Friday, November 10, 2017

SECOND CHANCE

*SECOND CHANCE*

```Na Mwl Proo```
~Mjumbe wa Matengenezo~
0762879363(whatsapp)

Bwana Yesu asifiwe! Mungu awape kuelewa mfululizo huu wa sauti ya Neno lake. Kwa sasa kuna watu ambao walikwisha okoka lakini nahimizwa kusema nao kama watu ambao hawana Yesu ila wanaitwa tena. Yesu anaweza kuyaacha maisha mtu ukimnyang'anya nafasi,maana umepewa uhuru wa kumpa maisha yako au ukiyahitaji maisha yako ukayatumie upendavyo unapewa uhuru,ndio maana unaweza kupanga mpango wa kwenda kuzini na ukaachiwa tuu,ukaendesha gari 🚗ukiwa unajua huku naenda kumtenda Mungu dhambi,wala usidhani kwamba ukifika uko ulikoweka promise na mtu utakuta fimbo ya ufalme(uume) 🙊Yesu ameung'oa,la asha!
Lakini anaweza kukuachia maisha yako kwa kuwa umeamua kumnyang'anya (Ingawa Roho Mtakaifu atabakia akiwa amezimishwa ndani yako 1Thes 5:19)

Luka 13 : 35 _*Angalieni, mmeachiwa nyumba yenu! Nami nawaambia, Hamtaniona tena kamwe, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana.*_

👆🏼👆🏼Swala la Yesu kuiambia Yerusalemu imeachwa sio jambo la dharura na kushtukiza bali ni baada ya jitihada za kutoa nafasi tena(SECOND CHANCE) aliwaambiaje

Luka 13 : 34 - Ee *_Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, MARA NGAPI(CHANCES TO REFORM) nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka(YOU WERE UNWILLING)._*

Baada ya jitihada hizo ndipo Yesu akasema Eh👐🏽Sasa basi mmeachiwa nyumba yenu(Fanyeni yenu) ,ila mimi hamtaniona hata mkiniimbia tena pambio za *mbarikiwa ni ajaye kwa Bwana*.

NDUGU YANGU MSOMAJI,UNAMUITAJI YESU KTK MAISHA YAKO KULIKO HATA BARAKA ZAKE. YESU MWENYEWE (JESUS IN PERSON) AWE KWAKO NA KUJAA TELE,WALA USIACHE AKUACHE KWA KUWA UMEMDAI MAISHA YAKO UYAISHI MWENYEWE,HATAKUNG'ANG'ANIA,ANATAKUTAKA UPENDE BURE(KWA UNYOFU WA MOYO) MWANA MPOTEVU ALIPODAI VYAKE AKAISHI ZAKE HUKO,BABA HAKUMKATALIA.

WA KWELI KWA MAISHA YAKO YALIVYO NA KONAKONA NA CHENGA NYINGI, KWA LILE SHOKA LILILOWEKWA SHINANI 🌴⛏,ULIPASWA KUWA UMEKWISHA KATWA.  LAKINI TUNAYE YESU MWOMBEZI WETU KWA BABA(1yohana 2:1b-2),AKAOMBA MUDA ZAIDI *(SECOND CHANCE)*

Luka 13 : 8
_*Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi;*_

👆🏼👆🏼KWA NJIA YA MAFUNDISHO KAMA HAYA,BWANA ANAJARIBU KUKUPALILIA NA KUKUTILIA SAMADI ILI AONE HUENDA UKAZAA MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA,YAANI ANAKUPA SECOND CHANCE

Ufunuo 2 : 21
_*Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.*_

HASHEM HA'TSIDKAT(MUNGU MWENYE HAKI) HAKURUPUKI KUADHIBU,INGAWA HATAKOSA KUUADHIBIA UOVU,KABLA HAJAADHIBU ATALETA *_WARNING/ONYO_* TENA NA TENA,KTK UVUMILIVU NA USTAHIMILIVU MKUBWA. MNAWAKUMBUKA WALE WALIOUAWA JANGWANI? MUNGU ALIVUMILIA MARA 10 WAKIMJARIBU KWA MAJARIBU MAZITO,NDIPO AKASEMA ISIWE TABU,NTAWAVUSHA WANAUME WAWILI TU KATI YA ZAIDI YA WANAUME LAKI 6

Matendo 13 : 18
_*Na kwa muda wa miaka kama arobaini akawavumilia katika jangwa.*_

Hesabu 14 : 22
_*kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu;*_

2 Petro 3 : 9
_*Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.*_

MUNGU HUVUMILIA KWENU(HE IS PATIENT WITH YOU) UMELALA USIKU KUCHA KWA MWANAUME AMBAYE SI MME WAKO UKIZINI,HAINA MAANA ASUBUHI YAKE ATAKUKATA🌴⛏,WALA HATAKUFANYIA VISA BODABODA ULIYOKODI KUTOKA KWENYE UZINZI IPATE AJALI,NO THANK YOU! ATATOA NAFASI YA ZIADA LABDA UTATENGENEZA!!  WENGINE WANAPOONA ILE SHWARI YA BAADA YA KUANGUKA DHAMBINI WANAAMUA KUMCHUKULIA POA YULE MUNGU MVUMILIVU. LISTEN📢,KUNA WATU HAWAKUWAHI KUZINI WALIKUFA VIFO VYA KULALIWA NA GARI KWENYE AJALI,KUNA WATU MAISHA YAO YALIKATWA SIKU ILEILE WALIPOFANYA JARIBIO LA KUVUNJA BENK KUIBA,NA WENGINE WAKIWA WABICHI KIUMRI WALIKUFA KWENYE AJALI ZA MELI,TRENI,MAGONJWA MEPESI AMBAYO WEWE UNAPONA ILA WAO WAKAVUNWA MARA MOJA NA WENGINE SIKU CHACHE BAADA YA KUOA WAKAVUNWA✝⚰☠
SIKU MOJA NILIKUWA NATAFAKARI LUKA 13:1-6 NDIPO BWANA AKANIFUNDISHA KUWA MNAYO SABABU YA KUFANYA TOBA NA WAKATI WOTE OMBA MOYO WA TOBA NDANI YAKO.
KISA KILICHOPO HAPO NI SIMULIZI AMBAYO HAIJAELEZWA KWA KINA,YESU ALIPEWA STORI ILIYOTOKEA KWA WAGALILAYA AMBAO KTK PASAKA FULANI ILIYOPITA WALIUAWA NA ASKARI KWA AGIZO LA PILATO,WAKIWA WANATOA DHABIHU ZAO HUKO HUKO WALIUAWA NA DAMU YAO IKACHANGANYIKA NA DAMU YA DHABIHU WALIZOKUWA WANATOA. YESU ALIWAHOJI HIVI MNAFIKIRI KUWA HAO WAGALILAYA WALIKUWA NA DHAMBI KULIKO WOTE? AKAONGEZEA TENA AU MWADHANI WALE WATU 18 WALIOANGUKIWA NA MNARA HUKO SILOAMU WALIKUWA WAOVU KULIKO WOTE? *AKASEMA LA HASHA,LAKINI NANYI MSIPOTUBU MTAANGAMIA VIVYO HIVYO* HUU NI UKWELI,SI VYEMA NIKAKUHUBIRI REHEMA ZA MUNGU PEKEE MPAKA NIKATOA MAWAZO KAMA YA MASHAHIDI WA YEHOVA WANAOAMUA KUAMINI MUNGU HAWEZI KUWATUPA WATU JEHANAMU MILELE,BIBLIA INASEMA KTK UFUNUO 20 KUWA WOTE AMBAO MAJINA YAO HAYAKUONEKANA KTK 📖✍🏽WATATUPWA KTK ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI,LAKINI WAO WANAAMINI KINYUME.

MPENDWA WANGU UNAYESOMA NAKUTAKA UUANGALIE WEMA WA MUNGU LEO HII,UNAJUA KUWA UMEOKOKA ILA ULIPOMPA BINTI UJAUZITO UKAMSHAWISHI ATOE ILI USIJHARIBIE SIFA KANISANI,AU UKAHAMA KANISA NA MKAFOJI KUFUNGISHWA NDOA PENGINE,WEWE BABA NI MWANANDOA ILA UNAJUA KUWA UMEZAA MTOTO NJE NA UMEMFICHA KABISA MKEO HUKU UKITUMA PESA NA MISAADA KINYEMELA NANYI WACHUMBA AMBAO HUWA MNAKUTANAGA KUTENDA YASIYO WAPASA *BWANA ANASEMA MSIUDHARAU WEMA WAKE* HAKO KAUSALAMA KENU,MAANA BADO HAJAUONDOA ULE UKIGO(FENCE) *Ayubu 1:10/Zekaria 2:5* YA ULINZI ILI WAJUMBE WA SHETANI WASIWABAMIZE AMEWAHIFADHI ILI MPATE KUTUBU *_HIYO NI SECOND CHANCE_*

Warumi 2 : 4 - 5
_*Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?*_
*_Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,_*

KUNA KAUVUMI KA HERESY,WATU UKIWAPA ONYO ACHA DHAMBI HII,ANAKUAMBIA YEYE HAMSIKILIZI KILA MTU ANASIKILIZA SAUTI MOJA YA BABAAKE WA KIROHO,HALI AKIFANYA KIBURI NA KUAMINI ATAKINGIWA KIFUA SIKU YA HUKUMU 🤔 RIGHT HUKO MBALI SANA SUBIRI SIKU YA UNYAKUO UTASOMA RAMANI VIZURI,TENA AT LEAST HATA UNGELISHIKA NENO LA HUYO BABAAKO LAKINI MBONA UNAYOTENDA BABA YAKO HATENDI WALA HAKUFUNDISHI KUTENDA HAYO,UMEYATOA WAPI WEWE?MWAKA HUU PEKEE UMEWAVULIA NGUO👙WANAUME WANNE TOFAUTI NGUO,NA HUKUWAHI KUFANYA TOBA YOYOTE YA KUMAANISHA KAKIBURI KAKO KAPO HAPO TU KUAMINI UNAYE BABA WA KIROHO,THE SAME SPIRIT OF PRIDE ILIKUWA NDANI YA WAYAHUDI NA NDIO MAANA MUNGU ALUAMUA KUWAACHA KWA HABARI YA WOKOVU HUU WA YESU (YOHANA 1:11,MATENDO 28:28ff) KILA JAMBO AMBSLO UNGEWAAMBIA WAYAHUDI, *_" WANGEJIBU SISI TUNAYE BABA YETU IBRAHIMU👴🏾"_* TENA KWA MAJIVUNO KAMA HAYO YAKO☺ WALIKUTANA NA YOHANA MBATIZAJI AKAWANYOOSHA
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽

Luka 3 : 8
*_Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto._*

Nasikia kulia 😭😭Mpendwa mtake Yesu,usimwache aende zake,wala usiyapore maisha yako mikononi mwake. Yesu sio wa kumgeuzia mgongo bali ni wa kumwandama sanaa,Wale akina Kleopa walipogundua kuwa huyu mtu sio wa kawaida wakamganda kusema, *_KAA NASI_* Luka 24:29  KWA NINI USIAMUE KUMTAKA YESU KULIKO CHOCHOTE? 

*NAMTAKA YESU NAMTAKA YESU NAMTAKA YESU NAMTAKA YESU NAMTAKA YESU NAMTAKA YESU*
Make it your prayer ,USIITUMIE SECOND CHANCE KUENDELEA KUHARIBU,IMETOSHA KWA MUDA ULIOPITA KUUTUMIA KUTENDA YASIYOPASA,SASA ANZA MWAMBIE YESU NIPE KUTEMBEA NA WEWE  NIKUINE WEWE,UWE KILA KITU,YESU NI NAMBA MOJA WANGU,YEYOTE/CHOCHOTE ANATAKA KUICHUKUA NAFASI YAKE MWAMBIA *AWAY WITH YOU(TOKA ZAKO)!!!* MCHUMBA ANAYEKUTEMBELEA USIKU ANATAKA KUMFUKUZA YESU WAKO HILI NI JIBU LA KUMPA *_AWAY WITH YOU_* HUYO BOSI ANAYEKUAMBIA USIENDE KANISANI HADI JUMAPILI NAYE MWAMBIE *_AWAY WITH YOU_* KAMSHAHARA KA LAKI MBILI KANIKOSESHE IBADA MIEZI SITA _*AWAY WITH YOU*_ ,ANAYEKUTUMIA VIMESEJI VYA MAPENZI ILI AKUTOE UWEPONI NAYE MWAMBIE *_AWAY WITH YOU_* NATAKA KUKAA NA YESU MIMI HALELUYA!!!!!✋🏾✋🏾✋🏾✋🏾✋🏾

Mbarikiwe Jumatatu njema

Mwl Proo
071892662
0762879363(whatsapp)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment