Friday, November 10, 2017

MUNGU WAKO HAKUKUPA RUHUSA, KUFANYA HAYO!

*_```MUNGU WAKO, HAKUKUPA RUHUSA KUTENDA HAYO```_*

*Na Mwl Proo*
0762879363(whatsapp number)

Shalom Shalom!

Neno la Mungu(Rhema) laweza kuwa nadra (1Samwel 3:1) ,likishapunguka inasababisha wakristo kukosa nidhamu *_(discipline)_*, Nidhamu ni uwezo wa kujizuia(refraining) kutenda mambo fulani fulani na kuyafanya yale tu yanayotakiwa kwa sababu yanafaa zaidi. Zama za Eli kuhani kulikosekana na Neno na mafunuo ya dhairi na watu hawakujizuilia,Kuhani mwenyewe alishindwa kuwazuilia wanawe Hofni na Finehasi wakafanya mtendo ya utovu wa nidhamu ,wali-misappropriate zile nyama za madhabahu🍗🍖🍤,kama hiyo haitoshi waliamua kuwaonja (kwa ngono🙊)wale mabawabu (wadada waliosimama kwenye   mlango wa nyumba ya Bwana (nb: hekalu halikuwa limejengwa)).

MUNGU HAKUTUACHA SISI WATU WAKE BILA MIONGOZO YAANI KANISA LIWE *_LIBERAL CONGREGATION_* WALA HAKUNA KITU TUNAWEZA SEMA KUWA HILI HATUNA MAELEKEZO YA MUNGU,MAANA NENO LA BWANA LINA TARATIBU KTK YOTE (2Samwel 23:5)

SHERIA YA KIEBRANIA(HEBREW LAW) INA MAGAWANYO MAWILI YA MAKUU.
*_1.)APODICTIC LAWS_* HIZI NI SHERIA ZENYE AMRISHO LA KIMUNGU ZENYE NENO FANYA/USIFANYE HIZI ZINALENGA KUWAFANYA WATU WAWE NA UHUSIANO MZURI NA MUNGU (VERTICAL RELATIONSHIP).
*_2.)CASUISTIC LAWS_* HIZI NI SHERIA ZENYE KUWEKA UCHAGUZI,KUWA UKIFANYA HILI ITAKUWA HIVI(DEUTORONOMISTIC VIEW)  KUNDI HILI LA SHERIA LINALENGA KUWAFANYA WATU WA MUNGU WAWE TOFAUTI NA MATAIFA HATA KWA MWENENDO/MWONEKANO N.K HAWAPASWI WATU WA MUNGU KUWA SAWA KABISA NA MATAIFA..
TUSOME

Esta 3 : 8
_*Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.*_
WANA WA ISRAEL ZAMA ZA AHASUERO MFALME,WALIONEKA KTK MAJIMBO YOTE YA UMEDI NA UAJEMI KUWA SHERIA ZAO (CASUISTIC LAWS) ZIKO TOFAUTI KWA HIYO WALIKUWA WANALETA GUMZO/KIWINGU MITAANI. INFACT SHERIA ZA MUNGU HUYU WA ISRAEL ZILIKUWA ZA STANDARD YA JUU KABISA HATA MIFUMO YA SHERIA KTK MATAIFA YA LEO YANA MSINGI WA ILE _*MOSAIC LAW*_

Kumbukumbu la Torati 4 : 8
_*Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo.*_

MUNGU ALIWAKINGA WATU WAKE WASIIGE KUTENDA KWA MFANO WA MATAIFA. KWA HIYO YAKO MAMBO AMBAYO HAKUWA RUHUSA KUTENDA (APODICTIC LAWS)

Kumbukumbu la Torati 18 : 14
*_.........bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo._*

LEO HII SISI TUNAYO SHERIA YA ROHO WA UZIMA KTK KRISTO YESU,HAKUNA NAMNA YA KUKUSOMEA KILA SHERIA YA MUSA ILI UIFUATE,ILA WALE WALIO WA ROHONI TUNAJUA KIPI NI *_ETERNAL MORAL PRINCIPLE_* NA IPI  _*CONTEXTUAL MORAL PRINCIPLE*_ KWA MFANO KUTOFUATISHA MAMBO YA MATAIFA,SHERIA YA MUSA ILIAGIZA NA AGANO JIPYA LINAHIMIZA KITU HICHO. HAPA NITARUDI KUELEZA ZAIDI

NDUGU WAPENDWA TUMEONA PRINCIPLE YA MUNGU KUWAFANYA WATU WAKE WAWE TOFAUTI,LEO ALAMA YA MPAKA IMEONDOLEWA( MITH 22:28) MAMBO AMBAYO HATUKUTAZAMIA YAFANYWE NA WANA MUNGU NDIYO YANAYFANYWA. MUNGU ALIPOKATAZA YALE MATENDO YA KIMATAIFA. ALIJUA KUWA ZIKO MADHABAHU ZA GIZA NA ZA MUNGU WA KIGENI ZINAZOZALISHA YALE MATENDO.
MFANO HATUTARAJII KUMWONA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI AKAPANDA JUKWAANI AKIWA 100%  KAMA DIAMOND PLATINUMZ ,HAIJALISHI UKISASA ALIONAO,MADHABAHU INAYOMVUVIA YULE WA MATAIFA SIO HII YA MUNGU,TUKIONA UMEKOPI YOTE LAZIMA TUKUPE SOMO KUWA MUNGU WAKO HAKUKUPA RUHUSU KUTENDA HAYO!.

KAMA WEWE NI KIJANA UMEOKOKA LAKINI UMEVUTIWA SANA NA KUCHORA TATUU(TOTTOO) KISA ULIONA WASANII KWENYE TV NA UMECHORA SIJUI NGE/NYOKA 🦂  🐍MKONONI,UJUE UNAJILETEA UVAMIZI WA KIJINI,THEN ULIVYO NA NGUVU CHACHE UMEZIDIWA NA MATABIA YA DHAMBI KUMBE KUNA WAGENI ULIWAALIKA KWA NJIA YA TATUU. BIBLIA UNASEMAJE?

Leviticus 19:28 (NIV)
_*“‘Do not cut your bodies for the dead or put tattoo marks on yourselves. I am the LORD.*_

👆🏼👆🏼👆🏼Mungu anajua hiyo tabia imebeba uvuvio wa kipepo,so you are attracting unnecessary warfare kwa hayo matatuu yako, wakati nguvu yako ni chache👌🏽..Mungu wako hakukupa ruhusa kufanya hayo

Haya kitaalamu muziki wote ni sawa/mmoja ila tofauti ipo kwenye hali ya moyo/madhabahu inayohudumiwa kwa muziki pamoja ujumbe. Sasa mtu anaweza imba Zouk au Rumba au Reggae  lakini kwa sababu ya hali yake ya moyo kukawa hakuna shida.Ila hawa ambao wanaimba style hizo ila kwa kuiga kila kitu kama walivyojifunza kwa msanii wa kidunia,Au mtu akaimba muziki aina ya Singeli lakini akakopi na dancing zote kama zile za kwenye vigodoro au madogori akatuletea kanisani,hapo kachanganya madesa. Mungu wako hakukupa ruhusa ya wewe kutenda hayo. Nilimkuta pia mwimbaji wa worship ila anajifunzia sauti kwa Lady Gaga,Rihanna,Celine Dion etc Yupo bize kuaikiliza hizo kuongeza ujuzi😤😤 foolish Christian wanatuaharibia kumbe ukiabudisha unaweka usharobaro mwingi wa sauti kama ulivyosikia kwa hawa malkia wa freemason/illuminati msituwashie moto🔥 wa kigeni madhabahuni please👐🏽👐🏽. Kama vipi kaumba secular zotezote

NINI KINAWAFANYA MSHINDWE KUCHUJA?? WATU HAWAJAAMUA KUISHI MAISHA YAO KWA AJILI YA YESU, FULL KU-COMPROMIZE NA DUNIA IN THE NAME OF MODERNITY(UKISASA) UMEMWONA RAPPER WA HOLLYWOOD SIJUI NI STRIKER WA ARSENAL AMENYOA NYWELE KIJOGOO/KIDUKU NAWE KESHO YAKE UNAWAHI BARBER SHOP MTINDO ULEULE UMEUBEBA KUJA KUTUONESHEA MADHABAHUNI UNAWAKOSESHA WATU AMANI NI KIDUKU CHAKO BASI TU WANAVUMILIA HAWANA MPIGAJI MWINGINE WA DRUMS NA KINANDA LAKINI UMEKUWA KWAZO KWA COPYING ZAKO,

BIBLIA INASEMAJE?

Mambo ya Walawi 19 : 27
_*Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.*_

👆🏼👆🏼Hatuishi kwa sheria hizi sasa,huu ni ukweli. Lakini hiki ni kivuli cha kutusaidia inaweza kuwa nu contextual moral principle ambayo ikatusaidia kujua namna ya kutoufuatisha ulimwengu huwezi kule kuvutiwa na styles zote za wana giza hali ukijiona uko sawa tu,No Mungu aliyekataza hapo alikuwa na mlengwa wa kuwafanya watu wake wawe tofauti  hata kimwonekano, fanya vitu ktk kiasi the rest hujapewa ruhusa kufanya hayo.

Kwa mfano hakuna tatizo kwa uliyeokoka  kwenda kula good time beach🏊🏽🏄🏽🚣🏽😎ukapozi zako kupumzika wikiend. Lakini kwa nino unaenda kwenye beach ambayo kumejaa (Nudity 👙) kila ukigeuka upande huu you only see women in Bikkini sasa unatazama visivyofaa kutwa nzima huku unajifanya kufumba macho  na kukemea kwa jina la Yesu,shindwa shetani (Zaburi 119:137) mwishowe unazidiwa na tamaa ukirudi uraiani unasaka wakupractice nae. Very sorry HUJAPEWA RUHUSA KUTENDA HAYO KWA NINI USIENDE PENGINE?

Kuna mambo yanaendelea leo yamefuta picha yote ya ule wokovu tulioupokea maana tumeng'ang'ania yasiyo yetu,yaani  sitaki kuamini walokole mnaishi mkiwa sawasawa na mataifa ktk kila kitu hamna mahali mnagongana,kwamba sheria zenu za maisha ya kiroho zimegoma ku-concur/cohere na ulimwengu,mko poapoa tu ktk yote😳 Now way! There must be something wrong somewhere. Ulipaswa ukitokeza tu kwenye halaiki ya watu waanze kusema mtumishi mtumishi,lakini kwako wewe binti tuvazi twako hatushawishi wakuheshimu,bali inawafanya wakuone *_DEMU WA KUTONGOZWA_*  I hate the name demu it sounds devilish. Lakini ulivyo aisee umestaili kuitwa hivyo

MUNGU ATUPONYE TUJUE YOTE AMBAYO HATUJAPEWA RUHUSA TUSIJIFICHE NYUMA YA MSEMO WA AMANI YA KRISTO IAMUE,WENGINE NDIO IMEWAAMULIA KUVAA BIKKINI 👙NA KUSHINDA BEACH,WEWEEEEE📢 THERE MUST BE STANDARDS FOR HOLY LIVING TUACHE KUGUSHI NA KUGHOSHI

mie nimemaliza aisee

Mwl Proo
0762879363(welcome to our watsapp group)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment