Tuesday, July 17, 2018

Kuhusu kutotajwa jina Mungu katika kitabu cha Esta

*KWA NINI KITABU CHA ESTA, HAKIJATAJA  MUNGU KABISA WALA KWA MAJINA YAKE MENGINE?*

_Mwl Proo_

Shalom, hili sio somo, bali ni jibu la swali hilo kwa ufupi tu. Kitabu ambacho kipo katika vitabu vinavyokubalika (Canonical Books), katika Biblia lakini hakija taja jina la Mungu/BWANA kabisa ni hiki cha Esta.

Ziko sababu kadha wa kadha za kutoandikwa Mungu wala majina yake mengine. Jambo hili lilifanya wasomi wahoji, uhalali wa kitabu hiki kuwepo katika Kanoni ya Biblia

*Majibu*

1. Vyanzo vya kiyahudi vinadai kuwa Modekai (Mordecai) ndiye mwandishi. Aliandika akiwa afisa kwa mfalme Xerxes (Ahasuero), na hivyo kama afisa katika serikali hiyo aliandika uhusika wa Mungu YEHOVA kwa hali ya juu sana ila bila kumtaja jina. Sababu ni kwamba alitaka kiweze ku-fit katika muktadha wa imani ya miungu wengi (Polytheistic context of Susa) ya huko Shushani, hivyo hakutaka kutoa credits kwa YHWH kama ndiye aliyewaletea wokovu ule kwa wazi. Hivyo matukio waliyofanya ya kufunga na kuomba ameyaeleza kwa kificho lakini ameeleza wokovu wa Mungu kwa viwango vya juu.
2.  Wanazuoni wa kisasa wa thiolojia (Modern Scholars), husema kwamba kitabu hiki kiliandikwa kuwa cha kihistoria tu *(Pure Secular Book of History)*, ndiyo sababu yake pia kutotajwa katika yale magombo ya chuo ya Bahari Mfu (Dead Sea Scrolls).

Katika zama fulani, wako waliokiongezea idadi ya sura kitabu (Apocryphal part of the Book of Esther), na wakapachika jina "Mungu", ambapo badae kiliingizwa katika Kanoni ya Maandiko matakatifu ya Katoliki. Lakini haihitajiki kuisaidia Biblia kwa namna hiyo, maandiko haya yana uvuvio bila hata kuongezea neno/jina Mungu/BWANA. Mungu amejionesha kwa namna ya ajabu katika kitabu cha Esta, jinsi ambavyo pamoja na kujificha uso wake, na taifa la watu wake kwenda utumwani, hakuwaacha. Aliwaadhibu kwa dhambi zao huku akiendelea kukumbuka agano lake kwa Israel, na wakiwa huko alikuwa pamoja nao, ili awaokoe.

Mbarikiwe

No comments:

Post a Comment