*KULITUMIA KWA HALALI, NENO LA KWELI*
*_Rightly Dividing The Word Of Truth_* (2Timothy 2:15b)
*SEHEMU YA KWANZA*
_Mwl Proo_
0762879363
Ili kuepusha ufafanuzi wa mchongo wa torati ya Musa... Wayahudi wana Talmud (yenye Mishnah na Gemara) ambayo ni fasihi andishi iliyotokana na simulizi za mdomo za desturi za utekelezwaji wa Torah.
Leo katika mafundisho ya kanisa, kuna ufafanuzi mwingi wa mchongo (falsely manipulated teachings) uliosababishwa na kuepuka kanuni za kutafsiri maandiko.
Maandiko katika Biblia (ni mkusanyiko wa taarifa nyingi zikiwemo nabii mbalimbali, hadithi, maagizo ya Mungu, simulizi za desturi za kiyahudi, na taarifa zingine nyingi zilizokusanywa pamoja, zikawa 'documented'.
Humo ndani kuna mambo ambayo yanaweza kutafsiriwa kwa namna tatu kimsingi;
1. Literally (kwa kawaida tu kama yanavyosomeka
mfano (a):- Ukisoma labda mtume Paulo anaandika Salamu.. kwamba watu wa nyumbani mwa Akila na Priska wanawasalimu, au Wasalimieni watu wa nyumbani mwa Arkipo (Hii ni salutation/maamkizi tu ya kawaida).. Utaitafsiri literally bila ku-Manipulate kuepusha upotoshwaji usio na sababu.
mfano (b):- Umesoma zako Isaya 6:1, Mwaka ule aliokufa Uzia nalimwona Bwana. Katika zama za uandishi wa Biblia hususani Biblia ya Kiyahudi (Tanakh) ilikuwa ni kawaida kuandika rejea ya muda kwa kutaja tukio gani lingine kubwa (notable) lilitokea. Mfano Amosi 1:1 anasema miaka miwili kabla ya tetemeko la nchi/ardhi (Earthquake) ikiwa ni namna nyepesi ya kukumbushia majira gani hilo lilitokea. Ni namna hiyo hiyo Isaya anataja mwaka aliokufa Uzia kama muda rejea wa maono yake. MANIPULATIONS (ufafanuzi wa mchongo) utadai, Uzia alimzuia Isaya kumwona Mungu. Kwenye maisha yako kuna Uzia ambaye inabidi afe.. Asipokufa Uzia huwezi kumwona Mungu.. Uzia anaweza kuwa ndoa au kazi yako au simu yako... It sounds vizuri midomoni mwa wahubiri.. na mwingine atadai ni ufunuo.. Hapana, ufunuo uliopo humo kwa Biblia ni mwingi mno tu bila hata ku-Manipulate kwa sababu ya kukiuka kanuni za kutafsiri....
NB:- *MAANDIKO YA KWENYE BIBLIA HAYAWEZI LEO KUMAANISHA KITU AMBACHO MWANDISHI HAKUKIKUSUDIA WALA KUKIMAANISHA*
Hiyo ya kudhani watu wanafunuliwa cha kuelezea ndicho kimetufikisha kwenye vituko vingi kwenye kanisa la leo.. na wengine wakiona wanalalamika tu kumbe ilisababishwa kwanza na ufafanuzi wa mchongo wa maandiko ya Biblia, na kutojua nini hasa kinapaswa kuwa fundisho katika kanisa.
2. Allegorically (Hii ni namna ya ujumbe kuwasilishwa lugha ya picha, fumbo, mfano uliofichwa kwenye kitu kinachojulikana, na lugha za alama 👉 figures of speech (figurative language), symbolisms...
Ni muhimu kama unataka kuepuka makosa, kabla ya kutumia kitu kilicho katika maandiko kama kilivyoandikwa (literally), ujiulize je! sio lugha ya picha (allegory...) NB:- parables (mifano) ni allegories fupi.. ingawa zina tofauti, ila hayo yako kwa somo jingine.
Mfano:- Unasoma zako kitabu cha Ufunuo... Unakutana na maandiko yakimtaja Yesu kama Mwana-Kondoo (Lamb), mara Yesu ni Mwana-Kondoo aliyechinjwa.... Je! ni kweli kwamba Yesu alichinjwa au alifia kwenye kinyongeo cha askari wa Rumi? Hizi ni lugha za picha kutokana na kujulikana kwake kwa hadhira (familiarity). Hata kusema huyo mwanakondoo alichinjwa kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu akiwa anataka aoneshe maongeo ya mpango wa Mungu wa ukombozi tangu zamani, tangu milele. Hatari ya ufafanuzi wa mchogo ni kuleta mafundisho yenye makosa, yenye kuwakosesha sana waamini. Kila ambapo maandiko yenye lugha picha (figures of speech/allegories) yakifafanuliwa kawaida (literally) yanakosesha shabaha lengwa...nk
3. Contextually (kimuktadha)... Ingawa jambo hili nitalizungumzia sehemu ya pili ya fundisho hili, ila kwa uchache.. Kuna maandiko mengi yanapaswa kufafanushwa baada ya kufahamu muktadha husika (history of the text & history in the text). Kubeba kitu kinyume na muktadha kinaweza pelekea kuzalisha fundisho lenye makosa.
Mfano:- Mtu akisoma 1Korintho 11:13-14, kisha akawasomea wanawake wabongo kuwa mkija kanisani, mnapaswa kufunika vichwa.. Ameamua kupuuzia maandiko yenye muktadha husika na kuyaapply kama yalivyoandikwa kwa kawaida _literally_. Ulipaswa kufahamu mambo kadhaa ikiwemo ukweli kuwa kitabu/barua ya Paulo kwa waamini wa Peloponnese (Corinth) ilikuwa ni majibu ya maswali waliyomwuliza yeye kabla, kwa issues zilizoinua disputes za hapa na pale. Kwa wanawake wa huko Uyunani hususani (elderly women, na wengine baada ya kuolewa) hawaoneshi nywele zao kwa hadhara... Kwa kufanya hivyo wanakuwa wametii desturi *_Traditional Notions of Propriety_*.. Maana mwanamke akiacha nywele ni labda kahaba au ana cheo kisiasa... Huo ndio muktadha kwa ufupi. Hivyo ni makosa, kuchukua andiko hilo la wanawake kufunika vichwa wakati wa sala, kuwasomea wandengereko, wamakua, wabena, na wamasai ukiwataka nao wafunike nywele zao wakija kanisani... Haliwahusu, halina maana hiyo, halipaswi kutumika kwa muktadha tofauti na ule wa kwenye mji wa Uyunani alikoipeleka ile barua, hata mtume Paulo hakutoa maagizo au maelekezo hayo kwa makanisa mengine kwa sababu kwao hawana tafsiri sawa na mji wa Korintho nchini Greece 🇬🇷 . Maandiko yanayohitaji kutafsiriwa kimuktadha ili kutumika.. lazima ufuate kanuni.. or else ufafanuzi wa mchongo utahusika.
USIKOSE SEHEMU YA PILI NA YA TATU YA FUNDISHO HILI, YATAKUSAIDIA SANA TU KUTOENDELEZA MAKOSA, NA UTAJIPATIA NJIA NZURI YA KUTUMIA KWA HALALI, NENO LA KWELI
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment