Sunday, November 12, 2017

LO! HIS PRESENCE IS SO SWEET

*LO, HIS PRESENCE IS SO SWEET 😋*

*_Uwepo wake mtamu mno_*

```Na Mwl Proo```
0762879363(whatsapp#)

©2016

Haleluya!!

Leo nazungumza na watu wa chumba cha ndani _*(inner room)*_, wale ambao hawana desturi za kuingia chumba chao ndani nitawatia wivu waanze (1Falme 6:21,Math 6:6). Kuna wakristo ambao, daima wanakaa ua wa nje hawaingii ndani! Hawajajua haswa utamu wa uwepo wa Mungu. Hold on!✋🏾Kuna kitu kipya cha kujifunza usiwaze kile ulichozoea.

BWANA ILI ANISHIKE MOYO WANGU, ALINIONJESHA UTAMU WA UWEPO WAKE. PAMOJA NA UKWELI WA KWAMBA NILIJAZWA ROHO MTAKATIFU KWA NGUVU SANA SIKU NILIPOAMINI, THAT IS NOT ALL ABOUT HIS PRESENCE! MUNGU NI HALISI NA UWEPO WAKE NI HALISI, NA ANATAMANI KUKUTEMBELEA KIBINAFSI LAKINI HAJAPATA NAFASI AMBAYO WEWE UNAUTULIZA MOYO WAKO KWAKE (1Yoh 3:19) MUDA WA KUTOSHA.
NAKUMBUKA WAKATI FULANI MWAKA 2005 KIU YA UWEPO ILINIINGIA, NA NILITAMANI SANA KUUONA UWEPO WA MUNGU KWA WAZI MAANA NILIKOSA SABABU YA KUMFANYA MUNGU AWE MBALI. NIKAWA NA SHAUKU KWAMBA MUNGU HIVI ULE UWEPO WAKO AMBAO ULIKUWA UKIMTOKEA MUSA MLIMA HOREBU/SINAI UKAWA UNAMFANYA ANAKAA HUKU HATA SIKU 40 HATAKI KUBANDUKA UMEENDA WAPI? NI KWELI NIISHIE KUNENA KWA LUGHA NA HAKA KAUWEPO KADOGO KA UVUVIO IWE BASI, JE KWANI MUNGU UKINITEMBELEA SITAJUA? (SWALA KWAMBA MUNGU ANAFANYA MAKAO NDANI YETU LIMEZINGATIWA). SASA SIKU HIYO MUNGU ALIMTUMIA MAMA MMOJA (WA CHUMBA CHA NDANI), KUNENA HABARI ZANGU AKANIELEZA HALI YANGU YA KIROHO, NAMI NIKAKUBALI. USIKU WA SAA NNE TUKIWA TUNASOMA (NIKIWA PUGU SECONDARY SCHOOL) UMEME UKAKATIKA. KUKAWA NA FUJO ZA WANAFUNZI KURUDI MABWENINI KULALA NA KULIKUWA NA GIZA TOTORO. NIKIWA NAMI NAELEKEA BWENINI MOYONI LIKAINGIA WAZO HIVI KWA NINI NISIRUDI DARASANI NIKAOMBE NIUENJOI UWEPO WA MUNGU. THAT WAS MY FIRST DAY KUTEMBELEWA, KWENYE UWEPO WA MUNGU HUTASIKIA HOFU, WALA HUTAKUMBUKA MAMBO MENGINE. NIKATAFUTA DARASA LILILO WAZI NIKAINGIA, NILIJITAHIDI KUMKWEPA MLINZI ALIYEKUWA NA TOCHI🔦ASIWAZE KUWA KUNA MWANAFUNZI KARUDI MADARASANI KWENYE GIZA KALI SANA. NIKABANA KWENYE KONA YA DARASA, NIKAANZA KUMSHUKURU MUNGU KWA UZURI WA UTAKATIFU, NILITUMIA TU SAUTI YA CHINI NA MANENO MENGINE NILITAMKA MOYONI,  WAKATI NAMSHUKURU HATA KWA KUMTUMIA MTU MWINGINE KUNIONYA (UFU 3:19), HALI NIMETULIA KIMYA, NGUVU YA MUNGU ILIANZA KUSHUKA KWA NAMNA YA AJABU, NILIHISI MOTO 🔥 UMENIDONDOKEA MGONGONI, UNAANZA KUSAMBAA NA NGUVU  NYINGINE IMEKAMATA MWILI WOTE (NIKAWA OUT OF MY CONTROL), MOYO WANGU UKAWA UNASIKIA KUMWABUDU MUNGU KWA MANENO YALIYOTUKUKA, PAMOJA NA KWAMBA HUO MOTO🔥 KUWA NA JOTO KALI LAKINI HAUKUNILETEA KUTESEKA ILA NILIHISI RAHA YA KIMUNGU ISIYO YA KAWAIDA, NIKITAMANI ISINIACHIE. NIKAWA NAOGOPA HATA KUSOGEZA MGUU PEMBENI NIKIHISI HUENDA NIKAUKATA HUO UWEPO. LAKINI ILE NGUVU IKAWA IMEKAMATA MWILI WOTE NIKAIHISI IMEKAMATA UBONGO WANGU MAANA NILIUHISI UBONGO UMESHIKWA NA GANZI KALI, MWILI WANGU ULIINAMISWA KAMA NAANGUKA BILA KUSHIKILIWA NA CHOCHOTE LAKINI SIKUANGUKA BALI NI KAMA NILIKUWA NAELEA. SIJUI NILITUMIA MUDA GANI KTK UWEPO HUO, NA SIJUI MUNGU ALIFANYA NINI JUU YANGU HASA, LAKINI MAISHA YANGU YALIPATA SURA TOFAUTI. NA NILIPOONA UWEPO ULE UMEKATA, NIKAWA NASIKIA KUMFURAHIA MUNGU SANAAA. NIKAWA NARUDI BWENINI NAHISI UJASIRI WA KIMUNGU MKUU, NATAMANI HATA NIKUTANE NA ♿WANAOTUMIA WHEELCHAIRS ILI NIWAINUE TOKA KTK UWETE. NA BAADA YA HAPO SASA NIKAWA PAMOJA NA MAOMBI YALE YA PAMOJA, NILIPENDA KUTAFUTA MASAA YANGU BINAFSI ILI NIOMBE NA KUUENJOI UWEPO WA MUNGU.

Sitengenezi fundisho la watu la uwe na maombi ya jinsi rasmi, Lakini pia usiklemu maombi yako ya kukemea wakuu wa giza na majeshi ya pepo kila uombapo. Uweponi mwa Mungu ni kutamu, na hao maadui unaoshughulikia hawaji huko. Lakini pia sikupi hili ili uklemu style ya uwepo wa Mungu, maana shetani akijua mmeunda fundisho kwa hiyo experience ya mtu fulani, atatengeneza  kitu feki (Counterfeit) 2Kor 11:14, Ili kupoteza watu, kumbuka ukiwa ktk uwepo huo unachoambiwa utatendea kazi kuliko mahubiri yote uliyowahi kusikia. Mimi baada ya hapo nikawa nikitamani uwepo wa Mungu nilikuwa naenda mbele za Bwana mpaka aniguse, na hapo sasa sikuwa na ratiba ya muda, ni mpaka BWANA aniguse. *_TAHADHARI_*
Huko mbele Shetani aliwahi kuja kufanyia uwepo bandia, Lakini Mungu akanipa kujua kanuni za uwepo wake. Shetani aliwahi iga kitu cha jinsi hiyo, lakini moyoni kulikuwa kunapata shida, kwanza uwepo ulikuja hata bila kuukaribisha, halafu umeshuka kwenye ibada, ibada yote naiona kame, huku nawaza iishe fasta nikalale moja kwa moja. Mungu akanijulisha kuwa huo ni uvamizi, so nikatafuta wanamaombi wanaofahamu vita ya rohoni *(Jitahidi upate article yangu inayoitwa VITA VYA ROHONI)* Tukaenda usiku huohuo kwenye kuwanja cha Basketball tukafanya vita kama Saa moja hivi, kukawa na shwari kuu. Na mipango yote iliyoletwa na uke uwepo feki ikasambaratika.
Lakini tangu hapo nikawa mtu wa chumba cha ndani, natamani zaidi uwepo wa Mungu kuliko chochote, NIKAANZA KUPENDA VITU VINAVYONIWEKA KARIBU NA UWEPO WA MUNGU, NIKAANZA KUPENDA NYIMBO ZA TARATIBU ZENYE MANENO YA KUABUDU (WENGI HUZIITA NYIMBO ZA KUABUDU), HIYO IMEKUWA TABIA YA MAISHA YANGU YOTE. HAPA NINAANDIKA UJUMBE UJUMBE WA USHUHUDA HUU NIKIWA NASIKILIZA NYIMBO HIZO ZA KUABUDU TANGU SAA TISA USIKU MPAKA HII ALFAJIRI, NA ILE KIU ILIFANYA NIZITAFUTE KWA GHARAMA YOYOTE MAANA KWA MIAKA KARIBIA MINNE NILIKUWA NALALA NA REDIO KUBWA KITANDANI📻🛌, ILIPOFIKIA WAKATI ZILE STESHENI ZIKAPUNGUZA KUPIGA NYIMBO ZA KUABUDU USIKU WA MANANE, NILIENDA KUOMBA  WANIUZIE NYIMBO NYIMBO ZA KUABUDU. KWA HIYO NIKAMFUATA MTANGAZAJI NIKIWA NA FLASH DISK MAALUM, LAKINI SIKUPEWA BURE NILILIPA PESA.   WANAONIFAHAMU WATAJUA HILI KILA NINAPOISHI NINAFANYA KWA NAMNA YOYOTE NYIMBO ZA KUABUDU ZI-PLAY ALL NIGHTLONG, KWA NINI ZILINIKAMATA, NI KULE KUNIRAHISISHIA (LUBRICATION) KUUINGIA UWEPO MAANA BADO TUPO KWENYE DUNIA YENYE MASUMBUFU MENGI AMBAYO YANACHOSHA NAFSI. NA HAPO NDIPO WENGINE WALIHISI NAFANYA MAIGIZO, MAANA NILIPORUDI LIKIZO NYUMBANI KWA MARA YA KWANA NIKAGUNDUA PAMOJA NA UPENZI WANGU KWA SOCCER⚽ ILA KIU IMEKATWA NA ULE UWEPO, SWALA LA KUKESHA KUANGALIA UEFA-CHAMPIONS LEAGUE LIKAWA HAPANA KWA KWELI, MAANA KWANZA NIMETEGA ALARM CLOCK⏰ SAA SABA KUOMBA NIKIUKUMBUKA UTAMU WA ULE UWEPO, NASAME UEFA-LEAGUES POLE SANA I CANNOT GO WITH YOU TENA. NDIVYO KWA NAMNA HIYO HIYO TU HUU MWAKA WA 11 SIJAWAHI KUFUATILIA MECHI YOYOTE YA MPIRA SIO KWAMBA NI DHAMBI NO!  KUNA MAUTAMU HUKU NDANI KWA MUNGU AISEE. KUNA SIKU AMBAYO NILISINZIA NIKIWA UWEPONI HATA NDOTO NILIYOOTA NILIAMKA NACHEKA KWA FURAHA 😅😅, YAANI NILIONA NDOTONI NASOMA KITABU CHA EZEKIEL, LAKINI KILA UKURASA NINAO USOMA NAONA NA VITI HALISI VILIKUAJE, YAANI NAONA NYUSO ZAO ZILIONEKANAJE  HATA VYOMBO VYA UDONGO NA MATERIALS NYINGINE, NIKASHTUKA NASIKIA RAHA KWELIKWELI. NILIKUWA MPENZI WA TAMTHILIA/+MAIGIZO ZINAZOVUMA SANA NYAKATI HIZI, ILA KWA KUWA NAZO NILIZIONA *THEIR MAIN THEME* NI MAPENZI, NIKAONA HIZI ZITANIKATISHA UTAMU WA UWEPO WA MUNGU, NAZO ZILIYEYUSHWA NILITAZAMA TAMTHILIA YA MWISHO ILIITWA *_LA MUJER DE MI VIDA_* MWAKA 2005 MWANZONI KAMA SIKOSEI IKAWA NDIO MWISHO KABISA, SIKUWAHI KUTOA MUDA WANGU HATA NUSU SAA KUFUATILIA TENA HIZO VITU, KWA HIYO BAADAE NILIKUWA NIKISIKIA TU MAJINA, LAKINI MIMI UWEPO WA MUNGU ULE UNAOKUJA VIVIDLY&TANGIBLY ULINIVUTIA KULIKO VYOTE, NIKAHESABU VITU VYOTE NILIVYO VIPENDA MWANZO KUWA *RUBISH* ILI NIPATE KRISTO.

TUJIFUNZE MANENO YA WALIOJIZOEZA KUKAA UWEPONI WANASEMAJE??

Zaburi 27 : 4
_*Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.*_

Zaburi 42 : 2
_*Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?*_

HUYU ANAYEONGEA NI MFALME AMBAE HANA SHIDA ZA UGALI🍚 KAMA WEWE LAKINI ALITAMBUA UTAMU WA UWEPO WA MUNGU, NDIO MAANA SHAUKU NA KIU YAKE KWA MUNGU HAIKUWA NDOGO (ZABURI 84:10) ANATAMANI AWEPO TUU HEMANI MWA BWANA ILI AUENJOI UWEPO WA MUNGU.

NB:-
_*NEVER LET THE CARES OF LIFE, ROB YOUR CHANCE TO ENJOY GOD'S PRESENCE*_

AKINA MUSA WENZETU WALIONA BILA UWEPO WA MUNGU NO ,HATUWEZI ENDELEA (BILA UWEPO WAKO KWENDA NASI, USITUCHUKUE TOKA HAPA)! KUTOKA 33:15  LAKINI AJABU LEO UNAKUBALI KUENDELEA NA MAMBO YAKO BILA UWEPO WAKE

MIONGONI MWA MAMBO UTAENJOY UKIJIZOEZA KUKAA UWEPONI MWAKE NI,
✝KUZIJUA SIRI ZAKE (ZABURI 25:14) , UTAKUWA UMEFURIKA SIRI NZINGI ZA KIMUNGU. HUWEZI KUWA NA TAARIFA NYINGI ZA DONALD TRUMP KULIKO ZA MUNGU HATA KAMA HIYO HABARI KWA SASA NDIO *_HOT NEWS_* KWENYE MEDIA, WEWE UTAJAA TAARIFA ZA MUNGU KULIKO HIZO.

✝UTAKUWA NA FURAHA ISIYOELEZEKA, THE TRUE JOY AMBAYO HAIJATOKANA NA MAMBO YANAYOENDLEA KWENYE MAISHA, MAANA UWEPONI MWAKE KUNA UKAMILIFU WA FURAHA (_In thy presence, is fullness of joy Zaburi 16:11)

UWEPO WANGU UTAKUPA KUTUMIA MUDA MWINGI MBELE ZA MUNGU BILA KUCHOKA. NAKUMBUKA ZAMA ZA NEHEMIA ☺

Nehemiah 9 : 3
_*Basi wakasimama mahali pao, wakasoma katika kitabu cha torati ya Bwana, Mungu wao, muda wa robo ya siku; na robo nyingine wakaungama, wakamwabudu Bwana, Mungu wao.*_

HAWA WATU WANATUMIA MASAA SITA KUSOMA TU NENO, THEN WAKIUNGAMA NA KUABUDU KWA MASAA MENGINE 6, THEY SPENT 12HOURS TIRELESSLY!

SASA NIKUSIHI NDUGU MPENDWA CHAGUA FUNGU JEMA, LA KUKAA UWEPONI MWA MUNGU, KUMBUKA MUNGU ANAKUWA NA WEWE UNAPOKUWA NAYE (2Nyak 15:2)
KAMA UNATAMANI KUWA NEW LIFESTYLE, FRIENDLY TO GOD'S PRESENCE MUNGU AKUSAIDIE.
UKIHITAJI NYIMBO ZA TARATIBU NITAFUTE UKIWA FLASH DISK/ SD-CARD/ EXTERNAL HARD DISC NTAKUPEA NYIMBO ELFU TANO NA MIA NNE (5,400) ZA KUABUDU BURE KABISA, TENA SIO KIINGLISH TU UKASEMA HUELEWI, ZA KISWAHILI ZA KUABUDU KWA 70% YA HIZO.

*~TOO MUCH OF GOD IN YOU, PUSHES THE WORLD AFAR, AND TOO MUCH OF THE WORLD IN YOU KEEPS HIS PRESENCE AWAY FROM YOU~*

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment