Sunday, November 26, 2017

ILI UMWONE MUNGU, LAZIMA MISINGI IBADILIKE

*ILI UWEZE KUMWONA MUNGU (BILA UKOMO), NI LAZIMA MISINGI YA MFUMO WAKO IBADILIKE!*

10/10/2016
_```Na Mwl Proo```_
*0762879363*

Bwana Yesu apewe sifa. Kuna watu ambao hawaridhiki na viwango ambavyo wanamwona Mungu, wanatamani kuongezeka hata kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. Here is your portion

➰ *MSINGI*
>Msingi unaokuwa chini, ndio unaobeba vyote vinavyokuwa juu, mambo ya juu tutaya-thaminisha kwa msingi wake.  Wajenzi husema, *_"It is the foundation which determines the structure to be built"_*.

>Msingi unaweza kuwa mbovu au kuharibika
Zaburi 11:3
*_3 Kama misingi ikiharibika,Mwenye haki atafanya nini?_*

➰ _*ASILI ZETU (Tamaduni, Desturi+Mila, Malezi+Makuzi na Dini) ZILISIMAMA KAMA MISINGI,  ZIKATUUNDIA MFUMO AMBAO UNAZUILIA SANA, TUSIMWONE MUNGU KWA KIWANGO KINACHOTAKIWA.*_

Kuna muda mtu anaweza kuhisi labda zile nyakati za Ibrahimu au Eliya Mtishbi zilikuwa ni nzuri zaidi, au Mungu alikuwa karibu zaidi. Jibu ni La Hasha! Nyakati tulizo nazo ni nzuri zaidi maana wao, katika roho walichungulia nyakati hizi👀 wakazi-admire mno😍😋. Walitamani ingewezekana hizi nyakati ziwakute.

Luka 10 : 24
*_Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie._*

Hata malaika wanayachungulia haya mambo kwa shauku 👼🏻👀
1Petro 1:12b
*_..............Mambo hayo wanatamani kuyaangalia._*

SASA SHIDA IPO KATIKA MFUMO ULIOTOKANA NA MISINGI ISIYO SAHIHI. KAMA MIUJIZA INAADIMIKA KANISANI KWENU, AU MAISHANI MWAKO BINAFSI, HUZISHUHUDII KAZI ZA LIVE NA MATENDO YA KIMUNGU YA LIVE, MBALI NA KUAMINI KUWA UZIMA NILIONAO NI MUNGU KANILINDA. LAKINI MAISHA YETU YALIPASWA KUJAA NA AJABU ZA MUNGU KILA UPANDE, SIO ILI KUTUFANYA TUAMINI, MAANA HERI NI WALE AMBAO PASIPO ISHARA YA MIUJIZA BADO WANAAMINI (YOH 4:48, 20:29).

➰ *MUNGU ANA TARATIBU ZAKE*
Hata Shetani akijitahidi kucopy na kufanya counterfeit (feki), bado la Mungu tutalijua tuu. Sasa Mungu anazo taratibu zake, ambazo ili aonekane, sharti uwe ndani ya hizo. Ukiwa nje ya hizo *_HUTAMWONA_* au _*UTAMWONA KWA KIPIMO KIDOGO SANA*_.

Waamuzi 6 : 26 *_ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake;_*

Nehemiah 13 : 14
_*...... Ee Mungu wangu, wala usifute fadhili zangu nilizozitenda kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, na kwa taratibu zake.*_

SASA KUNA MAHALI YESU ALIENDA, AKAKUTA WANA MFUMO WAO WA KUTOAMINI HATA WAKISHUHUDIA WAZI MUUJIZA BADO, WATADAI AAAH HAPO AMETUMIA NGUVU ZA MKUU WA PEPO BELZEBUL/BELZEBUB👹. YESU AKIONA MFUMO WAKO MBOVU ANAWEZA ASITENDE KAZI AU ATENDE KIDOGO SANA

Mathayo 13 : 58
*_Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao._*

BILA SHAKA MNAMKUMBUKA MKOMA NAAMANI. ALITAKA KULETA UJUAJI WA MFUMO WAKE. AMEPEWA MAELEKEZO AENDE KUJICHOVYA KWENYE MTO YORDAN 🌊🏊🏽MARA SABA. YEYE ANAANZA OOH MIMI NILIDHANI ATATOKA HUKU NJE ANIWEKEE MKONO ✋🏾. MAANA MISINGI MIBOVU INAKUPA MFUMO WA KUKARIRI (WA DINI).

2Falme 5:12
*_12 Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira._*

NABII WA BWANA ELISHA BEN'SHAFAT KAMWELEKEZA MTO WA KUUENDEA, YEYE ANALISTI MITO YAKE. MUNGU ANAWEZA KUKUTAJIA MTO KUMBE HUKO NDIPO KAMSET MALAIKA👼🏻 AKUGUSE KWA UPONYAJI. SASA HUU NI MFANO TU KATIKA MENGI SANA, YANAYOKINGA TUSIMWONE MUNGU KWA VIWANGO.

MPAKA SASA KUNA MFUMO WA DINI, AMBAO SIO WA MUNGU; UMEZUIA MAELFU YA MAMILIONI YA WATU, WASIPONYWE NA MUNGU, WASIBARIKIWE, WASIMWONE MUNGU KUWA LAIVU KATIKA MAISHA YAO, HAWASHUHUDII CHOCHOTE ILI KUWAONESHA KWA HAKIKA WANA MUNGU MAIAHANI MWAO. ILA ULE MFUMO WA DINI UNAWATAKA WAENDELEE TU KUUSHIKA. ZIKO TARATIBU ZA KIJAMII AMBAZO HAZIENDANI NA TARATIBU ZA IMANI KATIKA MUNGU, NA HIVYO MUNGU HAONEKANI AKITENDA KWA WAZI MAISHANI MWA WENGI. GIDEON ALIELEKEZWA KUWA   BAADA YA KUBOMOA MADHABAHU ZA BAALI, KULIKOPELEKEA APEWE NICK-NAME YA YERUBAALI, MAANA ALIZITUMBUA MADHABAHU ZAKE. MUNGU AKAMWELEKEZA AJENGE MADHABAHU SASA, KWA TARATIBU ZAKE. MAANA YAKE ISIPOKUWA KWA TARATIBU ZAKE, HATASHUKA!!!. KUMBUKA ELIYA ALIOMBA MOTO UJE ULAMBE ILE DHABIHU NA YALE MAJI, LAKINI HAKUJENGA MADHABAHU KWA NAMNA YOYOTE, KASOME TARATIBU ALIZOTUMIA!

MIMI ZAIDI YA KUOMBEA WAGONJWA WAPONE, NAFURAHIA NINAVYO USHUHUDIA UPONYAJI HATA KWANGU MWENYEWE KWA MIUJIZA. KAZI AMBAZO SI ZA KAWAIDA (SUPERNATURAL) LAZIMA ZIYATAWALE MAISHA YANGU. SIKU MOJA NILIFANYA KOSA LA KUTUMA UJUMBE WA SIMU MAHALI AMBAKO SI SAHIHI, NA UNGEWEZA KULETA ATHARI KUBWA MNO 📱📲. UKAWEKA TICK ✔ YA KWANZA, LAKINI HATA KATIKA MAZINGIRA HAYO BADO LIKO JAMBO LA KUFANYA. MAENEO YA NAMNA HII, KAMA UMEJIZOEZA MAAJABU, NDIPO PA KUAPPLY SASA. NILIJUA HAKUNA NAMNA, HIVYO NILIMWAGIZA MALAIKA AIZUE ISIWE DELIVERED (✔✔). ZILIINGIA ZINGINE ZOTE ISIPOKUWA ILE MOJA IKASHIKILIWA. WAKATI FULANI NILIZIWEKEA MIKONO BETRI ZILIZOKWISHA NGUVU KABISA 🔋🔋🔌NA KUZICHAJI KWA VIDOLE, ILI ZIFANYE UTUMISHI NILIOUKUSUDIA, MAANA HAKUKUWA NA NAMNA NYINGINE USIKU HUO, NA ZIKAFANYA KAZI ALL NIGHT-LONG. NISEMALO NI HILI TUNAPASWA KUONA KAZI ZA AJABU KWA WAZI WAKATI  WOTE, KAMA WANA WA MUNGU.

KUNA WAZAZI WALIWAELEKEZA WATOTO WAO KWAMBA, USISHIKE SANA MAMBO YA DINI (MUNGU), UTAFELI! HUO NI MSINGI UMEKUUNDIA MFUMO MPAKA SASA, UNAFANYA VITU VYA MUNGU KWA KUGUSAGUSA TU, 85% YA MAISHA YAKO UNAFANYA MAMBO YAKO, YA KUMHUDUMIA MUNGU WAKO AITWAYE TUMBO. KUNA MAKABILA YANA UTAMADUNI KUWA SI VIZURI KUPIGA KELELE USIKU; SASA UNAKUTA MPO NA MTU, MKIOMBA USIKU ANAOGOPA KUTOA SAUTI, MATOKEO YAKE ANAOMBA DAKIKA 10 ANASINZIA. SHIDA IKO KATIKA ULE MSINGI WA KIMILA AMEOKOKA ILA HAJAACHA VYOTE VILIVYO VYA MILA ZAO. KUNA DESTURI ZINGINE ZA BAADHI YA JAMII, ZA KURITHISHA MAJINA YA MABIBI NA MABABU KWA WATOTO, MTU AMEOKOKA, LAKINI BADO HUO UTARATIBU BADO KAUSHIKA TU. KUMBE HAO MABABU NA MABIBI👴🏿👵🏿WALIWEKA MAAGANO NA ROHO ZA FAMILIA (FAMILY SPIRITS-MAPEPO) KUWA AGANO LAO LIPO KATIKA MAJINA. KWA HIYO UNAKUTA MTU ANATESWA NA MIZIMU, ANALAZIMISHWA KURITHI MIKOBA YA UCHAWI/UGANGA, KUMBE MMELIFANYA IMARA AGANO KWA JINA, KWA SABABU YA MSINGI WA MFUMO MBOVU. SASA MUNGU ANASEMA NAWE, KUWA ILI UMWONE KWA VIWANGO ANAVYOTAKA, MISINGI YA MFUMO WAKO, LAZIMA IBADILIKE.

*NI KWA NAMNA GANI BASI, WAWEZA BADILISHA MISINGI YA MFUMO WAKO, INAYOKUZUILIA MENGI YA MUNGU?*

Baada ya kuokoka (kuzaliwa mara ya pili), namna pekee ya kuweza kuishughulikia misingi mibovu ya kwanza inayoathiri mfumo wako wa maisha ya imani, unaokinzana na utendaji wa Mungu; *_NI LAZIMA ULIRUHUSU NENO HAI (GOD-BREATHED/RHEMA-WORD), LIKUBADILISHE.

2Timotheo 3:16-17

*_16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;_*
_*17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.*_

HAPO SIO TU SWALA KUJAA MAANDIKO KICHWANI, ANDIKO LIKISHAKAA NDANI YAKO LIMEVUVIWA NA ROHO, NA KUWEZESHWA KULIISHI LINAKUWA NENO, UNAPASWA KULIRUHUSU HILO LIKUBADILI. KAMA KWENU MNA DESTURI YA UKALI NA UKATILI (SIJUI UNADAI WEWE MKURYA 👊🏾✊🏽💪🏾🗡), MKURYA ANAYELIRUHUSU NENO HAI LA MUNGU LIMBADILISHE, ATAKUWA NA MOYO LAINI WA NYAMA (ULIOPONDEKA NA KUVUNJIKA Zaburi 51:17). HATAKUMBUKA KAMA KUNA KITU KINAITWA UGOMVI WALA KUPIGANA. HUENDA DESTURI YENU NI UBAHIRI UKO SO STINGY, HAUTOI KAMWE, LAKINI UKILIRUHUSU NENO HAI LA MUNGU LIKUBADILISHE-!- UKAKUTANA NA NONDO KAMA (MITHALI 11:24), NDIPO TUNAMUONA MTU WA KABILA LENYE WABAHIRI, ANATOA KIWANJA CHAKE KIJENGWE KANISA KWA MOYO MWEUPE BUREEEEE👌🏽. NI KWELI UMEOKOKA UKIWA NA DOCTORATE/PhD 🎓🎓🎓, UNATAMANI UKIJA IBADANI UPEWE HESHIMA YA KISOMI (YOU CLAIM TO DESERVE RECOGNITION), HAKO KAMFUMO KAKUTAKA HUMAN RECOGNITION,  KANAZUIA USIMWONE MUNGU. WENGINE WANA MITAZAMO NA MSIMAMO YAO TU MINGI AMBAYO SIO YA NENO HAI LA MUNGU, NA HIVYO WAMEJIFUNGIA MLANGO WA KUMWONA MUNGU KATIKA UKAMILIFU WAKE. NINAMAANISHA NINI HAPA KWENYE NENO HAI LA MUNGU? NENO LA MUNGU LIPO HAI (EBRANIA 4:12), LAKINI SIO KUSOMA TU MAANDIKO BILA ROHO MTAKATIFU KUKUFAFANUSHIA, MAANA HUMO KWENYE BIBLIA MENGINE NI MAUTAMADUNI TU YA KIYAHUDI, HAYANA KAZI KWA MAISHA YETU, UKIKAA KUKLEMU KUMTAHIRI MTOTO SIKU YA 8 BAADA YA KUZALIWA, HIYO HATA HAINA KAZI. BALI UKILISOMA NENO LA MUNGU HUKU ROHO MTAKATIFU AKIKUPA UFUNUO WA IPI NI KWELI YA MUNGU, NDIPO HAPO MISINGI YA MFUMO WAKO INABADILISHWA NA UNAPOKEA MISINGI MIPYA, ITAKAYOKUUNDIA MFUMO RAFIKI KWA UTENDAJI WA MUNGU!

Mwl Proo
(Prosper Kadewele)
(All Truth Whatsapp Group-0762879363)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment