*MKALIMANI*
_Mwl Proo_
0762879363
Bwana Yesu asifiwe sana sana!
Karibu tuendelee kuvumbua yale tuliyokirimiwa na Mungu, ili tusipate hasara tuwapo katika mwili huu.
Ayubu 33 : 23
_*Kwamba akiwapo malaika pamoja naye, Mkalimani, mmoja katika elfu, Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo;*_
Mstari huu umeficha mengi, ingawa tafsiri zimeongelea tu kama maneno ya Elihu ya kawaida. Lakini tuuchambue kwa kina. Neno Malaika/Mjumbe linalojitokeza hapo, limeonekana katika Biblia ya kiebrania kama Malach HaBrit pia Malach HaAdon. Yaani malaika mwenye agano *_"the angel of the covenant", מלאך הברית , malakh habrit_* pia malaika wa Bwana, yaani *_(מַלְאַךְ יְהוָה)Malakh YHWH "Messenger of Yahweh_* na hapo chini Elihu akasema ameona ukombozi, yaani huyo ni malaika wa ukombozi, *_redeeming angel", (המלאך הגאל), hamalak haggoel_*
👆🏼ELIHU ANASEMA AKIWEPO MALAIKA MMOJA, MKALIMANI/INTERPRETOR MMOJA KATI YA ELFU. JINA HILI MKALIMANI LIMEONEKANA KATIKA BIBLIA YA KIEBRANIA KAMA *_Melitz-(מליץ) yaani intercessor/advocate/mediator_* YAANI MWOMBEZI/WAKILI/MPATANISHI.
*KAZI YA HUYO MKALIMANI NI NINI?*
Katika hali ambayo inaonekana kuwa it is beyond remedy/hali isiyoweza kuponyeka tena, kama ni mgonjwa basi yupo ICU (intensive care unit), hakuna matumaini tena. Jaribu limefikia at peak. Unahisi kufa huku hapaa..⚰
Tusome....
AYUBU 33:19-22
*_19 Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;_*🛌💉💊
*_20 Hata roho yake huchukia chakula,Na nafsi yake huchukia nyama nzuri._*🍗🍖🍲
_*21 Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane;Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje.*_💀
*_22 Naam, nafsi yake inakaribia shimoni,Na uhai wake unakaribia waangamizi._*⚰
👆🏼👆🏼HIYO NI HALI TETE, AMBAPO KAMA NI JARIBU LIMEKUWA GUMU UNAHISI UNAWEZA KUACHIA NGAZI, KAMA NI MAGONJWA, YAMEKUKABA VILIVYO, HAPO UKILETEWA VYAKULA VILE UNAPENDAGA, UNAHISI KUVICHUKIA, ULIKUWA UKIITWA BONGE, LAKINI YOU ARE NOW SKINNY (NGOZI NA MFUPA). UKIKAA PEKE YAKO UNAWAZA UTAKAVYOKUFA, UNAWAZA KUJINYONGA, DENI LIMEKUNYIMA RAHA UNAWAZA KUTOROKA NCHINI, NDOA IMEKUWA CHUNGU UNAWAZA UBWIE SUMU ILI UVUTE⚰☠. MIONGONI MWA MAMBO AMBAYO HUPASWI KUFANYA KABISA, NI KUJIUA. SASA KATIKA HAYO MAZINGIRA YANAMHITAJI MKALIMANI, ATAKAYESIMAMA NA KUSEMA......
Ayubu 33 : 24 *_......Mwokoe asishuke shimoni;⚰ Mimi nimeuona ukombozi._*
KUNA WAKATI NABII AMOSI, ALIPOONA GHADHABU KUU JUU YA YAKOBO(ISRAEL), AKASIMAMA KAMA MKALIMANI NA KUMTAKA BWANA ASITISHE;
Amosi 7 : 5
*_Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, acha, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo._*
MKALIMANI AKISHATOA TAMKO, KUMBUKA HUYU NI MWOMBEZI/WAKILI/MPATANISHI(MTETEAJI), NDIPO ILE HALI ILIYO MBAYA SANA, UNAKUWA SHWARI KUU GHAFULA, MFIKILIE AYUBU MWENYE MAPELE KIASI CHA KUTUMIA VIGAE KUJIKUNA, YUPO KATIKA CRITICAL CONDITION. BAADA YA TAMKO LA MKALIMANI ANAKUWAJE?
Ayubu 33 : 25 *_Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto; Huzirudia siku za ujana wake;_*
YAANI MKALIMANI AKITOA TAMKO TU, KIFO ⚰KINAHAIRISHWA, ILE NGOZI YENYE UKURUTU NA MAGAMBA INAFANYWA LAINI KULIKO YA MTOTO, NA KAMA ULIKUWA NA MWONEKANO WA KIZEE 👴🏽👵🏾,TAMKO LA HUYU MKALIMANI, LINAKUREJEZEA UJANA, MAANA BWANA AMEAHIDI KUKUREJEZEA UJANA KAMA TAI (ZABURI 103:5), MAANA YAKE YOU WILL BEAR FRUITS EVEN IN THE OLD
AGE (YOU WILL FLOURISH).
SASA HATA KAMA UNA MAJANGA GANI MAKUBWA,MAGUMU!. MAISHA UNAPASWA KUYAISHI SIO KUYAEPUKA, UNACHOHITAJI NI MKALIMANI (ADVOCATE/MEDIATOR/INTERCESSOR). *SASA HUYU MKALIMANI NI YESU KRISTO, MAANDIKO YAMEMFUNUA KUWA HUYU MKALIMANI WA KWELI NI YESU KRISTO (RUMI 8:34, 1YOH 2:1-2, 1TIM 2:5). HUYU ANALO NENO LA KIFALME LENYE MAMLAKA, YA KUKUTOA ICU, AMBAKO WATU WAMEANZA KUKUSANYA PESA ZA MSIBA KABLA HUJAFA. HUYU ANAO UWEZO WA KUWAFANYA WALE WANAO KUDAI, WAKASEMA TUMEKUFUTIA DENI, AU AKAINUA MTU WA KULIPA DENI LAKO BILA SHARTI LOLOTE.USIMKATIE TAMAA, HAJAKUACHA, HAJAKUSAHAU, HAYUKO MBALI. MWITE YESU MKALIMANI MMOJA WA KWELI, AINGILIE KATI AYAFANYE MAISHA YAKO YAWE MAPYA TENA, HISTORIA IBADILIKE LEO, UKOSE SABABU YA KUJIUA NA UPATE SABABU ELFU ZA KUENDELEA KUMTUMIKIA.* MWITE HUYU MKALIMANI ILI NDOA ILIYOPOTEZA LADHA, IREJEZWE KAMA MWANZO AMBAPO MLITHUBUTU KULISHANA MPAKA CHAKULA 😋🍲, SALAMU ZOTE ZILIJAWA NA KISSES😘😘😘, NA WAKATI HUU NI FULL-MISONYO 😏😏😏 NA MABANZI 👋🏾👊🏾💪🏾, JESUS CAN RECONCILE/MEDIATE!!! JUST CALL ON HIS NAME, AND SEE HIS GOODNESS IN THE LAND OF THE LIVING. THE SMILE WILL BE RESTORED UPON YOUR FACE😣👈🏾👉🏾😊. HALELUYA HALELUYA
Nimemaliza hivyo😄
Mwl Proo
0762879363
All Truth Whatsapp Group
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment