*MKOGO*
_Na Mwl Proo_
0762879363
Bwana Yesu asifiwe!.
Wapenzi katika Bwana, mtu aliyewekwa huru, akikosa maarifa, ataonewa tena kama mfungwa na adui. Sasa soma hapa ili ule uhuru (Yoh 8:36) ulioupata uwe thabiti.
Bila shaka umeshuhudia mtu aliyeokoka tayari, akawa tena na viasharia vya vifungo na kuonewa. Sio kwamba ukombozi wa Yesu haufui dafu kwa kazi za Shetani, la hasha!! Lakini kuyakosa maarifa fulani sahihi, kutafanya uminywe na adui ingawa upo huku. Kwa nini? Shetani ni adui makini, hajawahi kukata tamaa pamoja na kichapo alichopokea tangu mwanzo wa anguko lake (Fall Of Lucifer). Amekuwa akifanya vita daima, na ndio maana hata baada ya wakati ule wa utawala wake kupitia Mpinga Kristo(pamoja na serikali za dunia zitakazo mpa mkono wa shirika), kushindwa katika vita ya Har-magedoni, hatakata tamaa kabisa kabisa. Bado atajipanga upya tena, na atafanya tena vita na kambi ya watakatifu, katika ile vita ya *Gogu na Magogu* (ambako atapokea kichapo cha lala salama). Sasa watakatifu wanapaswa kuijua kweli hii kuhusu adui.
Shetani alikuwa na haki ya kisheria, kutunyanyasa, (Dhambi ilimhalalishia hilo). Tulipozaliwa tayari asili ya kutenda dhambi (Sinful nature), ilikuwa ndani yetu. Ndio maana unaweza kukuta hata watoto wa miaka miwili wanaweza kuoneana wivu, wakachukizana kabisa, unaweza kumpa mmoja zawadi mwingine ukamnyima, utaona reaction ya nguvu ya dhambi. Sasa unaweza hoji walijifunza wapi dhambi?.
Na kwa sababu hiyo, Taurat ya Musa iliandika hukumu za dhambi (hati ya mashtaka), ambazo bado wanadamu hawawezi kuzishinda. Na katika ulimwengu wa roho, Shetani naye aliandika hati yake ya mashtaka (written code), yenye masharti (regulations), ili tusifurukute. Na hata kama Mungu angetaka kututetea ile hati, ingemhoji Mungu, kuwa wewe Mungu mwenye haki unaanzaje kuutetea uovu?
Wakolosai 2 : 14 *_akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;_*
ππΌππΌYESU KRISTO AKIWA KATIKA KILE KINYONGEO ✝ CHA WARUMI, ALIISHUGHULIKIA ILE HATI KWANZA, HAPA NI HATI KATIKA ULIMWENGU WA MWILI (HUKUMU YA DHAMBI YA TAURAT) NA WA ROHO (ILE AMBAYO SHETANI ALIKUWA ANAITUMIA KUJIHALALISHIA KUTUPA KIBANO).
Wakolosai 2 : 15 _*akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.*_
WATU WENGI WANAKIANGALIA KIFO CHA YESU KWA JINSI YA MWILI, HIVYO KINAWAHUZUNISHA. YESU ALIUMIA MWILI LAKINI KATIKA ROHO ALIKUWA NA MASHANGILIZO YA HATARI.
✝ALIIFUTA ILE HATA NA KUIGONGOMEA MSALABANI ππ©π¨
✝AKAZIVUA ENZI NA MAMLAKA (HAPA ALIFANYA DISARMING (DISARMAMENT)-MAANA KAMILI YA HILI NI HII. CHUKUA MFANO JESHI LA TANZANIA LINAPAMBANA NA JESHI LA UGANDA, KISHA TANZANIA IKALISHINDA LILE JESHI LA UGANDA, KWA KIASI CHA KUWANYANG'ANYA SILAHA ZAO ZOTE PIA π²πΎπ²πΎπ£π«π‘, HIYO NDIO MAANA INAYOELEZWA HAPA, *_THROUGH THAT CROSS JESUS DISARMED THE RULE (RULERS)/PRINCIPALITIES._*
✝KISHA AKAZIFANYA MKOGO KWA UJASIRI
*MOYO WA SOMO*
Yesu Kristo alizifanyia _*MKOGO*_ Zile hati za mashtaka, zile mamlaka za giza zilizotukandamiza, na ule UGONJWA MKUU yaani dhambi, ulipatiwa dawa rasmi.
Neno Mkogo (public spectacle/open demonstration/Shew) linaleta maana nzuri toka katika neno la Kijerumani *Schao*, maana yake ni GWARIDE LA MAONESHO, Yesu akafanya show kwa ulimwengu wa mwili na wa roho kwa wazi, kuwa kile kilichotoa haki ya adui kuwamiliki wanadamu kimepata suluhu. Mwili wake uliteseka kwa maumivu, lakini Biblia inasema Akizishangilia katika msalaba huo. Kumbe rohoni Yesu alikuwa ana πππ½, na mwishoni ule mwili wa nyama ukaungana na roho akasema *_IT IS FINISHED_* (Yohana 19:30).
SASA TANGU HAPO, SHETANI HANA SABABU YOYOTE YA KISHERIA YA KUKANDAMIZA, KUKUWEKEA MAGONJWA, WALA HAKUNA PEPO LENYE HALI YA KUKUTAWALA WALA KUKUINGIA. KINACHOFANYWA NA MAADUI ZETU KWA SASA, NI KUTUMIA TU UJANJA-UJANJA, WAKIGUNDUA HUNA MAARIFA, AU UMESIMAMA NJE YA MSTARI, BASI WANAFANYA TU KUVIZIA, KUIBIAIBIA. LAKINI KILA ANAYEIFAHAMU SIRI, YULE MWOVU HAMGUSI, MAANA AKIINUA KIDOLE TU KUKUGUSAππΎ, UKAMTAMBUA, NI SWALA TU LA KUHOJI, AKUπ€ UMEFUATA NINI HUKU SHETANI, KWENYE AFYA YANGU? UMEFUATA NINI KWENYE ELIMU YANGU? UMEFUATA NINI KWENYE NDOA YANGU? π‘π‘ FOR YOUR INFORMATION, HAKUNA PEPO/JINI LOLOTE LISILOITAMBUA KALIYOIFANYA YESU KWENYE KILE KINYONGEO ✝CHA ASKARI WA RUMI.
SASA LEO HII WEWE UNAO UWEZO WA KUMFURUMUSHA SHETANI πΉ NA MAPEPO YOTE, KILA KONA AMBAYO WATAJIBANZA, NI SWALA LA KUWAJULISHA KUWA UNAJUA KAZI YA MSALABANI, SO TUMIA LUGHA ZA MAMLAKA KUWAAMURU WAACHE KILA WANACHOJARIBU KUSHIKA, TENA UKIMNASA MAHALI SHETANI KAVAMIA JAMBO LAKO, MHOJI, *_"NANI KAKURUHUSUπ‘?"_*, THEN COMMAND HIM OUT!!!
Sasa tukikosa maarifa haya, tukitomaswa na adui ambaye alishakuwa *disarmed* (alinyanganywa silaha), tukaanza kulialia, tunaharibu kila kitu yaani ππ½. Na ndio maana ni muhimu ukiisha kuokoka kuacha dhambi kabisa, ili kuiheshimu ile kazi ya msalaba. Mtu aliyeokoka amepokea nguvu ya kuishinda dhambi kabisa, akifanya dhambi anakuwa ameamua tu mwenyewe, ila anayo nguvu ya kushinda dhambi yoyote (1Yoh 3:9, 5:4).
*MUNGU AWABARIKI MNAPOENDELEA UNAPOENDELEA KUJIZOEZA KUTEMBEA KATIKA MAMLAKA KAMILI, UKIMFANYIA ADUI MIKOGO, KUWA HANA KITU KWAKO. HAJABAKIWA NA SILAHA INAYOWEZA KUKUSHINDA, KAMA UTAKAA VIZURI NDANI YA YESU.*
Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment