*WAKATI UMEWADIA WA KUMTAFUTA BWANA*
🇲 🇼 🇱 🇵 🇷 🇴 🇴
*0762879363*
©2015
Nakusalimu mtakatifu wa Mungu, wewe ambaye Mungu, alipendezwa kukufanya wake. Ubarikiwe kwa jina la Yesu.
Neno la Bwana lililonijia ni hili; Katika zama hizi za uovu (Efe 5:16), watu watakaojitoa kumtaja Bwana katika kweli, watamwona Mungu kwa namna ya ajabu sana sana!. Yaani katika zama hizi zilizojaa uchafu wa kutamani na harufu ya zinaa kona zote, zama ambazo kukuta bikra ni muujiza, zama ambazo watu wanafunga ndoa na ujauzito tumboni, zama ambazo teenagers wote wameathiriwa na uchafu wa sinema za ngono, zama ambazo vijana hata waliookoka wako bize na sexchat, zama ambazo ngono za watu wasiopaswa kuhusiana kama mtu na shemeji yake (zinatungiwa nyimbo kuhamasisha kwamba hainaga ushemeji), zama ambazo watumishi wa madhabahu wamejizamisha kwenye matendo ya ngono mpaka kwenye vyumba vya ushauri na maombezi, zama ambazo wahubiri wameacha kutafuta Neno kwa Bwana, wanasaka mahubiri Google 🔎🌍, ndio maana wanaishia kuwatabiria watu wachafu kiroho, baraka za kimungu, zama hizi ambazo Shetani amehakikisha anapunguza makali ya wahubiri moto, kwa kuwazamisha nao katika uzinzi (Hakuna mwinjilisti aliyeanguka kwenye uzinzi, mwenye uwezo wa kukemea dhambi kwa standard stahiki, atang'ata kidogo na kupuliza mwenyewe), katika zama hizi ambazo television programs zote zimejawa na sex-sceens, sex-talks, sexy-dresses na mauchafu yote, you name them! *_Sasa katika zama hizi, mtu atakayesema mimi dhambi na uchafu 👐🏽👐🏽, atakaye sema moyoni nwake kuzini Nooo👐🏽, uongo Nooo👐🏽👐🏽, dhambi zote No! na akajitia nia na moyo kumtafuta Bwana katika kweli, hakika yake Bwana ataonekana kwako kwa namna ambayo hata kwenye Biblia hujaisoma. Yaani hapo inaitwa umetoa kisafi kutoka katika uchafu huu mwingi, Mungu ameahidi kukufanya spokesman wake. Si hivyo tuu bali atakufanye uwe kati ya watu wasimamao karibu yake..._*
Yeremia 15 : 19
*```Kwa sababu hiyo Bwana asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.```*
Zekaria 3 : 7
*```Bwana wa majeshi asema hivi, Kama ukienda katika njia zangu, na kama ukishika maagizo yangu, ndipo utakapoihukumu nyumba yangu, nawe utazilinda nyua zangu, nami nitakupa nafasi ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.```*
*MOYO WA UJUMBE*
Hosea 10 : 12 *_Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki._*
*✔JIPANDIENI KATIKA HAKI*
Haki hiyo inayotajwa wajipandie (wahakikishe wako/wamesimama katika haki, ni ile ipatikanayo kwa matendo ya sheria-Mosaic Law), lakini kwetu leo ile haki ambayo ilipaswa kupatikana kwa juhudi za matendo, tumeipata yote bure kwa kumwamini Yesu (Mdo 13:39). Zaidi ya yote, Mungu alimfanya Yesu, ambaye haijui dhambi, awe dhambi, ili sisi tuwe haki ya Mungu (2Kor 5:21).
*✔UCHIMBUENI UDONGO WA MASHAMBA YENU*
Anazungumzia readiness (Utayari wa kupokea toka kwa Bwana) kama kuna mambo uliyaacha ya haki, anza kuyatenda tayari kwa kukutana na Bwana (Break up your fallow ground), udongo wa shamba hili ulikuwa _*fallowed*_, ulipumzishwa bila kufanyiwa kazi, Sasa majira ya kukutana na mvua ya Mungu kiroho 🌧☔ yakija, Bwana anataka uchimbue huo udongo wa maisha yako ya kiroho. Kama uliacha kusoma neno, anza upya, kama uliacha kuomba na kufunga, anza upya, kama uliacha kumshuhudia Yesu, anza upya!.
*✔KWA MAANA WAKATI UMEWADIA WA KUMTAFUTA BWANA*
Ndugu yangu saa ya kwenye ulimwengu wa roho⏰, inasema hivi sasa ni saa ya kumtafuta BWANA (Day&Night). Na wakati huu anapatikana, nakusihi msomaji wangu, usiwe miongoni mwao wanaositasita (Ebrania 10:39). Usiwe miongoni mwa wale ambao wamemruhusu Shetani kavuruga mawimbi(waves) za kiroho, wananasa chenga na kukosa clear vision. Jitunze kwa Bwana katika hizi zama za uovu, Mungu anapatikana sana tuuuu
Isaya 55 : 6
*_Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;_*
Sefania 2 : 3 *_Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana._*
IKIFIKA HAPA, NDIPO NINAPOTAMBUA, KUWA KUNYAKULIWA SIKU YA UNYAKUO SIO BAHATI NASIBU, HUWEZI UKAISHI KWA ULE MSEMO WA *_"what will be, will be!"_* ETI LIWALO NA LIWE! KWA NINI USIBIRO AJALI, WAKATI MUNGU ANAPATIKANA SASA, NA UNAWEZA KUJIHAKIKISHIA UHUSIANO WAKO NA MUNGU SASA. MTU ASINITISHE MAANA YULE MUNGU WA BIBLIA, NAMWITA ANASHUKA KUNITENGENEZA MAISHA YANGU KILA SIKU. KWA HIYO SITASHTUKIZA ACCIDENTALLY KWAMBA MUNGU NIFIKIRIE, KAMA UHUSIANO NA MUNGU, UNA SHIDA NIUJENGE SASA!!! TENA NIWASIHI SANA, MSIACHE KUFANYA HUDUMA ZA KIROHO KATIKA KWELI, MAANA ZINA MCHANGO WA KUUTUNZA WOKOVU WENU. KWA MFANO MIMI SIWEZI KURUHUSU DHAMBI, UPUZI NA UDHALIMU KATIKA HEMA YANGU (MAISHA YANGU), MAANA NAJUA KUWA NAPASWA KUFANYA HUDUMA YA ROHO, KAMA HII. SASA HATA UJUMBE WA KUANDIKA NAJUA NAPASWA KUULIZA KWA BWANA, SO NAOGOPA KAMA NITACHAKACHUA MAPITO YANGU, NIKIMUULIZA HATANIJIBU (YOH 9:31, ZAB 66:18), NA SIPO TAYARI KUACHA MUNGU AONDOKE ANIACHE, NILIKUJA KWAKE KAPUKU (EMPTY SET), SASA KANIJAZA KILA WEMA NA UNONO.
Kungekuwa na Mana na Kware wanaoanguka tu wenyewe, natamani kazi yetu ingebakia kumtafuta Bwana tu. Sasa bado tunayo masumbufu ya maisha haya, unyakuo huenda usiwe labda hata usitokee for the next 500 years (ingawa hata ukitokea sasa tuwe tayari), kwa hiyo ni lazima na maisha tuyasake, tusife njaa kwa kusingizia imani. Lakini pamoja na cash unazosaka, MUNGU KWANZA, UFALME KWANZA (Luk 12:31)
Kijana wa kiume na wa kike, wewe mama na baba, hauna sababu ya kutomtafuta Bwana. Tena kama Mungu amekujalia ahueni kiuchumi, utulivu kwenye ndoa, wewe ndio umepewa neema hiyo ili umtafute sanaaaaaaaa. Maana wengine wenye majanga watamtafuta awaponye na majanga, ila wewe unamtafuta ili ukae na Bwana... Wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, natamani kuona vijana wako bize na ratiba za maombi na kufunga na huduma. Muda wa kuzunguka mlima Seiri kupoteza muda, mmezunguka sana, SASA VYATOSHA, SASA YATOSHA (Kumb 1:6, 2:3ff)
Mungu akupe neema kila mmoja, inuka sasa umtafute Bwana, maana shughuli hiyo inakuhusu wewe. Uaipojiingiza katika wingi hili la kumtafuta Bwana, utabaki kushinda na tudhambi ambazo wenzio tulishasahau zinafananaje.
KARIBUNI SANA, TWENDENI BARAZANI PA MUNGU.
Mwl Prosper Kadewele
0762879363( All Truth Whatsapp Group)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment