Thursday, March 8, 2018

MAAGANO

*MAAGANO YANAWEZA FANYWA IMARA (ESTABLISHING) AU KUDHOHOFISHWA (OBSOLETING), KUFANYWA UPYA (RENEWING) AU KUONDOLEWA KABISA (NULLIFYING)*

*Mwl Proo*
_*0762879363*_

_Ninawasalimu wasomaji, kwa jina la BWANA (Yesu), Yule mwenye kushika maagano (Daniel 9:4), Aliye Mwaminifu na Wa-Kweli (Ufunuo 19:11). Mungu alinitia moyoni nifundishe jambo hili la kukupa maarifa kamili._

🔒 *AGANO NI NINI?*

🔑Neno hili Agano/Covenant limetumiwa katika Biblia ya Kiebrania (Tanakh) mara 285 ambapo katika hayo yote limeandikwa *בְּרִית* linalosomeka *Bĕriyth/Berith* maana nyepesi kabisa ni *Patano*, Mwanazuoni *Warren Wiersbe* amefafanua neno hilo la Kiyahudi lina maana ya 1.Kula na/pamoja na (to eat with), ikiwa inazungumzia ushirika (fellowship),  2. Kufunga (to bind) ikiwa inazungumzia kujidhatiti kushika kwa kutenda (commitment), 3.Kugawa (to allot) inazungumzia kutoa/shirikisha (sharing), maalum kabisa ikizungumzia swala la Mungu akifanya Agano anakuwa amejidhatiti kabisa kutoa na kufanya yale aliyoyaahidi (keeping of promises).

🔑 Tafsiri ya pili ya maandiko matakatifu kwa lugha ya Kiyunani (Septuagint), ilitafsiri neno Berith/Agano kama *διαθήκη* linalosomeka *Diathéké*, neno hili Diathéké lilitumiwa katika ulimwengu ule wa *Greco-Roman World* kama Wosia wa Marehemu (Last will and Testament), ambapo maneno hayo hayakutanguliwa au kurekebishwa, na ndiyo pekee yalitumiwa katika kugawa mali za marehemu. Hata kama itadhaniwa marehemu hakutenda haki, alichosema ndicho last will (wishes) zake, haikudirikiwa kubadili neno.

🔑Nimetumia lugha za asili, kukupa chimbuko la neno Agano. Kwa ujumla wake twaweza jumuisha (consolidate) kuwa Agano ni patano, makubaliano kati ya pande mbili (two parties), yanayoambatana na ahadi/promises, vigezo na masharti (terms & conditions), yanayoweza fanywa kwa Oaths binding (Kula viapo 👉🏾 Agano la Maneno), mfano mzuri katika Biblia (Unequivocal Oathing Style) ni ule wa Daudi na Yonathani. Pia yanaweza kufanyika kwa damu *Blood ties* kwa njia ya sadaka za kuchinja kiumbe, au kama ile katika Semitic world ambapo watu waliweza kufanyika ndugu kwa kila mtu kunywa damu kidogo ya mwenzake.

🔒 *KUFANYWA IMARA/KUDHOHOFISHWA KWA AGANO*

🔑 Kwa kuwa Agano lina vigezo na masharti (terms/conditions), yakiendelea kushikwa kwa mkazo mkubwa (strict adherence to terms/conditions), yanapelekea Agano kuwa imara, upuuziaji wowote wa yale matakwa (requirements) yanaweza pelekea kudhohofika kwa Agano (Ingawa kudhohofika sio kuvunjika👉🏾 weakening of covenants is not abolishment).

*USHUHUDA No1*
Ushuhuda nilioukumbuka juu ya hili, ni wa mama mmoja aliyenunua gauni zuri la lenye vifungo/buttons za dhahabu 👉🏾👗👘👉🏾👙💎💎💎💎. Na mara baada ya muda kidogo tu, akaanza kuteswa na Pepo wachafu 👹👹👹. Alihangaika haswa, mapepo yakagoma kabisa, na hata yalipokubali kutoka, yakasema atatukuta nyumbani. Mwishoni akaamua kupeleka issue yake kwa mtumishi mwenye neema kubwa zaidi katika kufungua vifungo vya giza. Yule mtumishi alipoanza kuomba, akawa anaona vitu vinang'aang'aa, akakatisha maombi, akamwuliza yule mama, *"Nyumbani kwako kuna dhahabu?"*, yule mama akakataa, akaulizwa vitu vya dhahabu (gold-plated materials/assets), ndipo akakumbuka gauni lake amenunua kwa pesa nyingi lina vifungo vya dhahabu yenyewe 100%. Mtumishi alipoagizisha akakata vifungo na kuvitupa mbali, mapepo yaka-demonstrate, kisha yakaondoka, ikawa mwisho wa mchezo. Lakini katika kutafuta kujua habari, kwamba ni nini hasa kilitokea, ikapatikana habari, kuwa yule mfanya biashara alikuwa na maagano na majini kumsaidia kibiashara, na yakawa yanakaa kwa hivyo vifungo vya gauni. Lakini inaonesha yule mfanya biashara hakuendelea kuyashika masharti yote, hivyo majini/pepo yakaacha kufanya kazi yao ipasavyo ya kui-boost biashara, kumbuka gauni hilo hakuwa analiuza, alilitundika tu kama show. Lakini alipoona halitendi kazi sawa, akatafuta majini/mapepo mengine na lile akaliuza. Sasa kumbe maagano yake hayakuvunjwa, ila yalidhohofika tu, maana hakushika masharti yote, ndio maana mapepo yalibaki yakatesa mteja.

🔑 Katika Biblia tunaona Mungu anafanya Agano na Ibrahimu na vizazi vyake (Mwanzo 17:7), lakini mastari wa 9, anamwambia njia za kulifanya hilo Agano liwe hai/imara inategemeana na ushikwaji wa yale matakwa ya Agano

Tusome.....

*New Living Translation (NLT)*
(Mwanzo 17:9)
_Then God said to Abraham, "Your responsibility is to obey the *terms of the covenant*. You and all your descendants have this continual responsibility._

*NET Bible*
Mwanzo 17:9
_Then God said to Abraham, "As for you, you must keep the *covenantal requirement* I am imposing on you and your descendants after you throughout their generations._

🔒 *AGANO LAWEZA FUTWA/ABOLISHED, AU KUFANYWA UPYA*

🔑Maagano yanaweza fanywa kati ya pande sawa kwa ukuu, au mkuu akafanya mdogo (Superior//Inferior), kila upande unawajibika kushika Agano, na hapo ndipo Mungu anatajwa kuwa Yeye ni Mungu ashikaye maagano (Faithful to keep all of His promises). Inapotokea Mungu amefanya Agano, Yeye ni Superior, kama matakwa ya agano yakavunjwa kwa kiasi kisicho na tiba (non remediated), basi anaweza vunja agano.

1 Samweli 2 : 30
*Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu.*

👆🏽👆🏽Mungu aliagana na Ibrahimu lakini akalifanya imara Agano mpaka kwa Isaka (Mwanzo 17:21), kwa kuwa Isaka hakuwahi kuchakachua terms za Agano. Lakini katika mstari hapo juu, tunamwona bwana mdogo mwana wa Daudi, ambaye kwa kweli alivurunda. Huyu Sulemani ndiye haswa mwanzilishi wa kujenga *mahali pa juu (shrines/high places)* prompted by wale wanawake 700 aliowaoa kwa madhumuni ya kisiasa zaidi. Mungu ashikaye maagano, Uzalendo ulimshinda, akavunja Agano... Na ndio mwanzo wa Taifa la Mungu kugawanyika, yule mfanyakazi wa Ikulu ambaye alikuwa akielewa mwenendo mzima wa utawala (Yeroboam mwana wa Nebati), akatumika kama upanga, ufalme ukamegwa, makabila 10 yote ya Kaskazini (Taifa la Israel ) yakawa chini ya huyu mtu ambaye hakuwa katika kiapo cha Mungu kwa Daudi, ila Mungu kwa ajili ya Daudi mtumishi wake, akaona isiwe shida, akabakiza makabila mawili tu (Yuda+Benjamin) huku kusini (Taifa la Yuda). Haya ni madhara ya kuacha terms/masharti ya Agano.

🔒 *MAAGANO YA KIUKOO*
Katika somo langu la *NAFSI ILIYOJENGWA*, nilielez kuw nafsi inaweza kuuzwa. Sasa kuna mabibi na mababu walijiuza nafsi zao kwa pepo wabaya, wakafanya oath-bond (viapo) kwamba Agano hilo liwahusu na watoto wa watoto wao, mpaka vizazi vijavyo. Sasa maagano haya yanashikiliwa na hawa mapepo/majini/roho wabaya ambao kimakosa wamepewa jina la *roho za familia/family spirits*, kuwait kwa jina hili ni kuwapendelea hawa pepo wabaya, kisha ni pepo hawa hawa wanatafuta *Kick*  kwa kutumia sura za marehemu tofautitofauti katika ukoo, na kuwatokea watu kama mizimu *(IKUMBUKWE HAKUNA ROHO YA MAREHEMU INAYORUDI KUTOKA KUZIMUNI 👉🏾Ayubu 7:9-10)*, jitajidi usome somo langu la umilele, ili uyaelewe haya kwa kina. Lakini hakuna kitu kinaitwa mizimu ya mababu, ila ni mapepo ambayo mababu waliamua kujiuza nafsi zao kwayo, sasa yanachukua sura halisi, na kuja ku-disguise, eti yanawapa maelekezo. Yale mateso ambayo yanawakuta watu yakihusishwa na roho za familia/maagano ya ukoo, majaribio ya yale mapepo, katika kutafuta kuona hivi vizazi vipya vinashika matakwa yale ambayo waliagana na wazee wao. Kwa hiyo pepo linaweza kumtesa mtu (kwa magonjwa jata ya kurithi), kisha akiitwa mpiga ramli, anapandisha pepo, kwa mawasiliano ya kipepo inajulishwa kuwa unapaswa kufanya so and so, kumbe lengo, inakuwa ni *KULIFANYA IMARA AGANO AMBALO LIMEDHOHOFIKA*, ndio maana haipswi kamwe mtu mwamini, aliyekuwa kiroho na kuongezeka sana katika kimo cha cheo, eti ateswe na roho za familia au maagano ya mababu. Maana maagano hayo yalifanywa kati ya superior side (Mapepo/Majini) na inferior side (Mababu/Mabibi), Sasa ikija nguvu ya Msalaba wa Kristo na Damu ya pale Golgotha inakuwa na nguvu (Superior) kuyazidi majini/mapepo yote yaliyopata kuweko.

❌❌❌ *ONYO* 🚫🚫🚫
*KUNA MAMBO MENGI YA KITAMADUNI, HAYANA ASILI MWILINI BALI ROHONI, YALIKUWA _IMPOSED_, NA MAPEPO KAMA KACHUMBARI TU YA KUCHOCHEA MAAGANO ALONG ZILE TERMS/CONDITIONS ZA MAAGANO. HIVYO NI HATARI KWAKO MKRISTO/MWAMINI KUSHIRIKI OVYO MAMBO YA KIMILA/KIDESTURI UKITEMBELEA KIJIJINI KWENU. UNAWEZA KUTA MAMBO YA KUCHINJA MNYAMA KWA KUMSONGOA, KUPELEKA CHAKULA/POMBE MAKABURINI, MPAKA SOME TRADITIONAL DANCES (NGOMA ZA KIENYEJI-INGAWA SIO ZOTE), UWE MAKINI NA UKUBALI KUONGOZWA NA ROHO, KABLA HUJATAFUNWA NA JOKA🐍🐉*

🔒 *UCHAWI NA ULOZI*

🔑 Uchawi na ulozi unapofanyika, kinachofanya kazi sio vile vifaa vya kichawi 🌾🦇💀☠📿🏺📍🃏🎭🎲🎳, bali kuna mapepo ya ulozi na uchawi,ndiyo yanayoshikilia *VIAPO, MANUIZO, MAZINDIKO*, kwa hiyo hata kama mlichinja mbuzi, mkafukia kichwa mlangoni, kunakuwa na PepoJini anayeshikilia hilo Agano la Damu. Kama mtu amefungwa tumbo asizae. Na mganga au mchawi alichukua uzi mwekundu akaufunga kwenye kijiti au mfupa (ule uzi ni medium tu yaani mawasiliano ya kipepo ya physical article to spiritual altar), kinachofanya kazi kushikiliza lile tumbo lisishike mimba sio huo uzi, bali kuna Jinn/Pepo la Ulozi ambalo hiyo ishu inakuwa *entrusted* kwake, nalo litaifanya kazi hiyo kwa uaminifu. Kama huyu mtu akienda kwa mtumishi mwenye nguvu chache (kimo kidogo rohoni kwa cheo), akikemea kifungo kifunguke, PepoJini aliyekabidhiwa kushikilia kile kifungo, anaweza akaamua kushikilia maana nguvu/mamlaka iliyoamuru aachie ni ndogo (Kumbuka mzazi mwenye mtoto mwenye pepo bubu, ambaye alimpeleka kwa wanafunzi wakashindwa Mathayo 17). Kumbuka kuokoka haina maana kwamba utakuwa na nguvu kuzidi maadui wote wa kiroho (SHARTI UONGEZE UWEZO WAKO SANAA 👉🏾 Nahumu 2:1). Hawa majini/mapepo wanamtambua mwenye nguvu kubwa huwezi kuwavunga, waulize wana wa Skewa. Hivyo wakikutana na mwenye nguvu kubwa akiamuru utasa toka, huu utasa kwa kuwa ulisababishwa na kale kauzi ka kichawi, hili pepo lililokbidhiwa kazi ya kushikilia lita-salimu amri na kuachia, hata kama yule mlozi/mchawi akilituma tena, litatia mgomo, kwamba Mmmh, No! pale nimefukuzwa!

*HITIMISHO*

*Ndugu wapendwa, kama kuna maagano yoyote yanayokutumikisha, iwe ulifanya mwenyewe au yalifanywa ma watangulizi wako, yakabaki yanasumbua, tiba ya ku-nullify maagano yote ni Damu ya Yesu ya Agano na Msalaba. Maagano hayo yatavunjika kwa sababu mamlaka ya Yesu ni kubwa kuliko maadui wote wa kiroho na kimwili.*

*LAKINI PIA, MUNGU KATIKA NENO LAKE AMETUPA TERMS/CONDITIONS ZA KULIFANYA AGANO LAKE KWETU LIWE IMARA. AGANO HILO LIMEAMBATANA NA AHADI TELE. AHADI HIZO ZINAWEZA KUADIMIKA MAISHANI MWAKO KAMA UTAYAACHA MATAKWA YA AGANO. KWA MFANO UMEAHIDIWA UZIMA, AFYA NA KUPONA, UMEAHIDIWA KUFANIKIWA KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA, UMEAHIDIWA ULINZI, MUNGU AMEAHIDI KUWA ADUI WA ADUI ZAKO, AMEAHIDI KUWATAWANYA MAADUI WALIOKUJA KWA NJIA MOJA WATAWANYIKE KWA NJIA SABA, AMEAHIDI KWAMBA UTASHUKA KABURINI UKIWA UMESHIBA SIKU, AMEAHIDI KUKUFANYA KICHWA NA KUKUWEKA JUU TU, WANAFUNZI WA  BIBLIA WAMEHESABU JUMLA YA AHADI ZIKO 31,100, LAKINI AHADI HIZI ZINAZOAMBATA NA AGANO LAKE KWETU HATUZIRITHI BURE BURE, BALI KATIKA KUSHIKA SANA MATAKWA YA AGANO LAKE KWETU.*

KWA UFAFANUZI WA KINA KUHUSU AGANO LETU PAMOJA MASHARTI YAKE, USIKOSE SOMO LANGU LIJALO LIITWALO *"WAHUDUMU WA AGANO JIPYA*

*Mwl Proo*
_0762879363_

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment