*TUPO HUKU; TULIVUTWA!*
_By Mwl Proo_
0762879363
Shalom Aleichem!✋🏾
Wapendwa ktk Bwana nawasalimu kupitia jina kuu(Yesu Kristo)!
Je! Wewe ni miongoni mwa waliomwamini Yesu na kuokolewa? Sasa tambua haya kuijua thamani ya karama ya Mungu na huo mwito wake (Rumi 11:29) ambao hauna majuto.
Upo ndani ya ufalme wa Mwana wa pendo lake sio kwa bahati,sio kwamba kwa kuwa ulizaliwa ktk familia ya kikristo,wala si kwa sababu nyumbani yenu ilikuwa karibu n kanisa. Wewe upo ndani ya Yesu leo,kwa kuwa Mungu kwa mpango wa milele *alikuvuta kwake*, never take it for granted,you were privilleged kuwa huku,God pulled you to Himself.
Yohana 6 : 44 - *_Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, ~asipovutwa~ na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho._*
Yeremia 31 : 3 _*Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana ~nimekuvuta~ kwa fadhili zangu.*_
Mungu ambaye aliamua kujifunua kwa taifa la Israel,na wengine wote duniani wakaitwa mataifa kwa jinsi ya mwili,wasiotahiriwa etc
Waefeso 2 : 12 *_kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani._*
~HAMKUWA NA KRISTO
~MMEFARAKANA NA JAMII YA ISRAEL(WATU WA MUNGU)
~WAGENI WASIO NA MAAGANO YA AHADI ILE
~HAMNA TUMAINI
~HAMNA MUNGU DUNIANI
👆🏼👆🏼Hiyo ndio hali yetu ya kwanza,tena mataifa tuliishi tukiabudu miungu na mizimu,Lakini wakati huo wote tulikuwa mawazoni mwa Mungu,ili atupanishe na nafsi yake mwenyewe.
SASA WOKOVU ULE MKUU WA MUNGU,ULIKUFIKILIA HATA WEWE MNDENGEREKO SIJUI MMANG'ATI ULIYEKUWEKO KIJIJI CHA NDANI KABISA(INTERIOR VILLAGE) 🏰🐒🌳🌴, USIJARIBU KUUCHUKULIA WOKOVU POA,UKAWAZA DINI YAKO,UKAONA TU NI WAZUNGU WAMISHENARI WALITULETEA DINI ZAO ETC, NO WAY👐🏽 Mungu alikuwa na ratiba zake *_ILI ATUVUTE KWAKE_*
Hukuwa na sifa zozote za ushawishi ili upewe kipawa hili cha wokovu (Efeso 2:8) tena muda tunaitwa tulikuwa ktk worst situation😤
1 Wakorintho 1 : 26 _*Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;*_
Sikuzungumzii wewe mwanadini ambaye dini umeshika ila hujamjua Mungu huyu aliye haki yetu(Yer 23:6),Wewe mwanadini si unajijua? Umeshika dini ila fegi 🚬kama kawa,una mke💍🙎🏽 na unatongoza mwanamke mwingine whatsapp na facebook📱, unarudi nyumbani upo full tungi😞🍺,unampiga mkeo✊🏽👊🏾💪🏾👩🏻 Wewe bado kwanza,namzungumzia mtu ambaye ameokoka,ambaye hawezi kabisa kujatibu kutenda hayo.Wewe ndugu mpe Mungu utukufu,ulivutwa ungeweza kubaki ti mpagani na mwanadini asiyeujua wokovu.
JE! UNAIKUMBUKA STORI YAKO ULIFANYWAJE KUWA WA MUNGU,NAMNA ULIVYOITWA? *_IT IS SO FUNNY_* Nakumbuka tukio lilitokea 29/8/2004 linenifanya kuwa mimi Mwl Proo wa sasa, Kwa kuwa ilimpendeza Bwana wakati huo *ANIVUTE* basi hakuna aliyeweza kuzuia. Mwanzoni nwa mwaka huo Mungu alinivuta kwa ndoto,niliota nimejilaza kwenye ukoka mzuri na kukawa na mdudu mdogo 🐜anapanda anaizunguka huku na huko,nikaona nakashika na😏 haka ka nini bhana,na ghafla kale kadudu kakawa ndege mkubwa mwenye umbo la bata🦃 mkubwa kuliko mbuni,mwenye rangi nzuri za blue na nyeupe akawa amenibeba ananipaisha mawinguni☁🌨,Baada ya muda nilikuwa sehemu nasikiliza mahubiri, Akili ya mawazo yangu yakahamishwa ghafula nikaletewa ile ndoto huku mtu akinifafanulia kuwa yule mdudu🐜 ni wokovu ambao nausikia ila naona unaboa fulani,utaninyima uhuru.Lakini huo pekee ndio utakaonipeleka kwa Baba wa milele. Lakini mara nyingine tena nikiwa bado nasuasua kuamua,Nikaoteshwa kuwa mwisho umefika parapanda inalia,nikiwa usingizini nikashtuka nikabeba na ka-agano jipya ka kingereza tulipewa shule,nikakimbilia nje nilipoangalia nikaona watu wanamalizikia mawinguni wanatokomea huku wanaimba na mawingu yanazunguka.Nami nikahisi kauwepo ka unyakuo,nikanyakuliwa umbali wa mita 25 au 30 ,lakini akilini nilijihoji mbona sijabadilika mavazi,na muda huo nikaona siendelei kwenda juu bali kuna upepo unanipeperusha tuu hadi nikawaza nitadondokea wapi,na kweli nilishuka tena chini nikawaona na wachache ambao nao waliachwa.. Ikaniongezea presha kutaka kuokoka,Lakini kuuacha ulimwengu ilikuwa ngumu,maana nilijua nikiokoka itanipasa kuacha vyote ikiwemo miziki ya bongo fleva ambapo shuleni (Ruvuma day Sec) nilikuwa maarufu kama *_Mzee wa kushuka mistari_* na zile hiphop za marekani. Hivyo nikadelay tena kufanya maamuzi,ka ambavyo kuna wasomaji hapa wanajihoji na kusuasua,wanawazia dini zao na mambo yaoitakuwaje! Mwezi wa sita mwaka huo nilihama shule kuhamia Dar ambako familia yetu ilikuweko, wakati huo kiu ilizidi lakini nguvu ya dunia ilinizidi. Yesu akaamua kunitembelea kwa ndoto ili anivute aisee *_EVERYONE IS UNIQUE IN THE SIGHT OF GOD_* Mungu alinishughulikia peke yangu as if ni special case lakini anafanya hivyo kwa kila mtu Haleluyaaaaaa! *_WEWE NI SPECIAL CASE AISEE MTU ASIKUCHUKULIE POA_* Iligharimu vikao vingi kwenye Baraza la Mungu ili akupate. Tulikuwa tunaishi Mbezi Beach near Massana Hospital,nikaota tena mambo ya unyakuo,maana hilo ndilo somo lilikuwa akilini kuwa kuna siku wamchao Mungu kupitia Yesu watanyakuliwa. Nikaota ni majira ya saa mbili usiku dada zangu wanapika chakula nje,nami nipo pembeni yao nimesimama naimba nyimbo za dini,lakini nilipoangalia anga nikagundua nyota zipo karibu kuliko kawaida⭐⭐⭐⭐⭐,na kila nyota nilikuwa nikiikazia macho ilikuwa inageuka na kuandika maneno makubwa kwa kingereza,nikamshtua dada yangu mmoja alikuwa karibu(Dada Judy) nilipomwashiria aangalie juu,nikaona yeye na mwingine wamevikwa mavazi meupe kwa ghafla wameinua mikono yao🙌🏽🙌🏽 nami niliihisi ile nguvu hivyo niliinua mikono pia🙌🏽 kaa mtu anajiandaa kupaa,wengine walinyakuliwa,nikaona mimi hata kale kauwepo kamepotea mara baada ya wengine kunyakuliwa,mbele yangu nikamwona Yesu akaniambia maneno ambayo nayakumbuka,alisema *_"LAKINI WEWE SUBIRI KWANZA"_* akapotea..ghafla nikaona nipo na moja ya walimu wa kwaya tunashangaa anga jua lilikuwa limetiwa giza na lima wekundu kama wa damu.
Baada ya hapo nikaona ghafla kama tupo ktk barabara kubwa usiku,watu wengi tunakimbia kuelekea upande fulani ambapo kwa mbele kabisa ni kama kuna moto na kuna sauti kama za vilio. Ktk hiyo njia nikamuona tena yule aliyeniambia wewe subiri kwanza(Yesu) ,niakaona kwamba ktk hali hii ya hatari nikimpata huyu nitakuwa salama. Sasa nikaanza jitihada za kumkimbilia sikumpata nikashtuka. SASA NIKAJUA KUWA NAMHITAJI YESU. MWEZI MMOJA BADAE NIKAOKOKA NA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU KWA ISHARA YA KUNENA KWA LUGHA MPYA SIKU HIYOHIYO. HEBU TAFAKARI MUNGU KWA NJIA YA VIJINDOTO TUU KUMBE ANAJUA ANANIVUTA TO HIS ETERNAL LOVE! NAJUA KILA MTU AKISIMULIA ALIVYOVUTWA HAPA TUTATOKA MACHOZI,LAKINI NI HIVYO MUNGU ALIPENDA ATUFANYE WATU WAKE HASA
1 Samweli 12 : 22 *_Maana Bwana hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza Bwana kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe._*
Luka 12 : 32 _*Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.*_
KWA HIYO KUNA WATU HUMU AMBAO KAMA MCHEZO MLISEMA TWENDE TUKAANGALIA KWAYA ZA KILOKOLE KWENYE CRUSADE 😀,TWENA UKASEMA KWA KU-MOCK KUWA, *_"napenda wanavyocheza👯👯"_* 😀ULIPOENDA NAFSI YAKO IKAWA PIN-POINTED(📌) KWISHA HABARI YAKO, SASA NA LEO YOU STAND AS A MINISTER OF GOD'S KINGDOM! AISEE TUMBARIKI MUNGU WA MIUNGU KWA KUTUVUTA,UKISHAJUA HAYA PLEASE,USIWAHI KUFIKIRIA KUTOKA HUMU NDANI
*WITO MKUU*
Kaka zangu na dada zangu,kuna watu Mungu anawaita sasa kwake. Msipoteze muda zaidi.. Wako ambao madhehebu yamewashikilia huku yana ukataa wokovu. Sasa usipotezewe muda,maana ukiisha kuokoka utajilaumu kwa nini ulichelewa hadi Shetani akakugalagaza sana,kisa umefundishwa kuchukua mambo ya kuokoka,kuokoka sio kubadilisha dhehebu ni maamuzi ya dhati ya kumwamini yeye Yesu awe Mwokozi na Bwana,ikikulazimu kuhama dhehebu labda kama hawakubaliani na wokovu au unaona stock ya chakula cha kiroho haiendani na ulioamua kuyaamini, *_that is not my case today_* Lakini fanya maamuzi sasa,usikawie zaidi,maana Mungu ameamua kukuvuta. Come and enjoy, HUTAJUTA KAMWE,MAISHA YAKO YATAANZA KUANDIKA HISTORIA MPYA YA FURAHA KUBWA MNO
BARIKIWA SANA!!
Kwa msaada wa kiroho
Mwl Proo
0762879363(whatsap#)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment