Tuesday, November 28, 2017

FUNGU POSHO LANGU, NA SEHEMU YANGU MIELE

*FUNGU LA POSHO LANGU, NA SEHEMU YANGU MILELE!.*

*_Mwl Proo_*
*_0762879363 (WhatsApp)_*

Nawasalimu kwa jina la Yesu (Kristo)!. ✋๐Ÿพ

Kuna watu hawaishi kwa furaha kamili, maana wameruhusu tafsiri za ulimwengu, zisizo sahihi kuwa kiongozi chao. Utakuta mdada ni mnene kwa asili (bonge), kwa sababu ya wadada wachache wembamba (slimy) wanaom-pinpoint๐Ÿ‘‰๐Ÿพ, anakuwa hana amani na alivyo๐Ÿ˜€. Lakini ni hao hao wanaocheka ubonge, ndio wakioolewa wakapata na watoto wanakuwa mabonge zaidi, ila wanajiwekea tafsiri tofauti, kwamba uchumi na maisha yako ๐Ÿ‘๐Ÿฝ. Nakumbuka Lekchara wetu mmoja chuoni, alituambia ukiona mtu kapata kazi au kaolewa tu, then akafutuka (kanenepa ghafula), ni athari ya upande mwingine (side-effect), *kwamba hakuzoea maisha mazuri kabla*๐Ÿ‘Œ๐Ÿฝ. Wengine walizaliwa kwao ni weusi kwa asili ๐Ÿ‘‰๐Ÿพ๐ŸŒš๐Ÿ‘ง๐Ÿฟ, dad and mom wote๐Ÿ‘‰๐Ÿพ๐Ÿ‘ด๐Ÿฟ๐Ÿ‘ต๐Ÿฟ, sasa unatakaje uwe ๐Ÿ‘ง๐Ÿป, wachache wasiolewa wamejichubua kulazimisha tafsiri potofu ya ulimwengu ifiti maishani mwao๐Ÿ˜€. Wengine tumezaliwa na kimo cha kati tu kuelekea ufupi, na wengine super-talls kwa dunia ya sasa ambayo infact hakuna warefu, Goliath alikuwa na futi 9, lakini akina na Adamu na watu wa zama zao walikuwa na futi 12 kama boriti ile ndefu. Sasa wengine kwa kujikuta wako wafupi, wameji-look down na kujishushia thamani, wanabidii hao ya high heels๐Ÿ‘ ๐Ÿ‘ , ili kulazimisha tafsiri ya dunia ifiti maisha yao. Kabla ya kuweka sawa hoja yangu, nataka kuwatolea uvivu wakristo wa mwilini (carnal Christians) ambao hawajabadilishwa (of unregenerate nature), wasio na Roho wanafuata utashi wao (mere natural instincts), hawa ndio wanataabisha wenzao wajisikieje sijui. We unayesoma ujumbe huu mtu asikutaabishe (Gal 6:17), Ni kweli uko mweusi, haijatosha wao wakupende, ila weusi wako unalitosha kusudi la Mungu alilokuumbia, so ukijiangalia kwa kioo, jitamkie maandiko yanayo kuhusu, kwamba mimi ni mweusi-mweusi ๐Ÿ‘ง๐Ÿฟ lakini ninao uzuri (Wimbo 1:5), Tena kuna mwanaume fulani wa  nguvu, atakapokuona na rangi yako, moyo wake utavibrate๐Ÿ’— (Akisema, *_"My favourite colour๐Ÿ˜"_*), Wewe ambaye unachekwa na ubonge usijitaabishe na diet ya kujiua, tunafikiri unafunga kumbe unataka kuwa slim, huna haja, kama unadhani wote wwnatafuta slim/english figure pole, wa kwako huko aliko anaomba miss bantu fulani hivi mnene, nawe mwenye Zacchaeutic height (Urefu wa Zakayo) ulivyo unatosha kwa kusudi la Mungu, sio macho yote ya wanadamu. Kuna mtu alikuwa akikaa na mimi anaropokaropoka sijui mnaita Six-packs, aku๐Ÿ˜•, waniatazamia nianze Gym๐Ÿ‹๐Ÿพ kusaka hizo? Nani kasema mke wangu ajaye atakuwa anazipenda? Kwani mimi ni mali ya wanawake wote wa barabarani? Halafu nitazioneshea wapi kwa mfano?๐Ÿค” Maana Roho wa Mungu ananishuhudia wazi ndani yangu, kwamba maisha yangu nitayamalizia madhabahuni tuu, So unanitajia Six-packs nije kuwaonesha wa shirika, mavazi yangu yenyewe suti kwa sana, ondoa hizo habari!!!.

Ayubu amewasikiliza akina Sofari na Elifazi, akaona wanamsuta juu ya udhaifu, akawaondolea uvivu;

Ayubu 12 : 3
*_Lakini mimi pia, nina fahamu kama ninyi; Mimi si duni yenu ninyi; Naam, ni nani asiyejua mambo kama hayo?_*

AKAWAAMBIA MIMI SI DUNI YENU (I'M NOT INFERIOR TO YOU), YAANI NINYI MNA NINI CHA KUNIZIDI? HAO WANOLETA VIJIMANENO VYA KUKUSUTA, THEY HAVE THEIR DARKEST SIDE WAKO WCHOVU SANA, MAANA MAMBO YOTE YAMEJAA UCHOVU USIONENEKA (MHU 1:8), NA MUNGU NI KAMA ALI-BALANCE AISEE, ANAYESUMBUA WATU NA RANGI YAKE NYEUPE๐Ÿ‘ฉ๐Ÿป, ANAO UDUNI MAHALI PENGINE HATARI, ANAYESUMBUA WATU NA DIGRII ZAKE, ๐ŸŽ“๐ŸŽ“๐ŸŽ“ ANAYO MAUCHOVU ELSEWHERE NI SHIDA.

*MOYO WA SOMO*
Zaburi 16 : 5
*_Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unaishika kura yangu._*

Zaburi 73 : 26
*_Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele._*

Daudi baada ya tafakari kubwa juu ya maisha, akagundua kuwa Mungu ndiye fungu la posho lake, anayeishika kura yake (He maintains his lot). Na Asafu baada ya kujaribu kufanya mambo kwa nguvu zake ndipo akajua kuwa vyote vitashindwa lakini Mungu ndiye sehemu yake (portion forever) milele.

KUNA KITU UNACHOKIHITAJI, NACHO UKIWA NACHO HAKUNA UDUNI WOWOTE MAISHANI MWAKO, HAUNA CHOCHOTE CHA KUPENDEZA ZAID YA HICHO, IWE MBINGUNI WALA DUNIANI, UNAJUA NI NINI? (SOMA ZABURI 73:25). THERE IS NO INFIRMITY, NO FRAILTY THE LORD CANNOT FILL, KILE UNACHODHANIA NI UDUNI (INFERIORITY) AU UDHAIFU, NDICHO KINACHOLETA TASTE KWA MUNGU NA NGUVU ZAKE.

2 Wakorintho 12 : 9 *_Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu._*

KWA HIYO HIVI NILIVYO NDIVYO LADHA YA KIMUNGU INADHIHIRISHWA, USIPOTEZE MUDA KUJILINGANISHA NA WADADA UNAOWATAZAMA KWENYE TAMTHILIA ZA KIFILIPINO, WALE UNAOWAONA WALIPITISHWA KWENYE MCHUJO WENGI MNO, KUWAPATA HAO ACTRESSES. SASA NAWE UNAHANGAIKA WEEE. MUNGU ANAKUTAMANIA UWE HIVYO, NA ANAJUA JINSI YA KUTUMIA UDUNI WAKO (AMBAO SIO UDUNI INFACT, ILA DUNIA IMEAMUA KUTAFSIRI HIVYO) ILI AJITUKUZE. SIKU MOJA NIMEENDA KUHUDUMU KANISA FULANI, WALE WALIOJIANDAA KUNIPOKEA, WALIJUA WATAPOKEA JAMAA LA MIRABA MINNE MWENYE KITAMBI, BAADHI YA WAZEE WA KANISA WAKAVUNJIKA MOYO, KUONA MHUBIRI MWENYEWE๐Ÿ™†๐Ÿฝ๐Ÿ™†๐Ÿฝ๐Ÿ˜ž๐Ÿ˜ž. NIKAWATAZAMA NIKAWAJUA MIOYO YAO, NIKAWALIA POZI TUU๐Ÿ˜Ž. NILIPOPANDA MADHABAHUNI, AKILI ZAO ZIKAPOTEANA, NA WENGINE WAKAGUNDUA HATA ROBO YA UFAHAMU WANGU, HAWAJAUFIKIA, WALIANZA KUWARINGISHIA WACHUNGAJI JIRANI, HUYU NI MUHUBIRO WETU, MPAKA LEO WANATUMA MESEJI ZA KUULIZA MASWALI YA KIROHO NA KIBIBLIA, KWA NINI?

1 Wakorintho 1 : 27 *_bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;_*

๐Ÿ‘†๐Ÿผ๐Ÿ‘†๐ŸผUmeiona shughuli hiyo? Kwa hiyo hapa nilipo simtetemekei mtu kwa chochote, akiona kama nina uduni fulani, ajue pia ninayo mambo ambayo Mungu, pamoja na huo uduni, kanijaza mambo ambayo hata afanye hawezi kuwa nayo, nikikaa na mtu mwenye PhD, simtetemekei hata. Mtu mwenye anamiliki Hammer๐Ÿš˜ akiwq nami tutaenda sawa tu, mambo ya kumfanya anione inferior wakati mimi najua kuwa nafsini mwangu, ni mali zilizo njema zaidi (Ebra 10:34), wote tunapaswa kujua kuwa, hatutoshi sisi wenyewe,utoshelevu wetu, watoka kwa Mungu...

2 Wakorintho 3 : 5
*_Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu._*

NI KWELI UKIENDA KUOMBA KAZI, UWE MNYENYEKEVU. LAKINI WEWE BINTI UKIONA HRM AU BOSI WA KAMPUNI, ANAOMBA AKUONJE MWILI WAKO, ILI AKUSAINISHE MKATABA WA KAZI, MWAMBIE *_"AWAY WITH YOU JOB!"_* USIRUHUSU HUO UPUUZI, WALA USISEME SI NI SHOTI MOJA TUU, NOOOOOO!!!๐Ÿ‘๐Ÿฝ HIYO HIYO SHOTI MOJA๐Ÿ’ UTAKAYO MPA MWILI WAKO, ITATENGUA RATIBA ZA KIMUNGU NYINGINE, ULITEGENEA NDOA YA HESHIMA, SASA USIPOJUA KUWA UNAYE MUNGU ALIYE FUNGU LA POSHO LAKO NA BWANA ALIYE SEHWMU YAKO MILELE (UTAKUTA HIZO NDOTO ZOTE ZINAVANISH, KWA CHAKULA KIMOJA TUU KAMA ESAU). SISI TUNAYE MUNGU MTOSHELEVU WETU, UEHAIFU NA UDUNI WETU NI MTAJI WETU. AMBAVYO SINA LEO, NI SWALA MUDA TU. HIS DELAY IS NOT A DENIAL (HAJANINYIMA MUNGU, ANAKIANDAA KWA MUDA WA KUFAA ANALILETA)

*_~KAKA YANGU NA DADA YANGU, WEWE SIO DUNI WA CHOCHOTE, KWA KUWA UNAYE MUNGU, YEYE NI FUNGU LA POSHO LAKO NA SEHEMU YAKO MILELE, WAACHE WANAOFANYA SHOPPING NAKUMAT NA MLIMANI CITY, WEWE ENDELEA KWENDA KARIAKOO, KARUME NA MANZESE, ULICHO NACHO NDANI YAKO NI ZAIDI YA MLIMANI CITY, LAKINI NAKUMAT/MLIMANI CITY MALL , HUKO NAKO BWANA ATAKUPELEKA KWA HAKI, SIO KAMA HAO WANAOKULA PESA ZA WAUME WA WATU, WAKIJILETEA UVUNJIFU USIO KAWIA_*

~Kama umemaliza kusoma, jifungia chumbani, chukua tenzi za rohoni, imba ule wimbo wa Bwana  U sehemu yangu. Kisha omba dakika tano, neema ya mguso wa  Mungu, itakugusa mara, na kuna mahali Bwana atakuvusha wikiendi hii. Nawe utanishuhudia~

Mwalimu Proo nimemaliza tayari, alichonijaza moyoni kwa leo kimetoka.

0762879363 (All Truth whatsapp group)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment