*MAOMBI YA REHEMA ILI KUTANGUA MAVUNO MABAYA, AMBAYO NI HALALI YAKO KUYAPATA*
*_ʍաӀ Թɾօօ_*
*0762879363*
NAWASALIMU KWA JINA LA BWANA (YESU). NAAMINI MNASONGA MBELE, TUJIFUNZE KWELI YA NENO KWA UFUNUO HUU.
*NINI MAANA YA REHEMA?*
Neno rehema kama linavyotumika katika lugha za asili yaani kiebrania na kiyunani, hutajwa kama *hesed/רַחֲמִים* au *eleos/ἔλεος* ni neno ambalo linahusika na tabia za Mungu (It has to do with God's attributes), linamaanisha God's loving-kindness, limebeba ndani yake huruma, fadhili, msamaha (leniency, clemency, forgiveness, compassion, pity, pardon etc). Katika vyanzo kadhaa limefafanuliwa kimuktadha wa mahakama, mtu anayestahili kupata adhabu kwa halali kabisa, lakini akafutiwa hiyo adhabu, amepata rehema. Katika somo letu hili la kuomba rehema, ni kama kumtaka Mungu akukingie kifua dhidi ya mavuno mabaya ambayo kwa kanuni alizozi-establish, unayastahili hayo mavuno. Lakini kwa huruma zake aseme ni kweli huyu mkosaji ameyastahili haya lakini mimi Mungu namrehemu huyu. Na rehema za Mungu ndizo zinaweza kutangua kanuni alizoziweka, kwamba nilisema ukifanya hili utapatwa na hili, sasa umelifanya, ila kwa kuwa umeomba rehema, nakurehemu ili ile kanuni isizae matunda kwako.
Maombolezo 3 : 22
_*Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.*_
Zaburi 103 : 10
*_Hakututenda sawasawa na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu._*
Zaburi 102 : 13
*_Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia._*
SASA TWENDE PAMOJA
👇🏽👇🏽👇🏽
Isaya 28 : 10
_*Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo.*_
Mungu aliset principles, zinauongoza ulimwengu wote, zinafanya kazi katika ulimwengu usioonekana pia, ulimwengu wa roho wa nuru na wa giza kwa pamoja. Siku moja tulikuwa darasani katika kutafakari, kwamba, "Hivi Mungu hakuwa na namna nyingine ya kuokoa wanadamu, mpaka kwa mauti ya Mwana wake? Na ukisoma maandiko yanayozungumzia fidia ile ya msalabani tukajihoji Mungu alikuwa anadaiwa na nani? Si angeweza tu kusema mlikosea sasa nawarejeza bure bure". Mjadala ulienda mbali mwishoni tulifika kwenye swala la kanuni alizoziweka *(INGAWA HE IS THE SOVEREIGN LORD, GOD OF ALL SUPREMACY, hivyo hafungwi, yuko juu hata ya kanuni hizo)*, pia tukagundua mgongano wa sifa mbili za Mungu, Yeye ni wa Upendo lakini ni wa Haki (Haya nitayajadili katika somo jingine).
*KANUNI MOJAWAPO NI HII, UKIPANDA UTAVUNA, YOU SOW YOU REAP!*
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Mwanzo 8 : 22
*_Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno............................... havitakoma._*
Wagalatia 6 : 7
*_Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna._* (soma na mstari wa 8)
Wagalatia 6 : 9
*_Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho._* (And its vice versa is true ukitenda mabaya, utavuna kwa wakati wake usipoomba rehema)
Hapa sio kupanda na kuvuna mazao pekee, kanuni hii ipo katika mambo yote. Kuna mambo ambayo muda unayafanya, unaweza kusema, *"I don't care!"*, kisa ni sirini, lakini kwa kuwa unapanda sharti uvune, mavuno ni malipo, malipo ni hapa hapa duniani (Mithali 11:31). Ingawa kuna hukumu na adhabu ile ya baadae. Kuna mambo (mavuno)mabaya yanaweza kuwapiga watu kama mavuno kwao, lakini ufahamu ukikosekana, unaweza kuwa bize kuyakemea kwa jina la Yesu, kumbe kuna kanuni unai-overlook. Sio mambo yote yanahitaji kuyakemea na kuyaamuru yaondoke, bali yako mambo unahitajika kuomba rehema, maana ni mavuno halali. Reubeni ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo/Israel, alifanya jambo fulani akihisi ni siri, kumbe alikuwa anapanda, na akavuna. Baba yake alikuwa na wake wakubwa wawili na bi wadogo wawili. Yeye alikuwa akirudi home hamwoni babaake around anapanda kitandani na kushiriki ngono na mamaake mdogo; yaani Bilha (Mwanzo 35:22). Hiki alichofanya kilipekea litolewe tamko *USIWE MKUU!*, Yakobo alipowaita watoto kumi na mbili awabariki, utagundua hakuna baraka iliyoachiliwa kwa Reuben ila alitangua nafasi yake katika ulimwengu wa roho, kwa kosa la kumwingilia mwanamke ambaye baba yake pia huingia. Na hivyo hutasikia tena sifa ya Reubeni na uzao wake kwa mambo ya ukuu, au zile baraka zilizopaswa kuambatana na mzaliwa wa kwanza. Ni kwa namna hiyo hiyo, yako mavuno mabaya ambayo watu wanayavuna kwa halali. Yuko mkuu wa shule fulani ya Sekondari nilipewa ushuhuda wake namna alivyofanya uharibifu na ufuska wa kuvibikiri vibinti vya watu, alitumia cheo chake vibaya. Lakini haya aliyofanya alikuwa anapanda, na yeye akaja kupata watoto wakakua, sasa kiukweli watoto alio nao ni heri asingezaa tu. Watoto wake wamekubuu kwa uhuni, huwezi hata kuwatambulisha hawa ni wanangu, wakirudi kijijini ni aibu hata kupishana nao njiani, wanayofanya hayaambiliki (Ezekiel 18:2-20 imezingatiwa). Ndivyo ilivyo leo hii mwanaume unatoka na mke wa mtu, unashiriki naye ngono ukiwa na akili timamu huyu ni mke halali mwenye agano la ndoa kwa mumewe, huku unajitetea, "Alinitaka mwenyewe", hilo halitapita patupu, pando hilo lina vuno lake baya huko mbele, na mara nyingi watu wanavuna kitu walichokipanda, hawavuni mapapai kwenye migomba ya ndizi, kama ulitoka na mke wa mtu hukushikwa, wewe ipo siku wako utamkuta red handed na mchepuko, kama hukujua watu wanajinyongaje, utajifunza siku hiyo. Mwanaume umeishi kwa ufuska, una historia ya kuwaingilia wanawake kinyume na maumbile, Sasa upo kwenye ndoa unakutwa na majanga mara huna nguvu za kiume, mara sijui unapata magonjwa ya kuziba mirija fulani katika njia za uzazi (magonjwa ya siri ambayo yamejazana mijini kwa sasa), haya yakukutapo ni mavuno tu halali ya yale ulipanda. Binti ulitoa mimba kadhaa, uliflush viumbe hai kwa kumeza vidonge na kuwanyofoa, ikavuruga systems za uzazi, sasa upo katika ndoa, ujauzito unagoma, sio swala la maombezi na kumkemea shetani, hilo ni vuno baya, ambalo ni halali yako. Ulikataa maonyo ya Roho, ukiwa hujaolewa ukabeba mimba kadhaa na wanaume mtaani wakashuhudia, na wanakujua ni mwokovu, sasa kama unakutana na changamoto ya kukataliwa na wanaume kila ukiwajulisha una watoto uliowazalia nyumbani, usimlaumu Mungu au kufanya bidii ya kukimbilia maombezi ya kukanyaga mafuta ya upako, kule kukawia au kukataliwa au kukosa mtu ambaye kwa kweli ndiye haswa alipaswa awe wako, ni vuno baya, ambalo ni halali kabisa, kwa zile kanuni zilizowekwa, huku kidogo na huku kidogo maana yake imebalance kama *beam balance* ⚖ (Isaya 28:10), Ulifanya kazi ukawa unapiga panga change (chenchi) za boss wako, ukawa unachakachua taarifa za fedha, hayo ni mapando ambayo yana mavuno yake mahali, utakuja shangaa una site yako unajenga nyumba, mafundi wakakuchakachulia vifaa vya ujenzi au ukakuta simenti unayopeleka haifanani na kazi inayofanyika. Wewe ni Human Resource Manager, unawasaidia wadada kuzipata nafasi za kazi zilizotangazwa, lakini baada ya kuitumia miili yao, hawapendi dhambi, ila kazi wanazitaka, hivyo ukautumia huo uhitaji wao kuwanajisi wanawake ambao walitamani miili yao wakaitoe kwa waume zao wa ndoa, hii haiwezi kupita bure hilo ni pando kuna mahali utalazimika kuvuna, maana Mungu hazihakiwi. Umeokoka ila kwa wivu tu kuona hivi huyu anaolewa na mkaka huyu tajiri, ukasokomeza maneno ya hila, ukafanya uchumba uvunjike, hilo ni pando, nimetoa mifano hii michache lakini katika maisha ya kila siku tunapanda mengi.
*I WANT TO MAKE MYSELF CLEAR HAPA*
Najua wahubiri wahubirio neema wanaweza kuniwahi na *2Korintho 5:17*, kwamba ya kale yamepita. Ipo hivi, in some cases wako watu walifanya mabaya kabla ya kuokoka, walipofanya toba za kujutia maovu yao muda walipoamini, Mungu aliwarehemu, zile rehema zikafuta na athari hasi (mavuno mabaya) ambayo yalikuwa halali yao, ndipo unakuta mtu ameokoka, na ukimwi ukapona kabisa, ukimwi hakuupata kwa kuonewa, ukimwuliza mwenyewe atakusimulia alivyokuwa akijionesha umwamba katika kubadili wanawake au wanaume, hivyo alivuna vuno baya kwa halali, ila wokovu ukaja na Mungu alipomrehemu akapona, *BUT THIS IS NOT ALWAYS THE CASE!*, wako ambao baada ya kuupata wokovu wakasamehewa lakini madhara ya uovu kwa mfano alitoa sana mimba, akaharibu kizazi, ukakuta hili limebaki kama lilivyo, na hawa ni wengi zaidi kuliko wale wengine. By the way sina haja kukazia kuhusu maovu au makosa yaliyotendwa kabla ya kuamini, maana watu hata baada ya kuamini, wamepanda mapando mengi tu ambayo yanastahili mavuno mabaya.
*MAOMBI*
Tunapaswa kuomba rehema za Mungu, taani Mungu atukingie kifua juu ya kanuni zilizotupa mavuno mabaya, ili baada ya hapo kama ni kuomba uponyaji iwe mteremko. Nilimfurahia mtumishi mmoja wa Mungu wanaokuja na matatizo haombei tu hali akishindana na kanuni zilizowekwa, na kwa kuwa anatumiwa kwa karama za ufunuo, anapomhudumia mtu anagundua shida iko wapi kabla, incase hajafunuliwa lazima atamhoji mhusika maswali ya msingi kama amehisi huyu mtu anavuna vuno baya, ili kabla ya kufanya maombezi ambayo yako *rough* rohoni. basi ajue hili linastahili kwanza kutaka rehema za Mungu, ili kuitangua kanuni iliyoletea mavuno halali, kisha kuomba upomyaji, upenyo na muujiza inakuwa ni mteremko sana. Kumwuliza taarifa za msingi mhudumiwa, sio kwamba upo mwilini, Yesu alitumiwa kwa karama za ufunuo, lakini alihoji mzazi wa yule kijana aliyepagawa pepo, kwamba amekupatwa haya tangu lini (Marko 9:21). Na Paulo alipomzuia Timothy kuwahi kumwekea mtu mikono kwa haraka, ili ashiriki dhambi maana wengine inahitajika rehema kwanza (1Timothy 5:22).
*HABARI NJEMA NI HII; USIOGOPE*
*MUNGU NI MWINGI WA REHEMA, ANAREHEMU WATU ELFU ELFU, KAMA KUNA JAMBO LINAKUTESA, LINAKUSONGA, LINAKUCHOSHA, NA UKIKUMBUKA KWAMBA ULISABABISHA MWENYEWE UNAKOSA UJASIRI KULIKEMEA LITOKE, MUNGU ANALO JIBU LAKO LEO, OMBA REHEMA KWA MUNGU KWA AJILI YA MAPANDO ULIYOPANDA, MUNGU ATAKUKINGIA KIFUA, ATAKUFANYA MPYA KABISA, MAKOSA ULIFANYA KWELI, LAKINI MADHARA YAKE/ATHARI ZAKE ZITAFUTWA MARA MOJA, NAWE UTAUFURAHIA UHURU NA UPONYAJI MKAMILIFU*
Mwl Proo
+255762879363
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment