Thursday, November 9, 2017

ROHO ZIDANGANYAZO

*_ROHO ZIDANGANYAZO_*

-----------------
Na Mwl.Proo
0762879363
©2012

SOMO LINA SEHEMU 7

1.)UTANGULIZI
2.)ROHO ZIDANGANYAZO NI NINI/NANI
3.)ZINATENDA KAZI KWA KUPITIA NANI
4.)UTATAMBUAJE KUWA MTUMISHI HUYU ANATUMIKA CHINI YA ROHO ZIDANGANYAZO?(VIASHIRIA)
5.)HATARI KUU
6.)JINSI YA KUSIMAMA UPANDE SALAMA
7.)HITIMISHO

1.)UTANGULIZI:
BWANA YESU ASIFIWE..TUFUATANE KTK MFULULIZO WA FUNDISHO HILI LITAKALOTUPA KUBAKI SALAMA DHIDI YA UKENGEUFU WOTE WA NYAKATI HIZI.

WENGI WAMEKUWA NA WAKATI MGUMU,WAKISHINDWA KUPATA SULUHU/KUPAMBANUA KUHUSU MAMBO KADHAA
JE! MTU ANAWEZA TUMIA JINA LA YESU AKIWA BADO ANATUMIA NGUVU ZA GIZA?; JINA LA YESU LIKITAJWA SI LINALETA MOTO NA MTAFARUKU KWA NGUVU ZA MWOVU,INAKUWAJE MTU ANATUMIA NGUVU ZA GIZA ILA AKIWA ANATAMKA YESU? JE! HAWA MITUME NA MANABII WA SASA WALIOIBUKA KWA WINGI WANATOKANA NA MUNGU?KUNA BAADHI YA WAPENDWA WAMEWAHI HADI KUINGIA KWENYE MAOMBI NA MFUNGO KAVU ILI BWANA AWAJULISHE JE! HAO NI WATUMISHI WAKE? NIKUPE UHAKIKA WA KWANZA..MAOMBI HAYO HUTAPATA JIBU,UTAJIBIWA LABDA KAMA UNEFIKA VIWANGO VYA JUU SANA KIROHO, AMBAPO BADO UKIJUA UTATAFUTA NAMNA TA KUPONYA SIO KUBOMOBOA, OTHERWISE  HAJAJIBU YESU NI ROHO TUU NYINGINE ISIYOTOKANA NA MUNGU..YALE MAOMBI YA KUMUULIZA MUNGU ETI JE! TB JOSHUA NI MTUMISHI WAKO?AU KAKOBE AU MTUME MWINGIRA AU BENNY HINN AU GWAJIMA ETC ETC MAOMBI YA KUPELEKA LIST YA MAJINA ILI AKUJULISHE HUYU WANGU, HUYU SI WANGU NI MAOMBI YA VIWANGO VYA CHINI SANA.. NISEME TUU HUNA HAJA YA KUOMBA HAYO, BALI UNAHITAJI KUPATA TOCHI YA KIROHO (🔦) AMBAYO KILA UNAYEMSIKIA UNAMMULIKA MARA MOJA NA KUPATA JIBU..NAMI KATIKA MAELEZO YA FUNDISHO SITATHUBUTU KUTAJA JINA ETI YULE PASTOR CHRIS NI WA UONGO,YULE PROPHET BUSHIRI NI WA KWELI.. WATU WAKIKAA KUTAJA LIST YA WATUMISHI WAKIWASEMA HAWA WA UONGO HAWA WA UKWELI,KIKAO HICHO MUNGU HAKISIKILIZI(MALAKI 3:16) MNAHESABIKA TUU WATOTO WACHANGA KIROHO NA AKILI ZENU HAZIJA ZOEZWA KUPAMBANUA(EBR 5:12-14)SASA KWA HABARI YA ROHO ZIDANGANYAZO SIO KITU CHEPESI KUFUNDISHA NI MPAKA BWANA AWE AMEAMUA KUKUFUNDISHA UWAFUNDISHE WENGINE MAANA SI WOTE WATAPEWA KUPAMBANUA ROHO.WENGI WANAZUNGUMZA MISIMAMO YA MADHEHEBU YAO NA SIO ILE ' KWELI YOTE YA MUNGU..' UTASIKIA MTU ANASEMA, "UKIONA MTUMISHI ANAPAKA MAFUTA UJUE NABII WA UONGO" NA NILIMSIKIA MCHUNGAJI MMOJA WA EAGT AKIFUNDISHA KUSEMA,"UKIONA MTU ANAOMBEA ANATAMKA TOUCH AU POWER,UJUE NI FREEMASON NA ANATUMIA NGUVU ZA GIZA. 😃😃😃JE! NI HIVYO TUU KWELI..WAKRISTO WENGI HASA WALOKOLE AMBAKO HUO UVAMIZI NI MKUBWA WAMEJICHAGULIA SULUHU YAO YA KUKATAA VYOTE NA KUWAKATAA WOTE ILI KUJILINDA, NA WENGINE WAMETENGENEZA MAFUNDISHO AMBAYO NI YA WOGA TUU NA ILI KULINDA WASHIRIKA (UTASIKIA HUDUMA HIZO ZILIKUWA ZAMANI SAIVI HAZIHITAJIKI)..KWA HIYO KUNA WENGINE WAKISIKIA MTU KAITWA "NABII" AU "MTUME" NI HAPOHAPO WANAANZA KUTOMWAMINI WANAKUBALI MAJINA MENGINE YOTE MCHUNGAJI,MWALIMU,MWINJILISTI ETC..TATIZO NI NINI? YALIKOSEKANA MAFUNDISHO SAHIHI SASA WATU WANAMALIZA MALIGHAFI ZA KIROHO NA WANATUMIA BUNDUKI KUUA MENDE..

ZAIDI YA KWAMBA MUNGU AMENIPA NEEMA KUFUNDISHA HILI LAKINI ILI NIKAMILIKE KTK UJUZI WA ILE KWELI (2TIM 3:7) ILINIPASA WAKATI FULANI KUPEPETWA(NILIPOTELEA KTK IMANI POTOFU ILI NIYAJUE YOTE KWA UKAMILIFU WAKE,BWANA AKANIPA KUONGOKA ILI NIWAIMARISHA WENGINE (LUKA 22:31)

2.)ROHO ZIDANGANYAZO NI NINI/NANI

TUREJEE KATIKA ANDIKO LETU LA MSINGI (1TIMOTHEO 4:1)

1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

TUNAKUTANA NA JINA HILI "ROHO ZIDANGANYAZO" DECEIVING SPIRITS/SPIRITS OF DECEPTION..  HII/HIKI NI KITENGO/IDARA MAALUM YA SHETANI INAYOLENGA KUFANYA IN-CHURCH INVASION(INTERNAL DESTRUCTION) YAANI INALIVAMIA KANISA NA KULIHARIBU NA KULILETEA UKENGEUFU KUTOKEA NDANI (1YOH 2:19)

19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.

IKUMBUKWE UONGO UNATOKEA KWENYE UKWELI,YAANI LAZIMA KUWE NA UKWELI ILI UWEPO UONGO..ROHO HIZI HAZIDILI NA UONGO BALI UKWELI ILI KUUKENGEUSHA AND AS THE MATTER OF FACT HAZIJITOKEZI KTK MAENEO AMNAYO TAYARI YANAFUNDISHA UONGO TOKEA MWANZO,NO! HIZI ZINAVAMIA KUTOKEA KWENYE IMANI ILEILE AMBAYO IKO SAHIHI...UTANIELEWA VIZURI MBELE KIDOGO!

NB:
--
PERSONAL EXPERIENCE(UZOEFU BINAFSI) JUU YA ROHO ZIDANGANYAZO
MUNGU ALINIPITISHA KTK SHULE MBILI ZA KIROHO ILI KUFAHAMU KITENGO/IDARA HII YA SHETANI

SHULE 1 :

2004/2005 NIKIWA PUGU SECONDARY SCHOOL(DAR ES SALAAM) KULIINUKA KIJANA FULANI WA SDA,AMBAYE ALIKUJA HAPO SHULE AKIWA ANATOKEA KIJIJINI ..BAADA YA MUDA MFUPI AKAWA ANATOKEWA NA WACHAWI..NA KUPATA MATESO..MARA USIKU ANATOKA BWENINI MBIO KWA KUWA ALIKUWA AKIVAMIWA NA MAMA MCHAWI WA KIJIJINI KWAO ANAMCHAPA FIMBO NA KUMSEMA KWA NINI AMEONDOKA NA KUMWACHA BINTI YAKE ILI ASIMWOE,YEYE KAJA KUSOMA MJINI? HAYO MATESO YA WACHAWI YALIMZIDI NA YAKAWA YANAMJIA HADI MCHANA KWEUPE TUKIWA DARASANI AKAWA ANATOKEWA ANANYANG'ANYWA HATA MADAFTARI YAJE KIMAZINGARA YANAPOTEA NASI TUBASHUHUDIA..

BAADA YA MUDA MWINGI WA MATESO,AKAANZA KUTOKEWA NA MALAIKA WALIOKUWA WANAINGILIA KATI KUMTETEA DHIDI YA WALE WACHAWI..NA SASA AKAPATA NAFUU KUBWA..KILA WALIPOMJIA MALAIKA ALITOKEA NA KUMPIGANIA NA ALIWASHINDA WALE WACHAWI WAKAACHA KUMTESA.. SASA TULIPOHOJI  TUKAONA HAO WANAMTOKEA NI MALAIKA KABISA TUKILINGANISHA NA NENO LA MUNGU NA UFUNUO BINAFSI.. BAADA YA MUDA IKAWA ANAYEMTOKEA NI YESU SI MALAIKA PEKEE..KIJANA HUYU INGAWA KWA IMANI NI MSABATO LAKINI HAKUCHANGAMANA NA WASABATO,ALIANDAMANA NASI SANAA NA KILA RATIBA ZA IBADA NA MAOMBI AKAHAMIA ZA CASFETA JUMUIYA WA WANAFUNZI WA KIPENTEKOSTE.. TULIDUMU NAYE KARIBU MIAKA MIWILI TUKIENDELEA KUAMINI NA KUMSIKILIZA MAANA GHAFLA YEYE AKAWA NDIYE MSEMAJI NA MFUNDISHAJI NASI TUNAMSIKILIZA MAANA ALIKUWA NA OFFER YA KUTOKEWA NA YESU MARA NYINGI..NA KWA SABABU YA MAPITO ALIYOTOKA KUPITIA TUKAJUA BWANA AMEMPA OFA..MAANA SISI PAMOJA NA KUOKOKA KITAMBO,PAMOJA NA MAOMBI MENGI NA KUFUNGA NA KUFANYA HUDUMA KWA BIDII HATUKUWAHI KUMWONA BWANA KWA DHAHIRI VILE..HATA MIMI SANA SANA MUDA KABLA YA WOKOVU NILIMUONA KTK NJOZI AKINIITA NIOKOKE .SASA YA HUYU ILIKUWA NI YA VIWANGO..SASA WATU WOTE WAKAMWAMINI NA WENGI WALIKUWA WAKIMUULIZA NA MASWALI AWAULIZIE KWA BWANA..WENGI WALIPATA MAJIBU YA MAISHA YAO...EITHER MUNGU ALITUFUNGA MACHO AU VYOVYOTE ILI APATE KUTUFUNDISHA..BAADA YA MWAKA MMOJA NA NUSU  HIVI TUKAANZA KUONA MAMBO AMBAYO YANATUPA UTATA..KUHUSU YULE YESU WA YULE NDUGU HUENDA NI YESU MWINGINE(2KOR 11:4) MAANA TUNAAMBIWA NINI HAPA (2KOR 11:14)

14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
MARA AKAWA HAMWITI YESU ANAMWITA YULE JAMAA,TUKISHTUKA ANASEMA YESU..HUKU AKIHAMAKI HADI NISEME YESU.??😡 SASA AKAANZA KUTOA NAFUNDISHO MENGI AMBAYO SIO YA KWELI,YOTE AMEFUNDISHWA NA HUYO ANAYEMTOKEA KAMA YESU..NA HUYO JAMAA ALIMPA UJANJA MWINGI ILI KUTUZUGA WANA WA MUNGU...WENGINE WALIAMINI SANA KIASI KWAMBA KUKATOKEA MPASUKO KATI YETU  TULIOOKOKA,NAKUMBUKA VIONGOZI TULIINGIA KWENYE MAOMBI YA KAVU BWANA AWAREJEZE WENGINE MAANA HUYU MTU ALIWANASA VINARA WA KIROHO KTK FELLOWSHIP..
TO MAKE A LONG STORY SHORT NIIKATE KIHIVI.. KIJANA MMOJA AITWAYE DANIEL AKAAMUA KUINGIA KWENYE MAOMBI SERIOUS MCHANA KUTWA USIKU KUCHA BILA KUNYAMAZA..MAANA TULIKUWA TUMEANZA KUHISI KUWA ANAYEMTOKEA NI PEPO LA UTAMBUZI LILILOJIVIKA MWILI KAMA YESU ...MAANA NAMNA NYWELE ZILIVYO,YERUSALEM SANDALS NA ALAMA ZA MISUMALI KAMA YESU KABISA NA HUYU KIJANA KILA TUNALOMUULIZA ANAJIBU SAHIHI HATA YA SIRINI..SASA HUYU DANIEL AKASEMA BWANA KAMA HUYU JAMAA NI PEPO LA UTAMBUZI BASI NINALIFUNGA AKILI KWA HABARI YA JAMBO HILI...HUYU NDUGU ALILIFUTA LILE JAMBO LAKE KILA MAHALI ALIPOWAHI KUANDIKA NA ALILIFUTA HATA KWENYE UBONGO WA RAFIKI ZAKE ALIOWAHI KUWAJULISHA SIRI HIYO...IKUMBUKWE PEPO LA UTAMBUZI  LINAWEZA PATA HABARI HATA KWENYE AJILI YA MTU ULIYEWAHI KUMWAMBIA ISHU YAKO AU MUDA UNALIONGEA NA HUJAKIWEKEA NYWILA YAANI "PASSWORD" YA KIROHO..BAADA YA MAOMBI HAYO YA KUOMBA BILA KUMYAMAZA..ILIKUWA SIKU YA JUMANNE AKAMFUATA YULE KIJANA ..AKAMWAMBIA BWANA AKIKUJIA NAOMBA UNIULIZIE NENO HILI! KAMA KAWAIDA YULE MJUMBE AKAENDA KUULIZA...KWA MARA YA KWANZA YULE JAMAA ANAYETOKEA KAMA YESU AKATOA MAJIBU YA UONGO AMBAYO HATA TANZANIA HAYAPO...NI KAMA LILIVULUGWA LIKAKOSA UELEKEO..
TANGI HAPO TUKASHTUKA...

SASA HOJA YA MSINGI KTK SIMULIZI HII NI NINI?? SISI TULIOOKOKA KTK KWELI TULIENDELEA KUOMBA NA MTU ANAYETOKEWA NA YESU FEKI TUKIAMINI NI BWANA MKUBWA YESU KRISTO..NA SIO KWAMBA TULIKUWA WAVIVU KIROHO..HAPANA TULITUMIA MUDA MWINGI KUOMBA NA KUFANYA HUDUMA KULIKO CHOCHOTE...SASA MUDA TUNAPOTEA HIVI YULE YESU HALISI ALIKUWA WAPI? KWA NINI HUYU PEPO WA UTAMBUZI ANASTAHIMILI MAOMBI YOTE YA WATAKATIFU..ANAOMBA PAMOJA NASI ANAKESHA PAMOJA NASI KUMBE SIO...HIYO ILIKUWA COURSE YA KWANZA BWANA KUNIFUNDISHA KUHUSU ANDIKO HILI (2KOR 11:14)

1
[14:56, 20/11/2015] proo: SHULE 2:
MUNGU ALITAKA KUNIKAMILISHA KTK UJUZI HUU,HII SHULE YA PILI ILIKUWA MORE PRACTICAL. MWAKA 2007 NILIINGIA KTK IMANI POTOFU LAKINI ILIKUWA NI KWA KUSUDI KWAMBA NIKISHAONGOKA NIJUE KUWASAIDIA WENGINE..KWA HIYO NIKIMALIZA USHUHUDA HUU..SITAONGEA HISIA BALI VITU AMBAVYO NILIVIISHI NA KUVITENDA..NYAKATI HIZO KULIKUWA NA KUTOAMINI JUU YA MANABII WALIOKUWA WAMEZUKA KWA KASI SANA..NA WAKATI MWINGINE NILITOFAUTIANA SANA NA WAUMINI TOKA KTK HUDUMA HIZO ZILIZO CHINI YA HAO MITUME NA MANABII..KWANZA NILITOFAUTIANA NAO KWA KUYAPINGA MAFUNDISHO AMBAYO NILIYAONA YANAENDA KINYUME NA BIBLIA..PILI NI KAMA ROHO NDANI HAKUWA MMOJA ILI TUPATE UMOJA WA ROHO..(EFESO 4:4-5)..
LAKINI BAADA YA MUDA NILIWAHUSUDU HAWA WATU MAANA INGAWA NILIONA KWA HABARI YA NENO LA MUNGU WAKO DHAIFU..LAKINI WALIOKANA KUWA BA UPAKO ZAIDI..YAANI NGUVU YA UDHIHIRISHO ILIKUWA KUBWA ISHARA,MIUJIZA NA AJABU ZILIWAFUATA SANA..NA HATA RAFIKI ZANGU NILIOKUWA NAO  WAMOJA KIIMANI..WALIPOENDA HUKO WALIRUDI WABAUPAKO GHAFLA WALIANZA KUTUMIWA KWA MIUJIZA YA BILA KUPEPESAPEPESA.. NAMI NIKAJARIBIWA KUZITAMANI ZILE NGUVU...NAMI NIKAAZIMU NITAKWENDA KAMA WENZANGU NIPATE TUU HUU UJUZI NA UPAKO ILA SITAANDAMANA NAO WALA KUANDAMANA NA MAFUNDISHO..NIKAAZIMU NIENDE HUKO..NIKIPOKEA KAMA WALICHOPOKEA WAZANGU NITARUDI NA KUENDELEA NA HUDUMA YANGU YA KUFUNDISHA NA KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI (2TIM 2:15) ..SO NIKAENDA..NILIPOFIKA SEHEMU HUSIKA NAMI NIKAUPOKEA UPAKO HUO MAANA INGAWA HUKU NILIPOTOKA DHEHEBU LETU LINAPIGA VITA MATUMIZI YA ANOINTING OIL..LAKINI NILIJIKAZA ILI NIPOKEE THEN NISEPE ZANGU.. HIVYO HUYO MTUME AKANIPAKA MAFUTA YA UPAKO ..LAKINI NILIKUWA PAKE MGUU NJE MGUU NDANI YAANI NAAMINI NUSU..WENGINE WOTE WALIPAKWA MAFUTA WALIANGUKA NA WENGINE WALIKUWA KTK TRANCE(KAMA KU-FAINT) FULANI HATA NUSU SAA..LAKINI MIMI NILIKUWA KAMA NILIVYO SIKUHISI CHOCHOTE; TULIKUWA KAMA VIJANA 800. NILIPOONDOKA SIKU HIYOHIYO  NIKAANZA KUSIKIA SAUTI IKINIPA MAELEKEZO..NILISHTUKA USIKU NIKASIKIA SAUTI INANIAMBIA "TULIA USIKILIZE" ..... "KUELEWA NI MUHIMU SANA" BASI TANGU HAPO NILIKUWA NIKIONGOZWA KWA NDOTO KIBAO..NILIKUWA NAOTA NDOTO NYINGI SANAA NA NILIKUWA NAZIANDIKA KTK DIARY KUBWA..IKAFIKA WAKATI NILIWEZA HADI KUAMURU NIOTE NDOTO GANI..NA NIKISINZIA NAOTA HIYOHIYO! HAIKUISHIA HAPO RATIBA ZA KUFUNGA ZILIZIDI KWA GHAFLA SANA..NA IKAWA KTK KILA HUDUMA NINAYOPANGWA LAZIMA MIUJIZA ITOKEE... NA SASA HUDUMA/KARAMA ZILE NILIKUWA NASIKIA TUU NIKAANZA KUZIONA.. NILIKUWA NAENDA KANISANI NIKIWA NAJUA TAYARI NAJUA KUNA WAGONJWA GANI..WENGINE NILIPATA TAARIFA ZAO NIKIWA HATA STENDI YA DALADALA AU NIMEKAA SEBULENI NAANGALIA TV IKANIPA KUWA MAKINI MAANA MUDA WOWOTE NAPATA TAARIFA  ZA WATU/WAGONJWA

KWA MWEZI MMOJA TUU NILISHUHUDIA MAMBO YA AJABU NA KWA KASI..SASA HAYA YALIAMBATANA NA MAMBO MENGINE AMBAYO PIA YALINIPA SHIDA.. BAADA YA MUDA NIKAANZA KUJIGUNDUA KUWA SIPO KTK NJIA SAHIHI... LAKINI NIKAWA NAENDELEA ILA SINA UHAKIKA HIVI HAYA NI YA BWANA KWELI AU NI NJIA ZINGINE???  NILIENDELEA KUTATIZWA NA KUKOSA RAHA..NILITAFUTA UFUMBUZI SIKUPATA..SIKU MOJA NILITEMBELEA KANISA FULANI...NIKAKUTA HUYO ASKOFU ANAELEZA JINSI ALIVYOKUTA NA MKASA WA ROHO ZIDANGANYAZO MIAKA YA 1990's. NDIPO NIKAJUA KUKEMEA KWA JINA LA YESU NA KAZI ZIKAFANYIKA SIO KIGEZO KWAMBA ANAYEHUSIKA NI YESU (HILI NITALIFAFANUA HUKO MBELE KABISA) SASA NIKAJIGUNDUA NIMEPOTEA LAKINI NARUDIJE SASA?

NILIJIYAHIDI KUMTAFUTA HUYO MTUMISHI LAKINI KUMUONA NI MTIHANI MZITO.. NIKAAMUA KUPANGA MAOMBI YA WIKI TATU KUOMBA KWA BWANA NIREJEZWE..SIKUYAKAMILISHA VIZURI LAKINI  BWANA ALINIHURUMIA AKANIREHEMU..AKANIREJEZA KWA UPOLE (YEYE NI MPOLE WALA HAKEMEI...yakobo 1:5)SASA NITAUNGA HII HABARI HUKO MBELE

POINTS KUTOKANA NA SHULE HIZO MBILI:
ROHO ZIDANGANYAZO KAMA KITENGO HUSIKA CHA KU-OPERATE NDANI YA MWILI WA KRISTO ILI KUKENGEUSHA...HAKIKEMEWI KWA JINA LA YESU TOKA...MAANA ZINAUWEZO WA KUJICHANGANYA NA WANA WA MUNGU..NA KUVUMILIA HATA UWEPO WOTE WA MUNGU!

SEHEMU YA 3

III. ZINATENDA KAZI KWA KUPITIA AKINA NANI?

MUNGU ANATENDA KAZI NA/KWA KUPITIA KWA WATU (RUMI 8:28) SHETANI NAYE KAIGA HILO..KATIKA MUUNDA WA UTAWALA WA SHETANI/LUCIFER ZIKO ROHO ZIDANGANYAZO CHINI YA FALME NA MAMLAKA ZINAZOZALISHA IMANI POTOFU..
FROM THE TOP YUPO LUCIFER/SHETANI AMBAPO DARAJA LA PILI KUNA FALME NA MAMLAKA (KINGDOMS AND PRINCIPALITIES) NA NEXT TO THAT NI  MAJESHI YA PEPO WABAYA(MAPEPO/MAJINI) AMBAPO CHINI YAO KUNA WAGANGA,WACHAWI,WALIMU WA UONGO,MANABII WA UONGO,MITUME WA UONGO  ETC! ROHO ZIDANGANYAZO ZINAZOACHILIWA NA FALME NA MAMLAKA SIO YALE MAPEPO TUNAYOYAKEMEA YAKATOKA IKUMBWE HII NGAZI YA FALME NA MAMLAKA NDIYO INAYOAMUA ENEO HUSIKA LIWEJE KIIMANI,KIUCHUMI,KIJAMII,KIUTAMADUNI ETC..UWEPO WA DINI YA KIBUDHA HUKU MASHARIKI YA KATI AU HINDUISM AU TAOISM AU SIKHISM  AU GYNOSTICISM ETC ETC NI KAZI YA FALME NA MAMLAKA..SHETANI NI YULEYULE TUU KTK DINI ZOTE HIZO..ILA HIZI FALME NA NAMLAKA..

MAKUNDI MAWILI YA HAWA WATUMISHI:

1.)KUNDI LA KWANZA NI LA WALE AMBAO THEY WORK AS AGENTS..YAANI WANATUMIKA CHINI YA ROHO ZIDANGANYAZO IN FULL KNOWLEDGE..WANAJUA KABISA KUWA WANATUMIKIA NGUVU ZENYE MFANO WA HIZI ZA UTAUWA KUMBE WANAMKANA HANA MOLA WETU HAWA NI WENGI ZAIDI NA WAMEFANIKIWA KUPOTEZA WENGI..

2.)KUNDI LA PILI NI WALE WANAOTUMIKA CHINI YA ROHO ZIDANGANYAZO BILA KUJUA..KWA NINI HAWAJUI...?HAWA NI WALE AMBAO WALIKUWA TUU NA SHAUKU NA UPAKO LAKINI HAWANA MSINGI WA KWELI YA MUNGU WAKAKUTANA NA UVAMIZI WA ROHO ZIDANGANYAZO..MOST OF THEM WALIKOSA MABABA WA KIROHO (1KORINTHO 4:15) NA WALIANZA HUDUMA KWA MIFUNGO MINGI KAMA KUFUNGA SIKU 40 ,KULALA MILIMANI..WALIPOSIKIA SAUTI ZINAWAONGOZA THEY HAD NO MENTOR KAMA ELI KWA SAMWEL..WAZUNGU HUSEMA "WITHOUT A MENTOR YOU'RE A MENTAL!". SASA WENGI HUFUATISHA ZILE SAUTI NA KUJIKUTA WAMELOTELEA MBALI SANAAAA

2
[14:56, 20/11/2015] proo: KWA HIYO KUNAWEZA KUWA NA MTUME WA UONGO,NABII WA UONGO,MWALIMU WA UONGO MCHUNGAJI NA MWINJILISTI WA UONGO KAMA TUNAVYOONA KTK MAANDIKO YAFUATAYO

MANABII WA UONGO
15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. MATH 7

WALIMU WA UONGO
1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. 2pet 2:1ff

MITUME WA UONGO
2 Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;

WACHUNGAJI WA UONGO
Yeremia 23:1-27

KWA HIYO KUNAWEZA KUWA NA MTUME WA UONGO,NABII WA UONGO,MWALIMU WA UONGO MCHUNGAJI NA MWINJILISTI WA UONGO KAMA TUNAVYOONA KTK MAANDIKO YAFUATAYO

MANABII WA UONGO
15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. MATH 7

WALIMU WA UONGO
1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. 2pet 2:1ff

MITUME WA UONGO
2 Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;

WACHUNGAJI WA UONGO
Yeremia 23:1-27
Bible - YEREMIA - 1 Ole wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya! Asema BWANA.2 Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, juu ya wachungaji wanaowalisha watu wangu, Mmetawanya kundi langu, na kuwafukuza, wala hamkwenda kuwatazama; angalieni, nitawapatiliza uovu wa matendo yenu, asema BWANA.3 Nami nitakusanya mabaki ya kundi langu, katika nchi zile zote nilizowafukuza, nami nitawaleta tena mazizini mwao; nao watazaa na kuongezeka.4 Nami nitaweka juu yao wachungaji watakaowalisha; wala hawataona hofu tena, wala kufadhaika, wala hatapotea hata mmoja wao, asema BWANA.Chipukizi la Haki la Daudi5 Tazama siku zinakuja, asema BWANA, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.6 Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu.7 Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema BWANA, ambapo hawatasema tena, Aishivyo BWANA, aliyewatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri;8 lakini, Aishivyo BWANA, aliyewapandisha na kuwaongoza wazao wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi zote nilikowafukuza; nao watakaa katika nchi yao wenyewe.Manabii wa Uongo Wanaoahidi Tumaini Washutumiwa9 Katika habari za manabii.Moyo wangu ndani yangu umevunjika,Mifupa yangu yote inatikisika.Nimekuwa kama mtu aliye mlevi,Na kama mtu aliyeshindwa na divai;kwa ajili ya BWANA, na kwa ajili ya maneno yake matakatifu.10 Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki.11 Maana nabii, na kuhani, wote wawili wanakufuru; naam, katika nyumba yangu nimeuona uovu wao, asema BWANA.12 Kwa ajili ya hayo njia yao itakuwa kwao kama mahali pa kuteleza gizani; watatelemshwa na kuanguka hapo; kwa maana nitaleta uovu juu yao, naam, mwaka wa kujiliwa kwao, asema BWANA.13 Nami nimeona upumbavu katika manabii wa Samaria; walitabiri kwa Baali, wakawakosesha watu wangu Israeli.14 Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.15 Basi BWANA wa majeshi asema hivi, katika habari ya manabii, Tazama, nitawalisha pakanga, nitawanywesha maji ya uchungu; kwa kuwa kutoka kwa manabii hao wa Yerusalemu kukufuru kumeingia katika nchi yote.16 BWANA wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika kinywa cha BWANA.17 Daima huwaambia wao wanaonidharau, BWANA amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wo wote.18 Maana, ni nani aliyesimama katika baraza la BWANA, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno langu, na kulisikia?19 Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni dhoruba ya kisulisuli; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani.20 Hasira ya BWANA haitarudi, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtalifahamu neno hili kabisa.21 Mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; sikusema nao, lakini walitabiri.22 Lakini kama wangalisimama katika baraza yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu wangu maneno yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya, na uovu wa matendo yao.23 Mimi ni Mungu aliye karibu, asema BWANA, mimi si Mungu aliye mbali.24 Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.25 Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, Nimeota ndoto; nimeota ndoto.26 Je! Mambo hayo yatakuwa katika mioyo ya manabii wanaotabiri uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe?27 Wanaodhania ya kuwa watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao, wanazomhadithia kila mtu jirani yake, kama vile baba zao walivyolisahau jina langu, kwa ajili ya Baali.

Post 5

Inaendelea......

3
[14:56, 20/11/2015] proo: NB:

IKUMBUKWE ROHO HIZI ZIDANGANYAZO;HAZIJI KWA JINA LA SHETANI BALI LA YESU,USISUBIRI UKUTE HIRIZI NA VITENDEA KAZI KAMA VYA WAGANGA.. HIKI NI KITENGO KINGINE KABISA..LAKINI VINATUMIKA KWA LENGO LA KUPOTEZA NA KUKENGEUSHA YAMKINI HATA WATEULE..LAZIMA WATUMIE JINA LA BWANA

5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. (Mathayo 24)

Yeremia 14 : 14 - Ndipo Bwana akaniambia, Hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi; mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru, wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo, na uaguzi, na neno la ubatili, na hadaa ya mioyo yao.

KWA HIYO USIDANGANYWE  KWA KUWA KUNA PRAISE TEAM NZURI NA WAPIGA VYOMBO MAHIRI..UKAJUA BADO NI ROHO YULE YULE

KITOVU CHA UKENGEUFU :

ROHO ZIDANGANYAZO ZIMETEKA WENGI KATIKA WATEULE KWA SABABU ZINAKUJA "EXACTLY" KTK SURA ILEILE YA UKWELI YAANI NI KAMA KUCHUKUA COMPACT DISC MBILI UKIZIELELEKEZA UPANDE MWANGAVU 💿📀 ZINAKUWA ZINA SURA MOJA KUMBE CONTENTS NI TOFAUTI KABISAA!

MFANO KWA WALE WANAOTUMIWA KWA KARAMA ZA KUPONYA NA NENO LA MAARIFA...NAMNA ILE ILE AMBAYO ROHO WA KWELI ANAKUTUMIA NDIVYO HIZI ROHO ZINAVYO COPY NA KUFANYA...

IKUMBUKWE SHETANI NI MTAALAMU WA KUCOPY (COUNTERFEIT)MFANO UKIWA UNAHUDUMU UNAWEZA HISI MKONO UMEKUGUSA MGONGONI IKIWA NA MAANA UNAJULISHWA KUNA MTU KTK KUSANYIKO ANASHIDA HIYO..SASA HILI KWA ROHO WA KWELI LINAFANYIKA SAWASAWA HATA KWA ANAYETUMIWA NA ZILE ROHO ZINGINE..SABABU KUU NI KWAMBA SHETANI ANAWEZA FANYA MASQUARADING (2KOR 11:13-15)

Post 6

Inaendelea.....

SASA KATIKA SEHEMU INAYOFUATA TUTAINGIA NDANI SANAA KUJUA NAMNA YA KUWATAMBUA

MWINGINE AMBAYE HAJAGUSWA..ANAWEZA SEMA MIMI SITADANGANYWA..HUKU AKISEMA YULE ROHO WA KWELI LAZIMA ATANIAMBIA TUU.. SASA HII NI TAHADHARI TU ILI SIO UPONE PEKE YAKO BALI UWASAIDIE WENGINE PIA..

IV. UTATAMBUAJE KUWA MTUMISHI HUYU ANATUMIKA CHINI YA ROHO ZIDANGANYAZO? VIASHIRIA/INDICATORS

BIBLIA IMEWEKA TAHADHALI NYINGI JUU YA NYAKATI ZA MWISHO NA YALE YATAKAYOTOKEA..KTK VIASHIRIA HIVI 20 TUNAVYOKWENDA KUJIFUNZA..SI LAZIMA UVIONE VYOTE KWA MTUMISHI AU HUDUMA ILI UJIRIDHISHE KUWEPO KWA ROHO ZIDANGANYAZO...UKIKIIONA KIMOJA TUU INATOSHA NA CHUKUA TAHADHALI

VIASHIRIA:

1)MTU HUYU ATATAFUTA KUWA MKUU.. CHEO CHA KUWA MKUU NI CHA BWANA MUNGU MWENYEZI
MKUU NI YESU MWENYEWE PEKE YAKE
Matendo ya Mitume 5 : 31 - Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.

SASA WATU WENGI WALIOWAHI KUZUKA CHINI YA HIZI ROHO ZIDANGANYAZO WALIJINADI KUWA "WAKUU"

36 Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu. (Mdo 5)

Yule Simon

9 Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. (Mdo 8)

USHUHUDA..
NILIWAHI HUDHURIA KANISANI KWA MTUME NA NABII FULANI..NIKAMSIKIA AKISEMA MIMI NDIO NABII WA KWANZA AFRICA...AKAENDELEA KUSEMA HAPA DUNIANI KUNA MANABII WAKUBWA WATANO..WAWILI WAPO AMERICA MMOJA NI YEYE WA TATU KWA UKUU NA WAWILI WAPO ASIA.. SASA HOJA ZAKE ZOTE ZINALENGA KUMFANYA MKUU..NA AKASEMA YESU AMEMPA UPAKO MWINGI HAJAFIKISHA HATA NUSU KUUTUMIA
SASA SISI TUMEITWA TUJISEME KWA WATU NI WATUMWA TUSIO NA FAIDA (LUKA 17:10) HIVYO UKIONA MTU ANAJIBIDIISHA KUONEKANA YEYE NI MKUU,JUA WAZI KUNA UVAMIZI WA ROHO ZIDANGANYAZO

Post 7
Inaendelea....

4
[14:56, 20/11/2015] proo: 4.)KUWAFANYA WATU WAFUASI WATUMWA NA KWA MAFUNDISHO YENYE KUWATIA HOFU BADALA YA FARAJA YA BWANA
WAPENDWA MAMA MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT NILILOKUWA MSHIRIKA ALINASWA NA KUHAMIA KTK HUDUMA YENYE UTATA SANA.. JAMBO LA KWANZA UNAPOJIUNGA USHIRIKA KUNA (CONFESSION PRAYER) UNAONGOZWA ILI KUKUUNGANISHA NA MADHABAHU YA HUDUMA HIYO...MIONGONI MWA MANENO YANAYOTAMKWA NI HAYA.."NAJIUNGAMANISHA NA MADHABAHU HAYA,SIKU NIKIHAMA,KUFA NA NIFE".. SASA HADI KUJIOMBEA KIFO UKIHAMA IMALENGA NINI KAMA SIO KUKUFANYA MFUASI MTUMWA?
NILISIKIA WAKITOA FUNDISHO AMBALO LILINITIA HOFU NIKAAMUA KUZIMA REDIO TUU..MAFUNUO MENGINE BWANA DAAH!! ATI ALISOMA MITHALI 23:29 AKASEMW UKIONA UNA KOVU LOLOTE MWILINI MWAKO..HUKUMBUKI ULIUMIAJE BASI JUA KUWA UNA MAAGANO YA KUZIMU UJE NIKUFUNGUE..SASA LEO HII NIANZE KUKUMBUKA KILA KOVU NILIUMIAJE WAPI MAMBO HAYA? YANALENGA KUKUFANYA MTUMWA NA KUMHITAJI ZAIDI HUYO MTUMISHI KULIKO CHOCHOTE

5.)MAMBO AMBAYO NI YA AIBU HATA KTK JAMII YATAFANYWA NI YA KAWAIDA AS IF MPO VIWANGO VYA JUU SANA KIROHO

HIKI NI KIASHIRIA CHA WAZI.. NILIFANYA HUDUMA NA VIJANA WA HUDUMA FULANI IKO DAR.. NILIPATWA NA AIBU KUBWA..LAKINI WAO WANAONA SAWA TUU. NILIONGOZANA NAO KWENYE HUDUMA YA MASHULENI..SASA WAKAWA WANAWATOA PEPO WASICHANA WA SEKONDARI KWA NJIA YA KUWAMINYA MATITI..👙 NA UKWELI NI KWAMBA KILA ALIYEANGUSHWA NA MAPEPO WALIPOWATOMASA MATITI WALIFUNGULIWA WAKAWA HURU

SI HIVYO TU..NIKIWA KANISANI KWAO 2007 KATIKATI YA IBADA MTUME MMOJA TOKA MBEYE AKASEMA EBU KILA MMOJA AMBUSU JIRANI YAKE..THENI KILICHOFUATA NI 😘😘😘😘 YA SHAVUNI HATA KAMA UMEKAA NA MKE WA MTU UNABUSU SHAVU..

NILIMSIKIA MTUME MMOJA WA DAR KTK TV AMEFUNDISHA SOMO LINASEMA "KUKOMBOA MAKALIO" AKASOMA ZAB 1:1 THEN AKASEMA....wala hakuketi barazani pa....... AKAULIZA TUNAKETI KWA NINI..? WATU WAKAJIBU MAKALIO..THEN AKAAMURU WASIMAME NA KILA MMOJA AMPIGE MAKALIO JIRANI YAKE.. YAANI SIKUAMINI KUONA VIJANA WANAYAPIGA KOFI 👋🏾 MAKALIO YA WAMAMA..CHA AJABU WENGINE WALIPOPIGWA MAPEPO YALILIPUKA NA KUWATOKA.. NILIMSHUHUDI MTUME HUYU ALIHUBIRI NUSU SAA AKIWA NA BINTI AMEMKUMBATIA KIUNO..WASHIRIKA NILIOKAA NAO KARIBU BADALA WAHUZUNISHWE NA HILO WALIKUWA WAKISIFIA NA KUMUONEA WIVU YULE BINTI ..KWAMBA AKITOKA PALE ATAKUWA AMEPOKEA UPAKO MWINGI

AIBUU!!!!!!

MTUMISHI WA KWELI LAZIMA AYAKATAE MAMBO YA AIBU (2KOR 4:2)

Post 10

Inaendelea......

6
[14:56, 20/11/2015] proo: Continuation..VIASHIRIA

2.) UFUNUO KUINULIWA KULIKO NENO LA MUNGU

WAPENDWA YAKO MAENEO AMBAPO UKIENDA UNAWEZA UTAKUTA NENO LA MUNGU LIPO CHINI NA UFUNUO WAO BINAFSI UMEINULIWA SANA..KIUKWELI KILA UFUNUO NA UNABII HAUPASWI KUTWEZWA (1THES 5:20) LAKINI PIA HAYAPASWI KUAMINIWA BILA KUPAMBANULIWA (1KOR 14:29)
29 Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue

NA STANDARD TOOL YA KUPIMIA VYOTE HIVYO NI NENO LA MUNGU..KWA KUWA NENO LA MUNGU HALIPAMBANULIWI!UFUNUO UKIINULIWA JUU YA NENO JUA HAYO NI MAZINGIRA YA HIZI ROHO KUTENDA KAZI NA KULETA UKENGEUFU..KUNA KANISA MOJA DAR KARIBU NA NYUMBANI KWETU..NILIWAONA WANAUTUKUZA UFUNUO KIASI KWAMBA WAMEYAFUTA MAANDIKO MAWILI KTK BIBLIA KWAMBA YALIKOSEWA..MOJA KTK DANIEL JINGINE KTK UFUNUO WA YOHANA.. PIA WAMEBANDUA COVERS ZA BIBLIA KWA KUDAI ZINA NGUVU ZA GIZA SASA HAYA WAPI NA WAPI??MAMBO MENGI WANAYOYAFANYA EITHER HAYAPO KWENYE BIBLIA AU YANAPINGANA KABISA NA BIBLIA... UKIHOJI TUU..WANAKUJIBU MTUME AMESEMA KAMA ALIVYOFUNULIWA

Post 8

Inaendelea.........

3.) EXCESSIVE USE OF CULTIC OBJECTS(MATUMIZI YA KUPITILIZA YA KUTUMIA VISAIDIZI) KAMA MAFUTA,VITAMBAA,UNGA,SABUNI,MAJI ETC

SASA WAKO WATU KWA SABABU YA WOGA WA KUKENGEUSHWA..WAKIONA TUU MATUMIZI YA HIVI VITU BASI WANAKIMBIA..UKWELI NI KWAMBA HIVI VITU VIKO KIBIBLIA
MFANO MATUMIZI YA MAFUTA (MARKO 6:13,YAKOBO 5:14)

13 Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza.

14 Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.

MATUMIZI YA VITAMBAA NA VITU VINGINE YESU ALIFANYA NA MITUME PIA
Mdo 19:12

12 hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka.

KUTUMIA CHOCHOTE SIO TATIZO..SEMA UFUNUO KTK BIBLIA NI KITU TEMPORARY NA ROHO WA KWELI HATARUDIA RUDIA..NAMAANISHA FUNDISHO LINAJENGWA JUU YA NENO LA MUNGU NA SIO JUU YA UFUNUO WA MTU..
MFANO NILIMKUTA MTUME FULANI DAR ES SALAAM ANATOA PEPO KWA KUWAGUSA WATU KITOVU..SASA KAMA UKIFUNULIWA ON THE SPOT MGUSE KITOVU PEPO LITATOKA NI SAHIHI..BUT TUKIKUTA MMEJENGA FUNDISHO KABUSA..NA WATU WANAENDELEA KUGUSA VITOVU HATA VYA MABINTI ETI KUTOA PEPO HICHO NI KIASHIRIA CHA WAZI KUWA HAPO KUNA UVAMIZI

Post 9

Inaendelea......

5
[14:56, 20/11/2015] proo: 6.)KUNA KUWA NA UPAKO WA BURE USIO NA GHARAMA (SPOON-FEEDING ANOINTING)

MAENEO AMBAYO ROHO ZINATENDA KAZI HAKUNA MKAZO WA UTAKATIFU NA USAFI TWAJUA(POWER GOES AFTER PURITY) SASA HAWA MAJAMAA YOU DONT NEED TO BE HOLY ILI UPATE UPAKO..NILIWAONA WATU CHINI YA NABII FULANI NIKIWA NAO HUKO MTAANI WANATUKANA ,WANAPIGANA WANA MAZUNGUMZO MACHAFU SANA KUHUSU NGONO LAKINI WAKIWA KWENYE HUDUMA HATA WAKIPUNGA LESO ZAO TUU TEGEMEA WATU HATA 30 WATAANGUKA KUTOKA KWA VITI VYAO YAANI UPAKO..HUO NDIO NAMI NILIUFUATA NIKAUPOKEA LAKINI NI FEKI NA BWANA ALINITOA HUKO !!

Post 11

Inaendelea.....

7.)KUTODUMU MUDA MREFU

WENGI WANAOTUMIKA CHINI YA ROHO ZIDANGANYAZO HAWADUMU MUDA MREFU
TUONE MIFANO IFUATAYO
Ikawa, katika mwaka ule ule, mwanzo wa kutawala kwake Sedekia, mfalme wa Yuda, mwaka wa nne, mwezi wa tano, Hanania, mwana wa Azuri, nabii, wa Gibeoni, akasema nami ndani ya nyumba ya BWANA, mbele ya makuhani na watu wote, akisema, Basi nabii Hanania akafa, mwaka uo huo, mwezi wa saba.
YER. 28:1, 17 SUV
http://bible.com/164/jer.28.1-17.SUV

PIA TUSOME

Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu. Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika.
MDO 5:36-37 SUV
http://bible.com/164/act.5.36-37.SUV

HIVYO TUNAONA NABII HANANIA WA ZAMA ZA YEREMIA ALIZUKA AKAPOTEA PIA THEUDA NA YUDA MGALILAYA WOTE WANAVANISH IN ASHORT PERIOD OF TIME.. YAANI HII NI DHAHIRI KUNA MITUME HATA HAPA TZ WALIVUMA KWA GHAFLA NA HAWAPO TENA

SABABU KUU NI KWAMBA KWA KUTUMIKA CHINI YA ROHO HIZI WANAJILETEA UVUNJIFU USIOKAWIA

1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.

2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.

3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.

4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;

5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;

6 tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;
2pet 2:1-4

Post 12

Inaendelea......

8.)KUTATAWALIWA NA ELIMU MPYA YA KIGENI..

WAPENDWA MAHALI AMBAPO ROHO HIZI ZINAOPERATE KUNAKUWA ELIMU NYINGINE AMBAYO WATU WA MUNGU HAWAKUIJUA..LENGO NI KUWAFANYA WAAMINI WAMEPANDA VIWANGO.. NILIENDA KANISA MOJA DAR..WAHUDUMU WALINIULIZA UMEOKOKA? NIKAJIBU NDIYO WAKANIULIZA BAADA YA HILO SWALI WAKANIULIZA UMEFANYIWA "DELIVERANCE" MAOMBI YA UKOMBOZI..NIKAJIBU BADO KWA MTAZAMO ULE WA KWAO..THEN WAKANIAMBIA KAMA HUJAFANYIWA DELIVERANCE;HUJAOKOKA BADO!

SASA NILIYOKUTANA NAYO NDANI NI MAFUNDISHO YENYE ELIMU NGENI..IKANIFANYA NIWE KAMA NDIO NIMEKUWA MLOKOLE SIKU HIYO INGAWA KWA WAKATI HUO NILIKUWA NINA MIAKA MITANO YA UTUMISHI

MTUME HUYO ALIFUNDISHA KUANZA SAA SITA HADI SAA KUMI ALASIRI BILA KUSOMA MSTARI HATA MMOJA WA BIBLIA..ALITUAMBIA LEO NAWAPELEKS DARASANI...HIVYO ALITUFUNDISHA AINA 250 ZA MAPEPO NA JINSI YA KUYATOA..KILA PEPO ALITUELEZA ANAMWINGIAJE MTU,AKIINGIA ANAKAA WAPI NA NAMNA YA KUMTAMBUA MTU MWENYE FULANI HUSIKA NA NAMNA YA KUYATOA..KATIKA MAPEPO YALE ALIYOELEKEZA MENGI UNAYATOA KWA STYLES FULANI BILA HATA JINA LA YESU

KWA HIYO NILIJIKUTA NAJAZA DIARY KWA ELIMU NGENI KABISAA

TUSOME HAYA MAANDIKO

Waebrania 13 : 9 - Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida.
https://goo.gl/pE1TDH

Wakolosai 2 : 8 - Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
https://goo.gl/pE1TDH

1 Timotheo 1 : 3 - Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine;
https://goo.gl/pE1TDH

1 Timotheo 6 : 3 - Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,
https://goo.g

Wagalatia 1 : 8 - Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.

Post 13

Inaendelea......

9.)WENGI HUWAAMINISHA WAUMINI WAO KUWA WAO HAWATAKUFA NA KUWAPA TUMAINI LA KWAMBA KUNA NAMNA WATAWATETEA HUKO MBINGUNI

HAYA NIMEYASHUHUDIA SEHEMU NYINGI..MAANA MUNGU ALIPONIFUNDISHA HILI MWAKA 2007 NILIKUWA NIMETOKA KWENYE UKENGEUFU NA NILIZUNGUKA KWA MITUME NA MANABII KARIBU WOTE WA DAR ES SALAAM NA KWINGINEKO

ZAIDI YA MITUME NA MANABII WATATU HAPA JIJINI WAMEWAAMINISHA WAFUASI WAO KUWA WAO HAWATAKUFA WAPO SAA YA MWISHO KUWAPELEKA MBINGUNI.. KATI YA HAO WATATU MMOJA AMETANGULIA ALIPOENDA..ILA ALIWATHIBITISHIA KUWA HATA KUFA..HUYU ALITHUBUTU KUJIITA YEYE NI MUNGU WA MAJESHI ELIYA AJAYE KWA MFANO WA WILLIAM MARRION BRANHAMM NA INGAWA AMEKUFA NA KUZIKWA BADO HIZI ROHO ZILIBUNI UONGO KUWA AMEELEKEA KWENYE JUA KUSHINDANA NA NGUVU ZA FREEMASON..NDIVYO WOTE WALIO WA IMANI HIYO WANAVYOAMINI.. MWINGINE TENA BADO YUPO NAYE KAWATHIBITISHIA HATA KUFA..TENA ATAWATETEA KWA MUNGU.. SIKU MOJA NILIKUWA NAMSIKIA KWA TV AKAHUBIRI KUSEMA "ULOKOLE SII UJINGA" MMEO AKIKUSUMBUA MPIGE NA SUFURIA AU STULI..MBINGUNI NITAKUTETEA MIMI! PIA KAWAAMINISHA MBINGUNI KILA WATU WATAKAA KWA BABA YAO WA KIROHO (1KOR 4:15)

Post 14

Inaendelea......

SEHEMU YA TANO:

HATARI KUU

NDUGU WAPENDWA LIKO JAMBO LA HATARI SANA AMBALO MUNGU ALIWAHI KUNIJIBU.. NILIULIZA KWA BWANA ITAKUWAJE KWA WALE AMBAO WAMEOKOKA NA KUPATA MSAADA KUTOKEA HUKO..NA WAKAAMINI HABARI ZA YESU WAKIWA HUKO??

MUNGU ALINIPA JIBU LA AJABU SANA KUWA I'M NOT RESPONSIBLE " KWA WALE WATAKAOPOTEA...

NI KWELI MUNGU HAPENDI HATA MMOJA APOTEE (2PET 3:9) LAKINI WATAKAOPOTEA KWA ROHO ZIDANGANYAZO;HE IS NOT RESPONSIBLE.. ATAKACHOFANYA NI KUWEKA WATUMISHI WENYE KUIHUBIRI KWELI YOTE (YOHANA 16:13)ILI UKISIKIA UKIMBIE ..

KWA NINI HILI LA MANABII NA MITUME WA UONGO LIMEKUWA DHAHIRI SANA MUDA HUU??

UKWELI NI KWAMBA HAYA NDIYO MAJIRA HASWAA YA UKENGEUFU
2thes 2
3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; ak afunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;

4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?

6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.

7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.

8 Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;

9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
KUNA HATARI GULANI KUITUMIA HAPA MAANA HII KIHALISI INATAJA MAMBO YA WAKATI ULE BAADA UNYAKUO..LAKINI MAANDIKO YA KINABII HUWEZA KUBEBA MAMBO YENYE MAANA HADI SABA TOFAUTI..

SASA HUU NI WAKATI WA HUU UKENGEUFU KUWEPO..SHARTI MTU AIJUE KWELI ..

HAKUNA UDHURU (NO EXCUSE) WARUMI 1:20

6.)HOW TO STAND  IN THE SAFE SIDE

KAMA UPO SALAMA HAUJAINGIA KTK MTEGO HUU WA ROHO ZIDANGANYAZO SIMAMA IMARA KTK IMANI HII YA MUNGU-YEHOVA NA BWANA-YESU KRISTO ILIYOPEKEE YA KWELI NA TAKATIFU SANAA(YUDA 1:20)

KAMA UMEKWISHA NASWA UNAYONAFASI YA KUIKIMBIA...MAANA MWISHO WA HAWA WOTE WALIOCHINI YA HIZI ROHO ZIDANGANYAZO MWISHO WAO MBAYA.. NA LAZIMA UTAKUJA KUPATA ANGUKO LA KIROHO... THESE SPIRITS HAVE GOT THEIR PEAK.. LAZIMA WAWAFIKISHE KTK UZINZI YAANI KOSA KUU (AYUB 31:9-11) WANAJUA JINSI DHAMBI HII ITAKAVYOSAIDIA KUKUPA MOYO MBOVU.. SEHEMU NYINGI ZENYE ROHO HIZI FUATILIA THEN UTAELEWA JINSI UZINZI NA UASHERATI UNAVYOKUWA HAUEPUKIKI..NAANA VIONGOZI WA IMANI HUSAPOTI DHAMBI HIYO INDIRECTLY! NIKIWA KATIKA KUDHURURA ENZI ZANGU ZA KUKENGEUKA..NILIFIKA KWA MTUME NA NABII FULANI..SASA INAONESHA ANAPELEKEWA SANA KESI ZA WASHIRIKA WANAOZINI..KATIKATI YA MAHUBIRI AKASEMA KUNA WATU WASENGENYAJI...KILA SAA WANAKUJA OFISINI NA KUSEMA FULANI NA FULANI WAMEZINI NA NINA USHAHIDI.. BAADA YA KAULI HIYO AKASEMA "KWA TAARIFA YAKO UMBEA NI MBAYA KULIKO UZINZI.. THEN WATU WAKAPIGA MAKOFI NA KUSHANGILIA..HII SENTENSI ILIWANYAMAZISHA WATU WANAOSHUHUDIA UZINZI WA WASHIRIKA ULIOKUBUU..NA NANENO YA YULE NABII NI KAMA KUWATETEA WAZINZI NA KUWAPIGA STOP WALE WANAOTOA TAARIFA.. KWA HIYO UZINZI NI INGREDIENT YA HIZI ROHO ZIDANGANYAZO

KAMA UMENASWA GEUKA UKIMBIE..USIFANYE MAOMBI KUKEMEA

NB:
ROHO ZIDANGANYAZO HAZIKEMEWI BALI UNAPAMBANUA NA KUZIJARIBU UKIJUA HAZITOKANI NA BWANA UNAJITENGA NAZO ILI USIHARIBIKIWE KIROHO...

7.HITIMISHO

KWA WALE WOTE AMBAO WALIKUWA NA SWALI HILI; JE! INAWEZEKANA MTU KUTUMIA JINA  YESU SERIOUSLY LAKINI AKAWA ANATUMIA NGUVU ZA UFALME MWINGINE? TUMEPATA JIBU LA WAZI... KUWA  NDIO INAWEZEKANA! KWANI HII IDARA SPECIAL YA SHETANI HAITUMII MAPEPO/MAJINI YALE AMBAYO YAKISIKIA NENO YESU YANAUNGUA NA KUKIMBIA..NO! HIZI NI ZILE TUNAZOAGIZWA TUZIJARIBU (1YOH 4:4) HADI TUMAAMBIWA TUZIJARIBU NI KWA KUWA HAZIKO NJE ZIKO NDANI YA IMANI YETU,NA ZIMETOKA KWENYE IMANI YETU SAHIHI (1YOHAN 2:19)
TOFAUTI YA NGUVU ZA ROHO HIZI NA ILE YA ROHO WA KWELI NI HII.. NGUVU YA MIUJIZA YA MUNGU INALENGA KUUFUNUA UTUKUFU WA MUNGU (YOHAN 2:11) NA KUONDOA TATIZO.. NGUVU ZA UPAKO WA ROHO ZIDANGANYAZO AMBAO NAUITA SPOON-FEEDING ANOINTING MARA NYINGI ZINALETA SHOW(MAONYESHO) TUU

KUNA NABII ALIITA MWANAMKE MBELE THEN AKAMWAMBIA SHIKA POCHI YAKO.. THEN AKAITA WANAUME WENYE NGUVU WAWILI AKAWAAMBIA WAINYANG'ANYE ILE POCHI WAKASHINDWA THEN KANISA LOTE LIKAWA LINASHANGILIA... PIA ALIWAITA WADADA WAWILI AKAWAMBIA WAGEUKIANE VISOGO ..THEN WAKANASA ALIPOWAAMBIA WAACHANE WAKAWA HAWAWEZI;NA MAKUTANO YAKAWA YANASHANGILIA...

SASA SWALI LA MSINGI..HAWA WATU WANATATIZO GANI? NI WAZI ANAFANYA MAONESHO TUU..AMBAPO MUNGU SIO WA MAONESHO KABISAAAAA.

MIUJIZA YA MUNGU PAMOJA NA KWAMBA  INALENGA KUONDOA TATIZO..LAKINI PIA HATA YULE MTUMISHI ANAYETUMIWA KWA MIUJIZA NAYE YUPO MIONGONI MWA WANAOSHANGAZWA NA MIUJIZA HIYO HAIWI KAMA YEYE NI MASTER-CONTROLLER WA MIUJIZA..NAYE ANATUMIWA AKIWA ANAENDELEA KUMSHANGAA MUNGU

alltruth5ministries@gmail.com

🇲 🇼 🇱  🇵 🇷 🇴 🇴
Kwa maswali 0762879363

9

1 comment:

  1. Prosper Kdewele nimekuelewa vizuri sana kuhusu roho zidanganyazo
    Ni ukweli ambao kwa nafsi zetu kama wanadamu inatuchukuwa muda kugunduwa mapungufu yanapoanzia . Amani iwe nawe.

    ReplyDelete