*_YAKO MAGUMU AMBAYO YAKIKUKUTA MWAMINI, UNAPASWA KUYAPELEKA KWA MTUMISHI MWENYE NGUVU ZAIDI!_*
*Mwl Proo*
_0762879363_
MBARIKIWE NINYI NA BWANA! Ninawasalimu kwa Jina la Yesu aliye Kristo wa Mungu!
Nauandika ufunuo huu ambao nilifundishwana Bwana siku chache zimepita. Mimi ni miongoni mwa walimu ambao wanatia mkazo mkubwa katika kuwajengea uwezo waumini, wasiwe watu tegemezi, wasiwe watu wanaoburutwa na kubururwa na maadui, then wakimbilie maombezi. Ukiacha waamini wachanga (recent converts), wale wengine sharti wawe wamekua na kuongezeka nguvu rohoni (Luka 1:40, 80), kiasi cha kuweza kujisimamia maisha yao kiroho, hata kuzikabili vita za rohoni wao wenyewe.
*LAKINI PAMOJA NA HUO MKAZO WANGU KATIKA MASOMO MENGI, BWANA ALINIONGEZEA KITU, KWAMBA YAKO MAGUMU YANAWEZA SIMAMA KINYUME NA MWAMINI, YAKAHITAJI NGUVU KUBWA TOKA KWA MTUMISHI MWINGINE, IMVUSHE. VIWANGO VYA NGUVU INAYOTENDA KAZI NDANI YA WATU HAIKO SAWA (Efeso 3:20). KATIKA ULIMWENGU WA ROHO ZIKO RANKS (YAANI KIMO CHA CHEO CHA JUU SANA MPAKA CHINI SANA), HATA WATUMISHI NAO WANATOFAUTIANA KATIKA HIZO RANKS (CHEO). ROHO NI YULEYULE, BWANA NI YULEYULE NA MUNGU NI YULEYULE ATENDAYE KAZI KATIKA WOTE, LAKINI KIMO CHE CHEO HAKIKO SAWA, NDIVYO ILIVYO NA NGUVU ZINAZOTENDA KAZI NDANI YA MTUMISHI* (Utanielewa mbele kidogo)
*Katika somo langu la _"Roho Mtakatifu"_, nilijadili kuwa kimo cha cheo (madaraka ya rohoni) yanategemea mambo mawili; 1.Kiasi cha ufahamu na 2.Maarifa ya rohoni. Katika somo hili naomba kuongeza kuwa Wito na Kusudi (Call&Purpose) inaamua kimo cha madaraka yako kiroho. Na hapa ndipo tunapata tofauti ya hizo ranks. Hapa swala la bidii ya kumtafuta Mungu halihusiki hata, najua it sounds so strangely lakini ndio kweli yenyewe. Wako watumishi ambao Mungu aliwaita na kuwa-commission kazi fulani, muda anawaagiza kazi, aliwavika madaraka fulani ambayo rohoni ndiko yanaonekana zaidi, na viumbe vyote vya rohoni vinaiona hiyo level ya cheo chake (rank), na wengine kulingana na wito wa kusudi la Mungu kwao, aliwapitisha katika madarasa ya kiroho ambayo sio kila mtu anapitishwa.... Alipohitimu kuandaliwa kwa kazi akawa amevikwa kimo cha cheo chenye madaraka na nguvu kubwa. Hii hata sio ajabu, Mungu aliset protocols nyingi tu katika ulimwengu wa roho, pamoja na principles zinazousimamia ulimwengu wa roho wote na huku kwa corporeal world. Nilikuwa nikimsikiliza Duncan William akijadili kisa cha Yakobo kupigana mieleka/wrestling na Malaika na kumshinda, pia kisa cha Malaika Mikael na Shetani katika kuugombea mwili wa Musa, akajadili hoja za msingi za mipaka ya kiutawala pamoja na kimo cha cheo ambacho Shetani alikifikia yaani level ya Kerubi (Cherubim), nilimwelewa in relation to hiki naelekeza leo.*
*KWA NINI NAFUNDISHA HAYA?*
*SIJALENGA KUWAFANYA WAAMINI WAWE WAZURURAJI KWA WATUMISHI, HILI LA KUZURURA LINAFANYWA NA WATOTO WACHANGA KIROHO. MIE NAZUNGUMZA NA WAAMINI WAKOMAVU, KWA ROHO MTKATIFU WATAJUA TU JINSI YA KUJICONNECT NA MWENYE NGUVU KUBWA*
💿 _Ufahamu huu ukikosekana unaweza kuteseka na jambo miaka saba, kumbe ulihitaji single encounter na mtumishi mwenye nguvu zaidi, for your issue to be sorted out_
💿 _Yako mambo ambayo ulipaswa kuwa na kiasi cha nguvu ili kuzuia yasiharibiwe na adui. Lakini ulikutwa na nguvu chache yakaharibiwa, hapo sasa nguvu ile itendayo kazi ndani yako haitaweza kushughulika na madhara ya uharibifu kama hukuweza kwa nguvu zako kuzuia adui asiharibu_
💿 _Mambo yakiharibiwa utahitaji mwemye kimo kikubwa cha cheo aweze ku-revoke (aitangue ile nguvu ya adui na kuponya palipobomoka)_
💿 _Ukikosa kweli hii, unaweza kudumu ukimlilia Mungu miezi kadhaa, ukafikiri Mungu hakusikii. Kuna wakati wa kumlilia Mungu naye akatenda, na kuna wakati ambapo uharibifu ulifanyika kwa kuwa ulikuwa na nguvu chache, hapa hazihitajiki nguvu za kuzitafuta muda huo, bali mwenye nguvu kubwa ahusike kunasua, kuponya na kutangua yaliyowekwa na adui._
*MIFANO HAI*
🔥 👉Kuna mhubiri fulani nchini Kenya, alihubiri na kufanya maombezi huku akiusifu uweza wa Mungu ni zaidi ya wachawi wote, pamoja na kwamba alifanya makosa fulani hivi katika demonstration of power, aliiga mambo ambayo sio karama yake. Lakini maadui walijipanga kwa nguvu kubwa kuliko yake, Yesu hasindwi kamwe na nguvu za Adui Shetani na mawakala wake, lakini kiasi cha nguvu ndani ya mtu kinaweza amua tofauti...
NB:-
~*NAIWEKA SAWA ZAIDI, HAKUNA MTU ALIYEMWAMINI KRISTO NA KUOKOLEWA, NA KUWA NA MAARIFA/UFAHAMU WA ROHONI WA KUTOSHA, AKALOGEKA KWA UCHAWI, NEVERRRRRRRR! HUTU TUUCHAWI TWA KUCHUKUA MCHANGA MAHALI UMEKANYAGA, SIJUI KUFUKIA KAHIRIZI ILI UKARUKE, AU PEMBE, AU NDAGU ZA NAMNA ZOTE, NEVER NEVER NEVER! LABDA KAMA UMEDUMU KATIKA UCHANGA WA KIROHO MUDA MREFU SANA, UKADUMAA KABISA, UKAPOA KIASI CHA KUCHAFUA LILE VAZI ROHONI, NA KUPOTEZA IDENTITY YAKO KWA KURUDIA MAISHA YA DHAMBI BILA KUTUBU, HAPO YOU'RE PRONE AND VULNERABLE TO ATTACKS. LAKINI UKIWA KWA ILE NAFASI KWA UKAMILIFU HAULOGEKI, NA KAMA ADUI ATAKUJA KWA NGUVU KUBWA SANA KUZIDI NGUVU ULIYONAYO, ROHO MTAKATIFU ATAKUJULISHA ILI UONGEZE UWEZO BEFORE THE ATTACK (NAHUMU 2:1).. HUWA TUNAPENDA TU KUNUKUU HESABU 23:23 BILA UFAHAMU. HAYA MANENO YALITAMKWA NA MNAJIMU+MCHAWI BALAAM BIN BEOR, AMBAYE MUNGU ALIAMUA KUMWEKEA MANENO YAKE NDANI, LAKINI HUYU MCHAWI ANATUJULISHA SIRI, ALIPOKODIWA AWALOGE WAISRAEL, AKASEMA HUWA HAKUNA UCHAWI JUU YA ISRAEL WALA UGANGA JUU YA YAKOBO, YAANI ALL KINDS OF WITCHCRAFT NA NDUMBA ZOTE HAZIFANYAGI KAZI KWA HII JAMII, SO NI KUPOTEZA MUDA KUWALOGA. NA JAMII YA WAAMINIO NI ZAIDI YA WAYAHUDI KWA JINSI MWILI.*~
Nirejee kwa huyu mhubiri wa Kenya, yeye alipomaliza huduma ya jumapili, jioni yake wakampiga *juju* moja hatari, wakamtengua disc ya nyonga kwa uchawi na akaanza kutambaa chini kama mtoto, maana aliwasemea vibaya wachawi kumbe nguvu zake ni chache, waliporusha Scud💥 ikampatepo.... Sasa huu uharibifu umekwisha ingia, swala la kukaa kulia kanisani linaweza lisipate majibu, ukaumia sana as if Mungu hayupo. Ila huyu mtumishi alipata hii siri, ndipo alipoponea. Hakuwa na nauli aliuza kinanda 🎹 cha kanisa akawahi kwa mtumishi mmoja maarufu Duniani yuko huko Magharibi mwa Africa, kumbuka kanisani washirika waliomba sana na kumlilia Mungu with No smell of an answer from God. Ila alipofika tu kule, alihudumiwa sekunda 5 Disc ya nyonga ikawekwa sawa akainuka mwenyewe, akapewa msaada wa kimwili, kiroho, na akapewa maongozi ya huduma akirudi kwenye Ministry yake. Ukweli ni kwamba, nguvu inayotenda kazi ndani ya huyo mtumishi, kimo chake cha cheo kiroho, kipo juu mno, kiliruhusu *Revoking* ya ule uharibifu wa kichawi bila maombezi mengi, alitamka tu *In the mighty name of Jesus* ikatosha kabisa. Uharibifu huu hauhitaji kuanza maombi ya mfungo wa siku tatu kavu, yaani nguvu za kuzisaka kwa dharula, hapo ilitakiwa ambaye amevikwa nguvu kubwa yuko nayo muda husika.
🔥👉🏽Kuna dada na rafiki yangu, amenipa ushuhuda, alipata mchumba, ikiwa imebaki wiki moja yule mchumba alete barua home kwao, naye amekwisha sumbuka sana, maana alikuwa akimpenda sana na vigezo vyote aliona 100%. Lakini ndoto zinakuja zinamtatiza hajui afanye nini, mpaka akamwambia Mungu ruhusu niolewe, kama yakinishinda basi nita👉🏽💔, katika jitihada za kutafuta suluhu. Na kiukweli kuna mambo yalijificha sana, huyu mwanaume angekuwa Shetani in his fullness katika maisha ya huyu dada. Haya maeneo ndipo nikafundishwa umuhimu wa jambo gumu kulipeleka kwa mtumishi mwenye nguvu zaidi. Nini kilitokea? Huyu dada zikiwa zimebaki siku chache kabisa atolewe barua rasmi, alihudhuria harusi fulani, akiwa huko, akamwona mtumihi mmoja wa Mungu (anayetumika kwenye ofisi ya Nabii), akamfuata kumsalimu tu, ila walipokumbatiana tuu👉🏽🔭🔬🎥🛰vionea mbali vya nabii vika-sense some issues..Akamwambia *"""Mmmhh subiri! Kwa nini unataka kuolewa na mpagani hajaokoka, anafanya kazi kiwanda cha bia, mlevi and bla bla bla"""*. Alitoa habari zote za huyu mtu akiwa hajaambiwa chochote, basi huyu dada akasalimika kwa njia hiyo, akaenda kuuvunja uchumba kesho yake. Sasa utaona jambo gumu ambalo ameombea miezi na miezi, limekutana na Solution dakika 1 tu wakiwa katika shamrashamra za harusi nyingine.
*NB:-*
*_Mwenye kimo kikubwa cha cheo, ambaye amevikwa madaraka makubwa, hatazitafuta nguvu muda huo, bali anakaa nazo kwa sababu ya rank yake. Hivyo unaweza kwenda kwake ukamkuta yuko anacheza na watoto wake, lakini ukamfikia ile nguvu kubwa akakugusa au kukupa neno moja ukatoka katika ugumu._*
*Nami sifundishi watu wawe tegemezi kiroho, nakupa siri za ufalme wa Mungu. Hawa ambao wavivu kumtafuta Mungu, ila kazi yao kurukaruka kusaka miujiza, hawa hiki sio chakula chao, mioyo yao imeelekezwa katika kutaka dezodezo, kazi tu kutamka I receive! I connect!, hawana nguvu hata kidogo, shauri zao, watakutana na matapeli wa mjini, wasipoliwa pesa zao, wataliwa wao wenyewe, and that will not change God, Mungu atabaki kuwa Mungu, anadumu wa kuaminiwa (2Timothy 2:13)
*KUHUSU HIZO LEVELS/RANKS*
Wapenzi hii ni kama haiko vizuri kwa hekima ya juujuu, ni rahisi kuhisi tunawapimanisha watumishi, la hasha.... Ni muhimu kwa mtu mkomavu kiroho aelewe hilo, kama itatokea umekutwa na gumu fulani. Wala usiseme kwanza anayeponya ni Mungu au Mtumishi? Huyu Mungu wa Biblia anafanya kazi na watu (Rumi 8:28), na kuna mahali amekwisha invest ili kusaidia wengi, so protocol itazingatiwa. Kuna mwingine ni mtumishi ana juhudi mno za kufunga na kuomba na mikesha kwa wingi, lakini kwa sababu ya level of his spiritual understanding akawa na kimo kidogo cha cheo rohoni. Mwingine anaweza kuwa na ufahamu wa maswala ya rohoni sana, lakini aina ya wito wake haujampa kimo kikubwa rohoni, mwingine akawa na cheo kikubwa rohoni kumbe ni kwa sababu tu ya kusudi la wito wake. Mfano Mtu anaweza itwa katika Ofisi ya kitume, ukakuta karama za uweza/nguvu ziko too active kwake, au mtu akawa ameitwa kama nabii, ukakuta karama za ufunuo ziko to strong kwake. Na mwingine wakati wa kuandaliwa alipitia darasa sio la kawaida, namkumbuka askofu fulani hapa Dar, alitupa ushuhuda alivyoshindana na wakuu wa giza na majeshi ya pepo rohoni, mpaka akawa hoi lakini akafanikiwa mwishoni kuwashinda kabisakabisa, na anasema alivyomaliza hayo mapambano huko rohoni, alimwona malaika amekuja na chuma kama medali👉🏽🥇, akamvika shingoni. Hayo mambo mimi najua jinsi yalivyo halisi, kwa hiyo unakuta viumbe vya rohoni vinaiona hata hiyo medal, na vinatambua kimo chake cha uwezo kicheo. Na hawa watu tunawatambua katika utendaji wa kazi. What do I mean here, usife na tai shingoni 👔, ukikomalia msimamo kuwa Mungu anakusikia tu, kama uharibifu umefanya umepatikana na madhara tayari, iwe ugonjwa mbaya, iwe shambulio la kiroho ukaishiwa nguvu, iwe shambulio la kichawi, iwe uharibifu katika mambo ya uchumi, elimu, mahusiano, etc uharibifu huo ilikuwa rahisi kuuzuia usiingie. ila kuondoa madhara yaliyokwisha kukupiga pamoja na kuponya palipobomoka, take it to the higher authority...
_Mwl Proo_
*0762879363*
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment