*_MWILI WA ROHO_*
Expounded by _Mwl Proo_
0762879363(whatsapp only)
Bwana Yesu asifiwe sana,karibu ktk darasa.Yako masomo ninayofundisha yanahusika na kushughulikia maisha ya kiroho (edification-based teachings) lakini mengine kama hili la leo yamejikita ktk kukupa maarifa(knowledge-based),yale masomo yanayojenga nafsi yatakusaidia kuishi maisha ya wokovu bila kusitasita.Ila masomo ya maarifa kama hili,ni kukusaidia uweze ku-operate kwenye viwango vingine ktk maisha ya kiroho. Kuna maarifa fulani usipoyapata utabaki unaoperate kwenye *_dimensions_* zilezile umezoea.
YESU KRISTO BAADA YA KUFUFUKA,ALIJUA KUWA KUNA SHAKA NDANI YA WALE WANAFUNZI KUWA HUENDA AKAWA SI YESU YULE,IKAWA NI ROHO YAKE,NDIPO AKASEMA
Luka 24 : 39 *_Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo._*
👆🏼👆🏼👆🏼
KWA KUWA ROHO HAINA MWILI NA MIFUPA,POINT YA MUHIMU SANA.
LAKINI UKIACHA WACHACHE WENYE KUAMINI UKIFA,HAKUNA KINACHOENDELEA(LOW VIEW FOR AFTERLIFE) UKWELI NI KWAMBA HATA BAADA YA MTU KUKATA PUMZI YA UHAI(KUFA) YULE MTU WA NDANI AMBAYE NDIYE HALISI,HUONDOKA!
HUWA NAIPENDA HII KAULI USEMAYO MTU NI ROHO ANAYEISHI NDANI YA MWILI NA ANAMILIKI NAFSI,INAJARIBU KUTAKA KUELEZA KWA SEHEMU USAHIHI WA MTU.
*_Tusome_*
1 Wakorintho 15 : 44 *_hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko._*
KTK ANDIKO HILI TUNAKUTANA NA MANENO HAYA *MWILI WA ROHO* ,YESU ALISEMA ROHO HAINA MWILI MIFUPA YAANI HATA MTU AKIKIONA KIUMBE CHA KIROHO AKIENDA KUKISHIKA ANAWEZA KUTA UPEPO TUU NDIO MAANA AKAHIMIZA _*NISHIKENISHIKENI*_ (Luka 24:39) NA TAFSIRI YA NENO ROHO UKIENDELEA KULIFUATILIA MZIZI WAKE RUACH(LEV)/PNEUMA/GHOST/WIND/UPEPO(PEPO)/KIVULI NA WAYAHUDI WALIAMINI TRADITIONALLY MTU ANAYO ROHO(MALAIKA) YAKE INAYOWEZA KUTOKEA AKIWA KWA MWONEKANO KAMA YEYE LAKINI SI YEYE HALISI
Mathayo 14 : 26
*_Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli(ghost); wakapiga yowe kwa hofu._*
Matendo ya Mitume 12 : 15 *_Wakamwambia, Una wazimu. Lakini yeye akakaza sana, akasema ya kwamba ndivyo hivyo. Wakanena, Ni malaika wake._*
*JE! ILE ROHO YA MWANADAMU,INAYOTOKA ANAPOFARIKI MTU NDIO MWILI WA UFUFUO?*
ROHO NI ROHO SIO MWILI,ILA ROHO INAWEZA VIKWA MWILI KWA NAMNA YOYOTE. IKO MIILI YA MBINGUNI(ROHONI) AU YA ULE ULIMWENGU WA ROHO NA HAPO TUTAPATA CONCEPT NZURI YA MWILI WA ROHO.
1 Wakorintho 15 : 40 *_Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali._*
KTK UKRISTO TUNAAMINI KUHUSU KUFUFUKA/UFUFUO. KUFUFUKA KWA KUURUDIA MWILI WAKO *_EGEIRO/ANHISTEMI(KIYUNANI)_* INAHUSISHA ROHO ILIYOKWISHA ONDOKA KUJA KUURUDIA TENA MWILI,YALE MAMBO YA KUPIGA CHAFYA ZA MTU ALIYEFUFUKA NI ACTIVATION TUU YA SHUGHULI ZA KIBAILOJIA YA MWILI BAADA YA ROHO KUURUDIA MWILI(HII SIO SABABU YA CHAFYA KITABIBU).
Luka 8 : 55
*_Roho yake ikamrejea, naye mara hiyo akasimama. Akaamuru apewe chakula._*
STORI ZOTE ZA BIBLIA KUHUSU KUFUFUKA KULIHUSISHA ROHO KUURUDIA MWILI ULE WA ASILI(MORTAL BODY) HATA BWANA WETU YESU NAYE ALIURUDIA MWILI WAKE ULIOKAA KABURINI SAA ZISIZOPUNGUA 36(MORE THAN 36HOURS) NA ILIKUWA LAZIMA AURUDIE MWILI WAKE KABLA HAUJAOZA(DECAY) UTIMIE UNABII *Zaburi 16:10* ,INGAWA YEYE ALIPOFUFUKA ILIHUSISHA AINA YA UFUFUO NYINGINE YAANI ALIHUISHWA MWILI WAKE KWA KUTOHARIBIKA TENA,IKUMBUKWE KAMA MTU ATAFANYA MUUJIZA WA KUMFUFUA MTU(ANHISTEMI/ANASTASIS) YAANI MTU ANAFUFUKA KWA MWILI AMBAO LAZIMA AFE TENA,HAIFANANI NA ULE UFUFUO AMBAO MTU ANAFUFUKA KWA MWILI USIOKUFA TENA KAMA ULE WA *_ANABIOSKOMAI_*,NA YESU ANAITWA *_MZALIWA WA KWANZA KTK WAFU_* KWA MAANA YEYE NDIYE WA KWANZA KUFUFUKA ILI ASIFE TENA KTK HII NEW ERA.
ELIYA ALIMFUFUA MTOTO WA MAMA MJANE(1FALME 17:17-23),ELISHA ALIMFUFUA MTOTO ALIYEUMWA KICHWA NA KUFA(2FALME 4:30-31),MIFUPA YA ELISHA ILIMFUFUA MTU (2FALME 13:21),PETRO ALIMFUFUA TABITHA/DORCAS (MDO 9:36-42),PAULO ALIMFUFUA EUTIKO(MDO 20:7-12),KUNA WAFU WATAFUFULIWA WAKATI WA UNYAKUO,KUNA WAFU WATAKAO FUFULIWA WAKATI WA KUJA KWA YESU MWANZONI MWA MILENIA(UFUNUO 20:4),NA WENGINE BAADA YA MILENIA(UFU 20:5) WAKATI WA *WHITE THRONE JUDGEMENT* ,MAANA KUNA UFUFUO WA WENYE HAKI NA WASIO NA HAKI PIA(MDO 24:15), NA KTK FUFUO HIZO IKUMBUKWE SIO TU MIILI ITAKUWA IMEOZA BALI IMEBAKI MIFUPA NA MINGINE IMEPOTEA KABISA KWA SABABU YA GEOLOGICAL PROCESSES,LAKINI ROHO ZILE ZILIZOONDOKA WAKATI WA VIFO ZITAVIKWA MIILI MINGINE. YESU ALIMFUFUA KIJANA (LUKA 7:11-17),ALIMFUFUA BINTI YAIRO (LUKA 8:41-56),KTK FUFUO ZOTE ZILIZOWAHITOKEA KAMA MUUJIZA,WATU WALIIRUDIA MIILI YAO ILEILE KABLA HAIJAHARIBIKA KASORO KWA LAZARO AMBAYE BWANA WA UFUFUO MBALI NA KUIRUDISHA ROHO YAKE ILA ALIUHUISHA MWILI ULIKWISHA OZA NA KUTOA HARUFU *(NOTHING IS IMPOSSIBLE WITH GOD )* WALE WALIOFUFULIWA KWA KUHAMISHWA TOKA KUZIMU(MATH 27:51-53) KWENDA KWENYE *GAN ADEN* KUMEZINGATIWA *_(pata somo langu la umilele/eternity)_* kwa maarifa zaidi.NA KWA WALE AMBAO MUDA WA UNYAKUO WATAKUWA HAI MIILI YAO ITABADILISHWA KUTOKA KWENYE ULE MWILI WA ASILI KUWA ILE MIILI YA ROHO/YA UMILELE(1KOR 15:51-52)
*SASA TUJE KWENYE MOYO WA SOMO LETU LA MWILI WA ROHO.*
NAPENDA KUWEKA MSINGI WA KWANZA,KUWA KWELI YA MUNGU HATUPASWI KUIPATA KWENYE NDOTO NA MAONO NA MAFUNUO,BALI NDANI YA NENO LAKE TUU,NA VYANZO VINGINE VYOTE NI SECONDARY SOURCES LAKINI PRIMARY SOURCE NI NENO LA MUNGU KTK BIBLIA,NA TAARIFA YOYOTE KTK SECONDARY SOURCES IKIKINZANA NA BIBLIA,TUPA KULE👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾,UTAKAYOSIKIA KWENYE SHUHUDA AU MAFUNUO YA YULE NABII WENU NI *_SUPPLIMENTARY INFORMATION_* MKIYAFANYA KUWA NDIO MSINGI,MTAPOTELEA NDANI
WAPENZI TWENDE KTK DARASA HILI,NA UKWELI NI KWAMBA MUNGU ALIVIUMBA VITU KTK ROHO KABLA HAVIJAONEKANA KTK MWILI( *_the book of moses 3:5_*) WAPENZI NDIVYO ILIVYO ROHO YA MWANADAMU IS THE REAL BEING.SASA ROHO HATUITAZAMII IONEKANE KWA MACHO YA DAMU NA NYAMA MPAKA IVIKWE MWILI.KAMA AMBAVYO MBEGU HUPANDWA ILA MUNGU HUZIVIKA MIILI TOFAUTI NA ILE MBEGU ILIYOPANDWA
*1Korintho 15:38*
*_38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake._*
SASA JAMBO LA AJABU KUHUSU ROHO YA MWANADAMU,KAMA KAMA MTU ATAIONA KWA MACHO YA ROHONI,AU NAMNA AMBAVYO IKIWA KTK ULIMWENGU MWINGINE INAONEKA KWA NAMNA AMBAYO NI EXACTLY SAWA NA MTU HUYU WA NJE,NA INGAWA MAMBO MENGI HUANZIA ROHONI KABLA YA HUKU NJE,LAKINI AJABU NI KWAMBA ROHO HUWEZA KUONEKANA IKIWA NA HATA ALAMA AMBAZO MWILI WA DUNIANI WA UDONGO UNAZO ILA HAZINA KAZI YOYOTE NI KAMA IDENTITY TUU(HATA KAMA MTU ANA KOVU LA AJALI USONI) IKUMBUKWE ROHO YA MWANADAMU SIO MWILI WALO UFUFUO HAUIHUSISHI ROHO KUJA KAMA ROHO BALI ROHO LAZIMA IVIKWE MWILI FULANI. MALAIKA NI VIUMBE VYA KIROHO YAANI WAO NI ROHO (EBRANIA 1:14) LAKINI KUONA MALAIKA NI JAMBO DHAHIRI MNO HATA SASA,MTU ANAWEZA KUONA 👼🏻 EITHER MACHO YA ROHONI YAMEFUNGULIWA AONE AU MALAIKA WAKAJIVIKA MIILI YA KUONEKANA(INCARNATION) TUNASOMA KTK BIBLIA HABARI ZA MALAIKA WALIOMTEMBELEA IBRAHIMU HUKO MAMRE NA KTK WATATU WAWILI WALITEMBEA KWA MIGUU👣👣MPAKA MJI MWINGINE KWA LUTU,MALAIKA KUTEMBEA KWA MIGUU HADI KUCHAFUKA KWA VUMBI SIO ISHU NDOGO,WAO VIUMBE VYA ROHO *_VILI-INCARNATE_* ,
TUSOGEE MBELE KIDOGO. ROHO YA MWANADAMU INAYAJUA MAMBO KWA UHALISI ZAIDI KULIKO HUKU NJE KWA MWILI WENYE AKILI ZA NAFSI. KTK HUDUMA TUMEKUTA NA WATU AMBAO UNAKEMEA PEPO👹,LAKINI KILICHOPO NDANI YA MTU SIO PEPO/JINN WALE TUWAJUA BALI UNAKUTA KUNA NI *_human spirit_* YAANI UNAKUTA NI MGANGA AU MCHAWI ILA ROHO YAKE IKO NDANI YA MTU. NI KWA SABABU WACHAWI/WAGANGA KWA MAARIFA YA KISHETANI WANAWEZA KUIACHA MIILI WAKAENDA KUOPERATE MAHALI PENGINE WAKIWA NJE YA MIILI.SI WACHAWI TU BALI WENYE ZILE IMANI (DHARMIC FAITHS) KAMA WABUDHA,WAHINDU,WATU WA TAOSIM ETC WANAOFANYA TAFAKARI YA KINA *_YOGA_* WANAWEZESHWA KIPEPO KUIACHA MIILI NA ILE *_HUMAN SPIRIT_* HUTOKA KWENDA KUWASILIANA NA ROHO ZA MIUNGU KTK OTHER REALMS. ULE MWILI UNAOTOKA(ROHO) UITWAO _*ASTRAL BODY*_(telepathy) UNAKUWA UNA UWEZO KULIKO HUYU MTU ANAYEACHWA NA TUKIO HILI LA MTU KUUACHWA MWILI KWA HIARI HUITWA *_ASTRAL TRAVEL_* ( ~willful out of body experience~ )YAKO MATUKIO KTK BIBLIA YANAJADILIWA KUHUSISHA ROHO YA MWANADAMU KUSAFIRI TUKIO LA ELISHA/GEHAZI (2Falme 5:19-27)
mstari wa 26 ktk OJB version wasomeka
*_26 And he said unto him, Went not mine lev (spirit) with thee, when the ish turned again from his merkavah to meet thee? Is it a time to receive kesef, and to receive begadim, and zeitim (olive groves), and kramim, and tzon, and bakar, and avadim, and shefachot?_*
Ezekiel 3:12-15,Pia ktk Ezekiel 8:1-4,Ezekiel roho yake iliinuliwa kutoka ktk mji wa utumwa alienda kwa roho kwenda kutazama mambo huko Yerusalem,Pia habari za Yesu na Nathanael (Yohana 1:43-49) ,Paulo alisema hajui kama ile lift yake ilichukua roho au mwili (2Kor 12:2),Upo mjadala mzuri kuhusu ile *_LIFT_* ya kiroho,ambapo mtu husafirishwa kiroho lakini mwili nao hupanda ktk lift hiyo,Mwinjilist Filipo alipokea lift ya kiroho ,iliyombeba na mwili wake kutoka mji mmoja kwenda mwingine (Mdo 8:39). SASA ELIMU ZA JINSI HII HUITWA *_ESOTERIC_*(esotericism) YAANI UJUZI AMBAO HAUPASWI KUJULIKANA/KUFUNDISHWA KWA WENGI. INGAWA SWALA LA KUSAFIRI KIROHO LINAWEZEKANA,TENA NI RAHISI SANA KWA WATU WALIOKOKA,ELIMU HII HAIPASWI KUWA *_INCORPORATED IN CHRISTIAN DOCTRINE_* KWA SABABU ZA KIUSALAMA,MAANA MTU AKIUINGIA ULE ULIMWENGU NI RAHISI KUKUTANA NA ROHO WENGINE WAKAMKENGEUSHA ASIKUBALI TENA KUSAIDIWA,MAANA ATAAMINI ALIONANA NA MALAIKA WA KWELI AU HATA MUNGU MWENYEWE. RAFIKI WA AYUBU AITWAYE ELIPHAZI MTEMANI ALIYAONA MAMBO KTK ULIMWENGU MWINGINE,NA ROHO FULANI(PEPO) LIKAMPA TAARIFA AMBAZO ZINAKINZANA NA KWELI YA MUNGU,NAYE ANAKUJA KUSIMULIA KWA AYUBU AKIWA NA UHAKIKA KUWA NI MUNGU ,LAKINI UJUMBE WAKE ALIUPOKEA KWA ROHO ZA KIGENI SIO MUNGU (AYUBU 4:12-21) KWA HIYO KAMA MAFUNDISHO YA *_HUMAN SPIRIT_* YASIPOFANYIWA FILTERING NI RAHISI TUKAPOTEZA WATU KABISA,UJUZI HUO NI BORA UBAKI KWA INDIVIDUALS AMBAO AKILI ZAO KWA KUTUMIWA ZIMEZOEZWA KUPAMBANUA (EBRANIA 5:12-14) NAWAKUA WATUMISHI WENYE VIWANGO HIVYO VYA KUSAFIRI KIROHO WALA SIO KWA UWEZO WA KIPEPO,ILA *_SPIRITUAL CAPACITY_* INARUHUSU,WENGINE WENGI KTK WANADAMU ROHO ZAO HUSAFIRI KWA NJIA ZA NDOTO NA MAONO. BILA SHAKA UMEWAHI KUWA KTK MAZINGIRA HALAFU GHAFLA UNAKUMBUKA KWA ULIWAHI OTA NDOTO YENYE MAZINGIRA HAYO,TENA UNAKUMBUKA ULITAMKA MANENO HAYOHAYO NA ULIKUWA NA WATU HAOHAO,HIZI NDOTO SIO MPAKA UWE WA ROHONI HATA WALE WA TABIA YA ASILI ZINAWAKUTA KWA SABABU WANAZO ROHO. SASA ROHO HUWEZA SAFARI IKAYASHUHUDIA MAMBO YA MBELE HATA KAMA NI MIEZI KADHAA MBELE,SEMA MENGI KTK YALE AMBAYO ROHO INAYASHUHUDIA WENGI WAKIAMKA WANAKUWA WAMEYASAHAU.
*HITIMISHO*
NAJUA NIMEFUNDISHA VITU VIGUMU,LAKINI HUO NI UHALISIA,NA NILIPOPATA WAZO NIANDIKE HAYA NILISITA NIKAACHA,ILA MOYONI NILISHUHUDIWA NIANDIKE TUU,MAANA NILISHUHUDIWA MIMI NI MTU SAHIHI KUYAANDIKA HAYA _~hapo sio kujisifu wala kujiinua~_ (YAANI HATA NIKIACHA SIO WOTE WAMEPEWA KUYAJUA HAYA/NA LIPO KUNDI LA WATU WACHACHE AMBAO WATASAIDIKA KWA SOMO LA *MWILI WA ROHO*) TO THEM THIS IS DIAMOND💎 TO THE REST IS GARBAGE
For inquiries
Mwl Proo(Prosper Kadewele)
0718922662
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment