Friday, November 10, 2017

USISUBIRI MATATIZO YAJE, NDIPO UWAKUMBUKE WATUMISHI WA MUNGU

*USISUBIRI MATATIZO YAJE;ILI KUWAKUMBUKA WATUMISHI WA MUNGU*

_Mwl Proo_
0762879363(whatsapp)

Yesu Kristo aliye Bwana, apewe sifa!

Ndugu zangu ktk Bwana,mtu asipoishi maisha yake hali amepatana na Mungu anajikosesha mengi sana. Hakuna namna mwanadamu anaweza akafikia utoshelevu bila Mungu,hakuna!

Mungu ambaye amesema sehemu nyingi ktk maandiko akisema *UNIITE KTK SHIDA ZAKO*  hiyo sio ahadi kwa ajili ya yeyote  hata yule ambaye wakati wa amani yake alimgeuzia Mungu mgongo.  Mungu anasema ukiwa ktk shida (kama ulifanya amani na Bwana hata wakati wa shwari) utamwita naye atajibu  *_MIMI HAPA!_* (Isaya 58:9) maana yake hakuwa mbali (Yer 23:23),Hakuna katabia kabaya kama ka kumtaka Mungu ktk shida tuu(Yeremia 2:27).

Lazima ujifunze kufanya amani na Bwana daima,na siyo kutegea uvurunde mambo  then ukautupe mzigo kwa watumishi.By the way mfumo wa agano jipya kila mtu binafsi anaweza kumkaribia Mungu,sio kwa uwakilishi,ingawa Mungu anaweza kumweka mtu mbele yako akuongoze. Na wakati mwingine tunayachukua mambo yetu kwa watumishi waombe maana viwango vya kusikilizwa haviko sawa ingawa sote tumefanywa ukuhani (makuhani) wa kifalme (1Pet 2:9,Ufu 5:10),lakini tunayapeleka maana kiasi cha kuuchochea moto wa madhabahu🔥🔥 kinatofautiana,jambo ambalo umefunga weee ukalipeleka kwa mtu mwenye madhabahu yenye network full ukapata majibu mara moja! Lakini haipaswi kuyavuruga na Mungu then unaenda kui-dump hali yako kwa watumishi

1 Samweli 28 : 16 _*Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?*_

NI MTUMISHI ASIYE NA VIWANGO PEKEE ATAPOKEA SADAKA ZAKO AU KUKUHIMIZA UTOE SADAKA ILI MAMBO YAKO YAKAE SAWA WAKATI HUJAJITENGENEZA MOYO KWA MUNGU,WENYE UFAHAMU KAMA ELISHA ALIMUULIZA GEHAZI JE! HUU NI WAKATI WAKUPOKEA FEDHA NA NGUO,NA UNGA?

Kuhani Eli alisema,
1 Samweli 2 : 25 

*_Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa Bwana, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao,..........._*

SASA TWENDE KTK MOYO WA SOMO

TUNASOMA HABARI ZA YEROBOAMU,YEYE ALIPOKEA NENO LA UNABII TOKA KWA AHIYA NABII KUWA ATATAWALA JUU YA ISRAEL NA UZAO WAKE. TANGU HAPO HAKUWAHI KUTHUBUTU KUMFUATA MTUMISHI HUYO, ILI AJIFUNZE NJIA ZA MUNGU WALA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU, AKATENGENEZA MASANAMU YA CHUMA NA AKAMGEUZIA MUNGU MGONGO. ILA ALIPOONA MAJANGA YAMEMKUTA YAANI MTOTO WAKE ABIYA ANAYEMTAZAMIA AURITHI UFALME YUKO HOI ICU  🚑 ♿ 🛌 NDIO AKAKUMBUKA KUNA MTUMISHI NABII HUKO SHILO ALIWAHI KUMTABIRIA,AKAMWAMBIA MKEWE AJI-DISGUISE (AJIFANYISHE) KAMA SI MKE WAKE ETI WANA MPIGA CHANGA LA MACHO  NABII (kumbuka hakuna siri katika ulimwengu wa roho),TENA HAWAKUA KUMPELEKEA MKATE MTUMISHI HATA SIKU MOJA,ILA SASA ANAMWAMBIA.....
1Falme 14

_*3 Twaa mkononi mikate kumi, na kaki, na mtungi wa asali, ukamwendee; naye atakuambia kijana atakuwaje.*_

NI KWELI UMRI WA AHIYA NABII ULIKUWA MKUBWA MNO HADI AKAWA KIPOFU ILA SCALE YA KIROHO ILIKUWA INASOMA 100% ,MUDA AHIYA ANASIKIA TUU SAUTI YA NYAYO ZA MJE WA YEROBOAM AKAMTAJA KWA JINA *KARIBU MKE YEROBOAMU* AKIWA KIPOFU ILA ROHONI ANAONA,DILI LOTE LIKABUMBURUKA,KABLA HAJAELEZA SHIDA AKAMPA UNABII MBAYA KWA FAMILIA YA MFALME MWOVU YEROBOAM MWANA WA NEBATI. HII NI DESTURI YA MUNGU WANAOTAKA KUMTAFUTA YEYE WAKATI WA SHARI KWA MANABII WAKE LAZIMA AWAGONGE NYUNDO🔨KUWAPA SOMO,SIWAZUNGUMZII  MATAIFA WASIOKOLEWA WANAPOHITAJI MSAADA HAPANA NAWAZUNGUMZIA WANAOIJUA HAKI ILA HAWAITENDI.

Ndugu wapendwa tunao watu ambao walikwisha wahi okoka,then wakajikinai nafsi kwa sababu ya mazoea,wakajaribu kidogo kuishi maisha ya udhalimu(yaani mtu akatest kuishi bila kumtaka Mungu),Tunao wapendwa walizini mara moja tuu,wakisikilizia ile hali wakaona mbona kawaida,ooh badala ya kutubu na kuacha kabisa wakaona waendeleeendelee kidogo,kwa hiyo anazini tena sasa usidhani uone dhambi sio tamu la hasha maana Biblia inasema maji yalioibwa ni matamu na matamu na mkate ulioliwa kwa siri hupendezaa😋😋🍞 *_Mithali 9:17,20:17_*  Kwa hiyo unakuta mtu hatubu maana kuna mwingine ameshatongozana naye bado hawajatekeleza ahdi ya kutenda tendo la kirumi,huenda umekabidhiwa biashara kuna namna unaenjoi kumwibia Bosi wako na hutaki kutubu maana hako kamchezo kamekufanya kuwa mjanja in town,hii ni mifano michache lakini piga picha maisha yako.
(KUMBUKA KOSA/DHAMBI AMBAYO HUJAAMUA KWA NIA YA DHATI KUIACHA HAUWEZI KUITUBIA LAZIMA UTA-BUY TIME 🕔🕣🕚NAYO MAANA UNAJUA UKIPATA MWANYA LAZIMA UTAITAMANI UITENDE. KWA MFANO MTAZAMAJI WA VIDEO ZA NGONO AMBAYE HAJAAMUA KUIACHA HIYO DHAMBI,HUO UCHAFU WA KUTAMANI *_HAWEZI KUTUBU_* MAANA HATA WAKATI HUO BADO AMEJAZA CD 📀💿 NYUMBANI KWAKE,AMEJAZA CLIPS KWENYE 📱  💻 (SIMU,KOMPYUTA ETC) HAWEZI KUTUBU JUU YA HIYO.
Sasa hawa wandugu ni miongoni mwa wale ambao ujumbe huu unawahusu 100% Maana isije ukaona namjadili Mungu kama mwenye kuhukumu asiye na rehema la hasha,Mungu ejaa wema ukikaaa ktk wema wake,ila ukijichomoa lazima uenjoi UKALI wake (Rumi 11:22) Sasa ni hawa ndio huwa wanategea kuita watumishi muda wakiwa  hoi  vitandani,yaani wewe  hujamfanya Mungu rafiki(mchungaji) wako then unapitia kwenye bonde la uvuli wa mauti unasema naomba miniitie Mtumishi wa Mungu😱😱 ni kweli tumepewa huduma ya upatanisho (2Kor 5:18-19) lakini hapo kaka mkubwa usitarajie habari njema,Wale wanaosaka msaada kwa nyakati hizo watazamie Mungu kutoonesha ushirikiano zaidi,Yule mfalme Ahabu anajua kabisa alikuwa na bifu na Mikaya nabii,pia Mungu wa Israel. Lakini anataka tu kwa vita ndio aulize kwa Mungu eti vipi Mikaya,niupandie Ramoth-Gileadi? Mikaya  akampa makavu laivu,Nenda ila utapokea kichapo 💣🔪⚔🗡🔫☠⚰ ila utapokea kichapo heavy!! Hivi unapata hasara gani kuweka mambo yako sawa na Bwana?

MUNGU SIO WA KUPOKEA MAPOOZA TUU MUDA WOTE,YAANI USUBIRI SHETANI KAKUCHAKAZA WEE UNARUDI HUKU UKIWA *_SKINNY_* (ngozi na mfupa) yaani hata hutufai kwa kazi za ufalme,HUNA USHAWISHI TENA,HATA TUKUPE NGUO KALI 👔👖👞UKASHUHUDIA MTAANI HAZIKUTOI TENA,HAUNA MVUTO,ULIPOKUWA NA AFYA TELE MTU WA MIRABA MINNE MWENYE SIX PACKS🏋🏾ULITUMIA ULE UMARIDADI WAKO KWA KUISHI MAISHA YA KUNYWA UOVU KAMA MTU ANYWAVYO MAJI🍸,LEO HII UMEBAKI KIMBAOMBAO NDIO UNAITA WATUMISHI,HIVI UNADHANI MUNGU HAKUKUHITAJI KTK KULE KUPENDEZA UMTUMIKIE? KAMA SHETANI ANGEKUTENDA HAYO UKIWA HUMJUI MUNGU SI TATIZO MUNGU AWEZA KUKUFANYA MPYA KABISA,LAKINI NAZUNGUNZA NA WEWE ULIYEOKOKA USIJITOE KWENYE WEMA WA MUNGU KWA KUAMINI UTATUBU NEVER!!!! (MITHALI 27:1)  AMUA SASA KUMTAKA MUNGU HATA KAMA HUNA SHIDA,WATEGEMEZE WATUMISHI WAKE SASA HATA KAMA HUNA MATATIZO,TUMIA VITU VIZURI VYAKO VYENYE MVUTO KWA AJILI YA BWANA HATA KAMA UNA SURA SO CUTE KILA UKIPOST PICHA YAKO FB UNAPATA SHARE 100, LIKES 180k NDANI YA NUSU SAA HUO NDIO MUDA MZURI WA KUMTAJA MUNGU NA WOKOVU WAKE,WATU WAJIHOJI HATA HUYU DADA MZURI ANAMHUBIRI YESU😳😳!! Ila kama ukidhani ulipewa hiyo sura kama the vessel for show-off okey wait wajumbe wa adui waje kukuharibu na utukufu na umaridadi wote utapotea.

MIMI NAWEZAJE KUPOTEZA MASAA MAWILI KUANDIKA HAYA KWA SIMU,SINA HITAJI LOLOTE KWAKO ZAIDI YA HILI,TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO(isaya 38:1B),KABLA HAYAJAWA HAYATENGENEZEKI TENA!

*Mwl Proo(Prosper Kadewele)*
~Mjumbe wa Matengenezo~
0762879363(ATG whatsapp group)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment