Monday, January 1, 2018

CHOMBO KIMFAACHA BWANA

*CHOMBO KIMFAACHO BWANA (2Timotheo 2:21)*

_Mwl Proo_
0762879363

Shalom Aleichem!✋🏼

Nawasalimu kwa jina la Yesu.

Leo tujifunze kuhusu vyombo,mifano ni ile ambayo kila mtu ataielewa na ni dhahiri ktk maisha yako hapo nyumbani.

*_TUJIFUNZE AINA ZA VYOMBO_*

2 Timotheo 2 : 20 *_Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina._*

Ufunuo wa Yohana 18 : 12
*_.............. na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari_*

Tusomavyo ktk maandiko  hayo ndivyo ilivyo,tukiingia nyumbani kwenu leo,tutakuta vyombo tofautitofauti,kuna utofauti wa material iliyotumika kukitengeneza,rangi n.k na mara nyingi material iliyotumika inafanya chombo kiamriwe aina ya matumizi,na aina ya matumizi inakipa chombo kuwa cha heshima au kisicho na heshima; Themos ya chai haitalingana heshima na kopo la bafuni/kuogea.

Agano la kale ambalo ni kivuli cha mema haya ya sasa,linatoa picha nzuri kuhusu vyombo *_NA KILA CHOMBO KINAWAKILISHA MAISHA YA KIROHO YA VIWANGO FULANI_*

1.SIO VYOMBO VYOTE VILIFAA KWA UTUMISHI WA MUNGU

>Madhabahu ilihitaji chombo cha mawe,Mungu hakutaka chombo cha chuma ktk kuijenga madhabahu

Kumbukumbu la Torati 27 : 5
_*Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake.*_

>Vyombo vya hazina ya Bwana havikutakiwa kuwepo vya miti,bali vya shaba,chuma n.k

Yoshua 6 : 19
*_Lakini fedha yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na chuma, ni vitakatifu kwa Bwana; vitaletwa katika hazina ya Bwana._*

MUNGU ALIWEKA HESHIMA TOFAUTI YA VYOMBO

Warumi 9 : 21
_*Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?*_

KWA MFANO CHOMBO CHA MTI NA CHA UDONGO VILIKUWA NA TOFAUTI KUBWA KIHESHIMA. KAMA MTU MWENYE KISONONO ANGEGUSA CHOMBO CHA UDONGO BASI MAELEKEZO YA TAURAT NI KUKIVUNJA,ILA AKIKIGUSA CHA MTI BASI MNAKIOSHA TU

Mambo ya Walawi 15 : 12
*_Na chombo cha udongo ambacho amekigusa mwenye kisonono, kitavunjwa-vunjwa; na kila chombo cha mti kitaoshwa majini._*

LAKINI PIA CHOMBO CHA UDONGO KILIKUWA NA SIFA YA KUHIFADHI KITU KWA MUDA MREFU,TENA HAKIPATI KUTU,SO KILIFAA FOR PRESERVATIVE PURPOSES

Yeremia 32 : 14
_*Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Twaa hati hizi, hati hii ya kununua, hati hii iliyopigwa muhuri, na hii iliyo wazi pia, ukazitie katika chombo cha udongo, zipate kukaa siku nyingi.*_

2.SIO VYOMBO VYOTE VILIFAA KTK UTOAJI MAHARI
Kulikuwa na vyombo vyenye heshima ya kutumiwa ktk posa,na vingine havikufaa

Mwanzo 24 : 53 *_Kisha huyo mtumishi akatoa vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, akampa Rebeka; na vitu vya thamani akampa nduguye na mamaye pia._*

*AINA MBALIMBALI ZA VYOMBO VIFUATAVYO VINAASHIRIA HALI MBALIMBALI ZA MAISHA YA WATU_*
Wako watu walifanywa vyombo vizuri vya kufaa,na vya kupata heshima lakini waliyaharibu maisha yao kiroho na ile sifa ikabadilika

Maombolezo 4 : 2  _*Wana wa Sayuni wenye thamani, Walinganao na dhahabu safi, Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo, Kazi ya mfinyanzi*_

▶CHOMBO KISICHO NA KIFUNIKO

Kifuniko huwakilisha Roho Mtakatifu(Isaya 30:1)
Viko vyombo hata nyumbani kwenu ambavyo vikiisha poteza kifuniko,havifai tena,kama kilikuwa kinawekewa maji ya kunywa(ndani ya friji) basi kitapelekwa kuwekewa chumvi jikoni na vingine hutupwa

Hesabu 19 : 15
*_Na kila chombo kilicho wazi, kisichofungwa na kifuniko, ni najisi._*

👆🏼Huyu aliyekosa kifuniko,hawezi kujizuia,kila uchafu wa dunia humpata asiweze kuwa chombo cha kumfaa Bwana.

▶CHOMBO KIPYA
Chombo kipya,kina heshima yake,na halitafanyishwa kaI zile ordinary,huenda kikasubiriwa shughuli maalum ili kianze matumizi nyakati hizo,Elisha alihitaji chombo kipya ili aponye maji yenye kuzaa mapooza

2 Wafalme 2 : 20 *_Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea._*

Mungu kuna baadhi ya utumishi anahitaji akufanye chombo kipya ndipo utamfaa

Isaya 41 : 15
*_Tazama, nitakufanya kuwa chombo kikali kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha milima, na kuisaga; nawe utafanya vilima kuwa kama makapi._*

👆🏼Chombo Kikali(sharp) kuna watu maisha yao yamekuwa butu(dull) mtu amezoelea dhambi mpaka akitenda hashtuki tena,alikuwa huko nyuma akisema uongo anakosa raha mpaka atubu lakini sasa amekuwa butu(Chombo butu kisicho kikali,kinawakilisha dhamiri iliyokufa nafsini mwa mtu) Sasa Mungu anataka chombo kikali-kipya kimfae kwa kusudi lake

Isaya 28 : 27
_*Kwa maana kunde zile hazipurwi kwa chombo kikali, wala gurudumu la gari halipitishwi huko na huko juu ya jira ile, bali kunde zile hupurwa kwa fimbo, na jira ile kwa ufito.*_

▶CHOMBO KILICHOVUNJIKA
Bila shaka ukikagua ktk kabati unaweza kuta kuna chombo cha udogo au cha  kioo,either kina nyufa au kimevunjika,Sifa kuu ya chombo kilichovunjika ni kusahaulika. Yaani vumbi,buibui walikifanya makazi yao,Chombo kilichovunjika,huwakilisha watu wasiojitengeneza mioyo kwa Bwana,wasio na toba,wanakubali kuishi na uovu,wanapewa nafasi ya kutubu lakini hawataki(Ufunuo 2:21)

Zaburi 31 : 12 - _*Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa; Nimekuwa kama chombo kilichovunjika.*_

▶CHOMBO KISICHOPENDEZA

Viko vyombo ambavyo huenda bado vinatumika lakini kwa kuwa havipendezi havitapewa heshima,ya kuwekwa  pahala pazuri pa kuonekana,huenda kikafichwa stoo kwenye kila takataka ambazo zinadhaniwa kuhitajika bado. Kwa mfano kinu cha kutwangia,hakitapewa heshima ya kuwekwa sebuleni,kitawekwa ua wa nje kama ni jikoni kwenywe kona au stoo.

Yeremia 48 : 38
_*kwa maana nimevunja Moabu kama chombo kisichopendeza, asema Bwana.*_

Hosea 8 : 8
_*Israeli amemezwa; sasa wamo miongoni mwa mataifa kama chombo kisichopendeza.*_

▶VYOMBO VIPENDEZAVYO

Nahumu 2 : 9  *_Chukueni nyara za fedha; Chukueni nyara za dhahabu; Kwa maana ni akiba isiyoisha, Fahari ya vyombo vipendezavyo._*

Hosea 13 : 15
_*.............yeye atateka nyara hazina ya vyombo vyote vipendezavyo.*_

VIKO VYOMBO HATA MACHONI PA BWANA NI VYA KUPENDEZA,VIATU HATA VIKIWA VIPYA HAVIPEWI HESHIMA KUWEKWA JUU KWENYE DRESSING TABLE,HAVIPENDEZEI. LAKINI UNAONAJE KWA HABARI YA TV🖥 UKILINGANISHA NA KINU KIPI NI CHOMBO CHA KUPENDEZA HATA KUPEWA HESHIMA KIKAE SEBULENI?

▶VYOMBO VITUPU
Kuna watu ingawa wana muda mrefu ndani ya wokovu,lakini vyombo vitupu,mkimpa hata madhabahu dakika 10 hana cha kuzungumza,anaweza jitetea sio huduma yake,lakini umekosaje ushuhuda   wa matendo ya Mungu wakati unaye Mwana,kila aliye na Mwana hakosi huo ushuhuda wa wema wa Mungu,tatizo hapo ni chombo kuwa kitupu,na ndio maana hata ukikutana na mtu,unagundua ana shauku ya kusikia habari za Yesu,ila unamwelekeza pengine,maana wewe ni chombo kitupu

PIA VIKO VYOMBO VYA KUDHARAULIWA,VYOMBO VYA ANASA,VYOMBO SAFI VYA THAMANI N.K N.K (Yer 22:28,51:34,25:34)

Yeremia 14 : 3 - _*Hurudi, na vyombo vyao ni vitupu; Wametahayarika na kufadhaika, Na kuvifunika vichwa vyao.*_

~*_KIPO CHOMBO  KINAMFAACHO BWANA_*~

2 Timotheo 2 : 21
_*Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.*_

*NB:-*
KUNA MAMBO UNAPASWA KUYAACHA,KUYAONDOA ILI UWE CHOMBO CHA KUFAA

Katika 2Timotheo 2:21 Anakijadili chombo kimfaacho Bwana

🔴Basi ikuwa mtu amejitakasa kwa kujitenga,neno takasa maana yake set apart,weka wakfu kwa ajili ya .......... Sasa mstari huu unajadili wale akina Himenayo na Fileto wenye mafundisho potofu yaliyoenea kama donda ndugu,lakini anasema mtu akijitakasa kwa kujitenga na mambo hayo ya kina Himenayo na Fileto(ambao leo hufananishwa na uchafu wote wa dunia unaopingana na maisha matakatifu ....

Huyu mtu atakuwa chombo cha kupata Heshima. kama ulikuwa chombo cha mti Bwana  atakufanya cha fedha au dhahabu
Kwa maana hiki ndicho kimfaacho Bwana *KIMETENGENEZWA*
kwa kila kazi njema.

NDUGU WAPENZI MUNGU HANA UPENDELEO LAKINI KUNA WATU WAMEJITAKASA MAISHA,WAMEJITENGA NA UCHAFU KWA HIYO HUDHANIWA MUNGU KAWAPENDELEA WAMEPEWA KARAMA NYINGI(NUMBER OF RESPONSIBILITIES) KTK UFALME YAANI NI KAZI TELE,WANAFAA KILA MAHALI,KILA HUDUMA ANAYOIFANYA IMEJAA UTUKUFU,MNALINGAMA UMRI,MLIKUWA WOTE FELLOWSHIP,LAKINI LEO HII MWENZIO ANAHUDUMIA MAELFU  YA WATU KILA WAKATI,NAFASI HIZO HAJAJITENGENEZEA,LAKIJI KWA KUWA ALITENGENEZWA NA MUNGU,ANAFAA KWA KILA KAZI NJEMA,ANAANA KUIONA FUTURE YAKE,MAISHA YAKE YANAENDA KWA MWENDOKASI KUIKABILI DESTINY YAKE,KWA UMRI WAKE MDOGO WA MIAKA 25 AMEKWISHA INFLUENCE(POSITIVELY) HUMAN RACE,SASA UNATAKA KUWA CHOMBO KUMFAACHO  BWANA? JITENGE NA DUNIA,LAZIMA UWE SELECTIVE,SIO KILA KIPINDI CHA TV KINAKUFAA WEWE CHOMBO CHA BWANA,SIO KILA MAVAZI YA FASHENI ZOTE ZINAMFAA CHOMBO CHA BWANA

Isaya 52 : 11  _*Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana.*_

1 Samweli 21 : 5 - *_Naye Daudi akamjibu kuhani, akamwambia, Hakika tumejitenga na wanawake siku hizi tatu; napo nilipotoka, vyombo vya vijana hawa vilikuwa vitakatifu, ingawa ilikuwa safari ya  sikuzote; basi leo je! Vyombo vyetu havitakuwa vitakatifu zaidi?._*

Mithali 25 : 4
*_Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;_*

MIMI NIMEFANYA MAAMUZI YA KUWA CHOMBO KIMFAACHO  BWANA, KWA HIYO KUNA MAVAZI SIVAI,KUNA MANENO SITAMKI(NILIMSIKIA MPENDWA FULANI KILA SAA ANATAMKA ~*_kudadadeki_*~ SIJUI MAANA YAKE LAKINI NAHISI HALIFAI, KUNA VIPINDI VYA TV NILIVIKATAA, KUNA MOVIES📼📀📺,NILISEMA NO, KUNA MIZIKI NILIIKATAA (SECULAR MUSIC ZOTE), UKIANZA WIMBO WA YA MOTO BAND AU DIAMONDI KWENYE 📻REDIO YANGU SIUPOTEZEI KAMA VILE ETI NIPO BIZE, UKIANZA NAUZIMA AU NATYUNI KWINGINE, SWALA LA ZIKIPIGWA KWA DALADALA NI CASE TOFAUTI, NAFSI YANGU IMEJENGWA NITAUSIKIA, SITAUSIKILIZA. KUNA MAGRUPU YA WHATSAPP NIMELEFT HAYANA KITU CHA KUNIJENGA MIMI KAMA CHOMBO CHA  BWANA CHA KUPATA HESHIMA (KAMA LIKIWA SI LA KIROHO BASI LIWE LA KIJAMII LISILO NAJISI), UMEUNGWA KWENYE GRUPU LA WHATSAPP LA KUTUMA VITU VICHAFU WALA HAUTAKI KULEFT(KULEAVE) WEWE NI CHOMBO KISICHOFAA. TENGENEZA NJIA NA MATENDO YAKO,NA UJITENGE UMFAE BWANA KATIKA JINA LA YESU.

MBARIKIWE
Mwl Proo
0762879363 (whatsapp)
0718922662(calls/texts only)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment