_*NITAKUONDOLEA KINARA (🕎🕯) CHAKO MAHALI PAKE*_
By Mwl Proo
(Mjumbe wa Matengenezo)
0762879363
BWANA YESU KRISTO ASIFIWE!
Ndugu mpendwa usomaye ujumbe huu, baada ya kuokoka, mbinguni haipaswi uwaze kwenda kama kwa bahati nasibu. Kwa sababu unaweza kujitathmini unaishije na Mungu, mnaendelea vizuri na mahusiano yenu?
Mungu yuko *very smart na specific* katika mambo yote sio kama ambavyo taasisi za umma ziliweza kukaa na watumishi hewa, Mungu hawezi kuwa na wale hewa, akiacha magugu yamee na ngano sio kwa faida ya magugu bali anaondoa disturbance kwa ngano safi. Namaanisha nini, Mungu ameset standards kwa kuwa Yeye habadiliki (Mal 3:6,Yak 1:17) ila mtu akishuka chini ya viwango hivyo,kuna mambo yatanyamaza automatically kwa sababu umejibandua kwenye levels zake. *_UTANIELEWA HIVI PUNDE_*
UMEWAHI KUSHUHUDIA HALI HII, WAKATI ULIPOACHA KUFUNGA NA KUOMBA NA KUSOMA NENO NA *KUTUNZA ENZI YAKO*, KUNA MAMBO FULANI YAKA-MUTE(😷😷) NDOTO ZILE ZA KIMUNGU, MAONO YA WAZI, KUSIKIA SAUTI, KUONA VITU KTK ROHO, BUBUJIKO VYOTE VIKAPIGA MKAUSHO😷🤐. Halafu ulipozinduka ukayatenda matendo ya kwanza SIKU ILEILE YA KWANZA ULIPOFUNGA, UKATUBU, UKAJINYENYEKEZA NA KUMTAFUTA BWANA (USO WAKE) GHAFULA VILE VINDOTO VYA KIMUNGU VIKAREJEA, SAUTI ZILE ZA KUKUTIA MOYO NDANI ZIKARUDI ZIKIKUNENEA *_no matter what, wewe ni mwana wa Mungu_* SASA NINI KINATOKEA HAPO, MUNGU YUKO VERY SMART AISEE, UMEVURUNDA KIROHO ANAMYUTI(😷) ILI KUKUSAIDIA UWEKE VITU SAWA, WALA HAKOSEI MAHESABU... UNAPOONA UMEVURUNDA NA NI KAMA *_it is just okey_* UNAONA MAONO YAKO KAMA KAWA,NDOTO KWA WINGI SAUTI KWA WINGI KTK ROHO ILA UNAJUA KUWA ULIIONDOA MADHABAHU KTK MSINGI WAKE,USIJISEMEE MOYONI MWAKO KUWA NEEMA YA MUNGU KUBWA SANA,MAANA KUNA MTEGO WA ADUI ANAYETAMANI USIFIKILIE TOBA YA KWELI(2Pet 3:9b) ,KUNA WAKATI NILITOA USHUHUDA KUHUSU YULE KIJANA WA UGANDA,ALISEMA WAKATI BADO AKIFANYA ZILE KAZI ZA UFALME WA GIZA AMBAPO ALIKUWA ANATOKA ROHO YAKE NA KUUACHA MWILI NA KUUNGANA NA MAJESHI YA PEPO KTK KUSHAMBULIA MAKANISA NA MAISHA YA WALIOOKOKA BINAFSI. ALIELEZA KUWA WAKIISHA MUWINDA MTU MUDA MREFU IKATOKEA AMEFANYA DHAMBI AMBAZO ZIMEKAUSHA UWEPO WA MUNGU BASI WANAITUMIA HIYO CHANCE VIZURI SANA(IKUMBUKWE HUYU ALIYEOKOKA AKAJAZWA ROHO, AKITENDA DHAMBI ROHO MTAKATIFU HAINDOKI,ILA UTAMHUZUNISHA KIASI CHA KUMZIMISHA) *efeso 4:30,1thesalonike 5:19)* TUKIO LA YEYE KUONDOKA NA KUKUACHA KABISA SIO DOGO MAANA LINAKUONDOLEA SIFA YA KUWA MWANA WA MUNGU(rumi 8:14),NA HIYO HUTOKEA MTU AKIMKUFURU ROHO MTAKATIFU *(jitahidi ulisome lile somo langu la Mambo ya Kiroho yakiharibika;Tengeneza)* YULE KIJANA ALISEMA MTU AMBAE AMEHARIBIKIWA KIROHO,KIASI CHA YULE MALAIKA WAKE KUONDOKA, WALIKUWA NA UWEZO KUTUMA ROHO/PEPO MWINGINE WA UFALME WA GIZA AKAJA KUMPOTOSHA,YAANI AKAFANYA KUMWOTESHA NDOTO KAMA KAWAIDA,AKAMUONGOZA KWA SAUTI ILI MTU ASITUBIE MAMBO YAKE KUMTAFUTA MUNGU BALI AENDELEE TU KTK MAKOSA,NA WENGINE HADI WANAANZA HUDUMA WAKIWA KTK MAONGOZI YA HAWA PEPO WALIOKUJA KU-REPLACE KWA HILA NAFASI YA WALE WA KWELI *_HII NI HATARI KUU_*
BAADA YA UTANGULIZI HUO NAOMBA TUJE KTK MOYO WA SOMO
Ufunuo 2 : 5b
*_Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu._*
👆🏼👆🏼👆🏼😪😪😪
Wapendwa ulipokutana na Bwana ukafanywa mwana wa Ufalme ulifanyiziwa kinara(lampstand 🕎💡) ktk ulimwengu wa roho kipo dhahiri, na hicho ndicho sababu ya utukufu wa kimungu na ktk maisha yako naam na kubali popote uendapo, Hicho kinara ndicho kinachofanya viumbe vilivyo ktk ulimwengu wa roho vikitazama duniani🌍 vinaona *MIANGA* 💥💥💥💥💥ikitembea juu ya uso wa nchi (Wafilipi 2:15) Yaani hata ujichanganye na maelfu ya wapagani Shetani na mawakala wake wote wataona ule mwangaza wa kinara chako,hata wachawi wakiwa ktk uchawi wao wataona mmmh mnaona pale💥👀?? Maana tumefanywa moto🔥 na miali yake ni miali ya YAHU *waebrania 1:7*
SASA YESU ANASEMAJE KTK UFUNUO WA YOHANA 2:5B Ukivurunda ishu zako kiroho,na ukaona uendelee zako tu na mambo yako,Anasema atakuja na kukiondoa kinara chako mahali pake. Kinara kikiondolewa tuu. Uwepo wa Mungu unakata hata ukiudunduliza kwa kuweka Cd za kuabudu kama za John Lisu📀📺📻,nyimbo hizohizo zilizokuwa zinakububujisha😪🙌🏽🙏🏾 saivi ni bilabila 0=0😟
Mithali 25 : 20 - _*Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito, Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi; Ni kama siki juu ya magadi.*_
Muda huu utakuwa unatafuta kile kibali cha kimungu kwa kuforce bila mafanikio,ulikuwa unatamanika na kupendwa na kila mtu,watu wanatamani baada ya ibada uwatembelee kwao,saivi mmmh unajisalimisisha mfululizo bila mwaliko,Unajitahidi kuabudisha kwa nyimbo kanisani na tumachozi twa kufoji😢Hatujatokana na kuvuviwa bali unajikumbusha machungu yako binafsi mpaka kamchozi kanatoka,umekuwa mlokole mwenye migogoro na wapangaji wenzako,wafanyakazi wenzako maana kale kamng'ao 💥ka utukufu kame-vanish away,Sasa tukikukuta unazozana na konda(kondakta) wa daladala ni kama mpagani pure,kisa ulimpa nauli akasahau akakudai tena au alikupitiliza kituo kimoja,Ndugu mpendwa maisha ya mtu ambaye ameondolewa kinara chake mahali pake yanakosa MVUTO kabisa hata yeye mwenyewe moyoni mwaka hajikubali. Kama kinara kikiondolewa mahali pake,na mtu akadumu ktk hali hiyo ndipo huyarudia matendo ya giza kwa nguvu,kanaanza kuja kahamu ka sigara 🚬,pombe 🍺,zinaa 💏 etc etc Sababu kuu ni kwamba anakuwa hana sababu ya kuendelea kutenda haki.Si anajifikiria kwa nini aendelee kujizuia na hayo wakati moyoni anasikia ukame usio na Mungu hata chembe,ndipo tunamwona aliyekuwa mlokole mzuri leo hii anahudhuria club/disco ,hana sababu ya kuacha hizo viti tena hata kama hakuwahi kuhushuria kabla ya kuokoka,atajifunza kutongoza wanawake kwa bidii hata kama hiyo haikuwa tabia yake *ANAPOKEA UJASIRI WA KUTENDA DHAMBI* maana kinara kikiondolewa unakuwa huru mbali na haki,na ukiwa na kinara chako mahali pake unakuwa huru mbali na dhambi.
NB:-
KINARA KIKIONDOLEWA LAZIMA USHUKE/USHUSHWE VIWANGO
Amosi 5 : 3
_*Kwa kuwa Bwana MUNGU asema hivi; Mji uliotoka nje wenye watu elfu, utasaziwa watu mia, na mji uliotoka wenye watu mia, utasaziwa watu kumi, kwa nyumba ya Israeli.*_
SASA NDUGU MSOMAJI, KAMA UNASOMA NA KUJIGUNDUA UNA SHIDA YA KINARA CHAKO KUONDOLEWA, NI WAKATI WAKO WA KUAMUA KUMRUDIA BWANA KWA TOBA HALISI, YA KWELI. USIJIKAZE TAFADHALI .HII NDIYO SAUTI YA MUNGU KWAKO USIPOISIKIA UNAPEWA OLE NA BWANA
Sef 3:1-2
*_1 Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu!_*
_*2 Hakuitii sauti; hakukubali kurudiwa; hakumwamini BWANA; hakumkaribia Mungu wake.*_
OLE HII NI JUU YA TABIA NNE
a.)Hakuitii sauti (kwa ujumbe huu wa whatsapp/fb)
b.)Hakukubali kurudiwa
c.)Hakumwamini BWANA
d.)Hakumkaribia Mungu wake
ALIYEONDOLEWA KINARA ANAKUWA NA KILA SABABU YA KUTOOMBA, KILA SABABU YA KUJIMISISHA IBADA, ANA KILA SABABU YA KUTOAMKA USIKU KUSOMA BIBLIA NA KUSALI, ANA KILA SABABU YA KUTOTOA SADAKA YA MAANA, WALA HANA SABABU YA KUFUATA TARATIBU ZA KIMUNGU, MAANA NAFSI YAKE YAJUA SANA, KUWA HATA AKIFANYA HAYO *_HAWEZI KUMWONA MUNGU AKIMTEMBELEA_*
UNAYESOMA NA UNAONA MOYONI UNAUGUA NA KUSUMBUKA,WEWE UNA MOYO WA TOBA NA UNASAMEHEKA KABISAA WEWE NI WA BWANA, NENDA UKASEMEZANE NAYE HIZO DHAMBI AMBAZO ZIMEKUWA NYEKUNDU KAMA BENDERA 🇭🇰 🇦🇱 BWANA YESU ATAZISHUGHULIKIA. ILA WEWE AMBAYE UNAPOSOMA HAYA MANENO; sura yako ipo 🙁 halafu moyo ume👉🏾😏kabisa huku unasema *huyu naye* kwako wewe kalaga-bao..SUBIRI MJUMBE MKALI (MITHALI 17:11, 2Kor 12:7)
Mithali 17 : 11
_*Mtu mwovu hataki neno ila kuasi tu; Kwa hiyo mjumbe mkali atatumwa kwake.*_
Mjumbe mkali ambaye Mungu atamruhusu ni mbadala wa wito wa toba kwa ujumbe huu.Kwa hiyo kuna watu watatubu wakiwa wodi ya Mwaisela kule Muhimbili National Hospital 🛌💉🌡💊
ILA MUNGU MWINGI WA HURUMA ANAKUPENDA, ANAKUTAMANI KIASI CHA KUONA WIVU (yakobo 4:5). FANYA TU UJE NDUGU YANGU HE IS WAITING FOR YOU🤗AKUPOKEE NA KUKIRUDISHA KINARA MAHALI PAKE,USIPONISIKIA HILI NAKUAMBIA BASI.
*_```NIMEMALIZA MIMI PROSPER KADEWELE!!!```_*
Mwl Proo
0762879363
(Welcome to All Truth whatsapp group)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment