*ONDOKA LO-DEBARI*
*_(Get out of Lo Debar)_*
Na Mwl Proo
~_MjumbeWaMatengenezo_~
0762879363
BWANA YESU ASIFIWE!!
Mungu akiwaona wana wake, wanatanga mbali, hawamjii, anaona wivu maana anawatamani. (Yakobo 4:5)
Kulikuwa na kamji fulani katika nchi ya Gileadi, karibu na Mahanaimu kaskazini mwa Yaboki ulioitwa Lo-Debar. Maana ya jina la huu mji ni *Kukosa/Kutokuwa na...(not having)/Pasipo na malisho (No pasture)*, Watu walio sahaulika, wanyonge, masikini, wasio na future, wategemezi etc etc Wote walijazana huko. Watu wa huko kijamii, kisaikolojia hawakuwa sawa kabisa (Their souls were self-jailed).
KULIKUWA NA KIJANA AITWAYE MEFIBOSHETHI, MWANA WA YONATHANI (SWAHIBA WA DAUDI) MWANA WA SAULI, MWANA WA KISHI. HUYU KIJANA WAKATI BABA YAKE NA BABU YAKE SAULI WAKIWA VITANI, YULE YAYA (NESI) WAKE AKAMCHUKUA ILI AKIMBIE NA KWA USALAMA, KWA KUWA ALIONDOKA KWA MWENDOKASI MKUBWA BASI AKAMDONDOSHA, NA KUMTIA UWETE ♿ TANGU AKIWA NA MIAKA 5. KATIKA HALI HIYO AKAENDA KUHIFADHIWA NYUMBANI MWA MAKIRI HUKO LO-DEBARI. AKAENDELEA KUKUA NA SAIKOLOJIA YAKE IKAVIRUGWA, AKASAHAU KUWA UTOTO WAKE WOTE ALIUTUMIA IKULU, AKILA MASONTOJO 🍕🍗🍖🌮🍲🌭🍟🍦🍷🍹.
SASA NAFSINI MWAKE AKAWA ANAJIONA KAMA MBWA-MFU 🐕, LAKINI STAHILI YAKE KWA MFALME ILIKUWA NI NAFASI SAWA NA WALE PRINCES/PRINCESSES. MSIKIE ASEMAVYO MEFIBOSHETHI
2 Samweli 9 : 8 _*Akasujudu, akasema, Mimi mtumwa wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi?*_
MUNGU ALIMTUMIA DAUDI, KUMWONDOA MEFIBOSHETHI HUKO LO-DEBAR MAANA SIPO MAHALI PA RAHA YAKE (MIKA 2:10)
2 Samweli 9 : 5
*_Basi mfalme Daudi akatuma watu, akamwondoa katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari._*
Tunao watu leo hii, nafsi zao ziko Lo-Debar na sharti watoke huko, ili wamwone Mungu. Mefiboshethi alipotoka Lo-Debar, maisha yake yalikuwa ni kukaa ikulu tu, akawa anakula menyu (masontojo) ya mfalme daima. Mtu akiwa Lo-Debar anasahau thamani yake halisi, anasahaulishwa ahadi zote za Mungu katika maisha yake, badala ya Mungu kuwa rafiki anakuwa ni adui, na huyu mtu anaanza kumwepuka Bwana (Yona 1:3), Hivi mtu unaanzaje kumwepuka Mungu aliye chemichemi ya uzima wako? (Yer 2:13). Kuvunjika miguu kwa Mefiboshethi, hakuondoi nafasi yake kuwa yeye ni mjukuu wa mfalme wa kwanza wa Israel, Kama ambavyo wewe msomaji, nafasi yako ya kuwa ni mwana wa Mungu haijaondolewa na kosa lile ulilotenda. Kumbuka tulipokuwa wenye dhambi, Yesu alikufa kwa ajili yetu. There is no infirmity the Lord cannot fill. Umejifungia Lo-Debar, unashindwa kumwendea Bwana, huyu ambaye sifa yake kuu ni mpole (Math 21:5,11:29) tena wala hakemei (Yakobo 1:5). Eti kwa kuwa ulianguka kwenye dhambi ya uzinzi, basi umekuwa *_self-jailed_* huko Lo-Debar hutaki kutoka 🤔. Hivi unadhani kule kutoa mimba *(Abortion a.k.a kushusha injini)* ndio kunakufanya usahaulike kabisa? Ni watu waliopo Lo-Debari tu, ndio wanao sahaulishwa wema wa Bwana. ~*_(But you are not rejected at all)_*~ Hata kama ni kweli, ulishusha injini tena ukiwa umeokoka hivyo hivyo, hilo nalo sio sababu ya kuendelea kukaa Lo-Debar, BWANA ANASEMA TOKA HUKO LO-DEBAR, MAANA HATA HILO UKILITUBIA, MUNGU ATAKUSAMEHE KABISA. NARUDIA TENA ATAKUSAMEHE KABISA (Isa 55:7), IKIWA UNAONA ISHU YAKO IKO NYEKUNDU MNO LIKE SCARLET 🇲🇦, MUNGU ANASEMA ATAZIFANYA HIZO DHAMBI KUWA NYEUPE KAMA THERUJI (ISA 1:18).
Isaya 43 : 25
_*Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.*_
WATU WALIOKO LO-DEBAR, KAZI YAO KUBWA NI KUJIHUKUMU TU , MIMI NI MBWA MFU 😩, SASA WEWE MWANA WA KIFALME (ROYAL SON) MEFIBOSHETHI 😄😄 NANI AMEKWAMBIA WEWE NI MBWA?? NDIVYO WEWE UMEKAA UNASEMA, KWELI MUNGU ATANISAMEHE KWA HILI 😰, UNAJIPA LAANA NYINGI AMBAZO HAZIPO KWENYE RATIBA YA MUNGU. WAKATI FULANI MWAKA 2007, SIKUMBUKI MAKOSA YAPI HASA, LAKINI NILIJIHISI KUTENGWA NA MUNGU, NIKASHINDWA HATA KUOMBA. IKUMBUKWE KUENJOY MBELE ZA BABA YETU, MUNGU WETU SIO ZAWADI WANAYOPEWA ETI WATUMISHI PEKE YAO (HUSUSANI WALE FULL TIME). HAPANA HILO NI KWA KILA MKRISTO, UNAPASWA KWA MUDA WAKO UNAMWENDEA MUNGU, UMFURAHIE, MAANA KATUFANYA MARAFIKI ZAKE (YOH 15:15,ISAY 41:8). UNAWEZA KUWA NA NDUGU, LAKINI MIONGONI MWA NDUGU ZAKO, KUKAWA NA NDUGU AMBAYE AMEKUWA RAFIKI HASWA👬, SASA UHUSIANO WA URAFIKI NI MKUBWA MNO (MITHALI 18:24). SASA NIKIWA KATIKA HALI HIYO YA KUHISI KUTENGWA, NIKACHUKUA BIBLIA KUSOMA, NILIPOIFUNUA NIKAKUTANA NA
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Isay 44
_*21 Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi.*_
_*22 Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa.*_
👆🏼MANENO HAYO ILIKUWA NI KAMA MUNGU ANANIAMBIA LAIVU. NIKASIKIA FURAHA GHAFULA, SIKUANZA HATA KUTUBU, ILA NIKAJISAMEHE MWENYEWE, NIKAINUKA NAKUANZA SAFARI YA KUONDOKA LO-DEBAR. SIKU HIYOHIYO NIKAANZA MAOMBI YA USIKU, KWA FURAHA KUU. BADAYE NIKAJIHOJI, HIVI NINI KILIKUWA KINANIZUIA KUOMBA, NIKAWA NAJIHISI NI MWOVU TU, HATA SIKUWA NA SPECIFIC CHARGES OF OFFENCE, KWAMBA NIMETENDA NINI. SASA JIBU NI MOJA, NILIKUWA LO-DEBAR NA NIKAFANYA MAAMUZI YA KUTOKA HUKO.
NDUGU YANGU MSOMAJI. MTAKE BWANA SASA (ZABURI 105:4). WATU WENGI SANA, HAWANIELEWI KWA NINI NATOA MKAZO HUU MKUBWA KWA MNAPASWA KUTENGENEZA NA MUNGU NYAKATI ZOTE. KUNA WAKATI UTAYAFUTA MAFUNDISHO HAYA, HUTAYAPATA, UTAYAFUATA KATIKA BLOG, ILA UKIYASOMA HAYATAKUWA NA MSAADA TENA, KWA MAANA ROHO ALIYEYAVUVIA SASA KUKUSAIDIA, HATAKUWEPO TENA. NA NYAKATI HIZO UTAMTAKA MUNGU WALA HUTAMPATA, ANASEMA HAUTAMUONA HATA UKIMWIMBIA PAMBIO ZILE NZURI.
Luka 13 : 35 _*Angalieni, mmeachiwa nyumba yenu! Nami nawaambia, Hamtaniona tena kamwe, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.*_
SASA NI SAO YAKO, YA KUONDOKA LO-DEBAR KWA JINA LA YESU, MAAMUZI YAKO YA KUONDOKA LO-DEBAR YAFANIKIWE, WALA YULE MWOVU, ASIFANIKIWE KUKUZIBIA TENA NJIA WALA KUKUFUNGA AKILI YAKO. THE LORD IS PATIENTLY WAITING FOR YOU, YOU ARE WELCOME BACK TO YOUR ROYAL POSITION, WEWE NI WA THAMANI (ISAY 43:4, 1PET 2:9-10).
MBARIKIWE NYOTE
Mwl Proo
0762879363 (All Truth WhatsApp Group)
Amina mtumishi kwa neno hili limenitoa sehemu moja kwenda nyingine
ReplyDelete