Tuesday, November 21, 2017

UMUHIMU WA USIKU

*UMUHIMU WA USIKU, KWA MTU WA ROHONI*

_Na Mwl Proo_
0762879363

SHALOM ALEICHEM!!
Mungu awabariki, mnapoendelea kushiriki kujifunza, pamoja nami hizi siri!.

Kwa mtu uliyeokoka (Mtu wa rohoni 1Kor 2:15), kama unautumia usiku wako wote kulala, aisee nimetumwa kukushtua kuwa unapoteza sana. Fuatilia hili kwa makini. Mtu wa rohoni anatambua na anapaswa kutambua yote. Kwa mfano wale wazoefu wa vita vya rohoni, wanapaswa kujua kile kilichowavamia ni nini/nani. Huwezi tu kukemea kwa ujumla. Sio muda wote ukiona mashumbulio ya kiroho, basi unakemea wachawi, au mapepo. Ukiwa na Roho Mtakatifu katika utulivu atakuelimisha usahihi wake. Kuna wiki moja Bwana alitumia masaa ya usiku kunipambanulia. Siku ya kwanza nilimaliza kuomba usiku, nilipojilaza tu, nikashangaa naona mtu mweusi kuliko giza dirishani, na hakanyagi chini yupo juujuu. Nikajishtua usingizini papo hapo, na Roho akanijulisha kuwa nimevamiwa na mchawi, hivyo nilikemea kitu sahihi sio kubahatisha kwa kutaja maadui wooooote 👌🏽, No! Siku iliyofuata, nimemaliza kuomba nataka kulala, nikiwa macho kwenye chumba chenye giza, nikaona kinywa kama cha ng'ombe kimefunuka pembeni mwa godoro, hapo hapo Roho akanikumbusha kuwa hicho ni kiashiria cha mizimu, na nikakemea kitu sahihi. Na siku nyingine nilihisi uwepo wa adui umefunikiza chumba changu, Bwana akanijulisha kuwa mkuu wa giza/anga la mahali nilipo anafanya vita. Sasa ili kujua kwamba hapo ni majeshi ya pepo wabaya au ni vinyamkera/ndondocha tuu vya  kichawi, ni muhimu uwe na maarifa ya kiroho. _*(Ili kuyajua hayo, Jitahidi upate kile kitini changu cha somo la VITA VYA ROHONI🔫💣⚔)*_

Kwa mtu wa rohoni sio lazima ufuate taratibu zote za kisayansi/kitabibu. Yaani wakiweka ushauri wa kulala masaa nane, wewe mtu wa rohoni hautiwi chini ya uwezo wa kitu chochote (1Kor 6:12b). Sio lazima uanze kuzingatia kulala masaa nane, No-Thank you! Wewe unaishi katika two realms kwa mpigo, yaani ulimwengu wa mwili na wa roho. Kwa hiyo hupaswi kulala masaa yote hasa ya usiku, or else hutaweza kutweka mpaka vilindini *(JIPATIE SOMO LANGU LA TWEKA MPAKA VILINDINI)*.
Uzuri mwingine ni huu miili yetu hii, imepewa uwezo wa kufanya ADAPTATION (Kujizoelesha). Kwa hiyo ukiweka ratiba ya kuamka saa nane, basi baada ya muda mwili unazoea tu, wala hautakusumbua. Mara zisizohesabika huwa naamka saa nane usiku, then siku yangu inaanzia hapo, mpaka kunakucha navaa nguo naenda kazini, wala huko sinzii kamwe!. Sayansi ya Afya haitakuruhusu wewe ufunge kavu siku nyingi. Lakini hapa nilipo mchungaji wangu anafunga siku  10, bila kugusa chochote kinywani, na amezoesha vijana wote,wanakaa siku saba kanisani kwa mfungo mkavu bila kugusa chochote. Na hiyo ni ratiba ya mara kwa mara, hapo Sayansi imetupwa kule 👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾. Maana hawajawahi kupata shida yoyote, ila wote wamekuwa super gianta kiroho wana misuli 💪🏾💪🏾💪🏾.

*MOYO WA SOMO*

KWA WATU WOTE WA ROHONI, USIKU NI WA MUHIMU MNO *(PROFOUND RESOURCE)*. KWA KUKOSA MAARIFA, WENGINE WAMEJUA USIKU NI WA WACHAWI, KUMBE WACHAWI NAO WAMEJUA NAMNA YA KU-MAXIMIZE FAIDA YA KAZI ZAO, NI KUYATUMIA MAJIRA HAYO.
SASA USIKU SIO KWA AJILI YA UFALME WA GIZA (PAMOJA NA KWAMBA HUTENDA KAZI ZAIDI KWA MASAA HAYO), WEWE MTU WA ROHONI KUWA MCHANA NI WA MUNGU, NA USIKU NI WA MUNGU (Zabur 74:16).
Nature ya usiku, imekaa kwa kuleta HOFU fulani (Zab 91:5) kwa sababu giza halivutii (Mhubiri 11:7). Na matukio kama vifo vya ghafula hutokea (Ayubu 34:20). Mpaka Elihu akashauri usiutamani usiku (Ayu 36:20). Lakini ukweli ni kwamba usiku ndio wakati mzuri zaidi, ingawa Bwana hana mpaka wa majira na nyakati. Ila kwako binafsi leo jifunze siri hii.

*WAKATI WA USIKU/KULALA YANATOKEA HAYA*
Mungu anaitwa AFUNUAYE SIRI (the revealer of mysteries)-Daniel 2:29. Na masaa hayo ndiyo mepesi sana kwa Mungu apendaye utulivu, kukusemesha kwa namna nyingi, iwe sauti ya wazi (Verbal voice), ndoto, maono, na ufunuo wa ndani ya nafsi. Tusome

AYUBU 33

_*14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja,Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.*_
*_15 Katika ndoto katika maono ya usiku,Usingizi mzito uwajiliapo watu,Katika usingizi kitandani;_*
_*16 Ndipo huyafunua masikio ya watu,Na kuyatia muhuri mafundisho yao,*_
_*17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake,Na kumfichia mtu kiburi;*_

HUO NDIO WAKATI MUNGU ANAYAFUNUA MASIKIO YALE YENYE KUSIKIA VYA ROHONI ZAIDI. MUNGU ANAWEZA KUJIFUNUA KWA MAONO NA KUSEMA KWA NDOTO (Hesabu12:6).

UKIWEZA KUANDIKA UNAYOSIKIA, KUINA AU KUOTA NI VYEMA (AYUB 20:8,DAN 7:1, HAB 2:3), LAKINI IKUMBUKWE ZIPO NDOTO ZA UONGO (Zek 10:2, Yer 23:25-32). Hatuwezi kukwepa kuwa ziko ndoto za Mungu, ziko  ndoto zako (nafsi inafanya reflection-Mhubiri 5:3), Ziko za Shetani, na hivi karibuni Mwl C. Mwakasege alituongezea aina ya ndoto, zinazotokana na mahali ulipolala, nilifanya uberoya kujihakikishia kwa maandiko, nikaiona iko sahihi sana. LAKINI PAMOJA NA HAYO, SITAKI KUKUINGIZA KATIKA MFUMO WA UTUMWA IKAWA NI *_TOO MUCH DREAMING (Mhu 5:7)_* ni rahisi pia kukutwa na ukengeufu kama wa Elifazi Mtemani, Ayubu 4:12-16 (Pata somo langu la MWILI WA ROHO ujifunze hilo kwa kina).

➰USIKU NDIO MUDA MZURI WA KUPATA HABARI (ISAYA 21:11), YAANI MAMBO YA SIRINI, YAJAYO, UNAYOYAFIKIRI, YOTE, HUO NDIO WAKATI WA KUPATA COMMENTATION YA KIMUNGU. KWAMBA JUU YA HUYO MCHUMBA ULIYEMPATA, JUU YA HIYO BIASHARA UNAYOTAKA KUIANZA, JUU YA SAFARI ETC ETC. KUNA WAKATI NILIMU-APPROACH BINTI FULANI ILI TUWE WACHUMBA, THAT VERY NIGHT, NILIONA NATAKA KUMBUSU 😘 KWENYE PAJI LA USO, NIKASIKIA SAUTI IMETAMKA KWA KINGEREZA *_SHE IS NOT YOURS_*. NILIPOAMKA NIKAJUA MUNGU AMEKOMENT CHA KWAKE TAYARI, NILIMJULISHA NA YEYE, MAANA TULIKUBALIANA TUOMBE KWANZA.

➰WAIMBAJI WETU WENGI LEO, KWA KUWA HAWAJAJIFUNZA SIRI ZA KIROHO, WANATHUBUTU KUCHUKUA NYUMBO ZA YA-MOTO BAND, WANAWEKA MANENO YA DINI NA KUUTAKASA UWE WA MUNGU, AU KWAYA IMEKOPI KILA KITU DUNIANI, WAPIGAJI NAO, KUMBE SIRI NI NDOGO TUU, USIKU NDIO MUDA WA MUNGU KUWAPA NYIMBO NA STYLES HUSIKA (Zaburi 42:8, Ayub 35:10), NILIFURAHI KUSIKIA JINSI JOHN LISU ALIVYOUPATA WIMBO ULE WA KINABII UITWAO _*JEHOVAH YU HAI*_ Saa saba usiku, alimwona mtu amemjia anamwambia nimetumwa kuja kukifundisha wimbo. Na ghafla akaona wapigaji hajawahi kuwaona, wakaupiga wimbo mwanzo mwisho!

*MORE ABOUT NIGHT-TIME*
Hapa naomba niweke sawa, usiku hui ninaouzungumzia ni ule wa saa sita hadi saa kumi alfajiri, yaani zamu ya tatu (00:00-03:00-Kirumi) hadi mwanzoni zamu ya nne, au kwa makesha ya kiyahudi ni kuanzia, katikati mwa kesha la pili na nusu ya kwanza ya kesha la tatu. Haya nitayaeleza katika somo jingine.

➰Bwana kumtokea Paulo usiku (Mdo 23:11,18:9)
➰Maono ya kuona mtu akimwita (Paulo) Makedonia,Usiku (Mdo 16:9)
➰Malaika kumtokea Paulo katika safari, Usiku (Mdo 27:23)
➰Yusufu aonywa usiku kwa ndoto (Math 1:20)
➰Daniel aona mengi usiku (Dan 7:2,713,2:19)
➰Wale Mamajusi akina Gaspar,Merciory walionywa usiku ndotoni, juu ya mipango ya kesho (Math 2:12).
➰Abimeleki alipata usahihi wa habari usiku, ilibaki kidogo tu angesex na mke wa mtu (Mwanzo 20:3)
➰Yakobo aona mazuri ya Mungu kwa ndoto (Mwanz 28:12)
➰Yakobo aona kinachotokea pale mifugo iliposhika mimba, kuna mabeberu yenye madoadoa, marakaraka katika ulimwengu wa roho, usiku
➰Labani anaonywa na Mungu, kutomwambia chochote Yakobo (Mwanz 31:24)
➰Mnyweshaji na Mwokaji wanaona kwa ndoto ya usiku, hatma za maisha yao (Mwanz 40:5)
➰Farao anaona mambo ya nchi yake, Usiku (Mwanz 41:5ff)
➰Mtu mmoja za Gideon aliota juu ya ushindi kabla, wakati wa usiku (Amuz 7:13)
➰Sulemani akiwa Gibeoni, usiku ndipo alipoona mambo yampasayo (1Falme 3:5).

✝ *JIZOEZE KUMTAMANI BWANA NAFSINI MWAKO, WAKATI WA USIKU (ISAY 26:9).*
✝ *USIENDE KULALA ,UKIWA UMETOKA KUTAZAMA MAMBO MACHAFU, KAMA PORNOGRAPHIC CONTENTS (ZABUR 119:37), YANAONDOA UWEZEKANO WA KUFUNULIWA KWA YALE MASIKIO*
✝ *JIZOEZE KUAMKA USIKU KWA HAYO MASAA TAJWA, ILI UJITAJIRISHE KIROHO (MAOMBOLEZO 2:19, ZABUR 119:62)*

*HITIMISHO*
Ukijifunza matumizi sahihi ya nyakati za usiku, utauona usiku mtamu sana, tena mfupi. Usiwaze juu ya kusinzia masaa ya kazi, anza taratibu, baadae mwili utazoea, mimi naweza lala masaa mawili tuu usiku, na mchana sihisi hata chembe ya usingizi. Sijakupa siri zote za utamu wa kuutumia uaiku vyema, ondoa hofu, usiku sio kwa ajili ya wachawi. Kumbuka utakapoanza ni rahisi kushambuliwa kiroho, maana kelele za kwenye ulimwengu wa mwili (Luka 23:23, 1Kor 14:10) ,zina matter katika roho kwa nyakati za usiku. Unaweza kuta umeomba sana usiku, ndio ukavamiwa na Shetani kwa namna ya hatari na vita kubwa, usithubu ku-RETREAT, ukaacha. Kamatia hapohapo mpaka Adui ndio waache kukujia sio wewe uache kwa kuhofia vita. Utafika wakati utakuwa huru na usiku wako.

MUNGU AWABARIKI, YULE AWEZAYE KULIPOKEA NENO HILO, ALIPOKEE!

Mwl Proo
0762879363
(ATG whatsapp group)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment