Sunday, November 26, 2017

ALAMA YA MPAKA

*USIIONDOE ALAMA YA MPAKA*

πŸ‡² πŸ‡Ό πŸ‡±  πŸ‡΅ πŸ‡· πŸ‡΄ πŸ‡΄
*0762879363*

BWANA YESU KRISTO ASIFIWE!.
Mungu akubariki wewe ambaye hata hujachoka kujifunza. Unaliruhusu Neno la Mungu, likuchonge mpaka ufananie shepu anayotaka Bwana. Pokea Thawabu kamili kwa Bwana, kwa moyo huo (Ruth 2:12), Aliyeko hatarini ni yule aliyekomaa hadi akakoma.

*UTANGULIZI*
Wakati wa hukumu, hakuna ambaye hatahukumiwa kwa haki, maana kila mtu atajishuhudia mwenyewe kwa wazi, kwamba alikuwa anajua kwamba ipo haki ya Mungu, ila siifuati. Biblia inauliza, "Je wafanyao maovu hawajui?" (Zab 53:4). Wiki iliyopita nikiwa ofisini, mfanyakazi mwenzangu akaniambia,  *"Niwekee nyimbo za dini kama 12 hivi, kwenye simu yangu πŸ“±, ili ikiita watu waniheshimu, wasijue kuwa mimi ni mmataifa (gentile/asiyeamini)".* Unaisikia hii? Kumbe haki ya Mungu inajulikana kwake vyema, anajua kabisa kuna wamataifa na wana wa Mungu, ila hajachagua hili fungu jema (Luka 10:42), Pia kumbuka kuwa kwa maneno ya kinywa cha mtu atahukumiwa (Math 12:37, Mith 6:2). Ndugu mpendwa ukipata neema ya kujua haki hii ya Mungu, simama nayo (Yakobo 4:17), usiishi kwa mithali za kiafrika wala misemo ya wahenga. Eti kifo cha wengi ni sherehe, Jehanamu mkiwa wengi sana haikufanyi kuwe club au beach🏊🏽, *_Serious business needs serious people_*

BWANA AMEWEKA UJUMBE HUU MOYONI MWANGU, KUSEMA; "USIIONDOE ALAMA YA MPAKA". (Kumb 19:14, Mithali 23:10)

Mithali 22 : 28 *_Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako._*

Muktadha wa andiko hilo, lilikuwa ni maagizo ya Mungu anayependezwa na haki, akiwaonya watu waku, kutoondoa alama, ambazo ziliweza kuwa mawe au kitu kingine, ambacho kiliwekwa katika urithi wa ardhi na mali zingine, ziliwekwa na mababa wa zamani. Wengi baada ya muda, walikuwa wanashawishika kusogeza yale mawe, hasa kama wamiliki ni watu dhaifu au wanaishi mbali. Sasa watu wa ardhi, wanajua jinsi mambo ya mipaka yanavyo-matter. Tena hata ukipiga hatua moja tu kuingia kwenye mpaka wa mtu sio iahu ndogo hiyo.

MUNGU AMENIJULISHA KUWA SISI TULIOFANYWA WATU WAKE, BAADA YA KUOKOLEWA, TUMEWEKEWA ALAMA ZA MPAKA, AMBAZO HATUPASWI KUZIONDOA KWA SABABU YOYOTE. HAKUNA ALIYEOKOKA ANAYEPASWA KUYAISHI MAISHA YAKE MWENYEWE, BALI MAISHA/UZIMA ALIONAO KATIKA MWILI WAKE NI KWA AJILI YA KRISTO (GAL 2:20), NA KWA SABABU HIYO SASA, HUWEZI KUKOSA MIPAKA, YAANI WEWE UKAFANYA KILA KITU, UKAENDA KILA MAHALI, UKASHIRIKIANA NA KILA MTU, UKAOA YEYOTE, UKANYWA KINYWAJI CHOCHOTE, UKAONGEA MANENO YOYOTE. HAPANA, ZIKO ALAMA ZA MPAKA! NA KILA ALIYEJAZWA ROHO MTAKATIFU, KILA ANAPOTAKA KUVUKA MPAKA AU KUONDOA ALAMA YA MPAKA, TAA NYEKUNDU ITAWAKA NA KUPIGA ALARM 🚦πŸš₯🚨. NI MTU MWENYE KIBURI TU, NDIYE HASIKII ALARM, ANAENDELEA MBELE NA KUANGAMIA (Mithali 22:3).

KUNA MAENEO MTU WA MUNGU HUPASWI KWENDA. MAANA UKIENDA UNAJUA WAZI UME-RISK, KIROHO CHAKO, NA BWANA ALINIFUNDISHA ZAMANI, KUWA USIENDE MAHALI AMBAKO UNAJUA UTATENDA DHAMBI (AMOSI 4:4,5:5). Andiko hili linasema njoni Bethel mkakose, njooni Gilgali mkaongeze makosa. Sasa mstari huo mwingine, Mungu anaonya usiende huko, ambako una hakika utakosa. Uliyeokoka ukienda kuattend FIESTA, na umelipa kiingilio elfu 20, kiu yako ni kuona tu wasanii wa Bongo fleva laivu, Mambo utakayoyaona huko, yatakutia wazimu (Kumb 28:34, Zab 119:37), Kama Bwana amekutuma kuhubiri huko kama Bonnke, nenda!, kama hajakutuma usithubutu, maana ukienda huko ni majaribio ya kutupa lulu kwa nguruwe πŸ’ŽπŸ’ŽπŸ’ŽπŸ–πŸ–πŸ–.

Baba mwenye nyumba unamruhusu binti wa kusaidia kazi (House girl), kuingia master bedroom, na upo mwenyewe tu... Unaondoa alama ya mpaka, utakapoziwa na mwili wako ambao kwa kuwa huzingatii standards/qualities za kiroho, mwili wako una nguvu kuliko roho, lazima utaenda na maji 🌊. And its vice versa is true, kwako mama, houseboy unamruhusu mpaka chumbani mwako hali unajua kabisa, unaondoa alama ya mpaka?

Mnaweza kuwa mpo kwenye steji ya mwisho kabisa ya uchumba, ili kuingia kwenye ndoa πŸ’πŸ’πŸ’. Katika hali hiyo bado kuna alama ya mpaka, Msiiondoe. Nguvu zenu ni chache (Mithali 24:10) halafu mnafanya outing maeneo+mida yenye utata, wengine wanathubutu kulala gheto moja, eti wewe lala kitandani πŸ›Œ, mimi nalala kwenye kochi (MNAONDOA ALAMA YA MPAKA), mkianguka mnasingizia Shetani alijiinua πŸ‘‰πŸΎπŸ‘Ή. Yesu anasema alimwona akianguka (Luka 10:17, Rumi 16:20), hakuwa kumwona akiinuka tena, kama sivyo angelituambia, sasa ninyi mmejipa huduma ya kumwinua aliyeanguka, poleni sana πŸ‘ŒπŸ½.

NYAKATI HIZI, WALOKOLE NA WRNGINE WANAOUKIRI WOKOVU, WAMEVURUGA PICHA YOTE, MPAKA HATUELEWI HIVI, WALIPOKEAJE HAWA WATU, ALAMA ZA MPAKA ZIMEONDOLEWA KILA KONA. KUNA MAENEO YA MWILI HAYAPASWI KUWA PUBLIC KAMWE, HIYO SIO KWA MAADILI YA KIROHO, BALI SOCIAL ETHICS. LAKINI NJOO KANISANI NDIPO UTAKAPOJUA SASAπŸ€”. WANAWAKE WAMEKOPI TU KUYAPIGA JEKI MATITI NA KUTUONESHA WATU WOTE IBADANI. WANAJUA MAPAJA SIO SEHEMU ZA KUONESHA WATU, LAKINI KWA KUSUDI KABISA WANANUNUA NA KUSHONA NGUO ZA HIVYO, NA WENGINE WALE _*#TEAM-SELFIEπŸ“±πŸ“Έ#*_, SASA WALLS/TIMELINES ZAO ZA FACEBOOK UTAFIKIRI NI WEBSITES ZA PORNOGRAFIA, MAANA NI SHIDA TUPU. BWANA ANASEMA NA WEWE MWANAMKE KUWA WEWE ALIKUUMBA MZURI TAYARI, WALA HAIHITAJI UONESHE MATITI NA MAPAJA ILI KUFANYA THAMANI YAKO YA UZURI IJULIKANE, USIIONDOE ALAMA YA MPAKA, MAENEO MENGINE ANAPASWA KUYAONA MMEO AISEEπŸ˜•. NA NYAKATI HIZI NI RAHISI TU, KUMPIMA KIMEO-KIND OF WOMANI, UNACHEKI PROFILE YAKE TU, UKIONA FACEBOOK KAONESHA MAUNGO YAKE YA SIRI, MAANA YAKE MIZANI YAKE IMEKUFA (MITH 31:6), HATA KABLA HUJAANZA KUMMULIKA KWA DARUBINI YA ROHOπŸ”­πŸ”¬, UNAM-DISQUALIFY. KUNA WAKATI NILIUNGWA GRUPU LA WASAP AMBALO KILA MTU ANATUMA VIDEO YA NGONO ALIYONAYO, NILIOONA MOJA TU, NIKAJIANDAA USIKU, NIKAANDIKA MAHUBIRI MAKALI SANA YENYE KUUNGUZAπŸ”₯πŸ”₯,ALFAJIRI NIKAYATUMA KWA HILO GRUPU NA KULEAVE(LEFT). MAANA NINAZO ALAMA ZA MPAKA , SIWEZI TAZAMA VIDEO ZA NGONO, WEWE AMBAYE WAMEKUADD, UMEKAA HUMO UMEUCHUNA, HAUTAKUWA SALAMA. TULIOOKOKA HATUSIKILIZI SECULAR MUSIC, UKINUNUA CDπŸ“€ YA DIAMOND PLATINUM, UMEONDOA ALAMA YA MPAKA, WALIOOKOKA HAWAOI WALA KUOLEWA NA WASIOAMINI, UKIFANYA VINGINEVYO, UMEONDOA ALAMA YA MPAKA. TULIOOKOKA HATUNA MABOY-FRIENDS NA MAGIRL-FRIENDS, MNAENDELEA ZENU TU, NA KILA MKIHISI KULITAMANI LILE TENDO LA KIRUMI, MNAENDELEA ZENU 😞,MMEONDOA ALAMA YA MAPAKA.

*KUMCHA BWANA NI KUCHUKIA UOVU, USIIONDOE ALAMA YA MPAKA, ASEMA BWANA, AMBAYE JINA LAKE NI MTAKATIFU!*

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment