Wednesday, November 22, 2017

HANA KITU KWANGU!

*_HANA KITU KWANGU_*

Mwl Proo
0762879363(whatsapp)

Baruch B'shem Yahshuah! ✋🏾 (Ps 115:15)
Nawaandikieni wapenzi wangu, ili msitende dhambi, zinazompa Shetani ahueni/relief. Usiungane na ulimwengu, kumkampenia Shetani na mawakala wake kwa kuwapa sifa yoyote. Kufa na kufufuka kwa Yesu, kuliyageuza mambo UPSIDE-DOWN 👆🏼👇🏽. Hivyo Shetani hana kitu kwetu kama ambavyo hana kitu kwa Yesu. Kumbe huyu aliyeitwa Lucifer, anaitwa Shetani kwa maana ya adversary (mshtaki). Rejea somo la langu _*MKOGO*_. Tusome;

Yohana 14 : 30
*_......kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu._*

Mkuu wa Ulimwengu (Prince of this world-anamzungumzia Shetani), anasema *wala hana kitu kwangu/has nothing in me*; maana yake shetani hana mashiko/hold, hana madai/claims, haoni dhambi kwa Yesu,hakuna lolote ovu kuhusu Yesu (yupo mkamilifu kabisa wa utakatifu), bila hoja kinzani yupo juu ya dhambi na shetani mwenyewe *irrevocably!*.
SASA NI HALI HIYO NDIYO ILIMPA YESU KUSEMA, *_HANA KITU KWANGU!!_*  SASA NI KWA UKAMILIFU HUO WA YESU, TUNAPOBAKI NDANI YAKE TUNAFANANISHWA NA UKAMILIFU WAKE KAMA YEYE (UKIKAA NDANI YAKE). HAPO NDIPO NIWANG'ONG'E WALE WENYE KAULI YA, "HAKUNA MKAMILIFU/NO ONE IS PERFECT". WAKIWA NA MAANA KILA MMOJA ANA DHAMBI ZAKE, AMBAZO HAJAACHA. *_WHENEVER YOU ARE GIVING FORTH THAT UTTERACE, YOU ARE TELLING THE DEVIL THAT HE STILL HAS THE HOLD OVER YOU_* NAMAANISHA KILA UNAPOTAMKA HIYO SENTENSI, UNAMHIMIZA SHETANI KWA KUMWAMBIA BADO UNA KITU KWANGU. KILA UNACHOTAMKA IWE UMEMAANISHA AU WAFANYA MZAHA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO LINAHESABIKA NI NENO LA KIFALME TOKA KWA ALIYEFANYWA UFALME NA KUHANI,  YOTE YANA MAANA (1KOR 14:10, MATH 12:36). UNAWEZA KUMWAMURU SHETANI AONDOKE UKIWA UNA MWAMBIA UKO NA DENI LAKE?? MIMI NILIACHAGA HIZO VITU, NAUTUMIA UKAMILIFU WA YESU AMBAYE NINAKAA NDANI YAKE (YOH 15:1-7), KUMSUMBUA SHETANI KUWA WEWE HUNA KITU KWANGU! 👉🏾👹. KUNA SIKU NILISHTUKA USIKU NA CHUMBA CHANGU KILIJAA UWEPO WA SHETANI, NA NILIU-SENSE KABISA, AAAHH HUYU NI MWENYEWE. SIKUFANYA HOFU, ILA NAMI NIKAONGEA KWA KIBURI KABLA SIJAANZA KUSHINDANA, NIKASEMA, _*"Shetani si unajua kuwa leo utashindwa vibaya?"*_ HIYO ILIFANYA NIVIPIGE VITA NIKIWA SINA HOFU.

Mara kadhaa nimesikia, shuhuda za waliowahi kutumikia ufalme wa giza. Wale waliowahi kumwuliza mkuu wa ufalme huo, kwa nini nashindwa kuwadhuru jamii hii? (watu waliookoka kikwelikweli).  Kwa nyakati tofauti wote walijibiwa na yule jamaa, kuwa *_MUNGU WAO ANA NGUVU KULIKO MIMI!!_*💪🏾. Sitaki kutumia shuhuda za wachawi waliookoka kutengeneza fundisho, hapana!! Lakini ukweli usiopingika, ukikaa huku ndani ya njia hii vizuri. ULE UFALME MWINGINE HAUNA KITU KWAKO, HATA UJE UMEJIPANGA SANAA!. Mtu anaweza kuwa amejikoki kisawasawa katika ufalme ule mwingine, akikuta mmekaa kwenye kina kifupi cha kiroho, anaweza akawasumbuasumbua, ndio maana ni muhimu nawe uzame huku sana *_(pata somo langu la TWEKA MPAKA VILINDINI, ujifunze kwenda kwenye viwango ambavyo kila gia itakayotumiwa, ita-bounce)_*. Nakumbuka ushuhuda mmoja wa Kakonko Kigoma. Kanisa la kipentekoste wakiwa katika mkesha, wakasikia kitu kimeanguka nje paaaah⚡!!! Walipotoka wakamwona bibi kizee👵🏾, analalamika kwa kutaja jina la mwenzake, kuwa bibi fulani ndiye alinisababishia😕. Yaani walikuwa wanasafiri kwa zile rocket zao za kichawi. Ila walipofika maeneo hayo ya kanisa, yule wa mwenzake wa mbele, akagundua kuwa hapavukiki, akasogeza pembeni na kumshawishi atangulie, ndipo alipokuwa juu ya eneo la kanisa, ule ungo wake ukatunguliwa. Lakini wale wanamaombi waliomzunguka wakawa wanasikia vitu kama mishale inamtoka yule bibi inawaendea 🏹🏹. Yaani ana uvuvio mkubwa wa kuzimu kiasi cha hatari, alisimama na kuelekea mtaani kwenye makazi ya watu. Na kila alipokuwa anakatanisha kwenye mitaa watu ndani wakawa wanashikwa na homa za ghafula. Sasa hata adui ajikoki kwa style hii, ukiwa umekaa ndani ya Yesu vizuri, *_hana kitu kwako._*
Usikubali tena kuonewa. Kumbuka shetani, kabla hujaokoka alikuwa akikutesa maana ulikuwa duni yake (inferior to him), lakini ukiisha kukombolewa, hana kitu kwako hata akutese. Anachofanya ni kufanya vita na wewe, maana tayati position yako imewekwa juu kuliko yeye, na ahadi ya Mungu ni kumseta under our 👣 upesi (Rumi 16:20). Usikae kulialia mahali pa kutumia mamlaka. Sifundishi jambo lolote nisiloliishi mwenyewe (Rumi 2:21ff). Siku chache zimepita, nilihisi dalili za ugonjwa ambao nimeutibu medically💊💉 mwezi uliopita. Nikasema what??? Nikasema huu nitaushughulikia leo, kwanza nijue umekuja ni vita, au nimefanya yale makosa yaliouleta kwanza? Lakini iwe ni  mkono wa adui au ni natural disease, _*JESUS IS THE MASTER OF NATURE!*_ ila nilitaka kujiridhisha, ili nijue kiasi cha nuvu ya kutumia. Nikashindana katika roho, na kujivua ule ugonjwa, maana muda na nipo rohoni, niligundua nimevikwa tu, ili unikwamishe kwenye mpango wa ratiba ya kufunga/fasting niliyonayo. Kumbuka ukiwa na magonjwa kuna majukumu ya kiroho hutaweza kuyatekeleza, na itatumika akiba yako ya maombi ya nyuma (Zaburi 32:6, Efes 3:20) kukuvusha usifurikishwe 🌊na maji makuu.  Sasa nilifanya ishara ya kuuvua ugonjwa huku navua shati👔, niliamka asubuhi dalili zile strong, zikawa zimepotea kabisa, nikaendelea na fasting yangu. Sasa unachopaswa kufanya wewe uliyeokoka sio kulalamika, bali kila unapoona kuna kamkono ka devil, unamkumbusha kuwa wewe shetani usijitoe ufahamu *_HUNA KITU KWANGU_* you then command him out of your situations.
Sasa kwa mtu ambaye anakutana na wakati mgumu kufanya vita na kushinda, au mamlaka ni kama haifanyi kazi kwa ukamilifu, ni matokeo ya kutojichochea kiroho _*(tafuta somo langu liitwalo FANNING INTO FLAME)*_. Maana zile silaha za rohoni 💣🔫🔪⚔⛏🏹 zaweza kuwa butu/dull kama hujichochei.

Tembea katika ushindi uliopewa, maan adui yako hana kitu kwako. Pata sababu ya kutotenda dhambi, kuyarahishisha. Kinachotokea ukitenda dhambi, ni wewe mwenyewe unajihisi kutokuwa ndani ya Yesu, unakosa ujasiri kwake, na hivyo adui anapata kijinafasi cha kukanyagia/foothold👣 (Efeso 4:27)

Mungu awabariki kwa jina la Yesu.

Mwl Proo
All Truth Whatsapp Group (0762879363)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment