Friday, January 12, 2018

NISIWE WA KUKATALIWA!

     *NISIWE WA KUKATALIWA*😥

_Mwl Proo_
*0762879363*
~*_Mjumbe wa matengenezo_*~

*SHALOM ALEICHEM*

1 Wakorintho 9 : 27
*_bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa._*

Wakati mwingi umepita tangu Bwana atie moyoni mwangu neno hili, na sasa nimeona vema kuwaandikia. Neno hili lilinijia kama ombi kwa Mungu, nikiwa chumbani kwangu napiga gitaa 🎸, nikapokea simu toka kwa mdau/follower wa masomo yangu. Mtu huyu alipiga simu akiwa bado anabubujika, analia, ananena kwa lugha kwa furaha na kwa mguso usio wa kawaida, anaongea huku anaomba, ananiombea kwa simu huku akimtukuza Mungu, kwa kunitumia kuandaa somo ambalo alipolisoma Bwana alimtembelea na kuyagusa maisha yake. Muda huo hali yangu kiroho haikuwa nzuri kwa namna ile, yaani hata hilo bubujiko alilo nalo nililimiss (In short, I was not that much smarter spiritually). Sasa alipokata simu, nikaanza kuwaza, hivi Yesu unitumie kuponya na kuinua wengi, then mimi nichoke njiani, niharibu mambo na siku ile uniambie ondoka kwangu, sikukujua wewe!!! 😥😥😥 Baadhi ya masomo yangu yamevuka mipaka ya nchi, yanatumiwa kuimarisha wengi, kuna mchungaji toka nchi moja huko Afrika ya kati, aliniambia anayaandika kwa diary na kuwafundisha washirika wa kanisa analochunga, wanayafurahi na kumwona Mungu. Sasa nikafikiria hivi baada ya kutumika kama chombo, nami nikaendelea na maisha, nikachakachua on the way hapo kati, haifanyi nisamehewe kwa kuwa eti niliwahi tenda vizuri, hapana...

Ezekieli 18 : 24
*_Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa._*

*HATARI NI KWAMBA BAADA YA KUFANYA KAZI NZURI ELFU ELFU, BAADA YA KUFUNDISHA MASOMO MAZURI YA KUJENGA KAMA YA MWALIMU DCK, AU BAADA YA KUPONYA VIJANA KWA MAFUNDISHO KAMA YA MCH. MITIMINGI, AU MAFUNDISHO MAZURI YA NDOA KAMA YA DR.CHRIS MAUKI, AU BAADA YA KUFANYA UINJILISTI ULIOTUKUKA KAMA WA MOSES KULOLA, AU UINJILISTI WA KIMATAIFA KAMA TELEVANGELIST REINHARD BONNKE, AU UKAHUDUMU KWA MADHABAHU YA UIMBAJI KAMA DON MOEN, AU MWIMBAJI MASHUHURI AFRIKA, REBECCA MALOPE, KISHA UKACHEPUSHA ILE HAKI YAKO KWA KUTENDA MOJA YA MACHUKIZO, MWISHO UKAKUKUTA KATIKA KUHARIBIKIWA, BIBLIA INASEMA HALITAKUMBUKWA HATA MOJA KATIKA YALE MEMA YOTE YA UTUMISHI WAKO (Jitahidi usome somo langu linasema Maliza Vizuri)*

*🔋KUENDELEA KUTUMIWA KWA KAZI KUBWA KATIKA HUDUMA, SIO KIASHIRIA CHA KUWA UKO OKAY/SMART KIROHO, NA MUNGU*

🥢Kuna anga la kiroho ukishalifikia (spiritual firmament), utaendelea ku-operate pale juu, hata kama umetoka kuzini na hujafanya toba.
🥢 Balaam hakuwa mtumishi wa Mungu, alikuwa mchawi, mnajimu mwenye elimu za kijini. Lakini alikuwa na spiritual experience ya kutosha katika ulimwengu wa roho wa giza, ndio maana anakutana na malaika wa nuru hakustuka, bado akawa anajielezea adhma yake ya kutaka kumpiga yule punda 👉🏽🐴. Huenda katika ule umati wa waisrael ni wachache waliona laivu malaika, lakini huyu Balaam Bin Beor kwake haikuwa ishu, bila shaka katika kazi zake za ulozi, alishapambana nao huko rohoni. Hivyo Mungu alimtumia kutamka mambo mazito tunayoyasoma katika Hesabu 23, lakini hii haimfanyi awe wa Mungu, na bado katika Yoshua tunaona walimwua kama mchawi tu wa kawaida. Mungu alimtumia kwa yale maana kiwango chake kuyajua mambo katika spiritual realm kiliruhusu.

🥢 Mtu anaweza andaa mahubiri kwa kiwango cha juu sana kiufunuo, wote mkamtukuza Mungu kwa vipawa vya ajabu, lakini huyu mhudumu akawa yuko *rotten* kule rohoni, amechacha/amechina. Huyu mtu neno la Mungu lilifunuliwa kwake, na hivyo kwa ule ujuzi wa kweli, akapandishwa daraja rohoni, akawa ana-opareti na roho ya ufunuo kwa kiwango cha juu, hivyo haijalishi jana yake alifanya dili la kudhulumu kiwanja, bado anaweza kufunua Biblia akafundisha kwa ufunuo wa ajabu, maana kiwango cha nuru kwenye macho yake na level ya roho ya ufunuo aliyoifikia inampa kuyaona mambo kwa kiwango hicho.

🥢 Sauli Ben Kish, alikataliwa na Mungu mapema katika 1Samwel 16:1ff, lakini kuanzia hapo mpaka kufika 1Samwel 31, vita iliyogharimu maisha yake ni safari ndefu, aliendelea kutenda mambo makuu, ila hakuwa na Mungu. Ni huyuhuyu aliyekataliwa akiwa hana Mungu, alifanya mambo mazuri kiroho kama kufuta leseni za wachawi na waganga wote juu ya Israel (1Samwel 28:3ff), ni rahisi tukamsifu tukidhani anaongozwa na Bwana, lakini alikuwa amekataliwa, na aliwafukuza kwa kuweweseka tu, ndio maana mstari wa saba yeye mwenyewe anakimbilia Endori wa mpiga ramli. Hivyo unaweza endelea kumbe ni wa kukataliwa.

🥢 Yako mambo ambayo ni vipawa asili, ila yanatumika katika huduma za rohoni. yanaweza bakia kwa mtu hata kama amefanya machukizo makuu, na kwa kuwa wengi tunabarikiwa tu na vipawa hivi bila kutumia macho ya ndani, mhudumu huyu ataendelea zake mpaka mwisho bila kutengeneza. Kipawa kama cha kuimba, ni kapawa cha asili unaweza kukinoa kikafika mahali pazuri pa kupendwa sana, hata kama usiku wa jana umelala na mume wa mtu, tukikupa microphone  👉🏽🎤, tukakuvunjia makodi (chords) 👉🏽🎹🎸🎺🎻🥁🎷, tunaweza pata hisia kali ya uwepo, na Mungu anaweza shuka kabisa akagusa watu, ila wewe mhudumu usipoweka sawa unakuwa wa kukataliwa. Kipawa cha kuhubiri ni kipawa cha asili tu, ukawa unaongea kwa mitetemo na vibrato kali, mpaka tunahisi raha, hiyo itabaki tu, hata ukiharibu rohoni. Kuna mhubiri (mtume) mmoja yuko Dar lakini sio mtanzania wa kuzaliwa, kuna wanamuziki nilikuwa nao, walimtembelea kwenye ofisi yake ya  kanisa, wakamkuta ofisini yuko zake anatazama sinema za ngono (pornography), na wala hata hastuki kwa kuona wageni, huku muda huo kuna watu wapo nje wanasubiri masaa yatimie waanze kuingia, wamekuja kwa ajili ya ushauri na maombezi. Mungu atawafungua hawa watu kwa ajili yake Yeye mwenyewe, ila huyu mtu ambaye inaonekana dhamiri imekauka huko ndani kwake, anaweza kuwa wa kukataliwa.

🥢 Kama katika magawanyo ya Roho, ulipakwa mafuta, kwa karama za imani au za kuponya au matendo ya miujiza, hayataondolewa kwa kuwa umekosea na hujatubu, ingawa wengine Mungu akitaka kuwarejeza anaweza kuzi-freeze hizo karama ili urekebishe, lakini kwa ambao wamefika mbali sana kihuduma, na muda mwingi au wote wapo katika kuhudumia maelfu ya watu, huwa vinabaki tu. Vitaendelea ku-opareti kwa sababu mpaka ukatumiwa kwa kazi hizo, Roho anakuwa alikupa maarifa maalum ili akutumie, sasa unakuwa na ujuzi ambao bado you can minister tu hata kama umefanya uhalifu.

*🔋 HATARI NI HII*
Watumishi wote wa huduma yoyote, hata wale ambao kwa sababu ya kazi wanazotumiwa wananyenyekewa kiasi kwamba akitokea tu watu wote wanalala chini kama sio kupiga goti, bado huyu mtu naye ni mwanadamu, ana *human limits* bado, hajawa Mungu wala malaika. Binti mmoja aliuliza hivi hiini kweli au ananipima, baada ya kuona mtumishi mashuhuri anamtaka kimapenzi, kila wakionana anamhimiza, alifikiri labda anamjaribu aone kama amesimama, huyu ni mwanadamu kabisa akiacha zile qualities za kiroho anaweza anguka kama wengine. Mwezi Desemba nimepata ushuhuda wa mchungaji katika moja ya madhehebu makongwe ya kipentekoste. baada ya scandals za uzinzi kuwa nyingi, makao makuu yamemhamishia katika kanisa jingine pembezoni kidogo mwa jiji la Dar, huko alipohamishiwa yupo karibu na kanisa la dhehebu jingine (EAGT) analochunga mchungaji rafiki yangu, lakini bado anaendelea na biashara yake ya kuwinda mabinti, ingawa ana ndoa halali. Nilikuwa katika grupu jingine la WhatsApp linalosimamiwa na mtume machachari sana Tanzania. Tukiwa humo mtu mmoja akajoin via *invite link*, alipoingia akasema mnakubalije kuongozwa kiroho na mtu mchafu? Akasema kiongozi wenu ni Admin katika magrupu ya video za utupu, akatuma screenshots kadhaa, anatumia namba yake nyingine, lakini ni yeye kabisa, mimi nilijiridhisha maana nilikuwa nazo zote. Kwa zile screenshots chache niliona aliwa huko anatukana matusi yote ya nguoni, alimtusi kijama aliyenadili *icon* ya group kwa matusi mazito, na picha iliyokuwa ikionekana hapo ambayo kaiweka yeye ni ya binti aliyeufunua utupu wake na kuuanika wazi. Muda huo anashutumiwa kwa uchafu huo, katika grupu lake jingine alikuwa anaendesha semina ya neno la Mungu. Sasa haya mambo ndivyo yalivyo, watu wanaweza kuendelea kutumiwa huku wakiwa wachafu, na mwishoni *WAKAKATALIWA*, zisikumbukwe kazi zote njema walizofanya. Nimetoa mifano michache lakini mambo sio shwari kabisa.

*💊TUFANYE NINI BASI!!*💊
Kila mtu kunaweza kukawa na mambo una-struggle nayo kuya-fix, hilo ni la kawaida tu, Bwana anajua, na anaweza kutusaidia, akatusimamisha pasipo mawaa mbele zake siku ile (Yuda, 24-25).

💉 *Usikubali dhamiri ikanyauka, au ikafa kabisa*
Mungu ametusaidia kwa kutuwekea dhamiri ili usiende mbali sana katika kukosea. Ila dhamiri inaweza kufa na hapo njiani inapitia process za kuugua. Kama mtumishi, unaweza fanya mambo kama hayo hapo juu, lakini husikii kuumia wala kuugua ndani yako, wala you don't fight utoke hapo, tayari dhamiri iko na great damage, hiyo ni hatari sana. Huyu mtumishi kwa mfano kama ameweza kuwa admin wa magrupu ya video za ngono, anaweza fanya mengi mno machafu, na dhamiri haiko salama tena. Nilisimuliwa na rafiki yangu kuhusu mama mtumishi ambaye yeye mwenye kwa hiari yake, amemwomba kijana fulani mtaani kwake wawe wanashiriki ngono, mmewe akiwa safari za huduma (tena ni kijana asiyeamini) ila anajua kuwa anatembea na mama mtumishi, na bila shaka huyu mama mtumishi ndiye anashika huduma mume akisafiri, hapa hakuna usalama.

💉 *Ni kweli una udhaifu kama mwanadamu, lakini badala ya kuendekeza udhaifu, uwe na wakati wa kuingia chumba cha ndani na kumwambia Yesu kibinafsi, kwamba Bwana wangu Yesu, nisaidie. Nina lemewa na nichoka, nipe nguvu mpya (Isaya 40:29-31). Maombi utakayoomba binafsi Mungu akuangalie kama mtu aliyekuchagua, yatasaidia kukunasua.

💉 Mwambie Mungu akutakase na mambo ya siri.

Zaburi 19 : 12
*_Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri._*
Kuna mambo umaweza kuwa unafanya, hakuna mtu atakaa ayajue kamwe, na hayawezi kujulikana kabisa, na hata Mungu akimfunulia mtu unakuta hayaambiliki zaidi ya kukuombea. Sasa we cannot assume tu kwamba watu wao safi tu, hapana! Bedrooms, Hotels, Offices, hata simu tu za mkononi etc zimeficha mambo mengi mno. Na kwa namna yanafanywa kwa usiri. unaweza dumu nayo muda mrefu sana, mambo ambayo kama kifo kinakukuta au mwisho ule, ni wazi tu *UTAKATALIWA*, Sasa kama ni wewe wasoma somo hili, mlilie Mungu, akutakase na mambo ya siri, maana hakuna wa kuyajua makosa yako.

💉 Mlilie Mungu kwa machozi, huku ukimkumbusha kazi alizokutumia, mwambie Mungu kwa hizi nakusihi usiniache nipotee, *NINAPOCHOKA, USINIACHE NIPOTEE*

💉 Hakikisha moyo wako hautukuki kwa kuwa umeinuka sana kihuduma au kiuchumi, endelea kujinyemyekeza kwa Mungu. Ikiwezekana kama mtumishi ingawa mbele za watu unahudumu kwa ujasiri na madaha, ila ukirudi zako chumbani ukafanye kama Yesu 👉🏽 (Waebrania 5:7), nawe utafika salama mwisho, maana BWANA atakutegemeza mwenyewe.

MUNGU AWABARIKI WAPENDWA, KWALEO NI HAYA TU

Mwl Proo
0762879363
All Truth WhatsApp Group

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment