Thursday, December 22, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 7)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA SABA*

*CHANZO CHA NGUVU*

Mwandishi: *Mwl Proo*

Mmebarikiwa ninyi nyote mnaoendelea kuufuatilia mfululizo huu. Leo nimepewa kuzungumzia nguvu na chanzo chake.

Nguvu zote zilizopo, zilizokuwapo, zitakazokuja zote (za zamani zijazo) ni za Mungu, chanzo cha nguvu zote ni Mungu. Hata nguvu zinazotajwa kuwa ni za shetani (Mdo 26:18) zote ni za Mungu, na chanzo cha nguvu hizo ni Mungu. Suala la shetani ku-manipulate, au kuzitumia nguvu alizopewa kwa uovu, haibadili ukweli kama chanzo cha nguvu hizo ni Mungu. Hata zile nguvu maarufu ziitwazo za asili (natural powers), chanzo chake ni Mungu, ni za Mungu... Kama kuna nguvu inaizungusha dunia bila kupungua spidi yake, kama kuna mikandamizo ya hewa kukaleta upepo, kama kuna nyota na sayari katika miendo yake kuna aliyeamuru viwe vikawepo, alipoamuru aliruhusu nguvu zake kutekeleza na kuyashikilia mambo yote kwa uratibu wa hali ya juu (Isaya 40:26, Zaburi 8:3)

Andiko la Warumi 13:1b linatumia neno _'exousia_' kutaja uweza/nguvu/mamlaka. Neno hilo limetumika mara 29 katika Agano Jipya la Kiyunani na mara nyingine limetumika kwa kubadilishana (interchangeably) na neno dรฝnamis (dunamis ๐Ÿ‘‰ specifically to perform miracles) likitaja nguvu. Andiko hilo katika versions nyingi (mfano: KJB,  ASV, DRM) linasomeka, _Hakuna nguvu ila za kutoka kwa Mungu tu_
*For there is no power but of God: the powers that be are ordained of God.*

Nguvu za Mungu zinaweza kuwekwa katika vitu kutekeleza makusudi fulani fulani. Kwenye Biblia yote Agano Jipya na la Kale, viko visa vingi ambavyo nguvu za Mungu ziliruhusiwa kuwepo (transmit) katika vitu na vitu hivyo vikatumiwa kutekeleza kazi iliyokusudiwa. Hebu fikiria kisa cha Elisha katika 2Wafalme 4:29ff... Elisha alitransmit nguvu za Mungu kwenda kwenye fimbo yake, akampa Gehazi akamgusishe mtoto aliyefariki, ili afufuke. Nguvu za Mungu ndani ya Elisha hazikukaa tu ndani ya roho na nafsi yake hai, bali hata mwili, damu, nyama, na mifupa yake (soma 2Wafalme 13:21) utagundua mifupa yake ilisalia na nguvu zilizoweza kufufua mtu yeye akiwa amekufa kwa homa siku nyingi. Tunasoma katika Matendo 19:11, leso na nguo ambazo zilimgusa Paulo zilipelekwa kwa wagonjwa wakapona, na pepo wabaya wakawatoka. Matukio kadhaa yanaonesha nguvu za Mungu ndani ya watu zilikuwa transmitted kwa vitu (kumbuka kisa cha chumvi kwenye chanzo cha mto huko Yeriko, kumbuka kisa cha unga uliotiwa sufuriani ili kuiondoa mauti, kumbuka  pindo la vazi la Yesu, tope lenye mate ya Yesu, birika la Bethzatha na mengine mengi). _mwlproo_

Kuna upotoshaji mwingi unaotokana na kukosekana kwa maarifa. Kuna makelele mengi yanaleta aibu kama sio huzuni. Leo hii tuna watu ambao hiki kitu wamekipokea kimakosa utasikia sabuni, utasikia mafuta, utasikia maji, utasikia pipi, utasikia keki, utasikia stika, utasikia chumvi, utasikia udongo, utasikia kitambaa cheupe.... Vyote hivi vitaenda kwa jina la upako... Kwa miaka mingi vimekuwa vikiitwa visaidizi (erroneously), na miaka michache iliyopita nilimsikia mhubiri mmoja wa Dar akiviita vifaa vya kiroho, jina ambalo sasa linatumiwa na wengi. NDUGU ZANGU WAKRISTO VITU NILIVYOTAJA HAPO JUU VYOTE HAVINA NGUVU. NGUVU ZIKO NDANI YA WATU, NA WATU NDIO WANAOWEZA KURUHUSU NGUVU ZILIZO NDANI YAO ZIENDE KWENYE VITU (TRANSMISSION), NA KURUHUSU NGUVU ZIENDE KWENYE VITU KIBIBLIA NI PALE TU ROHO AMEKUPA UFUNUO (NENO LA HEKIMA) KWAMBA SHIDA HII IHUDUMIE HIVI ZIRUHUSU NGUVU ZIENDE KWENYE MAJI AU CHOCHOTE KIWE NA CONTACT NA MWENYE SHIDA TATIZO LIKAONDOLEWA, AU KWA NAMNA ILIVYO KATIKA MAZINGIRA NI NGUMU KU-ADMINISTER HUDUMA ZA KUPONYA NA MATENDO YA MIUJIZA KWA NENO LA IMANI, KWA KUOMBA, KWA KUWEKA MIKONO NA NAMNA NYINGINE YA UTENDAJI. HIZI NI NAMNA MBILI KWA MUKTADHA WA UKRISTO VITU HIVI VYAWEZA HAMISHIWA NGUVU ZILIZO NDANI YA MTU KURUHUSU VIKATENDE KAZI.

Dramas zinazoendelea leo hii Afrika ni nyingi mno. Wakristo wanakimbizana na hivi vitu kiasi cha wao kupumbazika kabisa kubakia watumwa mara billion ya walivyokuwa kwanza. Nilipewa ushuhuda wa mama aliyemwaga chumvi yake ya upako bahati mbaya na akasikitika sana na kilio juu. Nilishuhudia kwa macho yangu mhubiri mmoja huko Dar, aliivua tai yake ๐Ÿ‘”  na kuirusha kwa watu kwamba ina upako (sikatai maana upako unahamishika), lakini iligombaniwa sana na washirika, na kijana mmoja alifanikiwa kutoka nayo nje,  katika vutavuta mwingine aliikata kipande... wamama wawili wakamwomba wamlipe laki 3 awaachie kipande hicho cha tai. Dramas hizi za vile vinavyoitwa visaidizi au vifaa vya kiroho ziko Afrika kuliko mahali pengine popote palipofikiwa na pentecostal & charismatic movements, kwa nini haswa?

 Hapa Afrika vimekuwa maarufu kwa sababu ya imani za asili au za kienyeji kwa jamii ya watu wa Afrika. Maishani mwangu nilipata neema ya kusomea dini za asili za Afrika (African Traditional Religion ๐Ÿ‘‰  ATR). Kwenye dini zetu za asili na tamaduni vitu vya kuonekana, vya kushikika, manuizo, matambiko, ulozi, na mengine mengi yaliyohitaji vitu vya kuonekana yalihitajika sana. Fikiria jamii ambayo ilizoea wakitoka kwa mganga wa kienyeji,  wamechanjwa miili, wamepewa vitu vya kutia kwenye maji ya kuoga, wamepewa vitu vya kufunga mikononi, viunoni, shingoni, wamepewa vitu vya kulalia chini ya kitanda, cha kupaka ukutani, cha kumwaga na kunuiza kwenye kuta za nyumba, cha kuweka darini na kadhalika.... Haya yamekuwa mambo ya kawaida kwa karne nyingi Afrika, yamerithishwa vizazi vingi kiasi cha kuwa ni kama kitu cha kuzaliwa nacho. Kila atakayekuja Afrika akawa na vitu tangible vya kugawa kwamba vina nguvu za kusaidia atake au asitake lazima atafanikiwa kupata ufuasi mkubwa maana imegusa asili ya Afrika. Hapa sasa ndio sababu haswa ya kila mhubiri kwa sasa anakomaa na vitu hivi.. Hata mahali ambako angeweza kumgusa mgonjwa kwa mkono wake, atamwagiza ashike kitu, hata mahali ambako angetamka tu 'kansa kauka'... atatafuta kwenye briefcase ๐Ÿ’ผ  chupa cha mafuta aliyoyabeba toka Israel bila hata maelekezo ya Roho wa Yesu (mtu akiongozwa na anaweza kuthibitisha hilo hakuna tatizo) Lakini 95% ya watumiaji wa hivi vitu, hawana maelekezo yoyote ya Yesu... wanaunga-unga na kujaribu-jaribu tu, mambo yakitokea kweli wanaendeleza bila kujua nguvu zipo ndani yao.. Na matokeo yanatokea si kwa sababu wapo sahihi... Ni kama tu mtu kunywa sumu akiamini ni juisi tu, haitazuilia sumu kufanya kazi yake ya kumwua, au mtu anywe maziwa akiamini ni maji tu, haitaizuia maziwa yasimpe nutrients zinazopatikana kwenye maziwa. Lakini tatizo limekuwa kwenye kufanya waamini wasijue kuwa nguvu ziko ndani ya watu si ndani ya hivyo vitu.. Niliongea na rafiki yangu mmoja ambaye dada yake ni mhudumu (usher) kwenye huduma moja ya maombezi. Alisema waliuza maji ya uhai (katoni za kutosha) ambayo yaliombewa na mtumishi wiki nzima, yakaisha na watu bado walikuwa wengi, hivyo ikabidi maji yakanunuliwe direct toka dukani na kuuzwa kwa watu kama maji ya upako... bila hayo maombi ya siku saba. Guess what! Kwa sababu ya imani ya miujiza ndani ya hawa watu haya maji yaliyotoka dukani directly yakipelekwa kwa wenye shida yanawezaleta shuhuda pia. Lakini ufahamu wa juu kabisa kwa waamini ni kufahamu nguvu zote hizo ni za Mungu, na jamaa ya waamini (WOTE) walipobatizwa katika Roho wa Kweli nguvu hizo bila kipimo zilikuwa superimposed ndani yao. Waamini wote wanazo hizo nguvu, utendaji utatofautiana tu kulingana kiwango cha maarifa, na unafanya nini katika ufalme, na Roho Mtakatifu amekupea karama zipi, au wewe mwenyewe unatembeaje katika kutumia vilivyowekwa ndani yako tayari. KWA KUSEMA HIVYO WAAMINI HAWANA HAJA WAO WENYEWE KUKIMBIZANA NA CHOCHOTE, MAANA NGUVU ZENYEWE ZIKO NDANI YAO. KAMA KUNA NGUVU ZIPO KWENYE UDONGO WA ISRAEL, AU MAJI YA YORDAN, AU SABUNI, AU CHUMVI AU KITAMBAA KILICHOOMBEWA, NGUVU HIZO SI KWA AJILI YA MKRISTO YEYOTE MKOMAVU, MAANA YEYE MWENYEWE NDIYE MZALISHAJI WA HIZO NGUVU KUTOKEA NDANI YAKE ZIKASAIDIE WALIOFUNGWA NA ADUI HUKO NJE (YOH 7:38). MWAMINI ANAYEHISI KUWA KWA POSTI HII NINAWAPINGA WAO AU MHUBIRI YEYOTE HONGERA YAKE KWA KUCHAGUA KUWA MTUMWA WA DAIMA.. ENJOY YOUR SLAVERY, REMAIN CAPTIVE TO IGNORANCE. MIMI BINAFSI NGUVU ZIPO NDANI YANGU, NIKISTULIWA SAA NANE USIKU KUTOA HUDUMA YOYOTE YA KIROHO, NITATOKA NIKIWA NA NGUVU ZOTE BILA KUHITAJI KUTAFUTA KICHUPA FULANI ETI NIMEKIFICHA  KWA KABATI, HATA BAADA YA KUTRANSMIT NGUVU KWENDA KWENYE VITU, NIMEPEWA UWEZO KUJI-RECHARGE ๐Ÿ”Œ  ๐Ÿ”‹  MIMI MWENYEWE SI MIMI KUTEGEMEA VINGUVU NILIVYOVIHAMISHIA KWENYE KITU.


Tukutane sehemu 8, kuna mambo mazuri utayafahamu


alltruth5ministries@gmail.com

Tuesday, November 15, 2022

SWALI NA JIBU (KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*

_*Majibu ya swali nililoulizwa na mchungaji mmoja kwa inbox, kufuatia sehemu ya tano ya somo letu*_

Kufuatia sehemu ya tano ya mfululizo wa somo letu la *Kulitumia Kwa Halali Neno La Kweli*, sehemu iliyojikita kuzungumzia *UTOAJI/MATOLEO* nimeulizwa na mchungaji mmoja kuwa Je! kwa namna hiyo niliyofundisha mapato hayatapungua na kurudisha kazi ya Mungu nyuma?

Niseme hivi, watu wanachofanya sasa hivi ni matokeo ya mafundisho, utoaji uliopo sasa hivi (wa kichoyo) ni matokeo ya mafundisho (tena yenye makosa). Kwa fundisho sahihi la Ukristo juu ya utoaji lililojikita juu ya ukarimu (generosity), kanisa wala wahudumu wa injili hawakupaswa kubakia na mahitaji (Mdo 4:34, 2Kor 11:9,  Mdo 20:34-35, Filipi 4:16). Tatizo tulichagua mafundisho yaliyoumodoa Ukristo na watu wakaamini katika Ukristo, utoaji kiwango chake ni kuweka ka-kakapu (kitunga ) na kupokea masilesile ๐Ÿช™๐Ÿช™๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ, au Ukristo kiwango chake ni kutoa million 10 kila upatapo million 100. Ukristo kiwango chake cha utoaji ni kuhudumia mahitaji kwa ukarimu hata pasiwepo uhitaji. Ukipata million 100 kama kuna uhitaji wa million 85, unapambana kuondoa huo uhitaji kwa kadri cha kiasi cha ukarimu wako. Tutawatambua wakristo waliokomaa katika fundisho la Kristo kwa namna yao wanavyohudumia mahitaji ya kazi za injili, na namna wanavyosapoti wahudumu wa injili, ili kusiwe na mikwamo yoyote. Kama waamini wakifundishwa usahihi wa utoaji kiKristo wataacha uchoyo wa kutoa kidogo kwa asilimia wakati uhitaji ni mkubwa. Wakristo wakifundishwa fundisho sahihi la utoaji, mtaona ghafula tu mabadiliko, watu wataanza kutoa magari, hati za nyumba zitamiminika, viwanja vitamiminika, wafanyabiashara wakubwa na watu wenye tenda za mabilioni ya pesa wataacha uchoyo wa percents na badala yake vyombo vya matoleo vitajaa cheques (cheki) za benki zenye figures tu kubwa, mtu hataona kazi kuandika cheki yenye million 700 kuituma kanisani. Ila kwa sasa kwa kuwa mnafundishana uchoyo, mtu anaishi chini ya viwango vya ukristo huku akiamini amefika. Kwa wahudumu wa neno (mafundisho) wafundisheni waKristo mwenendo unaopatana na tabia mpya za asili yao mpya waliyoipata kwa kuzaliwa kwa njia ya Roho wa Yesu. Mapato ya kanisa hayatapungua, badala yake hakutakuwa na mahitaji tena, na itawapunguzia wahubiri kuwa na mahubiri ya mchongo ya *naona watu 50 wenye elfu 50 kwenye wallets ๐Ÿ‘›  zao, wazitoe na watapata upenyo ndani ya siku 50* ๐Ÿ˜€ Na wengine wametumia 1Samwel 9:7-9, kuweka gharama za kumwona mtumishi (consultation charges), mara ambatanisha sijui what. All sorts of kuambatanisha, kujiambatanisha kwa sadaka, kuifanya kama catalyst ichochee mchakato wa wewe kupokea ahadi au wema wa Mungu, katika Ukristo vyote hivyo ni vya mchongo. Usiulize swali juu ya haya majibu kama hujasoma sehemu ya 1, 2, 3, 4, 5 ya mfululizo huu. Ukiyakataa haya yakatae tu. Endelea kuufurahia uongo kwamba ikitokea sijui kama hujafanya jambo fulani la kimatoleo utalaaniwa, kwamba utakufa kama Anania na Safira, kwamba hutauona ufalme wa Mungu, kwamba sijui what you name them..... Hayo mmeyachagua kuyaamini kinyume na fundisho la Kristo, mitume wake na matendo yao.......

Asante! Tukutane sehemu ya 6 ambayo iko njiani

Mwl Proo- +255762879363

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 6)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
*_Rightly Dividing The Word Of Truth_* (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA SITA*

_MwlProo-0762879363_

*KUHUBIRI NA KUFUNDISHA (Mathayo 11:1)*
 
Karibu katika mfululizo huu wa kuifahamu kweli, jitahidi usome sehemu tano zilizotangulia utaelewa zaidi hapa. Leo napiga hatua kuingia ndani zaidi. Kuna kipindi fulani hivi katika kanisa, mafundisho mengi yalijengwa juu ya shuhuda za watu waliodai kuchukuliwa mbinguni na kuzimu ma kurudishwa. Wengi wa waliotoa madai hayo hawachukuliwa na shetani, wengi katika wale encounters zao zilikuwa za kweli. Kukatokea tatizo kwa kutojua msingi kamili wa fundisho la Kristo, na hawakuwa na namna sahihi ya kuyafikisha waliyoyaona. Kwa ufinyu wa maarifa ya imani ya Ukristo waliyatafsiri mambo kinyume na kweli, ikapelekea kuwa na vitu vingi kwenye mafundisho vyenye kuwakosesha target waamini. Nyakati hizo mtu angezuka kusema nimemwona mchungaji fulani kuzimu (aliyefariki kitambo) anateseka katika moto, kosa lake alizini kwa siri. Nimemwona bibi yangu kuzimu, kosa lake alikuwa mchawi. Yesu amenionesha kwenye maono wote wanaovaa hereni, mawigi na mikufu wapo motoni wanachomwa, Yesu amenionesha wasiotoa zaka kamili hawana nyumba zao mbinguni, na wanaotoa sadaka chache nyumba zao hazijafungwa lenta au hazina canopy. Kwa hiyo waamini wakawa wakirushwa huku na huko na kila upepo wa fundisho toka katika chanzo kisicho sahihi cha mafundisho na mahubiri. Sipo kinyume na shuhuda zao, nipo kinyume na uwasilisho na tafsiri zinazokinzana na kweli ya injili, pamoja na kutumia maono na ndoto za mbinguni na kuzimu kama chanzo cha mafundisho ya msingi ya kanisa. 

Kwa nini kumetokea makosa (errors) mengi kwenye mafundisho na mahubiri mengi kwenye mwili wa Kristo? Andiko nililoliweka hapo juu (Mathayo 11:1) tunaona wanafunzi wakitumwa kufundisha na kuhubiri. Kuna watu wamepewa karama ya kufundisha, na kuna watu kuhubiri, na inawezekana vyote vikawepo. Mtu ambaye hajapewa kufundisha anapolazimisha kufundisha ni rahisi sana kuwaingiza watu katika makosa. Kuna watu walijaliwa neema ya karama za Roho za matendo ya miujiza, karama za kuponya, na karama zingine zenye mvuto tu, wakaaminika kwamba kama wanaweza kutumika kwa karama za nguvu kiasi hicho wanaweza kufundisha, kwa bahati mbaya ikawa kinyume chake. Miongoni mwa ambao waliingiza chachu nyingi za kimafundisho ni watu waliowahi kutembea katika karama za nguvu _(Rejea somo langu la Karama za Roho)_ na wakaamini pia wanaweza kufundisha, kumbe hawakupewa kufanya hilo (Unaweza ukaelewa fundisho la mtu aliyetoka kufufua mfu, linavyoweza kuwa na nguvu, hata kama lina makosa. Watu waliondaliwa na kupewa huduma ya kufundisha wanayo neema ya kufanya uchambuzi wa maandiko (exposition of  scriptures) na kuleta *BALANCE* ya mambo yote yahusuyo imani. Nimesoma kisa fulani ambapo Kenneth Hagin alimwandikia mwalimu mmoja wa neno la Mungu kwa jina Gordon Lindsay (ambaye aliwahi kuwa manager wa mhubiri wa miujiza na uponyaji aitwaye William Branham), katika ujumbe wake alimwambia nimeona maono kadhaa moja wapo ilikuwa Bwana anamwondoa Branham kwa sababu ya damage anayoileta kwenye mwili wa Kristo kimafundisho. Baada ya miezi kadhaa kupita na mhubiri huyo kupatikana katika ajali ya gari na kuwa katika comma na badae kufariki, Lindsay alimjibu Hagin kuwa mtu uliyetoa unabii juu yake amefariki. Lindsay alisisitiza kusema, nilimwambia brother Branham wewe si mwalimu, unachanganya waamini, hubiri neno kisha tumia karama za miujiza na kuponya. Majibu ya Branham kwa Lindsay yalikuwa, "najua mimi si mwalimu, lakini nataka kufundisha, na nitafundisha". Unaweza kuwa na karama kuu za kiroho zenye mvuto mwingi, ila kama hukupewa kufundisha kila ufanyapo hivyo unaweza kuwaelekeza watu katika makosa. Kabla ya Lindsay kuondoka kwenye utumishi wa Branham alisaidia kuleta balance ya mambo mengi kimafundisho (NB:- SIPO KINYUME NA HAWA WOTE NILIOWATAJA AKIWEMO HUYO BRANHAM W.M, NIMETUMIA KISA CHAO KUFUNDISHA TU).

Siku moja nikiwa naandika ufafanuzi wa sura 12 za Daniel (April 2020), nilipofika sura ya 7, 8, 9, & 12 nikajigundua nimekaa nikiwa natumia nyenzo kadhaa mpaka scientific calculator (Niliandika masomo hayo baada ya Mungu kwa Roho Mtakatifu kuniahidi katika ndoto kuwa wiki hiyo atanipa kuelewa hicho kitabu). Nikasema Mungu kama imenibidi nipitie haya ili kukielewa kitabu hiki  Je! itakuwaje kwa wengine ambao labda hawana kipawa cha hivyo, ilikusudiwa wote waelewe? hapo hapo jibu la Mungu kwangu likawa, kila mahali kuna watu waliopewa vipawa vya kufanya uchambuzi wa maandiko (Labda kama hawatatumiwa, au kunyamazishwa). Na hapa niandike ushauri tu kwa viongozi wa makanisa, wasizime vipawa vya waliopewa kufundisha, kwa kuwa unaweza kuwa senior pastor lakini labda una neema ya kuhubiri tu si kufundisha, ukawa na watu dhaifu kwa upande wa fundisho la Kristo, wakasombwa na ukengeufu wowote utakaojitokeza, kumbe hawakupata nafasi ya kufundishwa. Nimesoma andiko la mtu mmoja kasema walimu wanaofundisha masomo ya neema wanapenda sana kutumia maneno ya kiyunani na kiebrania na wanatumia ufahamu wao zaidi kuliko ufunuo wa Roho. Walimu wanaweza kuwa na neema tofauti ya kufanya uchambuzi (exposition of scriptural text), ukiwaona huko kwako *WATUMIE*, USIWAPINGE, USISIMAME NAO KINYUME. Kama unakerwa na ufafanuzi wa kutumia Kiyunani na Kiebrania ni wazi tu, hukupewa eneo hilo kutumika na approach hiyo, shughulika na mzingo na mlinganyo uliopewa utumike kwa uaminifu, lakini waliopewa kipawa cha kufundisha wapewe nafasi hiyo ili kuleta balance ya kweli yote ya injili. Ilitolewa kazi kwa wanafunzi *Wafundishe na kuhubiri*,  watu hawawezi kujengwa kwa ukamilifu kwa kuhubiriwa peke yake, kuna mahali fulani hawatafika kimaarifa ya kiroho. Waamini waliojengwa katika kuhubiriwa pekee bila kufundishwa hawawi imara kiasi cha kusimama sana wao wenyewe. Hawa ndio ambao wakipata uhamisho wa kikazi mbali na mahubiri aliyozoeaga kumpiga *handel*, hasongi mbele, hawa ndio ambao mtumishi anayewaongoza kiroho akifariki na wao hawaendelei tena mbio zao za imani, hawa ndio kukitokeza kauvumi ka roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani yanawabeba alfajiri na mapema.

Kama nilivyotangulia kusema, imani ya Ukristo sio ya mchongo. Mafundisho yasiyojengwa au kutokana na kweli ya injili  lazima yawe *terminated*, mafundisho ambayo msingi wake ulikuwa ndoto na maono binafsi ya mtu huku yakikinzana na fundisho la Kristo, na mitume wake na matendo yao sharti liondolewe lisiweke kwazo wala kongwa la utumwa kwa waamini. Waliopewa kuhubiri wahubiri tu, wasijaribiwe kufundisha waka-infuse errors kwa mafundisho yenye makosa (false indoctrination). Waliopewa kufundisha, wafundishe kwa bidii, kwa ustahimilivu, wala wasichoke. Mwili wa Kristo (kanisa) ujazwe kwa maarifa sahihi ya neno la Mungu, na kuwasaidia waamini kuweza kusimama nyakati zote, na kuwa wazoevu wa maneno ya imani. Hawa wataweza kushinda purukushani zote za masuala ya kiimani katika dunia hii mbovu.


Mungu awabariki tukutane sehemu ya 7

alltruth5ministries@gmail.com

Wednesday, November 2, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 5)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ (2Timothy 2:15b)
*_Na Mwl Proo_*

*SEHEMU YA TANO* 

```MATOLEO/UTOAJI```

Ili kuepuka kuuliza maswali ambayo yamekwishajibiwa na mfululizo huu, tafadhali soma sehemu nne zilizotangulia. 
Mpaka hapa tulipofika tumeanza kuelewa kuhusu imani yetu ya kumfuata Kristo (Ukristo), tumejua kwa sehemu kubwa kuhusu mwenendo wa waamini, tumeanza pia kufahamu matumizi halali ya neno la kweli. Katika sehemu zilizotangulia tuliona kuwa imani ya kumfuata Kristo (Ukristo) sio imani ya kuunga-unga, haijakosa fundisho la msingi, haihitajiki kujiongeza (mafundisho ya mchongo) kana kwamba kweli haipo. Leo nitazungumzia suala moja tu la muhimu sana yaani UTOAJI (MATOLEO) kwa sura ya Ukristo. 

Nianze kwa kusema, *_"KAMA KUNA FUNDISHO LOLOTE LITAKALOKUELEKEZA WEWE MWAMINI UACHE KUWA MTOAJI, NI LA KULIKATAA, KWA SABABU UKARIMU NI TABIA YAKO KIASILI KWA ASILI MPYA ULIYOIPATA KWA KUWA NDANI YA KRISTO, KIUMBE KIPYA_* 

Pamoja na ukweli huo, bado unahitajika kujifunza usahihi wa utoaji. Hapa inahitajika uvue miwani ๐Ÿ‘“ ya kidini na kidhehebu, uweze kuufahamu usahihi wa maandiko na mafundisho kwenye imani hii. Haya ninayofundisha sasa si lazima sana yapatane na kile ulichowahi kufundishwa... Haya yanapatana na ile kweli ya injili, hicho ndicho nina hakika nacho 100%.

Mimi Mwl Proo ni mthiolojia kitaaluma, nilipata kujifunza _Jewish Korbanot Systems_ yaani mifumo ya matoleo ya kiyahudi. Matoleo ya sadaka ya dhambi, ya amani, za kuteketeza, za vyakula zote kwa aina zake na mitindo yake... mafuta, unga, ndege, wanyama na chochote vilikuwa ni mifano (typology) ya sadaka moja ya badae ambayo ilitolewa toka mwanzo. Bila ku-panic soma kwa utulivu tena (Waebrania 10:1-10). 

Jamii ya waamini, baada ya kufa na kufufuka kwa Kristo haiwi tena na mwenendo ule wa kivuli (Kol 2:17, Ebr 10:1), haiongozwi na kiongozi (Gal 3:24, Rumi 10:4) ambacho kiliwekwa kutuleta kwa Kristo tu.

Kutoka katika ufahamu huu, huwezi nyofoa kamstari katika Walawi, bila hata ufahamu wa kutosha wa matoleo ya kiyahudi, ukawaambia waamini jamani neno limesema sadaka ya kuinuliwa, sijui ya kutikiswa, hapana!. 

Leo hii kuna mafundisho mengi ya ovyo-ovyo kama sio ya kujichanganya na ya kinafiki (rough, hypocritic & confusing teachings) kuhusu utoaji, ni kwa vile kulikosekana nafasi ya fundisho la msingi la kanisa pahala pengi, hiyo ikapelekea matumizi yasiyo halali ya neno la kweli. Mafundisho mengi yana mzani wa hadaa (Double-Standard), yaani mtu anataka kwa wakati mmoja atumike na huduma ya mauti, wakati mchache badae atumike na huduma ya roho na ya haki (2Kor 3:7-11).

Leo ninawashangaza kidogo, kuwa mfumo wote wa utoaji, aina zote za matoleo, ikiwa ni pamoja na nia ya kutoa kama ilivyoelezwa kama picha kwenye Torah (Sheria ya Musa) hazihusiki kabisa kwenye imani ya Ukristo (THEY ARE ALL IRRELEVANT IN CHRISTIANITY). Sijachanganyikiwa, wala sijakopi fundisho la watu wala taasisi yoyote. Hiki ndicho kilichopo kwenye imani ya Ukristo, na nitakuonesheni.

 Ndugu zangu waKristo, katika utekelezaji wa sheria 613 (Decalogue inclusive) za Musa kama ulivyofafanuliwa vyema katika Talmud ya wayahudi, ni kosa kubwa kutimiza sheria 599 kwa ukamilifu ukaiacha moja ya 600 (Yakobo 2:10). Ni mchezo wa kuigiza (hypocrisy) katika ulimwengu wa torati kusema unatoa malimbuko (Walawi 23:10), halafu hautoi kodi ya Bwana (Hesabu 31:37, 38, 39). Kwa wasiojua Torati ya Musa, mbali na zaka ambayo kimsingi ni 23%, wayahudi waliamriwa pia kulipa *Kodi ya Bwana* ambayo ni 0.2%, ukitoa zaka ya fungu la kumi (Kumb 22:14), halafu ukaacha kulipa kodi ya Bwana ambayo ni 0.2% wewe ni mnafiki, mwigizaji, mvunja sheria yote, ustahiliye kupata hukumu (Jiulizeni huko kwenu, lini mlitoa kodi ya Bwana? jibu liwajuze kuwa mnaenenda kwa unafiki au kwa ujinga).

Kanisa la mitume (early church) waliweza kutofautisha utoaji kwa waamini, na utoaji waliouzoea mwanzoni wa kiyahudi (kama ilivyoamuru torati). Hawakuendelea na desturi zozote za utoaji za kiyahudi kwenye Ukristo. Kwa nini hawakuendelea nazo, hazikuwa relevant. Fanya study yoyote utakayoiweza ya kanisa lile la mwanzo, hutakutana na utoaji wowote kutoka katika _jewish korbanot system_. Ni wanafunzi wasio makini (careless learners) wa maandiko ndio wanaruka-ruka na mistari nje ya muktadha, utasikia Mathayo 23:23 na Luka 11:42, Yesu amesema wala msiache yale mengine ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚. The Bible Is The Book Of Context (Biblia ni kitabu cha muktadha), hao Mafarisayo (wa chini ya sheria) na Yesu mwenyewe amezaliwa chini ya sheria, walipaswa kuzingatia yote yaliyowahusu chini ya sheria.. iwe tohara, iwe sadaka za kuteketeza na vyakula n.k. Huwezi kurupuka na huo mstari uwasomee waamini kanisani, huku ukiwahimiza jamani Yesu alisema msiache yale mengine.. Huo ni udanganyifu, na matumizi yasiyo halali ya neno la kweli. Kaa chini ujifunze, Je! mitume wa Yesu, kanisa la awali, waliendelea na desturi za matoleo ya kiyahudi? Je! wakristo wa mwanzo huko Uyunani, Uturuki etc walipokutana kwenye makusanyiko yao (kwenye nyumba za watu) hata kabla hawajajenga majengo ya kuabudia, Je! walitoa matoleo ya kiyahudi yoyote? JIBU KUTOKA KATIKA HIYO STUDY YAKO NI *HAPANA*

Ni hivi, wale wa tohara, wale waliopewa sheria walipojaribu kuifuata sana sheria ili kuitenda, walionekana kumpendeza Mungu. Ila waKristo kila wajaribupo kuyafuata maelekezo ya sheria ya Musa kama namna na ya kumcha Mungu, wanamhuzunisha kwa huo ujinga. Najua kiu yenu kubwa sasa, ni Je! tutoeje sasa..!!!! Unasoma kitu sahihi sasa. Katika Ukristo kuna  aina mbili tu za matoleo, ambazo naweza kuzifundisha kwa Biblia, naweza andika vitabu vingi, naweza kueleza na kuthibitisha kwa ushahidi mwingi. Aina hizo za matoleo (utoaji), ni 

1. Sadaka za hiari. Watu kuamua wao wenyewe kwa ukarimu wao watoe nini kwa kiasi gani. Hapa hawapangiwi watoe ngapi, hawatishiwi wasipotoa kupatikana na mabaya yoyote...  (2Korintho 9:7)

2. Changizo (michango) ๐Ÿ‘‰ 1Korintho 16:1, Waroma 15:26

Sadaka za hiari (kutokana na ukarimu na tabia ya upendo), na changizo ndiyo matoleo yanayohusiana na imani ya Ukristo... mnaweza kuzipa majina mengi lakini kunabakia makundi hayo mawili. Wakristo hawapaswi kutoa kichoyo kama wale wa jangwani wenye mioyo migumu waliopewa torati. Wakristo wanatoa kwa kadri ya uhitaji, hata pasiwepo upungufu. Kama una million 200 na uhitaji ni million 180, utatoa million 180 kuondoa uhitaji uliopo na sio million 20, kuacha watu wapambane na uhitaji wa million 160. Katika ukristo kama kunahitajika ada za watoto wa mchungaji na jumla ya ada ni million 7, badala ya kuweka kaubunifu ka kitapeli (fraudulence)... kwamba nitagawa bahasha za kinabii (prophetic envelopes) ✉️✉️✉️✉️✉️ weka sadaka inayouma, uuguse moyo wa Mungu.... wekeni tu changizo kupata hizo million 7 basi. Matoleo katika Ukristo ni sadaka ambazo watu watatoa wenyewe kwa kuamua wao viwango, na nje hapo ni changizo (michango)..... *CHOCHOTE NJE YA HAPA NI CHA MCHONGO, SADAKA YOYOTE ILIYOAMRIWA NA MUSA IKILETWA KANISANI NI YA MCHONGO, HAINA UHUSIANO NA UKRISTO.* Usikasirike huu ni ukweli, hata kama baada ya hapa tutaendelea na desturi  za dini na madhehebu yetu, tuendelee na mazoea yetu tukiwa tumeshaufahamu ukweli na usahihi.
_mwlproo_
Kuna watu kadhaa wamejirudi wenyewe siku za usoni, huku wakisema katika Agano Jipya (ambalo nalo hawalijui wanahisi ni hivi vitabu/barua 27) kwamba tunatoa malimbuko na zaka kwa upendo sio kwa mujibu wa sheria. Kwa wakati huo huo bado wananukuu Malaki 3:8-11. Ili Malaki 3:8-11 iwe katika kutumika (in effect) ni lazima Malaki 4:4 iwe katika kutumika... Sheria na amri haziwekwi bila hukumu zake.... Yaani ukimriwa usizini, basi kuna hukumu yake ukiivunja upigwe mawe. Double Standards nilizozitaja mwanzo ni kuchagua kaupande kamoja, na kukatupa nje kaupande kengine (unafiki/ujinga ๐Ÿ‘‰ one of the two is correct).
Mara kadhaa nasikia watu wakiombea sadaka wananukuu Kutoka 34:20b, kwamba Mungu ulisema tusije mbele zako mikono mitupu. Nyie watu!!!!!!!  mnadhani kila agizo la torati mliambiwa ninyi? Kwa taarifa yenu Wakristo hawatoi matoleo kwamba wameagizwa, HAPANA! Tabia ya ukarimu (generosity) ya Baba yao (Mungu) ipo ndani yao tayari kwa kuzaliwa kwa pili... Kutoka katika huo ukarimu ndio wanatoa.. Kama hawatoi haina maana hawajazaliwa na Mungu, wafundishwe tu mafundisho sahihi ya injili, watambue asili yao mpya ina tabia zipi, watatoa mpaka hakutakuwa na uhitaji. Kuamini kwamba Mungu amewaagiza msiende mbele zake bila kitu mkononi ni kujifunga kwenye kongwa la utumwa.... PIA KILA ITAKAPOTOKEA UMEHUDHURIA IBADA UKIWA HUNA SADAKA, ITAHESABIWA KUWA NI DHAMBI. Wakristo wakomavu hawawezi kuwa kwenye makusanyiko ya ibada bila fedha na mali za kusapoti kazi ya Mungu, na kusapoti maisha ya wanaoitenda kazi ya Mungu. Lakini si kwa agizo la KUTOKA 34:20b, na hivyo kama hawana wasiache kuhudhuria, na wasipotoa hawakuhumiwi wala kulaaniwa. Yale mengine ya mchongo mfano:-kuhimizana kuwa ukiweka nadhiri (vowed offerings) inamhamasisha Mungu atende kwa haraka, ni maudambudambu tu ya kidini nje ya muktadha wa Kikristo. Baba yake Yesu ambaye ni Baba yetu hahitaji kupigwa _Handel_ ili kumhamasisha awe mwema au mkarimu. Hasubiri ahadi za 'ee Mungu nikipata ile kazi, nitanunua viti vya kanisani....' Yeye kwa njia Yesu, pamoja na Yesu amekupa vyote, unaweza kupata chochote (Waroma 8:32). Ila kama mnapenda kuwa na vitu vya mchongo endeleeni kuweka nadhiri mkiamini Yesu na mitume wake walipitiwa kuwafundisha tabia za Baba yenu wa Mbinguni!

*KUHUSU LAANA* 
Wakristo wapuuziaji (Careless Christians) ndio  pekee wanasoma Malaki 3:9 na kuamua kulibinafsisha hili andiko.... Kuwa nimelaaniwa kwa laana, na taifa hili lote.... kisa nini?????? Eti nilipewa elfu 2 ya nauli na sikuitolea 10% yaani  shilingi 200. So unahisi Yesu na Baba Yake (Mungu) wanashirikiana kukulaani kila wakigundua kuna msimbazi ulipewa 10,000/= na hukutoa buku (1000/=) bali uliitumia yote kulipa deni fulani pale  Mangi Shop????๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
_mwlproo_
Ndugu zangu katika Kristo, hakuna laana inayokuja kwa mtoto wa Mungu toka kwa Baba yake kisa amekosea au kutofanya jambo fulani bila ukamilifu. Si tabia ya Mungu, na wala shetani hawezi. Na huo ndio mvuto wa kuiamini injili. Hakuna mtu anayeweza kukulaani wewe mwamini, mwenye maarifa sahihi ya Yesu. Tena kama kuna kiongozi wa kiroho aliwahi kukulaani na ukalaanika, hii inawezekana tu kwa kuwa wewe umejiweka (submit)  chini yake kifundisho na maongozi ya kiroho.. Ambako hapo napo bado itategemea una-operate kwa kiwango kipi katika maarifa ya kiroho (ya kumfahamu sana Mwana wa Mungu, Yesu Kristo)... Otherwise mikwamo yote unayokutana nayo, sio matokeo ya kulaaniwa...USIIBIWE, unaweza kutoka tu kuyatumia mamlaka yako uliyoyapewa na Kristo na kufanya bidii ya kazi na matendo mema... 

*UKIRI*
Mimi ni mwamini, nimebarikiwa. Nitafanya kazi kwa bidii, nipate fedha na mali za kusaidia uhitaji na wahitaji. Nitatoa daima maana ndio tabia yangu katika Kristo. Bwana wangu Yesu amenionesha njia njema, kuwa ni bora kutoa kuliko kupokea (Matendo 20:35). Hivyo nitatoa, kama Bwana wangu alivyo mkarimu, mimi pia nitaonesha ukarimu kwa kutoa sana sana sana.


USIKOSE SEHEMU YA SITA (6) YA SOMO HILI TUTAPIGA HATUA KUINGIA NDANI ZAIDI

0762879363 (WhatsApp)

alltruth5ministries@gmail.com

Sunday, October 16, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 4)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ (2Timothy 2:15b) 
_mwlproo_

*SEHEMU YA NNE*

_YESU ALIMFUNUA MUNGU NA TABIA ZAKE KWA WATOTO WAKE_

Kama hujasoma sehemu ya kwanza, ya pili, na ya tatu ya mfululizo huu, usijaribu kabisa kusoma sehemu hii, haitaeleweka!.
Kama tulivyoona sehemu ya tatu, kwamba imani ya   Ukristo sio imani ya kuunga-unga, sio imani isiyo na fundisho la msingi kiasi cha kufanya kila mtu kujiongeza kwa chochote anachobahatisha kukisoma kutoka kwenye Biblia. Imani ya Ukristo (Kumfuata Kristo) inaongozwa na fundisho la Kristo na Mitume wake, na yote yaliyoandikwa kwenye Torati, Zaburi, na Manabii yaliyomweleza Kristo kwa picha (typologically), yataelezwa kwa kutokea kwa Kristo au Kristo kama kiini (Christocentrically). Kuna mahali nilihudhuria mkesha mwaka 2011, na somo la mkesha wa maombi lilikuwa, *KUKATALIWA NA BWANA*, mhubiri alitia mkazo mkubwa kwamba kama kuna jambo haukumtii Mungu, Mungu amekukataa tayari, hata kama umekuja kuomba, ila Mungu amekukataa.. huku akiongezea na andiko toka 1Samweli 16:1-2. Somo hilo linaonekana kuwa zuri, ila lina makosa mengi kwenye ujuzi wa Mungu kupitia Kristo. Lilifanya watu kuona hawastahili, wametengwa na Mungu, uhusiano wao na Mungu ni kama umeungwa kwa _Sellotape_, na kwamba makosa yao yanawafanya mara moja kuwa sio watoto wa Mungu tena. Watoto wa Mungu hawakataliwi na Mungu (Baba yao) kwa kukosea, pamoja na ukweli kwamba wanapaswa kujifunza namna ya kujenga tabia za uungu kama watoto wa Mungu wawe na mienendo isiyolaumika kabisa. Ili kuepuka makosa ya nini sio sahihi kuhusu Mungu, kipi sio sifa na tabia yake, yapi yasiyo matendo yake kwa watoto wake, ni lazima kujifunza kuhusu Mungu kwa kutokea kwa Mwanae, Yesu Kristo aliyemfunua (Yohana 1:18, Ebrania 1:1).

A. *MTAZAMO USIO SAHIHI WA KUWAJIBISHWA KWA KUKOSEA*

Watu wengi wametumia andiko kama Ufunuo 3:19, bila ku-exegete (rejea sehemu ya pili kuhusu exegesis), na kutoka na mahitimisho kuwa watu wa Mungu wanaweza kupigwa na Mungu, kupatwa na mabaya ikiwa ni sehemu ya kuonesha Mungu anawapenda, ili warudi watubu. Mtu anafanya matumizi ya mstari huo nje ya muktadha, bila kuzingatia ujumbe wote kwa kanisa la Laodikia, na kuupuza kabisa simulizi ya andiko kimuktadha (history of the text & history in the text). Dhana hii inaenda mbali zaidi ya hapo, wengi wenye dhana hii wamekuwa wakisoma vitu jumla jumla bila kuwa na msingi mzuri kwenye fundisho la Kristo na Mitume. wanachotumia ni kile kiitwacho kitaalamu *_DEUTORONOMISTIC VIEW OF HISTORY_*  yaani, "You  do good, you're rewarded. You do bad, you get punished". Hiki kimetawala sehemu kubwa ya mafundisho ya makanisani. Hakijasaidia kujenga wakristo kama namna ambavyo  kimewaletea mashaka tu, mpaka sasa watu walio ndani ya Yesu  wanaulizana ukifa sasa hivi utaenda wapi? Parapanda ikilia ๐ŸŽบ  utanyakuliwa kweli? Watu hata hawaelewi ni basi tu wanaendelea kujifariji kwa sala za kutubu za asubuhi, mchana, na usiku muda wa kulala. Mtazamo huo hauwasogezi watu kwa Mungu, unawaweka mbali. Upi mtazamo sahihi kwa imani ya Kikristo?? Endelea kufuatilia mfululizo huu, ukifika sehemu ya 10 utakuwa tayari na kilicho halisi kwa imani hii.

Unajua mtu anajisomea zake kitabu cha Yeremia, bila ufahamu wa kutosha   wa injili, anaibuka na taswira yake kuhusu Mungu kwa namna isiyo sahihi. Kuanzia Yeremia sura ya 14,  mpaka utimilifu wa unabii wa kwenda utumwani, kila mahali anasoma Mungu atawaletea njaa, atawapiga kwa tauni na upanga kwa kuwa mmemwudhi na kumtenda dhambi... Hivyo utamaliza umemfahamu Mungu kwa ufunuo wenye muktadha huo, kuwa Mungu amekaa zake huko, anasubiri ukosee ili akuadhibu kwa majanga fulani fulani. Hii imepelekea waamini (Wakristo) kudhania magumu mbalimbali, magonjwa, ajali, kupungukiwa kokote kunapowakuta (umaskini), ni adhabu na laana toka kwa Mungu. Hata yale ambayo walipaswa wao kwa mamlaka waliyopewa wayaondoe kutoka katika maisha yao, bado wanaendelea kulia nayo, wakiamini wanapaswa kusali kwa kuomba msamaha kwa Mungu. Haya yote hayako sahihi kwa mtazamo wa mafundisho ya  msingi katika Kristo.

*B. KUTUMIA NGUVU ZA MUNGU KUDHURU WATU*

Yesu aliyemfunua Baba yake wa upendo  (God of Love), ametufundisha njia sahihi ya kuzitumia nguvu za Mungu. Yesu hakuwahi kuzitumia nguvu za Mungu kuangamiza uhai, bali kuokoa na kuponya. Kama Yesu katika huduma yake angeua mtu mmoja, au wawili watatu, asingekuwa tofauti sana na Mtume Muddy (Muhammad) ambaye katika maisha yake mbali na kuagiza wafuasi wake kuua, aliwahi kupigana na mtu (Ubayyi ibn Khalaf) na kumwua. Kama Yesu angefanya kitu cha namna hiyo,  Mimi Mwl Proo, nisingekubali kumfuata, nisingemwamini. 

Hatujifunzi tabia za Mungu, wala mwenendo wa Ukristo mbali na tabia   zilizofunuliwa na Yesu. Ukichomoa-chomoa vifungu vya Biblia na kuvifanyia kazi ukiamini tu kwa kuwa vipo kwa Biblia basi vinakuhusu kama vilivyoandikwa, unaweza kuzitenda kazi za shetani kwa kutumia nguvu za Mungu. Ukisoma Luka 9:51-56, utaona kisa cha wanafunzi wa Yesu waliotaka kujifunza tabia za Mungu toka kwa Eliya... Na Yesu akawaambia sio kwa Roho wa Mungu wanataka kufanya hilo, bali wanasukumwa na roho nyingine, kuzitumia nguvu za Mungu kudhuru wanadamu. Yesu katika huduma yake hakuwahi kudhuru uhai wa mwanadamu aliyekuja kumfia, ampe uzima wa milele uliopotezwa. Aliwahi kuudhuru mtini (fig-tree), na labda kuruhusu wale pepo kuwaingia nguruwe, ambapo nguruwe wale walifia majini ๐Ÿ–๐Ÿ–๐Ÿ–๐Ÿ– ๐ŸŒŠ ,tunaweza kutaja kuhusu matumizi ya kikoto cha kambaa hekaluni? hakutoa uhai wa mtu zaidi ya kuleta order (utaratibu) hekaluni.  Ukiondoa visa hivyo vya Yesu ambavyo havihusishi uhai wa mwanadamu, Yesu hakuwahi kwa sababu yoyote kuangamiza. Hii ndiyo standard ya Ukristo, kuokoa sio kuua, kuponya na sio kuangamiza!

i.) Eliya alichinja watu na kuutoa uhai wao. Eliya alitumia upako wake kuruhusu moto uunguze watu... Moto ๐Ÿ”ฅ  ukashuka na kugeuza watu mishikaki... Wengi mkisoma mnafurahi, mnatamani kufanya kama yeye. Hilo kwa muktadha wa Ukristo ni matumizi mabaya ya nguvu za Mungu (Hatupaswi kuliiga hilo)

ii.) Elisha alipotaniwa na wale vijana (2Falme 2:23-24), aliwalaani kwa Jina la Bwana, wakaja dubu ๐Ÿป  ๐Ÿป . Ni Yeye Elisha aliutumia upako wa kiMungu ndani yake kufanya dubu waje kuwaua wale vijana. Mwenendo huo wa kina Elisha sio wa kiKristo, na wala waKristo hawajifunzi tabia za kuwadhuru watu wanaowaudhi.

iii.) Kuna mahali nilisema Petro ndiye aliyewaua Anania na mkewe Safira, na watu wakakataa, sikuwalazimisha maana nilijua nipo na watu ambao hawajafahamu kweli na neno la haki kwa  kiwango hicho. Lakini hebu nikuulize mtu mwenye upako wa Mungu ndani yake, ambaye akitembea kivuli chake kinaondoa maradhi yote kwa wagonjwa, mtu ambaye akimwinamia mfu  anafufuka mara moja. Je! kwa upako huo akiwa na shauku ndani kuona mtu ameadhibiwa mara moja kwa makosa yake, unadhani huo upako hauwezi kufanya mtu apoteze maisha?. Usianze kufikiria Petro ambaye ni mkamilifu sana, chukua picha ya Petro ambaye naye pia bado anakua katika neema, lakini upako unatenda kazi kwa kiasi kile. Soma maneno ya Petro kwa mke wa Anania, utagundua moyoni mwake alikuwa aki-execute hukumu ya kosa la wanandoa wale, upako ulio ndani yake ungeweza kuwaponya au kuwaua. Na ni wazi kwamba Petro alikuwa katika neema na kulifahamu pendo la Mungu, hakuna visa tena vya yeye kuruhusu upako wa kiMungu kuua watu. Hapo unachagua kujifunza kwa Yesu, aliyeonesha namna njema ya kutumia nguvu za Mungu ndani yako. Pia jiulize mambo mangapi huko kanisani kwenu mmevunja makubaliano yawe ni masuala ya fedha, mali, n.k, Je! mlipokosa uaminifu mmekufa? Mbona hatusikii vifo vya wakosaji huko kanisani kwenu??

iv.) Tunao waKristo wengi siku hizi, wanapita mbele kutoa shuhuda jinsi walivyoomba mpaka waganga, wachawi walivyokufa baada ya maombi yao. This is 'abuse of power' (matumizi mabaya ya nguvu). Kwenye Agano Jipya, wachawi, waganga, na washirikina wote ni wenye dhambi kama wenye dhambi wengine tu, hawana lolote la ziada. Makosa yale-yale niliyoyaeleza sehemu zilizopita yanafanya waKristo wasio na ufahamu wanukuu KUTOKA 22:18, na kuanza kuua wachawi. Mungu haui hao wachawi, ila ni ninyi wakristo mnaziruhusu nguvu za Mungu (zinazoweza kuokoa) ziwaue. Ni aibu kwa mwamini kupita mbele kushuhudia kuwa kuna mganga mtaani kwetu nilifunga siku tatu, na sasa kuna mazishi yake. 

*KUNA WATU UTASIKIA WAKISEMA, "UKRISTO SIO UJINGA". NI KWELI KABISA UKRISTO SIO UJINGA, ILA KUOMBA MAOMBI KUUA WAGANGA NA WACHAWI NI UJINGA. MNAO UWEZO WA KUHARIBU KAZI ZOTE ZA UCHAWI, NA UTENDAJI WOTE WA KIPEPO NA MASHETANI, ILA SIO KUUA WANADAMU WANAOTUMIKISHWA NA  ROHO HIZO ZA KICHAWI.*

*KAMA KUNA NGUVU ZA KICHAWI, ZA KIGANGA, ZA KIPEPO ZILIFANYA KAZI NA KUKUDHURU MWAMINI, HIYO NI MATOKEO YA WEWE MWAMINI KUKOSA MAARIFA TU. MAANA UKWELI NI KWAMBA, HAKUNA LEVEL YOYOTE KWENYE FALME ZA GIZA NA MAMLAKA ZOTE, ZINAZOWEZA KUMDHURU MTOTO WA MUNGU (MWAMINI), MWENYE MAARIFA SAHIHI YA KAZI ALIYOIFANYA YESU, NA NAFASI YA MWAMINI HUKO ROHONI. SO BADALA YA KUHANGAIKA KUUA WACHAWI, TAFUTA MAARIFA SAHIHI, WAFUNDISHE NA WENGINE*


C. *MATUMIZI MABAYA YA MAANDIKO YASIYO NA MUKTADHA WA KIKRISTO KWENYE MAHUBIRI NA NYIMBO ZA KIDINI*

Mtu yuko huru kuhubiri au kuimba ujumbe wa Biblia toka katika kitabu chochote tu, ila kiwango (standard) cha kupimwa kwa ujumbe huo ni fundisho la Kristo na Mitume wake. Huwezi kunyofoa andiko la Ayubu sura ya kwanza, kwamba Ayubu alinyoa kichwa chake baada ya kufiwa, nawe ukalitumia tu yaani, tukakuta msibani wafiwa waKristo mmenyoa vichwa vyenu. Nimesikia mahubiri, nyimbo zikitungwa kwa kutumia zaburi na kutumika kwenye muktadha wa Ukristo, haya mambo hayaendi hivyo ndugu zangu. Mfano Daudi akisema  wokovu (soter) hakumaanisha huu wokovu tulioupata kwa kufa na kufufuka kwa Yesu. Kwake wokovu ilikuwa ni yeye kufanikiwa kuua maadui zake, kuwapiga mishale ๐Ÿน  askari wa nchi jirani, akarudi jioni hajafa. Kumbuka aliwaua kabisa iwe kwa upanga, iwe mkuki au mawe ya teo, aliua wakubwa kwa wadogo, wanaume kwa wanawake.... (kwake mauaji hayo ndiyo anayaita wokovu una Bwana). Sasa ghafula anatokeza mwimbaji anafungua ZABURI 109:6-20, Naye anatunga wimbo akiwaombea wanaomwudhi na maadui zake (wanadamu) wakutwe na hayo aliyoyata Daudi yatimizwe kwa washtaki wake na maadui zake. Ukristo haufundishi hivi, tabia za Wakristo wanajifunza kwa Yesu, tabia za Mungu, na matumizi ya nguvu za Mungu ndani yao wanajifunza kwa Yesu Kristo. Hivyo utunzi wa nyimbo za kiKristo au mahubiri, lazima yawe sambamba na fundisho la msingi ndani ya Ukristo (The teachings, preachings, songs should be in-line with the truth of the gospel)

NAKUPA SHAURI, USIKOSE SEHEMU YA TANO (5) YA MFULULIZO HUU. TUTAJIFUNZA KITU CHA MUHIMU SANA CHA KUYAFAA MAKANISA YA MUNGU POPOTE YATAKAPOFIKA MAARIFA HAYO.

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail com

Monday, October 10, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 3)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ 2Timothy 2:15b

*SEHEMU YA TATU*

*_KIPI KINAPASWA KUWA FUNDISHO KWA WAAMINI?_*

Sikushauri uanze kusoma sehemu ya tatu (3) kama hujasoma kwa kuelewa, sehemu ya kwanza na ya pili, huu hapa ni mwendelezo tu. Sehemu ya pili ya somo nieleza namna mbili za kutafsiri maandiko yaani (Eisegesis na Exegesis). Leo nakuonesha kipi kinapaswa kuwa fundisho kwa waamini (Wakristo). Ukristo (imani ya kumfuata Yesu) sio imani ya mchongo, wala sio imani ya dini ya Kiyahudi (Judaism). Ukristo sio imani iliyokosa vyanzo vya kufundishia (sources & materials), au kwamba kuna mambo hayana mwongozo, na mtu yeyote anaweza akatengeneza kitu chake tu chochote (coined teachings); Hasha!

Natambua kuhusu magawanyo ya Roho (Ebrania 2:4), natambua kuhusu tofauti ya kutenda kazi (1Kor 12:6), natambua kuhusu neema mbalimbali za Mungu (1Petro 4:10). Lakini pamoja na hayo yote kusanyiko la waamini, hawafundishwi tu chochote atakachokinyofoa mtu kwenye Biblia. Mfano kama Torati ni kivuli, wala si sura halisi.... Kila utakapotaka kusoma kivuli utapaswa kukisoma kutokea kwa sura halisi (Kristo). La sivyo utaangukia katika upotovu mkubwa. Kwa kusema hivi simaanishi kamwe Torati au kitabu chochote cha Agano la Kale kisisomwe au hakiwahusu waamini katika Kristo (Warumi 15:4), hapa ni suala la matumizi yake ni yapi?? Ndio maana somo letu linaitwa *KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*

Kwa sababu ya kukosa msingi, nini haswa kinapaswa kuwa fundisho kwenye kanisa, Watu wameingiza chachu za kifarisayo nyingi sana, huku ikidhaniwa ni mafunuo. 

*MIFANO HAI YA MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA MAANDIKO*

1. Huwezi kuja kwenye kusanyiko la Wakristo, ukawasomea Kumbukumbu La Torati 22:8, na kuwaelezea wapendwa Mungu anatuagiza kujenga ukuta mdogo wa fensi (parapets/battlements). Hili sio agizo la Mungu kwa waamini katika Kristo.. Taratibu za ujenzi kwa waamini zitazingatia tu uwezo wao kifedha, vibali vya ujenzi toka manispaa, utamaduni wa majengo ya mahali walipo... Wala usiwaongoze kwa desturi hizo za kiyahudi.

2. Huwezi kwenda kwenye kusanyiko la waamini huko Uarabuni, ukawasomea andiko la Walawi 11:4 (Na kuwaambia jamani ndugu zangu Wakristo msile kabisa ngamia ๐Ÿช  ๐Ÿช  Mungu kakataza. Waamini hawajakatazwa kula ngamia.. Ni wewe hujatumia kwa halali neno la kweli. Suala la vyakula halali vya kuwafaa kwa afya vitategemea desturi za huko walipo, kanuni za afya kisayansi kama wanyama hao hawana madhara na sio kutafuta mwongozo wa Torati ya Musa kuwajuza wanyama wa kuliwa... (Torati ya Musa na Isaya imetaja kuwa panya ๐Ÿ€๐Ÿhawapaswi kuliwa, niwaambie tu kama kuna Wamakonde na Wayao wanaokula panya na ni Wakristo, hayo makatazo hayana uhusiano na imani yao.

3. Huwezi kwenda kwenye kusanyiko la waamini (waKristo),  ukawasomea Walawi 19:27, na kuwaambia ni chukizo kunyoa denge (cutting hair by sides). Umetumia neno isivyo halali, ulipaswa ujifunze kwanza maana ya maagizo hayo kabla ya kuwaambia Wakristo, labda msichonge ndevu zenu mkienda Saluni (Barber Shop). Kama Mkristo atakatazwa kunyoa au kuchonga ndevu, au nywele zake iwe ni katazo kwa sababu jamii yenu kitamaduni, hawalikubali hilo.... wala sio utii kwa makatazo ya Torati (maana kila katazo linalo muktadha wake).

4. Huwezi kwenda kwenye kusanyiko la waamini ukawaambia jamani Kumbukumbu la Torati 22:11, Biblia imekataza kuvaa nguo yenye aina tofauti ya vitambaa (two different linens) yaani nguo isiwe na satini, na pamba, au hariri, au sufu au kitani, au kitenge etc). Kwamba ukifanya hivyo ni machukizo.. Hicho ulichosoma ni kizuri ila sio maagizo ya Mungu kwa waamini. Kama kuna kitambaa utaacha kukivaa ewe Mkristo ni labda kama kwenye jamii yenu kinakataliwa kijamii, isiwe na correspondence yoyote kwa makatazo ya Torati.

Kuna watu wanasema Mwl Proo, unazuia watu kutumia vitabu vya Agano la Kale... La Hasha!.  Ninchofanya ni kuwaondolea utaji (veil) na kuwafanya waamini wapate kumwona Kristo hata kwenye Torati.

Ni aljebra rahisi sana hii hapa: Torati, Zaburi, na Manabii vilizungumza habari za Kristo kwa picha (Typologies)....  Ujumbe wa kuhubiriwa ni Kristo. Hivyo tu (Kolosai 1:28, 1Korintho 1:23). Yaani, ili watu wawe waamini (watoto wa Mungu) hawahitajiki kunakili (kuCopy) chochote kwenye desturi ya dini ya kiYahudi. Wanapaswa kuhubiriwa kuhusu Kristo (kazi aliyoifanya na kuikamilisha) wakiziamini hizi habari njema (Injili), wanapokea wokovu (kufanywa watoto wa Mungu). Na baada ya hapo watendelea kufundishwa kuhusu Yesu (Kuzaliwa kwake, kufa, kuzikwa, na kufufuka kwake), kumewafanyia nini wao (kumfunua Yesu), huku  pia wakifundishwa wao wamekuwaje kwa kupitia Kristo (kilichotendwa ndani yao, na nafasi zao wakiwa ndani ya Yesu)... Haya yanatosha kumfanya mwamini kuwa mtu mkamilifu, mwenye kuweza kutembea kwenye madaraka makamilifu, kama mtoto wa Mungu. Waamini wataendelea kujifunza kuhusu mwenendo ndani ya imani kwa Yesu (asili yao mpya baada ya kuzaliwa upya), na watakaa kwenye fundisho la Yesu na mitume wake. HABARI HIZI NI NYINGI ZINATOSHA KUZIHUBIRI NA KUZIFUNDISHA HATA KAMA ULE MWISHO UTAKAWIA KWA MIAKA MILIONI 10 BAADA YA SASA _(mwlproo)._ MKIPIGA CHENGA FUNDISHO LA KRISTO NA MITUME WAKE MNAJIINGIZA KWENYE MAFUNDISHO YA MCHONGO. MTAPEANA UTUMWA, HOFU, NA MAFUNDISHO MENGINE YA KUFANYA MSALABA UBATILIKE.
SIKU YA JANA KUNA MKRISTO AMENISHIRIKISHA KUWA JUMAPILI ILIYOPITA WAMESOMEWA EZEKIEL 16:1-5, NA KUFUNDISHWA NGUVU ILIYOSHIKILIA HATIMA, ILI WAWEZE KUOMBEA VITOVU VYAO VILIVYOKATWA MIAKA MINGI. ๐Ÿ˜€ NI KAMA MAFUNUO MAZURI VILE, SI NDIO!!! HAYA SIO MAFUNDISHO YA KUWAFUNDISHA WAAMINI. WAAMINI WANGEAMBIWA ALICHOFANYA YESU, NA WAO WAMEKUWAJE KWA KUZALIWA, KUFA, KUZIKWA, NA KUFUFUKA KWA YESU. HAKUNA LEVEL YOYOTE KATIKA UFALME NA MAMLAKA ZA GIZA INAYOWEZA KUWASHIKA WAO WALA HATMA ZAO.  MKIKATAA HAYA MNAWEZA KUCHAGUA KUENDELEA KUJIFUNZA UTUMWA AMBAO HAUPO, ILA UNAUMBWA KWA KUWA MMECHAGUA KUUSIKILIZA NA KUUAMINI. YOYOTE MTAKAYOYABUNI KWA KUNYOFOA VIMISTARI KWENYE BIBLIA NJE NA UJUMBE WA MSINGI (FUNDISHO LA KRISTO NA MITUME) MTAKUWA MMECHAGUA KUJIFANYISHA KAZI AMBAYO BWANA MKUBWA YESU KRISTO ALIIKAMILISHA. LEO HII UKIAMUA KUFINDISHA WATU LAANA ZA ARDHI ZINAVYOLETA UMASKINI, SIJUI SADAKA YA KUTANGUA MADHABAHU ZA MAGONJWA, MARA NAMNA DAMU ZA KAFARA ZINAVYOLETA MATESO KWA MKRISTO, NA TAKATAKA ZINAZOFANANA NA HIZI, NI UCHAGUZI WENU TU KUURUDISHA UTUMWA AMBAO HAUPO. NA ANAYEJARIBU KUSEMA YEYE NDIYE ANAWEZA KUWASAIDIA WAAMINI KUTOKA KWA HAYA ANAJARIBU KUJIPA KAZI YA KUWA MWOKOZI MSAIDIZI. WAAMINI WANACHO CHA KUFUNDISHWA SIO HAYO!

*CHRIST IS OUR MESSAGE (COLOSSIANS 1:28 TPT)*


NIKUOMBE SANA,USIKOSE SEHEMU YA NNE (4), UTAPATA MAMBO YA KUKUSAIDIA SANA KUIELEWA IMANI HII NA KUIFURAHIA

alltruth5ministries@gmail.com.

Wednesday, September 21, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 2)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
*_Rightly Dividing The Word Of Truth_* (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA PILI*

_Mwl Proo_ #0762979363

Sikushauri kuisoma sehemu ya 2, iwapo hujasoma sehemu 1. Sehemu ya kwanza tuliona namna maandiko ya Biblia yanaweza kutafsiriwa (Literally /kama yalivyoandikwa, Allegorically /lugha ya picha, Contextually/Kimuktadha ) ambazo nilizitolea mifano. Leo tusogee mbele zaidi!

Roho Mtakatifu anafanya kazi vile vile, kazi ile ile aliyoifanya ndani ya Mitume wa Yesu na wale wanafunzi waliopokea _Ahadi ya Baba_ pale ghorofani. Hakuna kilichopungua wala kubadilika. Pamoja na ukweli kwamba sehemu kubwa ya wanafunzi wa Yesu hawakuwa na elimu kubwa ya kidunia (Mdo 4:13, 1Kor 1:26), haikuwa kazi kwa wanafunzi wa Yesu kuelewa maelekezo waliyopewa na Yesu, wala kuelewa ufunuo wowote wa Roho juu ya imani na mwenendo katika Kristo.

Sasa yale waliyoyaandikwa wao, na kuja kusomwa na sisi miaka 2000 badae lazima kuwe na kanuni za kuzingatia katika kuyatafsiri, au sivyo, tutaangukia katika mtego wa kuwa na ufafanuzi wa mchongo (false manipulations). Kile kilichoandikwa na mitume pamoja na kuvuviwa, na kuongozwa na Roho bado ni kazi ya fasihi (It's a literature work). Hapo sasa usiseme ninaye Roho Mtakatifu atanitia katika kweli yote, ukipuuza kanuni you're prone to errors.

Kuna namna mbili ambazo watu huzitumia kufafanusha maandiko.. Kitaalamu hutajwa kwa *EISEGESIS* na *EXEGESIS*. Hiyo ya kwanza (eisegesis) ni namna ambavyo mtu anajaribu kueleza kile ambacho yeye amekielewa kutoka kwenye maandiko (scriptural text), na hiyo ya pili (exegesis) mtu anajaribu kuzingatia kanuni za kutafsiri maandiko ili aelewe mwandishi (author) alimaanisha nini?.

Mambo mengi yanayofundishwa kimakosa na yaliyoingiza ufafanuzi wa mchongo (false manipulations), ni matokeo ya kila mtu kujaribu kufundisha anachoelewa yeye (eisegesis), badala ya kujifunza kuelewa alichomaanisha mwandishi (exegesis)..... 

ANDIKO LETU LA MSINGI  KATIKA 2TIMOTHEO 2:15b RIGHTLY DIVIDING THE WORD OF TRUTH (kulitumia kwa halali neno la kweli;) Ndipo kunatupa mwanga wa kutafsiri maandiko kwa namna ya kuelewa alichomaanisha mwandishi *(Biblical Exegesis)*

Waliojikita kwenye EISEGESIS wanapenda kutumia mtindo wa kunyofoa-nyofoa vifungu (Proof-Text Method) bila kuzingatia kabisa kanuni. Ili tu anachotamani yeye Biblia iwe imekisema kionekane ni cha kweli. Wanajitahidi kuyasoma mawazo na mitazamo yao ndani ya Biblia.

SASA ILI KUEPUKA UFAFANUZI WENYE MAKOSA (FALSE MANIPULATIONS) KWENYE MAANDIKO, UNAPASWA KUZINGATIA KANUNI ZIFUATAZO.

1. Zingatia maandiko yaliyo nyuma ya mstari uliousoma (Pretext passages)

2. Zingatia mistari iliyo mbele/inayofuata (The post-text passages)

3. Zingatia muktadha (The context principle)... mind you ๐Ÿ‘‰  a text without the context is only a pretext, ndio maana kuna wakati utafiti huu unaweza kuhusisha kutafuta maana za maneno ya lugha za asili. 

4. Tafuta kujua kwa uchache tu historia ya kuandikwa ujumbe huo. Ukiweza tafuta kujua hadhira ilikuwaje? Utamaduni wao ulikuwaje? (Historical& Cultural Facts)

 5. Na kama itatokea passage moja inaonekana kukinzana na nyingine, angalia na passage ya tatu na zingine zinalizungumziaje suala hilo hilo.

NB:- *NI HATARI KUUNDA FUNDISHO LOLOTE LA MSINGI KWA KANISA HUKU LIKIWA LIMEJENGWA JUU YA TAFSIRI ISIYO SAHIHI YA MAANDIKO*

HAPA CHINI, NINACHAGUA SURA MOJA YA BIBLIA. NA KUKUONESHA NAMNA *_EXEGETICAL BIBLE INTERPRETATION_* INAVYOFANYWA. ... _mwlproo_

Mfano; Nimewahi kusikia mtu akijitetea kwa mwenendo wake mbaya, akisema hata mtume Paulo alisema, "Analolipenda halitendi ila asilolipenda ndilo analolitenda" (Warumi 7:15). Kwa haraka haraka unaweza kudhani andiko hilo limenukuliwa mahali sahihi. Lakini ukweli ni kwamba  hapa neno la kweli halijatumiwa kwa halali. Hivyo nakuonesha namna ya kufanya exegesis ya Warumi 7.

Kosa la huyo ndugu, kurukia mstari wa 15 (prooftext method), 
akiwa ameacha mstari 1-14

 wala hajahangaika kusoma kwa kina  mstari 16-25 (_mwlproo_)

Exegetically, tunapaswa kuanza mstari wa kwanza

nao na unasema,

*“Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai?”*
  — rom 7:1 (SUV)

1. Mstari wa kwanza, Paulo kwa mkono wa Tertio anataja jamii ya waamini anaozungumza nao, kuwa wanaijua Torati!

2. Akatoa mfano wa Ndoa (namna mke anafungwa mume akiwa hai)

3. Mstari wa 4&5 anazungumzia hali ya waamini baada ya kuifia dhambi, na anazungumzia hali yao ya kwanza wakiwa katika mwili.

4. Mstari wa 15 ambao wasomaji wengi wa Biblia wameshindwa kuuelewa, Paulo hazungumzii hali yake baada ya kuzaliwa kwa Roho wa milele, badala yake anazungumzia hali yake ya kimwili inavyokuwa na ugumu kuitekeleza Torati (ambayo ameitaja mstari  wa 14, kuwa asili yake ni ya rohoni...) Kwa Torati yenye asili ya rohoni ikimkuta yeye katika umwili wake inakuwa ngumu kuitekeleza _read between lines_ verse 13-15 upate muunganiko.

5. Mastari wa 16 Paulo mtume anasema *Nikitenda nisilolipenda, naikiri sheria kuwa ni njema*

i.e., Kama sheria imesema asiibe, na yeye ikitokea ameiba.. Basi hapo hana budi kuwa na confession kuwa ile sheria iliyomwamuru asiibe ni njema.

NB:- Sheria ndiyo inafanya kosa kuwa dhahiri... pasipo sheria hakuna kosa.

Kama mtu atajitahidi kusoma na kufika mstari wa 24, lakini kwa bahati  mbaya akaacha mstari wa 25 anakuwa amepoteza ujumbe wote unaojibu maelezo ya juu.

“Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.”
  — rom 7:25 (SUV)

*UFAHAMU WA ZIADA*
Unaposoma maandiko, kabla hujajikita kushikilia mstari, unapaswa kujua waandishi wa hivyo vitabu vyote vya Biblia hawakuweka mistari.

Mistari ya Agano la Kale (Tanakh) iliwekwa na Emperor wa Kiyunani miaka 250BCE, na Agano Jipya halikuandikwa na sura wala mistari, mpaka mwaka 1225 ambapo  Kadinali Stephen Langton  (1225) na Timu yake (For the Purpose of Readability) wakaigawanya kwa sura, na bado mistari unayotaka kukomaa nayo sana iliwekwa na Robert Estienne mwaka 1551. Hapa nakupa sababu ya kuisoma kama gazeti kuliko kukomaa na verses, inayokupelekea kuchanganya maana.

KWA NINI NIMEKUPA UFAHAMU HUO HAPO JUU KUHUSU SURA NA MISTARI?

Unachosoma kwenye Warumi 8:1-2 sio jambo jipya, anatoa majibu kusuppliment alichoongea kuhusu Torati/Sheria ๐Ÿ‘‰  Uhusiano wake na utu mpya Katika Kristo

Hebu soma,

rom 8 (SUV)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
² Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
³ Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;
⁴ ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

Soma mstari wa 3 hapa, unganisha na yale aliyoyaongea Paulo kwenye sura ya saba, ujue kwamba alipoandika hakuweka hizo namba. So usifungwe na namba 7 bila kujua kuwa namba 8 ametaja alichoelezea hapo nyuma.

KAMA WAKATI WOWOTE ULIWAHI FIKIRI KWA MANENO YA (WARUMI 7:15-17) LABDA PAULO ALIKUWA AKISTRAGOOOOOOO NA MWILI

NEVER NEVER NEVER 

KILIO CHA PAULO (Warumi 7:24) WAS NOT A CRY OF DERELICTION, BUT OF TRIUMPHANT VICTORY KWAMBA KWA NJIA YA YESU, HAKI YOTE INAYOTOKANA NA MAAGIZO YA TORATI NA MATENDO MEMA, AMEIPATA KWA KUWA NDANI YA YESU.

Umeona raha ya kutafuta kujua alichomaanisha mwandishi (EXEGESIS) dhidi ya kile unachojaribu kuelewa mwenyewe (EISEGESIS)???

USIKOSE SEHEMU YA TATU YA MFULULIZO HUU. UTANUFAIKA SANA SANA

alltruth5ministries@gmail.com

Monday, September 19, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO PART 1

*KULITUMIA KWA HALALI, NENO LA KWELI*
*_Rightly Dividing The Word Of Truth_* (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA KWANZA*
_Mwl Proo_
0762879363

Ili kuepusha ufafanuzi wa mchongo wa torati ya Musa... Wayahudi wana Talmud (yenye Mishnah na Gemara) ambayo ni fasihi andishi iliyotokana na simulizi za mdomo za desturi za utekelezwaji wa Torah.
Leo katika mafundisho ya kanisa, kuna ufafanuzi mwingi wa mchongo (falsely manipulated teachings) uliosababishwa na kuepuka kanuni za kutafsiri maandiko.

Maandiko katika Biblia (ni mkusanyiko wa taarifa nyingi zikiwemo nabii mbalimbali, hadithi, maagizo ya Mungu, simulizi za desturi za kiyahudi, na taarifa zingine nyingi zilizokusanywa pamoja, zikawa 'documented'.

Humo ndani kuna mambo ambayo yanaweza kutafsiriwa kwa namna tatu kimsingi;

1. Literally (kwa kawaida tu kama yanavyosomeka

mfano (a):- Ukisoma labda mtume Paulo anaandika Salamu.. kwamba watu wa nyumbani mwa Akila na Priska wanawasalimu, au Wasalimieni watu wa nyumbani mwa Arkipo (Hii ni salutation/maamkizi tu ya kawaida).. Utaitafsiri literally bila ku-Manipulate kuepusha upotoshwaji usio na sababu.

mfano (b):- Umesoma zako Isaya 6:1, Mwaka ule aliokufa Uzia nalimwona Bwana. Katika zama za uandishi wa Biblia hususani Biblia ya Kiyahudi (Tanakh) ilikuwa ni kawaida kuandika rejea ya muda kwa kutaja tukio gani lingine kubwa (notable) lilitokea. Mfano  Amosi 1:1 anasema miaka miwili kabla ya tetemeko la nchi/ardhi (Earthquake) ikiwa ni namna nyepesi ya kukumbushia majira gani hilo lilitokea. Ni namna hiyo hiyo Isaya anataja mwaka aliokufa Uzia kama muda rejea wa maono yake. MANIPULATIONS (ufafanuzi wa mchongo) utadai, Uzia alimzuia Isaya kumwona Mungu. Kwenye maisha yako kuna Uzia ambaye inabidi afe.. Asipokufa Uzia huwezi kumwona Mungu.. Uzia anaweza kuwa ndoa au kazi yako au simu yako... It sounds vizuri  midomoni mwa wahubiri.. na mwingine atadai ni ufunuo.. Hapana, ufunuo uliopo humo kwa Biblia ni mwingi mno tu bila hata ku-Manipulate kwa sababu ya kukiuka kanuni za kutafsiri....

NB:- *MAANDIKO YA KWENYE BIBLIA HAYAWEZI LEO KUMAANISHA KITU AMBACHO MWANDISHI HAKUKIKUSUDIA WALA KUKIMAANISHA*

 Hiyo ya kudhani watu wanafunuliwa cha kuelezea ndicho kimetufikisha kwenye vituko vingi kwenye kanisa la leo.. na wengine wakiona wanalalamika tu kumbe ilisababishwa kwanza na ufafanuzi wa mchongo wa maandiko ya Biblia, na kutojua nini hasa kinapaswa kuwa fundisho katika kanisa.


2. Allegorically (Hii ni namna ya ujumbe kuwasilishwa lugha ya picha, fumbo,  mfano uliofichwa kwenye kitu kinachojulikana, na lugha za alama ๐Ÿ‘‰  figures of speech (figurative language), symbolisms... 
Ni muhimu kama unataka kuepuka makosa, kabla ya kutumia kitu kilicho katika maandiko kama kilivyoandikwa (literally), ujiulize je! sio lugha ya picha (allegory...)  NB:- parables (mifano) ni allegories fupi.. ingawa zina tofauti, ila hayo yako kwa somo jingine.

Mfano:- Unasoma zako kitabu cha Ufunuo... Unakutana na maandiko yakimtaja Yesu kama Mwana-Kondoo (Lamb), mara Yesu ni Mwana-Kondoo aliyechinjwa.... Je! ni kweli kwamba Yesu alichinjwa au alifia kwenye kinyongeo cha askari wa Rumi? Hizi ni lugha za picha kutokana na kujulikana kwake kwa hadhira (familiarity). Hata kusema huyo mwanakondoo alichinjwa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu akiwa anataka aoneshe maongeo ya mpango wa Mungu wa ukombozi tangu zamani, tangu milele. Hatari ya ufafanuzi wa mchogo ni kuleta mafundisho yenye makosa, yenye kuwakosesha sana waamini. Kila ambapo maandiko yenye lugha picha (figures of speech/allegories) yakifafanuliwa kawaida (literally) yanakosesha shabaha lengwa...nk


3. Contextually (kimuktadha)... Ingawa jambo hili nitalizungumzia sehemu ya pili ya fundisho hili, ila kwa uchache.. Kuna maandiko mengi yanapaswa kufafanushwa baada ya kufahamu muktadha husika (history of the text & history in the text). Kubeba kitu kinyume na muktadha kinaweza pelekea kuzalisha fundisho lenye makosa.

Mfano:- Mtu akisoma 1Korintho 11:13-14, kisha akawasomea wanawake wabongo kuwa mkija kanisani, mnapaswa kufunika vichwa.. Ameamua kupuuzia maandiko yenye muktadha husika na kuyaapply kama yalivyoandikwa kwa kawaida _literally_. Ulipaswa kufahamu mambo kadhaa ikiwemo ukweli kuwa kitabu/barua ya Paulo kwa waamini wa Peloponnese (Corinth) ilikuwa ni majibu ya maswali waliyomwuliza yeye kabla, kwa issues  zilizoinua disputes za hapa na pale. Kwa wanawake wa huko Uyunani hususani (elderly women, na wengine baada ya kuolewa) hawaoneshi nywele zao kwa hadhara... Kwa kufanya hivyo wanakuwa wametii desturi *_Traditional Notions of Propriety_*.. Maana mwanamke akiacha nywele ni labda kahaba au ana cheo kisiasa... Huo ndio muktadha kwa ufupi. Hivyo ni makosa, kuchukua andiko hilo la wanawake kufunika vichwa wakati wa sala, kuwasomea wandengereko, wamakua, wabena, na wamasai ukiwataka nao wafunike nywele zao wakija kanisani... Haliwahusu, halina maana hiyo, halipaswi kutumika kwa muktadha tofauti na ule wa kwenye mji wa Uyunani alikoipeleka ile barua, hata mtume Paulo hakutoa maagizo au maelekezo hayo kwa makanisa mengine kwa sababu kwao hawana tafsiri sawa na mji wa Korintho nchini Greece ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ท . Maandiko yanayohitaji kutafsiriwa kimuktadha ili kutumika.. lazima ufuate kanuni.. or else ufafanuzi wa mchongo utahusika.


USIKOSE SEHEMU YA PILI NA YA TATU YA FUNDISHO HILI, YATAKUSAIDIA SANA TU KUTOENDELEZA MAKOSA, NA UTAJIPATIA NJIA NZURI YA KUTUMIA KWA HALALI, NENO LA KWELI

alltruth5ministries@gmail.com

Thursday, August 11, 2022

ROHO YA CHOYO

*ROHO YA CHOYO*

 Mwl Proo
+255762879363

Amani iwe kwenu! 


Andiko la msingi

*“Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.”*
— Luka 12:15 

Tabia nyingi zinazojidhihirisha kwa matendo, ni matokeo ya ushawishi (influence) ya roho/spirits. Hapa sasa hata mwamini asipokuwa na nuru ya kutosha inayotokana na maarifa ya neno la Kristo, naye anaweza akashawishiwa na roho nyingine isiyo ya Kristo. Mwamini tangu anapoifahamu ile kweli (hawezi tena kumilikiwa na pepo i.e., _demon-possessed_), lakini suala la kushawishiwa (being influenced) na roho isiyo ya Kristo bado litawezekana tu, itategemea ni kwa kiwango kipi nafsi yake imejengwa (1Korintho 14:4) na kiwango cha ufahamu na maarifa ya kiroho anayotembea nayo katika kumjua Kristo.

(Visit Mwl Proo Tv on YouTube for more sermons)

Napenda kuutumia mfano wa Petro, yeye kama mmoja wa watu waliokuwa karibu sana na Yesu, tunaona katika (Mathayo 16:16-17) anaongozwa/shawishiwa na Roho wa Mungu kumtambua Yesu. Lakini mtu huyo huyo mbele kidogo katika sura hiyo (Mathayo 16:22-23) anashawishiwa na roho isiyo ya Mungu kufanya jambo lingine, ambapo Yesu anamkemea akijua nyuma ya mawazo ya Petro kuna ushawishi wa shetani. Kumbuka pia kile kilichotokea kwa Yohana na Yakobo (Luka 9:54-55), wao waliona wako sahihi kabisa kushusha moto uwaue watu waliokataa kuwakirimu. Yesu alijua wazo hilo halijatokana na ushawishi wa Roho wa Mungu, ila ni roho nyingine ya uharibifu imewatia ushawishi. Huenda ukasema, hawa walionesha tabia hizi kwa kuwa ilikuwa ni kabla ya mauti ya msalaba, hebu fikiria tabia ya kinafiki aliyoionesha Petro (na akina Barnaba) akiwa amejaa Roho tayari yaani amezaliwa upya na amekuwa mtume mwenye uzoefu mwingi (soma Wagalatia 2:11-17). Hii inatuambia hata mwamini anaweza kushawishiwa na roho nyingine kutenda matendo fulani yasiyopatana na tabia za mtoto wa Mungu.


*MOYO WA SOMO*
Kwa kutambua hayo yaliyo katika utangulizi, hiki anachokisema Yesu  kwenye Luka 12:15, kujilinda na choyo ni zaidi ya tabia tu, bali tabia inayoshawishiwa na roho (roho ya choyo) ambayo hata mtoto wa Mungu asipoangalia anaweza kujiingiza katika mtego wa hii roho. Somo hili nimeliandika leo 11/8/2022 lakini nililipata mwaka 2017. Na lilinijia kama wazo baada ya kijana fulani ambaye nilikuwa naye kwenye kundi la VIJANA NA MAISHA la WhatsApp, kunifuata inbox kunisihi akisema,  *"Nenda kule grupuni, ukahamasishe watu watoe michango kwa ajili ya harusi yangu".*
Hapohapo nikakumbuka mtu huyu amekuwepo kwa hilo kundi tangu mwaka 2014, hajawahi kushiriki mambo ya watu yenye uhitaji wa fedha wala muda wake. Tumepitisha mikeka ya kuchangia harusi/send offs za wengine hakuwahi tokea. Tumepitisha mikeka ya kuchangia rambirambi za waliofiwa na waume/wake/wazazi akiwa humo humo hakuna mkeka uliwahi kuonesha jina lake hata kwa kutoa buku tu (1000/=). Muda natafakari naanzaje kuhamasisha watu wajitoe kwa mtu ambaye aligeuza kisogo kwenye mambo ya watu, ndani mwangu nikasikia kitu hicho *_roho ya choyo_*.

_mwlproo_

Roho ya choyo inamfanya mtu kuangalia mambo yake tu. Roho ya choyo inamfanya mtu atamani kukusanya na kujijazia na hata akiwa navyo vingi anabaki mnyimi hatoi kabisa, anaweza kuwa radhi hata kudhulumu (Ezekiel 22:12). Hebu soma haya maandiko hapa chini

*“Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.”*
  — Wafilipi 2:4 

*“Kuna atamaniye kwa choyo mchana kutwa; Bali mwenye haki hutoa wala hanyimi.”*
  — Mithali 21:26

*“Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe;........wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.”*
  — Isaya 56:11

Waamini lazima wajifunze kutenda kinyume na roho ya choyo, ndio namna bora ya kuishinda roho hii. Epuka uchoyo, epuka kuwa na umimi, kujiangalia mwenyewe, kujitanguliza mwenyewe. Unatakaje kuvuna kwa watu ambao hukupanda chochote? (Galatia 6:7), unaweza kusema huna hela, lakini hatupandi hela pekee. Panda muda wako kwa wengine, panda vitu, panda ukarimu, jitoe na jihusishe kwenye mambo ya watu. Hakuna kiwango cha kiroho kinachofanya usiweze kuhudhuria harusi za watu, misiba au kuwaona watu wakiwa mahospitalini, hata kwenda kuwaombea basi. Kuna mtu hela zake hakuna mtu anagusa, kuwabariki watu wenye uhitaji hata kwa chakula siku moja tu. Ni mara ngapi unakutana na vitu vizuri mtandaoni iwe ni masomo ya neno la Mungu, nyimbo za Kikristo, au vitu vingine, ukakumbuka hata ku-Copy na ku-Share? inakuwaje vinavyobariki uvienjoi  peke yako tu...!!??  Natumia tone ya maisha ya kisasa, kuna wale ambao wao kutwa-kuchwa wanatumia watu links za channels, pages na accounts zao za mtandaoni, wakihamasisha USISAHAU KU-LIKE, KU-SHARE, KU-SUBSCRIBE, NA KUWEKA NOTIFICATIONS ON ๐Ÿ””, swali mwenzetu ume-Like ๐Ÿ‘  za wenzako? ni roho ya choyo tu hapo. Unatuma links kibao kwenye whatsapp groups za watu, ila zikitumwa za kwao kwako unawa-remove dakika 0 tu, sio kawaida ni roho ya choyo tu hapo. Ni roho ya choyo inayokuelekeza nguo zilizokubana uzichome moto badala ya kuwakarimu wengine ambao zingewafaa. Ukiombwa michango ya harusi sijui send off unaweza kushindwa kutoa kiwango chote lakini usiuchune mazima.. tuma hata ka-elfu 5 tu, kuwa umekamatika na kusongwa kwa mengi... Haya ya kuhisi hutahitaji watu kwako yatakutokea puani.. Mambo ya kijamii yanahitaji jamii. Kuna wakati nilishuhudia kwenye mazishi ya ndugu yangu fulani, waliofuata mwili mortuary ni watu baki tu wa mtaani kwa marehemu, walioenda kuchimba shimo bila kudai hata 100/= tshs ni vijana tu wa bodaboda ambao marehemu aliishi akiwaheshimu na kuwasalimia kila akipita... Unapopanda kwa watu (Luka 6:38), unavuna toka kwa watu, na kama ukarimu wako ukiwa mwingi Mungu anaweza sukuma mioyo ya watu wakutegemeze na kukukirimu wewe wakati wa uhitaji (1Samwel 10:26).

Haihitajiki maombi mengi sana, ila kubadili nia/ufahamu kwa kufanya upya na kuanza kutenda kinyume na choyo. Vitu vya thamani kwako, vinavyokupendeza, unavyohisi kuvihitaji zaidi, unavyohisi vinakutosha wewe peke yako.... ๐Ÿ‘‰  Wape watu, wabariki wengine.... vitoe kanisani vikatumike nyumbani mwa Bwana, anza kujifunza kubadili matumizi yako ya luxury kwa kugharimia mahitaji ya lazima ya watu wanaokuhusu na wasiokuhusu. Na yale mambo yanayohitaji uwepo (physical presence) usitume wawakilishi au kutuma hela, kila inapowezekana nenda wewe mwenyewe... Kwa kutenda kinyume na choyo unainyamazisha roho ya choyo

Mungu awabariki sana
0762879363/0765713112

http://alltruthjohn1613.blogspot.co.ke/2016/?m=1

Wednesday, April 6, 2022

THE FLESH (UFUNUO JUU YA MWILI)

*UཽFཽUཽNཽUཽOཽ  JཽUཽUཽ  YཽAཽ  MཽWཽIཽLཽIཽ*

*T̸͟͞H̸͟͞E̸͟͞  F̸͟͞L̸͟͞E̸͟͞S̸͟͞H̸͟͞*

*สีกำ€ ินษพึ…ึ…*
_0762879363_

Amani na neema zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana wetu Yesu Kristo ziwe  nawe ndugu msomaji. Karibu ujifunze siri ya Bwana kwa somo hili...

๐Ÿ‘ค Tumekuwa na masomo mengi yanayotuonesha namna mwili ni adui wa roho, namna mwili unatukosesha, namna mwili hauyataki mapenzi ya Mungu, na kila somo lenye mwelekeo huo. Somo hili ni upande wa pili unaoachwa sana...

๐Ÿ‘ค Mwili huo wenye shida hizo zote, unatakiwa kuliko kawaida. Mungu ameleta ufunuo huu ambao haupingani na kweli bali kwa ajili ya kweli. Fuatilia kwa taratibu, utapata ufunuo ambao Mungu ameamua kutufundisha.

Zaburi 8:3-8, Mwanzo 1:26-27, Ebrania 2:7

(Zaburi 8 ) 
------------ 
*5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;*
*6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.*

Katika andiko letu la msingi mstari (5) neno linaonesha, mwanadamu aliumbwa punde kidogo kuliko Mungu (Little lower, little less than God)... Huenda Kiswahili kikawa hakijaeleweka sana hapo, lakini kinachotajwa hapa ni kwamba mwanadamu kaumbwa kwa nafasi (rank) ya juu yaani ilibaki kidogo tu awe kama Mungu. Baadhi ya tafsiri za kingereza wameondoa neno Mungu na kuweka neno malaika hapo. Sasa katika Biblia ya Kiebrania, neno pekee lililojitokeza hapo ni *ืֱืœֹื”ִื™ื* lisomekalo *สผฤ•lรดhรฎym* (el-o-heem)... Hakuna mahali jina Elohim liliwakilisha malaika. Lakini kimsingi andiko hili lilitaka kuonesha kuwa mtu aliumbwa kwa rank ya juu kuliko malaika (hayo ni mambo ambayo mwanadamu akiwa ndani ya mwili hayaelewi kwa wepesi). 

๐Ÿ”ฅ ``` Kama wanadamu wangeelewa kile walichonacho na nafasi zao, tusingekuwa na wanadamu wanaojiharibu miili yao, kwa uzinzi, kwa ulevi, kujiua etc maana nafasi yao ni kubwa sana, ni kwa wote wenye miili hii ya damu na nyama hata kama bado hawajaamini katika Yesu... (Imani katika Yesu inakuja kukufungua akili. na kuyaelewa yote uliyokirimiwa na Mungu).```

๐Ÿ”ด Mwanadamu ambaye amefanywa punde kidogo kuliko Mungu, ana thamani zaidi duniani na rohoni akiwa na mwili (huu wa mavumbi).

✍๐Ÿพ Mungu aliumba mtu rohoni. Na akiwa mtu-roho hangeweza kufanya lolote kwenye dunia. Kanuni ya Mungu kwa mtu-roho kuopareti kwenye ulimwengu unaoonekana kulipaswa kuwa na mtu-mwili. Na hii ni kanuni inayoongoza rohoni, kwamba roho zinapaswa kuwa na miili zikitaka ku-opareti duniani.

✍๐Ÿพ Hapa ndipo idea ya "roho kujivika miili" *incarnation* ilipoanzia. Kila utakaposoma katika maandiko kama ni malaika au viumbe wengine wa kiroho walipotaka kujichanganya na watu wenye mwili, walipaswa kujivika miili ya damu na nyama.. (Yesu angeweza kushuka kiroho-roho maana anao mwili wa roho, lakini alihitaji mtu-mwili, na kwa sababu hiyo alizaliwa kimwili kwa uwezo wa Roho). Rejea somo langu liitwalo *Mwili wa Roho*.  Viumbe vya kiroho (vilivyoumbwa kwa ratiba ya Mungu, viliumbiwa uwezo wa kujivika miili inapobidi (Rejea somo langu la *"Roho za wanadamu kuwezeshwa*)... Wana wa Mungu katika Mwanzo 6 (Watchers of heaven) walihitaji miili ya nyama ili kujichanganya na shughuli za wanadamu (Enoch chapters 6&7), Malaika waliomtembelea Ibrahimu kule Mamre hawakuja kwa miili ya rohoni, bali kwa miili ya nyama (they incarnated themselves).. ndio maana waliweza kula supu ya ndama na mikate ๐Ÿฅ˜๐Ÿ–๐Ÿ—๐Ÿฅฉ๐Ÿž๐Ÿž, na kwa miili ile walitembea kwa miguu umbali mrefu, wkachafuka kabisa, ingawa ni malaika walisafiri mpaka Soari hata kufikilia Sodoma kwa Lutu.

NB:-
*Miili ya damu na nyama inapatikana kwa njia za uzazi (procreation), Mungu aliestablish kanuni hiyo ya kuifanya miili itokee (mambo ya reproduction/kuzaa) hayatengezi roho za wanadamu bali miili (chombo cha kubebea roho). Mwili ni bidhaa adimu mno, kwa viumbe halali wa kiroho kama nilivyoeleza katika somo jingine, kuwa waliumbwa na uwezo ndani yao (built-in ability) wa kujivika miili, inapobidi (Sio kwamba kila aonekanapo malaika wa mbinguni amejivika mwili, bali mwanadamu anaweza funguka macho ya rohoni yanayofanya viumbe vya kiroho viwe physically visible).*

๐Ÿ”ด Kusudi la Mungu kumwumba mtu na mwana wa mtu (mwanadamu) duniani linawezekana tu, wakati huyu mtu akiwa na *mwili/basar* 
✍๐Ÿพ Kuuwakilisha ufalme wa Mungu hapa duniani (Mwanzo  1:27-28)
✍๐Ÿพ Kumwabudu Mungu na kumsifu (Isaya 38:18-19, 30:9, 6:5).... God created spirits then He formed bodies.... Ameweka kanuni hii moja ya msingi, kwamba hayo yote mtu atayafanya akiwa na mwili tu.

✍๐Ÿพ Mwanadamu akiupoteza mwili wa nyama na damu (iwe kwa kifo au njia nyingine) anapoteza uhalali wa kuendelea kubaki duniani. Roho za wanadamu zilizopoteza miili yao haziachiwi kuzagaa mahali popote (Ayubu 7:9ff), kuna mahali zitapaswa kuwepo (Rejea somo langu la *"Umilele"*).. Nimewahi sikia cases kadha wa kadha za watu ambao waliondoka duniani kwa bahati mbaya kwa kuipoteza miili yao. Nahifadhi jina la mwanamuziki wa kiKongo wa zamani, ambaye kwa simulizi niliyoipata alikuwa mtu wa kufanya *Astral travel (levitation)* yaani unauacha mwili unajichomoa roho yako na kusafiri kwa makusudi fulani ya ufalme unaoutumikia rohoni. Sasa katika hizo ziara za kiroho, kuna wakati alisafiri na akakawia sana kurudi, mwili ukaoza. Hivyo hakuweza kuuingia tena mwili wake na hivyo anaitwa huku nje amekufa, hana uhalali wa kuopareti duniani kwa ile roho yake, hana uwezo tena wa kuona familia yake na kuendeleza muziki wake, hayo angeyafanya kama lile limzoga lake (outer  carcass) lisingeoza (Swala la mizimu limezingatiwa katika somo la Umilele utapata ukweli wake). Miili ya damu na nyama halali kutenda kazi duniani permanently inapatikana kwa kuzaliwa na mwanamke, mtu akiupoteza mwili hakuna namna ya kuupata tena (Ni Yesu tu, anao uweza wa kuipa roho ya mwanadamu mwili mwingine, nje ya kanuni ya asili ya kuzaa, na nje ya kanuni ya uumbaji wa mwanzo). Ninao ushuhuda wa mwinjilisti toka Muleba, ambaye akiwa katika ufalme wa giza, mbele za shetani aliomba ruhusa akaoneshwe ziwa la moto. Shetani aliruhusu akaoneshwe kwa masharti kwamba awaachie mwili wake wa damu na nyama, ili kwamba hata kama atapata wazo la kukengeuka toka kwenye ufalme wa shetani basi asiwe na nafasi ya kurudi duniani, maana shetani anajua siri hii ya mwili kwa kina sana, kwamba ukipoteza mwili wako, kwisha habari yako. Na huyu mwinjilisti ameeleza katika huo ushuhuda kwamba alipoona ziwa la moto alimwona Yesu pia, na kulikuwa na tishio kuwa kule alikouacha mwili wake wanakusudia kuuchoma moto. Na Yesu alimwambia kuwa  mwili wako wanataka kuuchoma moto, lakini ninaweza kukupa mwili mwingine... (Sio kusudio langu kuleta shuhuda za kuzimu, nilikuwa najaribu kukazia maarifa).

✍๐Ÿพ Roho za watakatifu na mashujaa katika Mungu, hazina effect/athari yoyote katika ufalme wa giza. Kitendo cha hawa watu wa Mungu kuondoka duniani kwa kupoteza miili yao (kwa kifo), hawana athari tena... hata kama alikuwa nabii mkubwa sana mwenye upako kama wa Elisha Ben'Shaphat wa kufufua mtu kwa mifupa yake baada ya yeye kufa. Shetani haogopi watu-roho, anaogopa sana watu-miili wakiwa wanamjua Mungu na kukaa katika uwepo wa Mungu wakiwa na miili hii.... Ndio watu pekee wanaweza kumvurugia chochote katika ufalme wake..

๐Ÿ”ด Roho Mtakatifu hapa duniani anaihitaji miili yetu, hii ya damu na nyama.
Yoel 2:28, Mdo 2:17, 1Cor 3:16, 6:19
✍๐Ÿพ Mungu anaahidi kumwaga Roho wake juu ya wote mwili... kama kuna roho ina-Hang na haina mwili wa nyama ahadi hii sio yake... Bali ni juu ya wote wenye mwili, Mungu ni Mungu wa wote mwili..... 

✍๐Ÿพ Roho Mtakatifu akija kwa mtu anamzaa upya roho yake, lakini mwili wa huyu mwenye Roho wa Mungu, huuishwa (the body is quickened) Warumi 8:11... Na Roho wa Kristo huufanya mwili kuwa makao safi ya kumfaa, kumbuka Roho Mtakatifu yeye ni roho hakai kwenye roho zetu bali kwenye miili yetu...Miili yetu ni hekalu lake, hukaa humo.. Usisahau hili Roho Mtakatifu anauhitaji mwili wako, usiuharibu, ukiuharibu anachukizwa, naye anakuharibu wewe mharibifu (Naelewa sasa ule wimbo uitwao *Fill this temple* una verse isemayo _"let me be a holy habitation where your Spirit is pleased to dwell"_. 

๐Ÿ”ด Mashetani yanahitaji mwili, yakitaka kufanya mambo yao katika dunia.
Mashetani (Demons) wao ni roho, lakini waliwekewa amri ya kubaki duniani na hawana  miili... Malaika wa Mungu na malaika za Shetani (waasi/walioanguka) wanayo miili yao ya roho, na wanaouwezo wa kujivika miili tofauti-tofauti (2Kor 11:14-15)... Lakini mashetani ninayoyataja hapa (demons) ni roho ambazo hazina miili, miili yao ya nyama waliipoteza (Mwanzo 6), na kwa sababu hiyo kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Henoko 15:8-9 kwa roho za majitu (giants) yaani spirits of nephilims wataitwa pepo wabaya (roho chafu) na mahali pao patakuwa duniani, watasumbua wanadamu maana miili yao wameipoteza na wao asili yao ni mbinguni na hawana uhalali wa kuwa huko. Luka 11:24ff, Mathayo 12:43ff... Yesu anasema pepo mchsfu amtokapo mtu.......  then akikosa mahali (mwili mwingine wa mwanadamu au mnyama) anapata wazo la kuirudia nyumba yake... 

NB:- Hakuna wakati pepo wabaya wataacha kung'ang'ana na miili ya wanadamu, maana wameamriwa sehemu yao iwe hapa duniani, na miili yao waliipoteza. They wish ku-opareti katika dunia, lakini kanuni moja wapo ya kufanya mambo hapa duniani ni kuwa na mwili wa damu na nyama... Hivyo pepo wabaya shauku yao inatekelezeka tu wakiwa ndani ya mwili, bila mwili wa kiumbe hawana kazi yoyote.. Ndio maana katika case ya Mgerasi, pepo walimsihi Yesu aliwaamuru kwenda kwenye *Abussos* ambako hata wao hawakutaki kwa hilo shimo walidai ni bora awape ruhusa wawaingie nguruwe, katika kutafuta uhalali wa kuendelea kuopareti maeneo yale... (Wanaosema wanafuga majini, kuna jambo kubwa hawalijui).....

๐Ÿ”ด Mungu anailinda miili kuliko  hata roho zetu... maana hatari zinaweza kumkuta mwanadamu zinaweza kuuathiri mwili wake na sio roho yake... Mtu anaweza kanyagwa na gari akasagwa kabisa, akaungua moto akabaki kama mkaa au jivu kabisa, lakini hayo mateso na maumivu ya kifo yatautesa mwili roho yake itaondoka kwa salama. Lazaro maskini na mgonjwa mwenye *vidonda vingi* (Luka 16:19-31) alipokufa roho yake ilitokea katika ulimwengu mwingine bila maumivu ya vidonda... Ila mwili wake ule wa duniani wenye ulikuwa na kazi kubwa ya kumwandalia maisha yasiyokoma ya baada ya kuuacha ule wa mavumbi. Najua kuhusu andiko la Ayubu 10:12, maangalizi ya Mungu yanalinda roho zetu, lakini nikujuze kwamba miili yetu inalindwa zaidi (Zaburi 71:3, Ayu 33:24ff, Mathayo 10:29)..
Nimekumbuka na Biolojia ya kidunia, from the Conception (mimba kutunga) Mungu anailinda mpaka mtu muda anazaliwa... Tena kijusi (embryo) kikiwa huko ndani Mungu anakizungushia kimiminika *Amniotic fluid* chenye kazi ya kufyonza maumivu iwapo mama atajibamiza tumbo *Shock Absorbant*, kwenye hesabu za Mungu analenga kuusaidia huu mwili ukue utoke salama, ukatimize kusudi la kuweko kwake (Case ya watoto wanaofia tumboni, imejibiwa katika somo jingine Efeso 1:10)... 

๐Ÿ”ด Sisi wanadamu ni roho, tunaihitaji miili sana. Na hivyo, tunapaswa kuitunza, kuihifadhi, kwa yale yanayotuhusu kuyafanya ili miili iwe vizuri, tuyafanye kwa bidii.

๐Ÿ‘‰๐Ÿฝ Usipuuzie mambo yahusuyo afya, lishe, usafi. Maeneo mengi ya Afrika kwa sababu ya umaskini kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa maswala ya muhimu kwa kuutunza mwili. Watu kula vyakula vya ovyo, visivyofaa kwa afya mwadamu, uchafu kwenye vyakula, maji yasiyo salama, na vitu vingi vyenye kuuathiri mwili.Wengi wamepata shida na kuondoka duniani, huku watu wakiendelea kunukuu Ayubu 1:21b kwamba Bwana ametao na Bwana ametwaa (Msomaji wangu, Yesu akufungue akili sasa....Usile vyakula vinavyoharibu mwili na inajulikana hivyo,usile vyakula vichafu, au kukaa kwenye mazingira machafu na lolote linaloweza kuleta athari kwenye mwili, maana umepewa huo mmoja tu. Kama kazi unayofanya inahatarisha sana usalama wa mwili, mwombe Mungu na ukipata kibali badili kazi hiyo, kama ni michezo au mazoezi yanaleta tishio la mwili kuharibika, acha tu... Kwa maana when the body is struck by terminal injuries, the door to death is opened)... Na kama nilivyoeleza katika somo la umilele, roho ya mtu ikiona haiwezi kuendelea kuutumia mwili kwa kuwa umeharibika sana, inatoka (ndicho kifo hicho). 

๐Ÿ‘‰๐Ÿฝ Usikubali kuishi na magonjwa au maradhi. Magonjwa ni moja ya vyanzo karibu tisa vya kifo, nilivyoviainisha katika somo la umilele. Narudia tena, usikubali kuishi na magonjwa. Magonjwa yanaweza kumpata mtu yeyote akiwa katika mwili (Katika mwili huu twaugua)....  Lakini mtu anaweza kuiinua imani yake kwa kiasi cha kuyazuia magonjwa kabisa. Kama hiyo ni ngumu kwa baadhi ya watu, basi kila mKristo mwenye kuijua kweli ajifunze kutoishi na magonjwa... Sijasema mtu hataumwa chochote, ila usikubali kuishi na magonjwa permanently, kama imetokea umeugua, ukiwa na imani ya kupona kwa muujiza omba upone, na ujiridhishe umepona hata kwa kwenda kuupima ugonjwa. Kama unaona huo ugonjwa unaweza ukatumia dawa ya hospital mara moja na ukaondoka fanya hivyo... Ukiishi na magonjwa yanaweza kuleta shida kwenye mwili yakakuondoa muda wowote... Ni juzi nimesafiri kwa basi na njiani waliweka historia ya mwanaMuziki aitwaye Bob Marley, namna ambapo kijidonda kidogo sana cha kuchoma na kisindano akakaa nacho miaka minne kikawa kansa mbaya na kumwondoa duniani akiwa na miaka 26

๐Ÿ‘‰๐Ÿฝ Na kuna magonjwa ya hatari ambayo huwa yanakaa kwa mtu mpaka yamemwondoa duniani... Magonjwa mengi yanayodjambulia mifumo ya mwili (body systems) kama mfumo wa hewa, mfumo wa damu, mfumo wa chakula, mfumo wa uzazi, mfumo wa utoaji taka mwili, mfumo ya fahamu na mifumo mingine iliyopo... Magonjwa yanayovuruga mfumo mmoja yana desturi ya kuharibu na mifumo mingine.. Mtu akiwa na magonjwa haya, akaanza matibabu,na akajiridhisha na kuridhika kuwa yeye ni mgonjwa wa hayo magonjwa, akakubali kuendelea kuishi nayo, anakuwa amehalalisha safari ya kifo kwa amri ya ugonjwa. Mtu anajua ana presha (LBP/HBP) na anajua kuna muda presha inashuka mpaka anahisi anakufa. au inapanda mpaka anahisi amekwisha toweka duniani, then kama ataendelea kukubali kukaa nayo hiyo presha isiyo sawa, awe na uhakika kifo ameamua kuishi nacho...Unapopewa majibu ya hospitali kwamba ini lako lina shida, figo zako haziko sawa, mapafu yako yana shida, bandama yako ina shida, una shida kwenye utumbo mpana, una tundu kwenye moyo, una uvimbe unaoashiria kansa n.k n.k n.k taarifa hizi hazipaswi kupokelewa rohoni mwako, kama wewe msomaji ni mtu wa ile kweli... Shida ambazo hazitibiki kwa mara moja, zinataka kuwa lifelong uendelee na matibabu ya kuvutavuta siku zikiwa na mateso, USIZIKUBALI, NA USIYAKUBALI MAISHA HAYO, KAMWE USIKUBALI KUISHI MAISHA YA MFUMO WA KITABIBU, kwamba kuanzia sasa kwa kuwa una kisukari, hakuna kunywa hiki na kile, hakuna kula hiki na kile etc, ukijiingiza kwenye mfumo huu, utasaidia kuvutavuta muda wa kuishi kwa mateso lakini safari ikiwa sio yakini (uncertain) kwamba muda wowote ugonjwa ukichachamaa unaiacha dunia. 

*POINT YANGU NI HII*
Kwa wewe mwamini. mwenye kuijua kweli, option ya kwanza ni hii... Pambana katika roho kuhakikisha magonjwa ya kutisha uyajuayo ya kiMisri (Kumb 7:15) uyazuia yasiupate mwili wako, hili linawezekana kabisa kwa kuomba kwa bidii na kwa kuishika ahadi ya Bwana juu ya afya ya mwili wako... Hili litawezekana kabisa kama continually utaendelea kuishikilia afya ya mwili wako kwa maombi na kwa kushindana rohoni daima, na bila kusahau kama kuna mambo ambayo kwa dhahiri yandhuru mwili basi uyaache au kuyaondoa. 

*NB:-* Kumbuka hili ni rahisi zaidi kuzuia maradhi rohoni kwa imani, ili yasije... kuliko kuyaondoa yakiishafika.. Hivyo best option ni ya kuzuia kabisa, sisemi kwamba Mungu haponyi, Yeye ni YHWH Raphah anaponya ugonjwa wowote hata kama upo kwenye last stage ya ubaya (Kutoka 15:26)... Lakini hapa unaipata kweli ya Mungu kuhusu mwili ujue namna mwili unaoparet bila kusingizia vifo vyote ni mapenzi ya Mungu... Maana maradhi yakifikia kiwago fulani cha kuudhuru mwili, roho inaondoka... Elisha nabii  mwenye double portion anointing alikufa kwa homa tu.... 

๐Ÿ‘‰๐Ÿฝ Kama kwa namna yoyote tu ile, wewe mwamini umejikuta tayari ugonjwa upo ni ugonjwa wenye hatari ya kifo... Basi unaweza kung'ang'ana na uponyaji wa Mungu mpaka ujiridhishe kabisa kuwa ugonjwa umeondoka, kuendelea kuuguza miaka minne haina maana kuna usalama wowote, ila kwa kudumu nao utapata shida zingine... acha mambo mengine, simama kwa zamu yako ushughulikie mpaka ujiridhishe ugonjwa umeondoka...NA INAWEZEKANA KABISA

๐Ÿ•ฏ ๐Ÿ”ฆ USHUHUDA NO1
Mwaka 2006, nilipata shida ya moyo kwa ghafla tu... Nilikuwa nakimbia kwenye mvua kali, nikasikia kama shoti ya umeme (electric shock) eneo la moyo na maeneo mengine.... Basi tangu hapo nikawa nahisi maumivu ya moyo, presha inashuka mpaka nasikia ni kama moyo unataka kunyamaza kabisa, nikiamka asubuhi nahisi ganzi ya moyo mpaka kwenye vidole vya mguuni... ilidumu miezi kadhaa huku nafikiria kweli nami nitapelekwa India kwa shida ya moyo... na ndoto zote zikawa zinakuja za kuonesha nitapaswa nikatibiwe huko nje... Nililisikia neno moja tu toka kwa Mtumishi wa Mungu Askofu Zachary Kakobe (ibada ya kwanza ya mwaka 2007) basi, nilitoka nyumbani jioni nikaenda kanisani (EAGT), nikiwa pekeangu nilisema maumivu kwenye moyo mwisho wako ni sasa, niliamuru shida ya moyo itoke, na yale maumivu eneo la moyo, yalihama toka moyoni yakasogea karibu na bega, kisha yakasogea kama yanakuja kinywani,na kupotea kabisa..IKAWA MWISHO KABISA WA TISHIO LA TATIZO LA MOYO.

๐Ÿ•ฏ ๐Ÿ”ฆ USHUHUDA NO2
Mwaka 2017 October nilipatwa na Ulcers kwa sababu ya misbehaving ya ratiba za kula... Maisha ya kukaa bila kula (na nikiwa sijafunga)... Kuna tofauti sana kati ya kufunga na kukaa na njaa....  Na hapa wapenzi wa kuomba na kufunga, wafunga sena ila kwa akili... Ninazo picha za Mzee wa kanisa mmoja mkoani Iringa, ambaye miaka miwili ikiyopita alienda kufunga porini mfungo wa mwezi mzima, lakini walipomtafuta baada ya wiki kadhaa tangu aanze waliukuta mwili umekauka kabisa, kuna kitu hakikuwa sawa na mashauri ya kiroho yalikosekana, anaweza kwenda mbinguni, ila hasara aliyoisababisha kiroho ni kubwa kwa kuuharibu mwili wake. Mimi nilikuwa nakaa na njaa muda mrefu kwa sababu ya mazingira niliyokuwa nayo kazini, kurudi ghetto kupika chakula mchana na usiku ilikuwa ngumu sana. Sasa shida ilipozidi nilienda hospitali.. Nikakutwa na ulcers... Nilianza matibabu lakini pamoja na dawa zote nilishaambiwa hizi hazitibu kabisa-kabisa... Hivyo nikaamua kutumia njia ya pili ya imani, kuhakikisha ulcers zinakaushwa kabisa...  Naukumbuka usiku wa manane ambao nilishughulikia ulcers... Sikumwambia tu Mungu aniponye ulcers, ila nilijiondoa kabisa rohoni katika watu ambao wamewahi umwa ulcers... Na ili nijiridhishe nilipoamka nikaanza maombi ya kufunga mwezi mzima nione kama kuna shida yoyote, nikamaliza mfungo nikiwa sijawahi hata kuhisi maumivu, ndivyo nipo mzima mpaka sasa hata maombi ya kukaa masaa 72 bila kugusa chochote nafunga bila tatizo lolote.

☝๐Ÿฝ☝๐Ÿฝ☝๐Ÿฝ☝๐Ÿฝ☝๐Ÿฝ☝๐Ÿฝ☝๐Ÿฝ☝๐Ÿฝ

```Nimekupa shuhuda hizo mbili, ili ujue kwamba unao uwezo wa kuuondoa kabisa huo ugonjwa ambao vipimo vimethibitisha unao...  Ukiamua kuishi nao, ugonjwa utajiotesha mizizi na kuwa permanent..
Mimi nilikataa kuwa na ulcers maana niliona haviendani na mtu wa rohoni ambaye anataka kila wiki afunge, amtafute Bwana etc... Nawe hata kama shida ipo tayari komaa na uwezo wa kiUngu ulio ndani yako mpaka ugonjwa utoke.```

*NB:-*

_*KUNA SHIDA NYINGINE IMEKUPATA NA UNAONA KABISA JWA NGUVU ITENDAYO KAZI NDANI YAKO, HUWEZI KUIINUA IMANI YAKO KWA KIASI CHA KUUNG'OA HUO UGONJWA, TAFUTA NGUVU YA ZIADA, HATA KWA MTUMISHI WA MUNGU MWENYE NGUVU KUBWA ZAIDI, MAANA  HATUWI NA NGUVU SAWA  ROHONI INGAWA WOTE TUMEOKOLEWA NA KUJAZWA ROHO MMOJA... JITAHIDI UPATE SOMO LANGU LIITWALO "KUYAPELEKA MAGUMU KWA MTUMISHI MWENYE NGUVU KUBWA ZAIDI"*_

~*Mungu awabariki sana... Mwili wako huo, unahitajika, ni wa muhimu, swala la upo mrefu, mfupi, mnene, mwembamba, mweusi tiii, mweupe pee na chochote kila katika mwili wako hakina umuhimu kama umuhimu wa uwepo wa huo mwili wenyewe....Roho yako imebebeshwa mambo mazito  ambayo kabla ya kifo utapaswa kuyafanya, lakini hayo yote yatawezekana tu kama ukiwa na huo mwili... UPENDE MWILI WAKO KWA JINA LA YESU*~

_Mwl Proo_
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com