Wednesday, November 15, 2017

UCHAFU WA DUNIA, HAUTUZUII SISI KUWA WATAKATIFU!

*UCHAFU WA DUNIA, HAUTUZUII KUWA WATAKATIFU.*

```Na Mwl Proo```
~_(Mjumbe wa Matengenezo)_~
0762879363

Mungu awabariki nyote, unayefuatilia mfululizo wa masomo haya, mwisho wake utafaidika na kuwa na maisha yaliyojitengeneza kwa Bwana, katikati ya uharibifu wa machukizo. Wakati uwepo wa Mungu unaadimika, kwenye maisha ya watu binafsi, wewe utaogelea kama mwanzo na kuzidi, maana sharti utukufu wa pili uuzidi ule wa kwanza (Hagai 2:9).

Bado natafakari jibu alilolitoa Televangelist wa kimarekani, T.D Jakes. Alipoulizwa mwaka jana, unazungumziaje swala la U.S.A kubariki kisheria, Mapenzi ya watu wa jinsi moja👩‍❤️‍💋‍👩 👨‍❤️‍💋‍👨  👬 👭 *(Homosexuals-Gays/Lesbians)?.*
Hayo ni maswali kama yale ya kifarisayo, yanalenga kumchonganisha huyu mtumishi na serikali. Alitoa jibu moja tu, *_"LET THE WORLD BE WORLD, AND LET THE CHURCH BE THE CHURCH"_.* Hapo amekata mzizi wa fitna. Dunia imechagua hayo, tuiache na tufanye yetu kuuhubiri utakatifu wenye viwango katikati ya hii dunia chafu.
NI MUHIMU KUTAMBUA HILI, DUNIA KABLA HAIJAFANYA MAAMUZI, ISIMAME KWENYE UTAKATIFU AU KWENYE DHAMBI, TAYARI NI YENYE DHAMBI. YAANI NEUTRAL POINT YAKE TAYARI NI DHAMBI, NDIO MAANA NI LAZIMA UEPUKE KUIFUATISHA DUNIA.
WANA WA ISRAEL WALIPELEKWA KWENYE NCHI AMBAYO IMEJAA UCHAFU WA DHAMBI, HALAFU WANAPOKEA MAAGIZO YA KWENDA KWA UKAMILIFU MBELE ZA MUNGU. HAPO NDIPO NILIPOPEWA UJUMBE HUU, KUWA  UCHAFU WA DUNIA, HAUTUZUII SISI KUWA WATAKATIFU!

Ezra 9 : 11
*_Nchi ile, mnayoiendea ili kuimiliki, ni nchi ya uchafu, kwa sababu ya uchafu wa watu wa nchi zile, kwa ajili ya machukizo yao, yaliyoijaza tangu upande huu mpaka upande huu, kwa uchafu wao._*
👆🏼MSTARI UNAOFUATA, WANAPEWA INSTRUCTIONS, ZA KUISHI KWA UTAKATIFU KATIKATI YA UCHAFU.

MUNGU ANATUTAKA TUWE WATAKATIFU KABISA KABISA, _INSPITE OF_ MACHAFU YOTE YA DUNIA (1PET 1:14-16)

ILIPOFIKIA WAKATI NCHI NCHI NZIMA INA PRACTICE IDOLATRY(IBADA YA SANAMU), MUNGU ALIWATAZAMIA WANAOMPENDA WABAKI SALAMA. NA KWELI KULISALIA WATU ELFU SABA, AMBAO WALISEMA, NO!
1 Wafalme 19 : 18 *_Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu._*
HAIJALISHI NANI KAAGIZA, AKINA  SHEDRAKA, MESHAKI NA ABEDNEGO NA DANIEL HAWAKUIOGOPA AMRI YA MFALME (EBRANIA 11:23).

LUTU ALIISHI SODOMA, TAFSIRI YA JINA HILI NI _*Sodomy*_ yaani Ulawiti. Hukundiko kulijaa yale machafu niliyoyaeleza katika lile somo la *_Wamebuni mavumbuzi mengi (JITAHIDI ULIPATE)_*, Nadhani hata wale mabinti wawili wa Lutu, walijifunzia huko INCEST, mpaka wakajua kuwa huyu baba tukimnyeshwa hii Gongo sijui Safari Lager🍻🍺, akisha kuwa full tungi, tutamfanya atuingilie kimwili bila kujitambua, hilo wazo lisingewajia kwa wepesi wasingeshuhudia hizo vitu kule Sodoma.

UWEPO WA KUMBI NYINGI ZA STAREHE HAPA DAR, HAZINA EFFECT YOYOTE ILE KWETU, KUNAPOBUNIWA SURUALI ZA MTOBOKO ZINAZOONESHA MAPAJA YOTE HAZINA ATHARI YOYOTE KWETU,  KUKIZINDULIWA AINA NYINGINE ZA BIA KWENYE KIWANDA CHA TBL HAKUNA ATHARI YOYOTE KWETU.
TENA HAYA MABAYA YANAPOZIDI SANA, YANAFANYA NEEMA INAKUWA NYINGI ZAIDI, NA AMBAO TUMEYAKANA MAISHA YETU KWA KUJITENGA NA DUNIA, TUNAONGEZEKA MNG'AO WETU, INGAWA HIYO SABABU YA SISI KUCHUKULIA POA WOKOVU.  TUSOME HAPA KWA UTULIVU

_*1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?*_
_*2 Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?*_
*_3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?_*
_*4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.*_

RUMI 6:1-4 👆🏼
SISI KWA HABARI YA DHAMBI TULIKUFA, HATUPASWI KUITUMIKIA TENA (Rumi 6:11-12). SASA KUNA KIFA-UONGO (KUFA KWA UONGO). KUNA WADUDU FULANI 🐜🐜 WAKO KAMA SIAFU WAKUBWA, WANIWEZA HII TABIA YA KUFA KWA UONGO (KIFA-UONGO). UKITEMBEA UKAMKANYAGA ANAJIZIMISHA KAMA AMEKUFA, SASA UKISOGEA MBELE, UKAMTAZAMA, AKIONA KIMYA ANASIMAMA NA KWENDA ZAKE, UKIWAONA FANYA JARIBIO MKANYAGE KWA KIWANGO KISICHO CHA KUMUUA, ILA YEYE ATAFANYA IGIZO LA KUJIUA, ILI USIMSHAMBULIE ZAIDI. SASA WAPENZI WOKOVU NI HALISI, USIFANYE KIFA-UONGO, HUTAWEZA KUSHINDA YAKIINUKA MAZINGIRA MAGUMU YA DHAMBI. MUNGU ANATUTAKA TUKIISHA OKOKA, TUTUMIKE KATIKA UPYA WA UZIMA. NIWEKE SAWA HAPA; HAINA MAANA BAADA YA KUOKOKA NA KUJAZWA ROHO HUTASIKIA KABISA HATA HISIA KIDOGO, KWA MFANO YA TENDO LA NGONO, HAPANA!! LABDA KAMA UNA BIOLOGICAL DISFUNCTIONS. TOFAUTI YETU NI HII, KWA KUWA HATUNA NIA YA KUTENDA DHAMBI, WE DON'T ALLOW OUR MIND TO DWELL/SETTLE KATIKA MAWAZO YA DHAMBI. LINAWEZA KUJA WAZO LA ZINAA UNALIWAHI KWA HARAKA 👐🏽(AWAY WITH YOU-TOKA ZAKO). SIO NAWE UNAYA-INTERTAIN MAWAZO HAYO, MAANA KUZIWAZA DHAMBI NAYO NI DHAMBI. NA MBAYA ZAIDI NI PALE UMEONA KWA MACHO, UNAAMUA KUUELEKEZA MOYO WAKO PIA UAMBATANE NA MACHO;

Ayubu 31 : 7  *_Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, Na moyo wangu kuyaandama macho yangu............_*

UMEONA 👁KWA BAHATI MBAYA, LIISHIE HAPO, UKILIPELEKA MOYONI ❤ KUANZA KULI-PROCESS, MWISHO WAKE MOYO UTAZALISHA TAMAA AMBAYO INAKAMILISHWA  KWA KUTENDA.

TENA DHAMBI, ZINATABIA HII; UKIZICHUKIA (Mithali 8:13), MAZINGIRA YANAYOKUTAKA KUTENDA DHAMBI YANAPUNGUA, MAANA MKONO WA MUNGU NAO UTAKUEPUSHA NA HAYO MAJARIBU. HAPA NI MAJARIBU KWA MAANA YA TEMPTATIONS (HAYA NI KAMA HAYO YA KUTAMANISHWA NGONO NA KABINTI) NDIO MAANA AKASEMA OMBENI MSIINGIE MAJARIBUNI, USITUTIE MAJARIBUNI NI TEMPTATION, SIO YALE MAJARIBU AMBAYO NI TESTS/TRIALS, YALE NI VIPIMO AU MITIHANI YA KIIMANI AMBAYO LAZIMA UIPITIE TU ILI KUKUONGEZEA MISULI 💪🏾💪🏾🏋🏾YA KIROHO, YALE HATUOMBI KUYAINGIA WALA KUOMBA TUEPUSHWE, USIPOKUWA TUNAAMBIWA FURAHINI MKIANGUKIA KATIKA MAJARIBU HAYO.

SASA WEWE ULIYEOKOKA USIWE MPUUZI KAMWE. ETI MDADA UMEOKOKA, ILA UNAAMUA KUMFURAHISHA RAFIKI YAKO (HOSTEL ROOM-MATE), ETI KAKUOMBA UMSINDIKIZE NIGHT CLUB, NAWE UNALINDA UJIRANI MWEMA KWA KWENDA DISCO, ETI UNASEMA ILA MIMI SITACHEZA, NTAKAA NYUMA NAKUNYWA SODA 🤔, UMEMFANYA SHETANI NI TEENAGER FULANI HIVI MPWA WAKO. HUYU ANAYEITWA SHETANI, SIO WA KUMCHUKILIA POA NA KUMPA NAFASI (EFES 4:27), INFACT ALIKUWEPO MIAKA MINGI SANA MBINGUNI, WALA ANGUKO LAKE HALIKUWA KITU KIDOGO, NI WACHACHE SANA WANAOJUA SWALA LA *FALL OF LUCIFER* WHICH PRECEED PRE-ADAMITE ERA. WALA HATA ILE UFUNUO 12, LILE SIO LILE ANGUKO LA LUCIFER. HAYO YAPO KATIKA SOMO LANGU TOFAUTI. SASA UKIMPA KIDOLE SHETANI👉🏾, ANANG'ATA MKONO MZIMA. KABISA MLOKOLE WEWE UNAMSINDIKIZA MWENZIO NIGHT CLUB, UKIAMINI UTABAKI SALAMA😨, DHAMBI INAMVUTO BABA, MUULIZE DEMA MTUMISHI MWENZA WA PAULO, AMEZUNGUKA NA MTUME PAULO WEE KUFANYA GOSPEL OUTREACHES, ILA AKACHUNGULIA KIDOGO TU VYA DUNIANI, AKAUPENDA ULIMWENGU, AKAMWAMBIA PAULO AISEE MKUU, WE NENDA TU (2TIMOTHEO 4:9).
Eti binti una rafiki wa kiume hajaokoka, ila unataka asikuone mwanadini saaana, kwa hiyo unamtia moyo kwa kuonja kidogo Vodka, sijui Pilsner ice🍾🍷, Huo ndio ujinga sasa. Tena kwa kuwa hukuzoeleaga vilevi, kaglass kamoja tuu hoi😞,mpaka anakupeleka room anamaliza kabisa. Hakuna wa kumlaumu. Hizi sio zama ujinga (Mdo 17:30), Mimi siwezi kubali kizembezembe tu kuyaharibu mazuri ambayo Mungu ametukirimia kwa wokovu huu. Kama kwa maadili yale ya kufunzwa na wazazi nilijitunza bila kufanya uasherati, siuze baada ya kupokea uweza wa kimungu wa kushinda??? Wakati ambapo  dunia yote italazimisha, dhambi zionekane ni kawaida, lazima tusimame watu tutakaosema No!👐🏽 Tendo la Ndoa kabla ya ndoa (eti kisa ni wachumba), hapana; uongo, hapana; Kuibia kampuni, hapana; secular music, hapana; pornography, hapana;   mavaza ya nusu uchi, hapana; kutoa mimba, hapana; kuattend night club, hapana; kwenda kwenye beach ambazo watu wako almost nude 👙, hapana.
Epuka injili yoyote, inayoonesha kuwa kwenye hukumu ya Mungu, eti huyu kiongozi wako wa kiroho atakutetea mbele za Mungu, hiyo nafasi haitakuwepo. Na hicho ni kiashiria cha wazi kuwa unajiandaa kuachwa wakati unyakuo. Maana watakaonyakuliwa hawahitaji kwenda kutetewa, na kama atakutetea  wakati wa ile hukumu ya mwisho (ya Ufunuo 20), well and good jiandae kuachwa and enjoy dhiki kuu to the full.
*Hakuna mwanadamu atakayesimama kumsaidia Mungu, namna ya kuamua saa ya hukumu, naye atakuwa kikaangoni*
*Kama aliuhukumia uovu wa Musa, adhabu ya kutoiona Kaanani, ni mfano wa wazi kuwa tunao viongozi sasa, ambao wao wenyewe watakataliwa, kama hawajaishika haki ya Mungu (1Kor 9:27)*

SASA MSHIKE YESU, DUNIA IKIWA CHAFU SANA KWA HARUFU YA DHAMBI, SISI TUBAKI WASAFI SANA, TUKITOA HARUFU YA MANUKATO MBELE ZAKE MUNGU.

Mbarikiwe, mnapoendelea kutyuni frequencies za kiroho.

Mwl Proo
(Prosper Kadewele)
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

2 comments: