🇵 🇷 🇴 🇴
*KILA MWENYE MATUMAINI HAYA, HUJITAKASA*
*```Na Mwl Proo```*
0762879363
Mungu wetu mwenye wema na upendo wote(Omni-Benevolent God), ambaye amejifunua kwetu kwa Yesu Kristo, Asifiwe sana sana!
Miongoni mwa mambo yanafanya nisimchoke Mungu, ni ahadi zake na matumaini niliyoyapata kwake. Unajua katika zile dini kuu 19 na yale matabaka 270, ni dini tatu zina matumaini sana kuhusu kukaa na Mungu wao milele. Yaani Ukristo, Uyahudi na Uislam. Ingawa matumaini yenye utukufu mnajua yanapopatikana (JITAHIDI UPATE SOMO LANGU LISEMALO, IMANI KATIKA MUNGU-JEHOVAH NA BWANA YESU-KRISTO NDIYO ILIYO YA KWELI NA TAKATIFU SANA; ili ujifunze mambo ya dini zote zingine).
Sisi katika Kristo, hatuishi bora liende, No! Ziko ahadi, yako matumaini. Tufutane sasa
1 Yohana 3 : 3
_*Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.*_
2 Wakorintho 7 : 1 *_Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu._*
TUKIISHA KUOKOLEWA, TUNAVIKWA UTU MPYA (Efe 4:23-24). Halafu tunabaki hapahapa kwenye dunia hii mbovu (Gal 1:4). Sasa kuna kamchakato ka utakaso, huwa haka hakakomi, hakana mwisho wake, mpaka tukiyarithi yale tuliyoahidiwa.
KWA KUWA TUNA MATUMAINI HAYA, KUWA KUNA SIKU TUTAFUFULIWA, KUWA KUNA WAKATI TUTABADILISHWA TUFANANE NA YEYE, TUTAKAA NAYE MILELE KATIKA UTUKUFU. KWA KUWA TUNA AHADI NYINGI ZA MUNGU KTIKA DUNIA HII YA SASA NA ULE ULIMWENGU UJAO, NA MBINGU ZIJAZO, KAZI YETU KUBWA NI KUJITAKASA (CLEANSING/SANCTIFICATION).
KABLA YA KUOKOLEWA, TULIJAZWA KILA AINA YA UCHAFU, YAANI WA MWILI NA ROHO (2KOR 7:1), NA WALA HATUKUPATA FAIDA YOYOTE, WENGI WAKIISHA KAA MUDA FULANI, HUANZA TENA KUYAHUSUDU YALE YA KWANZA
Warumi 6 : 21
_*Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.*_
👆🏼👆🏼ULIPOKUWA UNABADILI WANAUME AU WANAWAKE WA KWENDA NAO GUEST HOUSE🏡💏, ULIPATA FAIDA GANI? ULIPOKUWA UNAPIGA PAFU ZA FEGI 🚬🚬, NA KUKESHA KLABU UKILEWA🍺🍻,ULIPATA FAIDA GANI?
Warumi 6 : 22
_*Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.*_
FAIDA KUBWA UNAYOIPATA BAADA YA KUOKOKA, NI KUTAKASWA. NA SIO SWALA LA MARA MOJA, BALI UNAKAA KATIKA UTAKASO
1 Wathesalonike 4 : 7 _*Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.*_
LEO HII NI RAHISI KUSIKIA DHAMBI NA UCHAFU, HATA KATI YA WALE WALIOOKOKA. NA KUNA VIUTARATIBU VIMEBUNIWA KIBINADAMU, UTASIKIA KWENYE MATANGAZO, KIJANA FULANI SIJUI JOSEPH, NA BINTI FULANI ANITA, WAMEFANYA UASHERATI, NA WAMEKUBALI, HIVYO TUNAWASIMAMISHA MWEZI MMOJA WASIFANYE HUDUMA. 🤔 KWA HIYO SEHEMU ZINGINE KUTANGAZA MAJINA YA WAZINZI NA WAASHERATI NI MIONGONI MWA MATANGAZO COMPULSORY. SASA HIVYO SIVYO TULIVYOPOKEA IMANI HII. BIBLIA INASEMA
Waefeso 5 : 3
_*Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;*_
ANDIKO HILI KATIKA KINGEREZA NIV IMEANDIKWA, _But among you,there should not be even a hint of sexual immorality, impurity,greed............_
SASA KWA WALIOOKOKA, HAIKUTAZAMIWA UZINZI+UASHERATI UWE STORI TENA. TENA ANASEMA KUSIWE HATA NA HINT, YAANI HATA DONDOO, LADHA, TETESI TU KWA MBALI, YAANI HATA MSIIGUSIE HIYO HABARI. TULITAZAMIWA VIWANGO VYETU MBALI SANA.
Neno "Takasa" tafsiri yake ni kutenga. Kwa hiyo kwa kuwa tupo kwenye dunia iliuojaa uchafu, Bwana anatutaka tujitenge. Usikae katika uchafu, nali ukitakase. Ujithibitishe mwenyewe uwe katika usafi. Ziko taratibu za dini ya Kiyahudi,tunazosoma kwenye _Halakah(Sheria/mafundisho ya kiyahudi_) , ambazo ni picha/kivuli ya maisha kamili ya kiroho leo. Tunaona jinsi ambavyo walijitahidi kujitakasa sana. Kwa mfano, Wale _Kofer_ waandishi (Scribes), kwa kujua kuwa Mungu ni Mtakatifu, Kila walipotaka kuandika jina la BWANA YAANI YAHWEH (YHWH) _יהוה_ walijitakasa sana, kwa nje ikiwa ni ishara ya kiroho (ritualistic cleanness). Tena ikumbukwe hilo jina waliacha kulitumia, akawa anatamka kuhani mkuu peke yake akiwa patakatifu pa patakatifu, tena siku ya upatanisho (Yom Kipur). Lakini wale waandishi walikuwa wakifika sehemu yenye Jina YHWH, walikuwa wanaenda katika visima/mabirika *Mikvah*, tena yaliyosahihi ni yale ambayo mtu mzima angeweza kuzama *Kosher Mikvah*, kisha waliingia kujitakasa humo, kisha anarudi kwenda kuliandika jina la YHWH (YAHWEH/YEHOVA), Tena hawakuandika jina lenyewe bali waliandika tu _השם_(HaShem/The Name), yaani ukiona hivyo ujiongeze kuwa wanamtaja JEHOVA-BWANA. SASA YULE BWANA AMBAYE HATA JINA LAKE LILIOGOPWA KUANDIKWA BILA KUJITAKASA, LEO HII KAFANYA MAKAO NDANI YETU, JE! HAIKUTAPASA SISI KUJITAKASA ZAIDI?
*MOYO WA SOMO*
Baada ya hizo stori, nilizo tanguliza, nikupe neno lake Bwana, kuwa ilitosha ule muda ulioutumia kuyongayonga katika uchafu. Huu ni wakati wa kujitakasa kama Yeye alivyo mtakatifu. Unapoendelea kukaa hapa duniani, usirudi nyuma wala usipige mark-time. Endelea kujitakasa!! Huu sio wakati wa kuendelea kujichafua, bali uchafu wote wa mwili na roho ujitenge nao. Katika ulimwengu wa leo ukikwepa uchafu katika Tv📺, basi utaukuta kwenye simu yako📱. Sio lazima uangalie kila kipindi, Sio lazima utumie kila mtandao wa kijamii. Na Shetani anakua akunaseje, Ukikuta page facebook inahusu Mambo ya Mungu, you don't Like/Follow✔. Ila page ikiandikwa Udaku, Sijui Utamu wa mahaba, Hiyo ndio unaichangamkia kuilaiki. Utapata faida gani kwa kupewa simulizi, ambazo jamaa fulani kajaa mapepo ameitunga. Yaani unapoisoma inakusisimua tu kihisia za ngono basi. Unajijua kuwa Simulizi za mapenzi unafuatilia mpaka sehemu ya 84, Lakini posts za Neno kama hii ni mtihani. Unapaswa kuzidi kujitakasa, na sio kujinajisi. Sasa simulizi yenyewe inaeleza ngono ambayo haikubaliki, Utakuta ni ya housegirl na baba mwenye nyumba, au kijana anahusiana na binti pamoja na mama yake, ila hiyo ndio umeutoa moyo wako wote huko. Hivi utaweza kuyabeba na mambo ya kimungu? Wewe kijana hizi sio nyakati za kudownload pornography kwenye internet, Huu ni wakati wa kuzidi kujitakasa. Huu sio wakati wa kukaa na picha za uchi, zinakusaidiaje kwa mfano? Huu sio wakati wa kufanya SexChat📱💏📲. Shetani kadaka wengi hapo, mara kadhaa nimepata kusikia, waliokutwa na bahati mbaya ya kutuma picha zao za uchi kwenye magrupu. Yule mwanakwaya wa Shinyanga, alikuwa anatumiana picha za uchi na kijana, akakosea, akatuma kwenye grupu la wanakwaya wenzake (AKAJINYONGA USIKU HUOHUO). Majuzi tu kule Limpopo kuna mchungaji wa Kipentekoste, ametuma picha ya uume wake kwenye grupu la Kanisa. Kumbe alikuwa anachat na hawara, akimjulisha kuwa mama mchungaji kasafiri, sasa aende kwa hiyo zawadi, itakauwa yake (Tena hayo maneno aliweka kama caption) NAYE KAJIUA. Sasa badala ya kuhangaika na hayo mauchafu, kwa nini tu tusifanye bidii kuendelea kujitakasa??
MIMI NAKUPA SHAURI, USIKUBALI KUUNGWA GRUPU LA WHATSAPP LENYE UCHAFU, UKAA UNAJIKAZA, UTANASWA TU. USITHUBUTU KULAIKI PAGE AMBSYO UMEJUA KUWA INA UCHAFU. MTU ANAYEWEKA VITU VICHAFU KWENYE MTANDAO FANYA FASTA KUM-UNFRIEND NA KUM-UNFOLLOW. SIMU YAKO IOMBEE, IFANYIE AGANO (ayub 31:1), MWAMBIE YESU SIMU YANGU, LAPTOP YANGU 📱💻 HAITATUMIKA, KAMWE KUTAZAMIA VITU VISIVYOFAA (ZABUR 119:37).
USISIKILIZE SECULAR MUSIC (MIZIKI YA KIMATAIFA) IKITOKEA UMEUSIKIA KWA BAHATI MBAYA UPO KWENYE DALADALA BASI USIUSIKILIZE (ATTENTIVELY), USIIHIFADHI KWENYE SIMU YAKO KAMWE. MUNGU ANATAKA UTAKASWE, ADUI ANALETA VITU VYA KUIJAZIA NAFSI UNAJISI. UKIWA NA RAFIKI AMBAYE ANAKULETEA STORI ZENYE UCHAFU TU, FANYA KUM-UNDO 💔. TAMANI KILA SIKU UZIDI KUPANDA VIWANGO VYA KUJITAKASA. FAIDA YA KUDUMU KATIKA UTAKASO, NA KUKAA NA UWEPO WA MUNGU, UTAIONA TUU SIKU FULANI.
Ufunuo 22:11
Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.
No comments:
Post a Comment