*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ 2Timothy 2:15b
*SEHEMU YA TATU*
*_KIPI KINAPASWA KUWA FUNDISHO KWA WAAMINI?_*
Sikushauri uanze kusoma sehemu ya tatu (3) kama hujasoma kwa kuelewa, sehemu ya kwanza na ya pili, huu hapa ni mwendelezo tu. Sehemu ya pili ya somo nieleza namna mbili za kutafsiri maandiko yaani (Eisegesis na Exegesis). Leo nakuonesha kipi kinapaswa kuwa fundisho kwa waamini (Wakristo). Ukristo (imani ya kumfuata Yesu) sio imani ya mchongo, wala sio imani ya dini ya Kiyahudi (Judaism). Ukristo sio imani iliyokosa vyanzo vya kufundishia (sources & materials), au kwamba kuna mambo hayana mwongozo, na mtu yeyote anaweza akatengeneza kitu chake tu chochote (coined teachings); Hasha!
Natambua kuhusu magawanyo ya Roho (Ebrania 2:4), natambua kuhusu tofauti ya kutenda kazi (1Kor 12:6), natambua kuhusu neema mbalimbali za Mungu (1Petro 4:10). Lakini pamoja na hayo yote kusanyiko la waamini, hawafundishwi tu chochote atakachokinyofoa mtu kwenye Biblia. Mfano kama Torati ni kivuli, wala si sura halisi.... Kila utakapotaka kusoma kivuli utapaswa kukisoma kutokea kwa sura halisi (Kristo). La sivyo utaangukia katika upotovu mkubwa. Kwa kusema hivi simaanishi kamwe Torati au kitabu chochote cha Agano la Kale kisisomwe au hakiwahusu waamini katika Kristo (Warumi 15:4), hapa ni suala la matumizi yake ni yapi?? Ndio maana somo letu linaitwa *KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
Kwa sababu ya kukosa msingi, nini haswa kinapaswa kuwa fundisho kwenye kanisa, Watu wameingiza chachu za kifarisayo nyingi sana, huku ikidhaniwa ni mafunuo.
*MIFANO HAI YA MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA MAANDIKO*
1. Huwezi kuja kwenye kusanyiko la Wakristo, ukawasomea Kumbukumbu La Torati 22:8, na kuwaelezea wapendwa Mungu anatuagiza kujenga ukuta mdogo wa fensi (parapets/battlements). Hili sio agizo la Mungu kwa waamini katika Kristo.. Taratibu za ujenzi kwa waamini zitazingatia tu uwezo wao kifedha, vibali vya ujenzi toka manispaa, utamaduni wa majengo ya mahali walipo... Wala usiwaongoze kwa desturi hizo za kiyahudi.
2. Huwezi kwenda kwenye kusanyiko la waamini huko Uarabuni, ukawasomea andiko la Walawi 11:4 (Na kuwaambia jamani ndugu zangu Wakristo msile kabisa ngamia 🐪 🐪 Mungu kakataza. Waamini hawajakatazwa kula ngamia.. Ni wewe hujatumia kwa halali neno la kweli. Suala la vyakula halali vya kuwafaa kwa afya vitategemea desturi za huko walipo, kanuni za afya kisayansi kama wanyama hao hawana madhara na sio kutafuta mwongozo wa Torati ya Musa kuwajuza wanyama wa kuliwa... (Torati ya Musa na Isaya imetaja kuwa panya 🐀🐁hawapaswi kuliwa, niwaambie tu kama kuna Wamakonde na Wayao wanaokula panya na ni Wakristo, hayo makatazo hayana uhusiano na imani yao.
3. Huwezi kwenda kwenye kusanyiko la waamini (waKristo), ukawasomea Walawi 19:27, na kuwaambia ni chukizo kunyoa denge (cutting hair by sides). Umetumia neno isivyo halali, ulipaswa ujifunze kwanza maana ya maagizo hayo kabla ya kuwaambia Wakristo, labda msichonge ndevu zenu mkienda Saluni (Barber Shop). Kama Mkristo atakatazwa kunyoa au kuchonga ndevu, au nywele zake iwe ni katazo kwa sababu jamii yenu kitamaduni, hawalikubali hilo.... wala sio utii kwa makatazo ya Torati (maana kila katazo linalo muktadha wake).
4. Huwezi kwenda kwenye kusanyiko la waamini ukawaambia jamani Kumbukumbu la Torati 22:11, Biblia imekataza kuvaa nguo yenye aina tofauti ya vitambaa (two different linens) yaani nguo isiwe na satini, na pamba, au hariri, au sufu au kitani, au kitenge etc). Kwamba ukifanya hivyo ni machukizo.. Hicho ulichosoma ni kizuri ila sio maagizo ya Mungu kwa waamini. Kama kuna kitambaa utaacha kukivaa ewe Mkristo ni labda kama kwenye jamii yenu kinakataliwa kijamii, isiwe na correspondence yoyote kwa makatazo ya Torati.
Kuna watu wanasema Mwl Proo, unazuia watu kutumia vitabu vya Agano la Kale... La Hasha!. Ninchofanya ni kuwaondolea utaji (veil) na kuwafanya waamini wapate kumwona Kristo hata kwenye Torati.
Ni aljebra rahisi sana hii hapa: Torati, Zaburi, na Manabii vilizungumza habari za Kristo kwa picha (Typologies).... Ujumbe wa kuhubiriwa ni Kristo. Hivyo tu (Kolosai 1:28, 1Korintho 1:23). Yaani, ili watu wawe waamini (watoto wa Mungu) hawahitajiki kunakili (kuCopy) chochote kwenye desturi ya dini ya kiYahudi. Wanapaswa kuhubiriwa kuhusu Kristo (kazi aliyoifanya na kuikamilisha) wakiziamini hizi habari njema (Injili), wanapokea wokovu (kufanywa watoto wa Mungu). Na baada ya hapo watendelea kufundishwa kuhusu Yesu (Kuzaliwa kwake, kufa, kuzikwa, na kufufuka kwake), kumewafanyia nini wao (kumfunua Yesu), huku pia wakifundishwa wao wamekuwaje kwa kupitia Kristo (kilichotendwa ndani yao, na nafasi zao wakiwa ndani ya Yesu)... Haya yanatosha kumfanya mwamini kuwa mtu mkamilifu, mwenye kuweza kutembea kwenye madaraka makamilifu, kama mtoto wa Mungu. Waamini wataendelea kujifunza kuhusu mwenendo ndani ya imani kwa Yesu (asili yao mpya baada ya kuzaliwa upya), na watakaa kwenye fundisho la Yesu na mitume wake. HABARI HIZI NI NYINGI ZINATOSHA KUZIHUBIRI NA KUZIFUNDISHA HATA KAMA ULE MWISHO UTAKAWIA KWA MIAKA MILIONI 10 BAADA YA SASA _(mwlproo)._ MKIPIGA CHENGA FUNDISHO LA KRISTO NA MITUME WAKE MNAJIINGIZA KWENYE MAFUNDISHO YA MCHONGO. MTAPEANA UTUMWA, HOFU, NA MAFUNDISHO MENGINE YA KUFANYA MSALABA UBATILIKE.
SIKU YA JANA KUNA MKRISTO AMENISHIRIKISHA KUWA JUMAPILI ILIYOPITA WAMESOMEWA EZEKIEL 16:1-5, NA KUFUNDISHWA NGUVU ILIYOSHIKILIA HATIMA, ILI WAWEZE KUOMBEA VITOVU VYAO VILIVYOKATWA MIAKA MINGI. 😀 NI KAMA MAFUNUO MAZURI VILE, SI NDIO!!! HAYA SIO MAFUNDISHO YA KUWAFUNDISHA WAAMINI. WAAMINI WANGEAMBIWA ALICHOFANYA YESU, NA WAO WAMEKUWAJE KWA KUZALIWA, KUFA, KUZIKWA, NA KUFUFUKA KWA YESU. HAKUNA LEVEL YOYOTE KATIKA UFALME NA MAMLAKA ZA GIZA INAYOWEZA KUWASHIKA WAO WALA HATMA ZAO. MKIKATAA HAYA MNAWEZA KUCHAGUA KUENDELEA KUJIFUNZA UTUMWA AMBAO HAUPO, ILA UNAUMBWA KWA KUWA MMECHAGUA KUUSIKILIZA NA KUUAMINI. YOYOTE MTAKAYOYABUNI KWA KUNYOFOA VIMISTARI KWENYE BIBLIA NJE NA UJUMBE WA MSINGI (FUNDISHO LA KRISTO NA MITUME) MTAKUWA MMECHAGUA KUJIFANYISHA KAZI AMBAYO BWANA MKUBWA YESU KRISTO ALIIKAMILISHA. LEO HII UKIAMUA KUFINDISHA WATU LAANA ZA ARDHI ZINAVYOLETA UMASKINI, SIJUI SADAKA YA KUTANGUA MADHABAHU ZA MAGONJWA, MARA NAMNA DAMU ZA KAFARA ZINAVYOLETA MATESO KWA MKRISTO, NA TAKATAKA ZINAZOFANANA NA HIZI, NI UCHAGUZI WENU TU KUURUDISHA UTUMWA AMBAO HAUPO. NA ANAYEJARIBU KUSEMA YEYE NDIYE ANAWEZA KUWASAIDIA WAAMINI KUTOKA KWA HAYA ANAJARIBU KUJIPA KAZI YA KUWA MWOKOZI MSAIDIZI. WAAMINI WANACHO CHA KUFUNDISHWA SIO HAYO!
*CHRIST IS OUR MESSAGE (COLOSSIANS 1:28 TPT)*
NIKUOMBE SANA,USIKOSE SEHEMU YA NNE (4), UTAPATA MAMBO YA KUKUSAIDIA SANA KUIELEWA IMANI HII NA KUIFURAHIA
alltruth5ministries@gmail.com.
No comments:
Post a Comment