Saturday, November 25, 2017

YAANGALIE HAYA WEWE MWENYEWE!

*YAANGALIE HAYA WEWE MWENYEWE!*

Na Mwl Proo
0762879363
Mjumbe wa Matengenezo

Haleluya watu wa Mungu!!

Baada ya kutafiti na tafakari ya muda mrefu, juu ya maisha ya wanadamu! Nimeliona hili tu;
*_"KUWA NA MUNGU, NDILO JAMBO LA PEKEE TUNALIHITAJI KABLA/KULIKO CHOCHOTE"_*

Wanadamu hawana neno jema na wewe, ila Mungu. Wanaokushabikia utende dhambi, wanaokupamba kwa uovu, wanaokushawishi kwa mazuri ya dunia, wanaokutaka u-compromize na ulimwengu, kwamba fanya tu jambo hili utatubu, kwani mwenye dhambi ni peke yako?, wanaotaka kutumia shida zako utoke kwa Mungu; _*HAO NDIO WATAKUWA WA KWANZA KUKUSUTA, NA WALA HUTAWAONA WALIPOTELEA WAPI,  UTAKAPOACHWA NA MUNGU*_.

Ujumbe wetu, una kichwa chenye sentensi ya kusuta  *_(MSUTO👌🏽👌🏽)_*, Wale wale, waliomtia ushawishi Yuda Iskariote, awafanyie dili la kumsaliti Yesu, yaani mtu ambaye alikuwa na standards za kuwa mtume akaharibiwa future yake kwa vipande 30 vya fedha (Shilingi 90 za kitanzania, haitoshi hata Andazi moja). Wakiwa wamemharibia, naye huenda alihisi Yesu angetumia uwezo wake kutoroka. Sasa alipogundua hadi hukumu imesomwa wala Yesu hajatoroka kimuujiza. Akawafuata wale waliomharibia future ya kitume. Akawarudishia pesa, na kulialia mbele zao, kuwa mlinishawishi vibaya 😫😫. Walichomjibu ni msuto wa hatari

Mathayo 27 : 4 *_Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi (YAANI INATUHUSU NINI SISI)? Yaangalie haya wewe mwenyewe(MAANA YAKE UTAJIJU NA TAMAA YAKO MWENYEWE👌🏽👌🏽)._*

Hivyo ndivyo wale mashoga zako mnaoenda kusukana, huku wanakushawishi, huwezi kukaa na mwanaume mmoja tuu, lazima nje uwe naye mwingine wa kukuhudumia matumizi nawe unamlipa tendo la ngono. Siku ndoa ikiharibika, watakuletea misuto classics😛😛👌🏽👌🏽👌🏽. Hapo ndipo utakapojua kupambanua kati ya yaliyo matakatifu na ya siku zote (Lawi 10:10).

*MUNGU ALITUTOA KATIKA HALI MBAYA, TULIPOOKOKA (TUSISAHAU HILO)*

EZEKIEL 16:4-14
🔴Alitukuta wachafu, hatuna msaada, wala hakuna aliyetuhurumia.

_*4 Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa.*_
_*5 Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile uliyozaliwa.*_

🔴Katika hiyo hali mbaya, ni Mungu pekee alitupenda, akatuhurumia. Akaiondoa hali ya ufu, iliotokana na dhambi, akatuhuisha, akatuongeza katika kila nyanja. Zaidi sana alitufichia ile aibu ya dhambi zetu za kwanza

_*6 Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai.*_
_*7 Nalikufanya kuwa maelfu-elfu, kama mimea ya mashamba, ukaongezeka, na kuzidi kuwa mkubwa, ukapata kuwa na uzuri mno; matiti yako yakaumbwa, nywele zako zikawa zimeota; lakini ulikuwa uchi, huna nguo*_
_*8 Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nalikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.*_

🔴Na baadaye akatutakasa, akatufunika kwa utukufu wake, mataifa wote wanatutamania, ameyapamba maisha yetu kwa kila uzuri, ndivyo tulivyo leo.

*_9 Kisha nikakuosha kwa maji; naam, nalikuosha kabisa damu yako, nikakupaka mafuta;_*
*_10 nikakuvika nguo ya taraza, nikakupa viatu vya ngozi ya pomboo, nikakufunga nguo ya kitani safi kiunoni mwako, nikakufunika kwa hariri._*
*_11 Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako._*
*_12 Nikatia hazama puani mwako, na pete masikioni mwako, na taji nzuri juu ya kichwa chako._*
*_13 Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikilia hali ya kifalme._*

SASA NENO ALILONIPA BWANA KWAKO NI HILI; USIYAHARIBU MAISHA YAKO, MAANA AMEKUTENGENEZA KWA GHARAMA (1KOR 6:20). USIJIANGALIE MWILINI, KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, UNAPENDEZA SANA, PAMOJA NA KWAMBA HUKU NJE UMEZOEA KUDUNGUA MITUMBA YA MANZESE 👗👕👚👘, KATIKA ULIMWENGU WA ROHO UMEVIKWA VITU VYA UKWELI AMBAVYO HATA FIRST LADY WA MAREKANI HAWEZI MUDU KUVINUNUA, ULIVIKWA NA MUNGU ULIPOOKOKA.

Kuna watu wanataka kujisahaulisha walipotoka. Wewe mdada ambaye leo unashika maikrofoni🎤 kutuabudisha kwa nyimbo, umesahau kuwa ni wewe ulikuwa unapanga foleni, pembeni mwa barabara ya Sinza, ukijiuza kwa ukahaba? Tena hata kingereza hamkukijua, ila mlitumia cha kuungaunga *_"take me, me good"_*. Yesu ameifuta historia yako ya ukahaba leo ni *PRAISE LEADER*. Wewe mwanaume ambaye ulikuwa unatoka Bar ukiwa chakari (full tungi ) 🍺🍻😞, unaokotwa mtaroni. Leo Yesu kakufanya eti ndio mzee kiongozi wa kanisa lake takatifu. Kumbuka kule ulipotoka, na alipokuweka Yesu sasa. Umeyapata yote huku kwa Yesu pamoja na heshima kubwa.

Usithubutu kuyaharibu maisha, ambayo kwa gharama kubwa ulitengenezwa. Ukiyaonja haya mazuri ya Mungu, ukajiangusha tena, kulipiwa tena ile gharama ya kwanza mmmh sijui (IT IS NOT GUARANTEED; Ebrania 6:4-6, 10:26).
USIFANYE MAMBO  YANAYO HARIBU MAISHA AMBAYO MUNGU AMEYAFANYA YAPENDEZE *_COLOURFUL_*
1.USITHUBUTU KUFANYA TENDO LA NDOA, NAWE HAUPO KWENYE NDOA, PENALTY ITAKUKUTA TU
2.USITHUBUTU KUTOA MIMBA, KAMA ULIANGUKA TUBU,VUMILIA UZAE TU ULEE KA-BABY👶🏾
3.USITHUBUTU KUTEMBEA NA MUME WA MTU UKAIHARIBU NDOA YA MTU (UKIHARIBU LAZIMA UHARIBIWE isaya 33:1) USISEME MME WAKE NDIYE ALINISHAWISHI.
4.USIKUBALI USHAWISHI, WA WATU KUIIBIA KAMPUNI (Mith 1:10)
5.USIKUBALI KUOLEWA NA MTU AMBAYE SI IMANI MOJA NAWE (KWA  MAANA YA efeso 4:4-5), SIZUNGUMZII DHEHEBU, MBAYA ZAIDI IMANI ISIYO YA YESU (ETI UNAONA KUKAWIA UKAPATA TAJIRI WA KIISLAMU, UKAJILIPUA 💣KWA KUOLEWA HUKO
6.USIVUNJE UAMINIFU WA NDOA, HATA KAMA MUME AU MKE YUPO MASOMONI ULAYA MUDA MREFU.
7.USIKUBALI KUWA NA MARAFIKI WA NAMNA YA YONADABU, ALIPOKWISHA MSHAWISHI AMNONI AMBAKE DADA YAKE KWA NGUVU, HATUJUI HATA ALITOROKEA WAPI MUDA MAMBO YAMEHARIBIKA.

NA MENGINE YOTE YANAYOHARIBU MAISHA _*YOU, NAME THEM!!*_ ILA KUMBUKA UKIWAJULISHA WALE WALIOKUSHAWISHI, WATAKUJIBU KWA MSUTO KAMA KICHWA CHA UJUMBE HUU. PIA KUMBUKA HALI YAKO YA MWISHO ITAKUWA MBAYA, KULIKO ILE AMBAYO MUNGU ALIKUKUTA NAYO, UTUKUFU UTAGEUZWA TENA KUWA AIBU. (Math 12:43ff, Hosea 4:7)

Nimemaliza alichoniwekea Bwana, moyoni.

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment