*NAWAAMSHA KWA KUWAKUMBUSHA*
*_By Mwl Proo_*
0762879363
Haleluya kwa Bwana!
NILIPOSHIKA BIBLIA TU KABLA SIJAFUNUA POPOTE NDANI YA NAFSI NIKASIKIA SAUTI IKISEMA *_NAWAAMSHA KWA KUWAKUMBUSHA_* NDIPO NIKAKUMBUKA MAANDIKO YENYE USEMI HUO.
Tuanze kusoma;
2 Petro 1 : 13
*Nami naona ni haki, maadamu nipo mimi katika maskani hii, kuwaamsha kwa kuwakumbusha.*
2 Petro 3 : 1 _*Wapenzi, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika zote mbili naziamsha nia zenu safi kwa kuwakumbusha,*_
Huu ni ujumbe kwa ajiri ya wasafiri(1Petro 2:11),Wasafiri hawawezi kuwa watu wa kujisahau,hauwezi kusafiri kwa basi 🚌 then ukajisahau kwa mambo ya njiani. Eti mmeshushwa hotelini kwa ajili ya chakula basi ukaanza kufanya as if umefika,ukakuta watu wanafuatilia mechi kwa tv📺nawe msafiri ukanogewa na kusahau safari,huwezi kaa kwa wachoma mahindi🔥🌽🌽na kusahau safari. Sasa Leo Bwana amenipa _*kuwaamsha kwa kuwakumbusha*_ maana kuna wasafiri wa kwenda mbinguni humu,wamepumbazwa na mambo yatokanayo(arising matters) njiani ,
✝Yaani safari yetu ya mbinguni haichangiwi na chochote kwa kuwa na ndoa au kutokuwa nayo lakini kuna watu ambao wamekomaa na hiyo ishu as if yaani hiyo ni kila kitu,Bwana ameniagiza kukuamsha kwa kukumbusha kuwa kuoa na kuolewa ni kitu tu cha duniani (Mathayo 22:30) Bwana akupe ndoa au asikupe isikubailishie uelekeo wa safari kamwe, Nisemalo ni hili,wakati ubakio sio mwingi kiasi cha wewe kupoteza energy kubwa kiasi hicho(1Kor 7:29) Amini kuwa Mungu anaweza kukubarikia ndoa njema lakini hata pasipo hiyo,bado yeye ni Mungu nawe ni msafiri usiyetakiwa kupumbazwa na mambo ya njiani. *(Na ambao mpo ktk ndoa,pamoja na kusaidizana kutimiza makusudi ya Mungu,fanyeni hima mhimizane kuwa msiikose mbingu,kama ndoa yako haina mchango wowote kukusaidia kukamilisha safari zaidi sana it pulls you back/down hiyo ni hasara.)* Hivi karibuni nimeshangaa kusikia habari za dada ambaye hata mimi nilifanya naye huduma miaka ya 2009 akiwa UDSM ila kwa sasa ameolewa kwa ndoa ya kiislamu,nilikuwa naona picha zake fb amevaa baibui sikujua huo mtoko,kumbe amempiga Yesu kibuti👢kapata bwana wa kiislamu👳🏾,amesahau Gospel outreaches zote alizoenda kufanya Zanzibar,Tanga etc akawahubiri waislamu wengi alihitaji kuamshwa kwa kukumbushwa bahati mbaya adui aliwahi kumnasa
✝Kuna watu ambao mlikuwa wanyenyekevu kwa Bwana,mkainuliwa kuwa watu mashuhuri. Na sasa everything about God bothers you. Si ndivyo? Bwana anasema nikuamsha kwa kukukumbusha,Kuwa watu wote wakubwa(Great people) duniani na wenye sifa *WALIKUFA* na wameona kuwa umashuhuri wao hauna fungu wala sehemu ktk uzima ule. Mkumbuke Mao Tsetoum pamoja na kuabudiwa kama Mungu lakini amekufa. Jitihada za kuuhifadhi mwili wake kwa madawa hazifui dafu maana wamebaki na maudongo yale ile yeye halisi yupo huko anavuna kiburi alichopanda. Bila shaka mnamjua Gadaffi pamoja na umashuhuri wa kuwa ikulu miaka 42 haimfanyi aendelee kuheshiniwa ktk ule ulimwengu wa zama zijazo. Na yule binti wa Sierra Leon ameeleza ktk ushuhuda wake alioutoa mbele ya raisi na wananchi maelfu kuwa ktk ambao aliwaona kuzimu na huyo jamaa alimuona(tafuta ushuhuda huo,swala la validity yake halizuii sisi kujifunza) kwa hiyo naiamsha nia yako isitumainie kabisa umaushuhuri wala utajiri wako usio yakini (1Timothy 6:17)
✝Kuna watu ambao kwa kweli life imekamata,mambo yamekuwa magumu mno,mpaka mnawaza kuchakachua na kuiacha njia ya BWANA,kwanza ni muhimu mfahamu Bwana anawawazia mema(Yer 29:11) Lakini usalama wako upo ktk kukaa kwa Yesu, Kitakachofanywa ukumbukwe ktk maisha ya sasa na yale ya badae sio kwa kuwa umeishi kwa dhiki sana huwezi kupata chai maana Kuishi kwa umaskini mkubwa na dhiki haitoi nafasi ya kuonewa huruma ktk zama zijazo kama hukuendelea kushikamana na ukamilifu wako (Ayubu 2:9),Pona yako ipo ktk kuendelea kubaki ktk wema wa Mungu/wokovu (Rumi 11:22)
NB:-
Wanadamu wa Agano Jipya lazima niwaoumbushe kwa kuwaamsha kuwa ktk zama za post-calvary covenant UJANJA WA MWISHO KABISA ni kuwa na Yesu kama kufa ufe ktk Bwana,maana hata waliouawa kikatili kama kuchomwa moto🔥,kuchunwa ngozi,kufa baada ya kubakwa na kundi la vijana,uliliwa na wanyama wakali,mlikuwa yatima mkafa kwa njaa na kulemewa na maisha,mlisombwa na mafuriko🌊 kifo kikawakuta *_HAKUTOI NAFASI YA MBINGU KUKUFIKIRIA KTK UZIMA ULE_*
Wewe ambae ilibaki kidogo tu uchoke na kukata tamaa Bwana ameniagiza,nikuamshe kwa kukumbusha kuwa *USIACHE* Ziko nyakati za burudiko zinakuja (Mdo 3:19) utaburidishwa nafsi yako sana,zile mbingu alizokuahidi Bwana Zitajaa raha zote zilizonenwa na manabii na mitume kwa hiyo usichoke maana pia ktk Ziwa la moto nako kutakuwa na matesho yote kama yalivyonenwa ktk maandiko.
✝Wale mnaomiliki mali nyingi mpo????📢Bwana kaniagiza niwaamshe kwa kuwakumbusha kuwa *_MALI ZENU HAZINA SEHEMU KTK UZIMA WA ZAMA ZIJAZO ZINAZOFANYA HARAKA KUTUJILIA (MHUBIRI 5:13-15).Ili usiwe miongoni mwa ambao mali zitawakosesha mbingu ,Fanya hili; mali ikizidi kuwa nyingi uitazame kwa macho tuu👁👁 usiitazame kwa moyo (Zaburi 62:10) yaani usiuruhusu moyo kuambatana na macho(Ayubu 31:7) kisha utakuwa salama.
✝Kuna watu wana kiburi cha uzima(1Yoh 2:16),Yaani kwa kuwa wako na afya tele sasa hawataki uwape diaturbance na mambo ya Mungu,na mwingine akiona ana miaka 25 anawaza aponde maisha maana anawaza kile kifo kitakacho nkuta na miaka 70 anaona kipo mbali sana nado ana salio la miaka 45 ya kula sembe na ngano ya Bakhressa,wewe wewe!👌🏽Muda wa maisha baada ya hii miaka 70/80 (Zabur 90:10) ni mwingi mno hauna mwisho wake,Mungu amekupa miaka hii michache ili uitumie kuandaa yale ya umilele. Kifo ni halisi pamoja na jitihada za kujisahaulisha,Takwimu zinaonesha kila siku moja watu 150,000 ambao ni watu 108 hufariki dunia(wanafarakana na hii sayari dunia) that is from all causes of death. Sasa watu jinsi mnavyoitia nia zenu kwa mambo ya muda ni hatari, kumbuka kuwa vinavyoonekana ni vya muda tuu (2Kor 4:8) SIWATISHII BALI NAWAAMSHA NIA ZENU KWA KUWAKUMBUSHA,haina maana uachw shughuli zako maana mimi ninayeandika haya ni mtumishi wa serikali ya *HAPA KAZI TU* Lakini nikiwa ofisini nayajenga maisha yangu ya umilele na popote pale niwapo siachi nikalala usingizi kama wengine(1Thes 5:6)
*KWA KUWA NYAKATI HIZI NI ZA HATARI NAAM ZAMA ZA UOVU,BASI HAYA HAPA CHINI NI MAMBO YA MUHIMU KTK KUZIAMSHA NIA ZENU ILI MSIJE MKAWA WA KUKATALIWA*
✝Hakikisha umeokoka kwelikweli,usienende sawa dunia *_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_*
Rumi 12:2
✝Usitende dhambi kwa makusudi. *_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_*
Hebrews 10:25,6:4-6
✝Omba Mungu akupe moyo wa toba,sio kujikaza na dhambi. *_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_*
Rumi 2:5
✝Azimia kumtumikia Mungu wewe na nyumba yako. *_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_*
Yoshua 24:15
Hagai 1:4
Yohana 9:4
✝Jinyenyekeze kwa Mungu daima hata kama,utajikuta upo kwenye cheo kikubwa kama Raisi,Waziri au Managing Director wa kampuni. *_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_*
Kumbu 8:12-17,32:15
✝Kila ulichonacho,kitumie kwa utumishi(Utukufu wa Mungu).una degrees zako 🎓🎓🎓,afya njema,pesa zako. *_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_* (Mithali 3:9)
✝Daima epuka kiburi ambacho ni matunda ya kusahau ulipotoka. *_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_*
1Yoh 2:16,1Petro 5:5,Isaya 2:17
✝Kila unapisikia kuchoka,tafuta nguvu kwa BWANA.
*_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_*
Zaburi 105:4
✝Tafuta kulijua kusudi/shauri la Mungu ktk maisha yako uliishi hilo,everybody is unique in God's sight. *_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_*
Mdo 13:36
✝Kamwe usirejee nyuma. *_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_*
Hebrews 10:39,Ezekiel 8:17
Kurudi nyuma kunasababishwa na ➖kuchoka
➖kuipenda dunia(2Tim 4:10)
✝Tengeneza mambo ya nyumba yako daima. Usikae na _suspended cases/issues_ ambazo hujazi-settle kiroho na kijamii.
*_(nakuamsha kwa kukukumbusha)_*
Isaya 38:1-2
*Amen and Amen... kazi ya kuwaamsha kwa kuwakumbusha imekamilika.*
Mwl Proo (Prosper Kadewele)
Karibu ktk familia yetu ya ALL TRUTH whatsapp group tuma neno add me kwenda 0762879363(whatsapp only)
au barua pepe
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment