Wednesday, January 17, 2018

ATG WHATSAPP LINKS

*MEMO*

_mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu (good manner and order)_
1Korintho 14:40

Wanandoa wa ATG kwenu hapa (Married couples )
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/Csu6gpSx5KjIEks17QguiM

Wale ambao ni Singles (Bachelors+Bachelorettes, kwenu hapa
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/Bqnm7lvJJyz6nQ4KGDnLTl

*_Ndugu wapendwa kigezo cha mtu kuwa kuwa katika subgroup  (ATG Singles au Married Couples) ni kuwa member katika main groups yaani ATG1, ATG2, ATG3 au ATG INT'L. Ikumbukwe kama sio admin unapaswa kuchagua group moja tu. Kigezo hiki kimewekwa ili usikose masomo ya neno la Mungu, ambayo hutumwa katika main groups tu na sio kwa subgroups_*

NB:-
Tunajali uhuru wa kuchagua, wapo ambao hawapendi usumbufu wa meseji nyingi za kule main rooms. Hivyo tunatoa uhuru wa member kuhamia anakopenda muda wowote, akiisha kutoa taarifa kwa viongozi.

Kama husumbuki na wingi wa meseji, basi fuata link ya ATG1
👇🏽
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/CsjUJmmrqk18CaaNq9UmcG

Kama unahitaji utulivu kiasi, fuata link ya ATG2

Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/3HalVOIyiYi64ZtlXtm0TP

Kama hauhitaji meseji za namna yoyote zaidi ya masomo ya neno la Mungu, fuata link ya ATG3
👇🏽

Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/4vpS4ZOQuVJKawrG9njaFs

Na kama hauhitaji posts za kiswahili ila za kiingereza pekee (kigezo cha humu kiwe huelewi vizuri kiswahili au sio lugha yako ya taifa. Fuata link ya ATG INT'L
👇🏽

Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/15iTI8YGP7bLOvFDTs5vkv

ALL TRUTH ADMINSTRATION

Friday, January 12, 2018

NISIWE WA KUKATALIWA!

     *NISIWE WA KUKATALIWA*😥

_Mwl Proo_
*0762879363*
~*_Mjumbe wa matengenezo_*~

*SHALOM ALEICHEM*

1 Wakorintho 9 : 27
*_bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa._*

Wakati mwingi umepita tangu Bwana atie moyoni mwangu neno hili, na sasa nimeona vema kuwaandikia. Neno hili lilinijia kama ombi kwa Mungu, nikiwa chumbani kwangu napiga gitaa 🎸, nikapokea simu toka kwa mdau/follower wa masomo yangu. Mtu huyu alipiga simu akiwa bado anabubujika, analia, ananena kwa lugha kwa furaha na kwa mguso usio wa kawaida, anaongea huku anaomba, ananiombea kwa simu huku akimtukuza Mungu, kwa kunitumia kuandaa somo ambalo alipolisoma Bwana alimtembelea na kuyagusa maisha yake. Muda huo hali yangu kiroho haikuwa nzuri kwa namna ile, yaani hata hilo bubujiko alilo nalo nililimiss (In short, I was not that much smarter spiritually). Sasa alipokata simu, nikaanza kuwaza, hivi Yesu unitumie kuponya na kuinua wengi, then mimi nichoke njiani, niharibu mambo na siku ile uniambie ondoka kwangu, sikukujua wewe!!! 😥😥😥 Baadhi ya masomo yangu yamevuka mipaka ya nchi, yanatumiwa kuimarisha wengi, kuna mchungaji toka nchi moja huko Afrika ya kati, aliniambia anayaandika kwa diary na kuwafundisha washirika wa kanisa analochunga, wanayafurahi na kumwona Mungu. Sasa nikafikiria hivi baada ya kutumika kama chombo, nami nikaendelea na maisha, nikachakachua on the way hapo kati, haifanyi nisamehewe kwa kuwa eti niliwahi tenda vizuri, hapana...

Ezekieli 18 : 24
*_Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa._*

*HATARI NI KWAMBA BAADA YA KUFANYA KAZI NZURI ELFU ELFU, BAADA YA KUFUNDISHA MASOMO MAZURI YA KUJENGA KAMA YA MWALIMU DCK, AU BAADA YA KUPONYA VIJANA KWA MAFUNDISHO KAMA YA MCH. MITIMINGI, AU MAFUNDISHO MAZURI YA NDOA KAMA YA DR.CHRIS MAUKI, AU BAADA YA KUFANYA UINJILISTI ULIOTUKUKA KAMA WA MOSES KULOLA, AU UINJILISTI WA KIMATAIFA KAMA TELEVANGELIST REINHARD BONNKE, AU UKAHUDUMU KWA MADHABAHU YA UIMBAJI KAMA DON MOEN, AU MWIMBAJI MASHUHURI AFRIKA, REBECCA MALOPE, KISHA UKACHEPUSHA ILE HAKI YAKO KWA KUTENDA MOJA YA MACHUKIZO, MWISHO UKAKUKUTA KATIKA KUHARIBIKIWA, BIBLIA INASEMA HALITAKUMBUKWA HATA MOJA KATIKA YALE MEMA YOTE YA UTUMISHI WAKO (Jitahidi usome somo langu linasema Maliza Vizuri)*

*🔋KUENDELEA KUTUMIWA KWA KAZI KUBWA KATIKA HUDUMA, SIO KIASHIRIA CHA KUWA UKO OKAY/SMART KIROHO, NA MUNGU*

🥢Kuna anga la kiroho ukishalifikia (spiritual firmament), utaendelea ku-operate pale juu, hata kama umetoka kuzini na hujafanya toba.
🥢 Balaam hakuwa mtumishi wa Mungu, alikuwa mchawi, mnajimu mwenye elimu za kijini. Lakini alikuwa na spiritual experience ya kutosha katika ulimwengu wa roho wa giza, ndio maana anakutana na malaika wa nuru hakustuka, bado akawa anajielezea adhma yake ya kutaka kumpiga yule punda 👉🏽🐴. Huenda katika ule umati wa waisrael ni wachache waliona laivu malaika, lakini huyu Balaam Bin Beor kwake haikuwa ishu, bila shaka katika kazi zake za ulozi, alishapambana nao huko rohoni. Hivyo Mungu alimtumia kutamka mambo mazito tunayoyasoma katika Hesabu 23, lakini hii haimfanyi awe wa Mungu, na bado katika Yoshua tunaona walimwua kama mchawi tu wa kawaida. Mungu alimtumia kwa yale maana kiwango chake kuyajua mambo katika spiritual realm kiliruhusu.

🥢 Mtu anaweza andaa mahubiri kwa kiwango cha juu sana kiufunuo, wote mkamtukuza Mungu kwa vipawa vya ajabu, lakini huyu mhudumu akawa yuko *rotten* kule rohoni, amechacha/amechina. Huyu mtu neno la Mungu lilifunuliwa kwake, na hivyo kwa ule ujuzi wa kweli, akapandishwa daraja rohoni, akawa ana-opareti na roho ya ufunuo kwa kiwango cha juu, hivyo haijalishi jana yake alifanya dili la kudhulumu kiwanja, bado anaweza kufunua Biblia akafundisha kwa ufunuo wa ajabu, maana kiwango cha nuru kwenye macho yake na level ya roho ya ufunuo aliyoifikia inampa kuyaona mambo kwa kiwango hicho.

🥢 Sauli Ben Kish, alikataliwa na Mungu mapema katika 1Samwel 16:1ff, lakini kuanzia hapo mpaka kufika 1Samwel 31, vita iliyogharimu maisha yake ni safari ndefu, aliendelea kutenda mambo makuu, ila hakuwa na Mungu. Ni huyuhuyu aliyekataliwa akiwa hana Mungu, alifanya mambo mazuri kiroho kama kufuta leseni za wachawi na waganga wote juu ya Israel (1Samwel 28:3ff), ni rahisi tukamsifu tukidhani anaongozwa na Bwana, lakini alikuwa amekataliwa, na aliwafukuza kwa kuweweseka tu, ndio maana mstari wa saba yeye mwenyewe anakimbilia Endori wa mpiga ramli. Hivyo unaweza endelea kumbe ni wa kukataliwa.

🥢 Yako mambo ambayo ni vipawa asili, ila yanatumika katika huduma za rohoni. yanaweza bakia kwa mtu hata kama amefanya machukizo makuu, na kwa kuwa wengi tunabarikiwa tu na vipawa hivi bila kutumia macho ya ndani, mhudumu huyu ataendelea zake mpaka mwisho bila kutengeneza. Kipawa kama cha kuimba, ni kapawa cha asili unaweza kukinoa kikafika mahali pazuri pa kupendwa sana, hata kama usiku wa jana umelala na mume wa mtu, tukikupa microphone  👉🏽🎤, tukakuvunjia makodi (chords) 👉🏽🎹🎸🎺🎻🥁🎷, tunaweza pata hisia kali ya uwepo, na Mungu anaweza shuka kabisa akagusa watu, ila wewe mhudumu usipoweka sawa unakuwa wa kukataliwa. Kipawa cha kuhubiri ni kipawa cha asili tu, ukawa unaongea kwa mitetemo na vibrato kali, mpaka tunahisi raha, hiyo itabaki tu, hata ukiharibu rohoni. Kuna mhubiri (mtume) mmoja yuko Dar lakini sio mtanzania wa kuzaliwa, kuna wanamuziki nilikuwa nao, walimtembelea kwenye ofisi yake ya  kanisa, wakamkuta ofisini yuko zake anatazama sinema za ngono (pornography), na wala hata hastuki kwa kuona wageni, huku muda huo kuna watu wapo nje wanasubiri masaa yatimie waanze kuingia, wamekuja kwa ajili ya ushauri na maombezi. Mungu atawafungua hawa watu kwa ajili yake Yeye mwenyewe, ila huyu mtu ambaye inaonekana dhamiri imekauka huko ndani kwake, anaweza kuwa wa kukataliwa.

🥢 Kama katika magawanyo ya Roho, ulipakwa mafuta, kwa karama za imani au za kuponya au matendo ya miujiza, hayataondolewa kwa kuwa umekosea na hujatubu, ingawa wengine Mungu akitaka kuwarejeza anaweza kuzi-freeze hizo karama ili urekebishe, lakini kwa ambao wamefika mbali sana kihuduma, na muda mwingi au wote wapo katika kuhudumia maelfu ya watu, huwa vinabaki tu. Vitaendelea ku-opareti kwa sababu mpaka ukatumiwa kwa kazi hizo, Roho anakuwa alikupa maarifa maalum ili akutumie, sasa unakuwa na ujuzi ambao bado you can minister tu hata kama umefanya uhalifu.

*🔋 HATARI NI HII*
Watumishi wote wa huduma yoyote, hata wale ambao kwa sababu ya kazi wanazotumiwa wananyenyekewa kiasi kwamba akitokea tu watu wote wanalala chini kama sio kupiga goti, bado huyu mtu naye ni mwanadamu, ana *human limits* bado, hajawa Mungu wala malaika. Binti mmoja aliuliza hivi hiini kweli au ananipima, baada ya kuona mtumishi mashuhuri anamtaka kimapenzi, kila wakionana anamhimiza, alifikiri labda anamjaribu aone kama amesimama, huyu ni mwanadamu kabisa akiacha zile qualities za kiroho anaweza anguka kama wengine. Mwezi Desemba nimepata ushuhuda wa mchungaji katika moja ya madhehebu makongwe ya kipentekoste. baada ya scandals za uzinzi kuwa nyingi, makao makuu yamemhamishia katika kanisa jingine pembezoni kidogo mwa jiji la Dar, huko alipohamishiwa yupo karibu na kanisa la dhehebu jingine (EAGT) analochunga mchungaji rafiki yangu, lakini bado anaendelea na biashara yake ya kuwinda mabinti, ingawa ana ndoa halali. Nilikuwa katika grupu jingine la WhatsApp linalosimamiwa na mtume machachari sana Tanzania. Tukiwa humo mtu mmoja akajoin via *invite link*, alipoingia akasema mnakubalije kuongozwa kiroho na mtu mchafu? Akasema kiongozi wenu ni Admin katika magrupu ya video za utupu, akatuma screenshots kadhaa, anatumia namba yake nyingine, lakini ni yeye kabisa, mimi nilijiridhisha maana nilikuwa nazo zote. Kwa zile screenshots chache niliona aliwa huko anatukana matusi yote ya nguoni, alimtusi kijama aliyenadili *icon* ya group kwa matusi mazito, na picha iliyokuwa ikionekana hapo ambayo kaiweka yeye ni ya binti aliyeufunua utupu wake na kuuanika wazi. Muda huo anashutumiwa kwa uchafu huo, katika grupu lake jingine alikuwa anaendesha semina ya neno la Mungu. Sasa haya mambo ndivyo yalivyo, watu wanaweza kuendelea kutumiwa huku wakiwa wachafu, na mwishoni *WAKAKATALIWA*, zisikumbukwe kazi zote njema walizofanya. Nimetoa mifano michache lakini mambo sio shwari kabisa.

*💊TUFANYE NINI BASI!!*💊
Kila mtu kunaweza kukawa na mambo una-struggle nayo kuya-fix, hilo ni la kawaida tu, Bwana anajua, na anaweza kutusaidia, akatusimamisha pasipo mawaa mbele zake siku ile (Yuda, 24-25).

💉 *Usikubali dhamiri ikanyauka, au ikafa kabisa*
Mungu ametusaidia kwa kutuwekea dhamiri ili usiende mbali sana katika kukosea. Ila dhamiri inaweza kufa na hapo njiani inapitia process za kuugua. Kama mtumishi, unaweza fanya mambo kama hayo hapo juu, lakini husikii kuumia wala kuugua ndani yako, wala you don't fight utoke hapo, tayari dhamiri iko na great damage, hiyo ni hatari sana. Huyu mtumishi kwa mfano kama ameweza kuwa admin wa magrupu ya video za ngono, anaweza fanya mengi mno machafu, na dhamiri haiko salama tena. Nilisimuliwa na rafiki yangu kuhusu mama mtumishi ambaye yeye mwenye kwa hiari yake, amemwomba kijana fulani mtaani kwake wawe wanashiriki ngono, mmewe akiwa safari za huduma (tena ni kijana asiyeamini) ila anajua kuwa anatembea na mama mtumishi, na bila shaka huyu mama mtumishi ndiye anashika huduma mume akisafiri, hapa hakuna usalama.

💉 *Ni kweli una udhaifu kama mwanadamu, lakini badala ya kuendekeza udhaifu, uwe na wakati wa kuingia chumba cha ndani na kumwambia Yesu kibinafsi, kwamba Bwana wangu Yesu, nisaidie. Nina lemewa na nichoka, nipe nguvu mpya (Isaya 40:29-31). Maombi utakayoomba binafsi Mungu akuangalie kama mtu aliyekuchagua, yatasaidia kukunasua.

💉 Mwambie Mungu akutakase na mambo ya siri.

Zaburi 19 : 12
*_Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri._*
Kuna mambo umaweza kuwa unafanya, hakuna mtu atakaa ayajue kamwe, na hayawezi kujulikana kabisa, na hata Mungu akimfunulia mtu unakuta hayaambiliki zaidi ya kukuombea. Sasa we cannot assume tu kwamba watu wao safi tu, hapana! Bedrooms, Hotels, Offices, hata simu tu za mkononi etc zimeficha mambo mengi mno. Na kwa namna yanafanywa kwa usiri. unaweza dumu nayo muda mrefu sana, mambo ambayo kama kifo kinakukuta au mwisho ule, ni wazi tu *UTAKATALIWA*, Sasa kama ni wewe wasoma somo hili, mlilie Mungu, akutakase na mambo ya siri, maana hakuna wa kuyajua makosa yako.

💉 Mlilie Mungu kwa machozi, huku ukimkumbusha kazi alizokutumia, mwambie Mungu kwa hizi nakusihi usiniache nipotee, *NINAPOCHOKA, USINIACHE NIPOTEE*

💉 Hakikisha moyo wako hautukuki kwa kuwa umeinuka sana kihuduma au kiuchumi, endelea kujinyemyekeza kwa Mungu. Ikiwezekana kama mtumishi ingawa mbele za watu unahudumu kwa ujasiri na madaha, ila ukirudi zako chumbani ukafanye kama Yesu 👉🏽 (Waebrania 5:7), nawe utafika salama mwisho, maana BWANA atakutegemeza mwenyewe.

MUNGU AWABARIKI WAPENDWA, KWALEO NI HAYA TU

Mwl Proo
0762879363
All Truth WhatsApp Group

alltruth5ministries@gmail.com

Thursday, January 11, 2018

MAOMBI YA REHEMA, KUTANGUA MAVUNO MABAYA!

*MAOMBI YA REHEMA ILI KUTANGUA MAVUNO MABAYA, AMBAYO NI HALALI YAKO KUYAPATA*

*_ʍաӀ Թɾօօ_*
*0762879363*

NAWASALIMU KWA JINA LA BWANA (YESU). NAAMINI MNASONGA MBELE, TUJIFUNZE KWELI YA NENO KWA UFUNUO HUU.

*NINI MAANA YA REHEMA?*

Neno rehema kama linavyotumika katika lugha za asili yaani  kiebrania na kiyunani, hutajwa kama *hesed/רַחֲמִים* au *eleos/ἔλεος* ni neno ambalo linahusika na tabia za Mungu (It has to do with God's attributes), linamaanisha God's loving-kindness, limebeba ndani yake huruma, fadhili, msamaha (leniency, clemency, forgiveness, compassion, pity, pardon etc). Katika vyanzo kadhaa limefafanuliwa kimuktadha wa mahakama, mtu anayestahili kupata adhabu kwa halali kabisa, lakini akafutiwa hiyo adhabu, amepata rehema. Katika somo letu hili la kuomba rehema, ni kama kumtaka Mungu akukingie kifua dhidi ya mavuno mabaya ambayo kwa kanuni alizozi-establish, unayastahili hayo mavuno. Lakini kwa huruma zake aseme ni kweli huyu mkosaji ameyastahili haya lakini mimi Mungu namrehemu huyu. Na rehema za Mungu ndizo zinaweza kutangua kanuni alizoziweka, kwamba nilisema ukifanya hili utapatwa na hili, sasa umelifanya, ila kwa kuwa umeomba rehema, nakurehemu ili ile kanuni isizae matunda kwako.

Maombolezo 3 : 22
_*Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.*_

Zaburi 103 : 10
*_Hakututenda sawasawa na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu._*

Zaburi 102 : 13
*_Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia._*

SASA TWENDE PAMOJA
👇🏽👇🏽👇🏽

Isaya 28 : 10
_*Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo.*_

Mungu aliset principles, zinauongoza ulimwengu wote, zinafanya kazi katika ulimwengu usioonekana pia, ulimwengu wa roho wa nuru na wa giza kwa pamoja. Siku moja tulikuwa darasani katika kutafakari, kwamba, "Hivi Mungu hakuwa na namna nyingine ya kuokoa wanadamu, mpaka kwa mauti ya Mwana wake? Na ukisoma maandiko yanayozungumzia fidia ile ya msalabani tukajihoji Mungu alikuwa anadaiwa na nani? Si angeweza tu kusema mlikosea sasa nawarejeza bure bure". Mjadala ulienda mbali mwishoni tulifika kwenye swala la kanuni alizoziweka *(INGAWA HE IS THE SOVEREIGN LORD, GOD OF ALL SUPREMACY, hivyo hafungwi, yuko juu hata ya kanuni hizo)*, pia tukagundua mgongano wa sifa mbili za Mungu, Yeye ni wa Upendo lakini ni wa Haki (Haya nitayajadili katika somo jingine).

*KANUNI MOJAWAPO NI HII, UKIPANDA UTAVUNA, YOU SOW YOU REAP!*
👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽
Mwanzo 8 : 22
*_Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno............................... havitakoma._*

Wagalatia 6 : 7
*_Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna._* (soma na mstari wa 8)

Wagalatia 6 : 9
*_Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho._* (And its vice versa is true ukitenda mabaya, utavuna kwa wakati wake usipoomba rehema)

Hapa sio kupanda na kuvuna mazao pekee, kanuni hii ipo katika mambo yote. Kuna mambo ambayo muda unayafanya, unaweza kusema, *"I don't care!"*, kisa ni sirini, lakini kwa kuwa unapanda sharti uvune, mavuno ni malipo, malipo ni hapa hapa duniani (Mithali 11:31). Ingawa kuna hukumu na adhabu ile ya baadae. Kuna mambo (mavuno)mabaya yanaweza kuwapiga watu kama mavuno kwao, lakini ufahamu ukikosekana, unaweza kuwa bize kuyakemea kwa jina la Yesu, kumbe kuna kanuni unai-overlook. Sio mambo yote yanahitaji kuyakemea na kuyaamuru yaondoke, bali yako mambo unahitajika kuomba rehema, maana ni mavuno halali. Reubeni ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo/Israel, alifanya jambo fulani akihisi ni siri, kumbe alikuwa anapanda, na akavuna. Baba yake alikuwa na wake wakubwa wawili na bi wadogo wawili. Yeye alikuwa akirudi home hamwoni babaake around anapanda kitandani na kushiriki ngono na mamaake mdogo; yaani Bilha (Mwanzo 35:22). Hiki alichofanya kilipekea litolewe tamko *USIWE MKUU!*, Yakobo alipowaita watoto kumi na mbili awabariki, utagundua hakuna baraka iliyoachiliwa kwa Reuben ila alitangua nafasi yake katika ulimwengu wa roho, kwa kosa la kumwingilia mwanamke ambaye baba yake pia huingia. Na hivyo hutasikia tena sifa ya Reubeni na uzao wake kwa mambo ya ukuu, au zile baraka zilizopaswa kuambatana na mzaliwa wa kwanza. Ni kwa namna hiyo hiyo, yako mavuno mabaya ambayo watu wanayavuna kwa halali. Yuko mkuu wa shule fulani ya Sekondari nilipewa ushuhuda wake namna alivyofanya uharibifu na ufuska wa kuvibikiri vibinti vya watu, alitumia cheo chake vibaya. Lakini haya aliyofanya alikuwa anapanda, na yeye akaja kupata watoto wakakua, sasa kiukweli  watoto alio nao ni heri asingezaa tu. Watoto wake wamekubuu kwa uhuni, huwezi hata kuwatambulisha hawa ni wanangu, wakirudi kijijini ni aibu hata kupishana nao njiani, wanayofanya hayaambiliki (Ezekiel 18:2-20 imezingatiwa). Ndivyo ilivyo leo hii mwanaume unatoka na mke wa mtu, unashiriki naye ngono ukiwa na akili timamu huyu ni mke halali mwenye agano la ndoa kwa mumewe, huku unajitetea, "Alinitaka mwenyewe", hilo halitapita patupu, pando hilo lina vuno lake baya huko mbele, na mara nyingi watu wanavuna kitu walichokipanda, hawavuni mapapai kwenye migomba ya ndizi, kama ulitoka na mke wa mtu hukushikwa, wewe ipo siku wako utamkuta red handed na mchepuko, kama hukujua watu wanajinyongaje, utajifunza siku hiyo. Mwanaume umeishi kwa ufuska, una historia ya kuwaingilia wanawake kinyume na maumbile, Sasa upo kwenye ndoa unakutwa na majanga mara huna nguvu za kiume, mara sijui unapata magonjwa ya kuziba mirija fulani katika njia za uzazi (magonjwa ya siri ambayo yamejazana mijini kwa sasa), haya yakukutapo ni mavuno tu halali ya yale ulipanda. Binti ulitoa mimba kadhaa, uliflush viumbe hai kwa kumeza vidonge na kuwanyofoa, ikavuruga systems za uzazi, sasa upo katika ndoa, ujauzito unagoma, sio swala la maombezi na kumkemea shetani, hilo ni vuno baya, ambalo ni halali yako. Ulikataa maonyo ya Roho, ukiwa hujaolewa ukabeba mimba kadhaa na wanaume mtaani wakashuhudia, na wanakujua ni mwokovu, sasa kama unakutana na changamoto ya kukataliwa na wanaume kila ukiwajulisha una watoto uliowazalia nyumbani, usimlaumu Mungu au kufanya bidii ya kukimbilia maombezi ya kukanyaga mafuta ya upako, kule kukawia au kukataliwa au kukosa mtu ambaye kwa kweli ndiye haswa alipaswa awe wako, ni vuno baya, ambalo ni halali kabisa, kwa zile kanuni zilizowekwa, huku kidogo na huku kidogo maana yake imebalance kama *beam balance* ⚖ (Isaya 28:10), Ulifanya kazi ukawa unapiga panga change (chenchi) za boss wako, ukawa unachakachua taarifa za fedha, hayo ni mapando ambayo yana mavuno yake mahali, utakuja shangaa una site yako unajenga nyumba, mafundi wakakuchakachulia vifaa vya ujenzi au ukakuta simenti unayopeleka haifanani na kazi inayofanyika. Wewe ni Human Resource Manager, unawasaidia wadada kuzipata nafasi za kazi zilizotangazwa, lakini baada ya kuitumia miili yao, hawapendi dhambi, ila kazi wanazitaka, hivyo ukautumia huo uhitaji wao kuwanajisi wanawake ambao walitamani miili yao wakaitoe kwa waume zao wa ndoa, hii haiwezi kupita bure hilo ni pando kuna mahali utalazimika kuvuna, maana Mungu hazihakiwi. Umeokoka ila kwa wivu tu kuona hivi huyu anaolewa na mkaka huyu tajiri, ukasokomeza maneno ya hila, ukafanya uchumba uvunjike, hilo ni pando,  nimetoa mifano hii michache lakini katika maisha ya kila siku tunapanda mengi.

*I WANT TO MAKE MYSELF CLEAR HAPA*
Najua wahubiri wahubirio neema wanaweza kuniwahi  na *2Korintho 5:17*, kwamba ya kale yamepita. Ipo hivi, in some cases wako watu walifanya mabaya kabla ya kuokoka, walipofanya toba za kujutia maovu yao muda walipoamini, Mungu aliwarehemu, zile rehema zikafuta na athari hasi (mavuno mabaya) ambayo yalikuwa halali yao, ndipo unakuta mtu ameokoka, na ukimwi ukapona kabisa, ukimwi hakuupata kwa kuonewa, ukimwuliza mwenyewe atakusimulia alivyokuwa akijionesha umwamba katika kubadili wanawake au wanaume, hivyo alivuna vuno baya kwa halali, ila wokovu ukaja na Mungu alipomrehemu akapona, *BUT THIS IS NOT  ALWAYS THE CASE!*, wako ambao baada ya kuupata wokovu wakasamehewa lakini madhara ya uovu kwa mfano alitoa sana mimba, akaharibu kizazi, ukakuta hili limebaki kama lilivyo, na hawa ni wengi zaidi kuliko wale wengine. By the way sina haja kukazia kuhusu maovu au makosa yaliyotendwa kabla ya kuamini, maana watu hata baada ya kuamini, wamepanda mapando mengi tu ambayo yanastahili mavuno mabaya.

*MAOMBI*
Tunapaswa kuomba rehema za Mungu, taani Mungu atukingie kifua juu ya kanuni zilizotupa mavuno mabaya, ili baada ya hapo kama ni kuomba uponyaji iwe mteremko. Nilimfurahia mtumishi mmoja wa Mungu wanaokuja na matatizo haombei tu hali akishindana na kanuni zilizowekwa, na kwa kuwa anatumiwa kwa karama za ufunuo, anapomhudumia mtu anagundua shida iko wapi kabla, incase hajafunuliwa lazima atamhoji mhusika maswali ya msingi kama amehisi huyu mtu anavuna vuno baya, ili kabla ya kufanya maombezi  ambayo yako *rough* rohoni. basi ajue hili linastahili kwanza kutaka rehema za Mungu, ili kuitangua kanuni iliyoletea mavuno halali, kisha kuomba upomyaji, upenyo na muujiza inakuwa ni mteremko sana. Kumwuliza taarifa za msingi mhudumiwa, sio kwamba upo mwilini, Yesu alitumiwa kwa karama za ufunuo, lakini alihoji mzazi wa yule kijana aliyepagawa pepo, kwamba amekupatwa haya tangu lini (Marko 9:21). Na Paulo alipomzuia Timothy kuwahi kumwekea mtu mikono kwa haraka, ili ashiriki dhambi maana wengine inahitajika rehema kwanza (1Timothy 5:22).

*HABARI NJEMA NI HII; USIOGOPE*

*MUNGU NI MWINGI WA REHEMA, ANAREHEMU WATU ELFU ELFU, KAMA KUNA JAMBO LINAKUTESA, LINAKUSONGA, LINAKUCHOSHA, NA UKIKUMBUKA KWAMBA ULISABABISHA MWENYEWE UNAKOSA UJASIRI KULIKEMEA LITOKE, MUNGU ANALO JIBU LAKO LEO, OMBA REHEMA KWA MUNGU KWA AJILI YA MAPANDO ULIYOPANDA, MUNGU ATAKUKINGIA KIFUA, ATAKUFANYA MPYA KABISA, MAKOSA ULIFANYA KWELI, LAKINI MADHARA YAKE/ATHARI ZAKE ZITAFUTWA MARA MOJA, NAWE UTAUFURAHIA UHURU NA UPONYAJI MKAMILIFU*

Mwl Proo
+255762879363

alltruth5ministries@gmail.com

Sunday, January 7, 2018

HAR-MAGEDONI

*_HAR-MAGEDONI_*
(armageddon-english)

*```Ufafanuzi by Mwl Proo```*
0762879363(whatsapp#)

HALELUYA!
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana!
Leo ninazungumzia jambo hili maana muda wa kulizungumzia umefika. Niseme hili kwa mtu ambaye amekwisha kumwamini Yesu sasa *_(AMEOKOKA)_* Hana haja ya kukaa akihofia lolote alilowahi kulisoma ktk kitabu cha Ufunuo. Zaidi ya yeye kujitunza na wokovu wake,hapaswi kuhofia Mpinga Kristo,wala ile 666,wala Yale mapigo kwa wajumbe wa Baragumu wala Vitasa wala zile Ole zitakazo kuwako. Kuna makosa ya tafsiri yaliyotokana na watu kutozingatia nyakati na majira *(chronos&kairos)*,and that results to have everything mixed up. HATUPASWI KUSAHAU KUNA MAMBO HAYALIHUSU KANISA LA KRISTO,KUNA MAMBO YANAHUSU TAIFA LA ISRAEL,NA MENGINE ULIMWENGU MZIMA PASIPO KULIHUSISHA KANISA. KWA MFANO DHIKI KUU HAINA UHUSIANO NA KANISA,VITA YA HAR-MAGEDONI HAINA UHUSIANO NA KANISA, BADO LAZIMA TUKUMBUKE TUKIO LA UNYAKUO WA KANISA,HALINA UHUSIANO NA UJIO WA PILI WA YESU ULE UTAKAOHUSISHA MATAIFA YOTE KUMWONA YESU NA KUMUOMBOLEZEA (MATH 24:30,UFUN 1:7), MITAZAMO YOTE ILIYO KINYUME HAIWEZI KUIBADILI KWELI YA MUNGU. JUU YA MPANGILIO SAHIHI WA MATUKIO YA MWISHO *(Escatological events under Chronology)* HAKIKISHA UNAPATA SOMO LANGU JINGINE LIITWALO *_"UFAFANUZI WA MATHAYO 24:1-51"_*  

*VITA VYA HAR-MAGEDONI*
Neno  Har-Magedoni linatokana na neno la kiebrania "Har Meghiddohn" au "Har-Magedone"  mahali patakapofanyika vita hii, kuna uwanda wa Megido uliotajwa karibuni mara 12 ktk Biblia,huu uwanda ni mashuhuri kwa Vita zaidi 200 za Israel na ushindi wao. Lakini neno hili Har-Magedon maana yake ni Mlima wa Megido unaoambatana na uwanda wa Megido ikijumuisha na uwanda wa Esdraelon,ulikuwa mji wa zamani ktk mpaka wa Israel. Iko hoja ya msingi kuwa hakuna mlima maeneo hayo,sasa bado neno *Har* halimaanishi mlima pekee even a hill bado kiebrania ni *Har* ,Lakini pia huojiwa kuwa hata kama ingeunganishwa na uwanda wa chini wa Yezreel bado  hautoshi kucontain yale majeshi yote yatakayohusika kwenye vita,Hii isitupe shida tujifunze usahihi wa vita hivi tutaelewa yote.

Jina hili Har-Magedon limejitokeza mara moja tuu ktk Biblia yaani
_Ufunuo 16:16_

*Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.*

Hii ni vita itakayohusisha serikali za kibinadamu kinyume na Mungu. Ni vita hii ndiyo itakayo komesha human governments (Dan 2:44) ambazo zimekuwa na desturi ya kutosubmit kwa utawala wa Mungu (Zab 2:2).  Kitu chenye mfano wa zile vita kuu za dunia ambapo kulikuwa na pande zilizo kinzana na mataifa mengine yalichagua kuwa upande upi,na kukawa na wasioshikamana na popote (NAM) wakati huu ikumbukwe itakuwa ni mwisho wa muhula wa pili (3.5years) wa utawala wa Mpinga Kristo (na nabii wa uongo) ,Mpango wa Mpinga Kristo utakuwa ni kuiangamiza  kabisa Israel,Na kutakuwa na mataifa (serikali za kibinadamu zitakazo unga mkono hiyo harakati), Kwa habari ya kile kitasa cha sita,ambacho ni maandalizi ya Harmagedon, *Ufunuo 16:12* tunasoma habari za hayo mataifa toka mashariki ambapo  ktk Biblia yenye lugha ya asili imetumia neno lenye maana ya *sun-rising* ushawishi kwa mataifa ya China,Japan,Urusi etc utatokana na zile roho za uchafu(evil trinity) zenye mfano wa vyura 🐸🐸🐸,Shetani ktk ukamilifu wa utatu wake wa uovu yaani Joka(Shetani),Mnyama wa kwanza(Mpinga Kristo) na Mnyama wa pili (Nabii wa uongo), Na tunaambiwa Mto mkubwa ule Frati utakaushwa kutengeneza njia ili kuruhusu majeshi ya hayo mataifa kupita(Tukio la Mungu kukausha mto huu,it is the sign that He is the One who will Orchestrate the War) .Vita ya Harmagedon itakuwa kiashiria cha ukomo wa dhiki kuu (Mathayo 24:21) ,Wakati majeshi hayo yaliunga mkono mpango wa Mpinga Kristo wa kuifuta Israel kabisa,na ktk uvamizi wao huo mkuu ambao haujawahi tokea na hapo ndipo tunaposoma mmbo ambayo yana CONTEXT ya Uyahudi pekee (Mathayo 24:16-22) ,Ndipo ambapo Yesu atayaongoza majeshi ya mbinguni kinyume na majeshi ya mataifa yaliyotii mpango wa Mpinga Kristo,ambayo yatakuwa yamejidhatiti kwa silaha nzito za kivita ambazo hata sasa zipo zinaendelea kuandaliwa. 💣🔫🚀🚁,KABLA YA KUTEKELEZA ADHMA HIYO NDIPO BWANA ATAINGILIA KATI IKUMBUKWE DHIKI KUU INAITWA PIA TAABU YA YAKOBO
Yeremia 30 : 7
*Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.*

Kutatokea *TETEMEKO*
🔴Lisilo na mfano,ktk historia ya matetemeko yote duniani hakutakuwa na tetemeko  lenye mfano wa hili.
🔴Mji mkuu utagawanyika mara tatu (unazungumziwa Yerusalemu)
🔴Na miji ya mataifa itaanguka (Hapa inatajwa   Mashariki ya kati na maeneo mengine ya Ulaya)
🔴Visiwa na milima kukimbia ni kielelezo cha nguvu ya uharibifu wa hili tetemeko (Collosal Magnitude of the Earth quake)

Nadhani kwa wakati huo  kipimo cha ukubwa wa tetemeko la ardhi *_Ritcher Scale_* hakitakuwa na namna ya kupima,kwani digits zilizo kwenye scale zitavukwa.Hii ni moja Silaha zitakazo tumiwa na majeshi ya Mungu yaani Tetemeko,Mawe makubwa toka mbingu(hailstones) yenye uzito wa ratri 7/pounds 100 sawa na Kilogramu 45.5 kila jiwe,yatakayoshuka kwa kani kubwa sana,moto na kiberiti(blimestone of fire/Sulphur),Radi,Magonjwa ya hatari pamoja na watu kuuana wenyewe wale wa upande wa adui,lakini nao watajua kuwa haya mapigo yanatoka kwa Mungu. (Ayub 38"22,23,Ezek 38:19,22,Hab 3:10,11,Zek 14:12,13.
Ikumbukwe kuwa majuma yale sabini ya Daniel yuu ya Israel (Daniel 9:24-27) yanatimia wakati wa ujio wa pili wa Yesu wakati wa ku-intervene hii *Armageddon* tangu mwaka 445 B.C ulipoandikwa waraka mkuu wa Artashasta Longimanus ,ndipo mwaka wa miaka 490 kwa zama za Wayahudi waliobaki unaangaliwa. Vita vya Harmagedon havitauacha ulimwengu ktk hali nzuri,itakayo hitaji muda wa kutosha kuisafisha maana damu itakuwa kama mito ya maji ,na kutakuwa na *karamu ya ndege* kushughulika na mizoga etc,na usafisho wa kuandaa *_Millenial Kingdom_*  , Na pia ikumbukwe vita hii sio ile ya Gog na Magog ambayo  tutaichambua ktk masomo yanayofuata.

*MAMBO YA MSINGI*
Kila uliyepata ujumbe huu,Sikutishii kwa neno lolote. ILA HAKIKISHA WEWE MPENDWA UOKOKE KWELI KWELI,NA UWE NA MAHUSIANO HAI NA MUNGU,UKIDUMU KTK KUJIFUNZA KWELI.  WAKO  WATU WENYE KIBURI CHA ELIMU,KWA KUWA WALIBAHATIKA KUSOMA VYUO VYA THIOLOJIA ULAYA,BASI WAKADHANI WANA KWELI YA MUNGU,HAKUNA KWELI YOTE YA MUNGU NJE YA ROHO MTAKATIFU KUPITIA NENO LAKE(KUTOKA KTK MAANDIKO MATAKATIFU),WALE AMBAO WAKO BIZE NA *_THEOLOGICAL SCHOOLS OF THOUGHT_*  NA WAKAJIKITA KUCHAGUA MTAZAMO UPI *_VIEW_* UNAWARIDHISHA BADO HAWATAKUWA SALAMA,WASIPO JIUNGANISHA NA MUNGU KWA ROHO YAKE/WAKE (1KOR 6:17) ILI AWAJULISHE KWELI YAKE NI IPI? NA SIO KUFAKAMIA TU TAARIFA  ZA KWENYE VITABU NA WEBSOURCES AMBAZO ZOTE ZINA PRESUPPOSITIONS ZAKE.

*_```ALL TRUTH IS GOD'S TRUTH,GOD'S WORD IS THAT TRUTH```_*

Mwl Proo( Prosper Kadewele)
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

Saturday, January 6, 2018

KICHO CHA BWANA!

*_KICHO CHA BWANA_*

Mwl Proo
0762879363 (whatsapp)
0718922662

Bwana Yesu asifiwe sana!. Karibuni tuzilishe roho zetu wana wa ufalme.

Kicho(Reverence) ina maana nyepesi ya hofu(Hofu ya Bwana/Fear of the LORD/honour/respect) na wa sio ile hofu ya kawaida tuijuayo,maana Mungu hakutupa roho ya woga(2Tim 1:7).

~*KWELI KUHUSU KICHO CHA BWANA*~

➖Huwezi kufanya ibada mbele za Mungu kama huna kicho cha Bwana,ibada nyingi zinafanyika,but haziwi mbele za Mungu,na ndio sababu haswa ya Mungu kutoonekana/kudhihirika.

Ayubu 15 : 4
*_Naam, wewe waondoa kicho, Nawe wazuia ibada mbele za Mungu._*

Waebrania 12 : 28 *_Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;_*

Daudi pamoja na kuwa ni mfalme,alicheza mbele za Bwana kwa namna ambayo haikuwa ya kawaida,ila sababu ni kwamba ilikuwa mbele za Bwana...

2Sam 6:21

*_21 Daudi akamwambia Mikali, Ilikuwa mbele za BWANA, aliyenichagua mimi juu ya baba yako, na juu ya nyumba yake, ili kuniweka niwe mkuu juu ya watu wa BWANA, juu ya Israeli; kwa hiyo mimi nitacheza mbele za BWANA._*

👆🏼👆🏼hiyo sentensi ya mwisho ''kwa hiyo nitacheza....'' katika NIV imeandikwa _*I will be even more undignified*_ yaani kwa kuwa yupo mbele za Bwana ktk sifa,ustaarabu wote tupa kule👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾
Ila ukiondoa kicho unazuia ibada mbele za Mungu

➖Mungu aliahidi kuwa kwetu sisi watu wa agano lililo bora zaidi atatia kicho ndani yetu

Yeremia 32 : 40
*_nami nitafanya agano la milele pamoja nao, kwamba sitageuka wala kuwaacha, ili niwatendee mema; nami nitatia kicho changu mioyoni mwao, ili wasiniache._*
Kwanza hii ni ahadi,hivyo waweza omba upewe kicho cha Bwana..Lakini Mungu anasema atatupa kicho ili tusimwache,hivyo kina kazi ya kukushikilia  usitoke ktk hali ya neema.

➖Namna pekee ya kufanya Mungu akuangalie,ni wewe kuishi ktk Kicho cha Bwana....

Isaya 66 : 2 *_..........lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu._*

➖Namna peke ya kuondokana na mazoea(getting used to) ktk wokovu na mambo ya Mungu,ni kwa wewe kuishi katika Kicho cha Bwana...Mungu hatakuja kuzoeleka kwa kiwango cha kumfanya kama mwanadamu,nilikuta sehemu wanalazimisha Mungu awe wa kawaida na hivyo wanamwita majina kama *_Mshua/Mshikaji_*🙊 ni kweli Mshikaji ni rejesta ya mtaani ina maana hiyo ya rafiki(Isay 41:8,Yohan 15:15) na sisi tumeitwa rafiki,lakini sio kwa kiwango cha kumwita Yesu mshikaji. Kuna kitu tu  *_Tཽeཽtཽrཽaཽgཽrཽaཽmཽmཽaཽton_* ,hii ni adabu ambayo wayahudi waliishika juu ya jina la BWANA,yaani hata ule uandishi wa jina YHWH waliandika wakiwa wamejitakasa sana,na pia kukosa vowels zaidi ya ule utaratibu wa Lugha yao,lakini ilikuwa kuepusha kulidharau jina... yaani ni kama una baba yako anaitwa Kenedy Lwambo. Sasa wewe mtoto ukamwita babaako kwa jina lake "Wewe Kenedy" utaenda kazini kesho?🙊 Can you do that to your earthly father?

Kolosai 2

*_12 Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka._*

➖Namna pekee ya kubaki kama mtu mwenye uheri/baraka siku zote,ni kudumu ktk Kicho cha Bwana...

Mithali 28 : 14
*_Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara._*

Mhubiri 8 : 12  *_Ajapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia, akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake;_*

➖Kila aliyeokoka,ni  lazima aende ktk kicho cha Bwana

Nehemiah 5 : 9b
*_..... je! Haiwapasi ninyi kwenda katika kicho cha Mungu wetu, kwa sababu ya mashutumu ya makafiri adui zetu?_*

➖Kicho cha Bwana ni kitakatifu,na kwa sababu hiyo lazima tutaweza kutfautisha mwenye kicho cha Bwana,na mkristo mwenye nidhamu ya woga ambaye tukimkuta maeneo fulani ya kwao hana ushuhuda,watu wanahoji na huyu kaokoka?

Zaburi 19 : 9
*_Kicho cha Bwana ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za Bwana ni kweli, Zina haki kabisa._*

➖Siku kwa siku ,Kicho cha Bwana kinapaswa kuongezeka ndani ya mwamini binafsi na katika kanisa,Kuishi miaka 30 ktk wokovu sio kigezo kwako uondoe kicho.. maana radha ya maisha ya wokovu huondoka kabisa,kama mtu ataondoa kicho

Matendo ya Mitume 9 : 31
*_Basi kanisa likapata raha.............,likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu._*

➖Kila anayemtumikia Mungu lazima atumike ktk kicho cha Bwana. Huwezi ukafanya huduma yenye kuzaa matunda yanayokaa,na wote tukatazamao tukasema huyu mtu anatumika ktk kweli tusipokiona kicho cha Bwana. wako watumishi wengi ambao hawamtumikii Shetani,bali ni Mungu wa kweli, *lakini sababu wamekiondoa kicho* wanatembea ktk makosa mengi ambayo watu huwadhani ni mitume na manabii wa uongo.

Zaburi 2 : 11  _*Mtumikieni Bwana kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka.*_

➖Ni wenye kicho cha Bwana,ndio wanaojibiwa maombi.Kicho cha Bwana maana yake Uchaji Mungu,Yesu akiwa ktk maisha yake ya Duniani alijibiwa kwa vile alivyokuwa mchaji Mungu

Waebrania 5 : 7  _*Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;*_

NDUGU MPENDWA,KICHO CHA BWANA KINAKUFANYA KUWA MTU HALISI,UKITAKA KUJITAMBUA WEWE KIUHALISIA WAKO,ANGALIA MAMBO UNAYOYAFANYA UKIWA PEKE YAKO,YALE NDIYO WEWE HALISI,NA SIO VITU UNAVYOVIFANYA UKIWA UMESHIKA MAIKROFONI🎤,KANISANI,LAKINI KICHO CHA BWANA KINAFANYA MPAKA UKIWA PEKE YAKO UNAJUA KUWA MACHO YA BWANA 👁👁 YANANIONA HATA HAPA (MITHALI 15:3,11).

KWANINI HADI NDOA ZA WALIOOKOKA ZINA MIGOGORO? JIBU NI MOJA WAMEONDOA KICHO, KICHO CHA BWANA KINGEKUFUNDISHA KUWA YOUR HORIZONTAL RELATIONSHIP AFFECTS THE VERTICAL RELATIONSHIP. YAANI HUWEZI KUMZABA MAKOFI MKEO👋🏾👋🏾 HALAFU MIKONO HIYOHIYO ISIYOTAKASWA UKAIINUE MBELE ZA MUNGU🙌🏽. HUWEZI KUWA UNAGOMBANA NA WAPANGAJI WENZAKO KISA WALICHOTA MAJI KWENYE NDOO YAKO,MKIWA MMEJERUHIANA KWA MANENO,THEN UNAJIVISHA NGUO NA KWENDA IBADA,OUR HORIZONTAL RELATIONSHIP MATTERS A LOT,YESU ALIPOSEMA UKITOA SADAKA,ILA UKAKUMBUKA NDUGU YAKO ANA NENO NA WEWE,IACHE SADAKA UKAPATANE NAYE THEN UJE UITOE,ALIKUWA ANATHIBITISHA UKWELI HUU. KICHO CHA BWANA,KITAKUPA KUTAFUTA KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE. WALE WANAOKUCHUKIA KWA WOKOVU WAKO,HIYO HAINA MADHARA (waombee tuu)

MUNGU MARA NYINGI ANATUSHANGAA TUNAPOKOSA KICHO,TUNAKUWA KINYUME NA UKIRI WETU,NA HIVYO ANATUHOJI KI WAPI KICHO CHANGU?

Malaki 1 : 6
_*Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? ~Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi?~ Bwana wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani?*_

Mungu akusaidie,kila mmoja uanze kutembea ktk kiwango kipya cha kicho,utamhofu Mungu wala sio wanadamu wafao..

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

Monday, January 1, 2018

CHOMBO KIMFAACHA BWANA

*CHOMBO KIMFAACHO BWANA (2Timotheo 2:21)*

_Mwl Proo_
0762879363

Shalom Aleichem!✋🏼

Nawasalimu kwa jina la Yesu.

Leo tujifunze kuhusu vyombo,mifano ni ile ambayo kila mtu ataielewa na ni dhahiri ktk maisha yako hapo nyumbani.

*_TUJIFUNZE AINA ZA VYOMBO_*

2 Timotheo 2 : 20 *_Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina._*

Ufunuo wa Yohana 18 : 12
*_.............. na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari_*

Tusomavyo ktk maandiko  hayo ndivyo ilivyo,tukiingia nyumbani kwenu leo,tutakuta vyombo tofautitofauti,kuna utofauti wa material iliyotumika kukitengeneza,rangi n.k na mara nyingi material iliyotumika inafanya chombo kiamriwe aina ya matumizi,na aina ya matumizi inakipa chombo kuwa cha heshima au kisicho na heshima; Themos ya chai haitalingana heshima na kopo la bafuni/kuogea.

Agano la kale ambalo ni kivuli cha mema haya ya sasa,linatoa picha nzuri kuhusu vyombo *_NA KILA CHOMBO KINAWAKILISHA MAISHA YA KIROHO YA VIWANGO FULANI_*

1.SIO VYOMBO VYOTE VILIFAA KWA UTUMISHI WA MUNGU

>Madhabahu ilihitaji chombo cha mawe,Mungu hakutaka chombo cha chuma ktk kuijenga madhabahu

Kumbukumbu la Torati 27 : 5
_*Na huko umjengee madhabahu Bwana, Mungu wako, madhabahu ya mawe, usitumie chombo cha chuma juu yake.*_

>Vyombo vya hazina ya Bwana havikutakiwa kuwepo vya miti,bali vya shaba,chuma n.k

Yoshua 6 : 19
*_Lakini fedha yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na chuma, ni vitakatifu kwa Bwana; vitaletwa katika hazina ya Bwana._*

MUNGU ALIWEKA HESHIMA TOFAUTI YA VYOMBO

Warumi 9 : 21
_*Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?*_

KWA MFANO CHOMBO CHA MTI NA CHA UDONGO VILIKUWA NA TOFAUTI KUBWA KIHESHIMA. KAMA MTU MWENYE KISONONO ANGEGUSA CHOMBO CHA UDONGO BASI MAELEKEZO YA TAURAT NI KUKIVUNJA,ILA AKIKIGUSA CHA MTI BASI MNAKIOSHA TU

Mambo ya Walawi 15 : 12
*_Na chombo cha udongo ambacho amekigusa mwenye kisonono, kitavunjwa-vunjwa; na kila chombo cha mti kitaoshwa majini._*

LAKINI PIA CHOMBO CHA UDONGO KILIKUWA NA SIFA YA KUHIFADHI KITU KWA MUDA MREFU,TENA HAKIPATI KUTU,SO KILIFAA FOR PRESERVATIVE PURPOSES

Yeremia 32 : 14
_*Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Twaa hati hizi, hati hii ya kununua, hati hii iliyopigwa muhuri, na hii iliyo wazi pia, ukazitie katika chombo cha udongo, zipate kukaa siku nyingi.*_

2.SIO VYOMBO VYOTE VILIFAA KTK UTOAJI MAHARI
Kulikuwa na vyombo vyenye heshima ya kutumiwa ktk posa,na vingine havikufaa

Mwanzo 24 : 53 *_Kisha huyo mtumishi akatoa vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, akampa Rebeka; na vitu vya thamani akampa nduguye na mamaye pia._*

*AINA MBALIMBALI ZA VYOMBO VIFUATAVYO VINAASHIRIA HALI MBALIMBALI ZA MAISHA YA WATU_*
Wako watu walifanywa vyombo vizuri vya kufaa,na vya kupata heshima lakini waliyaharibu maisha yao kiroho na ile sifa ikabadilika

Maombolezo 4 : 2  _*Wana wa Sayuni wenye thamani, Walinganao na dhahabu safi, Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo, Kazi ya mfinyanzi*_

▶CHOMBO KISICHO NA KIFUNIKO

Kifuniko huwakilisha Roho Mtakatifu(Isaya 30:1)
Viko vyombo hata nyumbani kwenu ambavyo vikiisha poteza kifuniko,havifai tena,kama kilikuwa kinawekewa maji ya kunywa(ndani ya friji) basi kitapelekwa kuwekewa chumvi jikoni na vingine hutupwa

Hesabu 19 : 15
*_Na kila chombo kilicho wazi, kisichofungwa na kifuniko, ni najisi._*

👆🏼Huyu aliyekosa kifuniko,hawezi kujizuia,kila uchafu wa dunia humpata asiweze kuwa chombo cha kumfaa Bwana.

▶CHOMBO KIPYA
Chombo kipya,kina heshima yake,na halitafanyishwa kaI zile ordinary,huenda kikasubiriwa shughuli maalum ili kianze matumizi nyakati hizo,Elisha alihitaji chombo kipya ili aponye maji yenye kuzaa mapooza

2 Wafalme 2 : 20 *_Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea._*

Mungu kuna baadhi ya utumishi anahitaji akufanye chombo kipya ndipo utamfaa

Isaya 41 : 15
*_Tazama, nitakufanya kuwa chombo kikali kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha milima, na kuisaga; nawe utafanya vilima kuwa kama makapi._*

👆🏼Chombo Kikali(sharp) kuna watu maisha yao yamekuwa butu(dull) mtu amezoelea dhambi mpaka akitenda hashtuki tena,alikuwa huko nyuma akisema uongo anakosa raha mpaka atubu lakini sasa amekuwa butu(Chombo butu kisicho kikali,kinawakilisha dhamiri iliyokufa nafsini mwa mtu) Sasa Mungu anataka chombo kikali-kipya kimfae kwa kusudi lake

Isaya 28 : 27
_*Kwa maana kunde zile hazipurwi kwa chombo kikali, wala gurudumu la gari halipitishwi huko na huko juu ya jira ile, bali kunde zile hupurwa kwa fimbo, na jira ile kwa ufito.*_

▶CHOMBO KILICHOVUNJIKA
Bila shaka ukikagua ktk kabati unaweza kuta kuna chombo cha udogo au cha  kioo,either kina nyufa au kimevunjika,Sifa kuu ya chombo kilichovunjika ni kusahaulika. Yaani vumbi,buibui walikifanya makazi yao,Chombo kilichovunjika,huwakilisha watu wasiojitengeneza mioyo kwa Bwana,wasio na toba,wanakubali kuishi na uovu,wanapewa nafasi ya kutubu lakini hawataki(Ufunuo 2:21)

Zaburi 31 : 12 - _*Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa; Nimekuwa kama chombo kilichovunjika.*_

▶CHOMBO KISICHOPENDEZA

Viko vyombo ambavyo huenda bado vinatumika lakini kwa kuwa havipendezi havitapewa heshima,ya kuwekwa  pahala pazuri pa kuonekana,huenda kikafichwa stoo kwenye kila takataka ambazo zinadhaniwa kuhitajika bado. Kwa mfano kinu cha kutwangia,hakitapewa heshima ya kuwekwa sebuleni,kitawekwa ua wa nje kama ni jikoni kwenywe kona au stoo.

Yeremia 48 : 38
_*kwa maana nimevunja Moabu kama chombo kisichopendeza, asema Bwana.*_

Hosea 8 : 8
_*Israeli amemezwa; sasa wamo miongoni mwa mataifa kama chombo kisichopendeza.*_

▶VYOMBO VIPENDEZAVYO

Nahumu 2 : 9  *_Chukueni nyara za fedha; Chukueni nyara za dhahabu; Kwa maana ni akiba isiyoisha, Fahari ya vyombo vipendezavyo._*

Hosea 13 : 15
_*.............yeye atateka nyara hazina ya vyombo vyote vipendezavyo.*_

VIKO VYOMBO HATA MACHONI PA BWANA NI VYA KUPENDEZA,VIATU HATA VIKIWA VIPYA HAVIPEWI HESHIMA KUWEKWA JUU KWENYE DRESSING TABLE,HAVIPENDEZEI. LAKINI UNAONAJE KWA HABARI YA TV🖥 UKILINGANISHA NA KINU KIPI NI CHOMBO CHA KUPENDEZA HATA KUPEWA HESHIMA KIKAE SEBULENI?

▶VYOMBO VITUPU
Kuna watu ingawa wana muda mrefu ndani ya wokovu,lakini vyombo vitupu,mkimpa hata madhabahu dakika 10 hana cha kuzungumza,anaweza jitetea sio huduma yake,lakini umekosaje ushuhuda   wa matendo ya Mungu wakati unaye Mwana,kila aliye na Mwana hakosi huo ushuhuda wa wema wa Mungu,tatizo hapo ni chombo kuwa kitupu,na ndio maana hata ukikutana na mtu,unagundua ana shauku ya kusikia habari za Yesu,ila unamwelekeza pengine,maana wewe ni chombo kitupu

PIA VIKO VYOMBO VYA KUDHARAULIWA,VYOMBO VYA ANASA,VYOMBO SAFI VYA THAMANI N.K N.K (Yer 22:28,51:34,25:34)

Yeremia 14 : 3 - _*Hurudi, na vyombo vyao ni vitupu; Wametahayarika na kufadhaika, Na kuvifunika vichwa vyao.*_

~*_KIPO CHOMBO  KINAMFAACHO BWANA_*~

2 Timotheo 2 : 21
_*Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.*_

*NB:-*
KUNA MAMBO UNAPASWA KUYAACHA,KUYAONDOA ILI UWE CHOMBO CHA KUFAA

Katika 2Timotheo 2:21 Anakijadili chombo kimfaacho Bwana

🔴Basi ikuwa mtu amejitakasa kwa kujitenga,neno takasa maana yake set apart,weka wakfu kwa ajili ya .......... Sasa mstari huu unajadili wale akina Himenayo na Fileto wenye mafundisho potofu yaliyoenea kama donda ndugu,lakini anasema mtu akijitakasa kwa kujitenga na mambo hayo ya kina Himenayo na Fileto(ambao leo hufananishwa na uchafu wote wa dunia unaopingana na maisha matakatifu ....

Huyu mtu atakuwa chombo cha kupata Heshima. kama ulikuwa chombo cha mti Bwana  atakufanya cha fedha au dhahabu
Kwa maana hiki ndicho kimfaacho Bwana *KIMETENGENEZWA*
kwa kila kazi njema.

NDUGU WAPENZI MUNGU HANA UPENDELEO LAKINI KUNA WATU WAMEJITAKASA MAISHA,WAMEJITENGA NA UCHAFU KWA HIYO HUDHANIWA MUNGU KAWAPENDELEA WAMEPEWA KARAMA NYINGI(NUMBER OF RESPONSIBILITIES) KTK UFALME YAANI NI KAZI TELE,WANAFAA KILA MAHALI,KILA HUDUMA ANAYOIFANYA IMEJAA UTUKUFU,MNALINGAMA UMRI,MLIKUWA WOTE FELLOWSHIP,LAKINI LEO HII MWENZIO ANAHUDUMIA MAELFU  YA WATU KILA WAKATI,NAFASI HIZO HAJAJITENGENEZEA,LAKIJI KWA KUWA ALITENGENEZWA NA MUNGU,ANAFAA KWA KILA KAZI NJEMA,ANAANA KUIONA FUTURE YAKE,MAISHA YAKE YANAENDA KWA MWENDOKASI KUIKABILI DESTINY YAKE,KWA UMRI WAKE MDOGO WA MIAKA 25 AMEKWISHA INFLUENCE(POSITIVELY) HUMAN RACE,SASA UNATAKA KUWA CHOMBO KUMFAACHO  BWANA? JITENGE NA DUNIA,LAZIMA UWE SELECTIVE,SIO KILA KIPINDI CHA TV KINAKUFAA WEWE CHOMBO CHA BWANA,SIO KILA MAVAZI YA FASHENI ZOTE ZINAMFAA CHOMBO CHA BWANA

Isaya 52 : 11  _*Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana.*_

1 Samweli 21 : 5 - *_Naye Daudi akamjibu kuhani, akamwambia, Hakika tumejitenga na wanawake siku hizi tatu; napo nilipotoka, vyombo vya vijana hawa vilikuwa vitakatifu, ingawa ilikuwa safari ya  sikuzote; basi leo je! Vyombo vyetu havitakuwa vitakatifu zaidi?._*

Mithali 25 : 4
*_Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji;_*

MIMI NIMEFANYA MAAMUZI YA KUWA CHOMBO KIMFAACHO  BWANA, KWA HIYO KUNA MAVAZI SIVAI,KUNA MANENO SITAMKI(NILIMSIKIA MPENDWA FULANI KILA SAA ANATAMKA ~*_kudadadeki_*~ SIJUI MAANA YAKE LAKINI NAHISI HALIFAI, KUNA VIPINDI VYA TV NILIVIKATAA, KUNA MOVIES📼📀📺,NILISEMA NO, KUNA MIZIKI NILIIKATAA (SECULAR MUSIC ZOTE), UKIANZA WIMBO WA YA MOTO BAND AU DIAMONDI KWENYE 📻REDIO YANGU SIUPOTEZEI KAMA VILE ETI NIPO BIZE, UKIANZA NAUZIMA AU NATYUNI KWINGINE, SWALA LA ZIKIPIGWA KWA DALADALA NI CASE TOFAUTI, NAFSI YANGU IMEJENGWA NITAUSIKIA, SITAUSIKILIZA. KUNA MAGRUPU YA WHATSAPP NIMELEFT HAYANA KITU CHA KUNIJENGA MIMI KAMA CHOMBO CHA  BWANA CHA KUPATA HESHIMA (KAMA LIKIWA SI LA KIROHO BASI LIWE LA KIJAMII LISILO NAJISI), UMEUNGWA KWENYE GRUPU LA WHATSAPP LA KUTUMA VITU VICHAFU WALA HAUTAKI KULEFT(KULEAVE) WEWE NI CHOMBO KISICHOFAA. TENGENEZA NJIA NA MATENDO YAKO,NA UJITENGE UMFAE BWANA KATIKA JINA LA YESU.

MBARIKIWE
Mwl Proo
0762879363 (whatsapp)
0718922662(calls/texts only)

alltruth5ministries@gmail.com

TAARIFA MUHIMU

Shalom

Ndugu wapendwa, kuna ambao wanaona narudia masomo, nafanya hivyo purposely, maana kuna walioipakua app wakakuta masomo 25 tu, hivyo narudia ya zamani, maana nikiyaweka kwa upya ndipo na wao wanayapata

MUNGU ANAJALI; ATAINGILIA KATI!

*MUNGU ANAJALI; ATAINGILIA KATI*
*_(God is concerned with your issues, before they get worse; He will intervene)_*

```By Mwl Proo```
0762879363
0718922662

Bwana Yesu apewe sifa zote!🙋🏽

Nasikia ujasiri ktk Mungu huyu aliyejifunua kwetu kwa njia ya Yesu Kristo (Ebrania 1:1-3),
Neno lake ni amini na kweli, akisema Yeye basi haliangauki lolote lililo la Neno lake (2Falme 10:10),na hata kama akinena ikapita miaka mia 800 au elfu bado atalitenda kama alovyosema (Omb 2:17). Mwamini Mungu tuu utajua ya kuwa Yeye Mungu, kamwe hasemi uongo,(Soma Tito 1:2, Hes 23:19, Ebra 6:18).

SASA BWANA AMEKUONA WEWE ULIYELEMEWA, NA UNAELEKEA KUVUNJIKA MOYO JUU YA YALE YANAYOKUSONGA PANDE ZOTE, WEWE AMBAYE UNAFANYA HUDUMA KWA UAMINIFU LAKINI MAMBO YAKO *_SO TIGHTY_*, YUKO MUNGU ANAYEJALI KABLA MAMBO HAYAJAWA MABAYA ZAIDI ATAINGILIA KATI. NA HAYAWEZI KUKUHARIBIKIA WAKATI YUPO MUNGU (IT CAN'T GET WORSE WITH GOD).

MUNGU HUYU TUNAYEMUABUDU ANA SIFA MBILI ZA MSINGI, HE IS A TRASCENDENTAL GOD (MUNGU AMBAYE KWA SABABU YA UKUU WAKE AMETENGWA YUKO MBALI HE IS AWAY THERE, ILI AKAE KAMA MUNGU MILELE). LAKINI MUNGU HUYU NI MUNGU ALIYE KARIBU SANA (HE IS AN IMMANENT GOD) YUKO KARIBU(YEREMIA 23:23, ISA 55:6) HE IS CONCERNED ABOUT ISSUES IN OUR DAILY LIVING, AND THAT IS JEHOVAH-GOD 💪 🏾

TWENDE KATIKA MAANDIKO

KUTOKA 3:7

Kutoka 3 : 7
*_Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;_*

👆🏼1.NIMEYAONA MTESO YAO
2.NAYAJUA MAUMIVU YAO (Katika NIV pameandikwa *_For I am concerned about their suffering_*)
Kamwe usidhani kuwa Mungu amekupotezea, huyu aliyeamua kukuchora viganjani, kuta zako yaani mahitaji and all cares and burdens of life yako mbele zake daima ( Isaya 49:15-16). Mungu anaona fahari kukutetea, Na hiyo mizigo inayokujia itapungua uzito wake mara utakapo tambua yuko Mungu atuchukuliaye mzigo wetu wote siku kwa siku (Zaburi 68:19).

SASA TURUDI KWA ANDIKO, KUMBE WAKATI WAISRAEL WANATESWA SANA CHINI YA UTAWALA WA FARAO MWINGINE ASIYEMJUA YUSUFU, YALE MAUMIVU YALIYOSABABISHWA NA WALE WASIMAIZI WA KAZI, KUJENGESHWA MAPIRAMIDI, KUFYATULISHWA TOFALI BLA KUPEWA NYASI ZA KUFUNIKIA, KULIKOPELEKEA TOFALI KUVUNJIKA, NA IKAWAGHARIMU KURUDIA KAZI HIYOHIYO TENA. MUNGU YULE AYASHIKAYE MAAGANO, ALIKUWA ANAONA, KAMA AMBAVYO ANAKIONA KILIO CHAKO CHA AJIRA NA KILE CHA NDOA NA KILE CHA AFYA YAKO ILIYOTESWA SANA. MUNGU; KABLA MAMBO HAYAJAHARIBIKA ALIINGILIA KATI, NA SIKU ILE AMBAYO ALIKUSUDIA KUWATOA, HAKUKUWA NA WA KUZUIA *SIKU ILEILE* (KUTOKA 12:51).

*_51 Ilikuwa siku ile ile moja, BWANA akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri kwa majeshi yao._*

KAMA AMBAVYO KWAKO IKO SIKU MOJA TU, MUNGU ATAINGILIA KATI NA ITAKUWA NI KAMA MTU AOTAYE NDOTO 😴💤(Zaburi 126:1-2).

TUSOME KISA CHA PILI HALAFU TUENDELEE KUUFAIDI UKWELI WA MUNGU.

Mathayo 1

*_19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri._*
*_20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu._*

👆🏼👆🏼😄😄MUNGU ANAYEJALI HATAACHA MAMBO YAKUHARIBIKIE. MARIAMU KOSA LAKE NI NINI? UJAUZITO UMEINGIA BILA YEYE KUCHAKACHUA UBINTI WAKE, SASA HUYU MCHUMBAAKE ALIKUSUDIA KUMWACHA KWA SIRI (ILI ASIMWAIBISHE, PIA KWA SHERIA YAO YA WAKATI HUO, ILIPASWA AKIJULIKANA KUSHIKA MIMBA HALI MCHUMBAAKE HAJAMKARIBIA, BASI APIGWE MAWE AFE). LAKINI NA HATA HIYO BADO SIO SOLUTION, MUNGU ANAYEJALI HAKUMWACHIA MARIAMU KAZI YA KWENDA KUJIELEZA NA KUJITETEA KWA MUMEWE MATARAJIWA. MUNGU ALIPOONA WAZO LA KUACHWA KWA MARIAMU AKAENDA KUUBEBA HUO MZIGO. MARIAMU HAKUFUNUA KINYWA, MALAIKA WA MUNGU AKATUMWA FASTAAAAA. AMINI AMIN NAKUAAMBIA HIYO ISHU UMEZUSHIWA OFISINI KWAKO ILI UTUMBULIWE, YUKO BWANA MKUBWA YESU KRISTO ATA-INTERVENE NAWE HUTAJITETEA MWENYEWE, GHAFULA MARIAMU ANASIKIA HODI🚪, KUFUNGUA ANAMKUTA MUME ALIYEBAMBIKIZIWA UJAUZITO ANAKUJA KUMCHUKUA TENA KWA AMANI KABISA, KWA KUWA YUPO MUNGU ANAYEJALI.

NDUGU WAPENZI, WENGI WAMETOKA KWENYE WOKOVU, WAMEJIHARIBU UHUSIANO WAO NA MUNGU PALE WALIPOJARIBU KUJITETEA MAGUMU YALIPOWAKUTA, YUKO MUNGU AMBAYE WEWE UKIPATA MAUMIVU YEYE ANAVAA *_KANIKI_*. KUMBUKA HUYU NDIYE MUNGU ALIYEJIVIKA ADHAMA NA NURI KAMA VAZI(ZABUR 104:1-2) SASA PAMOJA NA UTUKUFU HUO,WEWE UKIUMIA NA KUTESEKA YEYE ANAVAA KANIKI😰

Yeremia 8 : 21
_*Kwa sababu ya maumivu ya binti ya watu wangu nimeumia mimi; nimevaa kaniki; ushangao umenishika.*_

👆🏼MUNGU HAWEZI KUKUACHA KTK MAUMIVU YAKO, MAANA NAYE ANAUMIA PAMOJA NA WEWE. JE HUKUJUA, HUKUSIKIA? KUWA WEWE NA MUNGU MNASHEA ROHO MOJA, YAANI UMENYWESHWA ROHO WAKE NA UMEUNGWA NAYE KWA ROHO YAKE (1COR 6:17).

*_17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye._*

NA KWA SABABU HIYO, KAMWE HAYATAACHWA MAMBO YAKO YAHARIBIKE KABISA(THEY CANNOT GET WORSE). UTAKUWA UMESHAUONA WOKOVU WA BWANA, PALE ULIPOTAKA KUJITETEA KWA NAFASI YA MUNGU NDIPO ULIKOSA NA KUJIHARIBIA MBELE ZA MUNGU. HUNA HAJA YA KUCHAKACHUA MNGOJE BWANA.
MIEZI MICHACHE ILIYOPITA NILIENDA MKOA WA MBALI NA NINAKOFANYA KAZI, NIKIWA NAENDESHA SEMINA SIKU YA PILI TU NIKAAMBIWA HUKO OFISINI KUNA  UHAKIKI WA WATUNISHI HEWA, NA KWA KUWA SIKUWA NA RUHUSA MAALUM, ILIKUWA LAZIMA NIHESABIKE  KUWA HEWA, AU TUFANYE UCHAKACHUZI YAANI TUPANGE DILI  NA MKUU WANGU LABDA IANDIKWE BARUA YA FORGERY  TUDANGANYE LABDA NILIPATWA NA DHARURA KAMA MSIBA ETC, LAKINI  NILIPOPATA TAARIFA HIYO USIKU HUO NIKAMWAMBIA MUNGU HILI NI SIZE YAKO. SITATHUBUTU KUFANYA UDANGANYIFU WOWOTE, ITAKAPOBIDI KUTUMBULIWA NA NITUMBULIWE. KESHO YAKE NAMALIZA KUHUDUMU MADHABAHUNI NAPIGIWA SIMU KUWA MUDA WA UHAKIKI UMEONGEZWA.

YAKITOKEA MAMBO MAKUBWA MAGUMU YANAYOTAKA EITHER UMKOSEE MUNGU ILI UFANIKIWE, HUO NI WAKATI WA KUMWAMBIA MUNGU *_THIS IS YOUR SIZE_*, BAADA YA HAPO KAA UKIMTAZAMIA MUNGU ANAVYOICHEZA HIYO GAME!

JIFUNZE KWA MFALME ASA, ALIPOONA VITA INAMJIA YEYE AKAMPAMBANISHIA MUNGU, AKAMWAMBIA MUNGU UNAONA HII VITA. TAFADHALI SANA MUNGU *_ASIKUSHINDE MWANADAMU_*

2 Mambo ya Nyakati 14 : 11
*_Naye Asa akamlilia Bwana, Mungu wake, akasema, Bwana, hapana kuliko wewe aliye wa kusaidia, kati yake yeye aliye hodari, na yeye asiye na nguvu; utusaidie, Ee Bwana, Mungu wetu; kwa kuwa sisi twakutegemea wewe, na kwa jina lako tumekuja juu ya jamii kubwa hii. Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu wetu, asikushinde mwanadamu._*

Waebrania 6 : 15
_*Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.*_

Luka 21 : 19
_*Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.*_

Mika 7 : 7 
_*Lakini mimi, nitamtazamia Bwana; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia.*_

HALELUYA, SASA KATIKA MAMBO YAKO, JIFUNZE KUMTAZAMIA BWANA MAANA NI LAZIMA ATATENDA TU.

KWA TAARIFA YAKO, KILA AMBAYE UNASOMA UJUMBE HUU, MUNGU AMEKUANDALIA MAMBO MAKUBWA SANA NA UKUU HUKO MBELE (1KOR 2:9), JITAHIDI SANA USICHAKACHUE MAANA MBELE YAKO KUNA MAMBO MAZURI. SIRI PEKEE YA KUIJUA NI HII, UNAPOENDELEA KUMNGOJA BWANA KWA AHADI ZAKE, UISHIKE NJIA YAKE

Zaburi 37:34

*_34 Wewe umngoje BWANA,Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Wasio haki watakapoharibiwa utawaona._*

👆🏼👆🏼WAKO WANAWAKE WENGI WAMEMNGOJA BWANA AWAPE NDOA ZAO, SUBIRA IKAPUNGUKA, WAKAAMUA LIWALO NA LIWE (WHAT WILL BE WILL BE), WAKAAMUA KUZAA KWANZA MTOTO NA YEYOTE. OOOH ILIBAKIA KIDOGO SANA UIINGIE ILE NDOA YA UTUKUFU MKUU. UKIISHA CHAKACHUA BARAKA ILE HAITAKUJIA KWA UTUKUFU ULE ULE, ITAKUJA YA KUUNGAUNGA HALI IMEPUNGUKA UTUKUFU.

BWANA AKUPE NEEMA, YA KUMNGOJA YEYE MAANA NI MUNGU ANAYEJALI, UWE NA UHAKIKA ATAINGILIA KATI TUU.

MBARIKIWE SANA!✋🏼

alltruth5ministries@gmail.com
Mwl Proo
0762879363
0718922662

JITAJIRISHE KWA MUNGU

*_JITAJIRISHE KWA MUNGU_*

Mwl Proo
0762879363
0718922662

Halellujah!!
Neno la Mungu ni zuri,mimi linanibariki hata kabla sijaandika chochote,lipe nafasi ya kwanza ili liwe linafaa,kuna wakati nilikuwa nakaa nje ya nyumba yetu 💺nasoma Biblia,lakini kwa sababu ya utamu wa Neno 😋📖,nikawa nakatisha kusoma nasimama narukaruka kwa furaha💃🏼kabla ya kuendelea tena kusoma. Sasa usipoona utamu unaposoma Neno ni dalili ya kuwa kuna shida kwenye  swala la unyofu wa moyo,maana neno linamfaa mnyofu wa moyo(Mika 2:7b) ,Ok sio somo letu la leo hilo.

Leo nimejaa moyoni siri hii,KUJITAJIRISHA KWA MUNGU.

Wako watu hawakujua namna ya kumtaka Mungu na nguvu zake(Zaburi 105:4), yaani walipostareheshwa na BWANA kwa kupata kazi nzuri,akawa Managing Director sijui General manager yaani anaogelea pesa💵💴💶💷💰🏧,bajeti yake ya lunch ni zaidi elfu 40 kwa siku, ofisini kuna vinywaji vyote vizuri🍷🍹🍸🍾kila ukigeuka una unafungua jokofu. Sasa wengi ktk mazingira hayo hawakumbuki kuwa baraka hizo hazipo kukusahaulisha Mungu. Ukiwa ni wa standards hizo *_ILI USIMKOSE MUNGU NA ADUI ASIKUPIGE_*, TUMIA NAFASI KAMA HIZO KUJITAJIRISHA KWA  MUNGU.

*Luka 12 : 21*

*_Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu._*

SASA MTU OFISI IMEKUTENGEA PESA NYINGI KAMA MEAL ALLOWANCE,NAWE BADALA YA KUTUMIA HUO MWANYA KUUTEKA UFALME WA MUNGU(MATH 11:12,LUKA 16:16) KWA BARAKA ZIMEKUWA JARIBU YAANI HAPO HATA KUJITOA UFUNGE KWA MAOMBI ILI ILE LUNCH ALLOWANCE UIPELEKE MARA MOJAMOJA IKAFANYE KAZI YA MUNGU,UNAJUA KABISA KANISANI KWENU KUNUNUA MICROPHONE🎤 YA ELFU 80,WANACHAGISHANA WEEE👌🏽POVU LAWATOKA WATUMISHI MPAKA WANATOA VITU VIPIGWE MNADA,ILI INUNULIWE MAIKI AMBAYO WEWE NI PESA YAKO YA LUNCH SIKU MOJA TU. HAZINA YAKO UMEIWEKA KWA MUNGU WAKO TUMBO(MATH 6:19-21)

*Wafilipi 3 : 19*
*_mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani._*
KWA KUKOSA KIASI UMEISHIA TU KUPATA KITAMBI CHA AJABU AJABU UKIJANADI UMEBARIKIWA BADAE SANA UNAPOANZA KUSUMBUKA NA KISUKARI NA PRESHA ZA AJABU NDIPO UNATAKA KUMKUMBUKA MUNGU,SASA HIZO NDIZO TABIA ZA WATU WAJILIMBIKIZIAO KILA KITU ,WASIJITAJILISHE KWA MUNGU.
KAMA UTAWEZA KUTUMIA ULIYONAYO KUJITAJIRISHA KWA BWANA,UTAKUWA NA MWISHO MZURI WA AMANI,HATA UZEE WAKO UTAKUWA WA BARAKA NA UJANA WAKO UTAREJEZWA (ZABURI 103:5)

*Zaburi 37 : 37*

*_Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani._*

```JE! UNA AFYA NJEMA?```
wakati upo na afya safi kabisa,hakuna magonjwa yanakusumbua,huo sio wakati wako wa kui-enjoy dunia kwa kula maisha tuu bila kujitajirisha kwa Mungu,afya yako idhabihu kwa Mungu,yaani tumia huo mwanya kufanya ya Mungu kwa juhudi,tena huo ndio wakati wako wa kujiwekea akiba ya maombi na kumtafuta Bwana, maana kuna majira magumu ya hatari,yanaitwa majira ya kujiliwa kwako (Luka 19:44),Kama hukutumia hiyo nafasi hiyo ya wakati wa afya tele,kumsaka Mungu yale majira ya kujiliwa utakutwa dhaifu bila nguvu ya Mungu,na kupigwa utapigwa bila shaka, *HUTAWEZA KUSIMAMA SIKU YA UOVU*

*Zaburi 32:6*

*_6 Kwa hiyo kila mtu mtauwaAkuombe wakati unapopatikana.Hakika maji makuu yafurikapo,Hayatamfikia yeye._*
👆🏼Kuna wakati maji makuu yatafurika(kutatokea disasters mbalimbali ktk maisha yako,sasa yanapoinuka majanga hayo,kama ulijitajirisha kwa Mungu ,effects/athari ya hilo janga itakuwa *_Reduced to Zero_*. Ila kama wakati wa neema ulitumia nguvu kubwa kujifurahisha ktk udhalimu athari za maji makuu yafurikapo itakuwa *_at the maximum_*. Lakini kama umjitajirisha kwa Mungu hata ukiwa hoi kwa ugonjwa,there on  your sick-bed there will be God's hand to sustain thee (Zaburi 41:3)

*_3 BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.Katika ugonjwa wake umemtandikia._*

```JE! MUNGU AMEKUPA KAZI NZURI?```
Hiyo ni nafasi yako nzuri ya kumtukuza Mungu,muoneshe Mungu hapo kazini na penginepo,daima ukiri wako *_"IT IS ONLY GOD KWA KWELI"_* hiyo sio nafasi yako ya kubadili usemi na kutumia matamshi(Slang) ya kimarekani kuongelea kiswahili,na kujieleza bidii yako ukiwa masomoni,ujue kuwa ni Mungu tu kakuheshimu,maana kuna classmates wako walifariki siku chache baada ya Graduu🎓ya chuo. Kuna kaka mmoja alilelewa na CASFETA akiwa masomoni ila Mungu akamwinua sana baada ya kumaliza masomo,akawa kwenye ajira ya mapato makubwa sana. Sasa vijana walitumwa kwake kumwomba mchango wa kambi la pasaka la CASFETA,sasa akapokea barua ya mchango akaiweka kabatini. zikia zimebaki siku chache akapigiwa simu na mratibu kuulizwa hivi mpendwa ulipata barua ya mchango? alijibu kwa dharau, *_"niliipata, BUT THE WAY MLIVYOOMBA SIJAPENDA"_* yaani alitaka aabudiwe kwanza na anyenyekewa ndio asapoti kazi ya Mungu,hiki ni kiburi cha kusahau ulipotoka,wakati semisters kadhaa hata ada ulichangiwa na wanafellowship. Kumbuka *Downfall goes after pride*. Na Mungu anapingana na wenye kiburi(He resists them) na yale magumu ya wakati wa dhiki kuu atayaleta ili kukishusha kiburi cha wanadamu (Isaya 2:17)

```JE! MUNGU AMEKUPA NATURAL/INNATE  TALENTS NA VILE VIPAWA VYA KIROHO?```
Mungu alikupa  hayo kwa kuwa wewe ni kiungo,uwafae wengine,sasa wachache wasiojua siri za kujitajirisha kwa Mungu wanatumia hivyo kuusaka tu umaarufu,then kwa umaarufu wao na hali ya maisha wanatumia mwanya huo kutesa na kusumbua watu,utakuta kijana wa kiume aliyejaliwa vipawa vile vyenye mvuto,anaamua kutumia hiyo nafasi kuharibu mabinti,keshachumbia wengi na kuwaacha wengine aliwapa na ujauzito akawatosa baharini🌊, ~*(be sure of this,there is a time for your downfall)*~

KATIKA NAFASI YOYOTE ULIYO NAYO,JITAJIRISHE KWA MUNGU *_UNTIL IT BECOMES TOO MUCH OF GOD IN YOU_*  JINYENYEKESHE KWAKE,PRAY CEASELESSLY,TUMIKA CONTINUALLY,MTOLEE MUNGU NON-STOP IN A GOOD MEASURE,DUMU KTK UTAKATIFU WAKO. UKIJITAJIRISHA KWA MUNGU KTK ILE KAZI YAKO YA HESHIMA(WHITE COLAR JOB WITH GREEN PASTURE) HATA KUKIPITA TUMBUATUMBUA WEWE MKASI✂ WA KUTUMBUA HAUTAKUPITIA UTANUSURISHWA TU,NA KAMA MUNGU AKIRUHUSU UJUE AMEANDAA PALIPO PEMA ZAIDI
LAKINI WALE WASIOJITAJIRISHA KWA BWANA HUWA HAWANUSURISHWI NA WAKITUMBULIWA LAZIMA WASOTE MPAKA WANADODA ILI KIBURI KISHUSHWE.

*ALIYEJITAJIRISHA KWA MUNGU*

✝Ataona mambo ambayo  wengine hawajayaona and so to say,he/she will be having a clear insight in all endeavours of life
Mkumbuke Yusufu ktk umri wa miaka 17 alikuwa tayari  ni kijana aliyejitajirisha kwa Bwana kama angekuwa Tanzania iwa umri wake huo kijana  wa KIDATO CHA III ,mwenye kujua kumsikia Mungu kwa ndoto,what about David the son of Jesse ktk miaka 12 anamjua BWANA na kumtumaini,akiwa na umri huo yaani mwanafunzi wa darasa la 5B amejaa Mungu na Mungu alikuwa anam-admire mno (Mdo 13:22),lakini mibrother men akina Eliabu kaka zake Daudi walikuwa bize tu kuchat📱na kuangalia📺lakini hawakujitajirisha kwa Mungu ndio maana hawaku-qualify ktk uchaguzi wa Mungu nani awe mfalme. Je unamkumbuka Ezekiel nabii wa Roho,yeye alikuwa na watu wa uhamisho ktk mto Kebari mbingu zilifunguka wenzake hawakuona kitu ila yeye akaona yale maono mazito ya wenye uhai na magurudumu yenye roho zao,Je wamkumbuka Daniel  akiwa na watu wengi kando ya ule mto mkubwa Hidekeli,akaona maono mazito peke yake maana alijitajirisha kwa BWANA,pamoja na kuwa na cheo cha tatu cha juu ktk serikali ya Dario mfalme ,ila alikuwa akikumbuka mfungo/Saumu tena ya kujinyima chakula kitamu🍗🍖🌭🌯🌮🍹🍹🍷🍷 ili amtake BWANA na Nguvu zake. WEWE NDUGU YANGU UKO WAPI?

✝Atafanywa kuwa msemaji wa Mungu (God's spokesman)
Yeremia 15:19

19 Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika *_kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu(my spokesman)_*;
Funua kinywa chako nami nitakujaza,walijitajirisha kwa Mungu,hujazwa maarifa ya Mungu,na they are enriched with enough information about God,yaani mnasoma wote Biblia moja ila huyu aliyejitajirisha kwa Mungu ana uwezo mkubwa wa kufafanusha (Zaburi 119:130)

✝Mahali pa hatari kuu,utakuwa na jibu la Mungu kwa ajili yako na kwa ajili ya watu ulio nao

*Matendo 27*

*_1 Na walipokuwa wamekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paulo akasimama katikati yao, akasema, Wanaume, iliwapasa kunisikiliza mimi na kutokung'oa nanga huko Krete, na kupata madhara haya na hasara hii._*
*_22 Sasa nawapeni shauri, iweni na moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu atakayepotea, ila merikebu tu._*
*_23 Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami,_*

👆🏼👆🏼Eh bwana kitu hicho😋😋😅😅👌🏽👌🏽
*_24 akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe._*
*_25 Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa._*

👆🏼👆🏼😰Duu Neno la Mungu ni hatari sana

Aisee Bwana awabariki,mnapoweka mikakati ya kuanza kujitajirisha sana na wengine wengi ni mwendelezo tu ila daima wanajitajirisha kwa Bwana

For inquires
Mwl Proo
0762879363(WhatApp#only)

alltruth5ministries@gmail.com