*NILETEE NAIVERA*
Na Mwl Proo
0762879363 (whatsapp only)
Haleluya Haleluya!
Leo ninazungumza na wale walioupata ukuhani wa kifalme (royal priesthood). Kila aliyeokoka amefanyika kuhani. Miongoni mwa vitu muhimu kwa kuhani kwa habari ya mavazi (vestments) ya kuonesha yuko kamili katika priestly duty ilikuwa ni kujivika naivera(namna ilivyokuwa ikishonwa unaweza kuipata mtandaoni, au nione inbox nikutumie kuonekana kwake), pamoja na ile dirii ya hukumu iliyoweka mawe madogo (gemstones) mawili (Urimu na Thumimu ๐๐พIn Hebrew Lights & Colours ๐๐พGreen & Red) yaliyokuwa na alama ya *_Yes & No_* iliyosaidia kujua mapenzi ya Mungu ktk jambo husika. Lakini pia ilikuwa heshima kwa mfalme kuivaa ktk matukio ya furaha. Kwa ujumla wake ni kiashirio cha utayari wa kumwendea Mungu kwa majukumu ya kikuhani hasa kumkutanisha Mungu na situations unazohitaji *_Divine Intervention_*
Katika maisha ya hapa duniani, usipojua siri hii, kuna mambo Shetani ataku-oppress (kandamiza), yanaweza kuwa matatizo ambayo unafikiri ni ya kijamii tu, kumbe kuna mkono wa yule mwovu akifanya uonevu. Siri ambayo Bwana amenifundisha ni hii, kukitokea mambo magumu sana (toughest issues), Sio wakati wa kunyong'onyea na kulialia, huo ni wakati wako wa kujivika naivera na kumwendea Bwana. Present your case before the LORD, Ipeleke kwake maana hapo kuna ufalme upo unakinzana nawe. Sasa gonganisha hizo mamlaka mbili ili wewe uwe *_Out of Stress_* Hapa nazungumza zile ishu tafu sana, yaani zenye kuamua kati ya kufa au kupona, kupoteza kazi au kubaki nayo, kufukuzwa na mume au kubaki naye, kuachishwa masomo au kuendelea na zingine za namna hiyo. Ukikutwa na mambo ya namna hiyo, huo ndio wakati sasa wa kuitisha naivera kwa jinsi ya kiroho. UTANIELEWA HIVI PUNDE TU
Daudi alikutana na wakati mgumu sana, katika moja ya upinzani wa kivita dhidi ya Waamaleki. Hawa watu walivamia Negevi na Ziklagi, na huko waliuchoma mji wote wa Ziklagi, wakeze Daudi wote wawili ๐ฉ๐ป๐ง๐ฝyule Ahinoam Myezreeli na yule wa pili yaani Abigail mjane wa Nabali, wote walichukuliwa mateka, kumbuka waliochukuliwa mateka hawana ujanja kwa hiyo huenda hata Waamaleki wangeweza kuwaingilia kimwili. Sijaoa lakini najua tu mmmh ๐๐๐Mke amechukuliwa na wahuni, najua hapo moyo utachomwa๐ kama kwa moto ๐ฅ.
SASA KATIKA WAKATI KAMA HUO DAUDI ANARUDI, AKIDHANI ATAKUTANA NA FAMILIA YAKE ๐จ๐ฉ๐ง๐ฆ KUMBE HAKUNA KITU NA MJI UMECHOMWA WOTE. JE! UNAWEZA UKAWAZA ALIKUWAJE DAUDI, NAJUA UKIFIKA HOME ๐ก UKAAMBIWA MAJAMBAZI WALIVAMIA, WAMEPORA PESA, HAUTAMIA KAMA UKIAMBIWA WAMEMTEKA NA MKEO AU WAMEMNANILIU๐. SASA KUMBUKA PIA SAULI BIN KISHI, ALIKUWA AMEUA MAKUHANI WA BWANA WOTE HUKO NOBU, KWA KUWA ALIHISI WOTE WAKO UPANDE WA DAUDI NDIVYO ALIVYOMWAMBIA AHIMELEKI MWANA WA AHITUBU. LAKINI KUNA MWANA MMOJA WA HUYU KUHANI NAYE NI ABIATHARI, AMBAYE ALIKIMBILIA KWA DAUDI, ILA ALIKUMBUKA KUBEBA NAIVERA.
1 Samweli 30 : 7
*_Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko._*
DAUDI ALIPOITWAA NAIVERA NA KUJIVIKA AKAMPAMBANISHA MUNGU NA HIYO HALI NGUMU KUIBEBA KWA MISULI YA KIBINADAMU ๐ช๐พ. Mungu akampa _*Go Ahead*_ Na aliwafuatia na akarejeza kila kitu na kuwashinda kabisa kabisa!
Ndugu yangu mfuatiliaji, ziko zile hali ngumu ambazo zinataka kuamua mambo mawili tu, na unakuta option nyingine ni ya kukutoa kabisa kwa Mungu. Do not stress yourself jivike naivera na umwendee tu Mungu then relax tuu. Hilo ambalo ni gumu sana ukilibeba utatengeneza presha bure, utakuta swala limeisha halafu unaanza kuuguza presha ya kupanda na kushuka, kumbe kuna mambo uliyopaswa kumtwika Yesu, ukayabeba mwenyewe.
*_USHUHUDA_*
Miezi miwili baada ya kumaliza masomo yangu ya shahada ya kwanza, Nikapigiwa simu very urgent. Nikaitwa kwenye ofice ya Dean wa Kitivo, nikaelezwa kuwa nipo kwa hatari, ya kutoweza kuhitiimu masomo mwaka huo, na nitalazimika kuja mwaka mwingine kukamilisha kile ambacho kimekosekana kwenye database. Nilikuwa nasoma course ambayo nilikuwa ni mwanafunzi wa vitivo (faculties) mbili tofauti. Sasa taarifa ilitoka kitivo B kuja kitivo A, kuwa, *"Huyo mwanafunzi wenu hawezi kugraduate".* Ni kweli nikiwa semista ya mwisho, niligonganishiwa ratiba, ikanilazimu core-course fulani kuiacha ilikuwa na course-code (GE 305). Database ilipoonesha nimeiacha hiyo, walining'ang'ania kuwa *NOW WAY OUT*, lazima nirudi masomoni mwaka ujao, yaani somo moja linirudishe chuo, nilipe ada upya, nipange chumba sijui hostel, kwa ajili ya somo moja tu. Hao ni watu wa mataifa kwa hiyo they have got no mercy eti wanifikirie, No! Yuko Doctor mmoja wa kitivo A anaheshimiwa sana, Akaniambia nitahitajika kuja kwenye final senate meeting ya kuyajadili matokeo ya wahitimu. Akanitahdharisha kuwa weka documents zako sawa, ili ukijieleza na mimi nitatia uzito uachwe tu uweze kupata shahada yako. Wakati huo miaka mitatu ishachosha sana, kumbukeni yale mambo ya quizzes, assignments, tests, U.Es kwa wingi bila kusahau modules na pamphlets kibao ulizokuwa ukikesha kusoma, leo hii unaambiwa hautavuna kitu! Sasa Mungu alitaka kunipa darasa la nisimtegemee mwanadamu, Senate ilikuwa inakutana Jumatatu lakini siku mbili kabla yule Doctor mteteaji wangu akapata safari akaenda Nigeria kulikuwa na Synod Summit fulani huko. Kwa hiyo sasa nikabaki mwenyewe na wale ambao wamekomaa kuwa huyu lazima arudi chuo mwakani ๐ก๐ก๐ก. Tena kuondoka kwa yule Doctor kukaondoa hata nafasi ya mimi kuitwa nijitetee, wakabaki maadui peke yao waamua hatma yangu. Usiku huo nilipanga nikalale kanisani, ili nimlilie Mungu kabla ya Senate. Lakini ndipo nilipokumbuka kuwa, hiyo ishu nzito sio ya kuibeba mwenyewe, moyo wangu utayeyuka na nitamkosea Mungu. Nikachukua kipande cha karatasi nikalisti majina ya wakuu wote wa vitengo vinavyohusu tatizo langu, niliandika jina la kwanza la Dean of Faculty Doctor fulani mzungu, nikafuatia maassociates wote. Nikachukua hilo karatasi nikafunua kwenye ukurasa fulani wa Biblia ambapo ndipo kuna ahadi ya Mungu niliyoibeba wakati huo. Mungu alisema hatatulia wala hatanyamaza (Isaya 62:1ff), Nyuma yake nikaandika sentensi hii *"Mungu niliyekutumikia nikiwa hapa chuoni, nataka nikuone katika hili"*. Baada ya hapo nikawa nime-relax ๐, nikiamka asubuhi naenda zangu kanisani kupiga Keyboard ๐น. Nikapigiwa simu na mhadhiri fulani, ambaye ni raia wa Uganda na ndiye aliyenikomalia sana kwamba lazima nirudi kusoma. Akaniambia Hellow, Sasa tumekubaliana kuwa wewe tukuache u-graduate, Sisi hatuna mamlaka ya kukuamria uhitimu au usihitimu ila hao watu wa hicho kitivo A wakikubali basi, Ikumbukwe kitivo A ndicho kilikuwa na wateteaji wangu, basi hata sikusumbuka tena.Na ikumbukwe hapo kuwa Mungu aliingilia kati kile kikao cha ile Senate, hawakuipa nafasi Prospectus ili nikatwe (nitumbuliwe) ✂๐. Miezi mitatu badae kukawa na Graduation, kila mtu alikuwa anafurahi akiliona jina lake kwenye kitabu cha wahitimu halali, Nami nilipochungulia jina langu likawepo kama mhitimu halali.
SASA JIFUNZE SIRI HII, KATIKA MAMBO MAKUBWA MAGUMU, NI MAHALI SAHIHI YA KUITISHA _*NILETEE NAIVERA*_ ILI UMLINGANE BWANA KAMA YABESI, UONE ATAKALOTENDA BWANA. UKILIVUKA KWA KUSHINDA HILO GUMU, UTAPANDISHWA DARAJA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO. UKIANZA KUPANIC NA KULIALIA KUTAFUTA UONEWE HURUMA, UTAMPA NAFASI SHETANI AKUFANYIE *TORTURING* ZAIDI, NAWE UTABAKI KAMA MTU DHAIFU KATIKA ROHO. HALELUYA ✋๐พ
Mwl Proo
0762879363 (Whatsapp)
0718922662(calls/texts)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment