Tuesday, November 21, 2017

WAENDAO KWA MIGUU WAMEKUCHOSHA

*_WAENDAO KWA MIGUU 👣WAMEKUCHOSHA; UTASHINDANAJE NA FARASI?🐎🐎_*

```By Mwl Proo```
0762879363(whatsApp)

HALELUYA HALELUYA!

Yeremia 12 : 5
*_Ikiwa umepiga mbio pamoja na hao waendao kwa miguu, nao wamekuchosha, basi wawezaje kushindana na farasi? Na ujapokuwa katika nchi ya amani u salama, lakini utafanyaje hapo katika kiburi cha Yordani?_*

Tunalo neno la kutupa kujitafakari na kuongezeka. Watu hawatumii mabomu kushindana na mende🐞 💣🔫. Lakini ni vyema kupata ufahamu huu wa kiroho wa kujua kiasi cha uweza unaotakiwa ili kushindana na kuwashinda maadui. Shetani(Adui mkuu) hata baada ya kuasi,hakunyang'anywa nguvu kamwe bali nguvu alizonazo zililaaniwa. Sasa badala ya kuendelea na zile nyimbo za washangiliaji kwenye mikutano ya injili za kuimba *_Shetani kibogoyoX6 🎼🎤_*  wakati anatafuna mpaka wale walokole waliokuwa na sifa njema kawabana kwenye uzinzi,kaa hapa ujifunze mambo ya uweza.

✝NI MUHIMU UJUE KIASI CHA NGUVU ZAKO(SPIRITUAL CAPACITY) ,MAANA ADUI UNAYEPAMBANA NAYE HUJA KWA NAMNA NA UWEZO TOFAUTI

>Daudi alijitambua kiasi cha uwezo ndani yake 

Zaburi 131 : 1
*_....... Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu._*

Daniel na Ezekiel kuna baadhi ya maono waliyaona yanafanana hata kama sio message basi yalifanana *_mode&mechanism_* ,Daniel aliona maono mpaka mwili wake ukaugua kabisaaa👌🏽 yani homa ndiiii,Lakini Nabii Ezekiel (the prophet of the spirit) aliona mfululizo maono mazito bila shida,siwashindanishi watumishi hawa ila tujifunze.

Daniel 8 : 27 
*_Na mimi, Danielii, nikazimia, nikaugua siku kadha wa kadha; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami naliyastajabia yale maono, ila hakuna aliyeyafahamu._*

✝YESU ALITUFUNDISHA SIO VITU VYOTE VITAWEZEKANA KWA NGUVU ULIYONAYO,YAKO MENGINE(YA NAMNA HII HAITOKI)

Mathayo 17 : 21  *_[Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]_*

Wanafunzi wa Yesu waliklemu kutoa vipepo vidogodogo👹👹👹 wakadhani wote sawa tuu,Sasa wakakutana na pepo/jinn ambalo sio la *_One Touch_* kwamba 🗣toka.. Kwa wale wanajua elimu ya *_demonology_* wanafahamu hata mapepo sio yote sawa. Na yako mengine ni *_cha mtoto_* hayapo ktk sehemu ile ya roho waasi walioasi pamoja na Shetani na wengine ni supergiants walikwisha tumika sana hata mbele za huyu Mungu. Sasa *_USIMFAHAMU ADUI KWA UPANDE MMOJA WA SHILINGI_* hutaweza kumshinda.

KAMA UNAFANYA VITA VYA ROHONI ( *_hakikisha unapata article yangu yenye somo hilo la SPIRITUAL WARFARE_* )UKIFANYA UKIWA NA UFAHAMU WAKO MDOGO WA KUKEMEA TU WACHAWI WAKATI  VITA(KUSHINDANA) VYETU NI JUU YA FALME NA MAMLAKA,JUU YA WAKUU WA GIZA/ANGA NA JUU YA MAJESHI(LEGIONS) YA PEPO WA WABAYA,UTAKUWA UNACHOKONOACHOKONOA MAHALI AMBAPO HUPAWEZI NA UTAPIGWA BILA SHAKA.

SINA MPANGO WA KUMSIFIA SHETANI,ILA ANAZO NGUVU(MATHAYO 12:29) ,NA PIA ANAO UFALME WAKE,SISI WANA WA NURU TUNAPASWA KUWA NA MAARIFA MAKAMILIFU ILI TUVIPIGE VITA KWA USAHIHI NA TUSHINDE.

WENGI HAWATAKI KUJIFUNZA KISA CHA ZAMA ZA DANIEL.

Daniel 10 : 13
*_Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi._*

SASA WAPENZI HUU NI UHALISIA AMBAO HATUPASWI KUU-IGNORE,MUNGU KAMTUMA GABRIEL SIKU YA KWANZA TU YA MAOMBI YA DANIEL,LAKINI WAKUU WA GIZA/ANGA(THE THIRD RANK KTK UTAWALA WA SHETANI) WA SHETANI WALIMPIGA *_PIN_* 📌KUWA HAPA HUCHOMOKI,IKUMBUKWE ZILE WIKI TATU SIO RATIBA YA KINABII YA KUFUNGA(21DAYS) BALI NI SIKU AMBAZO MALAIKA WA MUNGU GABRIEL KACHELEWESHWA HAPO MITAA YA KATI NA WALE JAMAA 👹👹👹👹👹. KILICHOMPA KUCHOMOKA NI 👼🏻🗡MIKAEL ALIKUJA KUINGILIA KATI,NAYE HAKUJA NA KUSHINDA TUU INGAWA ALISHAWAHI KUWA KNOCK-OUT MBINGUNI LAKINI SIO SWALA DOGO.

SASA KAMA MALAIKA WENYE JINA LA MUNGU NDANI YAO,WANATOANA NAO JASHO MUDA WA KUTOSHA,WEWE KAMWE UICHUKULIE POA,BALI JIFUNZE USAHIHI WA VITA VYA KIROHO,ILI USHINDE DAIMA. MAANA KTK VITA HIVI *TWAWEZA SHINDA BILA SHAKA* (Hesabu 13:30)

HIVI KARIBUNI NIMEUSIKIA USHUHUDA AMBAO BAADA YA KUJIFUNZA NA KUREJEA MAANDIKO NIKAUJUA NI HALISI NA HAKIKA,ILA HAUKUNIPA KUVUNJIKA MOYO ILA ULINIPA KUJUA NAPASWA KUWA MAKINI NA KUONGEZA NGUVU/UWEZA ITENDAYO KAZI NDANI YANGU(Efes 3:20).
MWINJILISTI MMOJA TOKA UGANDA AMBAYE ALIKUWA MCHAWI NA MNAJIMU ALIYEKUBUU ALIYEKUWA AKIUACHA MWILI CHUMBANI NA ROHO YAKE ILIENDA ANGA LA KIPEPO KUUNGANA NAO KUSHAMBULIA MAKANISA, ALIELEZA VITU VYA AJABU SANA AMBAVYO NILIKOSA SABABU YA KUVIKATAA. ANASEMA WAKIWA KTK HIYO NGOME YAO AMBAPO HUTOKA NA KUSHUKA KUSHAMBULIA MAKANISA NA WATU WA MUNGU BINAFSI HUWA WANAONA VITU VYOTE,KWANZA AKIWA HAPO MTU ALIYEPO DUNIANI AKIANZA MAOMBI  WOTE WANAMUONA,NA MAOMBI HAYO HUONEKANA KAMA MOSHI🌫NA AKIENDELEA ZAIDI HULIPUKA NA KUWA MOTO🔥🔥 AMBAO WAO MAWAKALA WALIOJENGA NGOME YAO KTK ANGA KUZUIA,HUWA WANAZIDIWA NGUVU NA KUKIMBIA NAYO YANAPENYA MOJA KWA MOJA. NA KWA SABABU HIYO ALISEMA JITIHADA ZAO KUBWA INAKUWA NI KUTAFUTA NAMNA YA KUKUKATISHA USIENDELEE SANA KUOMBA,WANAWEZA KUKUTIA USHAWISHI UANGALIE SIMU 📱   📲 INAYOITA AU WAKAMSHAWISHI MWANADAMU MWINGINE AKUPIGIE,HILO WANAFANYA KWA KUTUMIA MAWAKALA WAO WALIOPO CHINI DUNIANI,AU WANAWEZA KUTIA UAHAWISHI UWAZE KWENDA KUNYWA MAJI SIJUI KWENYE DINING ROOM,AKASEMA HATA UKIKATISHA UKABADILISHA LOCATION,UNAKUWA UMEZIMA ITAKUPASA UANZE UPYA. NA ALIELEZA  WALE WENYE NGUVU KUBWA YA KUOMBA SIKU ZOTE WALA HAWAKATI TAMAA,HUWA WANATEMBEA KUKIWA NA NGUZO YA MOTO/UTUKUFU AMBAYO IMETOBOZA MOJA KWA MOJA TOKA JUU MBINGUNI IMEKATANISHA KTK NGOME/ANGA YAO MPAKA CHINI,NA HUWA WATU HAWA HATA WAKIMWEKEA MTU MKONO✋🏼ILE NGUZO IKIKUTA VIFUNGO VYOVYOTE VYA KIPEPO🔒🔒HUWA VINAJIFUNGUA🔓🔓🔓 VYENYEWE HATA ASIPOOMBA,NA HUWA MARA NYINGI WANAJITAHIDI KUFANYA BIDII KUKUTAFUTA WAPI UTAKOSEA UTENDE DHAMBI,ILE NGUZO IPUNGUE MAKALI ⚡🔥💥WAWEZE KUZIBA KULE JUU,NA JAMBO MOJA LA AJABU SANA ALISEMA KILA ALIYEOKOKA WANAMUONA YUPO NA MALAIKA👼🏻, TENA ALIELEZA BAADHI YA MAPEPO ALIYAONA KUFANANA KWA KARIBU SANA NA MALAIKA WALE WA MUNGU. KUNA MUDA WAKIWA KTK NGOME WANAWAONA MALAIKA WALE HUPANDA JUU KWA MUNGU,KISHA HUSHUKA WAKIWA WAMEBEBA MAJIBU YA MAOMBI YA WATAKATIFU. ILA WAO WAKIMUONA KABEBA 💰👶🏾🚗🏡HUENDA NI WATOTO NA MALI MBALIMBALI AMBAZO MTAKATIFU AMEOMBA HUWA WANAPANGA NAMNA YA KUMSHAMBULIA. SASA UDHAIFU WA YULE MTU ANAYELINDWA NA MALAIKA HUYO UNAWEZA KUWA SABABU YA HUYO MALAIKA ALIYEBEBA MAJIBU KUWA *~OVERPOWERED~* NA YALE MAJESHI. NA ALISEMA WALIKWISHA WAHI KUWATEKA MALAIKA KADHAA NA KUWANYANG'ANYA VILE WALIVYOBEBA,NDIVYO AMBAVYO UFALME WA GIZA UNAVITUMIA KUWAPA WALE WANAOCHAGUA KUTAFUTA BARAKA KWA SHETANI(ILA SHETANI HANA CHOCHOTE) JAMBO MOJA NILILI-NOTE,ALISEMA HAKUNA MALAIKA WA MUNGU ANAYEWEZA KUSHIKILIWA MILELE,MAANA ALIELEZA KUNA WAKATI MAOMBI YA WATU WENGINE TOFAUTI,AU UNAWEZA KUKUTA KANISA ⛪FULANI LIMEOMBA MAOMBI YENYE NGUVU KUBWA,BASI MAJESHI YA MBINGUNI HUSHUKA NA KUSHAMBULIA ZILE NGOME PIA HUWAKOMBOA WALE MALAIKA WACHACHE WANAOKUWA *_CAPTIVATED_* NA MAADUI. SASA NIMEJARIBU KUFUPISHA TUU,LAKINI VITA KTK ULE ULIMWENGU MWINGINE NI HALISI,UNAPASWA KUWA NA MAARIFA NA UONGEZE UWEZO WAKO SANA ILI USIKWAME DAIMA.

NINA RAFIKI YANGU MMOJA AMBAYE ALIKUWA VIZURI KIROHO,MARA KADHAA TUKIWA KWENYE MAOMBI YA KUKESHA ALIKUA AKIONA MALAIKA KWA MACHO YA ROHO👁👁,HATA KAMA TUNAOMBA KWENYE GIZA TOTORO 🌚ALIKUA ANANIAMBIA PROSPER NIMEONA MALAIKA MWENYE NGUVU NYINGI AMESHIKA UPANGA 👼🏻🗡 KWENYE KONA YA KANISA,SASA HATA KAMA TUPO WAWILI TULIENDELEA KUKESHA MPAKA ASUBUHI KWA USHINDI. SIKU MOJA RAFIKIANGU HUYU ALIONA JINI KTK MAONO, LIKIPITA HUKU LINAMTUKANA NA KUMFANYIA ISHARA ZA VIDOLE KUMKEJELI HUKU LIKIENDA ZAKE,AKATAKA KUMFUATA KWA HASIRA ILI KUPAMBANA NAYE,LAKINI ALINIAMBIA ALISIKIA SAUTI IKIMWAMBIA ACHA USIENDE *_nguvu yako ni ndogo kuweza kumshinda_*.
NDUGU MPENDWA SIKUTISHII,MAANA TUEPEWA MAMLAKA YA KUKANYAGA NYOKA(SHETANI MWENYEWE MKUU WAO) NA NGE(MAPEPO/MAJINI)  NA NGUVU NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI,WALA HAKUNA KITAKACHO TUDHURU(LUKA 17:10) LAKINI WEWE ULITEKUWA KIROHO NA KTK MAARIFA USIKARIRI ANDIKO HILO UKAENDA VITANI NA NGUVU CHACHE UKAZIMIA(MITHALI 24:10)

*_NENO LA BWANA KWAKO_*

Nahumu 2 : 1 
*_Yeye asetaye vipande vipande amepanda juu mbele  ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana._*

Mstari huo usome kwa kuurudiarudia,Huyo asetaye vipandevipande ni Adui yako/zako. Kupanda juu mbele zako,amekujia  kivita na nguvu kubwa zaidi..Hayo yanayofuata ni maelekezo ya yale yakupasayo kufanya ili ushinde kabisa kabisa

🔺ZISHIKE SILAHA
🔺ILINDE NJIA
🔺VITIE NGUVU VIUNO
🔺UONGEZE UWEZO WAKO SANA

JIFUNZE VITA VYA ROHONI KWA USAHIHI,FANYA MAZOEZI YA KIROHO ONGEZA MUSCLES🏋🏾🏋🏾💪🏾💪🏾KWA KUFANYA HEAVY DUTY EXERCISE YAANI KOMAA NA NENO,KUOMBA NA KUFUNGA,KUTAFUTA KWA BIDII UJUZI WA KIROHO...PRACTICE MAMBO YOTE UYASOMAYO(BE DOERS OF GOD'S WORD) ,JIOZE KUISHI MAISHA YA IMANI,MAISHA YAKO YAJAZWE NA MATENDO MAKUU YA MUNGU KUPITIA WEWE,FANYA MAZOEZI YA KUTUMIA MAMLAKA YA KRISTO UIONE INAFANYA KAZI KIASI GANI ILI UZIDI KUCHOCHEA(FLAMING IN FIRE🔥)

*YOU ARE MORE THAN CONQUERORS*

Mwl Proo (Prosper Kadewele)

(Unakaribishwa  ktk grupu letu la whatsapp tuma message *ADD ME* kwenda 0⃣7⃣6⃣2⃣8⃣7⃣9⃣3⃣6⃣3⃣)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment