungu na kumtafuta Yeye, aliyefanya Kilimia na Orioni. Watu wako bize kusaka ugali🍚🍲tuu kwa kanuni za dunia.

Kwa nini Nabii Amosi,  katika kuuleza ukuu wa Mungu, ametumia ajabu ya uumbaji?. Kuna mambo ambayo katika ulimwengu (universe) ambayo si ya kawaida. Leo naanza kukueleza hili la Kilimia na Orioni. Huu ni mfumo wa muunganiko wa nyota (Constellation/Galaxy), ambazo unakuta zinatoa umbile la uumbaji fulani. Hii iitwayo Kilimia (Pleiades-nyota saba) ni mkusanyiko wa nyota unaounda umbile la ng'ombe dume (bull 🐂) kwa muonekano. Ugiriki ya kale, walipoona kitu hiki angani, wakakiita ni mungu mwenza wa mungu wao Artemi, maana ni ajabu hakika.  Soma hapa

Ayubu 9 : 9
*_Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hicho Kilimia, Na makundi ya nyota ya kusini._*

HIZI ZINAZOTAJWA KAMA NYOTA ZA DUBU, NI ZILE AMBAZO KITAALAMU HUITWA  ARCTURUS. IKUMBUKWE KILIMIA KWA UKUBWA INAKARIBIA KULIZIDI JUA KWA UKUBWA, ☀KWA ZAIDI YA MARA 2,200,000,000,000,000,000 (Kwintilioni 2 na kwadrilioni mia mbili).
SASA HUYU NDIYE MUNGU, AMBAYE AMOSI NABII ANATUAMBIA MTAFUTENI YEYE AFANYAYE KILIMIA NA ORIONI. MUNGU NI MKUU, MKUU, MKUU MNO. NA AMETAMANI SISI TUWE SEHEMU YA UUMBAJI, UTAKAOENDELEZA UKUU HUO, ILI ATUKUZWE KATI YA MATAIFA (ZABURI 48:10).

KUMBUKA MUNGU AYAITAYE MAJI YA BAHARI, ALITUMIA UWEZA WAKE KWA KUSEMA TU, IKAWA!. NI KWA NAMNA HIYO HIYO, AMETUWEKEA SISI KUSEMA TU, NA AJABU KUBWA ZITOKEE (MITHALI 18:20,6:2). ANASEMA KATIKA ISAYA 57:19, ANAYAUMBA MATUNDA YA MDOMO. MIONGONI MWA VITU VINAMFANYA MUNGU AUONDOE ULE UWEZO WA VINYWA VYETU, NI KWA SABABU YA KUONGEA MANENO MENGI YASIYO NA MAANA (MATHATO 12:36, MITHALI 10:19), WATU WA MUNGU HAWANA FILTERS 🔍🔎. KILA USEMI WA DUNIA NAO WAPO, MENGINE MAFUNUO YA KUZIMU, NA WANASOMBA TU. NILIMSIKIA MTUMISHI MMOJA AKISEMA *_MOYO MASHINE_*, NIKAUPENDA HUO MSEMO, NIKIJUA NI UFUNUO KUTOKANA NA YEREMIA 17:9, NIKIWA KATIKA BASI NASAFIRI, WAKAWEKA MUZIKI WA DUNIA 📺, NDIPO NIKASIKIA NA KUONA HUO MSEMO ALIPOUTOA. SASA SITAKI UTETEZI WOWOTE, KAMA NAYE ANAPATA MAFUNUO KWENYE BONGO FLEVA OF WHICH 100% NI KAZI YA KUZIMU, NALIJUA MPAKA JINI 👹, LILILOPEWA JUKUMU NA SHETANI, KUWAVUTA WATU KWENYE MIZIKI HIYO, SASA LINI TUTAPATA UWEZO WA KINYWA, KAMA MUNGU, YULE MWENYE KUYAITA MAJI YA BAHARI????  KUNA MAMBO AMBAYO MUNGU ANATUTAZAMIA TUYATAWALE PAMOJA NAYE, TUTOE AMRI, MISIMAMO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO KAMA WALINZI, WATAWALA PAMOJA NAYE

Daniel 4 : 17
*_Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge._*

NITAKUJA KUENDELEA, MAANA HUYU MUNGU WA BIBLIA, KAMA NDIYE TUNAYEMWABUDU, BASI HATUPASWI KUWA NA SURA ZA UNYONGE TULIZONAZO. HAJABADILIKA, YEYE ALIYEKO, ALIYEKO NA ATAKAYE KUJA, BWANA WA MAJESHI NDILO JINA LAKE!!!!

Mwl Proo
0762879363
All Truth Group

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment