🇦 🇱 🇱 🇹 🇷 🇺 🇹 🇭
*HAKUMTAFUTA BWANA*
*_Mwl Proo_*
0718922662
BWANA Yesu awabariki nyote
Ninaomba tuanze kuangalia mstari huu
*2 Mambo ya Nyakati 16 : 12*
*_Akashikwa Asa na ugonjwa wa miguu katika mwaka wa thelathini na kenda wa kumiliki kwake; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini HAKUMTAFUTA BWANA katika ugonjwa wake, bali waganga._*
Katika mstari huu,baada ya ripoti ya ugonjwa wa Mfalme Asa,kuna maneno haya,"lakini hakumtafuta Bwana bali waganga". Ikumbukwe Neno la Mungu linatujulisha nia na mawazo ya Mungu ktk kila jambo,njia nyepesi ya kumsikia Mungu ni kwa sauti ya Neno lake (Hata muda umevurugwa na sauti nyingi za manabii wa kileo,rudi ktk kuisikia sauti ya neno lake (Zab 103 : 20)
*Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.*
Sasa ktk hiyo habari ya Asa tunaona nia/wazo la Mungu lilikuwa ktk ugonjwa Asa amtafute BWANA. Lakini ktk matazamio hayo ya Mungu akashangaa kuona jamaa anakesha kwa sangoma tuu.
Ndugu wapendwa zaidi ya ukweli kwamba Mungu ni mwenye wivu(Kumbu 4:24,Ebr 12:29) Lakini Mungu jina lake ni *Mwenye wivu* His name is the Jealous One
*Kutoka 34 : 14*
*Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu.*
Tutazame mifano miwili zaidi ya wale ambao ya Mungu aliwatazamia wamtafute yeye ila wakatafuta msaada pengine
>Mfalme Ahazi
*2 Mambo ya Nyakati 28 : 22*
*_Na wakati alipofadhaishwa, akazidi kumwasi Bwana, huyo mfalme Ahazi._*
>Mfalme Ahazia
*2Wafalme 1*
*2 Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu.*
*3 Lakini malaika wa BWANA akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni?*
*4 Basi sasa, BWANA asema hivi, Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. Eliya akaondoka.*
MUNGU NI MWENYE WEMA/UPENDO WOTE (OMNIBENEVOLENT GOD) MARA KADHAA ANAWEZA KUONGEZA PRESHA KWENYE MATATIZO AKIWA NA NIA YA KUKUVUTA KWAKE,MAANA AWAPENDAO ANAWAONYA NA KUWARUDI(Ufu 3:19) , SASA WENGI PRESHA IKIONGEZWA BADALA YA KUMTAFUTA BWANA WANATOKA KABISA NA KUVUKA REDLINE. AHAZI MFALME HAKUWA VIZURO NA MUNGU WA BABA ZAKE,SASA BWANA MUNGU WA ISRAEL AKAONGEZA PRESHA YA FADHAA,ILI LABDA YUMKINI ATATAFUTA MSAADA KWA MUNGU,LAKINI TUNASOMA ALIPOFADHAISHWA AKAZIDI KUMWASI BWANA
PIA TUNASOMA KUHUSU AHAZIA,ALIPATA AJALI YA KUANGUKA GHOROFANI🏣 SASA MUNGU ALITAZAMIA LABDA ATAMHITAJI KTK HILO JANGA,BADALA YAKE AKAKUMBUKA KUWA KUNA KA-mungu KAITWAKO Baal-zebubu HUKO Ekron BASI AKATUMA ETI KUULIZA HABARI ZA SHIDA YAKE,SASA MUNGU MWENYE WIVU ILIMUUMA HIYO
*MUNGU ANAJUA KTK MAISHA YAKO YAKO MAMBO MAGUMU,ZIKO SHIDA NZITO,YAKO MASWALI MAGUMU HAYO NI MTAJI WAKE WA KUKUPATA MOYO WAKO,NA HIVYO ANATAZAMIA WAKATI WOTE UATAENDA KUULIZA KWAKE*
*Yeremia 2 : 8*
*Makuhani hawakusema, Yuko wapi Bwana? Wala wana-sheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.*
*Yeremia 10 : 21*
*Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa Bwana; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika.*
*Hosea 7 : 10*
*Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote.*
*Isaya 30 : 2*
*waendao kutelemkia Misri wala hawakuuliza kinywani mwangu; ili wajitie nguvu kwa nguvu za Farao, na kutumainia kivuli cha Misri.*
KATIKA MAISHA YAKO KUNA WEZA KUWA NA UDHAIFU AU KUTINDIKIWA,MAUMIVU,UGONJWA MMBAYA SIO KIASHIRIA CHA UKATILI WA MUNGU ILA HALI ZA NAMNA HIYO ZIMERUHUSIWA ILI UMTAFUTE BWANA, BWANA ANAUTAKA MOYO WAKO TU
Tusome hapa
*Amosi 4*
6 Mimi nami nimewapa usafi wa meno katika miji yenu yote, na kutindikiwa na mkate mahali penu pote; *lakini hamkunirudia mimi*, asema BWANA.
7 Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikatika.
8 Basi kutoka miji miwili mitatu walitanga-tanga kuendea mji mwingine wapate kunywa maji, wasipate ya kuwatosha; *lakini hamkunirudia mimi*, asema BWANA.
9 Nami nimewapiga kwa ukavu na koga; wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu; *Lakini hamkunirudia* mimi, asema BWANA.
10 Nimewapelekea tauni, kama tauni ya Misri; vijana wenu nimewaua kwa upanga, na farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa matuo yenu na kuuingiza katika mianzi ya pua zenu; lakini *hamkunirudia mimi,* asema BWANA.
11 Baadhi yenu nimewaangamiza, kama hapo Mungu alipoiangamiza Sodoma na Gomora, nanyi mkawa kama kinga kilichonyakuliwa motoni; lakini *hamkunirudia mimi,* asema BWANA.
SASA TUFANYE REFLECTION KTK MAISHA YETU,HUWA TUNATAFUTA WAPI MSAADA? MAANA MUNGU KUNA MAMBO ANAYAONA YANAKUJIA KWENYE AFYA YAKO (ANAJUA HUU UGONJWA NI SIZE YAKE) ANAPOKUTAZAMIA UTAMWITA ANAKUKUTA KWA MCHAWI WA ENDORI😈 NA MAHALA PENGINEPO(YOU, NAME IT)
⭕NY🚫
*~(kama umekwisha mpa Yesu maisha,usijaribu kamwe kwenda kwa mganga wa kienyeji,NEVER TRY‼,katika ulimwengu wa roho kuna kitu mfano wa ID card ulivikwa ulipoamini,wao wa ufalme wa giza wanaiona kule,isije ukasema tulienda ili tu tumjue mwizi aliyetuibia,kaulize kwa Bwana au potezea,NI HATARI📛☠⚰)~*
KUNA PRESHA IMEONGEZWA KWENYE KAMPUNI YAKO YOU ONLY COUNT ON LOSSES,PRESHA IMEONGEZWA KWENYE DUKA LAKO KUBWA PALE KARIAKOO,MUNGU ANAWATUMIA TRA KUKUBANA NA KUONGEZA MKANDAMIZO(PRESHA) ILI UPATE MWANYA WA KUMWITA BWANA YAANI UMTAFUTE USO WAKE,BADALA YA HUO MKANDAMIZO KUKUSAIDIA KUMTAFUTA BWANA,UNAFANYA MBINU ZA KUWALAGHAI MAAFISA WA TRA HATA UNAZIDI KUMKOSA MUNGU,AMERUHUSU KONTENA YAKO IKWAME BANDARINI ILI UPATE KUMTAFUTA JUU YA HILO,MAANA ANAJUA UKIMTAFUTA JUU YA SHIDA YAKO,SIO TU UTAPATA JIBU LA TATIZO LAKO BALI UTAPATA NA MAMBO AMBAYO HUKUJUA KUWA UNAYAHITAJI NA NI YA MUHIMU KULIKO HAYO UNAHITAJI ,HII NDIO KWELI UKIWA UNAMTAFUTA BWANA KWA AJILI HITAJI LOLOTE,IWE NI KUKOSA MTOTO NA UNA MIAKA MITANO YA NDOA,HUTAPOKEA TUU MTOTO ILA UTAJULISHWA NA KUPOKEA MAMBO MAKUBWA,MAGUMU YA UFALME. DANIEL ALIPOTIA MOYO WAKE UFAHAMU BAADA YA KUSOMA MAGOMBO YA YEREMIA ALIGUNDUA MUDA WA KUKAA UTUMWANI UMEMALIZIKA,LAKINI ALIPOMTAFUTA BWANA JUU SHIDA HIYO,MALAIKA ALILETA "FULL HEAVENLY PACKAGE" AKALETEWA MAFUNUO YA MAMBO AMBAYO HAKUWAHI KUWAZA WALA KUOMBA(Efes 3:20) JE! ULIGUNDUA KUWA ULIPATA DIVISHENI ZERO ILI BWANA APATE NAFASI MOYONI MWAKO? JE UNAJUA KUWA KUWA ILE DISCONTINUE(DISCO) YA CHUONI ILIKUWA NI SAUTI YA KUKUVUTA MOYO KWA MUNGU,ULIPOKUTA BARUA OFISINI KWAKO KUWA KIBARUA KIMEOTA NYASI ULICHUKUA HATUA ZIPI? MKO AMBAO MLITUMIA MIANYA HIYO MKATOA RUSHWA ZA PESA/NGONO ETC IN ORDER TO RETAIN WHAT WAS ABOUT TO BE LOST.
NA HIKI NDICHO KILE KIZAZI KISICHOJITENGENEZA MIOYO KWA BWANA,WAKIFADHAISHWA WANAONGEZA UASI
*Zaburi 78 : 8*
*Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.*
WATU WENGI LEO WAMEKUWA WAPIGA DILI,WATOA RUSHWA WAZOEFU,WAMEJAA VIPATO VYA UDHALIMU MAANA WALIPOWEKEWA BARRIERS ILI WAMTAFUTE MUNGU,WAKAGOMA! SO OFTEN TIME WATU WANASAKA godfathers WAKUWAUNGANISHIA AMBAO WENGI WANAWAKOSESHA KWANZA,WADADA AMBAO WAPO KAZINI ILA WALIUFUNUA UTUPU👙 WAO KWANZA ILI JINA LAKE LIPITE NI WENGI MNO HAPA TOWN(TENA WAKIWA WAMEOKOKA),UKIONA MWANAMKE UNA MIAKA 35 NA BADO HAUONI DALILI ZA 💍💏💍 USIJIRAHISISHE KWA SHETANI,HIYO NI FURSA YAKO NZURI YA KUMTAFUTA BWANA,MAANA SIO UTAPATA FAMILIA PEKEE NA MENGINE MENGI AMBAYO MUNGU ANAKUWAZIA ILA UPO NJE YA POSITION NA HAUJASTAHILI KUYAPOKEA BADO,ILA UKIMTAFUTA BWANA. NDUGU ZANGU KTK KRISTO HAKUNA SABABU YA KUISHI NA FORGERIES AMBAZO ZITAKUHARIA NA MAISHA YAKO YA UMILELE,WENGI AMBAO WATAIKOSA MBINGU WAKIWA KULE KWINGINE (JAHANAM 🌊👉🏾🔥) WATAKUWA NA UCHUNGU MKUU HUKU WAKIJUA KWA HAKIKA KUWA *_"SIKUPASWA KUWEPO HUKU MIMI"_* ILA ATAKUMBUKA ISSUES ALIZOZIPUUZIA AKIWA DUNIANI. SASA TAMBUA ZIKIJA HALI NGUMU ZA KUKUKOSESHA (Mathayo 18:7-8) ZITUMIE HIZO HIZO KUMLINGANA BWANA MUNGU. HUU NDIO WAKATI WA KUMTAFUTA BWANA,USIWE KAMA WALE WALIOLEWESHWA NA ULIMWENGU,TANGU AFUNDISHWE UJASILIAMALI NDIO IMEKUWA NONGWA HANA NAFASI YA MUNGU,KAMA MUNGU AMEKUJALIA UNAMILIKI *A MULTI-BILLION COMPANY, THAT IS NOT OVER ABOUT LIFE,IT IS TRUE THAT YOUR INCOME IS MORE THAN REQUIREMENTS LAKINI THERE IS A SINGLE SECOND WITHIN A MINUTE⏰ YOUR HEART WILL STOP AND YOUR BREATH WILL CEASE,AND YOU WILL HAVE A JOURNEY TO THE WAY OF NO RETURN,IN THE FULL KNOWLEDGE NDIPO UTAKAPOJUA KUWA PAMOJA NA MASTER'S DEGREE KTK UHANDISI ULIPASWA KUMTAFUTA BWANA,KWA WAKATI HUO,ITAKUWA TOO LATE* KWA SASA HAUJACHELEWA,USIWE MIONGONI MWA WANAOKUFA KAMA WAFAVYO WAPUMBAVU KWA KUTOMTAFUTA BWANA....THIS IS THE TIME AND THE HOUR
*Hosea 10 : 12*
*Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.*
Mungu awatie nguvu nyote
Mwl Proo
0762879363 (whatsapp only)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment