*UZIMA WENU NI NINI?*
_Na Mwl Proo_
0762879363 (whatsapp)
Praise Adonai!
Mungu hapendi kuona unaishi miaka 70/80, yenye taabu (Ayubu 14:1, Zab 90:10), Kisha ukatumia maisha yako ya umilele mahali pabaya. Ndio maana katika mafundisho yangu kadhaa, nimekuwa nikitia juhudi ya kufundisha mambo ya maisha ya baada ya hapa duniani (Afterlife issues). Jitahidi upate masomo yangu mawili, lile la UMILELE, na lile la MWILI WA ROHO, ujipatie uhakikia wa yale yanayoendelea mara utakapokata pumzi ya uhai wa mwili huo. Yapate kupitia links hizi
👇👇👇👇
http://alltruthjohn1613.blogspot.nl/2016/09/sehemu-ya-somo-la-umilele.html?m=1
Na
http://alltruthjohn1613.blogspot.nl/2016/09/mwili-wa-roho.html?m=0
*MOYO WA SOMO*
Tusome andiko ambalo, limezaa somo hili nikiwa nipo ndani ya basi 🚌, natafakari.
Yakobo 4 : 14
_*walakini hamjui yatakayokuwako kesho. ~Uzima wenu ni nini?~ Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.*_
MMMH 🤔!!! WAPENZI WASOMAJI, MWANADAMU HATA AKIWA NA MVUTO VIPI, AU AKAWA FAMOUS (ANAJULIKANA SANA), MACHONI PA MUNGU, ANAONEKANA KAMA KAMDUDU FULANI 🐞, KAMA FUNZA TU AU BUU 🐛, YAANI KAMDUDU AMBAKO HAKAJAMALIZA HATUA ZA UKUAJI.
Ayubu 25 : 6
*_Siuze (sembuse) mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!_*
YAKOBO ANAHOJI SWALI LA MSINGI, KUWA UZIMA WENU NI NINI (UNA MAANA GANI)? KAMA MTU LEO TUNASHEREHEKEA HARUSI YAKE 👫💍💍, HALAFU UNASIKIA YULE ALIYEFUNGA NDOA, KAFARIKI ☠⚰. YAANI KINACHOWEZA ZUKA KWA SIKU MOJA TU HUKIJUI (Mithali 27:1). NI MUHIMU KUKUMBUKA UKIISHI DUNIANI KAMA NGANO MTAKATIFU (UTAVUNWA ⚰), NA PIA UKIISHI KAMA GUGU-MAISHA YA DHAMBI (BADO UTAVUNWA ⚰). HATARI NI HII, JE UTAVUNWA ILI UKAHIFADHIWE KATIKA GHALA KAMA NGANO SAFI, AU UTAVUNWA KAMA GUGU ILI UKAENJOI FIRE-MUSIC 🔥MILELE?
MWANADAMU HAWEZI KUKAA MILELE, KATIKA MWILI HUU WA MAVUMBI, LAZIMA URUDI MAVUMBINI. INGAWA KATIKA UKRISTO KUFA SIO LAZIMA, WAKRISTO WAVIVU WA KUSOMA MAANDIKO HUSEMA *_Kila nafsi itaonja mauti_*, HILO SIO FUNDISHO LA BIBLIA BALI NI QURAN (Surat al Imran (3)185), KATIKA UKRISTO TUNA MAMIA KWA MAELFU KAMA SIO MAMILIONI AMBAO HAWATAKUFA, WATABADILISHWA TU (1KOR 15:51-52). LAKINI KAMA YESU HATARUDI NDANI YA MIAKA 200 TOKA SASA, HAWA WANADAMU UNAWAONA, WOTE SHARTI WAFE, SIO KWAMBA WOTE WANAKUFA KAMA ADHABU; HAMNA LAKINI KIFO NDIO MLANGO WA KUUINGIA UMILELE, INFACT KIFO NI ADUI WA MWISHO KUSHUGHULIKIWA (1KOR 15:26). LAKINI WOTE AMBAO WAMESOMA SOMO LANGU LA UMILELE HAWAJAWAHI KUWAZA KUOGOPA KIFO TENA, KWAO WAKIFA NI KWA BWANA NA WAKIISHI NI KWA BWANA.
Tusome haya maandiko:-
Ayubu 14 : 2
*_Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe._*
Ayubu 14 : 5-6
_*Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;*_
*_Acha kumwangalia yeye, apate kupumzika, Hata atakapoitimiza siku yake, kama aliyeajiriwa._*
YAANI HAKUNA KITU KISICHODUMU KAMA MVUKE, AU KIVULI, AU UA🌺, UNAWEZA KULIKUTA ASUBUHI LIKO SAFI, UKAPITA JIONI LIMENYAUKA AU LIMEANGUKA TAYARI, NDIVYO ALIVYO MTU AFAYE. HATA KUFANYIKE JITIHADA ZA KUOKOA UHAI WAKO KWA KUKUPELEKA MADRASAT HOSPITAL AU APPOLOS HOSPITAL ZA KULE INDIA 💊💉🚑, UTANUSURIKA KWA MUDA, LAKINI LAZIMA UTAFIKA WAKATI UTAENDA TU MAN! HAKUNA NAMNA NYINGINE, MADAKTARI WATAKUFANYIA SURGERY ZOTE, MPAKA KUKUWEKEA VIUNGO BANDIA, AT THE END OF THE DAY, HUWA LINATOKA TAMKO LA KUKUTAKA URUDI MAVUMBINI
Zaburi 90 : 3 *_Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu._*
TUKIISHA SHTUKA KUHUSU LIFE'S UNCERTAINTY (MAISHA YASIYO YAKINI/UHAKIKA), TUNAPASWA KUWA MAKINI JUU YA UCHAGUZI SAHIHI WA MTUMIZI YA SIKU ZETU. MWIMBA ZABURI KWA HEKIMA ALISEMA;
Zaburi 90 : 12
*_Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima._*
KWANZA NIWAPONGEZE AMBAO WAMEJUA WITO WAO NA WAMEANZA KUUTUMIKIA KWA JUHUDI (MDO 13:36). KAMA HUJAFIKA HATA MIAKA 40, LAKINI UMO SHAMBANI MWA BWANA UKIMFANYIA BWANA KAZI, UNYO FAIDA YAKO. KILA MTU AKISHAOKOKA ANAPASWA KUUKUBALI ULE MWITO MKUU (HIGHER CALLING), NA WITO WA MUNGU HAUNA MAJUTO KAMWE (RUMI 11:29). HONGERA WEWW AMBAYE NI FULL-TIME MINISTER, UMEUBEBA MSALABA WAKO, WAKATI MWINGINE KWA SABABU YA HUDUMA UKALALA NJAA, INGAWA ULIKUWA NA UWEZO WA KUINGIA KITAA UKASAKA NOTI💰💵🏧. LAKINI MAISHA YAKO UMEYADHABIHU KWA BWANA, UKAKUBALI KUPATA HASARA YA VYOTE. NA KWA WALE AMBAO NI PART-TIME MINISTERS ENDELEENI KUWA WAAMINIFU, MAANA HATUWEZI KUWA WOOTEEE NI WACHUNGAJI, WOOOTE WAIMBAJI ETC. HAPANA, WENGINE WAMEITWA KUFANYA MENGINE NA WENGINE KUSAPOTI WATUMISHI ILI WAPATE THAWABU YA NABII (Mathayo 10:40-42). INGAWA NI MUHIMU KILA MMOKA KUJITOA KATIKA HUDUMA FULANI JITAHIDI UPATE MUDA, USOME SOMO LANGU, LIITWALO; "MAOMBI NA HUDUMA NI MUHIMU SANA. LIPATE KUPITIA LINK HII
http://alltruthjohn1613.blogspot.com/2016/09/maombi-na-huduma-ni-muhimu-sana.html
KAMA UTARUHUSU KUYASUMBUKIA MAISHA HAYA MPAKA MVI ZINAKUPATA 👴🏽👵🏾, UTAKUWA UMEISHI KWA HASARA KUBWA SANA. INFACT KILA AMBAYE ATAJISET VIZURI KIROHO NA KATIKA KUMTAFUTA BWANA KWA BIDII, ATAGUNDUA ANA KAZI YA KUFANYA. KWELI WEWE NI ENGINEER WA UJENZI NA MAJENGO, LAKINI KAMA MAISHA YAKO YOTE YATAKUKUTA UPO SITE ZA KUJENGA BARABARA, MPAKA MVI ZIKAKUKUTA HUKO, HUMTAFUTI WALA KUMTUMIKIA MUNGU, USIJIDHANIE KUWA KUNA TAJI YA KUWA ULIITUMIKIA KWA UAMINIFU KAMPUNI YENU. ILA MUNGU ALIKUPACHIKA HAPO UHUDIMIE FAMILIA YAKO IPATE UGALI 🍚, NA UWEZE KU-FINANCE HUDUMA, KAMA UNAPATA TENDA ZA MILIONI 700, WAKATI KANISANI KIWANJA CHA MILIONI 5 WANAWEKA MKAKATI WA MIAKA MITATU KUZIPATA, WEWE UPO UMEUCHUNA TU😷, UNAFURAHIA KUONA IBADA ZINAFANYIKA KWENYE UKUMBI WA HOTELI AU CLUB TENA WANAKODI KWA GHARAMA KUBWA???? UNGEIJUA SIRI YA UZIMA WAKO HUO, UNGEINVEST RESOURCES ZAKO ZOTE KWA BWANA. MIMI BINAFSI KWA SASA NI MTUMISHI WA SERIKALI, LAKINI KAMWE SITATHUBUTU KUYATUMIA MAISHA YANGU YOTE KWA KAISARI, SIPO TAYARI KUPATA TAJI YA NYASI AU MTI WAKATI ZIPO MBINGUNI TAJI ZA DHAHABU NA SHABA (1KOR 3:13).
UZIMA ULIONAO, NA MAISHA YAKO KATIKA MWILI HUO WA SASA YAISHI KWA AJILI YA KRISTO, IPO SIKU UNAWEZA KUKATWA GHAFULA, UKAVUNWA MAANA WAIHARIBU NCHI BURE, HAUZAI MATUNDA. KUNA WAKATI NILIWAHI KUKAA MUHIMBILI KARIBU WIKI TATU TUKIUGUZA. NDIPO NIKAJUA KIBURI CHA WANADAMU NI WAKIWA HUKU MTAANI, NILISHUHUDIA WAGONJWA WAKIFA KILA BAADA YA DAKIKA CHACHE, KUNA WALE WAHUDUMU WA MORTUARY, WANAKUJA NA KITANDA KAMA KABATI LENYE MATAIRI KUBEBA MIILI, HIYO NI SHUGHULI YAO KUTWA NZIMA. KIFO NI KITU HALISI, MSIJISAHAU NA KUJISHAUA KIASI CHA KUTOMTUMIKIA MUNGU, KUMBUKA TAKWIMU ZINAONESHA KILA SIKU (24HRS), KUNA WANADAMU 150,000 WANAFARIKI DUNIA, YAANI WATU 108 KILA DAKIKA DUNUANI WANASEPA ⚰⚰☠☠. UZIMA WAKO NI NINI? UTAFANYA JAMBO LA HEKIMA KAMA UTAYATUMIA MAISHA YAKO KWA MUNGU
Mungu awabariki sana!
Mwl Proo
0762879363(ATG whatsapp group)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment