*NENO LA MUNGU NI UFUNUO; UNAHITAJI ROHO YA UFUNUO ILI KUJUA KILICHOFUNULIWA KWA NJIA YA NENO LIILIONDIKWA (BIBLIA) AU KUTAMKWA (UNABII, MAHUBIRI, MAFUNDISHO)*
_*ʍաӀ Թɾօօ*_
*0762879363*
Ninakusalimu msomaji kwa jina la Bwana na Mwokozi, Yesu Kristo, amani na neema yake izidishwe kwako. Usomapo ujumbe huu Yesu akupe hatua na kiwango kingine rohoni, nimeanza kuandika nikiwa na-sense katika roho, neema ya kuinuliwa viwango kwa utakayesoma kwa moyo wa shauku na kumtaka Bwana.
Kichwa cha ujumbe kimekuwa kirefu maana nilitafuta kuainisha jambo la muhimu kuhusu Neno la Mungu. Tukisema *Neno La Mungu*, tupo na *Dimensions* mizania mitatu (3Ds), 1.) Yesu Kristo ni Neno Hai la Mungu (Personified, Living Word Of God), 2.) Maandiko Katika Biblia (Scriptures), Ni neno la Mungu lililoandikwa (Written Word of God), na mwisho tuna Neno la Mungu la kutamkwa (Spoken Word of God), hapa tunajumuisha vyote Unabii, mafundisho, mahubiri etc. Hizi dimensions tatu hazitenganishwi, ndio maana ukisema umetokewa na Yesu, kisha amekupa ujumbe unaokataana na Neno lililofunuliwa katika maandiko hatuwezi kukupokea na ujumbe wako, maana Yeye aliyesema msitweze unabii ndiye aliyesema tuujaribu Naam tuupambanue (1Thes 5:20-21, 1Kor 14:29, 1Yoh 4:1).
*☄NENO LA MUNGU NI UFUNUO*
Paulo anawaombea hawa wakristo walioko efeso kwamba
*_"Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;"_*
*(Waefeso 1: 17)*
✍🏾Neno ufunuo linalotajwa katika Biblia latokana na tafsiri ya kimuktadha ya kiyunani, neno linalotumika ni _*Apokaliptos /Apokalipsis👉🏾ἀποκάλυψις*_ (English 👉🏾Apocalypse). Chukua mfano huu, umewekewa sufuria (cooking pan), imewekwa mfuniko juu, unaambiwa utaje kuna nini ndani yake, nawe hukuwepo muda sufuria inafunikwa, huenda kuna chakula usichokijua kabisa, au hawajaweka kitu. Kitakachoweza kukupa kujua what exactly is inside the cooking pan, ni kufunuliwa kwa mfuniko (apocalypse ). Ni kwa namna hiyo hiyo Neno la Mungu ni ufunuo, vitu vilivyofichika vikafunuliwa, lakini msomaji na msikiaji anahitaji bado roho ya ufunuo kuyajua yaliyowekwa sirini, ndio maana Neno la Mungu linahitaji kufafanushwa, na Neno hili katika Biblia limebeba siri nyingi, maajabu mengi zaidi ya yale ambayo tunayashangaa, Daudi akasema Mungu fumbua/funua macho yangu nione maajabu yaliyo katika neno/sheria yako (Zaburi 119:130, 18).
✍🏾 Mungu ameniwekea moyoni ujumbe huu juzi, muda nasoma sura ya Biblia iliyojaa orodha (list) ya vizazi (genealogies), nikawaza hivi kutuwekea sura nzima fulani akamzaa fulani, fulani akamzaa fulani, you find it the whole chapter unasoma vizazi hivyo mpaka unakinai, ndipo macho yangu yakatiwa nuru nikapata ufunuo mkubwa juu ile orodha/list ya vizazi, na nikaamua kuheshimu vyote vilivyoandikwa. Pamoja na ukweli kwamba kuna sababu ambazo ni *jewish culture&context* zinazopelekea kuwekwa kwa uzito katika ku-identify vizazi, lakini kwetu sisi, kwa roho ya ufunuo, kilichopo kwenye maandiko na sura zote zenye kuorodhesha vizazi kuna siri kuu za kimungu beyond the cultural context ya kiyahudi ya kuweka vizazi na koo mbalimbali.
*☄NENO LA MUNGU NI UNABII/UFUNUO WA NYAKATI ZOTE*
*Maandiko ya msingi (Isaya 13:1, 14:28, 15:1, 17:1, 19:1, 21:1, 11, 13, 22:1, 23:1, 30:6, Ezek 12:10, Nahum 1:1, Habakuk 1:1, Zek 9:1, 12:1, Malak 1:1, Ufu 1:1*
✍🏾 Maandiko yetu ya msingi, yote yanaonesha kuwa hawa watu, walipokea ufunuo wa vitu walivyoongea na kuandika. Sio hisia zao, sio ufahamu wao. Wengi katika wajumbe/manabii ambao Waliona na kuandika hayo tusomayo, ni Mungu aliweka maneno vinywani mwao, mengine kwa Roho ya Bwana waliyaona na kuyasikia rohoni, na wakaweka matamko ya waliyoyaona na kuyasikia kama unabii wa nyakati zote. Na kila mahali ambapo Mungu amesema unakutana na usemi huu, *"Asema Bwana, that says/saith the Lord"* ikiwa na maana ya kwamba hayo mambo bado Mungu anaendelea kuyatangaza kwako na kwa dunia yote hata sasa.
*NB*
*NIMESIKIA BAADHI YA WATU WALIOKOSA UFUNUO WA ROHO KUHUSU MAANDIKO YA KINABII, WAKITOA CHANGAMOTO KUHUSU ISAYA 14:12ff, NA ILE EZEKIEL 28:14ff, KWAMBA HAZIMZUNGUMZII SHETANI. HAWA NI WATU AMBAO HAWAJAANZA KUELEWA LUGHA YA MANABII NA VITABU VYAO, ISAYA KATIKA SURA YA 13&14 ANAZUNGUMZIA ANGUKO LA BABEL NA KUREJEZWA KWA ISRAEL, LAKINI HUMO NDANI ANAYOYAONGEA NA KUYAONA ROHONI NI ZAIDI YA BABEL NA ZAIDI YA ISRAEL KUINULIWA TENA. EZEKIEL NAYE KATIKA SURA YA 28 ANATOA UNABII JUU YA MIJI YA TIRO NA SIDONI, HUMO NDANI AMEONGEA NA MAMBO YA KIROHO YA ZAMA ZA HATA KABLA YA ULIMWENGU WA SASA (I will prove this).*
_Tusome mfano huu..._
*(Yeremia 4 )*
------------
*_23 Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru._*
_*24 Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko.*_
_*25 Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao.*_
_*26 Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za Bwana, na mbele za hasira yake kali.*_
👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾 Katika mistari hiyo hapo juu kuna siri nyingi sana. Kama ambavyo Isaya BeneHa'Amoz anavyotambulisha kitabu chake kwamba ni unabii juu Yuda na Yerusalem (Isaya 1:1) lakini ukisoma unakuja kuta ameongea mambo ya zama zote kabla ya uumbaji na ya mpaka mwisho wa dunia, na ya baada ya mwisho wa siku na hata ya milele ijayo. Ndivyo ilivyo kwa Yeremia BeneHa' Hilkiah, aliona alisikia katika roho mambo zaidi ya yale aliyoyatolea unabii kwa zama zake. Mfano mdogo kwa wale wanao wanaotunisha misuli kwa ufahamu wao mdogo, Je! Yeremia 4:23-26, anazungumza habari gani? ni wakati gani huu aliouona yeye? Dunia ikiwa haina watu kabisa, haina ndege hata mmoja, wote wamekwenda zao, mbingu haina nuru, nchi iko ukiwa, miji imebobomoka. Ni wakati gani dunia ilipitia hali hii, au itapitia wakati huu? Wanathiolojia waliokubuu wanaishia kusema hii ni hali iliyotokea wakati wa gharika ya Nuhu, which can't be true, dunia ilibakia na watu nane safinani na pairs of sparrows 🕊🕊 na viumbe vingine. Wala katika mambo ya siku za mwisho (eschatological events) hata katika ghadhabu na mapigo ya Mungu, hakuna wakati kama huo. Lakini Yeremia aliona katika roho mambo yaliyotokea pale kutoka Mwanzo 1:1 mpaka Mwanzo 1:2, kulitokea ya kutokea mengi sitayafunua kwa somo hili bali somo jingine siku chache zijazo. Lengo langu hapo ni kukufanya uwe makini na maandiko ya manabii, maana hata ukisoma Kitabu cha Nabii Nahumu Mwelkoshi yeye alipewa unabii juu ya mji wa Ninawi (Nahumu 1:1), ukianza kusoma unagundua anaongea mambo ya unabii na ufunuo wa nyakati zote. Ukisoma Zekaria 9, unakuta nabii anatoa unabii juu ya nchi ya Hadraki na mahali pa kustarehe Dameski, ukienda mbele kidogo unakutana na *turnarounds* ghafula anatoa messianic prophecies na kumtabiria Yesu mwokozi aliyefika miaka 484 tangu muda Zekaria anatoa unabii. Hivyo niifunge hoja hii kwa kukusaidia kujua unatakiwa uombe roho ya ufunuo ili kuelewa ufunuo katika Neno la Mungu, unaposoma kitabu kama cha *Wimbo Ulio Bora* don't just read it like Novels or Magazines 📚🗞📰, ni kweli kabisa, Ule ni wimbo ambao Sulemani alimwimbia mwanamke Mshulami, lakini aliuimba katika roho na mle ndani kuna unabii na ufunuo mkubwa mno wala hauhusiki na mapenzi, sehemu kubwa sio mapenzi bali ni ufunuo wa Yesu Kristo na Bi Arusi wake (Lover & Beloved) na siri nyingi za kiroho.
NB:
*PROPHET SAW IN THE SPIRIT THINGS THAT HAD HAPPENED FROM BEFORE TIME, THINGS DURING THEIR LIFETIME, AND THINGS IN THE NEAR& FAR FUTURE, THINGS THAT HAPPENED AND YET TO HAPPEN AGAIN NDIO MAANA WATU WAKISOMA ANDIKO KAMA UFUNUO 12:7ff WANABAKI WAKICHANGANYA KWA KUTOELEWA PROPHETIC PRESENTATIONS)*
💡 *NAOMBA NIKUPE SHAUKU KWA KUFUNUA SIRI MOJA TU, ILI KUKUPA SHAUKU ZAIDI JUU YA KUOMBA ROHO YA UFUNUO ILI KUFAHAMU NA KUJUA KWA HAKIKA, SIRI ZILIZOFUNULIWA KWA NENO LA NENO LA MUNGU* 💡
_Bila shaka katika kusoma maandiko, umekutana sana na jina Lewiathani (Leviathan), (Ayubu 3:8, Zaburi 74:14, 104:26, Isaya 27:1). Ukitafuta kujua ni kiumbe gani huyu, unakuta kamusi zinataja tu ni mnyama mkubwa wa kufikirika (imaginary creature) aishie baharini, pahala pengine wametaja huenda akawa mamba, pengine wamesema ni joka la baharini)_
*Soma hapa....*
*"Katika siku hiyo Bwana, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini."*
*(Isaya 27:1 )*
_Sasa unaweza ona mnyama huyu amehusishwa na unabii mzito wa siku za mwisho hususani Armageddon na Hukumu ya mwisho, hivyo utagundua ni zaidi ya kuwaza ni mnyama tu fulani_
_Pia bila shaka katika Biblia yako umesoma katika maandiko yako kuhusu mnyama aitwaye *Behemoth*, waliotafsiri Biblia walijaribu kuangalia sifa zinazotajwa, wakajiongeza kuwa huenda akawa ni kiboko (Hippo). Nimechungulia katika English Dictionary mnyama huyu *Behemoth* wamenadika tu *A giant beast, God showed Job 👉🏾(Ayubu 40:15-24)* yaani mpaka hilo andiko lipo kwa Dictionary hiyo isiyo ya kidini._
_Nilipojaribu kutafuta maarifa what really are these creatures?, ndipo nikaja kujua God created two monsters female monster and male monster ndio hawa Behemothi na Lewiathani, moja anaishi katika jangwa na mwingine katika bahari, they are all invisible, habari kuwahusu viumbe hawa na siri uumbaji wao ni ajabu sana. Sitajadili pia kwa kina kuhusu hawa, ila natakaniamshe kiu tu, ujue jinsi ambavyo Neno la Mungu limejaa ufunuo na siri zisizo za kawaida, Usiache kamwe kusoma Neno. Usiache kamwe kuomba roho ya ufunuo ili ikuangazie nuru uweza kuyapata tuliyokirimiwa na Mungu. Kama Mungu aliwaonesha manabii wakaandika tafsiri yake ni kwamba Mungu ametsmani tuyajue, tusipoyajua ambayo Mungu anataka tuyajue, tutaishi chini ya kiwango, tutamfahamu Mungu chini ya kiwango. Bwana akujalie roho ya ufunuo katika jina la Yesu._
Tukutane katika somo lijalo, kuna mambo mazuri Mungu atatufundisha kwa Roho wake Mtakatifu.
*Mwl Proo*
+255762879363
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment