Friday, August 3, 2018

ROHO YA MAZOEA

*🐠WAKRISTO WENGI KUNGIA MOTONI, KWA SABABU  YA ROHO YA MAZOEA🐠*                 

🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

*_Hii ni baada ya kufika mbinguni, na kushuhudia ukumbi wanaoingia watakatifu, na kukuta ni wachache, wakati viti ni vingi, tena viko wazi. Wengi watataka kuingia lakini hawataweza.... (Mathayo 22:14, 7:13-14)._*

🔥🔥 Nakumbuka katika sehemu ya pili ya ushuhuda huu, niliandika kwamba; nilipoona idadi ya wanaoingia ni ndogo kuliko wingi wa watu wanaojiita wameokoka (yaani watu 7 kati ya 5,000), nilinilia na kuhoji kuwa mbona wachache hivi?😥. Pia nilipogundua kuwa wengi wa waliokufa tukidhani wameingia, kumbe hawakukidhi viwango vya kuingia, pia nilihoji wameenda wapi?🙇🏾‍♀.

🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

Katika awamu hii, Mungu alitaka kunijibu wako wapi niliowatafuta. Ukweli ni kwamba katika mambo yote, jambo ambalo nilipiga magoti na kuomba lisitokee ni habari kwenda kuzimu 😢😢. Niliomba sana nisipelekwe huko, kulingana na moyo wangu kuogopa, baada ya kusikia kunavyotisha. Lakini wajua atakalo Bwana yeye atatenda kwa utukufu wake (Zaburi 115:3).

Ilikuwa zamu nyingine tena! Hakukuwa na mazingira ya mawasiliano kati yangu na mbinguni. Siku hiyo kulikuwa na kukumbushwa kwingi, kuwa mbona nimenyamaza sifanyi kitu kuhusu nilichoona? Mbona siwaambii watu juu ya maono haya?. Ni kweli nilikuwa kimya tangu nianze kuona, ni watu wa karibu tu na walioamini ndio nilijaribu kuwajulisha. Na nikajiambia kuwa nitafute pesa, niende redioni nikalipie kipindi kisha nishuhudie. Kumbe kwa kuwaza hayo, nilikuwa nachelewesha kusudi la Mungu. Kwa hiyo mazingira ya kupelekwa kuzimu, hayakuwa na maandalizi, na ninajua Bwana alijua sitakuwa tayari kwenda. Hivyo nilijikuta tu tayari nipo sehemu ya ajabu!. Haina uhai kabisa, ni rangi kama jangwa na hakuna nuru ya jua. Kiuhalisia panatisha tu japo sikuona chochote kwa hatua ya kwanza, niliona tu ukiwa umejaa pale na niko peke yangu!. Nilishaogopa mbona niko hapa? Ghafla ndio nikashangaa kuona nakusikia vilio vya ajabu kugeuka naona ni moto umetapakaa hata sikuona mwisho wake!. Tayari nikajua, niko sehemu nisiyoipenda kuliko zote, na sitaki kuendelea kutazama wala kujua. Ila ole wangu!, Nilichukua mikono yangu nikauficha uso wangu na macho nikafumba🙈. Sitaki kuona haya! Sitaki kuona haya!🤦🏽‍♀ ndicho kilikuwa kilio changu. Ndipo nikasikia sauti ikitoka juu tena, na mimi niko bondeni pakutisha. Sauti ilikuwa ya kutisha na kali, si kama siku zingine. Iliniambia kwa lugha ya kiroho ambayo sijawahi kuisikia duniani wala popote. Ajabu ni kwamba, nilikuwa naielewa vizuri ile sauti ilichomanisha!. Iliniambia, *_"Nimekuleta hapa uone watu wangu wanaishia huku, na wewe nimekutuma kwao ungali umenyamaza!"_*. Nilikuwa sina tena uwezo wa kuzuia macho, ila naona sasa moto umewashikilia watu, ndani kuna vilio vyakutisha! visivyovumilika!. Na sauti za watu wengi zilikuwa za Wakristo, kwani walikuwa  wakilia kwa lugha za kikristo. Wengine walimtaja Bwana, yaani unaweza kujua kuwa hawa wanaolia wengi walimjua Yesu, na wengi waliishi katika vipawa na karama zake (walitambulika hivyo)!. Sikuvumilia sana sauti ile iliponikemea, nilikuwa tayari moyo wangu umeyeyuka kwa toba, nikitamani nitolewe pale haraka na nijikute duniani, ili naanze kazi mara moja!.

NB:-
*MOTO ULE ULIKUWA NA UWEZO WA KUMRUSHA-RUSHA MTU KAMA MPIRA 🏀 🏉 ⛹️, UNAMPELEKA MPAKA CHINI SANA NA KUMWIBUA TENA JUU, INATISHA SANA*

🔥 Lakini kati ya wengi walio kule, ni kwa sababu ya *roho ya mazoea*. Walizoelea Ukristo wao, wakaishi bila badiliko hadi mauti ikawakuta. Kweli usifanye mchezo kuzimu hata kwa matembezi hapafai, ni sehemu ya kutisha! Ni makao ya mauti, mwenye uhai huwezi vumilia. Acha kuuchezea wokovu wako, utaangamia siku usiyodhani. Nilipotoka hapo, nilirudi nikiwa nimepata majibu kuwa kweli tusijifariji na jina la Ukristo. Tukumbuke ilivyoandikwa, *_"Si wote waniitao Bwana! Bwana!, watakaoingia katika ufalme wangu"_* (Mathayo 7:21).

Namshukuru sana Bwana Yesu, hakuniingiza ndani huko ninakosikia wengine huingia, naamini alisikia maombi yangu nilipoomba. Pia atakuwa anaujua moyo wangu ulivyo, kwani hakika mimi ni mwanamke wa machozi😭😭. Mara nyingi nalilia kanisa, hata ninapoona vitu tu vya kawaida vyaniumiza sana.
Nilirudishwa tena duniani nikiwa na picha hii ya kutisha! Nilipata shida sana kutwa nzima, mimi nateswa na zile picha za haya maono. Niliingiwa huruma sana juu ya wakristo wenzangu, hata tunapokuwa pamoja nawatazama kwa huruma nikisema, _"Bwana msaidie huyu asiende kule nilikoona"_. Na ilikuwa, nikisikia Mkristo kafa au mtu kafa, mimi nikienda msibani nahangaika, nitafuatilia kwa ukaribu kwa familia ya marehemu hata kama sina ukaribu nao. Na nitamani kujua hatua za mwisho za huyo mtu alipoondoka duniani, Je! aliondokaje?. Nikiambiwa aliumwa na akafa, maelezo yakaonyesha hakupata toba ya kweli, naanza kulia kwa uchungu, hata hao ndugu wa marehemu watanishangaa (kwa sababu si mhusika wa karibu, lakini siri ya moyo ni nzito najua tayari kaenda kwenye sehemu ile). Na ilipotokea nimeenda msibani, nikafuatilia habari, nikaambiwa mazingira ya kifo cha huyo mtu kilikuwa cha usafi na utakatifu, nilikuwa nashukuru nakupata amani. Nilikuwa natembea duniani lakini mawazo yangu nitofauti, na ninaweza lia peke yangu hata njiani. Nikiona binti kavaa vibaya  👙👗👖, naogopa kuwa akifa hivi alivyo ataenda kule 😥.  .Nilikuwa nikijitahidi kumsimamisha kila mtu, nikimwambia habari za Yesu, ili atubu asiende kule kuzimu. Nilikuwa nahubiri kwenye daladala, masokoni n.k nilikuwa na mzigo mzito! Nikimhurumia kila mtu hata mme wangu! Nikawa nashangaa watu wana amani tu, wanatembea, wanaangalia TV, Wanafurahi. Mimi nikaona kuwa hawajui hatari iliyoko mbele yao. Bwana wasaidie! 😪🙌🏾.

Nikafika mahala mzigo huu ukawa mzito kwangu😭😭. Nikapiga magoti nikalia kwa sauti kuu ndani yangu, "Bwana nihurumie, maisha haya nimagumu kwangu. Nisaidie niishi duniani kama wengine maana nateseka, sina amani muda wote ninapowaona wanadamu, hasa wenye dhambi!. Naumia, nitaishi mpaka lini nikiteseka! 😣 Mbona wenzangu wanaishi kawaida! Hawajali!. Mimi nawahubiria wengine wananicheka, na kunidhihaki!. Hali hii ilinichochochea sana kuhubiri mitaan nk. Ila badae Mungu alianza kunipunguzia mzigo kidogo; japo mpaka sasa sipendi kusikia mwizi kachomwa moto; mtu kauawa ovyo, au mkristo kafa kifo cha ghafla. Naumia, nakumbuka makali ya moto ule na sehemu ile mbaya yakutisha!! Kweli sitaki mwanadamu aende kule😭 usikubali kushindwa, jitahidi, nakulilia mtu wa Mungu 😭😭😭. Nakuombolezea usiende kule, Kristo hataki tupotee. Badili mwenendo wako, acha dhambi, mizaha, mazoea, nk. Maanisha katika wokovu wako.

Asanteni 🙏🏾, wenu Mchungaji Mariamartha C. Kailembo.
Mjumbe wa uamsho. Amka amka ewe ulalaye... (Efeso 5:14, Yona 1:6)

Mhariri: Mwl Proo

Tuesday, July 17, 2018

ROHO YA MWANADAMU KUWEZESHWA!

*ILI ROHO YA MWANADAMU IWEZE KUTENDA KAZI KWA VIWANGO VYA JUU, NA KATIKA LIMWENGU ZA KIROHO;  SHARTI IWEZESHWE*

*_Human spirits are to be enhanced, for them to operate in higher dimensions, and in some spiritual realms_*

*ʍաӀ Թɾօօ*
+255762879363
+255718922662

*YALIYOMO/CONTENTS*

1⃣ *UTANGULIZI*
2⃣ *KANUNI YA UUMBAJI/CREATION AND ITS ORDER*
💿Roho za mbinguni
-Maserafi
-Makerubi
-Ofanini
-Malaika
💿 Malaika waasi & Mapepo (Majini)
💿 Roho za wanadamu
3⃣ *TAFSIRI YA ALAMA ZA LUGHA YA ROHO (ENCODING/DECODING OF THE SPIRITUAL LANGUAGE)*
💿 Kwa nini lugha ya kiroho ni ya mafumbo?
4⃣ *NAMNA GANI ROHO INAWEZA KUWEZESHWA/WHAT TO DO, SO AS TO RECEIVE THIS ABILITY?*

1⃣ *UTANGULIZI*

Haleluya kwa BWANA, Mpendwa unayefuatilia mafundisho ya rohoni ya Mwl Proo, ili kuongeza maarifa na ufahamu wa rohoni sasa tumefikia mahali pazuri pa kuchimbua vilindi (depths) vya kiroho. Zaburi 42:7 inasema 👉🏾 *Deep calls to deep*, waliotasfiri kiswahili hususani (SUV), wameandika "Kilindi chapigia kelele kilindi", haijanoga sana, lakini ili kuyapata ya kilindini sharti uwe kilindini; ukiwa kilindini, kilindi chenyewe kitayaita yanayopatikana huko vilindini. Hivyo nakukaribisha upate mlo wa kilindini, sio watu wote somo hili laweza kuwafaa (Ebrania 5:12-14). Kama mtu hajazoea kusoma documents zenye vitu vya kiroho sana, au hana uzoefu wa kiroho (personal spiritual experiences), anaweza  kutatizika. Nakushauri usome kama unapenda maarifa, kama unatamani kuwa na maisha ya kiroho binafsi yenye uzoefu wa kiroho mara nyingi, hakikisha unasoma. Kama unatamani kutumika kwa viwango vya juu vya kiroho katika safari yako ya utumishi, jenga msingi huu mapema, hakikisha unasoma sasa neno kwa neno. Na kama unaona bora uishi tu *ordinarily/kwa kawaida*, unaenjoy kuwa *church goer* pekee, huna vitu vya kiroho vya kuonesha unatembea na Mungu kwa viwango, basi fanya kuliacha. Nimeweka mawasiliano yangu ili jambo lisiloeleweka niulizwe. Tazama haya nimeyapeleleza ndivyo yalivyo, yasikie, uyajue, ili upate mema (Ayubu 5:27).
KARIBU

2⃣ *KANUNI YA UUMBAJI (CREATION & ITS ORDER*

🎴 *Leo natamani kwa sehemu tufahamu siri hizi za uumbaji. Najua desturi zetu za kujifunza zilitufunga namna yetu yakujifunza haikutupa kufahamu baadhi ya vitu. Mfano watu wengi wanaelewa mbinguni Mungu aliumba malaika tu, kumbe kwa viumbe vya mbinguni malaika ni moja tu viumbe wengi, na malaika nao waliumbwa wa aina nyingi.*

🎴 Uumbaji kilikuwa kitu cha rohoni zaidi kuliko huku nje, yaani Mungu ambaye ni Roho alikuwa amekwisha umba vingi rohoni kabla ya udhihirisho wake huku nje. Mfano wanaosoma vyanzo kadha wa kadha vya kiyahudi, wanaweza kujua hata wanyama ambao tunasoma literally katika Mwanzo 2:19-20, kuwa Adamu alietewa awape majina, tayari walikuwa na majina hayo katika roho, Adam kwa roho ya ufahamu aliweza kuyataja majina yao, 👉🏾 *_"and whatsoever Adam called every living creature, that was the name thereof"_* (Mstari wa 19b). Alikuwa akimwona 🦒, anamjua huyu ni twiga, akimtaja jina lake likawa ndilo hilohilo. Kabla ya Mtu kula tunda, aliona na kufahamu mambo kiroho zaidi ya kimwili (Mwanzo 3:6). Sasa Mungu ambaye ni roho aliumba roho kwa makundi mawili; roho za mbinguni na roho za duniani 👉🏾 {celestial spirits/spirits of heaven & terrestrial/earthly spirits}. Roho hizi zinatofautiana sana uwezo kulingana na matumizi na kusudi la kuumbwa kwake. Viumbe hivi vya roho viliumbwa vikiwa namna yake ya asili na utukufu *(proper domain/code of creation).*

🎴 Viumbe hivi haviwezi fanya kazi ambazo havikuumbiwa, au havikuwekewa uwezo husika muda wa kuumbwa kwake. Ni kama ambavyo Mbuni/Ostrich ni ndege, ila sio ndege wa angani, sio kwamba ni mzembe kuruka ila hiyo ndiyo *proper domain* ya kuumbwa kwake, hata kama kutatokea dharula akaruka kwa umbali fulani, atatua akiwa kachoka na maumivi tele, wakati ndege wengine wanaweza safiri wakahama nchi kabisa 👉🏾 🦅 🦅 🦅. Hivyo sasa roho au viumbe wa rohoni waliumbwa wakiwa na uwezo wa mambo kadhaa *(built-in abilities)*, mwanadamu naye ni roho kama viumbe vile vya rohoni, ila roho ya mwanadamu haikuwezeshwa kwa uwezo sawa na viumbe vya rohoni. Roho yake iliwekewa limitations/vizuizi kwa sababu ali-dizainiwa kama *terrestrial spirit* akae ndani ya mwili aishi duniani (Zaburi 115:16).

*I.) VIUMBE VYA ROHO ZA MBINGUNI*
_(spiritual creatures )_

Kama leo utapata neema ya kutwaliwa kwenda mbinguni kiroho (translated by the Spirit to heaven), haya utayakuta hivi. Katika kiti cha enzi cha Mungu 💺, kuna wanaomzunguka kwa order maalum (Zaburi 89:7). Mungu aliumba Maserafi (Seraphs/Seraphim), Makerubi (Cherubs/Cherubim), Ofanini (Ophanin), Malaika (Malaika wakuu/archangels, Malaika walinzi/Watchers of heaven, malaika wakuu wa miji ya dunia, Malaika walezi/walinzi wa watu (Guardian Angels), haya ni makundi makuu ya viumbe wa mbinguni (spirits of heaven) aliowafanya Mungu, hilo baraza la watakatifu hawakuumbwa mbinguni, ni wanadamu wachache waliowahi kutembea na Mungu kwa kiwango cha juu sana wakiwa duniani, wakainuliwa mpaka mbingu ya tatu wakapewa kusimama karibu kabisa na Mungu (Zechariah 3:7), wako ambao mimi Mwl Proo nafahamu wapo, ila sitawataja hapa kwa sababu watu wanaweza kuhoji chanzo cha taarifa, na ni cha ajabu hivyo tuendelee katika kuchambua kundi moja baada ya jingine.

🧚🏻‍♂ *MASERAFI/SERAPHIM*

🎴 Hii ndio inayosadikiwa na vyanzo vingi vya kiyahudi, kuwa ndiyo rank/cheo ya juu ya viumbe vya roho vya mbinguni. Niseme mambo kadhaa, mimi pia kwa roho ya ufahamu nimejua kwa kufunuliwa kuwa hawa ndio rank ya juu kabisa (Efeso 3:3). Nilipokuwa nikisoma Biblia nikakuta ni nabii mmoja tu Isaya (Isaya 6:2, 6), ndiye amewataja hawa Maserafi. Sifa alizozitaja zimewatofautisha na viumbe wengine, sifa moja kuu ni mabawa sita. Ezekiel aliona viumbe hawa wa mbinguni, lakini aliowaona walikuwa na mabawa manne (Ezekiel 10:21), na akaweka wazi kuwa ni Makerubi, Sifa za Makerubi katika Ezekiel wanafanana na wenye uhai wanne katika Ufunuo wa Yohana, lakini idadi ya mabawa ya wale viumbe katika Ufunuo 4:8 ni mabawa sita kama Maserafi. Mungu alinipa siri ya hawa maserafi kutotajwa sana katika maandiko, kwamba hakuwaumba kwa ajili ya dunia, wala kuhudumia wanadamu, nafasi yao haina uhitaji hata kutembelea dunia, hakuna mtu anaweza kuona Serafi asipokuwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, unaweza kuwaona kama umemwona Mungu, maana wao wapo juu ya kiti cha enzi 👉🏾 💺 (Isaya 6:2), Sio kwamba wamekikalia, La! Hasha! Hivyo hutasikia katika maandiko wala katika shuhuda zozote mtu kuona maserafi nje ya pale katika kiti cha enzi, hiyo ndiyo sababu kuu ya kutowaona katika simulizi zozote za dini ya kiyahudi. Kwa ujumla hawako involved kwa human affairs, kilichomfanya Serafi mmoja ahusike kutwaa koleo na kuchukua kaa la mawe toka katika madhabahu iliyo mbele ya kiti cha enzi, ni kwa kuwa huyu visitor Isaya Ben' AmoZ kafika pale akiwa hana viwango, lakini hawa hwahusiku na kuhudumia wanadamu (That's their proper domain).

🧚🏻‍♂ *MAKERUBI/CHERUBIM*

🎴 Hii ni aina ya pili ya viumbe vya roho vy mbinguni. Hawa wametajwa sana katika maandiko tangu kitabu cha Mwanzo mpaka vitabu manabii. Maandiko zaidi ya matano katik Biblia yameandikwa, "Wewe ndiwe Mungu uketiye juu ya makerubi". Ambapo katika kingereza pameandikwa *Between the cherubim*, hivyo unaweza pata mpangilio mzuri wa pale kwenye kiti cha enzi. Katika desturi za kiyahudi (Jewish traditions) hawa walijulikana sana, ni wazi kwamba kulikuwa na wengi katika mababa wa taifa la Israel waliwahi kuwa na experience ya kuwaona. Hata Musa alipopokea maelekezo namna ya ku-design Patakatifu pa patakatifu (Most Holy Place) ndani ya hema ya kukutania na kutengeneza makerubi (model cherubs) hakushangaa yeye wala waisrael, maana walijua hivyo viumbe vya mbinguni. Sasa viumbe hawa wanaweza kuhusika na mambo mengi tu ya wanadamu. Na Biblia inatuthibitishia hilo, kerubi aliwekwa ku-block path/entrance 🧚🏻‍♂🗡 ya njia ya kimwili (physical) inayoungana na ya ulimwengu roho kuiingia Eden bustani ya Mungu (Kuna siri nyingi hapo, hata kama Adamu au watoto wake wangetamani kurudi Eden waichungulie, wasingeiona hata bila hata yule kerubi kuwakata kwa panga).

🎴 Huyu ambaye anaitwa Mwovu, Ibilisi na Shetani hakuumbwa kwa lile daraja la juu la Maserafi, yeye alikuwa katika kundi hili la pili la Makerubi (Ezekiel 28:14). Aliumbwa akawa in charge wa majukumu kadha wa kadha ya mbinguni na duniani (Isaya 14:13-5). Ikumbukwe yale niliyoelezea katika somo lililopita kuwa sura hizi zinaongelea miji ya Tiro na Sidoni, na taifa la Babel, lakini nilieleza kwa namna gani imehusianishwa na Shetani, jitahidi upate somo lisemalo *NENO LA MUNGU NI UFUNUO*,

🎴 Pia tumeona maumbile yao hawa kama walivyoelezewa na Ezekiel (Ezekiel 10:10-21), sura zao, miili yao, mikono yao, idadi ya mabawa, idadi ya macho na kila kitu. Ila pia wanaweza kutokea wakiwa wamebadilika maumbile.

*NB*
*_VIUMBE HAWA WA ROHO ZA MBINGUNI (SPIRITS OF HEAVEN), WANAO UWEZO WA KUCHUKUA MAUMBILE MENGINE KATIKA UUMBAJI WA MUNGU, WAKAJIVIKA MIILI HIYO KWA MAKUSUDI FULANI (INCARNATION), HII NI ~BUILT-IN ABILITY~ KWA VIUMBE VYA ROHO WA ASILI YA KUWA ROHO ZA MBINGUNI, NDICHO HASA ALICHOKIFANYA SHETANI KATIKA MWANZO 3:1, INGAWA KWA ASILI YAKE HANA UMBO LA NYOKA (UFUNUO 12:7-12 IMEZINGATIWA), SHIKA HII TUTAITUMIA HUKO MBELE_*

🎴 Shetani katika ule mpango wake kuwaza kumpindua Mungu, hakushawishi Serafi hata mmoja, naam hakushawishi hata makerubi wenzake, kama alijaribu kushawishi hakumpata hata mmoja, alishawishi malaika ambalo ni daraja la chini zaidi (Ufunuo 12:4). Kama kungekuwa na Makerubi kadhaa ambao wangeungana naye basi kungekuwa Shetani wakuu kadhaa, maana wangelingana mengi na hao wengine. Najua unahoji kitu hapo, kwamba hawa sio malaika? twende polepole utayaelewa haya vyema.

🧚🏻‍♂ *OPHANIN (THE WHEELS)*

🎴 Hili ni kundi la tatu la viumbe wa roho za mbinguni, maana ya jina lao ni Magurudumu. Kwenye Biblia wametajwa kwa kificho kidogo, lakini katika maandiko ya kale ya kiyahudi (Ancient Jewish Writings) wametajwa sana. Sasa katika Ezekiel 10, hii Annunciation ya hapa ilihusisha kutembelewa na makundi haya mawili ya viumbe vya rohoni. Tusome maandiko haya hapa chini :-

*(Ezekieli 10 )*
------------
*13 Na magurudumu hayo yaliitwa Kisulisuli, nami nalisikia.*

*14 Kila mmoja alikuwa na nyuso nne; uso wa kwanza ulikuwa uso wa 🧚🏻‍♂  kerubi, na uso wa pili ulikuwa uso wa  🧑🏻 mwanadamu, na uso wa tatu ulikuwa uso wa 🦁 simba, na uso wa nne ulikuwa uso wa 🦅 tai.*
...
*16 Na makerubi walipokwenda, magurudumu yale yalikwenda kando yao; na makerubi walipoinua mabawa yao, wapate kupaa juu kutoka katika dunia, magurudumu yale hayakugeuka wala kutoka kando yao.*

Mstari wa 14, umeongeza kitu cha ajabu, katika Ufunuo sura ya 4, wenye uhai wanne wako exactly sawa na Makerubi, wa Ezekiel 10, lakini kule aliona uso wa nne ni wa ndama, huyu sura hiyo ameona ni ya kerubi. Sasa ukisoma kwa kurudiarudia hapa unagundua hapa kulikuwa na viumbe vya aina mbili, Makerubi na Maofanini (The wheels), ambao katika vitabu vingine vya kiyahudi wameelezewa na kutajwa sana.

🧚🏻‍♂ *MALAIKA/ANGELS*🧚🏻‍♂

🎴 Tunao msingi mmoja wenye makosa, nao ni kujiongeza wenyewe kuwa hao wote ni malaika, hiyo ni hatua ya kwanza kabisa ya uelewa kwamba viumbe vyote vya mbinguni ni malaika (malaika). Kwa mfano Maserafi ni Maserafi wala sio Maserafi ni Malaika, Biblia haisemi kamwe wala vitabu vingine vya kale, ni sisi tuliamua ku-generalize kuwa wote ni malaika tu, na baadhi ya watumishi katika kujaribu kusaidia uelewa, wakaamua kusema ni aina mbalimbali za malaika. Ingawa ukisema Serafi ni malaika umemshusha cheo kwa mujibu wa ile order of creation, yeye ameumbwa kama Serafi, kama Kerubi na sio malaika, wala viumbe hao hawafanani na malaika kwa mengi sanaaaaaa. Sasa malaika wako wa aina nyingi....

✍🏼  *MALAIKA WAKUU (ARCHANGELS)*

Wayahudi walitoka Babel na majina mengi ya malaika, lakini pia katika maandiko ya kiyahudi ya kale, yanataja malaika wakuu saba, kumbuka katika Daniel 10:13, Gabriel anamwambia Daniel kwamba akaja Mikael mmoja wa wakuu wasimamao mbele, kunisaidia. Hao wakuu tangu mwanzo ni hawa Anael, Gabriel, Mikaeli,, Raphael, Zakariel, Samael na Orifiel.

✍🏼 *MAJESHI YA MALAIKA/ARMIES*
🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂
🗡⚔🗡⚔🗡⚔💣💣💣🔥🔥
🎴 (Mathayo 26:53, 2Falme 6:14ff). BWANA YHWH anaitwa Bwana wa majeshi, anayo majeshi kama nilivyoeleza katika masomo yale (USHINDANI WA ROHONI & VITA VYA ROHONI, jitahidi uyapate hayo nimeyaandika mimi Mwl Proo). Sio malaika wote wanahusika na vita (battles), ndio maana kuna watu walistushwa na ule ushuhuda wa mwinjilisti wa Uganda kuwa katika matuo ya wakuu wa giza, walikuwa wanaweza hata kumteka malaika (hususani guardian angels, mimi hilo sishangai maana najua yaliyoko huko). Malaika wa kundi hili wako chini ya Mikaeli (ambaye jina lake lina maana ya "Kama Mungu"), wote wanapokea orders/instructions toka Mikaeli, kiasi cha kufanya waitwe malaika zake (Ufunuo 12:7-11), kama ambavyo malaika waliomcha Shetani huitwa malaika zake. Ukisoma katika maandiko majeshi ya BWANA, au matuo ya Bwana (forces of the LORD), inazungumzia kundi hili la malaika. Hawa wote mpaka mwonekano wao wako muscularly strong 💪🏾🗡 (always wako na drawn sword kwa mikono yao), hawa hutumwa mara kwa mara kulingana na ukubwa vita inayomkabili mtu au kanisa n.k, na kuna vita zingine wanapigana tu huko rohoni, (there is unceasing wrestling of spiritual forces kule rohoni, ni wachache wanaelewa haya, ndio maana watu wa Mungu hawapaswi kuacha kuomba siku zote day & night).

✍🏼 *WALINZI WA MBINGU (WATCHERS)*
🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂

🎴 Hili ni kundi jingine la malaika, ni tofauti kidogo na majeshi yale yaliyo chini ya Mikael ambayo specifically wao ni kwa ajili ya ushindani wa kivita. Hawa nao ni spirits of heaven, kama unasoma documents za kale, utakuwa umewahi kutana na visa vya hawa. Kwa mfano wale malaika 200 walioshuka katika mlima Hermoni zama zile za Vizazi vya mwanzoni baada ya Adamu, wakaingia kwa wanawake wa kibinadamu ni kundi hili hapa la *Watchers of Heaven*, waliongozwa na kiongozi wao Semjaza/Samyaza.

✍🏼 *MALAIKA WAKUU WA MIJI (PRINCES)*
🎴 Ufalme wa Mungu umejidhatiti kwa namna ya ajabu sana. Miji yote ina malaika/Prince(s), wa kuuchunga, na kama kuna mambo yoyote ya makusudi ya Mungu yanapaswa kutekelezwa basi yeye yuko in charge kwa kazi hizo. Yaani watu wa Mungu walipaswa kuwa na kiwango cha kutembea na Mungu kiasi cha kuweza kuwaona na kuwajua hawa. Nimefurahia ushuhuda wa Prophet Sadhu Selvaraj, akiwa Airport moja huko Marekani anasubiria flight ✈, akahisi kuna uwepo wa kiumbe karibu yake, akageuka na tazama kuna malaika yuko Giant mwenye upanga uliofutwa, akajitambulisha _*"I'm the Prince of this city"*_, na akamwonesha maeneo ambayo yatapatwa na tetemeko, ambapo Bwana Yesu alikuwa amekwisha mwonya mbele juu ya mji huo na uharibifu utakao tokea. Tusome maandiko

*(Ezekieli 9 )*
------------
_*1 Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake.*_
*_2 Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba._*

👆🏽👆🏽👆🏽👆🏽 These are angelic beings aliowaona Ezekiel, wametajwa kazi yao kuu ni kuusimamia mji. Kama kuna kusudi lolote la Mungu la kutekelezwa katika mji liwe baya au zuri, hawa watahusika kwanza.

✍🏼 *MALAIKA WALINZI/WALEZI WA WATU (GUARDIAN ANGELS*

🎴 Hili ni kundi jingine la malaika, hawa sasa wako so much involved na mambo ya wanadamu, ni Guardians, kama bodyguards hivi, wako kwa kila mwamini at least one. Wako kama reporters/wapelekao habari zetu kwa Bwana, uhusika na kuchukua majibu ya maombi katika kiti cha enzi na kumfikishia mhusika.

*_"Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni."_*
(Mathayo 18:10)

Unaweza kuona, wametajwa hapa malaika wao (guardian angels), wamakuwa na mtu, na kuna muda wao maalum hupeleka reports kwa Baba. katika Mhubiri 5:6, anaposema usimwambie huyo malaika kuwa umepitiliwa tu kufanya kosa fulani, anazungumzia guardian angels,na watu wa Mungu wanapaswa katika kiwango hata cha kuwaona hawa hata kamasio wakati wote.

*II MALAIKA WAASI NA MAPEPO/MAJINI*
🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂ versus 👹👹👹👹

🎴 Naomba kuweka sawa hoja kadhaa ambazo haziko sahihi, zinapishana na maandiko yaliyotangulia. Malaika waasi sio majini/mapepo wabaya hawa tunaowakemea watoke kwenye miili ya watu. Malaika waasi toka Mwanzo mpaka Ufunuo jina lao ni hilo Malaika waasi au Malaika za Shetani, na sio pepo wabaya/waovu. Malaika walioasi na Shetani wako katika maumbile yao ya asili 🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂🧚🏻‍♂, wamekosa utukufu wa Mungu tu maana wamejitenga na chanzo cha utukufu wao. Hawana masura hayo ya kutisha na mapembe 👹👹👹, wao kuna namna nyingi hawana tofauti na malaika walio watakatifu kwa Mungu, ukiacha na swala la utukufu wa Mungu ambao hawana. Tusome maandiko

*_"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."_*
(Waefeso 6:12)

👆🏽👆🏽👆🏽👆🏽 Hizi ranks za utawala wa Shetani, Mwovu, zimeainisha kitu cha muhimu sana.

1. Falme na Mamlaka
2. Wakuu wa giza/anga
3. Majeshi ya pepo wabaya

✍🏼 Sasa hizo ranks mbili za kwanza ni malaika waasi walioamua kushawishika na uasi wa Shetani juu ya Mungu, na yeye Shetani kawaweka kwa vyeo vya juu, anga ya mkoa mzima inaweza kuwa na mkuu wa giza mmoja na akachachafya kwelikweli, chini yake kutakuwa na majeshi ya pepo wabaya. Narudia tena malaika waasi sio hawa mapepo wabaya/waovu.

*PEPO  WABAYA WALITOKA WAPI??*

👹👹👹👹👹👹👹👹👹👹
Hili ni swali la muhimu sasa kwetu. Jibu moja linakubaliwa na vyanzo vya kale vyote ni hili, *mapepo wabaya ni roho za wanefili waliokufa (spirits of dead nephilims)*, hili linathibitishwa na the Jubilee, The Book of Jasher, The Book of Enoch etc. Ukikutana na myahudi mkristo, ukamwambia pepo wabaya ni malaika walioasi ataona unafanya comedy.  Tusome kidogo andiko hili;

_*8. Now the giants, who lave been born of spirit and of flesh, shall be called upon earth evil spirits, and on earth shall be their habitation. Evil spirits shall proceed from their flesh, because they were created from above; from the holy Watchers was their beginning and primary foundation. Evil spirits shall they be upon earth, and the spirits of the wicked shall they be called. The habitation of the spirits of heaven shall be in heaven; but upon earth shall be the habitation of terrestrial spirits, who are born on earth 9. The spirits of the giants shall be like clouds, which shall oppress, corrupt, fall, contend, and bruise upon earth.  (Enoch 15:8-9)*_

👉🏾 🧚🏻‍♂ Malaika walioasi hawaitamani miili ya wanadamu, wao hawana shida ya habitations.

👉🏾 👹 Pepo wabaya ndio wenye uhitaji na makao/habitation, maana wao walipoteza ya kwao. Baba zao wanefili ambao ni malaika walioacha makao yao *Proper domain* waliyoumbiwa walikamatwa na kufungwa katika *Tartarus*(Underground gloomy dungeon) Soma 👉🏾 2Perto 4:4, Yuda 1:6, Enoch chapters 7-9. Hawa malaika waliofungiwa hapa sio wale walioasi na Shetani, wale hakuna aliyefungwa, na muda wao bado kabisa. Sasa roho za wale wanefili ambazo ni products ya spirits of heaven kuungana na terrestrial spirits ndizo zikaitwa pepo waovu. Hazina kikao (habitation), wao ndio hawa tunaokemea watoke kwenye miili ya watu. Malaika waasi wao kama managing directors watahakikisha wanawakosesha wanadamu ili kuruhusu hawa mapepo sasa yawaingie, ila sio wao. Ndio maana vyanzo vya kle vinakubaliana katika hili kuwa hakukuwahi kuna pepo wabaya (demons) kabla ya gharika ya Nuhu. Pepo hawa ambao hawakuwa katika ratiba za uumbaji wa Mungu bali ni matokeo ya makosa ya malaika, wanasifa kadha wa kadha, mfano wanao uwezi wa kuji-multiply kiidadi.

👉🏾 Hizi roho za kipepo (demonic spirits), hazina sifa za roho za mbinguni kwa 100% ila their foundation is of heaven. Hazina ulinganifu na roho za wanadamu, na ndio maana hazina makao. Roho za wanadamu waliokufa kwa gharika kuna mahali zimehifadhiwa, ila hizi hazikustahili kwenda hata kule.

👉🏾 Wanefili wali-express tabia zote za hawa pepo wachafu wakiwa katika miili yao. Walileta kila ubaya, wali-exhaust chakula cha wanadamu, wakaanza kula mpaka wanadamu. Walitenda dhambi juu ya wanadamu, haikutosha wakaanza kuwaingilia hata wanyama, waliidhuru hata mimea, hakuna kilichobakia salama. Sasa gharika iliua wanadamu wote kasoro nane tu, na wanefili waliuawa, ila roho zao sasa zikawa pepo wabaya (Eno 15:8-9). Na kinachotokea ni nini, hizi roho zao zinatamani ku-express zile tabia zao, lakini they cannot kwa kuwa hawana miili chombo cha kuruhusu utendaji duniani. Hivyo mapepo yatafanya kila linalowezekana yapate makao ndani ya mwili wa kiumbe hai hususani mwanadamu, ili yapate fursa ya kufanya yao. Tabia zinazofanywa na wanaomilikiwa na pepo ni zilezile zilizokuwa zikifanywa na wale majitu na kuzidi sana.

👉🏾 👹👹 wanaweza kujivika sura tofautitofauti, lakini haya masura ya ajabuajabu ndiyo ya kwao, maana roho hizi sio wale malaika waliowahi kumtumikia Mungu mbinguni. Kuna jambo moja lisilojulikana sana kwa wasomaji wa Biblia pekee, nyakati za yale majitu kulitokea viumbe ambao ni *hybrid*, waliokuwa ni mchanganyiko wa species za wao majitu na wanyama, na watu etc etc, ikatoa viumbe hata majina hawana, wana maumbile ya ajabu ajabu. Na sehemu kubwa ya mapepo hupenda kuchukua sura zile za viumbe visivyoeleweka. Mimi nilipata kuona pepo kwa macho ya roho kwa ghafla nikiwa bwenini miaka 14 iliyopita, lilitokea dude kubwa lenye mikia kama pweza pande zote, likapotea kupitia ceiling board. Pepo wachafu (ambao kiarabu ni Jinn/Majini) wanazosifa zingine nyingi ambazo sitapenda kuweka hapa kwa sasa, maana hatupaswi kuyajua haya kuliko tunavyojua mambo ya upande wa nuru.

*III ROHO ZA WANADAMU*

🎴 Naweza kusema hapa ni mwanzo wa moyo wa somo. Leo tupate ujuzi huu, ili tuweze kuishi kwa standard sahihi tungali hai hapa duniani. Roho ya mwanadamu iliumbwa kwa namna ya roho zingine, lakini haikupewa uwezo sawa na roho za mbinguni. Pia roho ya mwanadamu inapokuwa ndani ya mwili wa udongo inakuwa kama imefunikizwa fulani, na kushindwa ku-opereti kama roho kwa 100%, ikiweza kuushiriki ulimwengu wa roho basi ni kwa njia ya maono, ndoto au roho kuondoka (sio kwa kifo), na hapa kuna namna nyingi kama nilivyoelezea katika somo langu la *MWILI WA ROHO*, nimeliandika mimi Mwl Proo, waweza kulipata. Hivyo roho za wanadamu zinahitajika kuwezeshwa, ili kutenda kazi katika limwengu za kiroho na kuoperet kwa viwango vya juu hata kama iko ndani ya mwili wa udongo. Wengi wenu mnaweza kuogopa mambo ya roho kusafiri (levitate/astral travel), nami siji kukihimiza hicho, ila naelekeza kitu cha kibiblia kwa manufaa ya watu wa rohoni (1Korintho 2:14-15). Kuna viwango ukitaka kutenda kazi za kiroho lazima roho iwezeshwe (iwe enhanced/enabled). Mwanadamu anao mwili (unakua 👉🏾 GROWTH), anayo nafsi (inahitaji kujengwa 👉🏾 edification 1Kor 14:4), na anayo roho (hii inahitaji kuongezeka nguvu na kuwezeshwa 👉🏾 Luka 1:80, 2:40). Roho inaongezeka nguvu na kuwezeshwa, inaweza kuwa kwa Roho wa Mungu au kw uwezo wa kishetani (Mika 3:8). Mwanadamu anao uwezo wa kufanya mambo makubwa sana akiwa katika mwili,akaoparet kiroho, akaona vitu vya rohoni, akawasiliana na viumbe vya rohoni, anaweza kuhisi kila linaloendelea rohoni kwa roho yake iwapo imewezeshwa. *The Spirit enables spirits*, siku ambayo Mungu alinifundisha hili kwa Roho Mtakatifu, niliomba Mungu anipe experience ya hiki kitu kilivyo halisi. Tangu hapo nimekuwa na maombi ya kuomba jambo hili, tayari linafanya kazi kwa sehemu lakini bado kabisa shauku yangu ni kubwa. Siku nilipoomba Mungu aiwezeshe roho yangu ili niongezeke viwango vya kutenda kazi na kuenjoy maisha ya kiroho, niliweza kusikia majadiliano ya watu ambao wapo mbali sana. Nikiwa Dar es Salaam nilisikia mazungumzo ya watu ambao wapo Kagera, ni kama nipo katikati yao. Kuna siku moja baada ya kumaliza maombi ya usiku nikalala tena, na baada ya muda nikamwona adui ananishambulia na kujificha, kisha nikaona ni kama nipo pembeni ya mwili wangu na adui anaubana ule mwili, ila na mimi kwa roho yangu nahisi kule kubanwa, sema nilikwisha jua somo hili ninalo andika, hivyo nikiwa katika hali hiyo roho yangu iliomba, nikimsihi Mungu nitie nguvu roho yangu ili nimshughulikie yule adui, Mungu alijibu kwa kutenda, kwa sekunde chache yule  adui nilimsambaratisha kabisa. Ziko karama za Roho Mtakatifu zinaweza fanya kazi ndani ya mtu iwapo roho yake imewezeshwa. Unaweza kuangalia baadhi ya watumishi wa Mungu, ukaona kutenda kazi kwao kukakutatiza, kumbe roho zao ziko *enhanced* kutenda hayo. Roho ya mwanadamu ikiwezeshwa inampa mwanadamu huyu kuweza kutumia miliango ya fahamu ya kiroho zaidi, roho ina masikio, ina macho, ina ngozi etc. Mtu ambaye roho imewezeshwa anaweza kuingia mahali pepo mapepo akaya-sense kwa moyo tu, na kuna hatua mpaka kwa mwili. Muda wote tumezungukwa na tupo *exposed* kwa viumbe wa kiroho, wawe wema wa Mungu au wabaya wa Shetani, wapo tu wamejaa, shida ni macho ya kuwaona yamefumbwa, kwa sababu roho ikiwa ndani ya mwili wa udongo inakuwa limited/restricted. Lakini ikiwezeshwa unaweza ona vyote vya rohoni, malaika wakishuka unawaona, kwa hatua ya awali at least you sense their presence.

👉🏾 Namfahamu muhubiri ambaye muda wa kuhudumia wenye mahitaji, wale wagonjwa na wenye shida wote anawaona mara mbili, anamwona mtu wa mwilini na wa rohoni kwa pembeni. Kwa hiyo akiombea kiwete ♿, akisema *you're free*, anakuwa amemwona yule wa rohoni keshasimama. Namfahamu mhubiri ambaye akiwa anafundisha hata kama yuko ofisini kwake anawaona malaika waliopo muda huo hapo ofisini, idadi yao, mavazi yao na kila kitu. Macho ya roho yake yametiwa nuru (Efeso 1:18), wengi wanatenda kazi na malaika lakini hawajui kwa kuwaona wala kwa ku-sense. Roho ikiwezeshwa maisha ya kiroho yanakuwa matamu zaidi, kwa sababu hakuna jambo litatokea ukiwa hujalipata kabla hata kama ni mambo ya kawaida yasiyo ya kiroho ila yanagusa maisha yako na kuweza kuleta athari au matokeo fulani, lazima utayapata kabla, roho inayouwezo wa ku-sense uwepo wa ajali, kifo, ugonjwa unaokuja, kupoteza kitu, baraka inayokuja, hata kama mchana wa kesho kuna kosa utafanya roho inaweza kuli-sense kosa hilo siku moja kabla, labda uwe mpuuziaji tu. Ndio maana nahimiza juu ya roho kuwezeshwa kwa Roho wa Bwana.

3⃣ *TAFSIRI YA LUGHA ZA ROHO*

🎴 Mapenzi makamilifu ya Mungu ni kusema nasi waziwazi bila mafumbo (without riddles). Sasa lugha ya kinabii imejaa mafumbo ya alama (Symbols & Signs). Watu wakiona maono au ndoto au maono ya wazi, wanaona vitu kwa lugha ya mafumbo yenye alama au viwakilishi.

*NB:*
_*Vitu vya kiroho ni vya kiroho mwilini, lakini ni vya kimwili rohoni. Yaani pepo mchafu ni wa kiroho huku mwilini, haumwoni, lakini ukiingia rohoni lile pepo ni la kimwili unaweza kumwona na anaonekanaje kwa umbile.*_

🎴 Vitu vya rohoni vinawekewa alama *(Encoding)*, kwa sababu roho ikiwa katika mwili haiwezi kufanya kazi katika roho 100%, na hivyo huwezi yaona mambo kama yalivyo, bali taarifa zinakuwa *encoded*, na kazi kubwa inayotakiwa hapo ni ufahamu wa rohoni kwa Roho Mtakatifu uweze ku *decode*, yaani zile taarifa zilizokuja kwa uwakilisho wa alama za mafumbo kuzitafsiri tena kuwa taarifa. Nakumbuka nilikuwa kwenye Conference ya wanafunzi, mhubiri muda anataka kuhudumia vijana kwa maombi aliita mabinti, akiwa anamwuliza Roho wa Kristo awaombee nini, ghafla akaona katika roho 👉🏾🌙🌘 mwezi, akasema Roho ananionesha mwezi sijui ni nini, muda huohuo akapata tafsiri kuwa wadada waliofika pale wengi wanashida katika Menstrual Periods zao na kifungo cha kipepo kimekaa hapo. Alipoomba pepo wachafu wakapiga kelele wakikiri waliwashika matumbo ya uzazi kupitia siku zao za hedhi. Ona jinsi ambavyo isingewezekana aone sehemu ya wadada na shida yao ikoje, lakini taarifa imekuja ikiwa imefungwa kwa alama ya mwezi 👉🏾🌘🌙 (encoded) na roho iliyowezeshwa inaweza ku-decode ili kutafsiri hilo fumbo la alama. Ndivyo ilivyo kwa lugha zote za rohoni. Lakini roho ya mwanadamu ikiwa rohoni kwa zaidi ya 90% haioni mafumbo, inaona mambo katika uhalisia wake. Nakusihi endelea kufuatilia masomo yangu ya siku za usoni, nitaweka kwa kina mambo ya hizi lugha za rohoni na swala zima la *ENCODING AND DECODING*, Ili usiwe mtumishi mpumbavu kwa kuona mengi ukashindwa kuyaelewa na kuyatia moyoni (Isaya 42:20).

4⃣ *NAMNA YA KUIFANYA ROHO YAKO IWEZESHWE*

🎴 Knowledge is power (ujuzi ni nguvu), kuyapata maarifa haya ni hatua ya kwanza na ya msingi sana. Wapo ambao kwa neema ya Mungu walijikuta tayari wanatenda kazi kwa viwango fulani vya kiroho na roho zao ziliwezeshwa kwa viwango fulani.

👉🏾 Wako ambao malezi ya kiroho waliyoyapata, na yale waliyoyasikia mara kwa mara, yalikuwa na mafundisho ya viwango ambavyo viliruhusu roho zao ziwezeshwe. Maana walitembea katika kina cha maarifa ya kiroho,na ikatoa mwanya huo.

👉🏾 Wako ambao waliambukizwa tu (spiritual impartation) sawa na Hesabu 11:16-17, na wakaanza kutembea na roho zilizowezeshwa.

👉🏾Mko wengi katika mnaosoma ambao sharti baada ya kupata maarifa haya, mwingie katika hatua ya kuyataka haya kwa BWANA (1Korintho 12:31). Ukianza kuomba kwa juhudi utafika katik kiwango kizuri cha kutenda katika roho, mimi pia sijafika natia juhudi katika kuzitaka karama zilizo kuu na haswa hili nililofunuliwa na Bwana.

👉🏾 Anza kutamani kuishi maisha ya mtu wa rohoni, tamani kuona katika roho, kusikia katika roho, kuhisi kwa roho. Sehemu kubwa ya maombi yako yawe ni kuomba vipawa vya rohoni na sio mahitaji ya mwili zaidi.

👉🏾 Tumia muda mwingi binafsi mbele za Mungu (Isaya 51:2), majra ya kuwa peke yako mbele za Mungu, tena muda wa kutosha ni mlango mzuri sana wa kuifanya roho yako iwezeshwe. Maana ni ngumu kumtumikia Mungu ambaye ni roho ukiwa haupo rohoni,au ukawa mgeni wa mambo haya nisemayo.

👉🏾 Jifunze kwa watumishi ambao wanaopearet katika limwengu za kiroho, ili kuku-equip kwa maarifa muhimu, wako waliofuata mambo ya kiroho bila maarifa wakapitea kabisa, wakaishia kuongozwa na pepo wachafu tu wakidhani ni Mungu.

*MUNGU AKUBARIKI KWA KUSHIRIKI NEEMA HII YA KUPATA MAFUNDISHO. KUNA MAMBO MENGI NIMEYAONDOA NA SOMO NIMELIKATISHA KWA KUWA NI REFU SANA, NITAENDELEA KUYAANDIKA KATIKA MASOMO YAJAYO*

Mwl Proo
0762879363
0718922662

alltruth5ministries@gmail.com

Kuhusu kutotajwa jina Mungu katika kitabu cha Esta

*KWA NINI KITABU CHA ESTA, HAKIJATAJA  MUNGU KABISA WALA KWA MAJINA YAKE MENGINE?*

_Mwl Proo_

Shalom, hili sio somo, bali ni jibu la swali hilo kwa ufupi tu. Kitabu ambacho kipo katika vitabu vinavyokubalika (Canonical Books), katika Biblia lakini hakija taja jina la Mungu/BWANA kabisa ni hiki cha Esta.

Ziko sababu kadha wa kadha za kutoandikwa Mungu wala majina yake mengine. Jambo hili lilifanya wasomi wahoji, uhalali wa kitabu hiki kuwepo katika Kanoni ya Biblia

*Majibu*

1. Vyanzo vya kiyahudi vinadai kuwa Modekai (Mordecai) ndiye mwandishi. Aliandika akiwa afisa kwa mfalme Xerxes (Ahasuero), na hivyo kama afisa katika serikali hiyo aliandika uhusika wa Mungu YEHOVA kwa hali ya juu sana ila bila kumtaja jina. Sababu ni kwamba alitaka kiweze ku-fit katika muktadha wa imani ya miungu wengi (Polytheistic context of Susa) ya huko Shushani, hivyo hakutaka kutoa credits kwa YHWH kama ndiye aliyewaletea wokovu ule kwa wazi. Hivyo matukio waliyofanya ya kufunga na kuomba ameyaeleza kwa kificho lakini ameeleza wokovu wa Mungu kwa viwango vya juu.
2.  Wanazuoni wa kisasa wa thiolojia (Modern Scholars), husema kwamba kitabu hiki kiliandikwa kuwa cha kihistoria tu *(Pure Secular Book of History)*, ndiyo sababu yake pia kutotajwa katika yale magombo ya chuo ya Bahari Mfu (Dead Sea Scrolls).

Katika zama fulani, wako waliokiongezea idadi ya sura kitabu (Apocryphal part of the Book of Esther), na wakapachika jina "Mungu", ambapo badae kiliingizwa katika Kanoni ya Maandiko matakatifu ya Katoliki. Lakini haihitajiki kuisaidia Biblia kwa namna hiyo, maandiko haya yana uvuvio bila hata kuongezea neno/jina Mungu/BWANA. Mungu amejionesha kwa namna ya ajabu katika kitabu cha Esta, jinsi ambavyo pamoja na kujificha uso wake, na taifa la watu wake kwenda utumwani, hakuwaacha. Aliwaadhibu kwa dhambi zao huku akiendelea kukumbuka agano lake kwa Israel, na wakiwa huko alikuwa pamoja nao, ili awaokoe.

Mbarikiwe

Friday, May 25, 2018

ROHO YA UFUNUO

*NENO LA MUNGU NI UFUNUO; UNAHITAJI ROHO YA UFUNUO ILI KUJUA KILICHOFUNULIWA KWA NJIA YA NENO LIILIONDIKWA (BIBLIA) AU KUTAMKWA (UNABII, MAHUBIRI, MAFUNDISHO)*

_*ʍաӀ Թɾօօ*_
*0762879363*

Ninakusalimu msomaji kwa jina la Bwana na Mwokozi, Yesu Kristo, amani na neema yake izidishwe kwako. Usomapo ujumbe huu Yesu akupe hatua na kiwango kingine rohoni, nimeanza kuandika nikiwa na-sense katika roho, neema ya kuinuliwa viwango kwa utakayesoma kwa moyo wa shauku na kumtaka Bwana.

Kichwa cha ujumbe kimekuwa kirefu maana nilitafuta kuainisha jambo la muhimu kuhusu Neno la Mungu. Tukisema *Neno La Mungu*, tupo na *Dimensions* mizania mitatu (3Ds), 1.) Yesu Kristo ni Neno Hai la Mungu (Personified, Living Word Of God), 2.) Maandiko Katika Biblia (Scriptures), Ni neno la Mungu lililoandikwa (Written Word of God), na mwisho tuna Neno la Mungu la kutamkwa (Spoken Word of God), hapa tunajumuisha vyote Unabii, mafundisho, mahubiri etc. Hizi dimensions tatu hazitenganishwi, ndio maana ukisema umetokewa na Yesu, kisha amekupa ujumbe unaokataana na Neno lililofunuliwa katika maandiko hatuwezi kukupokea na ujumbe wako, maana Yeye aliyesema msitweze unabii ndiye aliyesema tuujaribu Naam tuupambanue (1Thes 5:20-21, 1Kor 14:29, 1Yoh 4:1).

*☄NENO LA MUNGU NI UFUNUO*

Paulo anawaombea hawa wakristo walioko efeso kwamba

*_"Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;"_*
*(Waefeso 1: 17)*

✍🏾Neno  ufunuo linalotajwa katika Biblia latokana na tafsiri ya kimuktadha ya kiyunani, neno linalotumika ni _*Apokaliptos /Apokalipsis👉🏾ἀποκάλυψις*_ (English 👉🏾Apocalypse). Chukua mfano huu, umewekewa sufuria (cooking pan), imewekwa mfuniko juu, unaambiwa utaje kuna nini ndani yake, nawe hukuwepo muda sufuria inafunikwa, huenda kuna chakula usichokijua kabisa, au hawajaweka kitu. Kitakachoweza kukupa kujua what exactly is inside the cooking pan, ni kufunuliwa kwa mfuniko (apocalypse ). Ni kwa namna hiyo hiyo Neno la Mungu ni ufunuo, vitu vilivyofichika vikafunuliwa, lakini msomaji na msikiaji anahitaji bado roho ya ufunuo kuyajua yaliyowekwa sirini, ndio maana Neno la Mungu linahitaji kufafanushwa, na Neno hili katika Biblia limebeba siri nyingi, maajabu mengi zaidi ya yale ambayo tunayashangaa, Daudi akasema Mungu fumbua/funua macho yangu nione maajabu yaliyo katika neno/sheria yako (Zaburi 119:130, 18).

✍🏾 Mungu ameniwekea moyoni ujumbe huu juzi, muda nasoma sura ya Biblia iliyojaa orodha (list) ya vizazi (genealogies), nikawaza hivi kutuwekea sura nzima fulani akamzaa fulani, fulani akamzaa fulani, you find it the whole chapter unasoma vizazi hivyo mpaka unakinai, ndipo macho yangu yakatiwa nuru nikapata ufunuo mkubwa juu ile orodha/list ya vizazi, na nikaamua kuheshimu vyote vilivyoandikwa. Pamoja na ukweli kwamba kuna sababu ambazo ni *jewish culture&context* zinazopelekea kuwekwa kwa uzito katika ku-identify vizazi, lakini kwetu sisi, kwa roho ya ufunuo, kilichopo kwenye maandiko na sura zote zenye kuorodhesha vizazi kuna siri kuu za kimungu beyond the cultural context ya kiyahudi ya kuweka vizazi na koo mbalimbali.

*☄NENO LA MUNGU NI UNABII/UFUNUO WA NYAKATI ZOTE*

*Maandiko ya msingi (Isaya 13:1, 14:28, 15:1, 17:1, 19:1, 21:1, 11, 13, 22:1, 23:1, 30:6, Ezek 12:10, Nahum 1:1, Habakuk 1:1, Zek 9:1, 12:1, Malak 1:1, Ufu 1:1*

✍🏾 Maandiko yetu ya msingi, yote yanaonesha kuwa hawa watu, walipokea ufunuo wa vitu walivyoongea na kuandika. Sio hisia zao, sio ufahamu wao. Wengi katika wajumbe/manabii ambao Waliona na kuandika hayo tusomayo, ni Mungu aliweka maneno vinywani mwao, mengine kwa Roho ya Bwana waliyaona na kuyasikia rohoni, na wakaweka matamko ya waliyoyaona na kuyasikia kama unabii wa nyakati zote. Na kila mahali ambapo Mungu amesema  unakutana na usemi huu, *"Asema Bwana, that says/saith the Lord"* ikiwa na maana ya kwamba hayo mambo bado Mungu anaendelea kuyatangaza kwako na kwa dunia yote hata sasa.

*NB*
*NIMESIKIA BAADHI YA WATU WALIOKOSA UFUNUO WA ROHO KUHUSU MAANDIKO YA KINABII, WAKITOA CHANGAMOTO KUHUSU ISAYA 14:12ff, NA ILE EZEKIEL 28:14ff, KWAMBA HAZIMZUNGUMZII SHETANI. HAWA NI WATU AMBAO HAWAJAANZA KUELEWA LUGHA YA MANABII NA VITABU VYAO, ISAYA KATIKA SURA YA 13&14 ANAZUNGUMZIA ANGUKO LA BABEL NA KUREJEZWA KWA ISRAEL, LAKINI HUMO NDANI ANAYOYAONGEA NA KUYAONA ROHONI NI ZAIDI YA BABEL NA ZAIDI YA ISRAEL KUINULIWA TENA. EZEKIEL NAYE KATIKA SURA YA 28 ANATOA UNABII JUU YA MIJI YA TIRO NA SIDONI, HUMO NDANI AMEONGEA NA MAMBO YA KIROHO YA ZAMA ZA HATA KABLA YA ULIMWENGU WA SASA (I will prove this).*

_Tusome mfano huu..._

*(Yeremia 4 )*
------------
*_23 Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru._*
_*24 Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko.*_
_*25 Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao.*_
_*26 Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za Bwana, na mbele za hasira yake kali.*_

   👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾 Katika mistari hiyo hapo juu kuna siri nyingi sana. Kama ambavyo Isaya BeneHa'Amoz anavyotambulisha kitabu chake kwamba ni unabii juu Yuda na Yerusalem (Isaya 1:1) lakini ukisoma unakuja kuta ameongea mambo ya zama zote kabla ya uumbaji na ya mpaka mwisho wa dunia, na ya baada ya mwisho wa siku na hata ya milele ijayo. Ndivyo ilivyo kwa Yeremia BeneHa' Hilkiah, aliona alisikia katika roho mambo zaidi ya yale aliyoyatolea unabii kwa zama zake. Mfano mdogo kwa wale wanao wanaotunisha misuli kwa ufahamu wao mdogo, Je! Yeremia 4:23-26, anazungumza habari gani? ni wakati gani huu aliouona yeye? Dunia ikiwa haina watu kabisa, haina ndege hata mmoja, wote wamekwenda zao, mbingu haina nuru, nchi iko ukiwa, miji imebobomoka. Ni wakati gani dunia ilipitia hali hii, au itapitia wakati huu? Wanathiolojia waliokubuu wanaishia kusema hii ni hali iliyotokea wakati wa gharika ya Nuhu, which can't be true, dunia ilibakia na watu nane safinani na pairs of sparrows 🕊🕊 na viumbe vingine. Wala katika mambo ya siku za mwisho (eschatological events) hata katika ghadhabu na mapigo ya Mungu, hakuna wakati kama huo. Lakini Yeremia aliona katika roho mambo yaliyotokea pale kutoka Mwanzo 1:1 mpaka Mwanzo 1:2, kulitokea ya kutokea mengi sitayafunua kwa somo hili bali somo jingine siku chache zijazo. Lengo langu hapo ni kukufanya uwe makini na maandiko ya manabii, maana hata ukisoma Kitabu cha Nabii Nahumu Mwelkoshi yeye alipewa unabii juu ya mji wa Ninawi (Nahumu 1:1), ukianza kusoma unagundua anaongea mambo ya unabii na ufunuo wa nyakati zote. Ukisoma Zekaria 9, unakuta nabii anatoa unabii juu ya nchi ya Hadraki na mahali pa kustarehe Dameski, ukienda mbele kidogo unakutana na *turnarounds* ghafula anatoa messianic prophecies  na kumtabiria Yesu mwokozi aliyefika miaka 484 tangu muda Zekaria anatoa unabii. Hivyo niifunge hoja hii kwa kukusaidia kujua unatakiwa uombe roho ya ufunuo ili kuelewa ufunuo katika Neno la Mungu, unaposoma kitabu kama   cha *Wimbo Ulio Bora* don't just read it like Novels or Magazines 📚🗞📰, ni kweli kabisa, Ule ni wimbo ambao Sulemani alimwimbia mwanamke Mshulami, lakini aliuimba katika roho na mle ndani kuna unabii na ufunuo mkubwa mno wala hauhusiki na mapenzi, sehemu kubwa sio mapenzi bali ni ufunuo wa Yesu Kristo na Bi Arusi wake (Lover & Beloved)  na siri nyingi za kiroho.

NB:
*PROPHET SAW IN THE SPIRIT THINGS THAT HAD HAPPENED FROM BEFORE TIME, THINGS DURING THEIR LIFETIME, AND THINGS IN THE NEAR& FAR FUTURE, THINGS THAT HAPPENED AND YET TO HAPPEN AGAIN NDIO MAANA WATU WAKISOMA ANDIKO KAMA UFUNUO 12:7ff WANABAKI WAKICHANGANYA KWA KUTOELEWA PROPHETIC PRESENTATIONS)*

💡 *NAOMBA NIKUPE SHAUKU KWA KUFUNUA SIRI MOJA TU, ILI KUKUPA SHAUKU ZAIDI JUU YA KUOMBA ROHO YA UFUNUO ILI KUFAHAMU NA KUJUA KWA HAKIKA, SIRI ZILIZOFUNULIWA KWA NENO LA NENO LA MUNGU* 💡

_Bila shaka katika kusoma maandiko, umekutana sana na jina Lewiathani (Leviathan),  (Ayubu 3:8, Zaburi 74:14, 104:26, Isaya 27:1). Ukitafuta kujua ni kiumbe gani huyu, unakuta kamusi zinataja tu ni mnyama mkubwa wa kufikirika (imaginary creature) aishie baharini, pahala pengine wametaja huenda akawa mamba, pengine wamesema ni joka la baharini)_

*Soma hapa....*

*"Katika siku hiyo Bwana, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini."*
*(Isaya 27:1 )*

_Sasa unaweza ona mnyama huyu amehusishwa na unabii mzito wa siku za mwisho hususani Armageddon na Hukumu ya mwisho, hivyo utagundua ni zaidi ya kuwaza ni mnyama tu fulani_

_Pia bila shaka katika Biblia yako umesoma katika maandiko yako kuhusu mnyama aitwaye *Behemoth*, waliotafsiri Biblia walijaribu kuangalia sifa zinazotajwa, wakajiongeza kuwa huenda akawa ni kiboko (Hippo). Nimechungulia katika English Dictionary mnyama huyu *Behemoth* wamenadika tu *A giant beast, God showed Job 👉🏾(Ayubu 40:15-24)* yaani mpaka hilo andiko lipo kwa Dictionary hiyo isiyo ya kidini._

_Nilipojaribu kutafuta maarifa what really are these creatures?, ndipo nikaja kujua God created two monsters female monster and male monster ndio hawa Behemothi na Lewiathani, moja anaishi katika jangwa na mwingine katika bahari, they are all invisible, habari kuwahusu viumbe hawa na siri uumbaji wao ni ajabu sana. Sitajadili pia kwa kina kuhusu hawa, ila natakaniamshe kiu tu, ujue jinsi ambavyo Neno la Mungu limejaa ufunuo na siri zisizo za kawaida, Usiache kamwe kusoma Neno. Usiache kamwe kuomba roho ya ufunuo ili ikuangazie nuru uweza kuyapata tuliyokirimiwa na Mungu. Kama Mungu aliwaonesha manabii wakaandika tafsiri yake ni kwamba Mungu ametsmani tuyajue, tusipoyajua ambayo Mungu anataka tuyajue, tutaishi chini ya kiwango, tutamfahamu Mungu chini ya kiwango. Bwana akujalie roho ya ufunuo katika jina la Yesu._

Tukutane katika somo lijalo, kuna mambo mazuri Mungu atatufundisha kwa Roho wake Mtakatifu.

*Mwl Proo*
+255762879363

alltruth5ministries@gmail.com

Saturday, April 14, 2018

VITA VYA ROHONI

*VITA VYA ROHONI*
_(SPIRITUAL WARFARE)_
🔫⚔💣🗡🛡

By Mwl Proo
0762879363
©2011

Kwamba tumeokoka, haina maana tutakuwa mafundi wa kila aina ya ujuzi wa kiroho (Tunahitaji kufundishwa). Yako mambo ya kiroho ambayo ni ujuzi (Profession) maalum, haya utayajua tuu kama Roho Mtakatifu ameamua kukufundisha mwenyewe au kwa kufundishwa na watumishi   ambao Mungu amewapaka mafuta kwa ujuzi huo. Mungu hatamfundisha kila mtu maarifa yote, maana sio wote wame-tune on kwenye frequencies za kufundishwa ujuzi (profession) fulani wa kiroho. Vita vya kiroho ni ujuzi maalum (Profession).

*Mambo ya Ujuzi (Experience)*
Mifano ya kibiblia kuhusu kweli hii, ni jinsi ambavyo watumishi wa Mungu walivyoweza kupata experience kwa kuona na kufunzwa na watumishi ambao wao walipata direct toka kwa Mungu. Mfano; Musa alifundishwa na Mungu (Zb. 103:7) moja kwa moja (direct revelation). Lakini Yoshua hakuwa na wakati na Mungu kama Musa, lakini alitumiwa kwa ishara kubwa kama ile ya kusimamisha jua (Yosh.10:12). Amini ni zaidi ya asilimia 70 ya ujuzi wa kutembea na Mungu kwa kiasi cha miujiza, Yoshua aliupata kwa Musa. Jaribu kukumbuka habari ya Elisha na Eliya. Eliya alijifunza direct toka kwa Mungu, lakini asilimia zaidi ya 70 ya impact kwenye maisha ya Elisha (Ishara, maajabu na miujiza) ilikuwa ni Experience impartation toka kwa Eliya. Elisha naye ilimpasa kumfundisha Gehazi experience ya kimungu, lakini   katika kumwandaa, mtumishi wake Gehazi alikosea, na hivyo Elisha alikufa na ujuzi wake na upako wake bila ku-impart kwa yeyote. Baada ya hapo hatusomi tena nabii yeyote kutumiwa kwa mfano wa Eliya na Elisha. Hata wakati wa Yohana mbatizaji, pamoja na kazi kubwa ya Yohana mbatizaji, hakuna historia ya muujiza wowote aliotenda, hii bila shaka ni kwa kuwa, hapakuwepo mahali pa kupata Experience, wala hakufunuliwa direct (Lakini labda pia wito wake haukuhitaji miujiza)..

*KWA NINI TUJIFUNZE VITA VYA KIROHO.*
Vita vya kiroho ni ujuzi maalumu (Profession) na anayeweza kuvipiga lazima awe AMEHITIMU KUPIGANA (Wimbo ulio bora 3:7-8).
Pia tunasoma katika (2Falme 13:19), habari za Yehoashi mfalme, alichoma mshale mara tatu tuu, wakati Elisha alimtazamia achome mara tano au sita ili ashinde kabisa kabisa. Watu wa Mungu wengi wana mshinda shetani kidogo tuu, hadi inadhaniwa kuwa shetani ana nguvu sana. Kwa hiyo pata fundisho hili maalum (SPECIAL COURSE) ili uwe mshindi daima.

*MISINGI YA SOMO*
💫Katika vita vya kiroho, twaweza shinda bila shaka (HESABU.13:30)
💫Shetani adui mkuu ni kiumbe tu (He's just a creature. Ezek. 28:2, 6, 8, 15, 19)
💫Aliye ndani yetu ni mkuu kuliko adui yeyote aliyepata kuweko (1 Yoh. 4:4).
💫Jeshi la shetani halilingani na Jeshi la Mungu. Yoshua alikutana na malaika aliyejitambulisha kama Amiri wa jeshi la Bwana (Yosh. 5:14)
Malaika asingetaja majeshi hewa (kuna majeshi), na Mungu wetu asingejifunua kama BWANA wa majeshi, kama hana majeshi.
Majeshi ya Mungu kiidadi ni mengi kuliko ya shetani (soma 2 falm. 6:16)
Pia kithiolojia, 1/3 (theluthi moja) ya malaika walishawishiwa na kuasi pamoja na shetani (Ufun 12:4).
Hatujui idadi kamili, lakini tukiitumia hesabu ya kinabii ya majeshi ya Mungu ya bilioni ishirini (20,000,000,000 ya magari ya vita/chariots) soma (Zab. 68:17). Huenda hii isiwe takwimu kamili, lakini tujifunze. Kama theluthi waliasi,
(ni 6.5 billion) ya malaika, kwa hiyo bado kuna theluthi mbili ilibaki (13.3 billion). Okey tuachane na mahesabu maana sio kusudio langu la hizo hypothetical information.

*_UHALISIA WA VITA VYA KIROHO._*
Vita tunavyosoma katika Agano la kale, vilikuwa vya kimwili (Physical Fighting) ingawa in some cases, vita vilipigwa katika ulimwengu wa roho na kuleta matokeo (impact) katika ulimwengu wa mwili (physical world).
Yoshua 6:1-20, Amuz. 5:20, 25-26
Kutoka. 17:8-16, 2 Nyak. 20:15-24.
Vita ya kiroho ipo kwa mtu binafsi (individual level) hadi level ya bara zima (continental wise).

*The personal experience of spiritual warfare*

Mifano hii ni halisi, lakini kimaandishi haiwezi kuandikwa yote.
💫Siku wanafunzi wenzangu waliponisikia nikitoa sauti kama ya kilio fulani nikiwa nimelala. Nami nakumbuka kulikuwa na vita kali sana siku hiyo, kiasi cha kuona nilipekekwa sehemu nyingine.(Yaani niliondolewa kabisa mahali nilipokuwepo), Wakati huo nikiwa kidato cha kwanza (Pugu secondary school) na ni mchanga tu kiroho (Mwenye juhudi kubwa kiroho).
💫Siku moja nilipanda kitandani, nikaona baridi imeniangukia miguuni,inapanda kuja juu, ghafla, niliona ceiling board inayotenganisha Cubicals katika bweni, ikitikisika kama kitambaa, na dudu moja la ajabu, kubwa, lenye mikia mingi kama pweza 🐙👹, lilitokomea katika ceiling board hiyo.
💫Siku moja nikiwa macho, nyakati za usiku hakukuwa na umeme eneo lote, wala taa. (Kumbuka nguvu za giza, zinafanya kazi sana, kukiwa na giza). Nikiwa natembea niliona mkanda wa kufunga suruali unatetemeka na kuzunguka kwa nguvu. Nikaushika kwa mkono, ghafla ndani ya suruali nilihisi joto na baridi kwa pamoja, kisha nikahisi vita kali rohoni.
💫Siku niliposikia sauti ikiniambia, Kuna vita kubwa sana katika ulimwengu wa roho nilikuwa nimelala, nami nilihisi sauti ya vita.
💫Siku nilipohisi uwepo mwingi kama wa Mungu, but haukuwa halisi, kumbuka shetani anazo copies (nakala) za vitu vya kimungu, ila sio halisi. Lakini baadae nilishtuka kuwa ule uwepo haukuwa wa kimungu, ila ni UVAMIZI wa kiroho. Ingawa nilikuwa ibadani, Mungu alikwisha nifundisha kuwa uwepo wake unakuja kwa wewe kujiandaa, kuukaribisha na kuuhitaji sio kwa ghafla bila kuutaka.
💫Siku nilipoomba masaa zaidi ya manne usiku, kuanzia saa 5 usiku hadi saa tisa, nikiwa pekeangu, kwenye chumba chenye giza. Nilipomaliza na kulala, usingizi mzito ulinigubika kwa sababu ya shughuli za jana yake mchana. Niliposikia sauti kwa ghafla, ikinishtua kwa kusema, "Adui anakuja", vita ilikuwa kali siku hiyo, lakini Roho Mtakatifu alinipa kushinda. Hata baada ya kuamshwa na Roho Mtakatifu, sikuweza kuamka sababu ya uchovu mwingi, haikupita hata dakika moja, nguvu za adui zilinivamia, nilibanwa viungo vyote vya mwili, sikuweza kufurukuta. Kwa njia ya maandishi haitoshi kueleza yote na jinsi nilivyoshinda, HAYO NITAYAELEZA NIKIWA NAHUDUMU LIVE, NIMELIST TU KUJIKUMBUSHA.

NB:-
Ndugu msomaji, hiyo ya juu ni mifano michache ili nikupe picha ya uhalisia wa vita ya rohoni.
Unaweza kuwa macho au umelala, itakujia tuu. Ni muhimu kuwa na Roho Mtakatifu kama  Antenna ya ku-sense mashambulizi ya kiroho.
B. GROUP-WISE WARFARE. (Vita kwa kundi)
Vita ya kiroho inaweza kuwajia mkiwa kundi la watu either katika huduma au jambo lolote mnalofanya.
Tuliwahi kuwa katika mkesha, na wote tulishambuliwa; hatukufanya vita vya kiroho kwa ujuzi, na hivyo wote tulishambuliwa mwingine alikamatwa na kichomi, mwingine kwikwi isiyoisha, mwingine tumbo kujaa gesi, mwingine kichwa kuuma, kila mtu alishambuliwa kivyake, tukajikuta maombi hayaeleweki.
Paulo na wenzake walizuiwa na shetani waziwazi (1Thes. 2:18)

MFAHAMU ADUI
Ukipambana bila kumjua adui yako vizuri, unaweza kupigwa vibaya. Ni muhimu umjue adui yetu, nguvu zake, silaha zake na mbinu zake za kivita.
Shetani (Lucifer) ndiye adui mkuu.
Alikuwa malaika mwenye daraja la kwanza kwa cheo. Ezek. 28:14-16 Isay. 
14:12-14
Anatajwa kama Mungu wa dunia hii (2 Kor 4:4)
Dunia yote hukaa kwake ( 1 John. 5:19)
Anatajwa kuwa ni mwenye nguvu (Math. 2:29)
Anatajwa kuwa ni mwenye nguvu (Math. 12:29)
Anatajwa kama mkuu wa ulimwengu Yoh. 12:31, 16:11, 14:30.
Anao ufalme wake Mark. 3:22-27

*AUTHORITATIVE STRUCTURE OF SATAN'S KINGDOM*
(Pata kielezo cha chati kilichochorwa vizuri)

*MAELEZO YA CHATI*

Shetani kwa kujua kuwa ameasi kinyume chake yeye aliyemwumba, na upinzani atakaoupata, amejidhatiti kwa kuweka utawala na majeshi. Kumbuka katika ufalme  watawala na majeshi ni kitu muhimu sana.
Ngazi zilizo chini, zinapokea nguvu kwa ngazi za juu.
Zinatoa  report ya utendaji kwa ngazi ya juu.
Ngazi inayolemewa inaomba msaada sehemu nyingine.
FALME NA MAMLAKA
Hii ni ngazi ya kwanza ya cheo baada ya Lucifer. Inahusika na kuzuia au kupinga yanayotoka juu kwenda kwa watu wa Mungu. (Dan. 10:12-13)
Hapa utasoma habari ya wafalme wa Uajemi, falme na mamlaka hutumia jina ambalo juu yake wanatawala. Mfano tukiwa Dodoma au Tanga, usikemee wakuu wa uajemi, Wamedi na Waajemi (Medes and Persians) ni mashariki ya kati, hupaswi kutaja wakati wa kukemea, wewe utataja wakuu wa anga ya Dodoma au Tanga!

Na inapotokea yanayotoka chini kwa watakatifu kwenda juu, yakipenya ngazi zote, hapa lazima kutakuwa na kazi ya ziada ili wao nao waachie.
Kuna mambo ambayo watakatifu waliopo duniani, waliyataka toka juu, kiti cha enzi cha Mungu kikaachiliwa mahitaji na majibu, yakakwama hapa. Wao hawanufaiki kwa chochote wanapoyashikilia, ila walioomba kama hawataendelea kuomba, wataendelea kushikilia. Lakini kama jambo limepelekwa kwa force kubwa, wanapisha, wala hawazuii kabisa.
Falme na mamlaka zinaamua eneo husika liweje kiimani, kiuchumi au kisiasa.
Dini zote ambazo muasisi wake si YEHOVA BWANA, AU YESU KRISTO, ni kazi ya falme na mamlaka. Dini kama Buddhism, Hinduism, Taoism and all others, including traditional religion, zote hizi ni kazi za falme na mamlaka kutimiza uhitaji wa shetani (Lucifer) Kuabudiwa
WAKUU WA GIZA/ANGA
Efeso. 6:12, 2:2
Hii ni nafasi ya tatu toka kwa shetani, inapokea maelekezo toka kwa falme na mamlaka.
Katika eneo husika wanalo tawala wanajenga ngome (2 kor.10:4)
Wanatumia majeshi ya pepo kuachilia maasi/maovu/dhambi za namna yeyote mahali wanapokusudia.

Mfano 
Albino killings in Tanzania
Prostitution business in Las Vegas (U.S.A ) 
Abortion in United Kingdom.
Kuzuia maombi ya watakatifu (No break through)
Kupinga  mambo yote ya huduma ya kiroho 
Kwa kufanya mioyo ya watu kuwa migumu.
Kuifanya anga kuwa nzito (no anointing)

MAJESHI YA PEPO WABAYA 
Hii ni ngazi ya nne kwa cheo, imegawanyika makundi mawili.
Majini  (Lawi. 17:7) hapa kwa mara ya kwanza katika biblia, tunasoma neno hili Majini (Water/marine spirits kwa kiarabu Jinn(kilichofichika/unseen)).
Pepo wachafu (Evil spirits/ Demons) (Kumb. 32:17) Hapa tunasoma kwa habari ya mapepo kwa mara ya kwanza.
Majini (Water spirits)  na mapepo,yanaelezwa kuwa na tofauti kadha wa kadha na utendaji kazi wao.  Lakini ukweli hawa ni roho walewale tu wamoja.
Pepo wakiwa wengi kwa mfumo wa majeshi, Wakifikia 6,000 huitwa Legion
Mambo yote yaliyo kinyume na amani, furaha, raha, baraka, utulivu, afya njema, upendo, masaidiano, maendeleo, na kila lililo jema; yanasababishwa na pepo wachafu na majini.
Pia mapepo yanabadilisha matumizi ya asili (Luk . 8:27) - kuishi makaburini Rumi. 1:26-28
Yanafanya kazi kwa bidii, yakijua wakati wao sio mwingi Math. 8:29, Ufun. 12:12
BAADHI YA MAJINI/PEPO NA KAZI ZAO.
JINI HUSNA HUNAN AU JINI CHAFANYA KUU POPOBAWA (INCUBUS/SUCCUBUS)
INCUBI-Shambulio la kiroho la tendo la ndoa bila hiari katika ndoto kwa wanawake.
SUCCUBUS- Sawa na hilo hapo juu ila hapa, ni jini la kike kuvamia 
wanaume kwa ngono.

JINI KILOLINDI NA JINI WARIDI JEKUNDU (Kazi yake ni kuamsha hamu ya ushoga)
SUBIANI- (Kazi yake ni kubadili tabia za watu).
SUBISUBI- Jini wa vitisho
JINI SHEIKH- Jini mtawala
JINI SAHABINI ALWAH-JINI WA KUTOA MIMBA (ABORTION)
JINI MARUHANI- Jini linalozuia vitu kuingia au kutoka (No entry, no exit)
JINI MAKATA- Mtenda kazi wa siku 13 anayeishi kwenye milima kazi yake ni kuua na kutawanya.
JINI KASKASHI- KUSHOTO MWENYE KULETA MAUMIVU, HUZUNI NA Kadhalika.
JINI MEEKA- Jini anayewavuta watu kupenda muziki wa kidunia kama Bongo fleva.
JINI LUMYATA- Jini anayewanasa watu wa dini kwa ngono na kuwaleta kwa shetani.
JINI NYOKA ZEHEL- Pepo wa ushirikina wa aina zote.
Kuna umuhimu wa kutaja jina la jini husika, kama umegundua ni yupi anayefanya kazi, kama unajua jina.
Kama hujui jina usikisie, taja kazi ya pepo iliyojidhirisha.
Mfano:- roho ya mauti au ajali nakuamuru  toweka; au nasambaratisha pepo la ushirikina.
Kuna majini yanayo-operate sehemu Fulani, na sehemu nyingine hayatendi kazi, ila wanadamu wenyewe wana-transfer zile kazi.
Mfano:- Malkia wa baharini anatenda kazi sana kwenye Coastal regions. Au Roho ya Yezebel (Ufunuo. 17:1-5-kahaba mkuu) ufunuo: 2:20-22 Isaya. 3:1-3
Jina Yezebel unasoma kwenye biblia kama mke wa Ahabu mfalme wa Israel, lakini alikuwa na sifa ya uchawi na uzinzi (2 Flame. 9:22), Na ni roho kamili katika ulimwengu wa roho.
Kuna mambo yanayohamasisha uasherati ( fashion&style) yanasababishwa na  roho hii (tembelea

http://www.albatrus.org/english/church-order/women-matters/jezebel_in_our_society.htm

🗡Dalili za utendaji kazi wa roho hii mahali Fulani
Kushamiri kwa ibada za sanamu.

🗡Kujengwa kwa madhabahu ya shetani ndani ya kanisa.

🗡Kuenea kwa dhuluma na kupotea kwa haki za watu, (ufisadi).

🗡Kuuawa kwa wenye haki au wanaotetea haki.
Kuchochea uasi ndani/mbele ya watu.

🗡Kuenea kwa uasherati, uzinzi, ushoga na aina zote za uzinzi kwa kutumia viungo ambavyo havikuumbwa kwa makusudi hayo.

🗡Kutoa vitisho kwa watumishi wa Mungu, wanaosimamia kweli.

🗡Kushamili kwa  mambo ya ushirikina na unajimu.

🗡Usingizi  wakati wa ibada, kusoma neno. Huu ni mfano tu.

*WACHAWI, WAGANGA NA AINA ZOTE ZA USHIRIKINA*
Kwa mara ya kwanza tunasoma kuhusu wachawi na waganga kwenye (kut. 7:11) 
Hii ni ngazi ya mwisho katika utendaji wa shetani.
Ngazi inaofanya kazi moja kwa moja kwa wanadamu kwa kutumia na pepo/majini.
Upigaji ramli, kuloga, kuagua, kutuma majini, kuwafunga watu ni kazi zao kubwa.

*_WALIMU, MITUME NA MANABII WA UONGO NA IMANI POTOFU._*
Hii nayo ni ofisi ya shetani, inayolenga kuwanasa wanaomtafuta Mungu wa kweli.
Watumishi hawa wa uongo, wanatumiwa na pepo kuingiza fundisho ambalo ni kinyume na kweli, ili waamini washambuliwe kiurahisi.
Imani potofu nayo inapotosha watu kuabudu kitu kingine kwa kudhani wanamwabudu  Mungu wa kweli, inaiga  mifumo  ya ibada za kweli. (HILI NI SOMO JINGINE, HAKIKISHA UNAPATA SOMO LANGU LA *ROHO ZIDANGANYAZO*)

*SIFA ZA ANAYEWEZA KUVIPIGA VITA VYA KIROHO.*
Kama tulivyoona katika utangulizi, vita vya kiroho ni ujuzi maalum (Profession) hivyo kuna watu wenye sifa za kupigana vita hivi.
Lazima awe anamwamini YESU KRISTO, yaani AMEOKOKA.
Lazima awe amejazwa roho mtakatifu.
Lazima awe amefundishwa vita ya kiroho.
Lazima awe anamfahamu adui.
Lazima awe amevaa silaha.

Mwl Proo

*ASKARI WA KIROHO SAWA NA Efeso 6:10-18*

(Hakikisha unaona kielelezo hiki cha mchoro wa picha)

*SILAHA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.* 🔫💣⚔🛡🗡
Neno linasema, Bwana amefanya silaha za kufisha (Zb. 7:13), neno amefanya katika mstari huu maana yake, ametengeneza.
Silaha za mwili za ulimwengu huu hazina kazi katika ulimwengu wa roho (mwimba tenzi- mteteeni Yesu) Aliimba, Nguvu zenu za mwili hazitatufaa.
Mungu wetu ni wa vita (kut. 15:3) lazima awe na silaha.
Tunaagizwa kuvaa silaha. Efes. 6:11, Rumi. 13:12, Nah. 2:1
Kuna silaha makundi mawili 
🔴DEFENSIVE WEAPONS.(Silaa za kujilinda)
🔴OFFENSIVE WEAPONS. (Silaha za kushambulia)

Nchi kama ya TANZANIA ina defensive forces (JKT na JWTZ), Vikosi hivi vyote ni vya kujilinda, hatuna ARMIES Kwa ajili ya mashambulizi. Mataifa kama U.S.A, GERMANY, RUSSIA na CHINA yana OFFENSIVE ARMIES.

Ni muhimu kukumbuka, lugha ya neno (BIBLIA) ndio lugha ya roho (au inayotambulika sana rohoni)  so much pronounced!
Usiige misemo ya wana wa dunia kwenye vita ya kiroho.
Mfano: Ushindwe na ulegee kama usemi haupo kwenye maandiko, na  umebuniwa  tu na watu wa mwilini,  unakua ni mzaha kwenye ulimwengu wa  roho.
NB:
Ni muhimu kufahamu ulimwengu wa roho, umejaa uhalisia wa vitu vyote, sauti zina maana zaidi (1 kor. 14:10), hata ukiongea upuuzi, unasikika sana katika ulimwengu wa roho. Nguvu (forces) zinazofanya kazi ni nyingi kuliko za duniani/tunazo soma kwenye Physics /Geography. Kuna forces ambazo zinaweza kuumba kitu unachotaja hata kama hakijawahi kuwepo. Unaweza ukasogeza kitu popote kwa mwendo (speed) wowote. You can zoom in, zoom out kwa ukubwa ( size)  yoyote.

*SILAHA KUNDI NO. 1*
Tunazo silaha ambazo zina nguvu katika Mungu ( 2 kor. 10:4)

*JINA LA YESU*
Mdo. 4:12,2:21, Math. 12:21  Jina la Yesu lina mwali ya moto🔥, linatajwa,
kama YAHU (Zab. 68:4, 89:8 Wimbo. 8:6)
Mith. 18:10

Kwenye jina la Yes kuna 
🗡Mamlaka ya Mungu
🗡Uweza wa Mungu
🗡Kidole cha Mungu.

*DAMU YA YESU.*
Ebr 12:24, Math 26:28 (Damu ya Agano) Damu ya Yesu ni silaha kubwa kwenye ulimwengu wa roho, na hasa kwenye kuwafungua waliofungwa. Ushuhuda binafsi,  siku moja nikiwa katika  vita vya kiroho, kila nilipotaja damu la Yesu, nilisikia sauti kama ya risasi imefyatuliwa.🔫

*MSALABA WA KRISTO YESU*

(I Kor 1:18) Hii pia ni silaha kubwa kwenye mambo ya ukombozi, toka katika nguvu za giza.

NENO LA MUNGU
Ebr. 4:12, Efes. 6:17, Yer. 23:29, 5:14 Zab. 147:15, 18.

SIFA KWA MUNGU (PRAISE)
2 Chron. 20:16-20 Zab. 22:3, 149:6 sifa ina fananishwa na silaha ya vita.
Katika lugha ya asili ya Biblia (Kiebrania) sifa ina tafsiriwa kama Halal ambayo ni muunganiko wa aina nne za sifa yaani. Shaback- Shouting (Zab 63:3), Tehilla kuimba tenzi na zaburi (Zb 40:3) Towdah- Dhabihu ya kushukuru (Zb 100:4) na ya mwisho ni zomar- kuimba kwa 
kutumia vyombo vya muziki (zab. 33:2) sifa yenye mambo hayo manne ni silaha kubwa.

*WEAPONS IN THE STORE (GOD'S ARSENAL)*
Neno linasema, Bwana amefungua akiba yake silaha (ARSENAL), (Yer  50:25). Kumbe kwenye ulimwengu wa roho kuna storeroom ya silaha za kila aina, hizi hapa chini ni silaha unazoweza kuzitumia kwa kadili ya uhitaji wako.
💣Upepo wa mashariki [Kut 10:13, Zab 78:26, 18:15, Yona 4:8, Hos. 13:15 Hab. 1:9, Isa. 50:2, Isa. 11:15

💣Mishale, ngao, upinde na mikuki ya moto na umeme, zek. 10:4-5 Yer. 51:11, 50:29, Hab. 3:911, Zab. 35:2-3, 7:13 2Falme. 13:17, Yer. 45:3-4, Zab. 18:14, 9:14

💣Magari ya vita/moto yer. 47:3, Zab. 68:17, 2 Falm. 6:17, 2:11.

💣Radi na mvua ya mawe Zab. 18:13, mawe ya teo (SLINGSTONE) Zek. 9:15

💣Kuna misumari, Zek. 10:4

💣Chungu cha maji yenye nguvu, Hab. 3:15
💣Kuna minyororo, Nahum. 3:10

💣Kuchafua usemi (Lugha), Zab. 55:9, Gen. 11:7-9.

💣Kuna mapanga ya umeme kumb 32:41, Isa. 27:1

💣Kuna majembe, miundu na mikuki Yoel. 3:10, Yer. 50:36, Zab 7:12, Yer.47-6

💣Matuo ya Bwana (forces of the Lord) Yoel. 2:11.

💣Kuna moto (Yoe. 2:3, Ebr 12:29, Kumb. 4:24)

💣Kuna mawe ya barafu (Yoshua. 10:11)

💣Kuwapiga adui kwa 
usingizi wa milele (Yer. 51:39)

*JINSI YA KUVIPIGA VITA VYA ROHONI.*
Neno linasema, Bwana ananifundisha mikono yangu kupigana vita (2 Sam 22:40) ni muhimu kujua vita vya kiroho ipo kwa ajili yetu, ikikupata usimuulize Mungu, kwa nini! Wala usihoji wako wapi malaika wanaonilinda. Utajifunza mbele kidogo ni wakati upi malaika wanatumika katika vita.
Tukiwa na maarifa ya jinsi ya kuvipiga vita, hatutafanya kosa la sisi kukusanyika wengi kwa ajili ya adui mmoja. Mfano:- kukitokea na mkabaji mmoja, hawezi kuvamia kundi la watu 3, wala hana silaha yoyote ya kutisha).
Hesabu za kibiblia(Lawi. 26:8).. 5 of us will chase 100 enemies 100 of us will chase 10,000 enemies.
Pia katika, Yosh. 23:10 na Isa. 30:17, the Bible says,  .at a threat of one, thousand will flee, at a threat of five, all will flee.
Kwa hiyo ni muhimu kufahamu strategies and schemes, kwani shetani (Adui mkuu) anajua mbinu za kivita. 2Kor. 2:11 (schemes), Efes. 6:11.
Pia ni muhimu kufahamu structure ya vita vya mwilini, ambayo Mungu alimfundisha Daudi ndio muundo wa kupigana katika roho.
Mfano: kuweka waviziao (setting an ambush) 2 Nyak. 20:22, Amu. 20:29.
Lazima awepo anayeongoza. (AMU. 7:17), msifanye bila mpangilio (randomly). Jaribu  kupata picha, mnakemea pepo mchafu mwingine anamuuliza jina lako nani, mwingine anasema, funga kinywa mtoke, kila mtu anaamuru cha kwake.
Lazima muanze na kujiweka sawa, kwa kujitakasa (huenda yupo ambaye si safi, anaweza kuleta usumbufu) Yoel. 3:9.
Kuvaa silaha. (Yote haya yafanyike kwa mfumo wa confessional Prayers) kama kiongozi anavyo-direct.
Sehemu yaku-set ambush, mnaweza kunongona.
Lakini mkianza vita lazima ifanyike kwa sauti kuu (kelele) Yosh. 6:20, Luk. 23:23, Hesab. 10:5-9.
Ni muhimu kushambulia ngome, zilizojengwa na wakuu wa giza/anga (Yer. 48:41)
Ni muhimu kushambulia vituko (Yer. 51:32), katika ulimwengu wa roho kuna madaraja kama haya ya mwilini, yanawasaidia mapepo au majeshi 
mengine ya adui kuvuka toka upande mmoja kwenda upande mwingine, na kuna miundo mbinu mingi inaharibika wakati wa vita.
Maombi ya vita vya kiroho hayafanywi kwa utulivu, mnapokuwa kundi la askari wa Yesu, manavipiga vita lazima kuwe na MSHINDO (Yer. 50:22, Yoe. 2:5, Nah. 2:4).
Angusha kuta zote zote zilizosimamishwa na wakuu wa giza Yer. 51:44
Hatupaswi kupotosha safu zetu. Asiwepo anayechoka upesi, na kukatisha maombi kabla ya vita kuisha. Wote mpigeni adui sawa. (Yoel. 2:7-8)
Kumbuka kuzuia vyanzo vya msaada. 
wa adui. Tunasoma katika 2 Falme. 3:25 Jinsi wana wa Israel walivyoziba chemchem za maji kwa mawe, ili adui wasipate maji ya kunywa wawapo jangwani. Pia kama mnakemea pepo, mkiona hirizi au nyezo yoyote msiiache, choma moto.
Ni muhimu kuingia rohoni ili uweze kujua kama adui amekimbia au amejificha.
Mark. 9:26
Ni muhimu kulinda njia, yasije majeshi meingine ya mbali, ili kufupisha muda wa vita. (Nahum 2:1)

*MANENO MASHUHURI YA KIBIBLIA YA KUTUMIA WAKATI WA VITA.*

Yer. 1:1:10, 51:43, Isa. 6:11, Kut: 15:5, Efes. 6:16, Luk. 10:19, Isam. 2:10, Yer. 51:20, 2Kor. 10:4-5
Ninaangusha, nainashambulia, nainasambaratisha, ninangoa, ninaharibu, ninavunja, ninabomoa, ninafunga matita matita, ninapatiliza, ninateka nyara, ninayeyusha naangamiza, ninanyamazisha, ninaponda, ninakanyaga, ninadisconnect, ninafunga, ninatowesha, nasaza maganjo, nafanya ukiwa, ninavua enzi nafunikiza, na mengine  mengi utakayoyapata kwenye neno la Mungu.

*SOME WARFARE SITES IN THE SCRIPTURES..

Yer. 6:4-5 ( Kabla ya kuanza)
Yer. 46:3-4 (Kabla ya kuanza)
Yer. 46:5 (Baada ya vita)
Yer. 47:1-7 (Kabla ya vita)
Yer. 48:1-4 (Kabla ya vita)
Yer. 48:15-25-44 (Baada ya vita)
Yer. 50:21-32 (Kabla ya vita)
Yer. 50:34-46 (Baada ya vita )
Yer. 51:11-13 (Kabla ya vita)
Yer. 51:20-23 (Kabla ya vita)
Yer. 51:30-32, 37-56 (Baada ya vita )

Mwl Proo
(Prosper Kadewele)
©2011

alltruth5ministries@gmail.com

Visit website

Thursday, March 29, 2018

NIENDESHE MAHALI PANGU PALIPOINUKA!

_*NIENDESHE MAHALI PANGU   PALIPOINUKA*_
*(Make me walk on my high hills)*

*Mwl Proo*
_0762879363_

Haleluya kwa BWANA! Nawasalimu kwa Jina la Yesu Kristo, Mwokozi wetu. Naamini mnasonga mbele katika imani.

_WATU WA MUNGU, HUSUSANI WEWE AMBAYE UMEPATA NEEMA YA KUSOMA UJUMBE HUU; KUNA MAHALI AMBAKO MUNGU ANAKUSUDIA KUKUWEKA, KUNA MAHALI ULIANDIKIWA KWA MAJIRA YAKE UTAPASWA KUWA SEHEMU FULANI HIVI, MAHALI PA JUU SANA, IWE NI KATIKA HUDUMA, KIUCHUMI, KIJAMII (SOCIAL STATUS), NA KATIKA NYANJA ZOTE (IN ALL LIFE'S ENDEAVORS). KILA MWAMINI UNA MAHALI PAKO PALIPOINUKA, HUTAKUWA CHINI DAIMA, HUPASWI KUBAKI NA HALI ULIYO NAYO DAIMA, WEWE NI MCHUNGAJI UKO NA HUDUMA UNAISIMAMIA, NYUMBA YA IBADA HAIJAWAHI KUVUKA WATU 50, SHAUKU YAKO NI MAMIA KWA MAELFU, HAIJAWAHI KUWA KWELI HIYO NDOTO!, WEWE NI BABA WA FAMILIA UMETAMANI KWA MIAKA MIAKA MINGI UONDOKANE NA AIBU YA KUPANGA CHUMBA NA SEBULE HUKU FAMILIA YAKO NI KUBWA TAYARI, NDOTO HIYO HAIJAWAHI KUWA KWELI!, WEWE NI MAMA/MWANAMKE KATIKA NDOA, MIAKA IMEPITA NDOTO YAKO YA KUZUNGUKWA NA WATOTO WAKICHEZA KWA FURAHA HAIJAWAHI TIMIA!, WEWE NI MFANYA BIASHARA FAIDA ULIYOIOTA KUIFIKIA SIKU MOJA HAIJATOKEA, UMEBANGAIZA MPAKA UNAHISI MOYO WAKO UNAINAMA NDANI YAKO; UNA SAFARI NGUMU KATIKA ELIMU UME-RESIT UKACHOKA, CARRY OVERS/DISCONTINUE ZIMEKU-DISAPPOINT MPAKA UKASEMA HUENDA SIJAANDIKIWA MAFANIKIO KATIKA ELIMU; NA WENGINE WAMEPUNGUKIWA UTUKUFU NA FAHARI KATIKA MAISHA, WANAUGULIA NDANI YAO KUWA HALI ZAO ZA SASA NI MBAYA KULIKO ZAMANI_

*______ kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa."*
(Hosea 2:7 )

✍🏾 *Mungu hajawahi kuwaza kukusahau, hujasahaulika kabisa ewe mpendwa wangu (Isaya 49:15-16), kuta zako (your issues&situations) ziko mbele za BWANA daima. Lakini leo kuna jambo la kujifunza*

🚩 *HATMA ZILIZOCHELEWESHWA (DELAYED DESTINIES)*

🎯Ni kweli kwamba Mungu anakuwazia mema, na ni mambo tunapenda zaidi kusikia, yaani kutiana moyo kwa ahadi za Mungu, kiasi kila mtu anaweza kunukuu (Yeremia 29:11) kwa kichwa/moyo bila kusoma. Ni kweli kwamba makusudi ya Mungu hayawezi kuzuiliwa (His plans can't be thwarted) Ayubu 42:2, lakini Je! hayo mambo yako mepesi hivyo? Jibu hapana, ziko sababu zinaweza kawilisha mafanikio, hatma njema zenye utukufu.

🎯 Shetani kwa kupitia idara yake ya falme na mamlaka pamoja na wakuu wa giza, wameshikilia hatma nzuri nyingi sana, zisiwafikilie wahusika...

👉🏽Wakuu wa anga/giza hili wamejitahidi kuwapumbaza watu wa Mungu, maana bila kufanya hivyo hakuna falme za giza za kuweza kushindani na kanisa la Kristo (wala individual believers). Hivyo kwa kuwa wanajua kwamba hawa watu wakisimama sawa kwa Bwana watatoboza daima kuzielekea hatma zao njema (their brilliant futures/blossomed destinies), njia pekee ni kuwapumbaza.

👉🏽Ziko hatma njema, tuliandikiwa, lakini kuzipokea kunategemeana na hali ya kiroho ya wakati husika, yaani unaweza kuharibikiwa kiroho kwa kiasi ambacho Mungu akimwagiza malaika aachilie ule mbaraka wako, anakukuta haujastahili, hivyo kukawa na *waiting time* kuona kama utayaweka mambo sawa, ukayafua mavazi, na kuwa tayari kuzipokea ahadi (delaying).

👉🏽Kuna tabia za asili (matendo ya mwili) ambazo haziendani na hatma ya mafanikio uliyoandikiwa. Na hapa ni shida zaidi, wengi katika waamini baada ya muda wanajikuta wanapambana na utu wa kale tena. Wakuu wa giza wana desturi ya kujengea ngome (making strongholds/pinning) baadhi ya tabia za mwenendo wa kale, wakipata nafasi, kisha hata wao wakikaa pembeni, unabaki unashindana na ile tabia hali ukikawilishwa kuiingia hatma yako njema (2Korintho 10:4-5)

👉🏽Unaweza kujikuta mwaka mzima umeisha, hujawahi kuwa sawa kiroho, hatia, makosa, kushindana kumekuzinga kote, kila unapoponyoka toka katika vifungo vya zile ngome za wakuu wa giza (vya tabia za utu wa kale ambazo unakuta umechomekewa tu), unajiona ni mtu usiyestahili kuomba mahitaji, huna uhuru wa kuamuru mapambazuko yako, na badala yake unakuwa bize na maombi ya kutengeneza, kurekebisha njia, kujijenga upya, kutafuta tena connection ya kwanza, unatubu tena na tena na unahisi kama bado hivi, unarudia kuyatubia yaleyale, huu muda wa kutengeneza kiroho chako ukiwa prolonged (refushwa sana), unaweza kuta umekutana na wakati mwingine wa ukame kiroho. Hivyo kabla hujashughulikia kunasua hatma yako iliyoshikiliwa, unaanza upya ratiba ya matengenezo (circular repetitions).

👉🏽Uhuru wa kuomba mahitaji, kupeleka hoja zenye nguvu, hata kiwango cha kumwagiza Mungu (giving orders to God), kinaanzia na moyo usiohukumiwa, moyo ukiwa na ujasiri utaomba mahitaji na utakuwa huru kuamuru maadui walioshikilia jibu lako lolote njiani waachie, malaika waliokwama njiani kwa sababu ya makosa yako, kwa sababu ya wewe kutosimamisha madhabahu yako katika msingi wake, wataweza sasa kukufikishia waliyopewa kwa ajili yako. (Isaya 45:11, 41:21, 1Yohana 3:21).

🎯 Kwa sababu hizo hapo juu, kuna watu hatma zao zimecheleweshwa. Hajazuiwa Mungu, ila imezuiwa kwa kucheleweshwa hatma yako njema (mbaraka uliopaswa kukujia na kukupata). Hivyo muda wako kamili wa kukutanishwa na mume sahihi ulifika, huenda miaka mitatu imepita, ila hatma imekawilishwa, maana ukikaguliwa moyoni mwako, umejaa mashaka (doubts), umechoka kumngoja Bwana, binti umeona miaka 35 hii hapa na hakuna mwanaume anayekuja akiwa serious na ndoa, kila anayekuja anataka tu mvuane nguo kwanza.

*NB🔨*
_*THIS GOES TO ALL WOMEN OUTSIDE THERE, HUWEZI KUMTHIBITISHIA MWANAUME UNAMPENDA KWA KUMCHOJOLEA 👉🏽👙, AND AS THE MATTER OF FACT FROM PSYCHOLOGICAL POINT OF VIEW, WANAUME WENGI WAKIISHAFANIKIWA KUKUDINYA, KWENYE VILINDI VYA MIOYO YAO WANAKUWA WAMEFUTA SWALA LA KUKUOA. UKIOLEWA NA MWANAUME AMBAYE AMEKWISHA KUKUDUNGUNYUA UMEPATA BAHATI TU. MAANA KILE AMBACHO ILIBIDI AKIPATE KWA GHARAMA NYINGI ZA KIROHO NA KIJAMII NA HITIFAKI NYINGI ZA KIROHO NA KIJAMII, AMEKIPATA TU BURE KWA KUKUTUMIA TEXT MOJA, "naomba uje ghetto mara moja"*_

Hivyo dada miaka kufika 35 ukiwa bachelorett (single), sio sababu ya kuamua kugawa mwili, sio sababu ya kufanya maamuzi kama vile sio mwana wa Mungu, eti ngoja nizae zangu, niwe na mwanangu, tena kanuni haikosei, ukigusa ngono siku moja tu na mimba juu, mimba hazitoki kwa Mungu bali kwa kanuni ya asili ya uzazi tangu uumbaji, kwamba yai likirutubishwa na mbegu na hakuna matatizo yoyote (biological/reproductive dysfunctions) basi conception inatokea (Kinachotoka kw Mungu ni roho ya mwanadamu muda wa conception). Lakini nje ya kanuni za Mungu, na kwa kuwa umefanya kusudi kabisa (Ebrania 10:26), basi kurudi kwa ile nafasi yako ya kuaminiwa na Mungu kwa mambo makubwa, itachukua muda na gharama kubwa.

🚩 *HATUA YA KWANZA YA KUSHUGHULIKA NA HATMA ZILIZOKAWILISHWA NI KUTENGENEZA MAMBO YAKO KIROHO*

🎯Jitahidi sana, usome kwa utulivu somo langu lisemalo, "Mambo ya kiroho yakiharibika; tengeneza". Humo ndani utapata vitu vingi sana.

🎯Mambo ya kiroho yakiwa sawa👍🏽, wewe utajua na maadui zako wa kiroho watajua.

👉🏽Utakuwa huru kuomba mahitaji kwa ahadi za Mungu wala hutazuiliwa neno tena...

👉🏽Mambo ya kiroho yakiwa sawa, kuna vitu utapewa kama ofa, kama zawadi tu, maana mtoto haombi kila kitu kwa baba yake, mengine baba anajiongeza tu, kuwa mmmh mwanangu hana viatu, mmmh uniforms za shule zimepauka sana, ndivyo Mungu atafanya kwako maana njia zako zampendeza, (Isaya 65:24, Math 6:8).

🚩 *HATUA INAYOFUATA NI KUFANYA VITA DHIDI YA WAKUU WA GIZA NA MAJESHI YA PEPO WABAYA, WALIOHUSIKA KUSHIKILIA HATMA NJEMA, KWA KUWA WALIKUWA NA SABABU HALALI MWANZO*

🎯 Hapa unapaswa kuwa na maarifa kamili kuhusu kushindana kiroho. Jitahidi kusoma masomo yangu haya mawili
1⃣ VITA VYA ROHONI
2⃣USHINDANI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

🎯Hii ni muhimu, maana sio mara zote roho za kipepo zitaachilia nyara zako, kisa umetengeneza mambo yako na Mungu. Kuna wakati (so often times) unalazimika kuwafurumsha kule rohoni wakimbie waache nyara zote walizoteka wakati ukiwa katika usingizi/ukame/kuchoka kiroho.

👉🏽This is so real, kuna watu wamewahi tengeneza mambo yao kiroho. Walipofanya vita kwa usahihi, ndipo mafaili yakafunuliwa upya, wakakuta wanitwa kufanya interviews ya kazi walizoapply miaka mitatu iliyopita, wengine wakaanza kutafutwa na wachumba na waume zao waliowa-dump miaka ya nyuma, kuwataka warudiane/ waoane seriously, kilichotokea hapo ni kwamba roho za kuzimu zilizoshikilia hatma sasa zimeachilia.

*M̸͟͞O̸͟͞Y̸͟͞O̸͟͞ W̸͟͞A̸͟͞ S̸͟͞O̸͟͞M̸͟͞O̸͟͞*
_M̸͟͞w̸͟͞l̸͟͞ P̸͟͞r̸͟͞o̸͟͞o̸͟͞_

🚩 *MWAMBIE BWANA AKUENDESHE MAHALI PAKO PALIPOINUKA*

*_"YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka."_*
(Habakuki 3: 19)

🎯 *THIS IS GOD'S PROMISE, FANYA KUMBUKUMBUSHA TU, KWAMBA BWANA ULISEMA KWA KINYWA CHAKO, TENDA KWA MKONO WAKO SASA. HII NI AHADI YAKE, SPEAK HIS WORD BACK  TO HIMSELF, YEYENI MWAMINIFU ANALIANGALIA NENO LA AHADI YAKE, AMBALO AMELITUKUZA KUILIKO HATA JINA LAKE (YER 1:12, ZAB 138:2)*

🎯 *AIFANYE MIGUU YAKO KUWA KAMA KULUNGU, KULUNGU NI DEER👉🏽🦌*
*HILI NI OMBI LAKO KWAKE, HAPA ANAZUNGUMZIA SPEED&FINALITY, ATALITEKELEZA NENO LAKE AKILIMALIZA NA KULIKATA*

*_"Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata."_*
(Waruma 9:28)

*AHADI YA MUNGU KWAKO, UNAYOPASWA KUISHIKA MPAKA UIINGIE HATMA YAKO NJEMA, NI HII KWAMBA BWANA ULIAHIDI UTATOA NENO NALO LITATIMIA, HALITAKAWILISHWA, HAYATAKAWILISHWA*
Ezekiel 12:21-28

_*PRAY UNTIL SOMETHING HAPPEN, USIKUBALI KUKONDEANA NA KUSINYAA WAKATI UNAPO MAHALI PAKO PALIPOINUKA, UTAKAPONG'AA NA KUWA MTU WA KUTAMANIWA NA MATAIFA YOTE. MWAMBIE BWANA SASA, AKUENDESHE MAHAI PAKO PALIPOINUKA. NAFSI WANGU KWA NINI KUINAMA NDANI YANGU? MTUMAINI MUNGU ALIYE AFYA YA USO WAKO*_

Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com

Thursday, March 8, 2018

MAAGANO

*MAAGANO YANAWEZA FANYWA IMARA (ESTABLISHING) AU KUDHOHOFISHWA (OBSOLETING), KUFANYWA UPYA (RENEWING) AU KUONDOLEWA KABISA (NULLIFYING)*

*Mwl Proo*
_*0762879363*_

_Ninawasalimu wasomaji, kwa jina la BWANA (Yesu), Yule mwenye kushika maagano (Daniel 9:4), Aliye Mwaminifu na Wa-Kweli (Ufunuo 19:11). Mungu alinitia moyoni nifundishe jambo hili la kukupa maarifa kamili._

🔒 *AGANO NI NINI?*

🔑Neno hili Agano/Covenant limetumiwa katika Biblia ya Kiebrania (Tanakh) mara 285 ambapo katika hayo yote limeandikwa *בְּרִית* linalosomeka *Bĕriyth/Berith* maana nyepesi kabisa ni *Patano*, Mwanazuoni *Warren Wiersbe* amefafanua neno hilo la Kiyahudi lina maana ya 1.Kula na/pamoja na (to eat with), ikiwa inazungumzia ushirika (fellowship),  2. Kufunga (to bind) ikiwa inazungumzia kujidhatiti kushika kwa kutenda (commitment), 3.Kugawa (to allot) inazungumzia kutoa/shirikisha (sharing), maalum kabisa ikizungumzia swala la Mungu akifanya Agano anakuwa amejidhatiti kabisa kutoa na kufanya yale aliyoyaahidi (keeping of promises).

🔑 Tafsiri ya pili ya maandiko matakatifu kwa lugha ya Kiyunani (Septuagint), ilitafsiri neno Berith/Agano kama *διαθήκη* linalosomeka *Diathéké*, neno hili Diathéké lilitumiwa katika ulimwengu ule wa *Greco-Roman World* kama Wosia wa Marehemu (Last will and Testament), ambapo maneno hayo hayakutanguliwa au kurekebishwa, na ndiyo pekee yalitumiwa katika kugawa mali za marehemu. Hata kama itadhaniwa marehemu hakutenda haki, alichosema ndicho last will (wishes) zake, haikudirikiwa kubadili neno.

🔑Nimetumia lugha za asili, kukupa chimbuko la neno Agano. Kwa ujumla wake twaweza jumuisha (consolidate) kuwa Agano ni patano, makubaliano kati ya pande mbili (two parties), yanayoambatana na ahadi/promises, vigezo na masharti (terms & conditions), yanayoweza fanywa kwa Oaths binding (Kula viapo 👉🏾 Agano la Maneno), mfano mzuri katika Biblia (Unequivocal Oathing Style) ni ule wa Daudi na Yonathani. Pia yanaweza kufanyika kwa damu *Blood ties* kwa njia ya sadaka za kuchinja kiumbe, au kama ile katika Semitic world ambapo watu waliweza kufanyika ndugu kwa kila mtu kunywa damu kidogo ya mwenzake.

🔒 *KUFANYWA IMARA/KUDHOHOFISHWA KWA AGANO*

🔑 Kwa kuwa Agano lina vigezo na masharti (terms/conditions), yakiendelea kushikwa kwa mkazo mkubwa (strict adherence to terms/conditions), yanapelekea Agano kuwa imara, upuuziaji wowote wa yale matakwa (requirements) yanaweza pelekea kudhohofika kwa Agano (Ingawa kudhohofika sio kuvunjika👉🏾 weakening of covenants is not abolishment).

*USHUHUDA No1*
Ushuhuda nilioukumbuka juu ya hili, ni wa mama mmoja aliyenunua gauni zuri la lenye vifungo/buttons za dhahabu 👉🏾👗👘👉🏾👙💎💎💎💎. Na mara baada ya muda kidogo tu, akaanza kuteswa na Pepo wachafu 👹👹👹. Alihangaika haswa, mapepo yakagoma kabisa, na hata yalipokubali kutoka, yakasema atatukuta nyumbani. Mwishoni akaamua kupeleka issue yake kwa mtumishi mwenye neema kubwa zaidi katika kufungua vifungo vya giza. Yule mtumishi alipoanza kuomba, akawa anaona vitu vinang'aang'aa, akakatisha maombi, akamwuliza yule mama, *"Nyumbani kwako kuna dhahabu?"*, yule mama akakataa, akaulizwa vitu vya dhahabu (gold-plated materials/assets), ndipo akakumbuka gauni lake amenunua kwa pesa nyingi lina vifungo vya dhahabu yenyewe 100%. Mtumishi alipoagizisha akakata vifungo na kuvitupa mbali, mapepo yaka-demonstrate, kisha yakaondoka, ikawa mwisho wa mchezo. Lakini katika kutafuta kujua habari, kwamba ni nini hasa kilitokea, ikapatikana habari, kuwa yule mfanya biashara alikuwa na maagano na majini kumsaidia kibiashara, na yakawa yanakaa kwa hivyo vifungo vya gauni. Lakini inaonesha yule mfanya biashara hakuendelea kuyashika masharti yote, hivyo majini/pepo yakaacha kufanya kazi yao ipasavyo ya kui-boost biashara, kumbuka gauni hilo hakuwa analiuza, alilitundika tu kama show. Lakini alipoona halitendi kazi sawa, akatafuta majini/mapepo mengine na lile akaliuza. Sasa kumbe maagano yake hayakuvunjwa, ila yalidhohofika tu, maana hakushika masharti yote, ndio maana mapepo yalibaki yakatesa mteja.

🔑 Katika Biblia tunaona Mungu anafanya Agano na Ibrahimu na vizazi vyake (Mwanzo 17:7), lakini mastari wa 9, anamwambia njia za kulifanya hilo Agano liwe hai/imara inategemeana na ushikwaji wa yale matakwa ya Agano

Tusome.....

*New Living Translation (NLT)*
(Mwanzo 17:9)
_Then God said to Abraham, "Your responsibility is to obey the *terms of the covenant*. You and all your descendants have this continual responsibility._

*NET Bible*
Mwanzo 17:9
_Then God said to Abraham, "As for you, you must keep the *covenantal requirement* I am imposing on you and your descendants after you throughout their generations._

🔒 *AGANO LAWEZA FUTWA/ABOLISHED, AU KUFANYWA UPYA*

🔑Maagano yanaweza fanywa kati ya pande sawa kwa ukuu, au mkuu akafanya mdogo (Superior//Inferior), kila upande unawajibika kushika Agano, na hapo ndipo Mungu anatajwa kuwa Yeye ni Mungu ashikaye maagano (Faithful to keep all of His promises). Inapotokea Mungu amefanya Agano, Yeye ni Superior, kama matakwa ya agano yakavunjwa kwa kiasi kisicho na tiba (non remediated), basi anaweza vunja agano.

1 Samweli 2 : 30
*Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu.*

👆🏽👆🏽Mungu aliagana na Ibrahimu lakini akalifanya imara Agano mpaka kwa Isaka (Mwanzo 17:21), kwa kuwa Isaka hakuwahi kuchakachua terms za Agano. Lakini katika mstari hapo juu, tunamwona bwana mdogo mwana wa Daudi, ambaye kwa kweli alivurunda. Huyu Sulemani ndiye haswa mwanzilishi wa kujenga *mahali pa juu (shrines/high places)* prompted by wale wanawake 700 aliowaoa kwa madhumuni ya kisiasa zaidi. Mungu ashikaye maagano, Uzalendo ulimshinda, akavunja Agano... Na ndio mwanzo wa Taifa la Mungu kugawanyika, yule mfanyakazi wa Ikulu ambaye alikuwa akielewa mwenendo mzima wa utawala (Yeroboam mwana wa Nebati), akatumika kama upanga, ufalme ukamegwa, makabila 10 yote ya Kaskazini (Taifa la Israel ) yakawa chini ya huyu mtu ambaye hakuwa katika kiapo cha Mungu kwa Daudi, ila Mungu kwa ajili ya Daudi mtumishi wake, akaona isiwe shida, akabakiza makabila mawili tu (Yuda+Benjamin) huku kusini (Taifa la Yuda). Haya ni madhara ya kuacha terms/masharti ya Agano.

🔒 *MAAGANO YA KIUKOO*
Katika somo langu la *NAFSI ILIYOJENGWA*, nilielez kuw nafsi inaweza kuuzwa. Sasa kuna mabibi na mababu walijiuza nafsi zao kwa pepo wabaya, wakafanya oath-bond (viapo) kwamba Agano hilo liwahusu na watoto wa watoto wao, mpaka vizazi vijavyo. Sasa maagano haya yanashikiliwa na hawa mapepo/majini/roho wabaya ambao kimakosa wamepewa jina la *roho za familia/family spirits*, kuwait kwa jina hili ni kuwapendelea hawa pepo wabaya, kisha ni pepo hawa hawa wanatafuta *Kick*  kwa kutumia sura za marehemu tofautitofauti katika ukoo, na kuwatokea watu kama mizimu *(IKUMBUKWE HAKUNA ROHO YA MAREHEMU INAYORUDI KUTOKA KUZIMUNI 👉🏾Ayubu 7:9-10)*, jitajidi usome somo langu la umilele, ili uyaelewe haya kwa kina. Lakini hakuna kitu kinaitwa mizimu ya mababu, ila ni mapepo ambayo mababu waliamua kujiuza nafsi zao kwayo, sasa yanachukua sura halisi, na kuja ku-disguise, eti yanawapa maelekezo. Yale mateso ambayo yanawakuta watu yakihusishwa na roho za familia/maagano ya ukoo, majaribio ya yale mapepo, katika kutafuta kuona hivi vizazi vipya vinashika matakwa yale ambayo waliagana na wazee wao. Kwa hiyo pepo linaweza kumtesa mtu (kwa magonjwa jata ya kurithi), kisha akiitwa mpiga ramli, anapandisha pepo, kwa mawasiliano ya kipepo inajulishwa kuwa unapaswa kufanya so and so, kumbe lengo, inakuwa ni *KULIFANYA IMARA AGANO AMBALO LIMEDHOHOFIKA*, ndio maana haipswi kamwe mtu mwamini, aliyekuwa kiroho na kuongezeka sana katika kimo cha cheo, eti ateswe na roho za familia au maagano ya mababu. Maana maagano hayo yalifanywa kati ya superior side (Mapepo/Majini) na inferior side (Mababu/Mabibi), Sasa ikija nguvu ya Msalaba wa Kristo na Damu ya pale Golgotha inakuwa na nguvu (Superior) kuyazidi majini/mapepo yote yaliyopata kuweko.

❌❌❌ *ONYO* 🚫🚫🚫
*KUNA MAMBO MENGI YA KITAMADUNI, HAYANA ASILI MWILINI BALI ROHONI, YALIKUWA _IMPOSED_, NA MAPEPO KAMA KACHUMBARI TU YA KUCHOCHEA MAAGANO ALONG ZILE TERMS/CONDITIONS ZA MAAGANO. HIVYO NI HATARI KWAKO MKRISTO/MWAMINI KUSHIRIKI OVYO MAMBO YA KIMILA/KIDESTURI UKITEMBELEA KIJIJINI KWENU. UNAWEZA KUTA MAMBO YA KUCHINJA MNYAMA KWA KUMSONGOA, KUPELEKA CHAKULA/POMBE MAKABURINI, MPAKA SOME TRADITIONAL DANCES (NGOMA ZA KIENYEJI-INGAWA SIO ZOTE), UWE MAKINI NA UKUBALI KUONGOZWA NA ROHO, KABLA HUJATAFUNWA NA JOKA🐍🐉*

🔒 *UCHAWI NA ULOZI*

🔑 Uchawi na ulozi unapofanyika, kinachofanya kazi sio vile vifaa vya kichawi 🌾🦇💀☠📿🏺📍🃏🎭🎲🎳, bali kuna mapepo ya ulozi na uchawi,ndiyo yanayoshikilia *VIAPO, MANUIZO, MAZINDIKO*, kwa hiyo hata kama mlichinja mbuzi, mkafukia kichwa mlangoni, kunakuwa na PepoJini anayeshikilia hilo Agano la Damu. Kama mtu amefungwa tumbo asizae. Na mganga au mchawi alichukua uzi mwekundu akaufunga kwenye kijiti au mfupa (ule uzi ni medium tu yaani mawasiliano ya kipepo ya physical article to spiritual altar), kinachofanya kazi kushikiliza lile tumbo lisishike mimba sio huo uzi, bali kuna Jinn/Pepo la Ulozi ambalo hiyo ishu inakuwa *entrusted* kwake, nalo litaifanya kazi hiyo kwa uaminifu. Kama huyu mtu akienda kwa mtumishi mwenye nguvu chache (kimo kidogo rohoni kwa cheo), akikemea kifungo kifunguke, PepoJini aliyekabidhiwa kushikilia kile kifungo, anaweza akaamua kushikilia maana nguvu/mamlaka iliyoamuru aachie ni ndogo (Kumbuka mzazi mwenye mtoto mwenye pepo bubu, ambaye alimpeleka kwa wanafunzi wakashindwa Mathayo 17). Kumbuka kuokoka haina maana kwamba utakuwa na nguvu kuzidi maadui wote wa kiroho (SHARTI UONGEZE UWEZO WAKO SANAA 👉🏾 Nahumu 2:1). Hawa majini/mapepo wanamtambua mwenye nguvu kubwa huwezi kuwavunga, waulize wana wa Skewa. Hivyo wakikutana na mwenye nguvu kubwa akiamuru utasa toka, huu utasa kwa kuwa ulisababishwa na kale kauzi ka kichawi, hili pepo lililokbidhiwa kazi ya kushikilia lita-salimu amri na kuachia, hata kama yule mlozi/mchawi akilituma tena, litatia mgomo, kwamba Mmmh, No! pale nimefukuzwa!

*HITIMISHO*

*Ndugu wapendwa, kama kuna maagano yoyote yanayokutumikisha, iwe ulifanya mwenyewe au yalifanywa ma watangulizi wako, yakabaki yanasumbua, tiba ya ku-nullify maagano yote ni Damu ya Yesu ya Agano na Msalaba. Maagano hayo yatavunjika kwa sababu mamlaka ya Yesu ni kubwa kuliko maadui wote wa kiroho na kimwili.*

*LAKINI PIA, MUNGU KATIKA NENO LAKE AMETUPA TERMS/CONDITIONS ZA KULIFANYA AGANO LAKE KWETU LIWE IMARA. AGANO HILO LIMEAMBATANA NA AHADI TELE. AHADI HIZO ZINAWEZA KUADIMIKA MAISHANI MWAKO KAMA UTAYAACHA MATAKWA YA AGANO. KWA MFANO UMEAHIDIWA UZIMA, AFYA NA KUPONA, UMEAHIDIWA KUFANIKIWA KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA, UMEAHIDIWA ULINZI, MUNGU AMEAHIDI KUWA ADUI WA ADUI ZAKO, AMEAHIDI KUWATAWANYA MAADUI WALIOKUJA KWA NJIA MOJA WATAWANYIKE KWA NJIA SABA, AMEAHIDI KWAMBA UTASHUKA KABURINI UKIWA UMESHIBA SIKU, AMEAHIDI KUKUFANYA KICHWA NA KUKUWEKA JUU TU, WANAFUNZI WA  BIBLIA WAMEHESABU JUMLA YA AHADI ZIKO 31,100, LAKINI AHADI HIZI ZINAZOAMBATA NA AGANO LAKE KWETU HATUZIRITHI BURE BURE, BALI KATIKA KUSHIKA SANA MATAKWA YA AGANO LAKE KWETU.*

KWA UFAFANUZI WA KINA KUHUSU AGANO LETU PAMOJA MASHARTI YAKE, USIKOSE SOMO LANGU LIJALO LIITWALO *"WAHUDUMU WA AGANO JIPYA*

*Mwl Proo*
_0762879363_

alltruth5ministries@gmail.com