Thursday, November 16, 2017

PASIPOKUWA NA MWILI WANGU HUU; NITAMWONA MUNGU!

*PASIPOKUWA NA MWILI WANGU, NITAMWONA MUNGU!*

_Mwl Proo_
0762879363

Bwana Yesu asifiwe sana!
Watu wa nyakati hizi, wanatamani hata kumwelekeza mhubiri  aongee vitu gani. (Isaya 30:10ff) Yaani ukijikita kuhubiri mambo yasiyosisimua matamanio yao ya maisha ya mwilini, Amen zinapungua. Hiyo imetuletea kuwa na namna moja ya kusikia, passport mara visa ya Ulaya, kupanda ndege, mara utaolewa mwaka huu katika jina la Yesu! Tusikiapo habari isiyotutumainisha maisha ya mwili huu, tunavunja ushirikiano na mhubiri.
The balanced diet of the Gospel, haipaswi kuwa upande mmoja,  wajulishwe kuwa Mungu anawakusudia kuwa na maisha mazuri ya sasa (yasiyo yakini 1Timothy 6:17), pia anawakusudia wasipoteze ule umilele. Yaani Yesu alikuja ili wawe na uzima (wa sasa), kisha wawe nao tele (wa zama zijazo zisizo koma).

AYUBU ALIISHI MIAKA YA ZAMANI SANA, ZAMA ZA WAJUKUU WA ESAU. UFAHAMU WAO KUHUSU MUNGU ULIKUWA SO SPECIAL, INGAWA HAUFIKII WA ZAMA HIZI ZA ROHO. RAFIKIZE AYUBU WALIKAA NAYE SIKU ZOTE AKIWA KATIKA KUUGUA, WALIKUJA KUTOA FARAJA HUKU WAKIMSIMANGA. NAYE ALIWAITA WAFARIJI-WATAABISHAJI, NAAM MATABIBU WASIOFAA. BAADA YA KELELE NYINGI ZA AKINA ELIFAZI MTEMANI, AYUBU ALIGUNDUA KUWA, WAMEWEKA STRESS KUBWA KATIKA MAMBO YA MWILI ULIOHARIBIKA, WAKASAHAU UKWELI KUHUSU AYUBU HALISI, SI YULE ALIYEKAA NA KUJIKUNA MAPELE KWA KIGAE, BALI YUPO AYUBU HALISI. NDIPO AKASEMA

Ayubu 19 : 26
*_Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;_*

πŸ‘†πŸΌπŸ‘†πŸΌHILI NDILO TUMAINI KUU HATA SASA. HUU MWILI WA NJE USIKUPUMBAZE KAMWE MPENDWA WANGU, TENA HUU MWILI TUNAUITA OUTER-CARCASS (MZOGA WA NJE). JITAHIDI SANA USOME SOMO LANGU LIITWALO MWILI WA ROHO NA LILE LA UMILELE. _*Waweza kulipata la umilele kwa hii link*_

http://alltruthjohn1613.blogspot.com/2016/09/sehemu-ya-somo-la-umilele.html

AYUBU ALIJUA KWA HAKIKA, ATAPOFUNGA MACHO KWA MARA YA MWISHO. YATAFUMBUKA YALE YA UMILELE, NA BADO ATAMWONA MUNGU, MAANA ALIISHI KWA UNYOFU (AYU 1:1ff). HUPASWI KURUHUSU KUUHARIBU MWILI HUU WA NJE, MAANA HUU NDIO NYUMA YAKO YA KUPANDA YA BAADAE. KATIKA SOMO LA UMILELE NIMETIA MKAZO, USIKUBALI KUISHI NA MAGONJWA, MAANA HAYO YANAWEZA KUKUONDOA HAPA DUNIANI UKIYAENDEKEZA, MAANA MAGONJWA NI MLANGO MWEPESI WA KIFO CHA KIMWILI NA KIFO NI MLANGO WA UMILELE. USISEME NITAKUFA KWA RATIBA YA MUNGU, HALAFU UNAENDESA GARI LAKO CARELESSLY, AU KUTOZINGATIA MAMBO YA AFYA KABISA, HAPANA!!!! MWILI HUU UUTUNZE MAANA UNA FAIDA YAKE KUKUFANYA UYATIMIZE ULIYOPANGIWA, USIUHARIBU (1Kor 3:16-17). KUNA AMBAO WALIWAHI PATA AJALI, IKAVURUGA MISHIPA FULANI YA FAHAMU, NI IKAWA NDIO MWISHO WAO WA KUFANYA MAAMUZI YA MWILI HUU, YANAYOATHIRI ROHO ZAO NA UMILELE WOTE. KUNA MCHUNGAJI AMEFARIKI MWAKA JANA, LAKINI AKIWA HOSPITALI, ALIPATA NAFASI YA KUWEKA MAMBO YAKE YOTE SAWA AKIWA KATIKA MASKANI YA MWILI HUU. KILA ALILIKUMBUKA HALIKO SAWA, ALILIWEKA SAWA! ALIPOKUMBUKA KUNA MTU ALIMKOSEA ALITUMA UJUMBE WA KUMWOMBA WAWEKE SAWA. MAANA MADAKTARI WALIMWAMBIA KANSA IMELAMBA INI KWA STEJI AMBAYO, HAKUNA NAMNA KABISA. ANGEWEZA KUWEKA IMANI YA KUPONYWA, LAKINI YEYE MWENYEWE ALIJUA MUDA WAKE UMEFIKA. SASA SIO WOTE WAKIWA DAKIKA ZAO ZA MWISHO WANAPATA NAFASI YA KU-CLEAR DOUBTFUL WAYS, NA ZILE *SUSPENDED CASES*, YAANITU KUNA JAMBO AMBALO ANAJUA LINAMKINGA KIROHO, NA ANAPASWA KULIWEKA SAWA. YEYE MWENYEWE ANASEMA KABISA NDANI YAKE, KAMA KUNA JAMBO LINAWEZA KUNIKOSESHA MBINGU NI HILI. ILA LIKO SUSPENDED, ANASUBIRI SIKU MOJA APATE MWANYA WA KULISHUGHULIKIA. SASA HIYO NI HATARI KUKAA NA SUSPENDED ISSUES, KWAMBA UTATENGENEZA SIKU MOJA. KAMA KUNA JAMBO UMEMFICHA MMEO UNASUBIRI SIKU MOJA UTAWEKA SAWA, NI HATARI, UKIPATA SHIDA KAMA ZA AJALI, AU MWILI UKADHURIKA KATIKA MISHIPA YA FAHAMU, UNAWEZA KUWA KATIKA SEMI-CONSCIOUS STATEπŸ›Œ UKAWA WODINI KATIKA HALI YA COMA, LAKINI USIWEZE KUFANYA CHOCHOTE KILE. NA HIYO ITAKUWA NI NAFASI YAKO YA MWISHO KABISA. KWA HIYO MWILI UUJALI TU KWA SABABU HII, LAKINI HUU MWILI USIUPE FIRST PRIORITY, USIUANGALIE:-

Warumi 13 : 14
*_Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake._*
MWILI HAUPASWI KUANGALIWA SANA,UUJALI KWA KUULISHA NA KUUVIKA KWA STANDARD NZURI INAYOKUBALIKA KWA JAMII YA WASTAARABU. LAKINI UKITAKA UTENDE KILA KITU AMBACHO MWILI UNATAKA, HAUTASALIMIKA.
MWANAFALSA WA AWALI KABISA AITWAYE ARISTOTLE, ALISEMA MWANADAMU HAUFIKII UTOSHELEVU MPAKA AWE NA MUNGU (we only reach to our full satisfaction with God). SASA MWILI WAKO, UTAKUENDESHA MPAKA UTAMKOSA MUNGU NA MBINGU, UNAPOJITAHIDI KUUTOSHELEZA;

Mhubiri 1 : 8
_*Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.*_

Hagai 1 : 6  *_Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka._*

HAUTAUTOSHELEZA MWILI HATA SIKU MOJA, KUNA WATU WANANDOA NNE, NA DINI IMEMRUHUSU KUOA WANAWAKE WANNE, LAKINI BADO UTASIKIA ANA SCANDALS ZA SIDE-CHICKS (MICHEPUKO) KAMA KAWAIDA. UKIWA UNALIPWA MSHAHARA MILIONI 10 KWA MWEZI, MWILI UTASEMA NI NDOGO HIYO, PIGA DILI LA WIZI HAPO, THAT IS THE BODY (MZOGA WA NJE)!. ANAYELEWA KWA VILEVI, MWULIZE UNA MIAKA MINGAPI TANGU AUNZE KUNYWA POMBE? HAJAWAHI KUTOSHELEZWA MWILI UKASEMA ENOUGH!!✋🏾

SASA MUNGU AMENITAKA KUKUKUMBUSHA, KUWA USIUANGALIE MWILI WAKO, KIASI CHA KUTAKA KUUTIMIZIA YOTE, HATA UNAYOYAHITAJI KINYUME NA MAPENZI YA MUNGU. MAANA PASIPO KUWA NA HUO MZOGA WA NJE (MWILI), BADO UTAMWONA MUNGU, UTAMTAZAMA YEYE, WALI SI MEINGINE. MAISHA NA UZIMA ULIONAO KATIKA MWILI, UNAO KATIKA IMANI YA YESU, YAANI SI WEWE UNYEPASWA KUISHI, BALI YESU KRISTO NDANI YAKO (GAL 2:20). KAMA UNAVYOUPENDELEA MWILI WAKO KWA MAVAZI MAPYA, TENA NAMBA ZAKO UMEACHA KWENYE ZILE BOTIQUES, KWAMBA KUKIWA NA _*NEW ARRIVALS*_πŸ‘”πŸ‘šπŸ‘•πŸ‘™πŸ‘—πŸ‘˜πŸ‘ πŸ‘‘πŸ‘›πŸ’WAKUTONYE, SI VIBAYA!! LAKINI YESU ALITAMANI UZURI HUO NA HIYO CARE IANZIE ROHONI (3YOH 1:2). AKASEMA SAFISHA KWANZA NDANI, ILI NJE NAKO KUPATE KUWA SAFI. WALIOWAHI KUTOKA KATIKA MWILI HUU WAKAIONA MIILI HII WAKIWA NA MIILI MINGINE, WANASEMA WALITIA MGOMO KUIRUDIA HII TENA, MAANA WENGI WAO WANASEMA WALIIONA NI KAMA NGOZI YA KENGE ILIYOHARIBIKA. KUMBE PAMOJA NA SPECIAL SUITS ULIZOVAA, PAMOJA NA JITIHADA ZA KUPAKA WANJA, NA KUNYOA NYUSI HALISI NA KUWEKA ZA KUCHORA, MPAKA  KOPE UMEONGEZEA ZILE SYNTHESIZED EYELIDSπŸ‘, NA UMEJIPATIA UMASHUHURI MKUBWA KWA VIJANA NA WANAUME WAHUNI, AMBAO UKIPITA MBELE YAO UNAZUA GUMZO, BAD ENOUGH WENGINE ILITOKEA WANA MAUMBILE FULANI AMBAO ULIMWENGU WA LEO UNADAI NI YENYE MVUTO, BASI NAWE UKAKOLEZA ZAIDI NA GANI LILILOSHONWA KWA MSHONO UITWAO _*DUKA WAZI*_.  MPASUO HUO NI HATARI, UKIPIGA HATUA PAJA LOTE NJE πŸ€”. NA WAOVU HAWAONYI, BALI WAKIONA HIYO MINI-SKIRT YAKO YENYE USHAWISHI WA NGONO, UTASIKIA *_YOU HAVE DRESSED TO KILL_* HIYO NI PONGEZI AISEE SIO MAUAJI! SASA USIPOPATA TUTAKAO KUELEZA UKWELI UTAANGAMIA KWA UANGAMIVU MKUU, MAANA UKIISHA SHUKA KABURINI ,☠⚰HAKUNA UMASHUHURI WA KUONESHEA MAPAJA HUKO. MUNGU ALIPOKUPA MWILI HUO, HAKUUWAZIA UWE WA KUKUPOTEZA MILELE. ALITARAJIA UMTUKUZE NA UMHESHIMU KWA MWILI WAKO, WENGINE HUENDA HAWANA MWONEKANO KAMA WAKO UKO SO *_PRESENTABLE_*, YAANI TUKIKUWEKA KWA TV UHUBIRI VYA YESU, MPAKA WENGINE WAJISHTUKIE, KWAMBA KAMA HUYU ANASEMA YESU YESU YESU, NA SISI WENGINE JE TULIO DUNI (INFERIOR)???.

DADA YANGU NA KAKA YANGU, MUNGU ALINIPA NEEMA YA KUFAHAMU KWA SEHEMU KUBWA, MAMBO YA MAISHA NJE YA DUNIA HII, HATUWEZI SEMA TUACHE KAZI, TUSITAFUTE PESA, TUSIENJOI MAISHA, HAPANA KUFURAHIA MAISHA YAKO KATIKA DUNIA  HII NI HAKI YAKO, HATA KWENDA BEACH NA WIFE WAKO NI πŸ‘πŸ½πŸ‘«(Mhubiri 9:9). LAKINI MUNGU KUNA ANACHOHITAJI KWAKO, UJIDHABIHU MWILI WAKO KWA BWANA. UTAKAPOKUWA UNAUOMBEA MWILI WAKO USIUGUE MAGONJWA MABAYA, UWE NA HOJA YA MAANA KWAMBA, YOU CAN ONLY SERVICE THE PURPOSE/COUNSEL OF GOD UKIWA NA MWILI HUO SALAMA. OMBA MUNGU AKUJAZE UZIMA ILI UMTUMIKE, KATAA VIFO VYA GHAFULA, HASA KUSUDI LIKIWA BADO. USIWE BIZE KUINVEST DUNIANI TUU, AMBAKO UNAWEZA UKAONDOKA TU BILA GIA MAALUM (MATH 6:19-21, LUKA 12:15-21). KUNA WATU JUZI WAMEENDA KIKAZI MVUMI-CHAMWINO DODOMA, KWA KAZI ZA SERIKALI NA GARI LAO LA STJ, WAKIJUA WATARUDI WAKALIPWE POSHO ZA UTAFITI WAO, ILA HUO ULIKUWA NI MWISHO  WA KUIONA SAYARI IITWAYO DUNIA. WAKAUAWA KWA KUKATWA VIUNGO NA KUCHOMWA MOTO KWA KUNI, NA WANANCHI AMBAO KWA ULIMBUKENI HAWAKUJUA KAZI YAO.

SASA MIMI NIMEMALIZA, UKIPATA HASARA YA NAFSI YAKO, MUNGU ATAKUHUKUMU KWA HAKI, MAANA AMEKUPA KUYASIKIA HAYA LEO.

Mwl Proo
Reformer
Welcome to ALL TRUTH whtsapp group(via 0762879363)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment