*HATUTAIACHA NYUMBA YA MUNGU WETU!⛪*
By _Mwl Proo_
0762879363(Mwl Proo)
Bwana Yesu asifiwe!
Wapendwa katika BWANA, Mafundisho sahihi ya Neno la Mungu yanalenga kukusogeza kwenye mstari *_running track_*, ili Bwana akipita akukute, asikupite!
Kama kuna swali linalouliza, "Kwa nini maisha ya watu wengi wa Mungu, yako ktk hali duni?". Tusikimbilie kuanza kusomewa *Matendo 14:22*, Kwamba imetupaswa kuuingia ufalme kwa dhiki nyingi. Ha ha ha ha, Kukosa pesa za kununua unga wa ugali 🍚, kushindwa kumiliki hata kigari 🚗 second hand cha milion 6, hakuna uhusiano na ile dhiki inayotajwa, wala sio majaribu. Jibu jepesi sana, formula imekosewa na hawa watu wa Mungu, na hata wale wanaomiliki mali na utajiri hawajapata kwa formula za ufalme, walikinzana na kanuni za ufalme, wakatenda udhalimu ili wayapate walionayo. Baraka za Mungu hutajirisha, tena Mungu hachanganyi huzuni ktk hizo baraka (Mith 10:22). Kama ulipata daraja la kwanza (division one/first class GPA), Baada ya kuiba mtihani, kudesea/chabo (ukasovu feki), au hata kushiriki ngono na mkufunzi/mhadhiri ili akufanyie mpango, ukabanduka na GPA ya 4.8 , Kama ulifanikiwa kupata gari kwa kusaidiwa toka ulaya, lakini ilikupasa kuandika emails za uongo kuwa unahudumia watoto yatima, ukapiga picha na za watoto wenye hali ngumu, kumbe ndio gari 🚗 unapiga nalo misele tu, *Please usije kutushuhudia kanisani 👐🏽!!*
SISI TUNAYO KANUNI YA UFALME, NA TUKIIFUATA HIYO LAZIMA MIISHO YETU IWE SAFI (Zabur 37:37,Yer 29:11). KANUNI YETU INASEMA, *"UFALME KWANZA (Luka 12:31)"*
WANA WA MUNGU WAMEPINDUA FORMULA YA UFALME, NA SASA WANAPATA SHIDA KUBALANCE KATI KUWA NA HAKI YA MUNGU NA BADO KUWA NA MAFANIKIO YA KIMWILI.
DAUDI KUNA WAKATI ALIYATAMANI YALE MAJI YA KISIMA KILICHOPO BETHLEHEMU (2Sam 23:15-16), LAKINI WAFILISTI WALIKUWA WAMEWEKA KAMBI HAPO MTU ASIWEZE KUPITA, SASA WALE MABAUNSA 💪🏾⚔🗡WA DAUDI WAKAJITOSA KWENDA, WAKAFANIKIWA KUMCHOTEA KAGLASS KAMOJA🍷.SASA KWA VILE DAUDI ANAJUA KANUNI ZA UFALME, AKAJUA AKIYANYWA ATAONA KIU TU TENA, ILA KANUNI YA UFALME ISEMAYO MUNGU KWANZA, AKAYACHUKUA AKAYAMWAGA MBELE ZA BWANA, ALIJUA UKIWEKA KWA BWANA UTAPOKEA TENA KIASI CHA KUSUKWASUKWA NA KUMWAGIKA (Luka 6:38).
Daudi hakuwahi kushindwa vita, maisha yake yalijaa mapambano makali, lakini nia ya moyo wake ilikuwa inaendana na kanuni ya ufalme. Je! Wajua kuwa Daudi hakuagizwa kujenga hekalu bali ilikuwa mawazoni mwake, tena alikuwa na shauku ya nyumba ya Mungu kuliko chochote?
Zaburi 69 : 9
_*Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.*_
1 Wafalme 8 : 17 _*Basi ilikuwa moyoni mwake Daudi, baba yangu, kujenga nyumba kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli.*_
1 Mambo ya Nyakati 29 : 3
*_Nami tena kwa kuwa nimeiwekea nyumba ya Mungu wangu shauku yangu, nami ninayo hazina yangu mwenyewe ya dhahabu na fedha, naitoa kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, zaidi ya hiyo akiba niliyoiwekea tayari nyumba takatifu;_*
*SULEMANI*
Hapa ndipo napafurahia, pamoja na huyu kukuta hazina ya vyote vinavyohitajika kujenga hekalu tayari vipo, lakni alifanya viti vya tofauti. Aliifuata formula ya ufalme 👉🏾 *Mungu kwanza*.
Sulemani alipoingia kwenye ufalme, alianza na ujenzi wa hekalu kabla hata ya Palace/Ikulu yake, Jambo ambalo watu wa Mungu wa leo hawataki kumjaribu Mungu kwa njia hii. Akatumia miaka saba kujenga hekalu🏛 (1Falme 6:38b), Kisha akatumia miaka 13 kujenga Palace/Makazi yake ya kifalme (1Falme 7:1-2). Sasa sababu hasa ya kutumia muda mwingi ktk kujenga makazi yake ni kwamba hakuwa tena na materials zilizo kuwa tayari tayari ka kwa hekalu, na pia watu hawakujitoa kwa nguvu sana kama ktk kujenga hekalu. Ni nani leo yupo tayari kununua kiwanja cha kanisa,akiwa yeye bado anaishi kwenye chumba cha kupanga? Nani leo hii yupo tayari kuona sitting room yake haina sofa za ukweli, lakin sofa set ya kwanza kununua akaitanguliza kanisani, ili inayofuata iwe yake? , Mtanielewa tu, Maana Eliya Mtishbi aliponwambia yule mjane wa Sarepta, kwamba kwa hako kaunga kalikobaki konzi moja, nifanyie KWANZA MIMI kamkate🍞, lengo hasa ni kuzitibua mbingu ziachilie unga usiokoma. Njia ya kuruhusu pipa la unga lisikauke unaanza kufanya kwa ajili ya Mungu kwanza. Ukijitanguliza mwenyewe, utabakiwa na kile ulichonacho tu (Yoh 12:24). Sasa hilo tukii la Sulemani kumfanya Mungu kwanza, lilimwinua hatari sana, wakati wa Sulemani vyombo vyake vyote vilikuwa dhahabu safi 💎💎, yaani hata fedha(Silver) ilikuwa kama takataka, hakuwa na vyombo vya mti sijui nini plastic no 👐🏽 (1Falme 10:21)
TWENDE KATIKA ANDIKO LETU LA MSINGI
Nehemiah 10 : 39 _Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; *wala sisi hatutaiacha nyumba ya Mungu wetu.*_
👆🏼👆🏼KAMWE USITARAJIE KTK HALI YA KUIACHA NYUMBA YA BWANA, KAZI YA MUNGU (MUNGU HAJAWA KWANZA), HALAFU MBINGU ZITEME MIBARAKA YAKE, NEVER!! NASHANGAA WATU NYUMBA ZAO ZIMEPAKWA RANGI NA PAVEMENT FULANI AMAZING MPAKA KWENYE CAR PARK, ILA WANATAKA BWANA AWABARIKIE AFYA NJEMA KABISA, UTAKUWA HERI KAMA UTAFANYA KWA BWANA KWANZA. HUYU SULEMANI KUNA MAPAMBO ALIYAWEKA HEKALUNI AMBAYO HATA HOME KWAKE HAYAKUWEPO, ALIJAZA MIKUFU YA DHAHABU HEKALUNI, ILI KUWA NA MVUTO KULIKO IKULU
1Falme 6
*_21 Hivyo Sulemani akaifunika nyumba ndani kwa dhahabu safi. Akaitenga kwa mikufu ya dhahabu mbele ya chumba cha ndani; akapafunika na dhahabu._*
_*22 Akaifunika nyumba yote kwa dhahabu, hata ilipokwisha nyumba yote; tena madhabahu yote iliyokuwa ya chumba cha ndani akaifunika kwa dhahabu.Mapambo ya Hekalu*_
ALIPOMHESHIMU MUNGU KWA DHAHABU KIBAO HEKALUNI, MBINGU ZILIACHILIA DHAHABU KULIKO ZILE ZILIZOPATIKANA KTK MINERAL DEPOSITS ZA NCHI YAKE. WENGI LEO HII INEFIKIA HATUA WANAONA KAMA KUFANYA MAMBO YA MUNGU NI KUMPIGA KICK PASTOR HUSIKA, UTASIKIA NA KAUSEMI FEKI,TUNAMTEGEMEZA (YAANI HAJIWEZI SO MNABEBEA UDHAIFU) LOOH🤔, KUTOA KULIKOAMBATANA NA FIKRA KUWA MNAM-BUSTI MTUMISHI HAKUNA BARAKA HAPO, MAANA KUNAWATUKUZA JUU YAKE NA JUU YA MUNGU ALIYEMTIA MAFUTA. KWA NINI SADAKA YA KUTAJA KWA MAIKI 🎤 UNAAHIDI LAKI 2 LAKINI ILE YA KUTIA KAPUNI NI TSH 500/=? NI KWA KUWA BADO UNAFANYA MAIGIZO. KAMA TUNGENG'AMUA SIRI YA UFALME.
Nehemiah 13 : 10 _*Tena nikaona ya kwamba Walawi hawakupewa sehemu zao; basi wamekimbia Walawi na waimbaji, waliofanya kazi, kila mtu shambani kwake.*_
👆🏼👆🏼HASARA ZA MAKUHANI KUKIMBILIA MASHAMBANI (YAANI PASTOR YUKO BIZE KARIAKOO KWENYE FREMU YA BIASHARA WIKI NZIMA, ATAPUNGUKIWA UFUNUO WA NENO, MTAANZA KUMKINAI, NAYE ATABUNI MAFUNDISHO AMBAYO NI YA KUWAFANYA MTOE KWA SHURTI, NA SIKUIZI KUNA KAMTINDO PASTOR MWENYEJI, ANALETA MWINJILISTI MGENI AJE AHUBIRI UJUMBE WA KUAMSHA WATU WATOE. KWA HIYO ATAHUBIRI YALE MAHUBIRI YA KUTISHIANA LAANA KWA KUTOTOA ZAKA NA SADAKA, THEN MNAPOTOA KWA HOFU YA KULAANIWA NDIPO MILANGO YA BARAKA INAFUNGWA RASMI 🚪🚪🔒🔒🔐, MAANA UTOAJI WA AGANO JIPYA, NI ULE WA HIARI KWA MOYO WA KUPENDA, NA KUJIDHABIHU (2KOR 9:7).
UNAKUTA KANISA LINA WATUMISHI WA SERIKALI, LINA WAFANYA BIASHARA WAKUBWA, LAKINI MICROPHONE YA ELFU 80 🎤, NI MBINDE KUIPATA. HIYO ILIPASWA AFANYE MTU MMOJA BILA HATA CHANGIZO. MIMI NINAKUSUDIA, SIKU MOJA NICHUKUE MKOPO HATA WA MILIONI 15 WOTE NIUINGIZE KTK KAZI YA MUNGU KAMA UTANUNUA KIWANJA CHA KANISA AU VYOMBO SAWA, NAONA NI BORA NIBAKI NAKATWA MSHAHARA MIAKA MITANO, LAKINI KUNA MAHALI NILIHUSIKA NA UFALME WA MUNGU. NA HILO NAJUA NITALITENDA TU, NILIPOANZA KAZI SERIKALINI NILICHUKUA MKOPO WA KWANZA KABISA NIKANUNUA KINANDA CHA KANISA 🎹, KWA HUO MKOPO WOTE NIKIWA NIMEONGEZEA NA PEAA ZINGINE KTK SEHEMU NDOGO YA MSHAHARA ILIYOBAKI, NIMEKITOA KANISANI KWA MOYO MWEUPE KABISA. NA HUO NI MWANZO, NAMWAMINI MUNGU KWA VITU VIKUBWA KTK MAISHA LAZIMA NIFANYE MAMBO MAKUBWA PIA KWA AJILI UFALME, NIKIMNUKUU BABA WA UMISHENI KTK HISTORIA YA KANISA, AITWAYE WILLIAM CARLEY, AMBAYE ALIKUWA NI SHOESHINER 👞👢👟LAKINI KTK HALI HIYO ANASIFA YA KUWA FATHER OF MISSION, ALISEMA, *_"ATTEMPT GREAT THINGS FOR GOD, THEN EXPECT GREAT THINGS FROM GOD"_* Bado hii nukui iko ndani ya ile kanuni ya ufalme yaani _*MUNGU KWANZA*_ , LEO HII WAKRISTO WAMEKUWA SO *_STINGY_* WABANIFU KIASI CHA KUFANYA WATUMISHI WA MUNGU KUWA KAMA BROOKERS/BIDDERS YAANI UTADHANI WANAMDALALIA MUNGU, WANANADI KWA JUHUDI MPAKA KUONGEZA NA KAUONGO ILI WATU WATOE. KUMBE ANGEWEZA KUWAFUNDISHA TU KWELI YA MUNGU THEN WATU MJIONGEZE. NIMEKUTA MAHALI SADAKA UNAYOTAKA KUITOA LAZIMA UIINUE JUU💵💰, LENGO HAPO NYUMA NI WEWE MWENYE KIMIA TANO CHAKO UONE AIBU, MAANA WENYE UHURU HAPO NI WALE WENYE WEKUNDU WA MSIMBAZI BUKU TEN. NA PENGINE NIKAKUTA SOMO LA SADAKA YA UKOMBOZI, HUYO MHUBIRI AKASEMA, GIDEON ALITOA NG'OMBE 🐄, SASA NAWE SIJUI UNAANDAA SADAKA GANI YA KUVUNJI MADHABAHU ZA GIZA. HIYO NI TOZO KAMA YA TRA ETI ILI KUVUNJA MADHABAHU ZA MIZIMU INAYOKUFUATILIA, TAFUTA DONGE NONO💰🏧, HII NAYO NI HERESY, SI FUNDISHO SAHIHI, LAKINI WAFENYEJE SASA, LAZIMA YABUNIWE HAYA MAANA WANA WA UFALME, WAMEIACHA NYUMBA YA MUNGU.
Ndugu msomaji, kama umeokoka vizuri kabisa, hiyo inakupa hakika ya kuuishi umilele waki na Mungu. Lakini swala la kuenjoi baraka za mwilini ktk haki, bila hata kupiga dili zilizo kinyume na imani, usikwepe kazi ya Mungu, usikwepe nyumba ya Mungu, mfanye Mungu awe kwanza, mtumikie kwa mali zako, epuka roho ya choyo (Luka 12:15)
*TAMANI KUONA NYUMBA YA BWANA INA KILA KILICHO BORA, WATUMISHI WAKE NA KAZI YAKE KWA UJUMLA. I ASSURE YOU, MAISHA YAKO YATAKUWA YAKUTAMANIKA DAIMA*
Mwl Proo
0762879363(welcome to our whatsapp group)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment