*NANGA YENYE SALAMA⚓*
_*```Mwl Proo```*_
0762879363
Haleluya Haleluya!✋🏾
Kuna watu nawaona mmeanza kughafilika😀, mioyo yenu imeanza kuwahusudu wana wa giza wenye yale ambayo huitwa mafanikio (Zab 73:1-17). Wewe uliye ndani ya Yesu una heri isiyo na mfano wake, kwa kutotambua haya tumepata watu walioiacha imani. BWANA ameniagiza nikuambie wewe mwenye haki una heri (Isaya 3:10).
Zaburi 144 : 15
_*Heri watu wenye hali hiyo, Heri watu wenye Bwana kuwa Mungu wao.*_
MTU MWENYE MATUMAINI KATIKA YESU KRISTO, MAISHA YAKE YAMESHIKWA NA NANGA YENYE SALAMA; YESU KRISTO NI NANGA YA ROHO YENYE SALAMA... 🌊⚓🛥.
Waebrania 6 : 19 ⚓
*_tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,_*⚓
Kwa kuwa na Yesu ktk maisha yako sio guarantee ya kutokutana dhoruba kabisa. But you have the assurance never will you be tossed away, to and fro, here and then. DHORUBA INAWEZA KUKUKUTA UKIWA NA YESU WAKO KABISAA....
Marko 4 : 37 _*Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.
👆🏼👆🏼Hawa wajamaa walikuwa na Bwana mkubwa ndani ya chombo⛵ wakati upepo wa mbisho unawatandika. Hakika tuliyo nayo ni hii, *_No matter how intense the storm is, lazima tufike salama._* Na hilo linafanya nisiishi kwa hofu kabisa, kuna wahubiri na waimbaji wenye kuyahubiri/kuyaimba majaribu kuliko uhalisia wa utetezi wa kimungu mpaka watu wamejazwa hofu.
HAKUNA DHORUBA YOYOTE YA MAISHA KTK SAYARI HII DUNIA, INAWEZA KUMSOMBA MTU AMBAYE AMESHIKWA NA NANGA YENYE SALAMA, *_HAKUNA!!_* ZITASUMBUASUMBUA KWA MUDA, ILI MUNGU AJIONESHE UKUU WAKE NA MUDA ZINASUMBUA HAZIKUSOMBI KAMWE.
2Korintho 4
*_8 Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa;_*
_*9 twaudhiwa, bali hatuachwi; twatupwa chini, bali hatuangamizwi*_
Zaburi 118 : 12 *_Walinizunguka (mataifa/maadui/dhoruba) kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali._*
UNAWEZA KUWA KATIKA UGUMU WA KIFEDHA, UNATAMANI KUNYWA HATA SODA YA 500/=, BAJET YAKO HAIRUHUSU, UMEKOSA KABISA NAMNA YA KUFANYA ILI KULIPA ADA SIJUI MKOPO WA BIASHARA ULIOCHUKUA, UMESAKA KAZI WEEE MPAKA UNAANZA KUHOJI HIVI NI WEWE KWELI ULIISOMA HIYO DIGRII AU!, UGONJWA UMEKUSUMBUA, NDOA IMEKUMBWA NA UTATA, KUNA MATISHIO MENGI YA KUFILISIKA KWA BIASHARA YAKO, MATISHIO YA KIWANDA KU-SHUTDOWN, NAFSI YAKO NI KAMA INALEMEWA. NA UKIJICHEKI UPO VIZURI NA YESU. NDUGU YANGU MSOMAJI KATIKA HAYO YOTE HAKUNA MOJA WAPO LENYE KUWEZA KUKUONDOSHA. WEWE HUTAONDOSHWA KAMWE, HATA UKITUMIWA KOMBORA (intercontinental missile)🚀, LAZIMA UBAKI SALAMA BILA KUONDOSHWA, MAANA YUKO YESU AMBAYE HATA ACHA MGUU WAKO USOGEZWE, ISIJE ADUI AKAJISIFU YA MUNGU WAKO.
Zaburi 16 : 8 _*Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.*_
KAMA HUJAMWACHA BWANA, WEWE HUJASAHAULIKA. HAUJAKATALIWA, USHINDI JUU YA HAYO YOTE UPO NJIANI. NAKUMBUKA NILIKUWA NA DHORUBA FULANI NIKIWA MASOMONI, SIJUI KILITOKEA KITU GANI KABLA YA KUAPPLY CHUO KULIKUWA NA EXHIBITION YA TCU PALE BLUE PEARL(UBUNGO PLAZA) VYUO VYOTE VILIKUWA NA MABANDA YAO MLE NDANI. SASA COURSE NILIYOAPPLY NILIJIRIDHISHA KUWA INATOLEWA MKOPO NA BODI *_HESLB_* NIKAHOJI PALEPALE WAHUSIKA WOTE, LAKINI NILIPOAPPLY ONLINE KUPITIA *_CAS_*, SIVYO COURSE ILIVYOONEKANA KATIKA DATABASE YA BODI L, NA NIKAKOSA MKOPO. SASA KATIKA SEMISTA SITA NI SEMISTA MOJA YA KWANZA PEKE YAKE NILILIPA ADA BILA DHORUBA, SEMISTA TANO ZOTE NILILIPA ADA SIKU MBILI KABLA YA U.E(UNIVERSITY EXAMINATION) TENA KWA FAINI 🤔, MUNGU ALINIAMBIA KWA SAUTI KABISA, KUWA NITAMALIZA MASOMO!. SASA HIYO HAIKUONDOA DHORUBA ILA NILIKUWA NINA HAKIKA, *_COME WHAT, EVERYTHING WILL BE OK!,_* MTIHANI UNAANZA JUMATATU MIMI JUMAMOSI JIONI NIPO OFISI ZA EXAMINATION NASUMBUANA NAO ID-CARD YA KUFANYIA U.E, HAYO NDIYO YALIKUWA MAISHA KWA SEMISTER TANO ZOTE, WALA SIKUWAHI KUSHUKA MOYO, PENGINE MUNGU ALINIINULIA WATU WAKALIPA GHARAMA ZANGU ZOTE. UNGENIKUTA WAKATI HUO AMBAPO UNAPASWA EITHER UBEBE MABEGI UENDE KWENU AU VINGINEVYO, NILIKUWA BIZE KUFANYA HUDUMA KAMA KIONGOZI WA FELLOWSHIP (MUDA WOTE UNGENIKUTA NABEBELEA SPIKA KUPELEKA KATIKA UKUMBI WA IBADA), FADHAA ZA ADA NILIMTWIKA YESU KWAMBA SITAONDOSHWA HAPA. NIKIULIZA MSAADA WA FEDHA KWA WANADAMU MARA MOJA WAKIYONGAYONGA TU NAWAPOTEZEA MAANA MLANGO LAZIMA UTAFUNGUKA TU, HALELUYA!!
UKIWA NA IMANI YA KUTOUGUA MAGONJWA NI HERI SANA, LAKINI HATA HUO UGONJWA UKIWEPO, WEWE MWENYE YESU UPO NA NANGA YENYE SALAMA. UGONJWA ULIOUA WENGI, HUOHUO UTAKUACHA *_UNHARMED,_* MAANA KWAKO IKO NEEMA ILIYOZIDI (Yakobo 4:6).
Nakumbuka mwaka 2010 February,nilikuwa kitandani nimekamatwa na tumbo bacteria wa hatari walitambulikana kwangu kwenye vipimo, nikiwa katika kuumwa huko saa saba mchana nimejifunika shuka naisugua miguu kwa maumivu, niliisikia sauti ya wazi (verbal voice) ikatamka, *_"UTAPONA",_* ukumbuke BWANA anayo ahadi ya kila mahali anasemaje katika Zaburi 41:3 *_On his sick-bed God will sustain him._* Sasa hata uwe wodini hukohuko jua mkono wa Mungu utakuwepo kukuhifadhi, Unaweza kuwa Labour Ward na madaktari wanasema unaweza kuwa na Complicated Delivery, hayo ni maeneo tu ya kukaa huku unamwambia Yesu waoneshe hawa wewe ni nani.
Usiruhusu mazingira magumu yakutie hofu/shaka, ukayeyusha lile neno la imani toka kwa Mungu. Petro mtume alipiga hatua nyingi sana👣👣🌊 akiwa anatembea juu ya maji. Akaangalia wimbi moja lililorushwa na upepo na kuhofu nafsini mwake, akashangaa maji yaleyale yanamzamisha wakati amekwishwa tembea hatua nyingi. Nawe mpaka hatua ya mwisho baki unaamini tuu. Hata kama mazingira hayaonesho dalili za muujiza. Mambo ya imani hayahitaji supportive & favourable environment/situation, NEVER!!👐🏽
Mhubiri 11 : 4 _*Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.*_
HALELUYA, MUDA WATU WOTE WANALALAMIKA NDOA ZA SIKUIZI😣😣😣 (Wengine wana msemo ndoa bongo😲) YAANI UAMINIFU KWISHA KABISA, MUME ANAFANYA PLUNDER OFISINI NA WANAWAKE WENGINE, NA MKE NAYE ANAFANYA MEANDERINGS URAIANI; MUDA WATU WANALIA UCHUMI MGUMU (VYUMA VIMEKAZA 🔧🔩🔧🔒; MUDA WATU WANALIA KUTUMBULIWA (KUPUNGUZWA KAZI); MUDA WATU WANALALAMIKA MORAL DECAY; WEWE MWENYE YESU UMETHIBITISHIWA KWA NENO LA MUNGU KUWA UTAISHI KWA SALAMA!
Zaburi 46
*_2 Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari._*
_*3 Maji yake yajapovuma na kuumuka,Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.*_
MAJI MAKUU YAKIFURIKA🌊 JUU YA CHOCHOTE KINACHOKUHUSU, UTABAKI SALAMA *_OF THIS I'M SURE!!!._*
WAKATI MWINGINE UKIWA KATIKA MAOMBI SPEAK TO YOUR SITUATIONS, UZIAMBIE ZILE HALI NGUMU KUWA NAJUA KUWA WEWE SHIDA FULANI, WEWE UGONJWA FULANI, WEWE UTASA, WEWE UKAME WA FEDHA, WEWE KUKOSA KIBALI, WEWE DENI, WEWE HASARA KATIKA BIASHARA ETC ETC, I KNOW YOU'RE THERE BUT *_mene mene_*⚖ SIKU ZAKO ZINAHESABIKA ZA WEWE KUBAKI KATIKA HEMA YANGU. SIO MUDA WOTE IMANI NI KUSEMA NINA KAZI WAKATI HUNA, KUNA WAKATI YOU NEED TO FACE THE FACT, HICHO NDICHO KIMEANDIKWA KATIKA
WARUMI 4:19
INASEMA, _"WITHOUT WEAKENING HIS FAITH, ABRAHAM FACED THE FACT THAT HIS BODY HAD ALREADY DIED.......,"_ YAANI UKWELI NI KWAMBA MIAKA YANGU NI 100, NI KWELI SARA MKE WANGU NI TASA, LAKINI NITAPATA MTOTO KAMA BWANA ALIVYOSEMA. SO THERE IS THE TIME YOU NEED TO FACE THE FACT OF YOUR CIRCUMSTANCES AND YOU FLUSH THEM OUT BY FAITH. BAKI KWA YESU HUTAONDOSHWA KWANI YEYE NI NANGA YENYE SALAMA. NA AMBAYE BADO HUJAJIUNGA NJIA HII LISTEN TO GOD'S CALL KABLA HUJASOMBWA 🌊MKIMBILIE YESU (⚓) CHOMBO CHAKO KIWE SALAMA⛵, KWA KUWA NA YESU TUMEJITHIBITISHIA KUWA SALAMA KATIKA UZIMA WA SASA🌎 NA KATIKA ULE UMILELE WA ZAMA ZIJAZO.
Nimemaliza mimi kwa leo
*Mwl Proo*
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment