*BIKIRA SAFI*
_*Mwl Proo*_
*0762879363*
Bwana Yesu awabariki nyote, nawasalimu kwa jina la BWANA, Mungu, ambaye jina lake ni Mtakatifu!
Hili ndilo neno la Bwana kwetu leo, Bikira safi. Siwazungumzii bikira wale ambao hatukuwahi kufanya tendo la ngono kabisa, No! Twende darasani tupate ufunuo.
Bwana alinipa kazi ya kuwa mjumbe wa matengenezo; yaani wale ambao kwa namna yoyote walighafilika, wakajikwaa, wakatoka katika hali ile nzuri ya kukaa na Bwana, bado wasije kupotea kabisa. Kwa hiyo nimekuwa nikiwasaidia watu wa hivyo wajue kuwa pamoja na maanguko yao, Bwana hajawakataa. Watengeneze mambo yao, wasipoteze ule umilele na Mungu, eti kisa ulizini.
*Pamoja na jukumu hilo, matengenezo sio kusubiri watu waanguke, bali ni pamoja na kuzuia, kuwa na walokole wenye viraka na makovu ya kiroho.*
Ukiwa ndani ya Yesu, unakuwa kiumbe kipya, ya kale yanapita (2Kor 5:17), si ndio mstari wetu tulio ukariri? Sasa je ukijiondoa kwa Yesu unakuwaje? Au baada ya maanguko ya kiroho unakuwaje? Msamaha upo tu, kama hujfikia viwango vya kumkufuru Roho, kama nilivyofundisha katika somo langu la ~*_Mambo ya kiroho yakiharibika; Tengeneza (Jitahidi ulipate)_*~.
Hivyo badala ya kusubiri watu waanguke ili watengeneze, ambako viraka na makovu husalia tu (1Falm 15:5), ni bora kukujuza siri, ya kujitunza, usianguke, ili usalie bikira safi kwa mume mmoja uliyeposwa kwake ambaye ni Yesu. Tusome;
2 Wakorintho 11 : 2 *_Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi._*
Can you see?, Kumbe tulipoposwa kwa Bwana, tunayo hali ya ubikira katika roho, ukoje huo ubikira, unaharibiwaje? Tujifunze sasa.
MTU ALIYEKWISHA KULIPIWA ILE GHARAMA YA UKOMBOZI *_(PEDUT)_*, AKAZIONJA NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO, AKALISIKIA NA NENO ZURI LA MUNGU, AKAANGUKA BAADA YA HAYO, YAANI YULE ALIYEKWISHA KUFANYWA MWANA AKADROP OUT KIASI CHA KUPOTEZA ID💳 (Utambulisho) KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, KIASI CHA KUVAMIWA HATA NA PEPO (DEMON-POSSESSED), HUYU MTU HATA AKITUBU HALI YAKE BAADA YA TOBA HAITAKUWA KAMA MWANZO, ATAKUWA NA VIRAKA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO. MTU ALIYENUNULIWA KWA THAMANI (1KOR 6:20), AJE KUWA DEMON-POSSESSED TENA, YAANI NAFSI YAKE IKAMILIKIWA KULE ILIKONUNULIWA, AISEE ANAPOTEZA SIFA YA UBIKIRA. NI HERI UWE NA HISTORIA YA KUMILIKIWA NA MAPEPO KABLA HUJAOKOKA, MAANA HUKUWA NA SABABU YA KUTOMILIKIWA. ULIPOOKOKA YESU ALITIMIZA SHERIA ZA UKOMBOZI, ILI KUSIWE NA DENI TENI, KWA HIYO ULIHAMISHWA KWA HALALI TOKA KATIKA UFALME ULE ULIOKUTUMISHA MWANZO (KOL 1:13) *_(HAKIKISHA UMEPATA SOMO LANGU LIITWALO ~"MKOGO"~)_*, SASA KITENDO CHA KUMILIKIWA TENA, UJUE PIA MAPEPO SIO TU YAMEVAMIA, BALI YAMEZINGATIA SHERIA PIA (MAANA UNAYO CERTIFICATE OF REDEMPTION, AMBAYO LEGALLY INAWAONDOLEA UHALALI KUKAA NDANI YAKO), NAJUA MTANIELEWA, TWENDE MBELE KIDOGO.
Uhusiano wa Mungu na watu wake Israel, unalingana na uhusiano wa mume na mke, ndio maana Isaya nabii akaitangazia Israel kusema, Muumba wako ndiye mume wako (Isa 54:5). Wana waisrael walipothubutu kumtolea ibada mungu yeyote mwingine, waliitwa wazinzi/makahaba, wanaoenda kuzini mbali na Mungu wao na ndio hasa mfano ule wa Hosea kumwoa 💍 Gomer Bint'Diblaimu (Hosea 1:1-11).
Hosea 4 : 12b
*_maana roho ya uzinzi imewakosesha, nao wamekwenda kuzini mbali na Mungu wao._*
👆🏼Mungu mwenye wivu (Jealous God, anasikitishwa na tabia ya Israel kutafuta mchepuko), Yeye yupo kama mume kwao, anasikitika kwamba wameenda kuzini, mbali na Mungu wao!
*OHOLA NA OHOLIBA (Ezekiel 23:2-49)*
Mungu katika kuonesha umuhimu wa ubikira wa kiroho, ambao unaupata baada ya kuokoka, hata kama ulikuwa mzinzi kwa jinsi ya roho kabla, unapookoka na kuposwa kwa Yesu, unafanyika bikra kwa namna ya rohoni. Sasa Mungu alitumia ufunuo wa maumbo na mfano (Allegoric language) wa mabinti wawili, mkubwa Ohola na umbu lake Oholiba. Mungu akasikitika namna walivyo uharibu ubikira wao wa thamani, yaani Mungu anajua siri aliyoiweka kwenye ubikira (wa kiroho na kimwili), maana alisikitika hata namna walivyoruhusu matiti yao ya ubikira kuwa _*fondled and caressed (Eze 23:3)*_, Mungu alitaka yeye kamamume ndite awe mhusika na sio miungu ya misri wala vile vinyago vya kipagani (Pata muda usome binafsi sura yote, uone Mungu anavyoulilia ubikira wa kiroho, huo wa kimwili sio kesi yetu ya leo). Lakini mbele kidogo Mungu akaufafanua hiyo lugha ya mafumbo kuwa Ohola ni Samaria na Oholiba ni Yerusalemu, akahuzunishwa na tabia yao ya kufunua marinda (skirts) kwa kila mwanume/mungu wanaye muona, then Mungu akaenda mbali zaidi, kuwa kwa desturi makahaba wanalipwa pesa ili wafanywe hayo mambo ya kikahaba, lakini akasema watu wake Israel ndio wanaolipa pesa, yaani wao ndio wanajiuza, lakini ndio wanaolipa pesa,and the deadly worst blame, ni kwamba walifanya dhambi ya *_Promiscuity (Kuwa na wapenzi wengi)_*, yaani mara Ashuru, mara Misri, mara Babeli, mara Pekodi na Shoa na Koa etc etc 😤😤😤😤.
NDUGU YANGU MPENDWA, MIMI NAFAHAMU KAZI YA TOBA KATIKA KUKUSAFISHA UKIISHA JITAKASA. LAKINI KINACHOFANYIKA KWA MTU AMBAYE HAKUWAHI KUAMINI KABLA, NI TOFAUTI NA WEWE MKOMAVU WA KIROHO KUJIANGUSHA DHAMBINI TENA. NI RAHISI SANA KUYAONDOA MAPEPO NDANI YA MPAGANI AMBAYE AMEAMUA KUAMINI SASA, KULIKO MTU MWOKOVU AKAMILIKIWA TENA, MAANA YATAKUJA NA NGUVU KUBWA, YATAJIPANGA ZAIDI. FANYA BIDII USIWE NA MADOA NA MAWAA (SPOTS & DEFECTS), WAA LINAKUWAJE? CHUKULIA MFANO KUNA SHATI JEUPE 🖱👉🏾👔LIMEMWAGIKIWA NA MCHUZI 🍲, UKALISUUZA, KUKABAKI ALAMA KWA MBALI BAADA YA KUKAUKA, HILO NDILO WAA. SASA UNAYEJAZA MAVAA KATIKA VAZI LAKO LA HARUSI (MATH 22:12), UNAPOTEZA SIFA YA KUWA BIKRA, MAANA MABIKRA WANATAMBULIKA KWA KUTOKUWA NA MAWAA (RECORD ✍🏽 ZA MAANGUKO YA DHAMBI NA ZILE ZA KUJITOA KATIKA HALI YA NEEMA. TUSOME
2 Petro 3 : 14
*_Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake._*
Ufunuo 14
*_4 Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo._*
_*5 Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.*_
*SASA MPENDWA KATIKA BWANA, BADALA YA KUENDELEA KUWAZA UANGUKE UTATUBU, BADILISHA MTAZAMO, MWAMVIE YESU NITAUTUNZA UBIKIRA WANGU KWAKO, SITAWEKA RECORDS ZA MAANGUKO YA KIROHO, NA UFANYE SALA YAKO, KUMWOMBA YULE BWANA, AWEZAYE KUKULINDA USIJIKWAE, MPAKA MWISHO UFIKE KWAKE BILA MADOA WALA MAWAA, NAYE ATAKUSUDIA (YUDA 24), EPUKA KUIACHA IMANI, EPUKA KURUDI NYUMA, EPUKA MAANGUKO YA DHAMBI, KWA KUWA SASA UMEOKOKA USIMGEUZIE YESU KISOGO KAMWE, UMWANDAME YEYE TU, HUKU UKITUNZA UBIKRA WAKO.*
```MUNGU AWABARIKI, MIMI NIMETUA MZIGO TAYARI, NASIKIA MWEPESI MOYONI MWANGU.```
*_#Team#MabikraSafi#_*
Mwl Prosper Kadewele
0762879363 (WhatsApp)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment