Thursday, November 30, 2017

YUSUFU WA ARIMATHAYA

*KUHUSU YUSUFU ARIMATHAYA*

By Mwl Proo

©2017

Mtu huyu mwenyeji wa Arimathaya, ametajwa katika injili zote nne. Math 27:57, Mark 15:43, Luka 23:51, Yoh 19:38. Habari zake hazijaelezwa sana katika Biblia, maana Biblia haikueleza kila kitu. Kumbuka hili, theologically; *_The Bible does not contain all things, but it contains all things necessary for salvation._*  Hivyo habari za ziada kuhusu mambo mengine, ziko katika vitabu vingine, kwa mfano stories kumhusu Yusufu huyu ziko zaidi katika kitabu cha matendo ya Pilato (Acts of Pilate) na Injili ya Nikodemu. Yaani habari zote zipo katika Apocryphal+Non-canonical references. Huyu ndiye aliye-donate sehemu ya kuzikwa Bwana, inaelezwa na wanahistoria wa karne ya tatu, kuwa alifia Glastonbury, United Kingdom. Mjadala mzito wa kithiolojia ni juu ya swala moja, Je yeye ndiye aliyeifikisha injili Uingereza, wako wanaodai kuna mitume waliahajenga kanisa kabla yake.

Katika injili ya Nikodemu, imeeleza mgogoro wake na Nikodemu. Ingawa Nikodemu alimsaidia kuuomba mwili wa Bwana kwa Pilato, lakini alipoenda kuuzika kwenye makaburi yake kukawa na mzozo. Yusufu alijitahidi kutafuta suluhu na Nikodemu, lakini mgogoro ukawafikia wazee wa kiyahudi, ambao walimkamata na kumtupa gerezani huyu Yusufu. Alifungwa gerezani wakalitia makufuli kibaoπŸ”’πŸ”πŸ”’πŸ”πŸ”’πŸ” pande zote nne za gereza wakalilinda salama. Walipomtia gerezani alikwiasha waambia kuwa Yesu mliyemuua, atanitoa, na mabaya yenu yatawarudia. Walipoamka asubuhi kwenda gerezani, walilikuta limefungwa vizuri lakini Yusufu hakuwepo. Wakapata taarifa yuko kitaa huko Arimathaya. Wakatuma barua✉ ya kuomba radhi, wakimtaka waende awaeleze alitokaje?? Wazee wa kiyahudi walienda wakiwemo makuhani Caiphas na Annas. Akawasimulia kuwa akiwa amesimama katikati ya gereza anaomba usiku, kukatakea mwangaπŸ’₯akaanguka, mtu huyu alimsimamisha.. Na akamwagia maji toka utosini mpaka miguuni, akamwekea harufu ya manukato. Akambusu na kumwambia usiogope, amani iwe kwako. Yusufu akamuuliza wewe ni Eliya Nabii?? Akamwambia fumbua macho, mimi ni Yesu ambaye uliuhifadhi mwili wangu. Yesu akamchukua na kumwonesha mahali pale alipomlaza ⚰, kisha akamtoa gerezani akamsimamisha katikati ya nyumba yake huko Arimathaya akamwonya kwa siku arobaini usitoke huku Arimathaya, akamnyanyua na kumweka kutandani, yaani toka gerezani asubuhi alihamka home kwake πŸ‘πŸ›Œ. Walipomwita wale wazee wa kiyahudi mbele ya makuhani, Yusufu alisimulia kila kitu.  Akawaeleza kuwa Yesu alimjia kumtoa gerezani, lakini pia akaeleza kuwa Yesu alipofufuka, kuna watu walifufuka pia alieleza kitu chenye kulenga (Math 27:52-53) ingawa hiyo tunajua waliofufuka waliondolewa na kuuingia mji mtakatifu, maana ufufuo wa wakti ule uitwao  *ANABIOSKOMAI*, Ulihusisha kuzihamisha roho toka Sheol kwenda Gan Aden, kama nilivyoelekeza katika somo langu la *UMILELE*. Lakini yeye alieleza juu ya waliofufuka wachache na wamendelea kuishi duniani, kipekee aliwataja CHARINUS na LENTHIUS, watoto wa yule SIMEONI wa Luka 2:25-35. Makuhani na wazee wa kiyahudi walifunga safari kwenda Arimathaya ili kuhojiana na watoto wa Simeoni waliofufuka katika ufufuo wa Yesu. And the story is completely interesting aisee...
NB:-
Vitabu kutokuwa katika list ya vile Canonical, haivifanyi kuwa vya uongo, bali katika vile vigezo vinne vya CANONIZATION kili-fail, kama nilivyoeleza katika somo langu la *JINSI YA KUITHIBITISHA BIBLIA KUWA NI YA KWELI*.

Barikiwa sana....

Mwl Proo
0762879363

MUHTASARI WA HISTORIA YA KANISA

*MUHTASARI WA HISTORIA YA KANISA, TANGU MWAKA 34AD MPAKA 1600AD*

_Msimuliaji na mueleweshaji wako_
*Mwl Proo*
0762879363

Bwana Yesu asifiwe sana!.

*Tukijua tunapotoka, ni rahisi kushughulika na mambo yote ya sasa bila makosa....*

Leo tutaliangalia kanisa (Ukristo) kwa zama za kati.. Ili tujue tuliyonayo leo ni matokeo ya nini...

1.KANISA LA MWANZO/MAPEMA (EARLY CHURCH) Tunali-trace kuanzia mwaka 34 AD mpaka 311AD

2.KANISA LA KATI (MEDIEVAL CHURCH), Ambalo tunali-trace toka mwaka 476-1453

3. NA ZAMA ZA MATENGENEZO KUANZIA KARNE YA 15 MPAKA BADAE KARNE YA 20, AMBAKO MWAKA 1901 &1909 NI MIAKA MUHIMU SANA KWA KUFUFUKA KWA KITU KILICHOPOTEA CHA KANISA LA MWANZO.

Nitafanya Recap ya vipindi vingine yaani Kanisa la awali, lakini leo natamani tuangazie kwa ufupi... medieval church (period) na mianzo ya matengenezo (reformation).

KUANZIA MWAKA 30AD MPAKA MWAKA 311, KULIKUWA NA WATAWALA WA DOLA YA RUMI (EMPERORS) KWA IDADI JUMLA 54. KATIKA HAO WOTE, WAKO 12 WALILIUDHI KANISA KWA ADHA KUU (PERSECUTION), NA WAKO KUMI KATI YAO AMBAO HAO NDIO WALIKUWA TERRIBLY WORSE TO THE CHURCH. INAELEZWA KWAMBA KILE KILICHOANDIKWA KATIKA UFUNUO 2:10, KWAMBA KANISA LITAKUWA KATIKA DHIKI SIKU 10, INAWAKILISHA KIPINDI CHA MIAKA 200 CHA HAWA EMPERORS 10 HATARI SANA. MIONGONI MWAO YUKO NERO ALIYESHIKA DOLA BAADA YA CLAUDIUS, DOMITIAN, TRAJAN, MARCUS, SEPTIMIUS, DECIUS, DOCERTIAN ETC. KWA KUWA LEO SIJADILI KIPINDI CHA KWANZA BALI CHA KATI, HIVYO SITAJIKITA KUELEZA  YALIYOLIKUTA KANISA KWA ZAMA ZAO. ILI KUKUPA LADHA NITAELEZA KWA UFUPI YA WATAWALA WAWILI TU AU MMOJA. ILI TWENDE KWENYE KILICHOKUSUDIWA.

*🗡NERONIAN PERSECUTION (ADHA WAKATI WA NERO) 54-68AD*
Huyu jamaa alivuviwa upako wa Shetani haswaaa, mwonekano wake kuanzia miguu, tumbo na macho yake na kila alichokuwa nacho hakikuwa cha kawaida. Mama yake Nero aitwaye Agrippina, alimshawishi mmewe Claudius, baba wa kambo wa Nero, kwamba amchukue Nero nafasi ya mwanae mwenyewe, amweke mbele kwa ajili ya utawala badala yake. Pia kwa sababu za kutoridhika kimapenz i na mambo ya uzazi, huyu Agrippina alimuua Claudius. Hivyo kumfanya Nero kuwa mtawala akiwa na miaka 17 tu. Kwa wale mnaotumia programme ya computer iitwayo Nero 🔥💽💿ku-burn contents kwenye Cd. Jina lake Nero ukilitaja tu linahusisha kuunguza (Burn). Mtawala huyu mwenye wazimu, alimuua mama yake kikatili. Aliwahi kupata scandal ya uzinzi ya mke wake Octavia, akamkata kichwa fastaa. Na akaomba kichwa kipelekwe kufanyiwa show off kwa mhudumu wake aitwaye Poppea. Ili achunge sana la sivyo atamfanya kama hao. Baada ya muda huyo mistress wake naye akapata ujauzito katika mazingira ambayo Nero hayaelewi, akamuua pia.

Mtawala huyu alikuwa anapendezwa na damu na mauaji... Alikuwa na macho ya blue kabisa na ni mtata wa maaumizi, akiisha kuwaua ndugu zake wote, Senate ya dola ya Rumi, ikatoasadaka nyingi kwa miungu kwamba heshima imerudi mjini.. Hasa hasa alipomuua mkwe kwa ishu ya kuchepuka.

Baada ya hapo, kiu ya damu ilipomjia ndipo akawaza ukorofi gani afanye... Akauchoma mji wa Rumi kwa moto 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥. Kisha hiyo kesi akawapakazia wakristo, maana wengi walikuwa wayahudi, pia maeneo yao mengi moto haukuwaka...(Kumbuka Mungu anatabia ya kuwakinga watu wake na mabaya, kwa namna ileile aliyowahifadhi waebrania kule Goshen,vyura,chawa,giza,majipu,vifo, maji ya damu etc kila kilichoitandika Misri kiliruka mipaka ya Goshen kwa watu wa Mungu. Ambaye uko ndani ya Yesu (UMEOKOKA), upo Goshen mahali pa salama ambako majanga yakija yataku-pasaka (pita juu yako bila kukugusa). Dunia imeandaliwa mapigo mabaya mno kwa mikono ya malaika wa vitasa, baragumu na ole tatu. Lakini waliofichwa na Yesu kwa wokovu, watanasuliwa siku chache kabla ya mapigo hayo. Kwa kusema hivi, ni muhimu msomaji wangu wewe binafsi, ujihakikishe UMEOKOKA, usibaki mwanadini mwovu, maana utaabika vibaya.

Kwa kuwa wakati huo Petro naye alikuwa huko Rumi, tena ndiye kiongozi, basi kesi hii waliyopakaziwa wakristo, alipaswa kuibeba yeye. Kumbuka ni wakati huu wa Nero ndipo Petro na Paulo waliuawa, ikihusianishwa na scandal za kubuni za Nero. Pauli alikatawa kichwa mwaka 🗡68 A.D. Petro alipopata taarifa kwamba yuko suspected na huenda akakamatwa na askari wa Rumi muda wowote. Wakristo walioko Rumi, wakamficha, na usiku wakamsaidia kutoroka. Alipokuwa amekwisha vuka geti ili akimbie. Historia inaonesha, alikutana na Yesu. Yesu akamkunbusha aina ya mauti ambayo Yesu alimshamtabiria (Yohana 21:18), Alimwambia ukiwa kijana ulienda ulipotaka, lakini ukiwa mzee mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikotaka wewe✝. Petro alijirudisha mwenyewe Rumi. Na akakamatwa next morning, ambako waliamua wasimkate kichwa bali wamsulubishe kama Yesu wake. Naye akapata mwanya wa kuandika akiomba✍🏽. Msinisulubishe kama Bwana wangu. Mie kichwa kiwe chini na miguu juu, akakubaliwa  akawa UPSIDE-DOWN CRUCIFIED. Na Paulo naye miaka minne baadaye yakamkuta hayohayo. Yeye walimlaza mahali pa kuchinjia🗡, upanga maalumu ulishushwa karibia na kukata kichwa then, wakampa nafasi aikane imani ya Yesu, ili wamwache, alichowajibu kilifanya wamchinje kwa hasira... Aliwaambia *_Kwa nini mnanichelewesha!_*

KWA KUWA LEO SIO SIKU YA EARLY CHURCH, BASI NITAANGAZIA MATYRYDOM KUPITIA MTU MMOJA AMBAYE NI ASKOFU WA SMYRNA (APOSTLTLIC AND PROPHETIC TEACHER) AITWAYE POLYCARP. HUYU ALIKUWA MWANAFUNZI WA MTUME MZEE YOHONA RAFIKI WA YESU, ALIYEKUFA KIFO CHA KAWAIDA MWAKA 100AD, BAADA YA JITIHADA ZOTE ZA KUUA MWILI KUSHINDIKANA, ALIBURURWA KWA HORSE CHARIOTS, ALIFANYA NYAMA ROAST KWENYE PIPA LA MAFUTA YALIYOCHEMKA MPAKA BASI, NA KABLA YAKE WALIMTEST SUNGURA, WALIPOMCHOVYA TUU WAKAMTOA AKUWA TAYARI KWA KULIWA🍗🍖. LAKINI ALIPOINGIZWA YOHANA MAFUTA YALIKUWA MAJI YA KUOGA NA DAWA YA MAKOVU YA KULE KUBURWA NA MIJELEDI. Jitihada za kumkata viungo ziliwatokea puani, maana viungo walivyo mkata, walimkuta mtaani anavyotena. Ndipo wazo la kumtupa Patmo ili aliwe majoka huko. Shukuru Mungu, tukio hilo lilituletea kitabu cha ufunuo mwaka 98AD. Sasa huyu Polycarp akiwa mwenye miaka 86.kama Bishop wa kanisa, aliisimamia imani sana. Zama zake zilicross wakati wa watawala wawili Trajan (jina lake linazungumza sifa zake za kuharibu), na Marcus. Yeye walimuwinda ili amkufuru Yesu. Akaenda eneo la mbali. Walipofika kwake hawakumkuta, vijana wake wawili waliowakuta waliwapa kichapo heavy. Wakawapeleka alipo, alikuwa amejilaza ghorofani, alipoona misafara mikubwa angeweza kutoroka. Ila akashuka akawafuata, akawasalimia. Askari wakasema hivi, tunaanzaje kutumia nguvu kubwa kumkata kikongwe👴🏿 huyu. Akawakaribisha, wakapewa chakula, wakala. Akawaomba afanye maombi kidogo bila kuingiliwa, wakamruhusu. Akapiga maombi yale ya kipentekoste yaliyovuviwa kwa masaa mawili, askari wakiwa wanasikiliza👮🏾👮🏾👮🏾👲🏾👲🏾👲🏾🛡🛡⚔⚔🗡🔪⚔. Wakamchukua wakampeleka katika katika Stadium, kumbuka nyakati hizi ilikuwa ni adhabu kama tatu za lazima. Kuchomwa moto ukuwa hai, Kukatwa kichwa, kuliwa na wanyama wakali ukuwa uwanja wa taifa, na raia wanalipa kiingilio kuja kucheki gemu kama ya Simba na Yanga, wakati simba dubu wanawafanyia mmeng'enyo 🦁🐼.
Siku chache kabla hajakamatwa, Polycarp alikuwa katika maombi, aliona maono Pillow iko kichwani inawaka moto🔥,akawaambia wenzake kuwa nitachomwa moto nikiwa hai. Na kweli alipoingia uwanjani alikuta misumali sita mirefu imeandaliwa na vifaa kuchomea moto. Akiwa anaandaliwa kuchomwa, wakampa nafasi amkufuru Yesu, akawambia, Nimemtumikia Yesu mpaka sasa nina miaka 86 hakywahi kunifanyia baya, naanzaje kumkufuru Mfalme wangu? Muda anasogezwa eneo la kati, ikasikika sauti toka Mbinguni ikisema *Be strong!*, ilisikiwa na wengi, bila kuelewa nani kasema. Historia hii ya Polycarp iliandikwa na shuhuda wa jicho *_eye witness_* aliyekuwepo uwanjani. Alichomwa moto lakini mwili wake badala ya kuungua ulikuwa ni kama dhahabu inavyowekwa motoni (Ayu 23:10), inazidi kung'aa. Muuaji akaelekeza amchome kwa mikuki🏹. Alipofanya hivyo damu ilitoka nyingi ikauzima moto wote. The whole Stadium remained😳😳😳😳😳 or 🙄🙄🙄🙄 and some 🚶🏿🙇🏽🙇🏽🙇🏽🙇🏽

NAKATISHA STORI. YESU ALIWATIA ADABU KUWA FUNGUO ZA MAUTI NA KUZIMU NINAZO MIMI 🔑🗝(Ufu 1:18), Na kwamba hafi kwa kuwa ninyi mnamuua, nimeamua kumchukua kwa kifo hiki, ili niwafundishe wakristo wa zama zijazo.

*FUNDISHO*
Wakristo wa zama hizi, wanayo ya kujifunza. Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu (Math 11:12, Luka 16:16). Wokovu ambao leo tunauchukulia poa, watu walisimama mpaka kifo kibaya bila kugeuza sura. Nimeongea na dada mmoja, yaani amezini na kijana kizembe, kisa anamsindikizaga wakitoka ofisini. Sasa hivi kizazi hiki kitasimamaje? Maana hawa akina Polycarp na wengine walioifia imani (matyrs) ndio wanaoitwa wingu kubwa la mashaidi mashahidi (Ebra 12:1), Ukiulizwa kwa nini ulifanya hiki, ukajibu niliogopa kufukuzwa kazi na boss ndio maana nikakuasi Bwana, wataletwa watu wa namna yako walioshinda. Mungu akusaidie usimame imara. ACHA TABIA YA KUCHUKULIA POA WOKOVU, NEEMA IKO TELE, BUT USI-MISUSE NA KUMIS-BEHAVE. YESU KRISTO ANATAKA WATU WENYE NGUVU. HATUWEZI KUBEMBELEZA MLOKOLE UNA MIAKA MITANO KWENYE WOKOVU, UMEJAA ZIGZAG NA MEANDERINGS, TUTABEMBELEZA WASIOOKOKA NA WACHANGA SANA KIROHO. JITIE NGUVU ACHA UBABAISHAJI, WOKOVU ULIMGHARIMU MUNGU AWE MWANADAMU, AUAWE NA WANADAMU ALIOWAUMBA MWENYEWE ILI AKUOKOE. ETI LEO iPhone 7 📱UNAITUMIA KUM-DISVALUE YESU NA MSALABA WAKE, SHAURI YAKO AISEE, HUYU NI MUUMBE WA MUNGU KUKUONYA.
SASA TUANGALIE KIPINDI AMBACHO NILIKILENGA LEO

YAANI MWAKA 476-1453 KIITWACHO MEDIEVAL PERIOD.
UKO WAKATI AMBAO, KANISA LILIPATA AHUENI, YAANI ADHA ILIKOMA KABISA. UKRISTO UKAWA NI DILI (HABARI YA MJINI). NA HUO NI WAKATI AMBAO EMPOLEROR CONSTANTINE, ALIUKUBALI UKRISTO. ULIKUWA NA MANUFAA KADHAA NA ATHARI NYINGI ZA KUICHAKACHUA IMANI.

ELIMU KUHUSU MUNGU(THIOLOJIA) INAONESHA MAMBO MENGI YASIYO YA KIBIBLIA YALIINGIZWA WAKATI HUO. MFANO HAKUKUWAHI TOKEA UBATIZO WA MNYUNYIZO MPAKA WAKATI HUU YAANI KARNE YA NNE, AMBAPO KWA HESHIMA YA COSTANTINO ROMAN EMPORER ALIYEKUBALI KUWA MKRISTO, WALIAMUA KUMBATIZIA KTK PALACE YAKE KWA KUNUNYIZWA...
SWALA HILI LINAENDA SAMBAMBA NA UBATIZO WA WATOTO/WACHANGA)  "ANABAPTISM"  ULIOPITISHWA NA BARAZA LA NIKEA 787AD.
KITHIOLOJIA KUANZIA MWAKA 476BK---1453BK UNATAMBULIKA KAMA *"DARK PERIOD"* AU MEDIEVAL CHURCH,WAKATI HUU KANISA LILIKUWA TAASISI YA SERIKALI,HIVYO NI WAKATI MAFUNDISHO UNBIBLICAL&NONBIBLICAL MENGI YALIINGIA

KWA NINI UNATAJWA KAMA "DARK PERIOD" NI WAKATI WA GIZA BECAUSE (1.)THE CHURCH BECAME AN ORGANIZATION (2.) INTRODUCTION OF LITURGY (LITURUJIA)
MAMBO KAMA SACRAMENT OF CONFIRMATION(KIPAIMARA), KUABUDU SANAMU KULIIDHINISHWA NA BARAZA LA NIKEA 787BK, INTRODUCTION OF PRAYER BOOK (KITABU CHA SALA) MIFUMO AMBAYO ILIENDELEA KUKAUSHA UKIROHO WOTE ETC. HAPO SIJADILI UDHEHEBU AU KUBATIZWAJE NI SAHIHI. HAYO YAPO KATIKA SOMO TOFAUTI, LIITWALO *_UBATIZO WA MAJI KIBIBLIA_*.

SASA TUPATE KUJUA ILIKUWA KANISA LA RUMI (CATHOLIC CHURCH=maana yake the church of everywhere, this is the Christian mainline, iliubeba ukristo pamoja na kuuchakachua, mpaka hapo karne ya 15. Tujue sasa Lutherani ilitokeaje, Anglican ilitokeaje, Orthodox, Presbetyrian, Calvinism etc yalianzaje???

Mwl Proo
0762879363

MIDIEVAL PERIOD(476-1453)

*RISE OF PROTESTANTISM (KUINUKA KWA UPROTESTANTI)*

TUYAANGALIE MAMBO MACHACHE YALIYOINUKA KUANZIA ZAMA ZA MTAWALA CHARLAMAGNE(800 A.D) THE FRANKISH KING OF HOLY ROMAN EMPIROR.. KULIKUWA NA MAKUNDI MATATU  YALIOUFANYA WAKATI HUU UWE WA NAMNA YAKE..

*USKOLASTIKI-FALSAFA YA UANAZUONI (SCHOLARSTICISM)*
HILI NI JINA LA UJUMLA LA HARAKATI ZA THIOLOJIA ZA MAGHARIBI WALIOKUWA WAKIYATAFITI MAMBO YA UKRISTO KWA UMAKINI NA KISOMI NA WALITAFUTA USAHIHI WA IMANI YA KIKRISTO.. MWANZILISHI WA USKOLASTIKI NI ANSELM (1033-1109) NA WENGINE NI THOMAS AQUINAS (1225-1274) NA WILLIAM WA OCKHAM (1285-1347)

*UMISTISISTI(MYSTICISM):*

ULIANZISHWA NA BONEVENTURA (1217-1274)

SIFA 3 ZA MYSTICISM
(1.)WALISHUGHULIKA SANA NA UMASKINI,MAOMBI,KUSOMA MAANDIKO NA TAFAKATI(YOGA-DEEP RELIGIOUS MEDITATION)
2.)WALIKUWA NA UZOEFU KIDINI
3.)WALISHIKILIA SWALA LA KUWA NA UMOJA KAMA MUNGU

*UMONASTI/MONASTICISM(UTAWA)*

HILI NI KUNDI LINALOONESHA IMANI YA KIKRISTO KWA VITENDO VYA KIMWILI.WATU HAWA WALIKUWA MATAJIRI MNO,HII ROHO YA UTAWA ILIWAHI KUZUKA MWAKA 320AD KWA MTU AITWAYE ANTONY,NA KUNA MTU AMBAYE ANAITWA SIMON WA SYRIA (400AD) ALIWAHI KUJENGA MNARA (PILLAR SAINT) WENYE UREFU FUTI 60 NA UPANA FUTI 4 ILI KUJITENGA NA DHAMBI..NA ALIFANIKIWA KUISHI MIAKA 37 JUU YA MNARA.WALIKUWA NA MKAZO KTK POVERTY,CHASTITY(USAFI WA MOYO) NA CELIBACY(KUTOOA)

*KANISA NA SERIKALI KATIKA ZAMA ZA KATI:*

*KANISA LILIFANYA KAZI PAMOJA NA SERIKALI YAANI KANISA LILIKUWA NI TAASISI YA SERIKALI

*WATAWA WALILISHUTUMA KANISA KUWA KIBARAKA(STOOGE)

*PIA MFUMO WA UMWINYI(FEUDAL GOVERNING SYSTEM) ULITAWALA
*KANISA NA SERIKALI VILIPOINGIA KWENYE MASHINDANO MAKALI JUU YA NANI MWENYE MAMLAKA ZAIDI PAPA AU MTAWALA WA DOLA (EMPEROR) PAPA AKAANZISHW FUNDISHO LA "MONARCHIAL PAPALISM" YAANI UFALME WA KIPAPA AKIDAI MWENYE MAMLAKA YA KIROHO NDIYE ANAYETAWALA NA SERIKALI

NA PAPA INNOCENT III NDIYE ALIYEONGOZA KUCHAGULIWA  MTAWALA MPYA WA RUMI(1202AD)

PAPA BONIFACE VIII ALIISHI AVIGNON ALIKUWA AMEHAMA TOKA RUMI KWENDA UFARANSA TUKIO HILI LAITWA "BABYLONIAN CAPTIVITY OF THE PAPACY 1309AD (MIAKA 60).. MWAKA 1377 UPAPA UKARUDISHWA RUMI AMBAPO PAPA ARBANO VI ALITEULIWA(ANAKUMBUKWA KWA HARAKATI NYINGI ZA KUHAMASISHA WAKRISTO WAJITETEE KIVITA DHIDI YA UISLAMU

UPINZANI MKUU *(GREAT SCHISM):*
HILI LILITOKEA WAKATI KULIPOTOKEA NA MAPAPA WAWILI; MMOJA ALIKUWA AVIGNON UFARANSA (POPE CLEMENT VII) NA MWINGINE DOLA TAKATIFU YA RUMI (POPE CHARLES VI) ILI KUPATA SULUHU YA GREAT SCHISM.. BARAZA LA PISA LILIITISHWA NA WAKAAMUA KUWAFUKUZA MAPAPA WOTE WAWILI NA KUMCHAGUA MMOJA MPYA..MAPAPA WALIOFUKUZWA WALIPINGA KUWA THE COUNCIL OF PISA WAS ILLEGAL

KUKAITISHWA BARAZA LA CONSTANCE(1414AD) KUSHUGHULIKIA UWEPO WA MAPAPA WATATU;PIA KUSHUGHULIKA  NA FUNDISHO POTOFU(HERESY) YA JANN HUSS

BAADA YA BARAZA LA BASEL(1431) MATAIFA MENGI YA ULAYA YALIANZA KUPATA UHURU; KUKAWA NA KUKUA KWA ELIMU VYUO VIKUU VINGI VIKAANZA, PAMOJA NA PRINTING PRESS(HUMANISM) NA NYAKATI HIZI WASOMI WENGI WALIKUWA NI CLERGY(ORDAINED SERVANTS)

*RENAISSENCES!*

HII NI HALI YA UPINZANI ILIYOTOKA KWA WATU BAADA YA KUONA ELIMU INATOLEWA KWA WATUMISHI WA KANISA TUU IN SHORT IT REFERS TO INTELLECTUAL REACTION TO THE INTELLECTION DOMINATION OF THE CHURCH

UPROTESTANTI(PROTESTANTISM)
UPROTESTANTI NI UPINZANI DHIDI YA CATHOLIC CHURCH

*MAMBO MATANO YALIYOFANYA UPROTESTANT KUINUKA*

1)MABADILIKO YA KIJAMII..ELIMU KUFUATANA NA FALSAFA ZA AKINA PLATO,CICERO,ARISTOTLE
2)KUPANUKA UPEO..WATU WA KAWAIDA (LAITY) WA KASKAZINI MWA ITALI WAKIELIMIKA MKAZO ULIKUWA JUU YA (individualism,nationalism and corporeal world-secular)
3)UPINZANI TOKA KWA TAWALA ZA FALME
4.)UBEPARI
5)MAMBO YASIYO SAHIHI NDANI YA KANISA
*SIMONY(KUNUNUA HUDUMA ZA KIKANISA)
*THE SALE OF DISPENSATION AND INDULGENCES

DISPENSATION-HAKI AMBAYO MTU ALIPEWA KWA KULIPIA ILI AWEZE KUTENDA KOSA/DHAMBI KWA RUHUSA YA PAPA MFANO KUOA ZAIDI YA MKE MMOJA

INDULGENCES- HAYA NI MALIPO YALIYOLIPWA, KWA AJILI YA MSAMAHA WA NDUGU ZAKO WALIOKUFA. PESA HIZI ZILIITWA PETER'S SPENDING NDIZO ZILIZOJENGA ST.PETER BASILICA HUKO ROME

*WANAMATENGEZO WA AWALI (early reformers):*

1.)JOHN WYCLIFFE
HUYU ALIPINGA MASWALA KADHAA;
SWALA LA KANISA KUWA NA UTAJIRI MWINGI WAKATI WATU NI MASIKINI; MAMLAKA YA PAPA (SUPREMACY OF THE POPE); ALIKATAA ZILE VITA ZINAZOONGOZWA NA KANISA; ALIPINGA SWALA LA WATUMISHI KUTOOA (CLERGICAL CELIBACY) NA HUYU NDIYE ALIYEITAFSIRI BIBLIA KWA LUGHA YA KIINGEREZA KITU AMBACHO KILIKUWA KINYUME NA KANISA LA R.C.. WAFUASI WA .WYCLIFFE WALIITWA "LOLLARDS"
MWENDELEZO:
2.)JAHN HUSS(1419-1494AD)WAFUASI WAKE WALIITWA 'HUSSITES'. HUYU ALIKUWA PADRE AMBAYE ALICHUKUA MAFUNDISHO YA WYCLIFFE AKAYASAMBAZA ULAYA; KANISA LILIMTENGA (EXCOMMUNICATED HIM) KUKATOKEA VITA IITWAYO "HUSSITE WAR"

3.)MARTIN LUTHER
ALIZALIWA 10/11/1483 ALIKUFA 18/2/1546 AKIWA EISLEBEN GERMAN
HILO JINA LILIBADILIKA HANS LUDER BAADAE LUDHER BAADAE LUTHER
ALIKUWA
MONK(MTAWA)
THEOLOGIAN
MKUFUNZI WA CHUO KIKUU
BABA WA UPROTESTANT
MWANAMATENGENEZO(CHURCH REFORMER)

MARTIN LUTHER ALIPINGA UWEPO WA SACRAMENT 7 AKATAKA ZIWE MBILI
RC WANAZO HIZI SABA
1)HOLY EUCHARIST
2)UBATIZO
3)PENANCE/KITUBIO
4)HOLY UNCTION
5)ORDINATION
6)COMFIRMATION/KIPAIMARA
7)NDOA
MARTIN LUTHER ALISIMAMIA KUWA WOKOVU UNAPATIKA KWA IMANI TU(SOLA FIDE) YAANI KAZI YA KIDHABIHU YA YESU. PIA ALISIMAMIA MAANDIKO TUU(SOLA SCRIPTURA) NA ALIWEKA MLANGONI THESES 95. MALKIA WA UJERUMANI ALIMSAPOTI LUTHER KWA SIRI..

KANISA LA UINGEREZA:

IKO VITA IJULIKANAYO KAMA "THE WAR OF THE ROSE" ILIYODUMU MIAKA 30.. HII NI VITA YA FAMILIA MBILI ZA KIFALME (KING HENRY VII + KING RICHARD III) FAMILIA ZILIZO PIGANA NI LANCASTER FAMILY VERSUS YORK FAMILY.. HUYU MFALME HENRY VII ALIKUWA NA MTOTO AITWATE ARTHUR(KING HENRY VIII)..UFARANSA ILIPIGANA NA UINGEREZA MIAKA 100 NA WAKATI HUO VITA HII ILIPUNGUZA MAKALI YA VITA VYA FAMILIA ZA KIFALME NA ARTHUR AKAMWOA CATHERINE WA ARAGON JAMBO LILILOPUNGUZA UHASAMA..WATAWALA WA UINGEREZA WALIKUWA EITHER WACATHOLIC AU WAPROTESTANTI

HENRY VIII-RC
EDWARD VI-MPROTESTANT
QUEEN MARY-RC
QUEEN ELIZABETH ALIKUWA MJANJA AKAAPPLY TECHNIQUE IITWAYO "VIA MEDIA" YAANI NJIA YA KATI HAKUWA R.C WALA MPROTESTANT BALI ALIYABEBA YOTE KWA KUPITA KATIKATI

SIFA ZA UPROTESTANTI:

I.)IMANI KUU
-maandiko ndiyo mamlaka ya mwisho(sola scriptura)
-kila mtu ni kuhani anaweza ongea na Mungu
-sola fide-ni kwa imani tuu mwamini anahesabiwa haki

II.)KUKUA KITHIOLOJIA
-waliacha kutoa heshima kwa watakatifu(Veneration of saints)
-cross from crucifix(matumizi ya msalaba usio na kisanamu cha Yesu)
-Theotokos(waliachana na fundisho la Mama wa Mungu)
FIKRA ZA KITHIOLOJIA yaani fundamentalism/liberaism(kukubali mabadiliko) na pentecostalism
III.)MAFUNDISHO
-uhusiano wa moja kwa moja na Mungu
-kila mwamini ana haki ya kutafsiri maandiko
-umishenari kwa sana

*HARAKATI ZA KIMISHENARI ULAYA...*

ZILIIBUKA KARNE YA 17.. WANAHARAKATI WAPURITANTI(PURITANT MOVEMENT) WALIOLENGA KUWEPO NA KUIONESHA KWA USAHIHI IMANI YA KIINJILI (EVANGELICAL FAITH) HAWA WAPURITANTI WAKASHINDANA NA MALKIA ELIZABETH..MALKIA ALIFANYA NAO VITA WAKAKIMBILIA UHOLANZI(MIAKA 11) BAADA YA HAPO WAKAPANDA MELI IITWAYO MAYFLOWER AU WATERFLOWER KUELEKEA PLYMOUTH(NEW ENGLAND)1620 MAREKANI AMBAKO WALIPANDA KANISA LA KWANZA LA KIPROTESTANT.MIONGONI MWA WAPURITANTI MASHUHURI NI JOHN KNOX NA JOHN HOOPER

NB:
KUANZA KWA KANISA LA KILUTHER NA ANGLIKANI KUNA SABABU ZA KIJAMII NA ZA KISIASA KULIKO KIROHO..MFANO MGOGORO WA UJERUMANI NA ITALY ULIPELEKEA UJERUMANI KUMPA SAPOTI MARTIN LUTHER KUJITENGA ILI WAO PIA WASIWE CHINI YA UTAWALA WA KIPAPA CHINI YA RUMI; PIA MARTINI LUTHER NAYE ALITAKA KUOA NA SHERIA ZA R.C ZINAMKINGA ..BADAE AKAMUOA MJERUMANI AITWAYE KATHARINA VON BORA THOUGH AS THE PRIEST WAS NOT ALLOWED UNDER R.C..YEYE HAKUANZISHA DHEHEBU LA ULUTHER BALI WAFUASI WAKE. PIA KANISA LA ANGLICAN LILIANZISHWA NA MFALME HENRY VIII KWA KUWA NAYE ALITAKA KUWA HURU KUTOKA KTK UTAWALA WA KIRUMI CHINI YA PAPA..CHOCHOTE ALICHOFANYA ILIBIDI MPAKA APOKEE BARUA YA PAPA.. HIVYO ALIJITOA NA KUANZISHA DHEHEBU LAKE KAMA DINI YA ENGLAND YAANI ANGLICAN ILI AWE HURU KUOA MKE MWINGINE KULIKUWA NA SHIDA KTK NDOA YAKE YA MWANZO...MENGINE TUTAENDELEA KUJIFUNZA KTK SERIES ZINAZOFUATA

Mwl Proo
0762879363 (whatsapp)
0718922662

alltruth5ministries@gmail.com

YESU KRISTO YUMO NDANI YENU, ISIPOKUWA MMEKATALIWA!

*YESU KRISTO YU NDANI YENU; ISIPOKUWA MMEKATALIWA!*

_*Mwl Proo*_
*0762879363*

Shalom Aleichem!✋🏾
Nilipoanza kutafakari tu, naandika nini, moyoni ukaja ujumbe kwa kasi ya ajabu. Nilipotafakari sehemu ya mambo yanayopaswa kuwemo, nikamwambia Bwana, _"Mbona hili jambo ni gumu😰!!"_. Lakini hii ni dawa ya kuponya. Wale ambao ni wa Mungu, wanakwenda kuponywa, hata kama walitanga-mbali (2Timothy 2:19). Leo pamoja na kuzungumza na Wakristo wasio wahudumu (Laities) lakini walengwa haswa ni wahudumu katika utumishi (Clergies).
Tunakutana na kauli moja ngumu hapa, tuisome kwa pamoja;

2 Wakorintho 13 : 5 *_Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa._*

MANENO MAWILI YA MSINGI SANA, *JIJARIBUNI* NA *MMEKATALIWA*, NENO HILO JIJARIBUNI KATIKA BIBLIA YA KIEBRANIA KUMEANDIKWA _*BEDIKAH/BEDKOT*_ (Χ‘ְּΧ“ִΧ™Χ§ָΧ”), AMBALO NI NENO MAALUM LA UCHUNGUZI WA UKE WA MWANAMKE KAMA KUNA DALILI YA DAMU YA SIKU ZAO (INTERNAL EXAMINATION OF VIGINAL CANAL). KWA MUJIBU WA MAFUNDISHO YA KIYAHUDI (JEWISH TALMUD) WALAWI 15:19-30, 18:19, 20:18) YENYE KUIFAFANUA TORATI, MWANAMKE ALIPASWA KUFANYA UCHUNGUZI/UKAGUZI SIKU SABA KABLA YA KUINGIA KATIKA _*NIDDAH (Χ ִΧ“ָּΧ”)/MENSTRUAL PERIOD/SIKU ZAO ZA HEDHI*_, NAYO ILIKUWA INAFANYIKA KWA UMAKINI MKUBWA, ILI KUEPUSHA UNAJISI NA KUTENGWA. MWANAMKE ALIPASWA KUNUNUA KITAMBAA MAALUMU CHEUPE (TAHARAH), AMBACHO ALIKITUMIA KWA NJIA YA VIDOLE, KUIKAGUA DAMU KWA NDANI SANA KABLA HAIJAONEKANA NJE. NA KILE KITAMBAA BAADA YA UKAGUZI KILIPELEKWA KWA RABI ILI AJIRIDHISHE. HAYA MAMBO NI KIVULI (EBRANIA 10:1, KOL 2:17) CHA UTAKATIFU (KEDUSHAH) WA KWELI WA SASA. MUNGU ALIKUWA ANAWAFUNDISHA USAFI WA KIMAHUSIANO/FAMILY PURITY _*(TAHARATH HAMISHPACHA/Χ˜Χ”Χ¨Χͺ Χ”ΧžΧ©Χ€Χ—Χ” )*_.
NENO LA PILI NI KUKATALIWA. NENO LILILOTUKIKA KUTAJA AINA YA KUKATALIWA HUKU NI *_REPROBATE_*, IKIWA NA MAANA YA KUWA *(DISAPPROVED BY GOD, BECAUSE YOU ARE DAMNED SINFUL)*, YAANI MUNGU ANAKUTAFAKARI NJIA ZAKO, THEN ANASEMA AAAH NO! πŸ‘πŸΎWEWE HAPANA!!!!

Sasa kwa nini neno Bedikah limetumika, katika kuwataka watu wajijaribu/wajichunguze (examine)?. Ili kutia uzito, maana kuna uwezekano wa kukataliwa, hata kama ulikwisha itwa, usiwe mteule (Math 22:14). Paulo Mtume anatuonesha huo uwezekano;

1 Wakorintho 9 : 27 *_bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa._*

Pata picha namna ambavyo, wewe mtumishi unavyopiga kazi zito, saa nzingine unaletewa watu waliojengewa ngome nzito, deliverance zao zinakutoa jasho, washirika wanaondoka saa nane, wanakuacha upo mpaka saa kumi na mbili jioni, umekomaa na watu ambao, vifungo havifunguki kwa wepesi, koti la suti limeloa jasho kama umemwagiwa ndoo ya maji. Lakini eti siku ile, unamkumbusha Yesu, juu ya hizo kazi zote.. Naye anajibu......

Mathayo 7 : 23
*_Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu._*

Tena hatasema siwajui, bali sikuwajua; yaani mlikuwa mkiendelea na yote hayo ya huduma mkiwa mmekataliwa (hawajui).

Sikiliza mtumishi mwenzangu, huenda kuna wakati ulighafilika, ukajikwaa, ukaanguka labda katika uzinzi; the very day ulipoanguka, kabala hujaifikilia toba, ukaleta mgonjwa mwenye vifungo, ulipombandika mkono✋🏾, akafunguliwa mara moja. Ikakupumbaza, ukapotezea toba ya kweli (teshuvah), ukidhani may be God is just okey, with fornication. Kumbuka, miongoni mwa mambo yanasukuma kukataliwa, ni mrundikano wa dhambi zisizotubiwa *_(HAKIKISHA UNAPATA SOMO LANGU LIITWALO, "KUONDOLEWA KINARA")_*
Sasa kufunguliwa kwa wagonjwa na ile miujiza baada ya wewe kutoka katika hali ya usafi, haithibitishi kwamba uko πŸ‘πŸ½na Mungu. Not all times ukianguka, Mungu atanyang'anya upako, No!. Baada ya anguko zito la Lusifa (Shetani kwa sasa), hakunyang'anywa nguvu kabisa, ingawa na aamini zililaaniwa maana aliji-disconnect na chanzo cha utukufu wote (Mungu). Sasa ndivyo ilivyo leo, tunao wahudumu wengi ambao walikwisha kataliwa, lakini wanaendelea zao na maombezi. Ile shwari waliyoipata baada ya kucheza rough (rafu) kiroho, iliwadanganya, Mungu hawezi ku-overlook dhambi, hajifanye hajaiona fulani hivi (Mdo 17:30), hayo aliyafanya zamani, sasa anawaamuru watu wote watubu *_(HAKIKISHA UNAPATA MASOMO YANGU HAYA MAWILI, ILI DOZI πŸ’‰πŸ’ŠIKAMILIKE 1.ASEMAYE KWELI KWA MOYO WAKE, NA LILE LA 2. SECOND CHANCE)_* Maana lengo ni kuponya na sio kuleta vitisho.

Hakuna hatari kama hii, yaani ulishawahi kuifahamu kweli, then ukaanguka mikononi mwa Mungu. Hilo ni jambo baya sana na uchungu

Waebrania 10 : 31
*_Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai._*

Yeremia 2 : 19
*_...ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha Bwana, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, Bwana wa majeshi._*

KUNA WATU WANAENDELEA NA HUDUMA, LAKINI KUNA WAKATI ALIMPA UJAUZITO BINTI WA KANISANI, AKATUBIA UZINZI, LAKINI ILI KULINDA HUDUMA ALIPOGUNDUA MIMBA ILIINGIA, AKAFANYA MAUJUZI WAITOE. SASA ANAENDELEA LAKINI YALE MAUAJI AMEYAFUKIA, KUMBE KUTOFANYA TOBA YA KWELI, KUKAFANYA BADO AWEKO HUKU NDANI, LAKINI KAKATALIWA. MWINGINE ALIMTENDA MAMBO YA HIANA MKE WA UJANA WAKE, MWINGINE AME-DIVORCE KWA SABABU FEKI FEKI, MARA NIMEFUNULIWA WEWE SIO MKE WANGU, MARA NILIWAHI KUKUFUMANIA (HAPO NAPO WAKRISTO TUMECHAKACHUA), YESU HAKUTOA SABABU YA KUMWACHA MKEO, KWA VIWANGO VYA UKRISTO, UNAWEZA MFUMANIA MMEO/MKEO KABISA KITANDANI NA MWANAMKE NA UKAAMUA BADO KUMSAMEHE. _*(HAKIKISHA UNAPATA SOMO LANGU LA NDOA YA KIKROSTO)*_, ILI MAMBO YAKAE SAWA HAPO.

*WITO WANGU KWA WATUMISHI WA MADHABAHU KAMA MIMI*
Badala ya kuendelea kuja kushtukizwa unaachwa, unayo nafasi JIJARIBU SASA (JIFANYIE BEDIKAH), VIPI HUJAKATALIWA? KUMBUKA DHAMBI HAISAMEHEWI KWA SABABU IMEPITA MIAKA SITA TANGU UIFANYE, BALI KWA TOBA YA KWELI (TESHUVAH), NA KAMA MTU HAJAFIKIA ILE LEVEL YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU *_(ambako nimekufafanua katika lile somo la, "Mambo ya kiroho yakiharibika; Tengeneza")πŸ‘ˆπŸΎWaweza jipatia hili somo katika mtandao_* BASI KAMA HUJAFIKIA HUKO, WAWEZA TUBU, UKAYATENGENEZA MAMBO YAKO. MAANA ULICHOFANYA KINASAMEHEKA, NA UKIISHASAMEHEWA NA KULIPA GHARAMA YA TOBA, BWANA MWENYEWE ATAKUTENGENEZEA MAMBO YAKO (2Nyakati 29:36).

*HITIMISHO*
*_```KAMA UNAHISI MOYONI MWAKO, MUNGU ALIKUWA ANASEMA NA WEWE, NA UNATAMANI KUYAWEKA MAMBO SAWA. TAFUTA SOMO LANGU LIITWALO, "KATIKA TOBA KUNA TUMAINI, HATA KAMA KOSA NI KUBWA MNO". LITAKUPA YAKUPASAYO UYAFANYE, NAWE UTAJIHAKIKISHIA UMILELE MZURI BAADA YA TAABU YA DUNIA HII, SIO UKAMALIZIA UMILELE WAKO KWENYE MOTO WA JEHANAMUπŸ”₯πŸ”₯.```_*

Mwl Proo
~*Mjumbe wa Matengenezo*~
0762879363 (whatsapp only)

alltruth5ministries@gmail.com

KWA NINI KUOMBA!!!!

*KWA NINI KUOMBA??*
*_Why Praying?_*

*Mwl Proo*
*0762879363*

Wapendwa katika Bwana na Mwokozi, Yesu Kristo; Salaam!
Utakaye pata nafasi kusoma ujumbe huu, wewe ndiwe mtu Mungu amekukusudia. Leo sina jambo jingine, nazungumzia kuomba. Sitaki kabisa kufundisha maombi kwa liturjia zetu za kilokole. Kwanza niseme, kama uko mtu unajijua connection ya kimungu imekamata sawasawa, ng'ang'ania hapo. Kama unajua upo kwenye position ambayo unaomba consistently and ceaselessly, kamatia hiyo chanel usisogee nje, usiingize falsafa zozote zingine, zijiinuazo kinyume ja elimu ya Mungu.

Mpendwa msomaji usikubali, narudia tena, usikubali kuwa mlokole/mkristo koko (dull), ukawa butu/dull kwa kutoomba daima, ukawa miongoni mwa wale watakaokufa vifo vya kipumbavu (kama afavyo mpumbavu). Nazungumzia vifo vya kiroho na vya kimwili. Wasiodumu katika kuomba, wanakufa vifo vya kipumbavu. Nakumbuka shuhuda za waliokufa vifo vya kimwili kipumbavu, yaani wachawi walimtishia kabla kwamba hutamaliza huu mwaka, na kweli ndani ya miezi michache akapiga stroke, akapaooza/paralyse, ndani ya miezi minne akafa sawa na neno lililotoka kwa wachawi. HIKI NI KIFO CHA KIPUMBAVU KULIKO CHA ABNERI, na wapo waliokufa vifo vya kiroho kipumbavu. Nimepata ushuhuda wa binti aliyekubali kufa kipumbavu, eti mvulana ambaye ni classmate wake chuo, alimfuata hostel-room, akamkuta peke yake, binti kaokoka lakini kijana ni myebusi bado. Then kijana akamwomba binti ati aingize fimbo yake ya ufalme kidogo tu, sio yote, kwa ubembelezi mwingi, akaruhusu, na toka hapo akawa mzinzi wa kawaida tuu, HANA CONNECTION YA KIMUNGU TENA!!! HOW FOOLISH????!!!! Kuna mambo ya kuingiza nusu na yote kwenye dhambi??? Labda kama Shetani ni Admin wa grupu la Whatsapp, poa, KIFO HICHO CHA KIPUMBAVU. Vifo hivi vinawakuta watu butu kiroho, wasiodumu katika kuomba. Usiwe na kiroho kilichopoa kiasi cha kutoweza kuomba, wala usiwe na imani kubwa kiasi cha kutoaomba. Maana wako pia niliwasikia, they claim to have that level, ambako hawapaswi kuombea kila kitu, kwamba mengine Mungu anajiongeza mwenyewe, maana anajua unahitaji, so they travel🛫🚌 hakuna kuomba, they do business, huduma  etc, hakuna kuomba. Siamini sana juu ya imani kubwa, kiasi cha kutohitaji maombi, Maana ule mstari wa Filip 4:6 katika tafsiri za kingereza zimeandikwa *_"Worry about nothing, but pray for everything"_*. Kama sivyo Yesu angekuwa wa kwanza kuacha kuomba, lakini Yeye alitumia usiku wote kuomba (Luka 6:12), na hakuomba sala kama zako za muda wa kulala, au maombi yako ya kisomi na kistaarabu, bali maombi yake yalikuwa ya namna hii 👉🏽(EBRANIA 5:7), Wala mtume Paulo aliyejisifu kunena kwa lugha sana kupita Wakristo woteee wa Korintho, asingedai aombewe kiasi kile 👉🏽(1Thes 5:25).

USIACHE KUOMBA KWA SABABU YOYOTE. BUT PRAY CEASELESSLY, CONSISTENTLY!. MAANA MAOMBI YANAYOFANYA KAZI SANA, YANAYOLETA MAANA ZAIDI NI YALE UNAYOOMBA KILA SIKU, KILA UNAPOPATA NAFASI WAZI, MAADAM MUNGU ANAPATIKANA.

Zaburi 32 : 6
*_Kwa hiyo kila mtu mtauwa Akuombe wakati unapopatikana. Hakika maji makuu yafurikapo, Hayatamfikia yeye._*

NB:-
MAOMBI NI UFUNGUO WA VYOTE 🔑🗝. NA KUTOOMBA NI DHAMBI (PRAYERLESSNESS LIFE IS SINFUL LIFE) SOMA (1SAM 12:23), KUACHA KUOMBA NI DHAMBI!!!.
UKIPUNGUKIWA HEKIMA OMBA, UKIKOSA AMANI OMBA, UKIOTA NDOTO HATA KAMA HUZIELEWI, HUNA NJIA NYINGINE, OMBA HATA IKITOKEA HUJAPATA TAFSIRI, MAOMBI YATAFIX HIYO ISHU, UMEONA MAONO YAMEKUVURUGA, OMBA! MAMBO YAMRKWAMA PANDE ZOTE, OMBA; MAMBO YAMEKUNYOKEA 👍🏽✔✔ KILA UPANDE, BIASHARA, ELIMU, HUDUMA, OMBA SANA!! HUONI MBELE, HUELEWI NINI KINAENDELEA KATIKA ROHO, WEWE OMBA TU KWA JUHUDI. USIACHE KUOMBA. USANII NAMBA MOJA KWAKO MTU ULIYEOKOKA NI KUISHI HUOMBI. KUOMBA KUWE TABIA, OMBA MCHANA, USIUVUSHE USIKU BILA KUOMBA (KAMA NILIVYOELEZA KATIKA SOMO LA *UMUHIMU WA USIKU*), KAMA KUNA MIKESHA YA KANISA USIACHE KUHUDHURIA, OMBA MPAKA SURA YAKO IFANANIE MAOMBI, SAUTI YAKO UKIONGEA TUIGUNDUE IMEPAKWA MAFUTA KWA SABABU YA KUOMBA (SISEMI IKATIKE, IKITOKEA HIVYO SINA NENO NAWE). LAKINI OMBA, OMBA, OMBA, MPAKA MAISHA YAKO YALOANISHWE NA MAOMBI (FULL INUNDATED WITH PRAYER).

*UFUNUO MKUBWA JUU YA MAOMBI*

☄NAOMBA LEO NIKULETEE HIKI KITU CHA AJABU, TOKA KATIKA
*_ISAYA 21_* SURA YOTE. ISAYA ANASEMA AMEONA MAONO MAGUMU (mstari 2).
*_2 Nimeonyeshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu. Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote._*

☄KATIKA SURA HII, MAOMBI YAMEITWA ULINZI, NA MUOMBAJI AMEITWA MLINZI

_*5 Wanaandika meza, wanaweka ulinzi, wanakula, wanakunywa. Simameni, enyi wakuu, itieni ngao mafuta.*_
_*6 Maana Bwana ameniambia hivi, Enenda, weka mlinzi; aonayo na ayatangaze.*_

☄AYAONAYO NA AYATANGAZE.
Kwanza tunapaswa kufahamu, mlinzi anakaa juu ya kinara cha mlinzi (watchtower), ambacho huinuliwa mita kadhaa kama mlima, ili kumpa nafasi ya kuona mbali. Ni mtu anayeomba tuu, atakayeona mambo ya mbali, ili msishitukizwe na mabaya au mazuri. Kuna wakati ulifika kila jambo lilitokea hasa baya, nilirudi kujiuliza, hivi hili Mungu akishanionesha hili, nilienda kufunua diary 📖 niliyoandika mambo niliyoandika mambo niliyokuwa nikiyaona (Habakuk 2:2-4).

☄MUOMBAJI LAZIMA AWE MSIKIVU SANA KWA ROHO MTAKATIFU, ILI AELEWE ANAYOONESHWA, YANAWEZA KUWA YA SHARI, AMANI, BARAKA N.K

*_7 Naye akiona kundi la wapanda farasi, wakienda wawili wawili, na kundi la punda, na kundi la ngamia; asikilize sana, akijitahidi kusikiliza._*

☝🏽Mnaona hapo?? Kama akiona farasi🐎🐎 maana yake wanaokuja wapo kivita (shari), akiona punda au ngamia 🐴🐪 (ujio au utembeleo wa amani tuu, huenda mnaletewa hedaya 🎁)

☄KUDUMU KATIKA KUOMBA KUNAITWA KUKAA KATIKA KINARA MCHANA, NA USIKU

*_8 Ndipo akalia kama simba, Ee Bwana, mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana, na kila usiku ninakaa katika zamu ya ulinzi wangu._*

☄UKIDUMU KUOMBEA UNAYOYAONA, UTAPATA TAFSIRI, HIVYO USILETE KWA WATU MAFUMBO YAKO ULIYOYAONA, BALI TAFSIRI YAKE PIA. ISAYA ALIONA MAONO MAGUMU, LAKINI YOTE ALITUPA TAFSIRI YAKE. AKIWA JUU YA KINARA, ALIONA KUNDI LA WATU NA FARASI WANARUDI TARATIBU TOKA VITANI, AKAJUA HUKO WALIPOTOKA WAMESHINDA NA ADUI (BABELI) AMEANGUKA.

*_9 Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini._*

☄KUMBUKA TENA, NYAKATI ZA USIKU, NI MUHIMU KWAKO, NA NDIO WAKATI ANBAO UFALME WA GIZA WANA-MAXIMISE UTENDEJI WAO KWA DHAHIRI, HAKIKISHA KILA LINALOTOKEA MCHANA NA USIKU, WEWE ULIPATE WAKATI WA USIKU ILI ASUBUHI UTUPE HABARI KAMILI. USIUTUMIE USIKU WOTE KUFUATILIA MASHINDANO YA UEFA. KAMA NI MPENZI SANA WA SOKA, BASI BWANA AKUPE KIASI, ILI ISIWE TOO MUCH MWANA MAOMBI UPO CINEMAX ALL NIGHTLONG KAMA MSHANGILIAJI 😂🙌🏽 WA MPIRA ⚽📺🖥. SINA UGOMVI NA WEWE NDUGU MWANASOKA, ILA UPEWE KIASI, MIMI HAYO YALIGOMA KWENDA SAMBAMBA NA MAISHA YA KIROHO YALIYOZAMA.

*_11 Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku?_*

☄MUOMBAJI LAZIMA UWE NA ENOUGH INFORMATION (TAARIFA ZA KUTOSHA).

Hapa sisemi taarifa za ITV na TBC, wewe unapaswa kuwa na taarifa ya matukio muhimu yaliyobamba katika ulimwengu wa roho. Huenda ikawa taarifa iliyokamata vyombo vyote vya habari, lakini wewe uwe uliipata kabla katika ulimwengu wa roho, na unaielewa kwa mlengwa wa kiroho zaidi. Nakumbuka ushuhuda wa mtumishi huko Indonesia (2004) ambaye Mungu  alimwambia panda ndege ondoka🛫. Nadhani hakuwa na ratiba ya flight. Ile ndege yao inafly, huku chini TSUNAMIS IKAPIGA HATARI. Lakini siri yake ni maombi, na hata alipomuuliza Mungi kwa nini Tsunami imetokea, akawa na majibu tofauti na ya wataalamu wa natural catastrophies. SASA MENGI LEO HII YANATOKEA, WATU HAWANA HABARI, HATA WALE WANATUAMBIA WAO NI MANABII/WAONAJI, NAO WANAPITWA. LAKINI LENGO LA KUKAA KWENYE KINARA NI KUYAONA MAJANGA KABLA, FAIDA YA KUOMBEA WAHANGA/VICTIMS NI NDOGO, NI BORA KUJE TAARIFA TUOMBE ILI KUZIA JANGA, AU LIKITOKEA LIJE WITH ZERO-NEGATIVE EFFECT. NAJUA UKWELI KWAMBA HATA UKIWA NABII BADO MUNGU ANAWEZA KUKUFICHA JAMBO (2FALME 4:27), LAKINI SIO KAMA HIVI AISEE. MUOMBAJI SHARTI UWE NA INFORMATIONS TUJE KUULIZA KWAKO.

*_12 Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena._*

*KUMBUKA, KUFUATILIA SANA HABARI KWENYE TV, NA BLOGU ZA WATU, NA MAGAZETI, NA WHATSAPP, TWITTER NA FACEBOOK, HAIKUFANYI UWE WELL-INFORMED KIROHO, MAANA HIZO NI SECOND HAND DATA. WEWE ULIPASWA UZIDAKE ZAIDI KULE JUU YA KINARA KULIKO HIZO. HIZO ZA WHATSAPP NA MAGAZETI ZINAKUONGEZEA WINGI WA MANENO TUU, NA KUKUFANYA UISIKIE SAUTI YA MPUMBAVU NAFSINI MWAKO*

Mhubiri 5 : 3
*_Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno._*

Kama taarifa zako zote unazotendea kazi, ni zile za whatsapp 📱📲, unakuwa na sauti ya mpumbavu nafsini mwako. Ni hizo taarifa zitakuwa processed na kukuundia mfumo wa maisha. Hiyo haipaswi kuwa hivyo kwa muombaji.

MUNGI AKUBARIKI KWA KUELEWA. ANZA SASA KUOMBA KWA JUHUDI, MCHANA NA USIKU. ACHA KABISA ZILE EXCUSEA ZA KIPUUZI KWAMBA SHUGHULI ZANGU HAZINIPI NAFASI, HIYO HAIPO, USIMFANYE MUNGU KUWA MWONGO. HUWEZI KUOMBA KAMA HUOMBI, MAOMBI YANAOMBWA KWA KUOMBA, HAYAWI REPLACED NA KUIMBA NYIMBO ZA DINI, AU KUSIKILIZA MAHUBIRI SANA, HAYO YAFANYE ILA USIACHE KUOMBA

Mwl Proo
0762879363 (All Truth Whatsapp Grupu)

alltruth5ministries@gmail.com

Wednesday, November 29, 2017

KAA NASI!

*KAA NASI*

_*Mwl Proo*_
_*0762879363*_

Nawasalimu tena, kupitia jina la Yesu aliye Kristo na Bwana!.
Nasikia uvuvio wa kimungu sasa, maana kuna watu Mungu anakwenda kuwasaidia. Naomba nitoe tangazo nililolipata usiku wa kuamkia leo. _*MAANGUKO NI MATOKEO YA KUACHA KUKAA NA YESU*_, Nilipoamshwa saa 02:05am (usiku) kwa ajili ya kuomba, ile nainuka nikasikia tamko hilo, linaongea moyoni, akilini mwangu kama mtu anatangaza πŸ“’. Sasa uliyewahi kuanguka na ambaye hujawahi kuwa na maanguko *(hapa nazungumza kuanguka dhambini, kushindwa kumaintain standards za wokovu, na yale yote ambayo wewe mwenyewe ukiyakumbuka unajua mmmmmh!😨katika hili na lile, kwa kweli nilishindwa kusimama na Yesu/nilimweka pembeni, na kushindwa kuilinda imani).* Sasa neno la Bwana kwetu liko wazi, kwamba maanguko ni matokeo ya kuacha kukaa na Yesu. Yesu ni *MCHUNGAJI MWEMA (Yohana 10:1-16)*, asiyeweza kuacha kondoo zake zishambuliwe na kuondolewa kundini, hilo linafanikiwa kondoo akijicholopoa kundini (Akiacha kukaa na Yesu). Mpendwa msomaji, ukiamua kukaa peke yako dakika mbili katika utulivu, kujihoji, hivi mimi nipo na Yesu Kristo, unapata jibu moja kwa moja. Mwingine ambaye njia zake tayari zimeingia virusi, akijitafakari, ana-conclude mwenyewe, *_"Mmmh! Kwa kweli Mungu mwenyewe anisaidie tuu"_*.

Kama uliangukaga kwenye matendo ya uzinzi, it was never an accident, uliacha kukaa na Yesu moyoni, lakini ukaendelea kuivumilia hiyo hali ndio anguko likaja. Yuda hakumkana Yesu kwa dharura, ukisoma injili zote nne, tayari alikuwa ni mpinzani wa Yesu, pamoja na Yesu kumpendelea cheo cha kuwa Chief Accountant. Tunaambiwa alikuwa akichakachua pesa za Bwana mkubwa. Yesu kapakwa mafuta ya manukato, jamaa anasajesti kwa upinzani, kwamba why this waste😏, yangeuzwa yanathamani ya mshahara wa miezi nane, tungesaidia maskini. Sasa tayari moyoni mwaka hakuwa upande wa Yesu, Shetani ikawa mtelezo tu kupata msaliti. Ndivyo kunavyokuwa na mtelezo kwako kuangushwa dhambini.
Ukikaa na Yesu wewe utajua, na wanaokuzunguka watajua. Tena usiombe mpagani ambaye alikuwa anakutamania ulivyo na Yesu, aka-note kwamba haukai na Yesu tena, akaja kukwambia mbona mtumishi siku hizi haupo kama zamani?. Utajitutumua kumvunga kwamba upo sawa tu, huku ukijaribu kumjulisha na jitihada zako za nje ya kundi, *_tena kwa taarifa yako hapa nimefunga!_*, Kumbe ni maombi/fasting ya 12hours ya kwaya, umefunga kwa sababu mwenyekiti wa kwaya alitishia sanaaaaaaa, usipofunga umevunja maagano 😑!! Kwa hiyo ukasombwa bila hiari. *When you start doubting your faith in the LORD, that doubt is real/true*. Msomaji wangu, unaweza kuwa huna elimu ya kueleweka, lakini ukikaa na Yesu, utakuwa na kaharufu kazuri kuliko waridi🌹, tutakutamania pamoja na hako kasetifiketi ka form four. Muulize Petro na YohanaπŸ˜€

Matendo 4 : 13
_*Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.*_

Wasomi walipocheki, hawa watu *_No School_*, why are they so bright?πŸ€”Wakapata jibu, haaah hawa watu walikaa na Yesu miaka mitatu.

*MOYO WA SOMO*

HAKUNA KITU KITAMU AISEE KAMA KUKAA NA YESU. HAKUNA KITU KIZURI KAMA KUMWEKEA TUMAINI LOTE YESU, HAWEZI KUKUANGUSHA KAMWE. AKINA KLEOPA WALIZUNGUMZA NA YESU, WAKIWA BADO HAWAJAWA NA HAKIKA, LAKINI WALIKUWA WASHAHISI HUYU TULIYENAYE LEO πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½, WAKAMSHAWISHI YESU ASIONDOKE, MAANA YESU ALIJIFANYA KAMA ANATAKA AENDELEE NA SAFARI ILI AWAPIME..

Luka 24 : 29 *_Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao._*

AMBAO WAMESHAWAHI KUTEMBELEWA NA YESU AU WAKAPATA UTEMBELEO WOWOTE WA KIMUNGU (ANNUNCIATION-DIVINE VISITATION) KWA NAMNA YOYOTE, WATAKUWA MASHAHIDI WAZURI, JINSI AMBAVYO LAZIMA UTATIA MGOMO USIACHWE, YAANI UBAKI KATIKA HALI HIYO TAMU. UNGEWEZA KUWAULIZA PETRO, YOHANA NA YAKOBO SIKU ILE YESU ALIPOBADILIKA WANGEKUAMBIA. PETRO ALIKUWA NA MKE NA WATOTO NA MPAKA MAMA MKE YUKO HOME KWAKE (EXTENDED FAMILY). LAKINI AKASAHAU MAJUKUMU, ANAWAZA AJENGE VIBANDA MLIMANI. YESU NI MZURI BWANA!!! YESU PEKE YAKE NDIYE AMBAYE HAWEZI KUKUANGUSHA WALA KUKUVUNJA MOYO, BUT THE WORLD WILL ALWAYS DISAPPOINTS YOUπŸ‘‰πŸΎπŸ˜”. UNAKAZI NZURI, IPO SIKU UNAKUTA BARUA KWA SEKRETARI, UMETUMBULIWA πŸ’‰. UNABIASHARA NZURI IPO SIKU UNAWEZA KUTA HITIRAFU YA UMEME IMETOKEA ENEO LA BIASHARA KILA KITU MAJIVU. UNAWEZA KUWA NA MTOTO BRIGHT KAKULETEA DIVISHENI NA G.P.A NZURI IPO SIKU UNAWEZA PEWA TAARIFA ZAKE KUWA NI MWATHIRIKA WA UKIMWI, AU YUKO ICU BAADA YA COMPLICATIONS KATIKA TUKIO LA ABORTION (KUSHUSHA INJINI), ALILOLIFANYA KWA SIRI. MOYO WAKO UTACHOMWA NA KUSHUKA CHINI. ONLY JESUS,  WON'T  DISAPPOINT KABISA, UKIKAA NAYE

*NI RAHA KUWA NA WAZAZI*
Hao nao usiwawekee tumaini, wanaweza kukuacha aiseee usiamini kwamba ni wao. Lakini hata hao wazazi wakisema tangu leo tafuta wazazi yuko Yesu atakukaribisha kwake.

Zaburi 27 : 10
_*Baba yangu na mama yangu wameniacha, Bali Bwana atanikaribisha kwake.*_

*NI VIZURI KUWA NA VIONGOZI WAWAJIBAKI KAMA RAISI WETU*
Huyo naye tusimwekee tumaini, ipo siku anaweza kugeuka fumba na kufungua, akafanya maamuzi kwa mamlaka yake, yatakayo kutia jereha za moyo hutaamini nakuambia, hapa kazi tu!

Zaburi 118 : 9
_*Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu.*_

Mika 7 : 5 _*Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari.*_

_*HIVI SI UNAYE SHOSTI WEWE, SI UNAYE MCHUMBA?*_

Huyo naye unaye mwamini, umempa moyo wako, siri zako zote unamwambia, mpaka meseji za siri unazochat na mchumba wako, naye unamwonesha eti, wait and see the disappointment that will follow toka kwa huyo shostiako, na mchumbaako,atakapotunga sauti ya Mungu feki, eti Bwana kaniotesha kuwa wewe sio mke wangu, nimekosa amani...Mungu wa hivi hayupogo ❌❌❌πŸ™…πŸ½πŸ™…πŸ½πŸ™…πŸ½πŸ™…πŸ½. Tena kwa wale waaminifu katika kumsikia Mungu, siku unapotia wazo la kumpenda huyo mtu,atawahi kutoa comments zake, ukiwa mgumu, siku utakayo mtamkia, ukiwa mgumu zaidi mwanzoni mwa uhusiano, ukiwa mgumu zaidi atatumia watu, lengo ni kwamba kabla hajayatia sana moyoni, msitishe, maana Mungu ametupa huduma ya kuganga mioyo sio kujeruhi. So hizo sauti na ndoto unazootesha mwenyewe, kumbe umeona panadoli (πŸ‘©πŸ») mwingine hapo sio Mungu ni mungu tamaa yako. Lakini kwako uumizwaye ni bora ujue siri hii, tumaini lte liweke kwa Yesu tu, awezaye kukupa shoshti na mchumba ambaye hayuko tayari uumie moyo.

Zaburi 41 : 9
_*Msiri wangu (shosti) tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.*_

NB:-

*Hakuna mtu aliyeumizwa kwenye mahusiano, anayeweza kuoparet kwenye kiwango kizuri cha karama za rohoni au huduma kwa huduma, kama ni mwimbaji vurugana na mchumba au vunja ndoa, halafu katoe single track studioπŸ’Ώ, kuanzia muda unaimba unagundua, mmmh!!!???...*

MAKE THIS YOUR PRAYER TODAY!! OOH LORD JESUS, STAY WITH ME, STAY WITH US. KAA NAMI BWANA, UKAE NASI, KAA NA FAMILIA YETU!! AMEN AND AMEN

God bless you all
*Mwl Proo (Prosper Kadewele)*
Mjumbe wa Matengenezo
0762879363(All Truth Whatsapp Group)

alltruth5ministries@gmail.com

Maana ya Mtakatifu

NENO MTAKATIFU KWA ASILI YAKE, SIO KUTOTENDA DHAMBI

mwl proo

Neno la kiebrania קָדוֹשׁ (Qadosh/Kadosh/Gudosh/Kadesh) phoenetic spellings (Khaw-Doshe) ina maana ya kutengwa/takasa/consencrate/ lile andiko la Petro I (3:14b/15) lisemalo mioyoni mwenu mtakaseni Kristo neno hilo maana yake Set Christ apart in your hearts. Sasa kitu kilichotengwa kikawa sacred ni kitakatifu. Swala kutotenda dhambi linakuja baadae sana,Lakini waliotengwa tu ni watakatifu

Swala la holy living linakuja badae...

Ndio maana kuna siku niliuliza je mtu aliyeokoka akitenda dhambi jina lake jina lake linafutwa mara moja mbinguni? halafu akitubu linaandikwa twena??? Jibu la hasha
Sasa mjadala kuhusu utakatifu uanze ktk mlengwa huu kuwa mtakatifu sio mtu asiyetenda dhambi bali aliyetengwa..Athari za dhambi kwa aliyetengwa ni kitu cha badae maana Mungu ni mkuu kuliko dhambi zenyewe kwa aliowaridhia

Tuesday, November 28, 2017

WENYE USHUHUDA MKUBWA, HUWINDWA ZAIDI!

*WENYE USHUHUDA MKUBWA, HUWINDWA ZAIDI!*

*Mwl Proo*
*0762879363*

Bwana Yesu asifiwe sana!

Mapambano yetu na adui hayatakoma, mpaka wakati tunayaacha haya maskani ya sasa. Na kwa sababu hiyo, tunapaswa kudumu katika mafundisho ya takayofunua siri mbalimbali za maadui, ili asituzidi ujuzi akatushinda (2Kor 2:11)

2 Wakorintho 2 : 11 *_Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake._*

Bwana alinifundisha siri hii, ambayo leo tutaiangalia kwa kina zaidi. Watu wenye ushuhuda mkubwa, huwindwa zaidi. Hapa sizungumzi kwa upeo mdogo ule wa shuhuda za matendo ya Mungu, kwamba, "Haleluya, Mungu aliniepusha na ajali ya gari". Ushuhuda ninaousema hapa ni kitu kikubwa cha kimungu kilichobebwa ndani ya mtu chenye matokeo/impacts kubwa katika kuujenga ufalme wa Mungu na kuufilisi ufalme wa giza (Pia matendo makuu ya Mungu yaweza kuwa sehemu ya ushuhuda huo). Watu waliobeba vitu vya namna hivyo, watawindwa sanaa, tokea mbali mno.

*_ADUI HUMWONA MTU MWENYE USHUHUDA TOKA MBALI SANA_*

Wapendwa, Shetani na mawakala wake wanaweza mgundua mtu mwenye ushuhuda hata kabla hajazaliwa. Au akazaliwa tu, siku hiyo hiyo waka-note🤔, huyu aliyezaliwa mmmh! Kwa mfano, mapepo yanaweza soma taarifa za kiumbe kwa kupitia hata nyota⭐⭐, either nyota yake au nyota ya Mzazi inaweza kuonesha kuwa huyu mtu kabeba kiumbe kitakacholeta shida ~*(JITAHIDI UPATE SOMO LANGU LINALOHOJI JE! NI HALALI KUTUMIA ELIMU YA NYOTA KWA WALIOOKOKA?)*~ Katika somo hilo nilieleza jinsi ambavyo vitu vyote hasa viumbe hai vina muunganiko na celestrial phenomena. Yaani mahali fulani katika dunia🌍 kilipo kitu *_NADIR_* Ukitazama kwa usawa wa kwenda juu kule juu katika point ileile ya kiumbe yaani _*ZENITH*_, basi nyota inayopatikana kule inataarifa za kiumbe na maisha yake yote kabla na baada ya kuzaliwa na kufa, hata matukio yote kwenye maisha yake. Sasa maadui wanaweza kutumia njia hii au nyingine kujua mtu mwenye ushuhuda mkubwa.

_*SWALI KUBWA LA MAADUI WAKIISHA KUMGUNDUA MWENYE USHUHUDA MKUBWA NI HILI........*_

Matendo ya Mitume 4 : 16 - wakisema, *_Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana._*

Maadui wakijua, mkakati mkubwa ni huo hapo kuu, tumfanyeje huyu? Huwa kuna magumu yanapangwa kukwamisha huyu mtu kufikia wakati wake wa kuyafanya yale makubwa. (Sasa uko ambaye unataka kuniwahi kutaja kifungu cha Ayubu 42:1-2, Kamba makusudi ya Mungu hayawezi kuzuiliwa, huo ni ufahamu wa kati usiojua uhalisia wa mambo katika ulimwengu wa roho). Yako mambo ambayo Mungu aliyapanga, lakini ili yasizuiliwe aliweka walinzi (Isa 62:6), Yule Simeoni na Hanna wa Fanuel, waliwekwa kushikilia swala la Yesu kuzaliwa kwa salama, maana wanajimu kama akina Balaamu Ben'Beor walishaona kupitia nyota⭐ kuwa kuna atazaliwa mtu mkubwa huyo (Hesabu 24:17). Maombi yao yalinasua hatari zote za maadui. Maadui hawa wa kiroho, wanaweza leta complications katika uzazi, kumbe wanashindana na mwenye ushuhuda mzito (Msipoomba wanaweza kufanikiwa). Wachawi wanawaita wale watoto wanaofia tumboni, kuwa ni watu wasiopitia duniani. Sasa sio wote waliofia tumboni au mimba kuharibika (breech-birth/miscarriage/premature birth) ni matatizo ya kawaida,mengi ni jitihada za wakuu wa giza kushindana na wenye ushuhuda. Na kama watamtambua kabla hajatoka katika viuno vya baba yake. Watamsonga huyu baba kwa magumu na mabaya mengi, ili akija akute mazingira mabaya, asiwe na access ya kutoa alicho nacho ndani. Hivi karibuni, nimepewa ushuhda na mwinjilisti mmoja rafiki yangu, akiwq anamwombea binti mmoja, ambaye karudia form four awamu zote zinazoruhusiwa kazimaliza, pamoja na akili nyingi hapati hata ka-credit, hakuja shida. Lakini alipoanza kumhudumia tu, mapepo 👹👹👹yakapiga kelele kusema *"Tumeishikilia digrii 🎓 yake"*, Waweza ona binti yuko form 4, lakini mapepo wanamwona akitunukiwa shahada yake UDSM, na hivyo wanashindana na future yake iliyobeba ushuhuda wa kimungu. (Lakini kwa maombi, hata kama alibanwa, atachomolewa huko alikofinywa na kuletwa mahali panapo nafasi Zabur 18:19).

*MOYO WA SOMO*

Yohana 12:11-12

*_10 Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye;_*
*_11 maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walijitenga, wakamwamini Yesu._*

SASA TUJE HAPA TUONE, KUMBUKA WANACHOFANYA MAADUI WA MWILINI NI MWAKISI/REFLECTION WA TABIA YA MAADUI WA ROHONI, TENA WENGI HUWA PROMPTED NA MAADUI WA ROHONI KUFANYA HAYO. UNAWEZA IBIWA KITU NYUMBANI NA WEZI, LAKINI WEZI WAMEKUWA PROMPTED NA WEZI WA KIROHO (KAMA WALIKUSHINDWAKULE, WANAWACHOCHEA WEZI WA KIMWILI). SIKU MOJA NILIKUWA KATIKA DALADALA 🚌 TOKA MWENGE KWENDA MBEZI BEACH, NIKASINZIA SEKUNDE KAMA 10, NIKAOTA NIMEBEBA KAPU KWA HIZO SEKUNDE NILIONA MWIZI KAINGIZA MKONO KUCHOMOA KITU, NILIPOSHTUKA SIKIONA HATA KAPU, THEN MUNGU AKANIFUNDISHA SOMO TOKA MATHAYO 13:25ff, JINSI MAADUI WANAPANDA MAGUGU MUDA UMELALA KIROHO. TABIA ZILEZILE ZA MAADUI WA MWILINI ZINAAKISI ZA WALE WA ROHONI.

YESU KRISTO, AKIISHA KUMFUFUA LAZARO, ILIKUWA SHIDA KWA MAADUI. MAANA ALIKUWA NI MTU MWENYE USHUHUDA MKUBWA. ALIKWISHA OZA KABURINI ⚰☠SAIVI AMEKAA ANAKUNYWA JUICE YA DEL MONTE 🍹, MAADUI WAKAONA KWA AJILI YAKE, WENGI WANAMWENDEA YESU NA KUMWAMINI, WAKITAMANI NA LAZARO AWAPE  STORI ZA HUKO ALIKOKUWA, HIVYO WAKAANZA DILI LA *_KUMUUA ALIYEFUFUKA_*

Yohana 12:11-12

*_10 Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye;_*

WAKO WATU AMBAO MNASOMA UJUMBE HUU. MMEBEBA USHUHUDA MKUBWA, NA UNAWEZA UKAGUNDUA HILO KULINGANA NA MUNGU ALIPOKUTOA WAKATI MWINGINE. YAANI UKIKUMBUKA ULIVYOKUWA USTADH👳🏾, LEO HII WAMPENDA YESU SANA. UKIKUMBUKA ULIVYOTOLEWA NA MUNGU TOKA KATIKA DINI ZA KUABUDU MIZIMU, LEO HII UKO HUKU KWA YESU. UKIKUMBUKA YESU ALIVYOKUNUSURU NA KIFO CHA WAZI KWENYE AJALI ILIYOUA WENGI, UKIKUMBUKA JINSI AMBAVYO KABLA HUJAOKOKA LAKINI YESU ALIKUPONYA NA MAKUCHA YA WACHAWI, JINSI AMBAVYO ULIKAA ICU MIEZI MITATU UKATOKA HAI, NA MENGINE MENGI. USHUHUDA MKUBWA SIO HAYO MATENDO YA WOKOVU MKUU TOKA KATIKA MAJANGA, LAKINI HAYO MAENEO TATA ULIYONUSURIWA/NASULIWA NI KIASHIRIA KUWA UMEBEBA NDANI YAKO USHUHUDA MKUBWA. LAKINI ADUI HAKUACHI UTOBOZE KAMWE, KWA JINSI GANI?

*_SILAHA ANAZOTUMIA SHETANI NA MAWAKALA WAKE KUMNYAMAZISHA MWENYE USHUHUDA MKUBWA_*

Kama jitihada za kuzuia usizaliwe zilifail. Basi watajipanga huku mbele kwa silaha kama hizi

1.) KUKUTENGENEZEA DILI LA KUKUANGUSHA DHAMBINI (HASA KWENYE UZINZI).
Adui anajua silaha upi, inakata uwezo wako kwa haraka. Watu wengi wenye ushuhuda mkubwa, hawagundui shida ni nini, lakini vitaipo kwao kwa sababu ya ushuhuda alioubeba. Unakuta kaokoka ana-struggle na kuacha zinaa, kaweka ratiba ya kavu saba kukemea roho ya zinaa, akimaliza anaachiwa kawiki kamoja tuu, analetewa binti atakayejirahisisha au kumshawishi sana, mpaka na yeye anasema ngoja nifanye mara ya mwisho, then akimaliza anajuta majuto makuu, na anagundua ule uwepo aliousaka kwa kufuka siku saba wote umenyaushwa na uasherati wa siku moja. Watoto wengi wa watumishi kuna namna wamebeba kitu kikubwa cha kimungu, na unakuta wanabanwa hatari, watu wengi hulaumu tuu bila kuwaombea, kuwa watoto wa wachungaji hawaokoki, kisa wamesikia kawapa mimba wanakwaya kadhaa, kinachowindwa ni ushuhuda mkubwa wenye impact kubwa. Huyu mtu ambaye anajua kuwa akiwaeleza watu alitofanyiwa na Mungu, wengi watatetemeka na kumkimbilia Mungu, anaishiwa pozi akikumbuka uzinzi wake. Na hivyo maadui wanapongezana 👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽👍🏽👍🏽👊🏾👊🏾👊🏾 wanapeana Hi5, wamemnyamazisha mwenye ushuhuda mkubwa.

2.) KUMBANA KWA MAGONJWA NA DHIKI KATIKA MAISHA.

Wengi ambao wana kitu kikubwa cha kimungu, wamekamtwa, walipaswa kuwa kwenye Tv 📺 wakiueleza ulimwengu kuhusu Mungu mkuu, lakini hivi tunavyoongea, yuko wodini anauguza magonjwa sugu kwa muda mrefu, au yuko chini ya ardhi huko Geita anahangaika kuchimba madini, wala hajatoka kimaisha miaka kumi sasa, ananusurika tu kuangukiwa vifusi bila kupata maisha yoyote. Unakamatwa kwenye dhiki na magonjwa, ili muda wako uutumie kwa mamvo nje ya kusudi. Maana kusudi limefungwa ndani ya muda, ukishtuka hivi tayari you are aged 50 👴🏿👵🏿, nafsini unashuhudiwa kuwa kuna shauri la Mungu (Mdo 13:36) haujalitumikia na maisha yako yanaelekea saa kumi na mbili jioni.

*KIFANYIKE NINI*
✅JIZOEZE KUOMBEA UZAO WAKO, HATA UNBORN BABIES
✅WANAWAKE OMBEENI MATUMBO YA UZAZI, KWA BIDII.
✅KAMA WEWE NI MUHUSIKA, UNAJUA ULIPOTOLEWA NI ISHARA YA UNA USHUHUDA MKUBWA, USIKUBALI KUPITWA NA MUHULA WAKO (YER 46:17), JINASUE YAANI INUKA UKAANGAZE
✅TUKUMBUKE KUOMBA KWA AJILI YA WATAKATIFU WOTE, ILI WALE AMBAI WAMENASA, NA HAPANA MWOMBEZI, MUNGU AYATUMIE MAOMBI YETU KUWANASUA WENYE USHUHUDA MKUBWA.
✅UKIHISI DALILI YA KUMILIKIWA NA UFALME WA ADUI, TAFUTA UKOMBOZI, MAANA WANASHINDANA NA USHUHUDA

Mungu akubariki, nimeandika hii kama fremu tu, Roho wa kweli atakutia katika kweli yote, unapochukua hatua

Mwl Proo
0762879363( whatsapp group)

alltruth5ministries@gmail.com

FUNGU POSHO LANGU, NA SEHEMU YANGU MIELE

*FUNGU LA POSHO LANGU, NA SEHEMU YANGU MILELE!.*

*_Mwl Proo_*
*_0762879363 (WhatsApp)_*

Nawasalimu kwa jina la Yesu (Kristo)!. ✋🏾

Kuna watu hawaishi kwa furaha kamili, maana wameruhusu tafsiri za ulimwengu, zisizo sahihi kuwa kiongozi chao. Utakuta mdada ni mnene kwa asili (bonge), kwa sababu ya wadada wachache wembamba (slimy) wanaom-pinpointπŸ‘‰πŸΎ, anakuwa hana amani na alivyoπŸ˜€. Lakini ni hao hao wanaocheka ubonge, ndio wakioolewa wakapata na watoto wanakuwa mabonge zaidi, ila wanajiwekea tafsiri tofauti, kwamba uchumi na maisha yako πŸ‘πŸ½. Nakumbuka Lekchara wetu mmoja chuoni, alituambia ukiona mtu kapata kazi au kaolewa tu, then akafutuka (kanenepa ghafula), ni athari ya upande mwingine (side-effect), *kwamba hakuzoea maisha mazuri kabla*πŸ‘ŒπŸ½. Wengine walizaliwa kwao ni weusi kwa asili πŸ‘‰πŸΎπŸŒšπŸ‘§πŸΏ, dad and mom woteπŸ‘‰πŸΎπŸ‘΄πŸΏπŸ‘΅πŸΏ, sasa unatakaje uwe πŸ‘§πŸ», wachache wasiolewa wamejichubua kulazimisha tafsiri potofu ya ulimwengu ifiti maishani mwaoπŸ˜€. Wengine tumezaliwa na kimo cha kati tu kuelekea ufupi, na wengine super-talls kwa dunia ya sasa ambayo infact hakuna warefu, Goliath alikuwa na futi 9, lakini akina na Adamu na watu wa zama zao walikuwa na futi 12 kama boriti ile ndefu. Sasa wengine kwa kujikuta wako wafupi, wameji-look down na kujishushia thamani, wanabidii hao ya high heelsπŸ‘ πŸ‘ , ili kulazimisha tafsiri ya dunia ifiti maisha yao. Kabla ya kuweka sawa hoja yangu, nataka kuwatolea uvivu wakristo wa mwilini (carnal Christians) ambao hawajabadilishwa (of unregenerate nature), wasio na Roho wanafuata utashi wao (mere natural instincts), hawa ndio wanataabisha wenzao wajisikieje sijui. We unayesoma ujumbe huu mtu asikutaabishe (Gal 6:17), Ni kweli uko mweusi, haijatosha wao wakupende, ila weusi wako unalitosha kusudi la Mungu alilokuumbia, so ukijiangalia kwa kioo, jitamkie maandiko yanayo kuhusu, kwamba mimi ni mweusi-mweusi πŸ‘§πŸΏ lakini ninao uzuri (Wimbo 1:5), Tena kuna mwanaume fulani wa  nguvu, atakapokuona na rangi yako, moyo wake utavibrateπŸ’— (Akisema, *_"My favourite colour😍"_*), Wewe ambaye unachekwa na ubonge usijitaabishe na diet ya kujiua, tunafikiri unafunga kumbe unataka kuwa slim, huna haja, kama unadhani wote wwnatafuta slim/english figure pole, wa kwako huko aliko anaomba miss bantu fulani hivi mnene, nawe mwenye Zacchaeutic height (Urefu wa Zakayo) ulivyo unatosha kwa kusudi la Mungu, sio macho yote ya wanadamu. Kuna mtu alikuwa akikaa na mimi anaropokaropoka sijui mnaita Six-packs, akuπŸ˜•, waniatazamia nianze GymπŸ‹πŸΎ kusaka hizo? Nani kasema mke wangu ajaye atakuwa anazipenda? Kwani mimi ni mali ya wanawake wote wa barabarani? Halafu nitazioneshea wapi kwa mfano?πŸ€” Maana Roho wa Mungu ananishuhudia wazi ndani yangu, kwamba maisha yangu nitayamalizia madhabahuni tuu, So unanitajia Six-packs nije kuwaonesha wa shirika, mavazi yangu yenyewe suti kwa sana, ondoa hizo habari!!!.

Ayubu amewasikiliza akina Sofari na Elifazi, akaona wanamsuta juu ya udhaifu, akawaondolea uvivu;

Ayubu 12 : 3
*_Lakini mimi pia, nina fahamu kama ninyi; Mimi si duni yenu ninyi; Naam, ni nani asiyejua mambo kama hayo?_*

AKAWAAMBIA MIMI SI DUNI YENU (I'M NOT INFERIOR TO YOU), YAANI NINYI MNA NINI CHA KUNIZIDI? HAO WANOLETA VIJIMANENO VYA KUKUSUTA, THEY HAVE THEIR DARKEST SIDE WAKO WCHOVU SANA, MAANA MAMBO YOTE YAMEJAA UCHOVU USIONENEKA (MHU 1:8), NA MUNGU NI KAMA ALI-BALANCE AISEE, ANAYESUMBUA WATU NA RANGI YAKE NYEUPEπŸ‘©πŸ», ANAO UDUNI MAHALI PENGINE HATARI, ANAYESUMBUA WATU NA DIGRII ZAKE, πŸŽ“πŸŽ“πŸŽ“ ANAYO MAUCHOVU ELSEWHERE NI SHIDA.

*MOYO WA SOMO*
Zaburi 16 : 5
*_Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unaishika kura yangu._*

Zaburi 73 : 26
*_Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele._*

Daudi baada ya tafakari kubwa juu ya maisha, akagundua kuwa Mungu ndiye fungu la posho lake, anayeishika kura yake (He maintains his lot). Na Asafu baada ya kujaribu kufanya mambo kwa nguvu zake ndipo akajua kuwa vyote vitashindwa lakini Mungu ndiye sehemu yake (portion forever) milele.

KUNA KITU UNACHOKIHITAJI, NACHO UKIWA NACHO HAKUNA UDUNI WOWOTE MAISHANI MWAKO, HAUNA CHOCHOTE CHA KUPENDEZA ZAID YA HICHO, IWE MBINGUNI WALA DUNIANI, UNAJUA NI NINI? (SOMA ZABURI 73:25). THERE IS NO INFIRMITY, NO FRAILTY THE LORD CANNOT FILL, KILE UNACHODHANIA NI UDUNI (INFERIORITY) AU UDHAIFU, NDICHO KINACHOLETA TASTE KWA MUNGU NA NGUVU ZAKE.

2 Wakorintho 12 : 9 *_Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu._*

KWA HIYO HIVI NILIVYO NDIVYO LADHA YA KIMUNGU INADHIHIRISHWA, USIPOTEZE MUDA KUJILINGANISHA NA WADADA UNAOWATAZAMA KWENYE TAMTHILIA ZA KIFILIPINO, WALE UNAOWAONA WALIPITISHWA KWENYE MCHUJO WENGI MNO, KUWAPATA HAO ACTRESSES. SASA NAWE UNAHANGAIKA WEEE. MUNGU ANAKUTAMANIA UWE HIVYO, NA ANAJUA JINSI YA KUTUMIA UDUNI WAKO (AMBAO SIO UDUNI INFACT, ILA DUNIA IMEAMUA KUTAFSIRI HIVYO) ILI AJITUKUZE. SIKU MOJA NIMEENDA KUHUDUMU KANISA FULANI, WALE WALIOJIANDAA KUNIPOKEA, WALIJUA WATAPOKEA JAMAA LA MIRABA MINNE MWENYE KITAMBI, BAADHI YA WAZEE WA KANISA WAKAVUNJIKA MOYO, KUONA MHUBIRI MWENYEWEπŸ™†πŸ½πŸ™†πŸ½πŸ˜žπŸ˜ž. NIKAWATAZAMA NIKAWAJUA MIOYO YAO, NIKAWALIA POZI TUU😎. NILIPOPANDA MADHABAHUNI, AKILI ZAO ZIKAPOTEANA, NA WENGINE WAKAGUNDUA HATA ROBO YA UFAHAMU WANGU, HAWAJAUFIKIA, WALIANZA KUWARINGISHIA WACHUNGAJI JIRANI, HUYU NI MUHUBIRO WETU, MPAKA LEO WANATUMA MESEJI ZA KUULIZA MASWALI YA KIROHO NA KIBIBLIA, KWA NINI?

1 Wakorintho 1 : 27 *_bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;_*

πŸ‘†πŸΌπŸ‘†πŸΌUmeiona shughuli hiyo? Kwa hiyo hapa nilipo simtetemekei mtu kwa chochote, akiona kama nina uduni fulani, ajue pia ninayo mambo ambayo Mungu, pamoja na huo uduni, kanijaza mambo ambayo hata afanye hawezi kuwa nayo, nikikaa na mtu mwenye PhD, simtetemekei hata. Mtu mwenye anamiliki Hammer🚘 akiwq nami tutaenda sawa tu, mambo ya kumfanya anione inferior wakati mimi najua kuwa nafsini mwangu, ni mali zilizo njema zaidi (Ebra 10:34), wote tunapaswa kujua kuwa, hatutoshi sisi wenyewe,utoshelevu wetu, watoka kwa Mungu...

2 Wakorintho 3 : 5
*_Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu._*

NI KWELI UKIENDA KUOMBA KAZI, UWE MNYENYEKEVU. LAKINI WEWE BINTI UKIONA HRM AU BOSI WA KAMPUNI, ANAOMBA AKUONJE MWILI WAKO, ILI AKUSAINISHE MKATABA WA KAZI, MWAMBIE *_"AWAY WITH YOU JOB!"_* USIRUHUSU HUO UPUUZI, WALA USISEME SI NI SHOTI MOJA TUU, NOOOOOO!!!πŸ‘πŸ½ HIYO HIYO SHOTI MOJAπŸ’ UTAKAYO MPA MWILI WAKO, ITATENGUA RATIBA ZA KIMUNGU NYINGINE, ULITEGENEA NDOA YA HESHIMA, SASA USIPOJUA KUWA UNAYE MUNGU ALIYE FUNGU LA POSHO LAKO NA BWANA ALIYE SEHWMU YAKO MILELE (UTAKUTA HIZO NDOTO ZOTE ZINAVANISH, KWA CHAKULA KIMOJA TUU KAMA ESAU). SISI TUNAYE MUNGU MTOSHELEVU WETU, UEHAIFU NA UDUNI WETU NI MTAJI WETU. AMBAVYO SINA LEO, NI SWALA MUDA TU. HIS DELAY IS NOT A DENIAL (HAJANINYIMA MUNGU, ANAKIANDAA KWA MUDA WA KUFAA ANALILETA)

*_~KAKA YANGU NA DADA YANGU, WEWE SIO DUNI WA CHOCHOTE, KWA KUWA UNAYE MUNGU, YEYE NI FUNGU LA POSHO LAKO NA SEHEMU YAKO MILELE, WAACHE WANAOFANYA SHOPPING NAKUMAT NA MLIMANI CITY, WEWE ENDELEA KWENDA KARIAKOO, KARUME NA MANZESE, ULICHO NACHO NDANI YAKO NI ZAIDI YA MLIMANI CITY, LAKINI NAKUMAT/MLIMANI CITY MALL , HUKO NAKO BWANA ATAKUPELEKA KWA HAKI, SIO KAMA HAO WANAOKULA PESA ZA WAUME WA WATU, WAKIJILETEA UVUNJIFU USIO KAWIA_*

~Kama umemaliza kusoma, jifungia chumbani, chukua tenzi za rohoni, imba ule wimbo wa Bwana  U sehemu yangu. Kisha omba dakika tano, neema ya mguso wa  Mungu, itakugusa mara, na kuna mahali Bwana atakuvusha wikiendi hii. Nawe utanishuhudia~

Mwalimu Proo nimemaliza tayari, alichonijaza moyoni kwa leo kimetoka.

0762879363 (All Truth whatsapp group)

alltruth5ministries@gmail.com

BIKIRA SAFI

*BIKIRA SAFI*

_*Mwl Proo*_
*0762879363*

Bwana Yesu awabariki nyote, nawasalimu kwa jina la BWANA, Mungu, ambaye jina lake ni Mtakatifu!

Hili ndilo neno la Bwana kwetu leo, Bikira safi. Siwazungumzii bikira wale ambao hatukuwahi kufanya tendo la ngono kabisa, No! Twende darasani tupate ufunuo.

Bwana alinipa kazi ya kuwa mjumbe wa matengenezo; yaani wale ambao kwa namna yoyote walighafilika, wakajikwaa, wakatoka katika hali ile nzuri ya kukaa na Bwana, bado wasije kupotea kabisa. Kwa hiyo nimekuwa nikiwasaidia watu wa hivyo wajue kuwa pamoja na maanguko yao, Bwana hajawakataa. Watengeneze mambo yao, wasipoteze ule umilele na Mungu, eti kisa ulizini.
*Pamoja na jukumu hilo, matengenezo sio kusubiri watu waanguke, bali ni pamoja na kuzuia, kuwa na walokole wenye viraka na makovu ya kiroho.*
Ukiwa ndani ya Yesu, unakuwa kiumbe kipya, ya kale yanapita (2Kor 5:17), si ndio mstari wetu tulio ukariri? Sasa je ukijiondoa kwa Yesu unakuwaje? Au baada ya maanguko ya kiroho unakuwaje? Msamaha upo tu, kama hujfikia viwango vya kumkufuru Roho, kama nilivyofundisha katika somo langu la ~*_Mambo ya kiroho yakiharibika; Tengeneza (Jitahidi ulipate)_*~.
Hivyo badala ya kusubiri watu waanguke ili watengeneze, ambako viraka na makovu husalia tu (1Falm 15:5), ni bora kukujuza siri, ya kujitunza, usianguke, ili usalie bikira safi kwa mume mmoja uliyeposwa kwake ambaye ni Yesu. Tusome;

2 Wakorintho 11 : 2 *_Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi._*

Can you see?, Kumbe tulipoposwa kwa Bwana, tunayo hali ya ubikira katika roho, ukoje huo ubikira, unaharibiwaje? Tujifunze sasa.

MTU ALIYEKWISHA KULIPIWA ILE GHARAMA YA UKOMBOZI *_(PEDUT)_*, AKAZIONJA NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO, AKALISIKIA NA NENO ZURI LA MUNGU, AKAANGUKA BAADA YA HAYO, YAANI YULE ALIYEKWISHA KUFANYWA MWANA AKADROP OUT KIASI CHA KUPOTEZA IDπŸ’³ (Utambulisho) KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, KIASI CHA KUVAMIWA HATA NA PEPO (DEMON-POSSESSED), HUYU MTU HATA AKITUBU HALI YAKE BAADA YA TOBA HAITAKUWA KAMA MWANZO, ATAKUWA NA VIRAKA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO. MTU ALIYENUNULIWA KWA THAMANI (1KOR 6:20), AJE KUWA DEMON-POSSESSED TENA, YAANI NAFSI YAKE IKAMILIKIWA KULE ILIKONUNULIWA, AISEE ANAPOTEZA SIFA YA UBIKIRA. NI HERI UWE NA HISTORIA YA KUMILIKIWA NA MAPEPO KABLA HUJAOKOKA, MAANA HUKUWA NA SABABU YA KUTOMILIKIWA. ULIPOOKOKA YESU ALITIMIZA SHERIA ZA UKOMBOZI, ILI KUSIWE NA DENI TENI, KWA HIYO ULIHAMISHWA KWA HALALI TOKA KATIKA UFALME ULE ULIOKUTUMISHA MWANZO (KOL 1:13) *_(HAKIKISHA UMEPATA SOMO LANGU LIITWALO ~"MKOGO"~)_*, SASA KITENDO CHA KUMILIKIWA TENA, UJUE PIA MAPEPO SIO TU YAMEVAMIA, BALI YAMEZINGATIA SHERIA PIA (MAANA UNAYO CERTIFICATE OF REDEMPTION, AMBAYO LEGALLY INAWAONDOLEA UHALALI KUKAA NDANI YAKO), NAJUA MTANIELEWA, TWENDE MBELE KIDOGO.

Uhusiano wa Mungu na watu wake Israel, unalingana na uhusiano wa mume na mke, ndio maana Isaya nabii akaitangazia Israel kusema, Muumba wako ndiye mume wako (Isa 54:5). Wana waisrael walipothubutu kumtolea ibada mungu yeyote mwingine, waliitwa wazinzi/makahaba, wanaoenda kuzini mbali na Mungu wao na ndio hasa mfano ule wa Hosea kumwoa πŸ’ Gomer Bint'Diblaimu (Hosea 1:1-11).

Hosea 4 : 12b
*_maana roho ya uzinzi imewakosesha, nao wamekwenda kuzini mbali na Mungu wao._*

πŸ‘†πŸΌMungu mwenye wivu (Jealous God, anasikitishwa na tabia ya Israel kutafuta mchepuko), Yeye yupo kama mume kwao, anasikitika kwamba wameenda kuzini, mbali na Mungu wao!

*OHOLA NA OHOLIBA (Ezekiel 23:2-49)*
Mungu katika kuonesha umuhimu wa ubikira wa kiroho, ambao unaupata baada ya kuokoka, hata kama ulikuwa mzinzi kwa jinsi ya roho kabla, unapookoka na kuposwa kwa Yesu, unafanyika bikra kwa namna ya rohoni. Sasa Mungu alitumia ufunuo wa maumbo na mfano (Allegoric language) wa mabinti wawili, mkubwa Ohola na umbu lake Oholiba. Mungu akasikitika namna walivyo uharibu ubikira wao wa thamani, yaani Mungu anajua siri aliyoiweka kwenye ubikira (wa kiroho na kimwili), maana alisikitika hata namna walivyoruhusu matiti yao ya ubikira kuwa _*fondled and caressed (Eze 23:3)*_, Mungu alitaka yeye kamamume ndite awe mhusika na sio miungu ya misri wala vile vinyago vya kipagani (Pata muda usome binafsi sura yote, uone Mungu anavyoulilia ubikira wa kiroho, huo wa kimwili sio kesi yetu ya leo). Lakini mbele kidogo Mungu akaufafanua hiyo lugha ya mafumbo kuwa Ohola ni Samaria na Oholiba ni Yerusalemu, akahuzunishwa na tabia yao ya kufunua marinda (skirts) kwa kila mwanume/mungu wanaye muona, then Mungu akaenda mbali zaidi, kuwa kwa desturi makahaba wanalipwa pesa ili wafanywe hayo mambo ya kikahaba, lakini akasema watu wake Israel ndio wanaolipa pesa, yaani wao ndio wanajiuza, lakini ndio wanaolipa pesa,and the deadly worst blame, ni kwamba walifanya dhambi ya *_Promiscuity (Kuwa na wapenzi wengi)_*, yaani mara Ashuru, mara Misri, mara Babeli, mara Pekodi na Shoa na Koa etc etc 😀😀😀😀.

NDUGU YANGU MPENDWA, MIMI NAFAHAMU KAZI YA TOBA KATIKA KUKUSAFISHA UKIISHA JITAKASA. LAKINI KINACHOFANYIKA KWA MTU AMBAYE HAKUWAHI KUAMINI KABLA, NI TOFAUTI NA WEWE MKOMAVU WA KIROHO KUJIANGUSHA DHAMBINI TENA. NI RAHISI SANA KUYAONDOA MAPEPO NDANI YA MPAGANI AMBAYE AMEAMUA KUAMINI SASA, KULIKO MTU MWOKOVU AKAMILIKIWA TENA, MAANA YATAKUJA NA NGUVU KUBWA, YATAJIPANGA ZAIDI. FANYA BIDII USIWE NA MADOA NA MAWAA (SPOTS & DEFECTS), WAA LINAKUWAJE? CHUKULIA MFANO KUNA SHATI JEUPE πŸ–±πŸ‘‰πŸΎπŸ‘”LIMEMWAGIKIWA NA MCHUZI 🍲, UKALISUUZA, KUKABAKI ALAMA KWA MBALI BAADA YA KUKAUKA, HILO NDILO WAA. SASA UNAYEJAZA MAVAA KATIKA VAZI LAKO LA HARUSI (MATH 22:12), UNAPOTEZA SIFA YA KUWA BIKRA, MAANA MABIKRA WANATAMBULIKA KWA KUTOKUWA NA MAWAA (RECORD ✍🏽 ZA MAANGUKO YA DHAMBI NA ZILE ZA KUJITOA KATIKA HALI YA NEEMA. TUSOME

2 Petro 3 : 14
*_Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake._*

Ufunuo 14

*_4 Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo._*
_*5 Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.*_

*SASA MPENDWA KATIKA BWANA, BADALA YA KUENDELEA KUWAZA UANGUKE UTATUBU, BADILISHA MTAZAMO, MWAMVIE YESU NITAUTUNZA UBIKIRA WANGU KWAKO, SITAWEKA RECORDS ZA MAANGUKO YA KIROHO, NA UFANYE SALA YAKO, KUMWOMBA YULE BWANA, AWEZAYE KUKULINDA USIJIKWAE, MPAKA MWISHO UFIKE KWAKE BILA MADOA WALA MAWAA, NAYE ATAKUSUDIA (YUDA 24), EPUKA KUIACHA IMANI, EPUKA KURUDI NYUMA, EPUKA MAANGUKO YA DHAMBI, KWA KUWA SASA UMEOKOKA USIMGEUZIE YESU KISOGO KAMWE, UMWANDAME YEYE TU, HUKU UKITUNZA UBIKRA WAKO.*

```MUNGU AWABARIKI, MIMI NIMETUA MZIGO TAYARI, NASIKIA MWEPESI MOYONI MWANGU.```

*_#Team#MabikraSafi#_*

Mwl Prosper Kadewele
0762879363 (WhatsApp)

alltruth5ministries@gmail.com

HUWEZI KUULIZA KWA BWANA, UKIWA UMETENDA DHAMBI!

*HUWEZI KUULIZA KWA MUNGU, UKIWA UMETENDA DHAMBI;  HATAJIBU!*

Na Mwl Proo
*0762879363 (whatsapp)*

Bwana Yesu asifiwe wapendwa wangu. Usichoke kupokea haya mafundisho ili kuufurikisha moyo wako kwa neno jema (Zaburi 45:1).
Kuishi maisha yenye uhusiano mzuri na Mungu, hakupo kwa ajili ya watumishi ambao ni full time, hata kama wao watakuwa na muda mwingi zaidi mbele za Bwana. Lakini kila aliyeitwa na Mungu kwa njia Yesu Kristo, akazaliwa upya, anapaswa kuishi akiufurahia uhusiano wa karibu na Mungu (Mungu awe rafiki). Iko siri ya kumfanya Mungu kuwa makao yako (Zaburi 91:9), Mungu hapaswi kuwa kama mgeni mwenye kukaa usiku mmoja tu (Yer 14:8), na kumbe kesho yake hayupo.

Usiishi ukiwa na bifu (mgogoro/unsettled matter) na Mungu. Mungu ambaye ni nuru, ndani yake giza haliwezi kukaa, yaani kitu pekee Mungu hawezi ku-tolerate ni dhambi (Yesu alichukuliana na udhaifu wetu akiwa amejivika mwili wa utumwa, lakini katika utukufu anawaamuru watu wote watubu (Mdo 17:30). Wala usiwe miongoni mwa wale wanaonukuu Zaburi 130:3, kusema Bwana ungehesabu maovu nani angesimama. Na wananukuu ili kukwepa maonyo ya dhambi na uovu wanaounywa kama mtu anywavyo maji. Sasa hiyo sio ya Mungu. Kuna mambo mawili ambayo siku zote nasema hayana faida (Udhuru/excuse na Kujitetea/self-defending) mahali panapo kuhitaji uweke mambo sawa. Kama kuna dhambi inakuzinga kwa upesi (Ebra 12:1), tafuta muda kwa Bwana, mwambie akushindie na ukusudie kuiacha kabisa. Kuna uwezekano wa kuishi maisha ya standards, kiasi kwamba wewe ukijitafutiza huoni tena dhambi kwa vipimo vyako, ila utapanda daraja na kumwambia Mungu, kama iko ambayo yeye anaiona, basi akujulishe nayo unam-ahidi kuwa akikujulisha tu nayo utaiacha. Hicho ndicho kiwango tunasoma katika

Ayubu 34 : 32 *_Nisiyoyaona nifundishe wewe; Kama nimefanya uovu sitafanya tena?_*

Unapata wapi amani, ya kwenda kitandani kulala usingizi 🛌😴💤ukiwa unajua hujaweka mambo yako sawa na Mungu? Huwezi ukaendelea na shughuli zako duniani, ukiwa hujapatana bado na mwenyewe aliyeiumba hii dunia🌍. Hakika ya kwamba utaamka mzima unaitoa wapi? Nisemalo ni hili, unaweza kumfanya Mungu awe rafiki yako, na sheria zake hazitakuwa nzito tena.

*KIINI CHA UJUMBE*

MIOYO YA WANADAMU, IMEUMBIWA KUJUA KUWA IKO NGUVU INAYOWAZIDI (SUPERNATURAL POWER), NA KUWA HOJA ZAO NGUMU NA MASWALI YAO, YANA UVUMBUZI HUKO. WENGI WETU LEO WANATAMANI KUPATA MAJIBU YA MUNGU ILI WAVUKE KATIKA MASWALA MENGI MENGI KATIKA MAISHA. LAKINI HALI YAO YA KIROHO WANAYOSHUHUDIWA NA DHAMIRI ZAO WENYEWE, WANASEMA KWA HII HAPANA!!!! MUNGU HAWEZI KUNISIKIA, HATANIJIBU! TUSOME;

Ezekieli 20 : 31
*_Tena mtoapo matoleo yenu, na kuwapitisha watoto wenu motoni, je! Mnajitia unajisi kwa vinyago vyenu vyote hata leo? Na mimi je! Niulizwe neno nanyi, Enyi nyumba ya Israeli? Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sitaulizwa neno na ninyi._*

HAWA WAHESHIMIWA, WALIPOPASWA KUKAA SAWA NA MUNGU, HAWAKUTAKA, ILIPOKUJA SWALA GUMU KITAIFA, WAKAKUMBUKA YUKO MUNGU, WAKAMUOMBA NABII, KATUULIZIE KWA MUNGU. MUNGU ALIKUWA ANAWASUBIRI KWA HAMU KWELI ATOE DUKUDUKU LAKE, AKAWAAMBIA FINE!!
HIVI NINYI SIKU ZOTE MNAPITISHA WATOTO WENU MOTONI 👶🏽👶🏽👶🏽🔥🔥🔥......... KUMBUKA HIYO TABIA YA KUTOA MATOLEO KWA MUNGU MOLEKI, KWENYE BONDE LA MWANA WA HINOMU (2Falme 23:10), NI MIONGONI MWA TABIA ZA KIPAGANI, AMBAZO MUNGU ALIONYA NA KUHIMIZA WASITHUBUTU KAMWE (Kumb 18:9-11), LAKINI WAKAJITIA KWA HIZO TABIA KINYUME NA MAAGIZO YA MUNGU, THEN SASA MAJI YAMEWAFIKA SHINGONI, NDIO WANAMTAJA BWANA! MUNGU AKAWAAPIA KUSEMA, *_"KAMA MIMI NIISHIVYO, SITAULIZWA NENO NA NINYI"._* TENA WATU AMBAO HAWAKO KATIKA MSTARI, WANABAHATISHA TU, KWAMBA TUULIZE LABDA (PERHAPS) ATATUSIKIA, LAKINI MTU ASIPOHUKUMIWA MOYONI, HUWA NA UJASIRI KUWA NIOMBAPO ANISIKIA.

Yeremia 21 : 2 *_Tafadhali utuulizie habari kwa Bwana; kwa maana Nebukadreza, mfalme wa Babeli, analeta vita juu yetu; labda Bwana atatutendea sawasawa na kazi zake zote za ajabu, ili aende zake akatuache._*

UJASIRI MBELE ZA BWANA, UMEWAPOTEA KABISA, ETI LABDA MUNGU ATA...........  WAKO WATU WENGI KATIKA BIBLIA AMBAO WALITAKA KUULIZA KWA BWANA, LAKINI MAISHA YAO, YAKAWA TANZI.

〽 *TUSOMA KUHUSU MFALME WA ISRAEL*

Katika 1Falme 22:1ff, tunasoma habari za mfalme wa Israel, aluyekabiliwa na vita kubwa toka Shamu, rafikiye Yehoshafati mfalme wa Yuda, akwambia niko tayari kwenda nawe kupigana vita. Lakini uliza kwa Bwana kwanza kama kuna nabii wa Bwana. Alikuwepo Mikaya Bin'Imla nabii, lakini huyu mfalme asiyejitengeneza moyo wake kwa Bwana hakuwa radhi kumwuliza Bwana kupitia kwake, maana hakuwa katika mstari wa kimungu. Je! niupandie Ramoth-Gileadi? Hili ndilo swali la muhimu la mfalme wa Israel. Leo hii wewe unayo yako!.

〽 *TUNASOMA HABARI ZA AHAZIA*
Mfalme huyu wa Israel, taifa lenye Mungu wa kweli, kwa kutojitengeneza moyo wake kwa Bwana, alishindwa kuuliza kwa Mungu. Alipoanguka ghorofani 🏣, akapata jereha kubwa, akaona bora aulize kwa mungu Baal-zebubu wa ekroni. You know the rest of the story, of our Jealous God. Lakini shida ni nini? You cannot inquire of the Lord, if you have sinned, He can't answer!.

*UFANYE NINI SASA?*

MUNGU ANATUJUA VYEMA, HATA MAWAZO YETU, KABLA HATUJAOMBA (Math 6:8, Isaya 65:24), YEYE AICHUNGUZAYE MIOYO AIJUA NIA YA ROHO ILIVYO. MKAZO WANGU MKUBWA HAPA UPO KATIKA KUKAZA KUMPENDA MUNGU (ZABUR 91:14), KUWA NA MOYO USIOGAWANYIKA MBELE ZAKE, MAISHA YALIYOTENGENEZWA KWA KUMFANYA MUNGU KUWA RAFIKI (ISA 41:8, YOH 15:15). ILI UWE HURU KUULIZA KWA BWANA, MAANA KUNA MAMBO AMBAYO UTAYAAMUA VIBAYA, NA KUPATA MAJUTO MAKUU MBELENI. KWA UPANDE WANGU, NAJIBIDIISHA KUUTUNZA URAFIKI NA MUNGU, AND AS THE MATTER OF FACT, MAMBO MENGI HATA BILA KUMUULIZA RAFIKI YANGU MUNGU, ANANISHAURI MAPEMA. NIKIWA NINA JAMBO NIMELITIA MOYONI, KABLA SIJALIPELEKA KWAKE ATANIWAHI, ATASEMA PROO HOLD ON! ✋🏾 THAT IS NOT. NA KWA SABABU YA UBIZE WA MAMBO YA MAISHA, HATA KAMA NIKIWA NINA LISAA LIMOJA LA KULALA 😴💤. HUWA NAMWAMBIA RAFIKI YANGU MUNGU, NAOMBA UUTUMIE HUU MUDA, KAMA KUNA MAMBO NAPASWA KUYAJUA NIJUZE BASI, NA NIKISHTUKA USINGIZINI NINAKUWA NA KAZI YA KUFANYA ANALYSIS JUU YA MAMBO KADHA WA KADHA, AMBAYO BWANA AMEYALETA. AND OUR GOOD-GOD IS ALSO SOCIAL-GOD, USIMDHANIE YUPO COMPLICATED (BWANA MGUMU 😡), MWENYE MIHASIRA YAKE, NO! AKIWA RAFIKI, ANAANZA KUJISHUGHULISHA NA VITU AMBAVYO NI VYA KAWAIDA SANA. JANA NIMEAMKA ASUBUHI, MUNGU PAMOJA NA VITI VINGI VYA KIROHO ALIVYONISEMESHA, ILA ALINIPA MAELEKEZO MPAKA KUHUSU MAJI YANGU, NINAYOHIFADHI KWENYE DIABA NA YALE YA KWENYE NDOO, HAPA KWENYE NYUMBA NILIYOPANGA (KULIKUWA NA HOJA ZA KIUSALAMA FULANI, SIKUZIWAZA,TENA AKANI-DIRECT NIBADILI HATA MTU ANAYENIUZIA MAJI. OK NIYAACHE HAYO, LAKINI MUNGU YUKO SO SOCIAL, UKIWA MBABAISHAJI KIROHO, KILA UKIENDA UTAMWONA NA SURA YA UKALI 👉🏾😒, WAKATI HE IS SUCH A FINE-FACED GOD 👉🏾😊

Mungu awabariki, mimi nimemaliza kwa leo.

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

ULIMWENGU WA ROHO

*UJUZI KUHUSU ULIMWENGU WA ROHO, UTAKAO KUWEZESHA KU-OPARETI (TENDA KAZI) KWA KIWANGO CHA JUU ZAIDI*

*_Mwl Proo_*
0762879363

Haleluya Haleluya!!
Naomba tuingie darasani. Jambo moja la ajabu, kuna mambo ambayo Roho Mtakatifu hawezi kukutumia, mpaka upate mtu akufundishe ujuzi (experience). Unaweza kufundishwa kwa usahihi jambo fulani, then likaanza kutenda kazi kwako kwa nguvu. Nilikuwa na rafiki yangu mwana maombi wa kufunga kavu saba mara kwa mara anaitwa Willick Gervas, sijui yuko wapi sasa. Lakini alikuwa na shauku ya kunena kwa lugha mpya kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, haikutokea. Siku tuliyokaa mpaka saa tano usiku, tukiwa tunafundishana habari za ujazo wa Roho Mtakatifu, ikafungua njia. Kesho yake tulienda kwenye kapori fulani (mzeituni), ambako tulikuwa tunafanya maombi huko Pugu Sekondari, akiwa na ufahamu kamili sasa. Tulipoanza kuomba, mimi nilisikia sauti kama gariπŸš™ limetufuata porini, na hakuna njia ya gari, sauti ilikuwa ya sekunde mbili tu vuuuu, ilipokata nikamsikia keshakamatwa lugha imebadilika. Kwa hiyo nakualika katika darasa hili la leo, maana kuna mambo yamekaa pending (yako suspended), yanasubiri uwe na maarifa.

MKRISTO ASIYE NA UJUZI KUHUSU ULIMWENGU WA ROHO, ANAISHI CHINI YA VIWANGO, HAPIMIKI KWA MIZANI YA KIROHO. NAMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YA MTUME PAULO, AMBAYE MUNGU ALIMTUMIA KUTUWEKEA HABARI NYINGI ZA IMANI SAWA, TUPO BIZE KUJADILI KARAMA ZA KIROHO, HUDUMA ZA BWANA, LAKINI MTU ALIYETUMIWA KUWEKA HIVI VITU KWA STANDARD YA MTAALA KAMILI, NI MTUME PAULO, PETRO KWA KUWA HANA KINYONGO AKAM-VOUCH UPπŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½ PAULO, KWA NYARAKA ZAKE KAJAZA SIRI AMBAZO DAAH!!! (2Petro 3:15-16).

Sasa ni mtume Paulo pekee ameutaja ulimwengu wa roho kwa jina la wazi kuwa unaitwa ulimwengu wa roho, katika barua moja tuu ya Waefeso, ambako limejitokeza mara tano (Efeso 1:3, 20, 2:6, 3:10, 6:12). Wengine wote walitaja tu kuwa wameona hiki na kile bila kusema ni wapi huko, akiwemo Yesu, alisema tu nilimwona Shetani akianguka kama umeme toka mbinguni (Luka 10:18). Katika Agano la Kale, ulimwengu wa roho umetajwa sehemu nyingi lakini, kwingine ulitajwa tu mbinguni, ukiwa na maana ya ulimwengu wa rohoni, na ndio maana kwa kiingereza hutajwa kama heavenly realm (spiritual realm), mfano:-

Waamuzi 5 : 20 *_Walipigana kutoka mbinguni, Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera._*

KATIKA MSTARI HUU (AMU 5:20), NI WIMBO BAADA YA USHINDI. VITA VILIONGOZWA NA NABII MKE DEBORA. JAMBO LA KUSHANGAZA NI HILI, JEMEDARI MKONGWE WA VITA AITWAYE SISERA THE COMMANDO, ALIKIMBIA KAMA KICHAAπŸƒπŸΎπŸ’¨, NA BADO AKAUAWA NA MWANAMKE (Yaeli) AMBAYE ANAOGOPA HATA PANYAπŸ€. KILICHOLETA USHINDI NI KWAMBA VITA VILIPIGANWA KUTOKA MBINGUNI (ULIMWENGU WA ROHO), KULIKUWA NA NYOTA (MALAIKA) WALIOONGEZA PRESHA UPANDE WA ADUI ILI WAKONG'OTWE. HAYO NITAELEZA MBELE ZAIDI.

Ulimwengu wa roho, umegawanyika sehemu mbili, upo ulimwengu wa roho wa nuru, na upo ulimwengu wa roho wa giza. Ulimwengu wowote katika hii unamaanisha usioonekana, ila tofauti hiyo imetokana na akina nani watendaji waku na ufalme unaoutawala (main actors/controller). Wanao-opareti katika ulimwengu wa roho wa nuru, wanaweza kuuingia (access) na ule wa giza wakafanya watakayo, ila wale wa giza wana limit katika huu wa nuru. Kwa mfano mazingara/mazingaombwe (Conjuring) mengi yanahusisha kufunika mambo katika ule ulimwengu wa giza, kwa hiyo watu wa macho haya mwili, hawaoni. Nakumbuka aliyekuwa mratibu msaidizi wa Casfeta mkoa fulani, akiwa kwenye huduma kijiji fulani, eneo la soko na vilabu vya pombe. Roho Mtakatifu akamwambia angalia juu ya mti 🌳, akaona mtu mzima amefungwa anahangaika, lakini watu wote wanaendelea na biashara hawamwoni. Yeye alifunguliwa macho kuona, kisha Roho wa Yesu, akamwambia unaona wale wazee wanaocheza bao pale chini? Wale wamemwandaa wamtumie kama biskuti yao πŸ˜‹πŸͺ uaiku wa leo. Hakuagizwa kufanya chochote. Ila anajua kuwa aliliwa na wachawi usiku huo.

SASA VIWANGO VYA KIROHO VYA MTU, VITAMPA KU-OPARETI KWA NAMNA KUBWA AU NDOGO KATIKA ULIMWENGU HUO.

▶WAKO WATU AMBAO HUWEZA KUYAOMA MAMBO YA ULIMWENGU, MPAKA WAWE USINGIZINI, ILI WAOTESHWE AU ROHO IHUDHURISHWE KATIKA ULIMWEGU HUO.

HILI NI KUNDI KUBWA ZAIDI, NA SIO KWAMBA HII LEVEL INAFAA, LAKINI KUKISEKANA KWA MAFUNDISHO YA UJUZI, NA MAARIFA SAHIHI, NA KIWANGO KIDOGO CHA UWEZO WA KIROHO, MUNGU HUTUMIA NJIA HIYO, ILI WASIPITWE KABISA.

▶WAKO AMBAO MACHO YAO YA NDANI YAMETIWA NURU FULANI πŸ‘πŸ‘πŸ’‘.

HAWA HUWEZA KUONA MAMBO YA ULIMWENGU WA HATA KAMA AMEKAA KWENYE BASI 🚌. KUNA KUWA NA UWEZO MKUBWA WA KUONA KWA MFUMO WA PICHA, VIDEO NA KADHALIKA. HIKI NI KIWANGO CHA KATI NA NI KIZURI TUU.

▶WAKO AMBAO, SIO KWAMBA WAMETIWA NURU πŸ‘πŸ’‘, BALI WANA MACHO KAMILI YA ROHONI YENYE FULL SIGHTINGπŸ‘πŸ‘. WENGINE WANATEMBEA BARABARANI NI KAMA WAPO NA SCREEN πŸ“ΊπŸ–₯, DARUBINI πŸ”­πŸ”¬πŸ•Ά, NA HIVYO HUWEZA KUONA BILA KIZUIZI CHOCHOTE. ANAWEZA KUWA ANAOMBEA MIFUPA YA NYONGA ILIYO DISLOCATED AKIWA ANAIONA KAMA IMEUNGA, IMESOGEA MAHALI PAKE AU LA, ANAWEZA KULIKEMEA PEPO NDANI YA MTU, AKAJUA LIMEKIMBILIA KIUNGO KIPI CHA MWILI BILA PHYSICAL INDICATION. (HIKI NI KIWANGO KIZURI NA CHA JUU). HAYO NIMEELEZA KWA KINA KATIKA LILE SOMO LANGU LA *_WAENDAO KWA MIGUU WAMEKUSHINDA, JE UTASHINDANA NA FARASI ?(HAKIKISHA UNAPATA SOMO HILO)_*

Sasa namna pekee ya kuenjoy maisha ya kiroho na huduma, ni kwa kuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu ulimwengu wa roho. Na unapopata maarifa ya kutosha kuhusu huo ulimwengu ndivyo namna yako ya kuoparet ina-improve.

Siku moja nilikaa kitandani, kuna andiko nilikuwa nasoma silielewi. Narudia tena huo msamiati hadi nikafikiri umekosewa,  ghafla, nikaona ndani ya sekunde mbili kama movie πŸ“ΊπŸ“Ό, nilichokiona kilifafanulia ule mstari nikauelewa vizuri sana. Sasa ulimwengu wa roho hauna umbali. Hauhitaji safari. Nikinukuu maneno ya Askofu Silvester Gamanywa, alisema,  *_"hata pua na mdomo viko mbali sana, ukilinganisha na tulipo na ulipo ulimwengu wa roho"_* Kwa maneno mengine hakuna distance, lakini mtu anahitaji tu awe transformed au awe na macho mengine.

*KWA NINI UUPATE UJUZI KUHUSU ULIMWENGU WA ROHO NA MACHO YA ROHONI?πŸŒπŸ‘πŸ‘*

▶Mambo mengi yanayotokea katika ulimwengu wa mwili, yalishafanyika katika katika ulimwengu wa roho.
Kuna rafiki yangu nikiwa Sekondari, aliacha wokovu, lakini tukiwa likizo ndefu, Mungu alinionesha katika ulimwengu wa roho, ameacha mapambano, nilimwona anaweka silaha chini, wakati mapambano yamepamba moto. Hivyo Ukiufahamu ulimwengu wa roho vizuri, unaweza kufuta matukio mengi utakayoyaona katika ulimwengu wa roho, utafuta vifo kwa walioandikiwa kufa kinyume na mapenzi ya Mungu, utafuta ajali na uharibifu wowote wa maadui. Unaweza kulibadilisha jambo huko kabla halijatokea katika ulimwengu wa mwili.

▶Macho ya rohoni yatakusaidia kupata picha na videos, katika ulimwengu wa roho. Pia yatakusaidia kuelewa ujumbe ambao umekujia na hujauelewa vizuri. Jumbe nyingi za kiroho zinaambatanishwa na vielelezo (illustrations). Usiku wa leo, majira ya saa nane na nusu usiku, nikiwa naomba, nikasikia ndani kwangu sauti imesema *_Dakika 5_*, muda huohuo pembeni niliona vipimo kama timazi (ruler) ikipima huo muda, na roho wa ufahamu, alinisaidia kuelewa kwamba napaswa kunyamaza dakika 5 bila kuomba. Nikakaa dakika moja mbili, huku nikiuliza kwa Roho Mtakatifu, Je kuna jambo unataka kunifundisha? Nilipoona kimya nilifanya kosa la kuiruhusu akili yangu inihubirie. Nikahoji mmmmh kweli Mungu anistopishe kuomba???? Nikaanza kunukuu mistari michache kama ile ya Ombeni bila kukoma (1Thes 5:17, Luk 18:1). Lengo ilikuwa ni ili niendelee  kuomba, kunyume ja lile katazo. But haikupita dakika mbili, nilisikia mlango wa nyumba jirano ukifunguliwa, nikakaa kimya, na kwa kuwa madirisha ni ya vioo tupu, nilifunua pazia, na niliyoyaona nikaelewa kwa nini, nilipigwa break kwa dakika 5 nisiombe. Kwa maana wangesikia kelele ya maombi, wasingefanya walichofanya.

▶ *MAMBO MENGI YAKO HALISI ZAIDI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, MITEGO NA SIRI NYINGI ZITAFICHUKA KWAKO, UKIWA NA UJUZI WA KUTOSHA*

Kuna baadhi ya watu, wamekutwa na majanga, maana viashiria vyote katika ulimwengu viliwapita, yaani decoder/ving'amuzi vyao vilichelewa kudaka taarifa, mpaka wakala chakula cha sumu, wakaingia kwenye ajali, wakategeshewa kichawi wakanasa. Ni muhimu sana kuufahamu ulimwengu wa roho na kuwa na macho ya rohoni.

*UFANYE NINI, UANZE SAFARI YA KU-OPARETI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO KWA VIWANGO?*

✔Jizoeze kuzingatia mambo ya kiroho.
Yaani unayoyaona katika ndoto, unakuwa bize kuyaombea. Tabia hiyo itafanya Roho wa kweli, aongeze ufunuo juu ya yale uliyoyaona.

✔Maombi ya kina (kuzama) katika roho. Ni muhimu sana kuwa na maombi ya binafsi, ya kuomba katika Roho (Yuda 1:20). Kuomba katika Roho, niliwahi eleza ina maana gani *(Pata somo la NAMNA YA KUIJENGA NAFSI)*

✔Epuka kujaza mambo machafu nafsini mwako (moyoni/akilini), kwa kupitia milango ya kuingiza vitu nafsini, kama macho na masikio (Zab 119:37, Kumb 28:34). Ili antena zako zisijase chengachenga katika ulimwengu wa roho, yakatae mambo ya aibu (2Kor 4:2), Usiruhusu uchafu hemani mwako.

✔Jifunze kwa watumishi waliokutangulia, waulize maswali juu ta yale unayotamani kujua, kumbuka kuna viwango utaanza ku-opareti baada ya kuelezwa hayo mambo yanfanyikaje, ingawa wapo ambao Roho Mtakaatifu atawafundisha direct, kulingana na mission yao na wito wao kwa Bwana.

✔Punguza kuwa mtu wa maneno mengi, kuruhusu nafasi ya kusikia zaidi (Yakobo 1:19, Mithali 10:19). Mtu mwenye kelele na maneno mengi, signals za kiroho nyingi zitampita bila kushtuka. *_The less you speak your feelings, the more  you get revelation_*

*Tutaendelea.......*

Mwl Prosper Kadewele
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

WAKATI UMEWADIA WA KUMTAFUTA BWANA

*WAKATI UMEWADIA WA KUMTAFUTA BWANA*

πŸ‡² πŸ‡Ό πŸ‡±  πŸ‡΅ πŸ‡· πŸ‡΄ πŸ‡΄
*0762879363*

©2015

Nakusalimu mtakatifu wa Mungu, wewe ambaye Mungu, alipendezwa kukufanya wake. Ubarikiwe kwa jina la Yesu.

Neno la Bwana lililonijia ni hili; Katika zama hizi za uovu (Efe 5:16), watu watakaojitoa kumtaja Bwana katika kweli, watamwona Mungu kwa namna ya ajabu sana sana!. Yaani katika zama hizi zilizojaa uchafu wa kutamani na harufu ya zinaa kona zote, zama ambazo kukuta   bikra ni muujiza, zama ambazo watu wanafunga ndoa na ujauzito tumboni, zama ambazo teenagers wote wameathiriwa na uchafu wa sinema za ngono, zama ambazo vijana hata waliookoka wako bize na sexchat, zama ambazo ngono za watu wasiopaswa kuhusiana kama mtu na shemeji yake (zinatungiwa nyimbo kuhamasisha kwamba hainaga ushemeji), zama ambazo watumishi wa madhabahu wamejizamisha kwenye matendo ya ngono mpaka kwenye vyumba vya ushauri na maombezi, zama ambazo wahubiri wameacha kutafuta Neno kwa Bwana, wanasaka mahubiri Google πŸ”ŽπŸŒ, ndio maana wanaishia kuwatabiria watu wachafu kiroho, baraka za kimungu, zama hizi ambazo Shetani amehakikisha anapunguza makali ya wahubiri moto, kwa kuwazamisha nao katika uzinzi (Hakuna mwinjilisti aliyeanguka kwenye uzinzi, mwenye uwezo wa kukemea dhambi kwa standard stahiki, atang'ata kidogo na kupuliza mwenyewe), katika zama hizi ambazo television programs zote zimejawa na sex-sceens, sex-talks, sexy-dresses na mauchafu yote, you name them!  *_Sasa katika zama hizi, mtu atakayesema mimi dhambi na uchafu πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½, atakaye sema moyoni nwake kuzini NoooπŸ‘πŸ½, uongo NoooπŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½, dhambi zote No! na akajitia nia na moyo kumtafuta Bwana katika kweli, hakika yake Bwana ataonekana kwako kwa namna ambayo hata kwenye Biblia hujaisoma. Yaani hapo inaitwa umetoa kisafi kutoka katika uchafu huu mwingi, Mungu ameahidi kukufanya     spokesman wake. Si hivyo tuu bali atakufanye uwe kati ya watu wasimamao karibu yake..._*

Yeremia 15 : 19
*```Kwa sababu hiyo Bwana asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.```*

Zekaria 3 : 7
*```Bwana wa majeshi asema hivi, Kama ukienda katika njia zangu, na kama ukishika maagizo yangu, ndipo utakapoihukumu nyumba yangu, nawe utazilinda nyua zangu, nami nitakupa nafasi ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.```*

*MOYO WA UJUMBE*

Hosea 10 : 12 *_Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki._*

*✔JIPANDIENI KATIKA HAKI*
Haki hiyo inayotajwa wajipandie (wahakikishe wako/wamesimama katika haki, ni ile ipatikanayo kwa matendo ya sheria-Mosaic Law), lakini kwetu leo ile haki ambayo ilipaswa kupatikana kwa juhudi za matendo, tumeipata yote bure kwa kumwamini Yesu (Mdo 13:39). Zaidi ya yote, Mungu alimfanya Yesu, ambaye haijui dhambi, awe dhambi, ili sisi tuwe haki ya Mungu (2Kor 5:21).

*✔UCHIMBUENI UDONGO WA MASHAMBA YENU*
Anazungumzia readiness (Utayari wa kupokea toka kwa Bwana) kama kuna mambo uliyaacha ya haki, anza kuyatenda tayari kwa kukutana na Bwana (Break up your fallow ground), udongo wa shamba hili ulikuwa _*fallowed*_, ulipumzishwa bila kufanyiwa kazi, Sasa majira ya kukutana na mvua ya Mungu kiroho 🌧☔ yakija, Bwana anataka uchimbue huo udongo wa maisha yako ya kiroho. Kama uliacha kusoma neno, anza upya, kama uliacha kuomba na kufunga, anza upya, kama uliacha kumshuhudia Yesu, anza upya!.

*✔KWA MAANA WAKATI UMEWADIA WA KUMTAFUTA BWANA*
Ndugu yangu saa ya kwenye ulimwengu wa roho⏰, inasema hivi sasa ni saa ya kumtafuta BWANA (Day&Night). Na wakati huu anapatikana, nakusihi msomaji wangu, usiwe miongoni mwao wanaositasita (Ebrania 10:39). Usiwe miongoni mwa wale ambao wamemruhusu Shetani kavuruga mawimbi(waves) za kiroho, wananasa chenga na kukosa clear vision. Jitunze kwa Bwana katika hizi zama za uovu, Mungu anapatikana sana tuuuu

Isaya 55 : 6
*_Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;_*

Sefania 2 : 3 *_Mtafuteni Bwana, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana._*

IKIFIKA HAPA, NDIPO NINAPOTAMBUA, KUWA KUNYAKULIWA SIKU YA UNYAKUO SIO BAHATI NASIBU, HUWEZI UKAISHI KWA ULE MSEMO WA *_"what will be, will be!"_* ETI LIWALO NA LIWE! KWA NINI USIBIRO AJALI, WAKATI MUNGU ANAPATIKANA SASA, NA UNAWEZA KUJIHAKIKISHIA UHUSIANO WAKO NA MUNGU SASA. MTU ASINITISHE MAANA YULE MUNGU WA BIBLIA, NAMWITA ANASHUKA KUNITENGENEZA MAISHA YANGU KILA SIKU. KWA HIYO SITASHTUKIZA ACCIDENTALLY KWAMBA MUNGU NIFIKIRIE, KAMA UHUSIANO NA MUNGU, UNA SHIDA NIUJENGE SASA!!! TENA NIWASIHI SANA, MSIACHE KUFANYA HUDUMA ZA KIROHO KATIKA KWELI, MAANA ZINA MCHANGO WA KUUTUNZA WOKOVU WENU. KWA MFANO MIMI SIWEZI KURUHUSU DHAMBI, UPUZI NA UDHALIMU KATIKA HEMA YANGU (MAISHA YANGU), MAANA NAJUA KUWA NAPASWA KUFANYA HUDUMA YA ROHO, KAMA HII. SASA HATA UJUMBE WA KUANDIKA NAJUA NAPASWA KUULIZA KWA BWANA, SO NAOGOPA KAMA NITACHAKACHUA MAPITO YANGU, NIKIMUULIZA HATANIJIBU (YOH 9:31, ZAB 66:18), NA SIPO TAYARI KUACHA MUNGU AONDOKE ANIACHE, NILIKUJA KWAKE KAPUKU (EMPTY SET), SASA KANIJAZA KILA WEMA NA UNONO.

Kungekuwa na Mana na Kware wanaoanguka tu wenyewe, natamani kazi yetu ingebakia kumtafuta Bwana tu. Sasa bado tunayo masumbufu ya maisha haya, unyakuo huenda usiwe labda hata usitokee for the next 500 years (ingawa hata ukitokea sasa tuwe tayari), kwa hiyo ni lazima na maisha tuyasake, tusife njaa kwa kusingizia imani. Lakini pamoja na cash unazosaka, MUNGU KWANZA, UFALME KWANZA (Luk 12:31)

Kijana wa kiume na wa kike, wewe mama na baba, hauna sababu ya kutomtafuta Bwana. Tena kama Mungu amekujalia ahueni kiuchumi, utulivu kwenye ndoa, wewe ndio umepewa neema hiyo ili umtafute sanaaaaaaaa. Maana wengine wenye majanga watamtafuta awaponye na majanga, ila wewe unamtafuta ili ukae na Bwana... Wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, natamani kuona vijana wako bize na ratiba za maombi na kufunga na huduma. Muda wa kuzunguka mlima Seiri kupoteza muda, mmezunguka sana, SASA VYATOSHA, SASA YATOSHA (Kumb 1:6, 2:3ff)

Mungu akupe neema kila mmoja, inuka sasa umtafute Bwana, maana shughuli hiyo inakuhusu wewe. Uaipojiingiza katika wingi hili la kumtafuta Bwana, utabaki kushinda na tudhambi ambazo wenzio tulishasahau zinafananaje.

KARIBUNI SANA, TWENDENI BARAZANI PA MUNGU.

Mwl Prosper Kadewele
0762879363( All Truth Whatsapp Group)

alltruth5ministries@gmail.com