Wednesday, November 8, 2017

SEMA KWELI KWA MOYO

*SEMA KWELI KWA MOYO*

_Mwl Proo_
~Mwana-matengenezo~
0762879363

*Bwana Yesu(Kristo) asifiwe!*

Bwana amenipa ujumbe wa kusaidia kutengeneza(reforming) kwa wale watakaokuwa tayari kufanya hivyo ili wakae na BWANA!

Tusome Zaburi 15:2

*_Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake,_*

👆🏼ASEMAYE KWELI KWA MOYO WAKE🤔,TUNAPOTEZA SANA KWA KUFANYA VITU VYA NJE-NJE NA HAVIKO MOYONI AU KINYUME NA UKWELI WA MIOYO. MUNGU ANAPENDEZWA KAMA KUNA KWELI MOYONI(MAHALI PA SIRI) SIO HUKU NJE KUKAWA NA SURA TOFAUTI NA NDANI.(YOUR MOUTHWORK IS INCOHERENT WITH YOUR HEART'S INTENT)

Zaburi 51 : 6  _*Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri,*_

Kuna watu wanachagua kufanya vitu ambavyo ni forgery,yaani wanataka wauigize wokovu *disguise* ,wanaigiza utakatifu,wanaigiza utumishi,wanajikaza na kujitutumua🤔, SIKU MOJA NILIELEZA KUWA NENO UNAFIKI KWA ASILI YAKE KTK KIYUNANI NI *HUPOKRISIS* AMBAYO TAFSIRI YAKE NI *_MCHEZO WA KUIGIZA_* ,KWA HIYO UTAKAPOKUWA UNASOMA MATHAYO 23 AU LUKA 11, UNAPOKUTA YESU ANAWEKEMEA MAFARISAYO KUWA *_"ENYI MAFARISAYO WANAFIKI"_* ALIKUWA AKIWAAMBIA ENYI MAFARISAYO MFANYAO MAIGIZO. SASA UNAJUA NINI,YALE MAIGIZO YAO YALIWASAIDIA KUWAPUMBAZA WANADAMU WAVIVU KIROHO WAWAPE HESHIMA KWA KUKIKALIA KITI CHA MUSA HUKU WANAIGIZA TU. NDIVYO KWAKO USIYESEMA KWA MOYO(MNAFIKI/MUIGIZAJI) UMEFEKI(COUNTERFEIT) WOKOVU UTABAHATIKA KUMNASA BINTI/KIJANA WA KIUME ASIYEKAA NA BWANA VIZURI UKAMZINISHA,LAKINI HAYO YOTE HUJAMFICHA MUNGU KITU. MUNGU ALICHAGUA KUSHUGHULIKA NA MOYO,NDIO MAANA ANAITWA *ALIYE SIRINI,AONAYE SIRINI!*

Yeremia 17 : 10  *_Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake._*

1 Mambo ya Nyakati 28 : 9
*_kwa kuwa Bwana hutafuta-tafuta mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, ataonekana nawe; ukimwacha, atakutupa milele._*

👆🏼👆🏼HUTAFUTA-TAFUTA(CHUNGUZA)

Mathayo 6 : 18
_*ili usionekane na watu..............ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.*_

WOKOVU HAUIGIZWI,WOKOVU NI KITU HALISI MTU ANAKIPATA KWA KUKUTANA NA YESU BINAFSI. UKIISHA KUIGIZA HAIVUNGI WALA KUMFUMBA MACHO MUNGU,UTAJIGUNDUA WEWE MWENYEWE KILA UKIWA MWENYEWE HAUMHISI MUNGU KAMWE *(YOU DON'T FEEL GOD).* KWA KUWA MUNGU ANAJUA MOYONI MWAKO HAKUNA KUMHOFU YEYE (Yer 2:19) ,

*HAKUNA JAMBO TAMU KWENYE MAISHA HAYA YA SASA,KAMA KUKAA NA BWANA*
Sasa huyu Mungu aitwaye BWANA hawezi kuvungwa akajichanganya kukaa na muigizaji, *NEVER!*

HAKAI NA YEYOTE!

Zaburi 15 : 1
_*Bwana, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu?*_

ANASEMAJE!

Isaya 57 : 15
*_Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu._*

Isaya 33

_*14 Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?*_
*_15 Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung?utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu._*
*_16 Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.Nchi ya Mfalme Mkuu_*
*_17 Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri wake, yataona nchi iliyoenea sana._*
_*18 Moyo wako utatafakari hofu ile; Yuko wapi yeye aliyehesabu? Yuko wapi yeye aliyeupima ushuru? Yuko wapi yeye aliyeihesabu minara?*_

KUKIWA NA WATU BILIONI 2,IDADI HIYO HAIMCHANGANYI MUNGU,WALE WANYOFU WA MIOYO HATA WAKIWA 8 TU ATAWABAINISHA.
MUDA UNAENDELEA *KU-MASQUERADE*(JIBADILISHA KWA KUIGILIZA) HUKU NJE,HUPATI FAIDA YOYOTE,IPO SIKU YA KUJILIWA KWAKO WEWE MWIGIZAJI,HUTASALIZIWA JIWE MOJA JUU YA JINGINE(LUKA 19:44),MUNGU ANATUTAKA TUSAFISHE KWANZA NDANI,HUKU NJE IKO *GUARANTEED* KWAMBA UKISAFISHWA NDANI KWA KWELI(YOHANA 17:17) NJE KUTAKUWA SAFI,NA SIO KUWA BIZE KUPAKA MAKABURI CHOKAA.
Mathayo 23 : 26
_*Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi.*_

👆🏼👆🏼KWA NINI NI MUHIMU KUWA BIZE KUSAFISHA NDANI? ILI MUNGU YULE MWENYE KUWAINUA NA KUWATUKUZA WATU  AKUONE. ZAMA ZILE ZA MFALME SAULI BIN KISHI,MUNGU MWENYE KUTAFUTA-TAFUTA MIOYO ALIMUONA MKWELI WA MOYO ALIYEKO MACHUNGANI

Matendo ya Mitume 13 : 22
_*Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.*_

UKIISHA KUWA MKWELI MOYONI HUNA HAJA YA KUFANYA SHOW-UP WALA SHOW-OFF (KUJIONESHA) BALI MUNGU ATAKUJAZI,ATAKUCHOMOA MAFICHONI ILI AKUTUKUZE,JITIHADA ZA MAOFISA NA MAMENEJA KUFICHA FAILI LAKO HAYATAFUA DAFU KWA MKONO WA MUNGU,ATAMNYIMA USINGIZI MKURUGENZI AU YEYOTE MWENYE NAFASI YA KUKU-PROMOTE KAMUULIZE MODEKAI,AHASUERO MFALME ALIITISHA VITABU (MAFAILI) VYOTE NA NDIO UKAWA MWANZO WA KUINUKA KWA  HUYU MYAHUDI AKIWA UGENINI.

HIZI NI NYAKATI ZA HATARI, AMBAZO UIGIZAJI UMEKUBUU,TUNAO WALOKOLE  WANAOWEZA KUZINI NA KUBAKI WAME-RELAX 😎 *_until further notice_*

Mithali 30 : 20
_*Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu; Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu.*_

👆🏼👆🏼UMEIONA HIYO KALI? KWA TAARIFA YAKO UAIPOSHUGHULIKIA UZINZI KWA KUUPELEKA MSALABANI(MITH 28:13) IKIWA NI PAMOJA NA KUUKIRI KWA KUUNGAMA *_I BET YOU_* UTARUDIA TU TENA KWENYE SAFARI YAKO HIVI KARIBUNI. UNAONA NI UJANJA KUPANGUSA MIDOMO NA KUSEMA SIJALA MIMI🙊,UTAPATA HASARA YA NAFSI. KITU KIBAYA ZAIDI NI KUKOSA KUKAA NA MUNGU NA UNAMKOSA MUNGU(KUNA KUMKOSEA MUNGU NA KUMKOSA MUNGU) UKIMKOSEA SI MBAYA KAMA KUMKOSA(MWANZO 39:9) WANAOFANYA MAIGIZO WAPO KWENYE HATARI YA KUMKOSA MUNGU,USIOMBE UKUTWE NA DISASTERS/MAJANGA YOYOTE KWENYE MAISHA YAKO,MAANA UKIMWITA MUNGU ATAKUWA ANAKUCHEKA TU 😂😂😂

mithali 1

*_24 Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa;Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;_*
_*25 Bali mmebatilisha shauri langu,Wala hamkutaka maonyo yangu;*_
_*26 Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu,Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;*_
*_27 Hofu yenu ifikapo kama tufani,Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli,Dhiki na taabu zitakapowafikia._*
_*28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika;Watanitafuta kwa bidii, wasinione.*_

_*JE! UPO TAYARI KUSEMA KWELI KWA MOYO WAKO,ILI YALE UNAYOYATENDA NA KUYASEMA HUKU NJE YAWE YANAAKISI MOYO WAKO?CHAGUA FUNGU JEMA NA UACHE MAIGIZO KWA MUNGU*_

KUNA DADA NILIKUTANA NAYE AKANIAMBIA TUKIWA KTK STORI,KUWA AMEMWAMBIA MUNGU,KAMA AKITOKEA KIJANA WA KUMCHUMBIA,MIONGONI MWA MAMBO ATAKAYOMJULISHA,NI PAMOJA NA NA KUWA YEYE SIO BIKRA🙉,IT SOUNDS SHAMEFUL ETI! SASA HIZO NI TABIA ZA WALE WASEMAO KWELI KWA MOYO,HUYO KAAMUA AKAE NA MUNGU HANA HAJA YA KUFICHA ILI YULE WA MUNGU AWE RADHI MWENYEWE,SIO WEWE UNAYEFANYA UIGIZAJI *UMESHUSHA INJINI*(ABORTION) MARA TATU UKIWA MWOKOVU HIVYO HIVYO NA UNAFICHA KAMA MTEGO,ILI IKITOKEA HAUSHIKI UJAUZITO KWENYE NDOA,USUMBUE WANAOFANYA MAOMBEZI😒😒 NDIO MAANA BIBLIA ILISEMA USIFANYE HARAKA KUMWEKEA MTU MKONO✋🏾 KUMWOMBEA

1 Timotheo 5 : 22  _*Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.*_

HATARI YA KUKURUPUKA KUWEKEA MKONO NI KUSHIRIKISHWA DHAMBI ZA MTU,WANAOKUJA NA SHIDA YA KUTOZAA,WAHOJI MMOJA MMOJA PRIVATELY ILI KAMA ZIKO ISSUES KAMA ZA KUSHUSHA INJINI BASI MZIFANYIE TOBA KWANZA. KINYUME NA HAPO UMEAMUA TU NGUVU ZIFYONZWE IN VAIN.
UPO TAYARI KUSEMA KWELI KWA MOYO KTK  WOKOVU? UPO TAYARI KUSEMA KWELI KWA MOYO KTK NDOA NA MAHUSIANO? UPO TAYARI KUSEMA KWELI KTK KAZI/OFISINI? FANYA HAYO NAWE UTAMWONA MUNGU KWA HAKIKA

*```HITIMISHO```*
Nakupa shauri,nina uzoefu wa kiroho kuhusu kuharibikiwa mambo ya kiroho,na kutengeneza na Mungu tena kwa namna nyingi. Yanapokufikia haya then ukaamua ku-buy time,au ukashindwa kulipa gharama ndogo ya kutubu na kuacha,ukaendelea na hayo maigizo kwa muda,vitu vitakuharibikia kukawa na gharama kubwa zaidi ya kumkaribia. *HAKIKISHA UMEPATA SOMO LANGU LILE LIITWALO _"mambo ya kiroho yakiharibika tengeneza"_*

NIMEMALIZA!!

Mwl Proo(Prosper Kadewele)
0762879363(whatsapp#)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment