*NAMNA MASAA (ZAMU) YALIVYOHESABIWA KIBIBLIA*
~_*MwlProo*_~
Shalom...! Nimeandika posti hii fupi, kujibu swali lililoulizwa na mwanakundi mwenzetu kuhusu *Zamu ya nne*
Tangu Adamu babaye Sethi mpaka karne zaidi ya 14 baada ya Yesu, hakukuwa na kifaa chochote "kitunza muda" kwa namna ya saa (watch/clock). ππΌππΌ π§⏱⏰ . Kila mahali duniani watu walikuwa na namna tofauti za kuhesabu masaa. Mpaka mwaka 1656 ambapo m-Dutch (a polymath&horologist) mmoja mwerevu sana na fundi saa (inventor) aitwaye Christiaan Huygens alipogundua saa... Na kuanzia hapo mpaka miaka ya 1930's saa ziitwazo *_Pendulum clock & Spiral-hairspring_* ziliendelea kutumika.
*ZAMA ZA BIBLIA*
Biblia imeandikwa kwa miaka karibu 1,500, Yaliyoandikwa Agano la Kale (iwe muda au mambo mengine lazima yamulikwe kwa jicho la kiEbrania) na yaliyoandikwa Agano Jipya lazima yamulikwe kwa jicho la kiYunani (lugha iliyotumika kuandika Agano jipya) na kiRumi yaani dola iliyokuwa inatawala wakati huo. Mifumo miwili iliyotumika kuhesabu saa katika Biblia ni mifumo ya Kirumi na Kiyahudi. Warumi waligawanya masaa ya usiku katika Zamu Nne (4), Hivyo masaa 12 yalikuwa na mgawanyo wa makesha manne (Four Watches of Night), Kuna jambo ambalo nitaliondoa katika posti hii kufupisha maelezo, lakini kwa ufupi Warumi waliweza kuwa na tofauti ya muda wa kuanza kesha la kwanza kutegemea na majira ya mwaka au vipindi vinne (i.e., Spring Equinox kesha la kwanza lilianza saa moja jioni, Summer Solstice kesha la kwanza lilianza saa mbili usiku, Autumnal equinox kesha la kwanza lilianza saa kumi na mbili jioni, na Winter Solstice kesha la kwanza lilianza saa kumi na moja jioni. Makesha au Zamu nne ni hizi, yaani Vigilia Prima (ZAMU YA I) kuanzia 1700hrs (saa kumi na moja jioni) mpaka 2000hrs (saa mbili usiku). Kisha kuna Vigilia Secunda (ZAMU YA II) Kuanzia 2000hrs (saa mbili usiku) mpaka 2300hrs (Saa tano usiku) kisha kuna Vigilia tertia (ZAMU YA III) kuanzia saa 2300hrs mpaka 0200hrs (saa nane usiku). Na kisha kuna zamu ya nne iitwayo Vigilia quarta kuanzia 0200hrs mpaka 0500hrs (saa kumi na moja alfajiri).. Huu ni mfano wa zamu nne kwa majira ya (Winter Solstice) saa la kwanza la zamu likibadilika masaa yote yatakuwa tofauti.
Wayahudi walikuwa na zamu tatu tu (Kesha la kwanza/Zamu ya kwanza ππΌ Omb 2:19, kesha/zamu ya kati/middle watch ππΌ Amu 7:19, na kesha/zamu la asubuhi ππΌ Kut 14:24, 1Sam 11:11, walianza saa 6pm mpaka 10pm (ZAMU YA I), kisha 10pm mpaka 2am (ZAMU YA II), na mwisho ni kuanzia saa 2am mpaka 6am (ZAMU YA TATU). Mfumo wa Wayahudi uliingiliwa na mfumo wa dola tawala hivyo nao mgawanyo ukaongeza zamu moja ya nne, na masaa yakawa hivi ππΌ1st (6pm – 9pm); ππΌ2nd (9pm – 12am); ππΌ3rd (12am – 3am); ππΌ4th (3am – 6am). Zamu hizi ziko sawasawa za zamu nne za kiRumi zilizoanzia saa 1800hrs kwa msimu wa *Autumnal equinox*. Na huu ndio mfumo unaowasilishwa katika Mathayo 14:25
NB:-
_mwlproo_
Ikumbukwe wanapotaja zamu ya nne, halitajwi saa moja. specific bali ni saa yoyote tangu saa 3.00am mpaka 6.00am (iwapo tutatumia zamu za kiYahudi zilizorekebishwa wakiwa chini ya utawala wa kirumi). Katika mgawanyo wa zamu za mchana utakuta katika Biblia kumetajwa sana yapata saa tatu, yapata saa sita, yapata saa tisa....Walikuwa wana-estimate tu muda ndani ya zamu (Ingawa warumi walikuwa na kifaa _era Sundial_ ambacho kiliweza kuonesha muda kwa kivuli kupita juu ya alama zao walizozichora juu ya mwamba uliochongwa vizuri). Na hapa ndipo tunaweza jibu swali la Je! Yesu alisulibiwa saa tatu asubuhi (Marko 15:25) au saa sita mchana (Yohana 19:14)? Fahamu kwamba si rahisi ku kukuta muda mfano saa mbili na nusu, au saa nane kasoro-robo maana mfumo haukuruhusu. Na kama mpo zamu ya pili mwishoni (let say saa tano asubuhi), uko huru kuuita huo muda ni saa tatu (according to Mark), na muda huohuo unakaribia zamu ya tatu inayoanza saa sita, hivyo Yohana hakukosea pia kuita ni saa sita (mmoja ka-refer zamu ya pili mwishoni na mwingine zamu ya tatu mwanzoni)..
Naamini kwa sehemu umepata mwanga.. Maelezo ya ziada kuhusu hizi tofauti na mengine mengi, yapo kwa kina katika somo langu Mimi Mwl Proo, liitwalo *Kutofautiana kwa taarifa kwa injili zinazofanana yaani Different reporting in Synoptic Gospels*
No comments:
Post a Comment