Wednesday, November 29, 2017

KAA NASI!

*KAA NASI*

_*Mwl Proo*_
_*0762879363*_

Nawasalimu tena, kupitia jina la Yesu aliye Kristo na Bwana!.
Nasikia uvuvio wa kimungu sasa, maana kuna watu Mungu anakwenda kuwasaidia. Naomba nitoe tangazo nililolipata usiku wa kuamkia leo. _*MAANGUKO NI MATOKEO YA KUACHA KUKAA NA YESU*_, Nilipoamshwa saa 02:05am (usiku) kwa ajili ya kuomba, ile nainuka nikasikia tamko hilo, linaongea moyoni, akilini mwangu kama mtu anatangaza ๐Ÿ“ข. Sasa uliyewahi kuanguka na ambaye hujawahi kuwa na maanguko *(hapa nazungumza kuanguka dhambini, kushindwa kumaintain standards za wokovu, na yale yote ambayo wewe mwenyewe ukiyakumbuka unajua mmmmmh!๐Ÿ˜จkatika hili na lile, kwa kweli nilishindwa kusimama na Yesu/nilimweka pembeni, na kushindwa kuilinda imani).* Sasa neno la Bwana kwetu liko wazi, kwamba maanguko ni matokeo ya kuacha kukaa na Yesu. Yesu ni *MCHUNGAJI MWEMA (Yohana 10:1-16)*, asiyeweza kuacha kondoo zake zishambuliwe na kuondolewa kundini, hilo linafanikiwa kondoo akijicholopoa kundini (Akiacha kukaa na Yesu). Mpendwa msomaji, ukiamua kukaa peke yako dakika mbili katika utulivu, kujihoji, hivi mimi nipo na Yesu Kristo, unapata jibu moja kwa moja. Mwingine ambaye njia zake tayari zimeingia virusi, akijitafakari, ana-conclude mwenyewe, *_"Mmmh! Kwa kweli Mungu mwenyewe anisaidie tuu"_*.

Kama uliangukaga kwenye matendo ya uzinzi, it was never an accident, uliacha kukaa na Yesu moyoni, lakini ukaendelea kuivumilia hiyo hali ndio anguko likaja. Yuda hakumkana Yesu kwa dharura, ukisoma injili zote nne, tayari alikuwa ni mpinzani wa Yesu, pamoja na Yesu kumpendelea cheo cha kuwa Chief Accountant. Tunaambiwa alikuwa akichakachua pesa za Bwana mkubwa. Yesu kapakwa mafuta ya manukato, jamaa anasajesti kwa upinzani, kwamba why this waste๐Ÿ˜, yangeuzwa yanathamani ya mshahara wa miezi nane, tungesaidia maskini. Sasa tayari moyoni mwaka hakuwa upande wa Yesu, Shetani ikawa mtelezo tu kupata msaliti. Ndivyo kunavyokuwa na mtelezo kwako kuangushwa dhambini.
Ukikaa na Yesu wewe utajua, na wanaokuzunguka watajua. Tena usiombe mpagani ambaye alikuwa anakutamania ulivyo na Yesu, aka-note kwamba haukai na Yesu tena, akaja kukwambia mbona mtumishi siku hizi haupo kama zamani?. Utajitutumua kumvunga kwamba upo sawa tu, huku ukijaribu kumjulisha na jitihada zako za nje ya kundi, *_tena kwa taarifa yako hapa nimefunga!_*, Kumbe ni maombi/fasting ya 12hours ya kwaya, umefunga kwa sababu mwenyekiti wa kwaya alitishia sanaaaaaaa, usipofunga umevunja maagano ๐Ÿ˜ก!! Kwa hiyo ukasombwa bila hiari. *When you start doubting your faith in the LORD, that doubt is real/true*. Msomaji wangu, unaweza kuwa huna elimu ya kueleweka, lakini ukikaa na Yesu, utakuwa na kaharufu kazuri kuliko waridi๐ŸŒน, tutakutamania pamoja na hako kasetifiketi ka form four. Muulize Petro na Yohana๐Ÿ˜€

Matendo 4 : 13
_*Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.*_

Wasomi walipocheki, hawa watu *_No School_*, why are they so bright?๐Ÿค”Wakapata jibu, haaah hawa watu walikaa na Yesu miaka mitatu.

*MOYO WA SOMO*

HAKUNA KITU KITAMU AISEE KAMA KUKAA NA YESU. HAKUNA KITU KIZURI KAMA KUMWEKEA TUMAINI LOTE YESU, HAWEZI KUKUANGUSHA KAMWE. AKINA KLEOPA WALIZUNGUMZA NA YESU, WAKIWA BADO HAWAJAWA NA HAKIKA, LAKINI WALIKUWA WASHAHISI HUYU TULIYENAYE LEO ๐Ÿ‘๐Ÿฝ๐Ÿ‘๐Ÿฝ๐Ÿ‘๐Ÿฝ๐Ÿ‘๐Ÿฝ, WAKAMSHAWISHI YESU ASIONDOKE, MAANA YESU ALIJIFANYA KAMA ANATAKA AENDELEE NA SAFARI ILI AWAPIME..

Luka 24 : 29 *_Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao._*

AMBAO WAMESHAWAHI KUTEMBELEWA NA YESU AU WAKAPATA UTEMBELEO WOWOTE WA KIMUNGU (ANNUNCIATION-DIVINE VISITATION) KWA NAMNA YOYOTE, WATAKUWA MASHAHIDI WAZURI, JINSI AMBAVYO LAZIMA UTATIA MGOMO USIACHWE, YAANI UBAKI KATIKA HALI HIYO TAMU. UNGEWEZA KUWAULIZA PETRO, YOHANA NA YAKOBO SIKU ILE YESU ALIPOBADILIKA WANGEKUAMBIA. PETRO ALIKUWA NA MKE NA WATOTO NA MPAKA MAMA MKE YUKO HOME KWAKE (EXTENDED FAMILY). LAKINI AKASAHAU MAJUKUMU, ANAWAZA AJENGE VIBANDA MLIMANI. YESU NI MZURI BWANA!!! YESU PEKE YAKE NDIYE AMBAYE HAWEZI KUKUANGUSHA WALA KUKUVUNJA MOYO, BUT THE WORLD WILL ALWAYS DISAPPOINTS YOU๐Ÿ‘‰๐Ÿพ๐Ÿ˜”. UNAKAZI NZURI, IPO SIKU UNAKUTA BARUA KWA SEKRETARI, UMETUMBULIWA ๐Ÿ’‰. UNABIASHARA NZURI IPO SIKU UNAWEZA KUTA HITIRAFU YA UMEME IMETOKEA ENEO LA BIASHARA KILA KITU MAJIVU. UNAWEZA KUWA NA MTOTO BRIGHT KAKULETEA DIVISHENI NA G.P.A NZURI IPO SIKU UNAWEZA PEWA TAARIFA ZAKE KUWA NI MWATHIRIKA WA UKIMWI, AU YUKO ICU BAADA YA COMPLICATIONS KATIKA TUKIO LA ABORTION (KUSHUSHA INJINI), ALILOLIFANYA KWA SIRI. MOYO WAKO UTACHOMWA NA KUSHUKA CHINI. ONLY JESUS,  WON'T  DISAPPOINT KABISA, UKIKAA NAYE

*NI RAHA KUWA NA WAZAZI*
Hao nao usiwawekee tumaini, wanaweza kukuacha aiseee usiamini kwamba ni wao. Lakini hata hao wazazi wakisema tangu leo tafuta wazazi yuko Yesu atakukaribisha kwake.

Zaburi 27 : 10
_*Baba yangu na mama yangu wameniacha, Bali Bwana atanikaribisha kwake.*_

*NI VIZURI KUWA NA VIONGOZI WAWAJIBAKI KAMA RAISI WETU*
Huyo naye tusimwekee tumaini, ipo siku anaweza kugeuka fumba na kufungua, akafanya maamuzi kwa mamlaka yake, yatakayo kutia jereha za moyo hutaamini nakuambia, hapa kazi tu!

Zaburi 118 : 9
_*Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu.*_

Mika 7 : 5 _*Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari.*_

_*HIVI SI UNAYE SHOSTI WEWE, SI UNAYE MCHUMBA?*_

Huyo naye unaye mwamini, umempa moyo wako, siri zako zote unamwambia, mpaka meseji za siri unazochat na mchumba wako, naye unamwonesha eti, wait and see the disappointment that will follow toka kwa huyo shostiako, na mchumbaako,atakapotunga sauti ya Mungu feki, eti Bwana kaniotesha kuwa wewe sio mke wangu, nimekosa amani...Mungu wa hivi hayupogo ❌❌❌๐Ÿ™…๐Ÿฝ๐Ÿ™…๐Ÿฝ๐Ÿ™…๐Ÿฝ๐Ÿ™…๐Ÿฝ. Tena kwa wale waaminifu katika kumsikia Mungu, siku unapotia wazo la kumpenda huyo mtu,atawahi kutoa comments zake, ukiwa mgumu, siku utakayo mtamkia, ukiwa mgumu zaidi mwanzoni mwa uhusiano, ukiwa mgumu zaidi atatumia watu, lengo ni kwamba kabla hajayatia sana moyoni, msitishe, maana Mungu ametupa huduma ya kuganga mioyo sio kujeruhi. So hizo sauti na ndoto unazootesha mwenyewe, kumbe umeona panadoli (๐Ÿ‘ฉ๐Ÿป) mwingine hapo sio Mungu ni mungu tamaa yako. Lakini kwako uumizwaye ni bora ujue siri hii, tumaini lte liweke kwa Yesu tu, awezaye kukupa shoshti na mchumba ambaye hayuko tayari uumie moyo.

Zaburi 41 : 9
_*Msiri wangu (shosti) tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.*_

NB:-

*Hakuna mtu aliyeumizwa kwenye mahusiano, anayeweza kuoparet kwenye kiwango kizuri cha karama za rohoni au huduma kwa huduma, kama ni mwimbaji vurugana na mchumba au vunja ndoa, halafu katoe single track studio๐Ÿ’ฟ, kuanzia muda unaimba unagundua, mmmh!!!???...*

MAKE THIS YOUR PRAYER TODAY!! OOH LORD JESUS, STAY WITH ME, STAY WITH US. KAA NAMI BWANA, UKAE NASI, KAA NA FAMILIA YETU!! AMEN AND AMEN

God bless you all
*Mwl Proo (Prosper Kadewele)*
Mjumbe wa Matengenezo
0762879363(All Truth Whatsapp Group)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment