*_JITAJIRISHE KWA MUNGU_*
Mwl Proo
0762879363
0718922662
Halellujah!!
Neno la Mungu ni zuri,mimi linanibariki hata kabla sijaandika chochote,lipe nafasi ya kwanza ili liwe linafaa,kuna wakati nilikuwa nakaa nje ya nyumba yetu 💺nasoma Biblia,lakini kwa sababu ya utamu wa Neno 😋📖,nikawa nakatisha kusoma nasimama narukaruka kwa furaha💃🏼kabla ya kuendelea tena kusoma. Sasa usipoona utamu unaposoma Neno ni dalili ya kuwa kuna shida kwenye swala la unyofu wa moyo,maana neno linamfaa mnyofu wa moyo(Mika 2:7b) ,Ok sio somo letu la leo hilo.
Leo nimejaa moyoni siri hii,KUJITAJIRISHA KWA MUNGU.
Wako watu hawakujua namna ya kumtaka Mungu na nguvu zake(Zaburi 105:4), yaani walipostareheshwa na BWANA kwa kupata kazi nzuri,akawa Managing Director sijui General manager yaani anaogelea pesa💵💴💶💷💰🏧,bajeti yake ya lunch ni zaidi elfu 40 kwa siku, ofisini kuna vinywaji vyote vizuri🍷🍹🍸🍾kila ukigeuka una unafungua jokofu. Sasa wengi ktk mazingira hayo hawakumbuki kuwa baraka hizo hazipo kukusahaulisha Mungu. Ukiwa ni wa standards hizo *_ILI USIMKOSE MUNGU NA ADUI ASIKUPIGE_*, TUMIA NAFASI KAMA HIZO KUJITAJIRISHA KWA MUNGU.
*Luka 12 : 21*
*_Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu._*
SASA MTU OFISI IMEKUTENGEA PESA NYINGI KAMA MEAL ALLOWANCE,NAWE BADALA YA KUTUMIA HUO MWANYA KUUTEKA UFALME WA MUNGU(MATH 11:12,LUKA 16:16) KWA BARAKA ZIMEKUWA JARIBU YAANI HAPO HATA KUJITOA UFUNGE KWA MAOMBI ILI ILE LUNCH ALLOWANCE UIPELEKE MARA MOJAMOJA IKAFANYE KAZI YA MUNGU,UNAJUA KABISA KANISANI KWENU KUNUNUA MICROPHONE🎤 YA ELFU 80,WANACHAGISHANA WEEE👌🏽POVU LAWATOKA WATUMISHI MPAKA WANATOA VITU VIPIGWE MNADA,ILI INUNULIWE MAIKI AMBAYO WEWE NI PESA YAKO YA LUNCH SIKU MOJA TU. HAZINA YAKO UMEIWEKA KWA MUNGU WAKO TUMBO(MATH 6:19-21)
*Wafilipi 3 : 19*
*_mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani._*
KWA KUKOSA KIASI UMEISHIA TU KUPATA KITAMBI CHA AJABU AJABU UKIJANADI UMEBARIKIWA BADAE SANA UNAPOANZA KUSUMBUKA NA KISUKARI NA PRESHA ZA AJABU NDIPO UNATAKA KUMKUMBUKA MUNGU,SASA HIZO NDIZO TABIA ZA WATU WAJILIMBIKIZIAO KILA KITU ,WASIJITAJILISHE KWA MUNGU.
KAMA UTAWEZA KUTUMIA ULIYONAYO KUJITAJIRISHA KWA BWANA,UTAKUWA NA MWISHO MZURI WA AMANI,HATA UZEE WAKO UTAKUWA WA BARAKA NA UJANA WAKO UTAREJEZWA (ZABURI 103:5)
*Zaburi 37 : 37*
*_Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani._*
```JE! UNA AFYA NJEMA?```
wakati upo na afya safi kabisa,hakuna magonjwa yanakusumbua,huo sio wakati wako wa kui-enjoy dunia kwa kula maisha tuu bila kujitajirisha kwa Mungu,afya yako idhabihu kwa Mungu,yaani tumia huo mwanya kufanya ya Mungu kwa juhudi,tena huo ndio wakati wako wa kujiwekea akiba ya maombi na kumtafuta Bwana, maana kuna majira magumu ya hatari,yanaitwa majira ya kujiliwa kwako (Luka 19:44),Kama hukutumia hiyo nafasi hiyo ya wakati wa afya tele,kumsaka Mungu yale majira ya kujiliwa utakutwa dhaifu bila nguvu ya Mungu,na kupigwa utapigwa bila shaka, *HUTAWEZA KUSIMAMA SIKU YA UOVU*
*Zaburi 32:6*
*_6 Kwa hiyo kila mtu mtauwaAkuombe wakati unapopatikana.Hakika maji makuu yafurikapo,Hayatamfikia yeye._*
👆🏼Kuna wakati maji makuu yatafurika(kutatokea disasters mbalimbali ktk maisha yako,sasa yanapoinuka majanga hayo,kama ulijitajirisha kwa Mungu ,effects/athari ya hilo janga itakuwa *_Reduced to Zero_*. Ila kama wakati wa neema ulitumia nguvu kubwa kujifurahisha ktk udhalimu athari za maji makuu yafurikapo itakuwa *_at the maximum_*. Lakini kama umjitajirisha kwa Mungu hata ukiwa hoi kwa ugonjwa,there on your sick-bed there will be God's hand to sustain thee (Zaburi 41:3)
*_3 BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.Katika ugonjwa wake umemtandikia._*
```JE! MUNGU AMEKUPA KAZI NZURI?```
Hiyo ni nafasi yako nzuri ya kumtukuza Mungu,muoneshe Mungu hapo kazini na penginepo,daima ukiri wako *_"IT IS ONLY GOD KWA KWELI"_* hiyo sio nafasi yako ya kubadili usemi na kutumia matamshi(Slang) ya kimarekani kuongelea kiswahili,na kujieleza bidii yako ukiwa masomoni,ujue kuwa ni Mungu tu kakuheshimu,maana kuna classmates wako walifariki siku chache baada ya Graduu🎓ya chuo. Kuna kaka mmoja alilelewa na CASFETA akiwa masomoni ila Mungu akamwinua sana baada ya kumaliza masomo,akawa kwenye ajira ya mapato makubwa sana. Sasa vijana walitumwa kwake kumwomba mchango wa kambi la pasaka la CASFETA,sasa akapokea barua ya mchango akaiweka kabatini. zikia zimebaki siku chache akapigiwa simu na mratibu kuulizwa hivi mpendwa ulipata barua ya mchango? alijibu kwa dharau, *_"niliipata, BUT THE WAY MLIVYOOMBA SIJAPENDA"_* yaani alitaka aabudiwe kwanza na anyenyekewa ndio asapoti kazi ya Mungu,hiki ni kiburi cha kusahau ulipotoka,wakati semisters kadhaa hata ada ulichangiwa na wanafellowship. Kumbuka *Downfall goes after pride*. Na Mungu anapingana na wenye kiburi(He resists them) na yale magumu ya wakati wa dhiki kuu atayaleta ili kukishusha kiburi cha wanadamu (Isaya 2:17)
```JE! MUNGU AMEKUPA NATURAL/INNATE TALENTS NA VILE VIPAWA VYA KIROHO?```
Mungu alikupa hayo kwa kuwa wewe ni kiungo,uwafae wengine,sasa wachache wasiojua siri za kujitajirisha kwa Mungu wanatumia hivyo kuusaka tu umaarufu,then kwa umaarufu wao na hali ya maisha wanatumia mwanya huo kutesa na kusumbua watu,utakuta kijana wa kiume aliyejaliwa vipawa vile vyenye mvuto,anaamua kutumia hiyo nafasi kuharibu mabinti,keshachumbia wengi na kuwaacha wengine aliwapa na ujauzito akawatosa baharini🌊, ~*(be sure of this,there is a time for your downfall)*~
KATIKA NAFASI YOYOTE ULIYO NAYO,JITAJIRISHE KWA MUNGU *_UNTIL IT BECOMES TOO MUCH OF GOD IN YOU_* JINYENYEKESHE KWAKE,PRAY CEASELESSLY,TUMIKA CONTINUALLY,MTOLEE MUNGU NON-STOP IN A GOOD MEASURE,DUMU KTK UTAKATIFU WAKO. UKIJITAJIRISHA KWA MUNGU KTK ILE KAZI YAKO YA HESHIMA(WHITE COLAR JOB WITH GREEN PASTURE) HATA KUKIPITA TUMBUATUMBUA WEWE MKASI✂ WA KUTUMBUA HAUTAKUPITIA UTANUSURISHWA TU,NA KAMA MUNGU AKIRUHUSU UJUE AMEANDAA PALIPO PEMA ZAIDI
LAKINI WALE WASIOJITAJIRISHA KWA BWANA HUWA HAWANUSURISHWI NA WAKITUMBULIWA LAZIMA WASOTE MPAKA WANADODA ILI KIBURI KISHUSHWE.
*ALIYEJITAJIRISHA KWA MUNGU*
✝Ataona mambo ambayo wengine hawajayaona and so to say,he/she will be having a clear insight in all endeavours of life
Mkumbuke Yusufu ktk umri wa miaka 17 alikuwa tayari ni kijana aliyejitajirisha kwa Bwana kama angekuwa Tanzania iwa umri wake huo kijana wa KIDATO CHA III ,mwenye kujua kumsikia Mungu kwa ndoto,what about David the son of Jesse ktk miaka 12 anamjua BWANA na kumtumaini,akiwa na umri huo yaani mwanafunzi wa darasa la 5B amejaa Mungu na Mungu alikuwa anam-admire mno (Mdo 13:22),lakini mibrother men akina Eliabu kaka zake Daudi walikuwa bize tu kuchat📱na kuangalia📺lakini hawakujitajirisha kwa Mungu ndio maana hawaku-qualify ktk uchaguzi wa Mungu nani awe mfalme. Je unamkumbuka Ezekiel nabii wa Roho,yeye alikuwa na watu wa uhamisho ktk mto Kebari mbingu zilifunguka wenzake hawakuona kitu ila yeye akaona yale maono mazito ya wenye uhai na magurudumu yenye roho zao,Je wamkumbuka Daniel akiwa na watu wengi kando ya ule mto mkubwa Hidekeli,akaona maono mazito peke yake maana alijitajirisha kwa BWANA,pamoja na kuwa na cheo cha tatu cha juu ktk serikali ya Dario mfalme ,ila alikuwa akikumbuka mfungo/Saumu tena ya kujinyima chakula kitamu🍗🍖🌭🌯🌮🍹🍹🍷🍷 ili amtake BWANA na Nguvu zake. WEWE NDUGU YANGU UKO WAPI?
✝Atafanywa kuwa msemaji wa Mungu (God's spokesman)
Yeremia 15:19
19 Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika *_kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu(my spokesman)_*;
Funua kinywa chako nami nitakujaza,walijitajirisha kwa Mungu,hujazwa maarifa ya Mungu,na they are enriched with enough information about God,yaani mnasoma wote Biblia moja ila huyu aliyejitajirisha kwa Mungu ana uwezo mkubwa wa kufafanusha (Zaburi 119:130)
✝Mahali pa hatari kuu,utakuwa na jibu la Mungu kwa ajili yako na kwa ajili ya watu ulio nao
*Matendo 27*
*_1 Na walipokuwa wamekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paulo akasimama katikati yao, akasema, Wanaume, iliwapasa kunisikiliza mimi na kutokung'oa nanga huko Krete, na kupata madhara haya na hasara hii._*
*_22 Sasa nawapeni shauri, iweni na moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu atakayepotea, ila merikebu tu._*
*_23 Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami,_*
👆🏼👆🏼Eh bwana kitu hicho😋😋😅😅👌🏽👌🏽
*_24 akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe._*
*_25 Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa._*
👆🏼👆🏼😰Duu Neno la Mungu ni hatari sana
Aisee Bwana awabariki,mnapoweka mikakati ya kuanza kujitajirisha sana na wengine wengi ni mwendelezo tu ila daima wanajitajirisha kwa Bwana
For inquires
Mwl Proo
0762879363(WhatApp#only)
alltruth5ministries@gmail.com
Asante sana kwa somo nzuri nimebarikiwa snaa Mungu zaidi kukuweka 2018 ukawe kwako wa baraka zaidi pia Mungu akupe wa kufanana nae ili Huduma uliyonayo ikafike mahali pa kusaidiana watu wengi wanaohitaji kukuwa kiroho
ReplyDeleteAsante sana kwa somo nzuri nimebarikiwa snaa Mungu zaidi kukuweka 2018 ukawe kwako wa baraka zaidi pia Mungu akupe wa kufanana nae ili Huduma uliyonayo ikafike mahali pa kusaidiana watu wengi wanaohitaji kukuwa kiroho
ReplyDelete