Wednesday, April 6, 2022

THE FLESH (UFUNUO JUU YA MWILI)

*UཽFཽUཽNཽUཽOཽ  JཽUཽUཽ  YཽAཽ  MཽWཽIཽLཽIཽ*

*T̸͟͞H̸͟͞E̸͟͞  F̸͟͞L̸͟͞E̸͟͞S̸͟͞H̸͟͞*

*ʍաӀ Թɾօօ*
_0762879363_

Amani na neema zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana wetu Yesu Kristo ziwe  nawe ndugu msomaji. Karibu ujifunze siri ya Bwana kwa somo hili...

👤 Tumekuwa na masomo mengi yanayotuonesha namna mwili ni adui wa roho, namna mwili unatukosesha, namna mwili hauyataki mapenzi ya Mungu, na kila somo lenye mwelekeo huo. Somo hili ni upande wa pili unaoachwa sana...

👤 Mwili huo wenye shida hizo zote, unatakiwa kuliko kawaida. Mungu ameleta ufunuo huu ambao haupingani na kweli bali kwa ajili ya kweli. Fuatilia kwa taratibu, utapata ufunuo ambao Mungu ameamua kutufundisha.

Zaburi 8:3-8, Mwanzo 1:26-27, Ebrania 2:7

(Zaburi 8 ) 
------------ 
*5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;*
*6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.*

Katika andiko letu la msingi mstari (5) neno linaonesha, mwanadamu aliumbwa punde kidogo kuliko Mungu (Little lower, little less than God)... Huenda Kiswahili kikawa hakijaeleweka sana hapo, lakini kinachotajwa hapa ni kwamba mwanadamu kaumbwa kwa nafasi (rank) ya juu yaani ilibaki kidogo tu awe kama Mungu. Baadhi ya tafsiri za kingereza wameondoa neno Mungu na kuweka neno malaika hapo. Sasa katika Biblia ya Kiebrania, neno pekee lililojitokeza hapo ni *אֱלֹהִים* lisomekalo *ʼĕlôhîym* (el-o-heem)... Hakuna mahali jina Elohim liliwakilisha malaika. Lakini kimsingi andiko hili lilitaka kuonesha kuwa mtu aliumbwa kwa rank ya juu kuliko malaika (hayo ni mambo ambayo mwanadamu akiwa ndani ya mwili hayaelewi kwa wepesi). 

🔥 ``` Kama wanadamu wangeelewa kile walichonacho na nafasi zao, tusingekuwa na wanadamu wanaojiharibu miili yao, kwa uzinzi, kwa ulevi, kujiua etc maana nafasi yao ni kubwa sana, ni kwa wote wenye miili hii ya damu na nyama hata kama bado hawajaamini katika Yesu... (Imani katika Yesu inakuja kukufungua akili. na kuyaelewa yote uliyokirimiwa na Mungu).```

🔴 Mwanadamu ambaye amefanywa punde kidogo kuliko Mungu, ana thamani zaidi duniani na rohoni akiwa na mwili (huu wa mavumbi).

✍🏾 Mungu aliumba mtu rohoni. Na akiwa mtu-roho hangeweza kufanya lolote kwenye dunia. Kanuni ya Mungu kwa mtu-roho kuopareti kwenye ulimwengu unaoonekana kulipaswa kuwa na mtu-mwili. Na hii ni kanuni inayoongoza rohoni, kwamba roho zinapaswa kuwa na miili zikitaka ku-opareti duniani.

✍🏾 Hapa ndipo idea ya "roho kujivika miili" *incarnation* ilipoanzia. Kila utakaposoma katika maandiko kama ni malaika au viumbe wengine wa kiroho walipotaka kujichanganya na watu wenye mwili, walipaswa kujivika miili ya damu na nyama.. (Yesu angeweza kushuka kiroho-roho maana anao mwili wa roho, lakini alihitaji mtu-mwili, na kwa sababu hiyo alizaliwa kimwili kwa uwezo wa Roho). Rejea somo langu liitwalo *Mwili wa Roho*.  Viumbe vya kiroho (vilivyoumbwa kwa ratiba ya Mungu, viliumbiwa uwezo wa kujivika miili inapobidi (Rejea somo langu la *"Roho za wanadamu kuwezeshwa*)... Wana wa Mungu katika Mwanzo 6 (Watchers of heaven) walihitaji miili ya nyama ili kujichanganya na shughuli za wanadamu (Enoch chapters 6&7), Malaika waliomtembelea Ibrahimu kule Mamre hawakuja kwa miili ya rohoni, bali kwa miili ya nyama (they incarnated themselves).. ndio maana waliweza kula supu ya ndama na mikate 🥘🍖🍗🥩🍞🍞, na kwa miili ile walitembea kwa miguu umbali mrefu, wkachafuka kabisa, ingawa ni malaika walisafiri mpaka Soari hata kufikilia Sodoma kwa Lutu.

NB:-
*Miili ya damu na nyama inapatikana kwa njia za uzazi (procreation), Mungu aliestablish kanuni hiyo ya kuifanya miili itokee (mambo ya reproduction/kuzaa) hayatengezi roho za wanadamu bali miili (chombo cha kubebea roho). Mwili ni bidhaa adimu mno, kwa viumbe halali wa kiroho kama nilivyoeleza katika somo jingine, kuwa waliumbwa na uwezo ndani yao (built-in ability) wa kujivika miili, inapobidi (Sio kwamba kila aonekanapo malaika wa mbinguni amejivika mwili, bali mwanadamu anaweza funguka macho ya rohoni yanayofanya viumbe vya kiroho viwe physically visible).*

🔴 Kusudi la Mungu kumwumba mtu na mwana wa mtu (mwanadamu) duniani linawezekana tu, wakati huyu mtu akiwa na *mwili/basar* 
✍🏾 Kuuwakilisha ufalme wa Mungu hapa duniani (Mwanzo  1:27-28)
✍🏾 Kumwabudu Mungu na kumsifu (Isaya 38:18-19, 30:9, 6:5).... God created spirits then He formed bodies.... Ameweka kanuni hii moja ya msingi, kwamba hayo yote mtu atayafanya akiwa na mwili tu.

✍🏾 Mwanadamu akiupoteza mwili wa nyama na damu (iwe kwa kifo au njia nyingine) anapoteza uhalali wa kuendelea kubaki duniani. Roho za wanadamu zilizopoteza miili yao haziachiwi kuzagaa mahali popote (Ayubu 7:9ff), kuna mahali zitapaswa kuwepo (Rejea somo langu la *"Umilele"*).. Nimewahi sikia cases kadha wa kadha za watu ambao waliondoka duniani kwa bahati mbaya kwa kuipoteza miili yao. Nahifadhi jina la mwanamuziki wa kiKongo wa zamani, ambaye kwa simulizi niliyoipata alikuwa mtu wa kufanya *Astral travel (levitation)* yaani unauacha mwili unajichomoa roho yako na kusafiri kwa makusudi fulani ya ufalme unaoutumikia rohoni. Sasa katika hizo ziara za kiroho, kuna wakati alisafiri na akakawia sana kurudi, mwili ukaoza. Hivyo hakuweza kuuingia tena mwili wake na hivyo anaitwa huku nje amekufa, hana uhalali wa kuopareti duniani kwa ile roho yake, hana uwezo tena wa kuona familia yake na kuendeleza muziki wake, hayo angeyafanya kama lile limzoga lake (outer  carcass) lisingeoza (Swala la mizimu limezingatiwa katika somo la Umilele utapata ukweli wake). Miili ya damu na nyama halali kutenda kazi duniani permanently inapatikana kwa kuzaliwa na mwanamke, mtu akiupoteza mwili hakuna namna ya kuupata tena (Ni Yesu tu, anao uweza wa kuipa roho ya mwanadamu mwili mwingine, nje ya kanuni ya asili ya kuzaa, na nje ya kanuni ya uumbaji wa mwanzo). Ninao ushuhuda wa mwinjilisti toka Muleba, ambaye akiwa katika ufalme wa giza, mbele za shetani aliomba ruhusa akaoneshwe ziwa la moto. Shetani aliruhusu akaoneshwe kwa masharti kwamba awaachie mwili wake wa damu na nyama, ili kwamba hata kama atapata wazo la kukengeuka toka kwenye ufalme wa shetani basi asiwe na nafasi ya kurudi duniani, maana shetani anajua siri hii ya mwili kwa kina sana, kwamba ukipoteza mwili wako, kwisha habari yako. Na huyu mwinjilisti ameeleza katika huo ushuhuda kwamba alipoona ziwa la moto alimwona Yesu pia, na kulikuwa na tishio kuwa kule alikouacha mwili wake wanakusudia kuuchoma moto. Na Yesu alimwambia kuwa  mwili wako wanataka kuuchoma moto, lakini ninaweza kukupa mwili mwingine... (Sio kusudio langu kuleta shuhuda za kuzimu, nilikuwa najaribu kukazia maarifa).

✍🏾 Roho za watakatifu na mashujaa katika Mungu, hazina effect/athari yoyote katika ufalme wa giza. Kitendo cha hawa watu wa Mungu kuondoka duniani kwa kupoteza miili yao (kwa kifo), hawana athari tena... hata kama alikuwa nabii mkubwa sana mwenye upako kama wa Elisha Ben'Shaphat wa kufufua mtu kwa mifupa yake baada ya yeye kufa. Shetani haogopi watu-roho, anaogopa sana watu-miili wakiwa wanamjua Mungu na kukaa katika uwepo wa Mungu wakiwa na miili hii.... Ndio watu pekee wanaweza kumvurugia chochote katika ufalme wake..

🔴 Roho Mtakatifu hapa duniani anaihitaji miili yetu, hii ya damu na nyama.
Yoel 2:28, Mdo 2:17, 1Cor 3:16, 6:19
✍🏾 Mungu anaahidi kumwaga Roho wake juu ya wote mwili... kama kuna roho ina-Hang na haina mwili wa nyama ahadi hii sio yake... Bali ni juu ya wote wenye mwili, Mungu ni Mungu wa wote mwili..... 

✍🏾 Roho Mtakatifu akija kwa mtu anamzaa upya roho yake, lakini mwili wa huyu mwenye Roho wa Mungu, huuishwa (the body is quickened) Warumi 8:11... Na Roho wa Kristo huufanya mwili kuwa makao safi ya kumfaa, kumbuka Roho Mtakatifu yeye ni roho hakai kwenye roho zetu bali kwenye miili yetu...Miili yetu ni hekalu lake, hukaa humo.. Usisahau hili Roho Mtakatifu anauhitaji mwili wako, usiuharibu, ukiuharibu anachukizwa, naye anakuharibu wewe mharibifu (Naelewa sasa ule wimbo uitwao *Fill this temple* una verse isemayo _"let me be a holy habitation where your Spirit is pleased to dwell"_. 

🔴 Mashetani yanahitaji mwili, yakitaka kufanya mambo yao katika dunia.
Mashetani (Demons) wao ni roho, lakini waliwekewa amri ya kubaki duniani na hawana  miili... Malaika wa Mungu na malaika za Shetani (waasi/walioanguka) wanayo miili yao ya roho, na wanaouwezo wa kujivika miili tofauti-tofauti (2Kor 11:14-15)... Lakini mashetani ninayoyataja hapa (demons) ni roho ambazo hazina miili, miili yao ya nyama waliipoteza (Mwanzo 6), na kwa sababu hiyo kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Henoko 15:8-9 kwa roho za majitu (giants) yaani spirits of nephilims wataitwa pepo wabaya (roho chafu) na mahali pao patakuwa duniani, watasumbua wanadamu maana miili yao wameipoteza na wao asili yao ni mbinguni na hawana uhalali wa kuwa huko. Luka 11:24ff, Mathayo 12:43ff... Yesu anasema pepo mchsfu amtokapo mtu.......  then akikosa mahali (mwili mwingine wa mwanadamu au mnyama) anapata wazo la kuirudia nyumba yake... 

NB:- Hakuna wakati pepo wabaya wataacha kung'ang'ana na miili ya wanadamu, maana wameamriwa sehemu yao iwe hapa duniani, na miili yao waliipoteza. They wish ku-opareti katika dunia, lakini kanuni moja wapo ya kufanya mambo hapa duniani ni kuwa na mwili wa damu na nyama... Hivyo pepo wabaya shauku yao inatekelezeka tu wakiwa ndani ya mwili, bila mwili wa kiumbe hawana kazi yoyote.. Ndio maana katika case ya Mgerasi, pepo walimsihi Yesu aliwaamuru kwenda kwenye *Abussos* ambako hata wao hawakutaki kwa hilo shimo walidai ni bora awape ruhusa wawaingie nguruwe, katika kutafuta uhalali wa kuendelea kuopareti maeneo yale... (Wanaosema wanafuga majini, kuna jambo kubwa hawalijui).....

🔴 Mungu anailinda miili kuliko  hata roho zetu... maana hatari zinaweza kumkuta mwanadamu zinaweza kuuathiri mwili wake na sio roho yake... Mtu anaweza kanyagwa na gari akasagwa kabisa, akaungua moto akabaki kama mkaa au jivu kabisa, lakini hayo mateso na maumivu ya kifo yatautesa mwili roho yake itaondoka kwa salama. Lazaro maskini na mgonjwa mwenye *vidonda vingi* (Luka 16:19-31) alipokufa roho yake ilitokea katika ulimwengu mwingine bila maumivu ya vidonda... Ila mwili wake ule wa duniani wenye ulikuwa na kazi kubwa ya kumwandalia maisha yasiyokoma ya baada ya kuuacha ule wa mavumbi. Najua kuhusu andiko la Ayubu 10:12, maangalizi ya Mungu yanalinda roho zetu, lakini nikujuze kwamba miili yetu inalindwa zaidi (Zaburi 71:3, Ayu 33:24ff, Mathayo 10:29)..
Nimekumbuka na Biolojia ya kidunia, from the Conception (mimba kutunga) Mungu anailinda mpaka mtu muda anazaliwa... Tena kijusi (embryo) kikiwa huko ndani Mungu anakizungushia kimiminika *Amniotic fluid* chenye kazi ya kufyonza maumivu iwapo mama atajibamiza tumbo *Shock Absorbant*, kwenye hesabu za Mungu analenga kuusaidia huu mwili ukue utoke salama, ukatimize kusudi la kuweko kwake (Case ya watoto wanaofia tumboni, imejibiwa katika somo jingine Efeso 1:10)... 

🔴 Sisi wanadamu ni roho, tunaihitaji miili sana. Na hivyo, tunapaswa kuitunza, kuihifadhi, kwa yale yanayotuhusu kuyafanya ili miili iwe vizuri, tuyafanye kwa bidii.

👉🏽 Usipuuzie mambo yahusuyo afya, lishe, usafi. Maeneo mengi ya Afrika kwa sababu ya umaskini kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa maswala ya muhimu kwa kuutunza mwili. Watu kula vyakula vya ovyo, visivyofaa kwa afya mwadamu, uchafu kwenye vyakula, maji yasiyo salama, na vitu vingi vyenye kuuathiri mwili.Wengi wamepata shida na kuondoka duniani, huku watu wakiendelea kunukuu Ayubu 1:21b kwamba Bwana ametao na Bwana ametwaa (Msomaji wangu, Yesu akufungue akili sasa....Usile vyakula vinavyoharibu mwili na inajulikana hivyo,usile vyakula vichafu, au kukaa kwenye mazingira machafu na lolote linaloweza kuleta athari kwenye mwili, maana umepewa huo mmoja tu. Kama kazi unayofanya inahatarisha sana usalama wa mwili, mwombe Mungu na ukipata kibali badili kazi hiyo, kama ni michezo au mazoezi yanaleta tishio la mwili kuharibika, acha tu... Kwa maana when the body is struck by terminal injuries, the door to death is opened)... Na kama nilivyoeleza katika somo la umilele, roho ya mtu ikiona haiwezi kuendelea kuutumia mwili kwa kuwa umeharibika sana, inatoka (ndicho kifo hicho). 

👉🏽 Usikubali kuishi na magonjwa au maradhi. Magonjwa ni moja ya vyanzo karibu tisa vya kifo, nilivyoviainisha katika somo la umilele. Narudia tena, usikubali kuishi na magonjwa. Magonjwa yanaweza kumpata mtu yeyote akiwa katika mwili (Katika mwili huu twaugua)....  Lakini mtu anaweza kuiinua imani yake kwa kiasi cha kuyazuia magonjwa kabisa. Kama hiyo ni ngumu kwa baadhi ya watu, basi kila mKristo mwenye kuijua kweli ajifunze kutoishi na magonjwa... Sijasema mtu hataumwa chochote, ila usikubali kuishi na magonjwa permanently, kama imetokea umeugua, ukiwa na imani ya kupona kwa muujiza omba upone, na ujiridhishe umepona hata kwa kwenda kuupima ugonjwa. Kama unaona huo ugonjwa unaweza ukatumia dawa ya hospital mara moja na ukaondoka fanya hivyo... Ukiishi na magonjwa yanaweza kuleta shida kwenye mwili yakakuondoa muda wowote... Ni juzi nimesafiri kwa basi na njiani waliweka historia ya mwanaMuziki aitwaye Bob Marley, namna ambapo kijidonda kidogo sana cha kuchoma na kisindano akakaa nacho miaka minne kikawa kansa mbaya na kumwondoa duniani akiwa na miaka 26

👉🏽 Na kuna magonjwa ya hatari ambayo huwa yanakaa kwa mtu mpaka yamemwondoa duniani... Magonjwa mengi yanayodjambulia mifumo ya mwili (body systems) kama mfumo wa hewa, mfumo wa damu, mfumo wa chakula, mfumo wa uzazi, mfumo wa utoaji taka mwili, mfumo ya fahamu na mifumo mingine iliyopo... Magonjwa yanayovuruga mfumo mmoja yana desturi ya kuharibu na mifumo mingine.. Mtu akiwa na magonjwa haya, akaanza matibabu,na akajiridhisha na kuridhika kuwa yeye ni mgonjwa wa hayo magonjwa, akakubali kuendelea kuishi nayo, anakuwa amehalalisha safari ya kifo kwa amri ya ugonjwa. Mtu anajua ana presha (LBP/HBP) na anajua kuna muda presha inashuka mpaka anahisi anakufa. au inapanda mpaka anahisi amekwisha toweka duniani, then kama ataendelea kukubali kukaa nayo hiyo presha isiyo sawa, awe na uhakika kifo ameamua kuishi nacho...Unapopewa majibu ya hospitali kwamba ini lako lina shida, figo zako haziko sawa, mapafu yako yana shida, bandama yako ina shida, una shida kwenye utumbo mpana, una tundu kwenye moyo, una uvimbe unaoashiria kansa n.k n.k n.k taarifa hizi hazipaswi kupokelewa rohoni mwako, kama wewe msomaji ni mtu wa ile kweli... Shida ambazo hazitibiki kwa mara moja, zinataka kuwa lifelong uendelee na matibabu ya kuvutavuta siku zikiwa na mateso, USIZIKUBALI, NA USIYAKUBALI MAISHA HAYO, KAMWE USIKUBALI KUISHI MAISHA YA MFUMO WA KITABIBU, kwamba kuanzia sasa kwa kuwa una kisukari, hakuna kunywa hiki na kile, hakuna kula hiki na kile etc, ukijiingiza kwenye mfumo huu, utasaidia kuvutavuta muda wa kuishi kwa mateso lakini safari ikiwa sio yakini (uncertain) kwamba muda wowote ugonjwa ukichachamaa unaiacha dunia. 

*POINT YANGU NI HII*
Kwa wewe mwamini. mwenye kuijua kweli, option ya kwanza ni hii... Pambana katika roho kuhakikisha magonjwa ya kutisha uyajuayo ya kiMisri (Kumb 7:15) uyazuia yasiupate mwili wako, hili linawezekana kabisa kwa kuomba kwa bidii na kwa kuishika ahadi ya Bwana juu ya afya ya mwili wako... Hili litawezekana kabisa kama continually utaendelea kuishikilia afya ya mwili wako kwa maombi na kwa kushindana rohoni daima, na bila kusahau kama kuna mambo ambayo kwa dhahiri yandhuru mwili basi uyaache au kuyaondoa. 

*NB:-* Kumbuka hili ni rahisi zaidi kuzuia maradhi rohoni kwa imani, ili yasije... kuliko kuyaondoa yakiishafika.. Hivyo best option ni ya kuzuia kabisa, sisemi kwamba Mungu haponyi, Yeye ni YHWH Raphah anaponya ugonjwa wowote hata kama upo kwenye last stage ya ubaya (Kutoka 15:26)... Lakini hapa unaipata kweli ya Mungu kuhusu mwili ujue namna mwili unaoparet bila kusingizia vifo vyote ni mapenzi ya Mungu... Maana maradhi yakifikia kiwago fulani cha kuudhuru mwili, roho inaondoka... Elisha nabii  mwenye double portion anointing alikufa kwa homa tu.... 

👉🏽 Kama kwa namna yoyote tu ile, wewe mwamini umejikuta tayari ugonjwa upo ni ugonjwa wenye hatari ya kifo... Basi unaweza kung'ang'ana na uponyaji wa Mungu mpaka ujiridhishe kabisa kuwa ugonjwa umeondoka, kuendelea kuuguza miaka minne haina maana kuna usalama wowote, ila kwa kudumu nao utapata shida zingine... acha mambo mengine, simama kwa zamu yako ushughulikie mpaka ujiridhishe ugonjwa umeondoka...NA INAWEZEKANA KABISA

🕯 🔦 USHUHUDA NO1
Mwaka 2006, nilipata shida ya moyo kwa ghafla tu... Nilikuwa nakimbia kwenye mvua kali, nikasikia kama shoti ya umeme (electric shock) eneo la moyo na maeneo mengine.... Basi tangu hapo nikawa nahisi maumivu ya moyo, presha inashuka mpaka nasikia ni kama moyo unataka kunyamaza kabisa, nikiamka asubuhi nahisi ganzi ya moyo mpaka kwenye vidole vya mguuni... ilidumu miezi kadhaa huku nafikiria kweli nami nitapelekwa India kwa shida ya moyo... na ndoto zote zikawa zinakuja za kuonesha nitapaswa nikatibiwe huko nje... Nililisikia neno moja tu toka kwa Mtumishi wa Mungu Askofu Zachary Kakobe (ibada ya kwanza ya mwaka 2007) basi, nilitoka nyumbani jioni nikaenda kanisani (EAGT), nikiwa pekeangu nilisema maumivu kwenye moyo mwisho wako ni sasa, niliamuru shida ya moyo itoke, na yale maumivu eneo la moyo, yalihama toka moyoni yakasogea karibu na bega, kisha yakasogea kama yanakuja kinywani,na kupotea kabisa..IKAWA MWISHO KABISA WA TISHIO LA TATIZO LA MOYO.

🕯 🔦 USHUHUDA NO2
Mwaka 2017 October nilipatwa na Ulcers kwa sababu ya misbehaving ya ratiba za kula... Maisha ya kukaa bila kula (na nikiwa sijafunga)... Kuna tofauti sana kati ya kufunga na kukaa na njaa....  Na hapa wapenzi wa kuomba na kufunga, wafunga sena ila kwa akili... Ninazo picha za Mzee wa kanisa mmoja mkoani Iringa, ambaye miaka miwili ikiyopita alienda kufunga porini mfungo wa mwezi mzima, lakini walipomtafuta baada ya wiki kadhaa tangu aanze waliukuta mwili umekauka kabisa, kuna kitu hakikuwa sawa na mashauri ya kiroho yalikosekana, anaweza kwenda mbinguni, ila hasara aliyoisababisha kiroho ni kubwa kwa kuuharibu mwili wake. Mimi nilikuwa nakaa na njaa muda mrefu kwa sababu ya mazingira niliyokuwa nayo kazini, kurudi ghetto kupika chakula mchana na usiku ilikuwa ngumu sana. Sasa shida ilipozidi nilienda hospitali.. Nikakutwa na ulcers... Nilianza matibabu lakini pamoja na dawa zote nilishaambiwa hizi hazitibu kabisa-kabisa... Hivyo nikaamua kutumia njia ya pili ya imani, kuhakikisha ulcers zinakaushwa kabisa...  Naukumbuka usiku wa manane ambao nilishughulikia ulcers... Sikumwambia tu Mungu aniponye ulcers, ila nilijiondoa kabisa rohoni katika watu ambao wamewahi umwa ulcers... Na ili nijiridhishe nilipoamka nikaanza maombi ya kufunga mwezi mzima nione kama kuna shida yoyote, nikamaliza mfungo nikiwa sijawahi hata kuhisi maumivu, ndivyo nipo mzima mpaka sasa hata maombi ya kukaa masaa 72 bila kugusa chochote nafunga bila tatizo lolote.

☝🏽☝🏽☝🏽☝🏽☝🏽☝🏽☝🏽☝🏽

```Nimekupa shuhuda hizo mbili, ili ujue kwamba unao uwezo wa kuuondoa kabisa huo ugonjwa ambao vipimo vimethibitisha unao...  Ukiamua kuishi nao, ugonjwa utajiotesha mizizi na kuwa permanent..
Mimi nilikataa kuwa na ulcers maana niliona haviendani na mtu wa rohoni ambaye anataka kila wiki afunge, amtafute Bwana etc... Nawe hata kama shida ipo tayari komaa na uwezo wa kiUngu ulio ndani yako mpaka ugonjwa utoke.```

*NB:-*

_*KUNA SHIDA NYINGINE IMEKUPATA NA UNAONA KABISA JWA NGUVU ITENDAYO KAZI NDANI YAKO, HUWEZI KUIINUA IMANI YAKO KWA KIASI CHA KUUNG'OA HUO UGONJWA, TAFUTA NGUVU YA ZIADA, HATA KWA MTUMISHI WA MUNGU MWENYE NGUVU KUBWA ZAIDI, MAANA  HATUWI NA NGUVU SAWA  ROHONI INGAWA WOTE TUMEOKOLEWA NA KUJAZWA ROHO MMOJA... JITAHIDI UPATE SOMO LANGU LIITWALO "KUYAPELEKA MAGUMU KWA MTUMISHI MWENYE NGUVU KUBWA ZAIDI"*_

~*Mungu awabariki sana... Mwili wako huo, unahitajika, ni wa muhimu, swala la upo mrefu, mfupi, mnene, mwembamba, mweusi tiii, mweupe pee na chochote kila katika mwili wako hakina umuhimu kama umuhimu wa uwepo wa huo mwili wenyewe....Roho yako imebebeshwa mambo mazito  ambayo kabla ya kifo utapaswa kuyafanya, lakini hayo yote yatawezekana tu kama ukiwa na huo mwili... UPENDE MWILI WAKO KWA JINA LA YESU*~

_Mwl Proo_
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment